Tutaishije
-
Upload
nelson-opany -
Category
Documents
-
view
274 -
download
5
description
Transcript of Tutaishije
TUTAISHIJE?
Mazingira mazuri kama yetu
Kitu gani kinatufanya twaribu?
Elimu tunayo ya kutosha
Rasilimali zetu kuhifadhi
Naam! Wakati umefika
Wa sisi kuchukua hatua
Kwa ajili ya ulimwengu wetu
Na kuutnza utajiri wetu
Ni wasaa wa kusema kweli
Kuhusu mabadiliko ya tabia nchi
Na kamwe kutorudi nyuma
Vita hivi kuviendeleza
Tutaishije dunia yetu ikigeuka? Tutaishije miti ikikatwa na mito kukauka?
Tutaishije hewa yet ikichafuliwa?
Tutaishije mimea na wanyama wakiathirika?
Nina imani
Kwa mazingira yenye ubora wa kudumu
Kwa maendeleo yakuboresha maisha kikamilifu
Na kwa ulimweng wenye ufanisi
Jukumu ni letu sisi
Kuchukua hatua sasa
Kulinda ulimwengu tunaouenzi Kwa ajili yetu na vizazi vijavyo
Lau sivyo, sijui tutaishije?
Shairi limetungwa na
Nelson Ochieng Opany (Al-Ustadh Weledi)