MATUMIZI BORA YA MALIASILI IDODI NA PAWAGA (MBOMIPA); JUMUIYA YA … · 2018-06-12 · za...

12
Uanzishwaji wa Visa Asili vyampango wa Ikweta Masuluhisho endelevu ya kienyeji kwa maendeleo kwa watu, asili, na jamii thabitizinazohimili matatizo Tanzania MATUMIZI BORA YA MALIASILI IDODI NA PAWAGA (MBOMIPA); JUMUIYA YA UHIFADHI WANYAMAPORI Empowered lives. Resilient nations.

Transcript of MATUMIZI BORA YA MALIASILI IDODI NA PAWAGA (MBOMIPA); JUMUIYA YA … · 2018-06-12 · za...

Page 1: MATUMIZI BORA YA MALIASILI IDODI NA PAWAGA (MBOMIPA); JUMUIYA YA … · 2018-06-12 · za wanyamapori na kupewa mamlaka na faida ya moja kwa moja kutoka kwa rasilimali hiyo, vinginevyo

Uanzishwaji wa Visa Asili vyampango wa IkwetaMasuluhisho endelevu ya kienyeji kwa maendeleo kwa watu, asili, na jamii thabitizinazohimili matatizo

Tanzania

MATUMIZI BORA YA MALIASILI IDODI NA PAWAGA (MBOMIPA); JUMUIYA YA UHIFADHI WANYAMAPORI

Empowered lives. Resilient nations.

Page 2: MATUMIZI BORA YA MALIASILI IDODI NA PAWAGA (MBOMIPA); JUMUIYA YA … · 2018-06-12 · za wanyamapori na kupewa mamlaka na faida ya moja kwa moja kutoka kwa rasilimali hiyo, vinginevyo

UANZISHWAJI WA MFULULIZO WA VISA ASILI VYA MPANGO WA IKWETA WA UNDPWanajamii wenyeji duniani kote wanaendeleza suluhisho za maendeleo endelevu ambazo zinaweza kufanya kazi kwa watu na kwa asili. Vitabu vichache au chunguzi kifani hutupa hadithi kamili ya jinsi ambavyo mipango hii hukua, upana wa athari zake, au jinsi zinavyobadilika kwa wakati. Chache zaidi bado zimejaribu kutoa hadithi hizi na jamii tendaji zenyewa zikielekeza usimulizi. Uanzishwaji wa Ikweta unalenga kujaza pengo hili.

Mpango wa Ikweta wa UNDP, kwa kushirkiana na ENDA Tiers Monde (ENDA), Open Society Initiative for Southern Africa (OSISA), United Nations Convention to Combat Desertification (UNCCD), na kufadhiliwa na Global Environment Facility (GEF), ulitambua mifano ya ustadi wa ndani, uvumbuzi, na uongozi katika Sustainable Land Management (SLM, Usimamizi Endelevu wa Ardhi) katika nchi kavu za Sahara Afrika. Kisa asili kifuatacho ni moja ya mfululizo ambao unaeleza mazoea ya usimamizi ya SLM yaliyotathminiwa na kupitiwa, unaolenga kuhamasisha mazungumzo ya sera yanayohitajika kuongeza mafanikio ya ndani, kuboresha msingi wa ujuzi wa kimataifa kuhusu mazingira na suluhisho la maendeleo, na kuwa kama mfano kwa ajili ya kuweza kufanyika sehemu nyingine.

Bonyeza katika ramani ya miradi ya Equator ili upate kupata habari zaidi.

WahaririMhariri Mkuu: Joseph CorcoranMhariri Mtendaji: Alan PierceWahariri wa Kuchangia: Eva Gurria

Waandishi WaliochangiaAlan Pierce, Eva Gurria, Annie Virnig, Elizabeth Shaw, Anthony von Arx, Joshua Voges, Qiang Li, Kathryn McCann

KubuniKimberly Koserowski

ShukraniUanzishwaji wa Ikweta unatambua kwa shukrani kwa Matumizi Bora ya Malihai Idodi na Pawaga (MBOMIPA) Eneo la Usimamizi wa Wan-yamapori. Picha zote kwa hisani ya MBOMIPA. Ramani kwa hisani ya CIA World Factbook na Wikipedia. Ufasiri kwa hisani ya Lucy Ann W. Njagi na marekebisho ya ufasiri kwa hisani ya Aloisia Shemdoe.

Dondoo LililopendekezwaUnited Nations Development Programme. 2016. Matumizi Bora Ya Maliasili Idodi Na Pawaga (Mbomipa); Jumuiya Ya Uhifadhi Wanyamapori, Tanzania. Mfululizo wa Uchunguzi Kifani wa Mpango wa Ikweta. New York, NY.

Page 3: MATUMIZI BORA YA MALIASILI IDODI NA PAWAGA (MBOMIPA); JUMUIYA YA … · 2018-06-12 · za wanyamapori na kupewa mamlaka na faida ya moja kwa moja kutoka kwa rasilimali hiyo, vinginevyo

MUHTASARI WA MRADIMBOMIPA ni kifupisho cha maneno ya kiswahili; Matumizi Bora ya Maliasili Idodi na Pawaga. Ni jumuiya ya uhifadhi wa wanyamapori inayoundwa na vijiji 21 vyenye wakazi zaidi ya elfu sitini na mbili (62,000) wanaoishi karibu na hifadhi kubwa kuliko zote nchini Tanzania na Afrika Masharika ya Ruaha inayohusika na usimamizi endelevu wa rasilimali za asili katika eneo la Ruaha. Jumuiya hii ilianzishwa kwa lengo la kusimamia rasilimali za asili na kitamaduni zinazopatikana katika maeneo haya kwa lengo la kukuza kipato kwa vijiji wanachama na kuzifanya ziwe endelevu.. Mapato yatokanayo na jumuiya hugawanywa kwa vijiji wanachama kwa lengo la kutumika katika miradi mbalimbali ya maendeleo kama vile kama huduma ya afya, elimu na miundo mbinu. Pamoja na jukumu la kuhifadhi wanyamapori, vile vile jumuiya inahusika na suala la kuzuia migogoro iliyopo kati ya wanyamapori na binadamu. Eneo hili lilipewa hadhi ya kuwa jumuiya inayoweza kujiendesha yenyewe na kutangazwa katika gazeti la serikali mwaka 2007 na kutumiwa kama jumuiya ya mfano wa kuigwa katika uhifadhi wa wanyamapori nchini Tanzania

UKWELI KUHUSU JUMUIYA YA MBOMIPAMshindi wa Tuzo la Ikweta: 2014

Ilianzishwa: 2002

Mahali: Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Mkoa wa Iringa, Kusini kati mwa Tanzania

Wanufaika: Vijiji wanachama 21 vyenye Jumla ya wakazi 62,000

Maliasilii:: Wanyamapori, misitu , Maji, mawe, uoto wa asili

3

JEDWALI LA YALIYOMO

Historia na Muktadha 4

Shughuli Muhimu na Uvumbuzi 6

Athari 7

Athari kwa viumbehai 7

Athari za Kijamii na Kiuchumi 8

Jinsia 8

Athari za Kisera 9

Uendelevu 10

Utoaji nakala 10

Wabia 10

MATUMIZI BORA YA MALIASILI IDODI NA PAWAGA (MBOMIPA); JUMUIYA YA UHIFADHI WANYAMAPORITanzania

Page 4: MATUMIZI BORA YA MALIASILI IDODI NA PAWAGA (MBOMIPA); JUMUIYA YA … · 2018-06-12 · za wanyamapori na kupewa mamlaka na faida ya moja kwa moja kutoka kwa rasilimali hiyo, vinginevyo

44

Matumizi Bora ya Maliasili Idodi na Pawaga (MBOMIPA), ni jumuiya inayoundwa na vijiji 21 vinavyopatikana katika tarafa za Idodi na Pawaga, Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Mkoa wa Iringa nchini Tanzania. Eneo hili la jumuiya lipo kilometa 600 Kusini magharibi mwa jiji la Dar es Salaam, mji mkuu wa kiuchumi na kitamaduni a Tanzania. Eneo hili linapakana kwa karibu na hifadhi ya Taifa ya Ruaha na lipo upande wa Mashariki.

Hifadhi ya Taifa ya Ruaha ina jumla ya kilomita za mraba 20,226 na ndio hifadhi kubwa kuliko zote nchini Tanzania na Afrika Mashariki.Hifadhi hii ni sehemu ya mfumo wa ikolojia wa Ruaha-Rungwa-Kizigo-Muhesi, ambao ina jumla ya a kilomita mraba 45,000 zinazolindwa. Hifadhi hii ina idadi kubwa ya Tembo na makazi ya Simba ambapo duniani inashika nafasi ya pili. Wanyama wengine wanaopatikana katika hifadhi hii ni pamoja na chui, duma, mbwa mwitu, kiboko, nyati, twiga, pundamilia, swala, pofu, nungunungu mkubwa, bweha, fisi, kongoni, kuro, ngiri, kudu mkubwa na mdogo (eneo pekee duniani ambapo wanapatikana pamoja), paa mkubwa, swala, mhanga, nguchiro na mbweha aliye na masikio. Safu za usangu ni miongoni mwa maeneo yaliyohifadhiwa na linatambulika kimataifa kwa kuwa na aina 570 za ndege ambazo zimerekodiwa ikiwa ni pamoja na mdiria, hondohondo, jua ndege na korongo. Hondohondo domo jekundu wa Ruaha ni moja kati aya ndege waliopo katika eneo hili na hawapatikani katika eneo lolote jingine duniani.

Hifadhi hii hupata mvua kati ya 500-800 mm kwa mwaka na joto lenye wastani wa nyuzi joto 28. Msimu wa kiangazi huwa kati ya mwezi wa sita (Juni) na wa kumi (Oktoba). Kuna mandhari za aina mbalimbali; kama vile Bonde la Ufa, ardhi nyevu, misitu, nyika, milima, chemichemi za maji ya moto na mabonde ya mbalimbali pembeni mwa Mto Ruaha Mkuu. Mwinuko wa hifadhi hii ni kati ya mita 750 hadi 1,900 kutoka uswa wa bahari. Vile viel ni hifadhi inayotambulika kwa kuwa na uoto wa aina mbili za mimea mbayo ni uoto wa maua ya Zambezi na Sudani na kuna aina nyingine nyingi za mimea zipatazo 1650 ambazo zinatambulika kisayansi. Aina ya

misitu inayopatikana katika hifadhi hii ni pamoja na misitu ya Acacia, Miombo, na mibuyu ambayo hupatikana kwa wingi.

Vijiji wanachama wa jumuiya vinamchanganyiko wa makabila mbalimbali kama vile Wahehe, Wagogo, Wabena, Wakinga, Wamaasai, Wabarabaig, na Wasukuma ambapo chanzo chao cha mapato ni kilimo na ufugaji. Mazao ya chakula ni pamoja na mahindi, mtama, uwele na mchele. Katika maeneo haya, migogoro baina ya wanyama na binadamu inatokea hususani uharibifu wa mazao kutoka kwa tembo, nyani, nguruwe na kiboko na uvamizi katika mifugo unaofanywa na wanyama wanaokula nyama kama vile simba, fisi, chui , bweha, duma na mbwa mwitu. Baadhi ya changamoto kwa jumuiya hii ni pamoja na ujangili, mioto kichaa, ufugaji uliokithiri, ukataji miti na na kuenea kwa magonjwa kutoka kwa wanyamapori kwenda kwa mifugo na binadamu.

Historia ya Jumuiya na Muktadha

Page 5: MATUMIZI BORA YA MALIASILI IDODI NA PAWAGA (MBOMIPA); JUMUIYA YA … · 2018-06-12 · za wanyamapori na kupewa mamlaka na faida ya moja kwa moja kutoka kwa rasilimali hiyo, vinginevyo

5

Maeneo ya Usimamizi wa Wanyamapori Maeneo ya Jumuiya za uhifadhi wanyamapori

Mwishoni mwa miaka ya 1980 na mwanzoni mwa 1990, Tanzania ilikumbwa na tatizo la ujangili wa hali ya juu ambapo nusu ya tembo na faru weusi wote waliuwa na kusababisha mamlaka husika kujitathimi upya namna ya utendaji wao wa kazi. Kikosi Kazi cha Tathmini ya Sekta ya Wanyamapori, kilichoitishwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kushughulikia suala hilo, kilihitimisha kuwa, “Ni muhimu kwa mustakabali wa uhifadhi wa wanyamapori katika Tanzania kuhusisha jamii zinazoishi karibu na maeneo ya hifadhi za wanyamapori na kupewa mamlaka na faida ya moja kwa moja kutoka kwa rasilimali hiyo, vinginevyo juhudi hizi za uhifadhi zitakuwa zimegonga mwamba.” Kutokana na hali hiyo, mwaka 1998, serikali ya Tanzania ilirekebisha sera ya wanyamapori na kuruhusu ushiriki wa jamii katika kulinda na kuhifadhi wanyamapori. Sera hii iliruhusu wananchi wanaoishi pembezoni mwa maeneo yaliyohifadhiwa na kumiliki rasilimali za wanyamapori wanaopatikana katika maeneo yao kwa manufaa yao wenyewe.

Jukumu la usimamizi lilikabidhiwa kwa jumuiya za uhifadhi wa wanyamapori yaani Wildlife Management Areas (WMA). Dhumuni la kuanzishwa kwa jumuiya hizi ni (1) Serikali kukabidhi jukumu la kusimamia wanyamapori kwa wananchi ili waweze kupata faida kupitia shughuli za utalii wa picha na uwindaji (2) Kuboresha maisha ya wana jamii kutokana na faida zitakazokuwa zinapatikana kutokana na uhifadhi wa wanyamapori (3) Kupunguza shughuli zenye uharibifu wa mazingira na kufanya maeneo ya jumuiya kuwa yenye kuvutia (4) Kuongeza idadi ya wanyamapori na kufanya faida zinazopatikana kuwa endelevu kwa kizazi cha sasa na cha baadae Baadaye sheria ilianzisha mchakato kwa jamii kupata hadhi ya WMA, ikiwa ni pamoja na; malezi ya asasi ya kijamii na usajili kwenye Wizara ya Mambo ya Ndani na mpango mkakati wa WMA iliyopendekezwa; mipango ya matumizi ya ardhi ambazo zimefanyiwa utafiti na zimewekwa kwenye ramani na kusajiliwa; tathmini ya athari za mazingira; maandalizi ya

sheria za kusaidia mipango ya matumizi ya ardhi; mpango wa eneo la usimamizi wa rasilimali; na maombi ya hadhi ya jumuiya yenye Mamlaka, haki ya mtumiaji wa rasilimali ya wanyamapori wa ndani ya WMA na uanzishwaji wa maeneo ya uwindaji (kama WMA inavyotaka).

Utawala

MBOMIPA ilitambuliwa kisheria kama jumuiya mwaka 2002, na kuwa hifadhi ya kwanza ya asili na jumuiya ya maendeleo kipekee nchini Tanzania. Vyombo halali vya jumuiya ni pamoja na katiba ya jumuiya na makala ya Chama. MBOMIPA inaongozwa na baraza kuu lenye wawakilishi 42 (wanachama 2 kutoka kila kijiji mwanachama). Baraza kuu huteua wanakamati wanne kusimamia kamati ya mipango na na fedha, nidhamu na utalii, Kupambana na ujangili na miundombinu. Wanachama kutoka kamati hizi huunda kamati tendaji, ambayo ina jukumu la kutekeleza shuguli za kila siku za jumuiya na kufanya maamuzi. Kamati tendaji inasimamiwa na mwenyekiti aliyechaguliwa, makamu mwenyekiti, katibu mtendaji na mtunza hazina. Akaunti za fedha za jumuiya zinakaguliwa na kampuni mbili tofauti, moja iliyolichaguliwa na jumuiya na nyingine iliyochaguliwa na Idara ya Wanyamapori ili kuhakikisha uwazi unakuwepo katika fedha za jumuiya.

Kama ilivyoainishwa kwenye katiba ya MBOMIPA, malengo ya jumuiya ni pamoja na;

Kuhifadhi na kutumia vizuri maliasili, hasa wanyamapori, misitu na samaki waliopo katika eneo la jumuiya;

Kutoa elimu kwa wananchi juu ya uhifadhi wa wanyamapori na masuala muhimu kama vile ugonjwa wa ukimwi (kusaidia jamii katika shughuli mbalimbali za maendeleo kama vile shule, hospitali, zahanati, maji na huduma nyingine muhimu;

Kuuza bidhaa zinazopatikana na kuzalishwa eneo la jumuiya.

Page 6: MATUMIZI BORA YA MALIASILI IDODI NA PAWAGA (MBOMIPA); JUMUIYA YA … · 2018-06-12 · za wanyamapori na kupewa mamlaka na faida ya moja kwa moja kutoka kwa rasilimali hiyo, vinginevyo

6

Shughuli Muhimu na Uvumbuzi

Uanzishwaji wa jumuiya ya hifadhi ya wanyamapori Idodi-Pawga

Vijiji wanachama vilitoa jumla ya hekari 777 kwa ajili ya uanzishwaji wa jumuiya kwa dhumuni la kujipatia kipato na kuboresha maisha ambapo upande wa kusini jumuiya hii inapakana na hifadhi ya Taifa ya Ruaha. Eneo hili la jumuiya ni muhimu sana kwani inapakana vile vile na mto ruaha mkuu ambao ndio chanzo muhimu cha maji kwa wanyama pori. Wanyama wanaopatikana katika hifadhi ya taifa ya Ruaha, vile vile wanapatikana katika katika eneo la jumuiya. Mito iliyo katika WMA ni makazi ya aina 38 ya samaki, fisi maji na ota wa kiafrika wasio na kucha. Reptilia pia wanapatikana ni kama vile mamba, kenge, chatu na mamba mweusi. WMA pia ina maeneo ya chemichemi za maji moto, maporomoko ya maji na mapango ambayo ni vivutio vya utalii.

Eneo jumuiya limegawanyika katika kanda kuu nne ambazo zimewekewa matumizi tofauti kama ifuatavyo;: utalii wa picha, utalii wa kawaida, uwindaji wa kitalii na uwindaji wa wakazi (uwindaji unaofanywa na Watanzania, mara nyingi wafanyabiashara kutoka maeneo yaliyo jirani na Iringa). Msimu wa kuwinda na masharti ya shuguli zilizokubaliwa katika kila eneo yametajwa na kuonyeshwa katika mpango wa matumizi na usimamizi wa eneo. Ufugaji nyuki, ukusanyaji endelevu wa mimea ya dawa na ibada za jadi na shughuli za kitamaduni kwa ujumla zimeruhusiwaa ndani ya kila eneo (pamoja na baadhi ya maeneo yanayofungwa katika msimu unaoingiliana na msimu wa uwindaji) kwa kufuata taratibu ambazo jumuiya imejiwekea. Mpango wa usimamizi wa eneo pia huanzisha maeneo maalum ya kilimo na mifugo katika eneo la ushoroba la WMA katika juhudi za kupunguza migogoro na wanyamapori.

Pamoja na hayo yote , jumuiya ina jumla ya askari jamii yaani Village Game Scouts (VGS) wa wanyamapori 37 ambao wanajukumu la kufanya doria na kuzuia wanyama waharibifu. Baadhi ya VGS wamepatiwa mafunzo ya uhifadhi wa wanyamapori na kupewa sare maalumu.

Page 7: MATUMIZI BORA YA MALIASILI IDODI NA PAWAGA (MBOMIPA); JUMUIYA YA … · 2018-06-12 · za wanyamapori na kupewa mamlaka na faida ya moja kwa moja kutoka kwa rasilimali hiyo, vinginevyo

7

Athari

ATHARI KWA VIUMBEHAIMBOMIPA hutumia njia kuu mbili kupunguaza ujangili, ambazo zinajumulisha mipango ya elimu ya mazingira na uhamasishaji kwa jamii na kutumia askari wa wanyamapori wa vijiji. Mikutano katika vijiji wanachama huhamasisha watu wazima kuhusu thamani ya wanyamapori na kuwaelimisha kanuni na sheria zinazosimamia WMA na hifadhi ya taifa ya Ruaha. Programu ya elimu ya mazingira katika shule za msingi za vijiji hufundisha vijana thamani ya uhifadhi katika umri mdogo. Pamoja na shuguli za kupambana na ujangili, maskauti wa vijiji wa wanyamapori pia hulenga katika kuzuia uvunaji haramu wa miti na asali ndani ya WMA.

Jumuiya hii inapakana na hifadhi kubwa na hivyo kutoa fursa ya kuwa na wanyama wengi ambao wanapatikana katika hifadhi ya taifa. Utumiaji makini wa mioto iliyodhibitiwa, uthibiti wa mioto mikali na usimamizi wa uoto wa asili umeimarisha makazi ya wanyamapori na mimea tofauti katika eneo la WMA. Doria zinazofanywa na VGS wa MBOMIPA na taarifa za msingi hukusanywa ili kuelewa mabadiliko katika idadi ya wanyamapori. Mpango wa matumizi ya ardhi wa vijiji wanachama umepunguza kwa kiasi migogoro baina ya wanadamu na wanyamapori ambao umetoa mfano wa mzuri wa jinsi ya kuunganisha ardhi ya jamii na ile ya jumuiya katika masuala ya kulinda viumbe hai.

Page 8: MATUMIZI BORA YA MALIASILI IDODI NA PAWAGA (MBOMIPA); JUMUIYA YA … · 2018-06-12 · za wanyamapori na kupewa mamlaka na faida ya moja kwa moja kutoka kwa rasilimali hiyo, vinginevyo

8

ATHARI ZA KIJAMII NA KIUCHUMIJumuiya hujipatia mapato kutokana na shughuli za uwindaji wa kitalii pamoja na utalii wa picha ambapo fedha hizo hutumika kwa ajili ya shughuli za maedeleo katika vijiji wanachama na zinazobaki hupelekwa katika shughuli zingine za jumuiya kama vile uboreshaji wa miundombinu.

Mapato na ajira

Uwindaji na utalii wa picha huwapatia wanavijjiji kazi za muda mfupi na wakati mwingine huuza bidhaa zao mbalimbali. Kati ya mwaka wa 2010 na 2012, Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani-USAID lilianzisha mpango wa kazi kwa pesa katika vijiji vya MBOMIPA ambao jumla ya wakazi 100 walipata ajira ya muda mfupi. Mpango uliboresha kiwango cha miundombinu ya WMA i ikiwa ni pamoja na ujenzi wa barabara pamoja na kambi za askari Kijiji cha Tungamalenga,ndio lango kikuu la watalii. Wakati mwingine Jumuiya hutoa ajira za muda kwa akina mama na vijana. Uwepo wa shughuli za utalii katika eneo hili umeweza kusababisha kukua kwa baadhi ya biashara ambazo hufanywa na wananchi kama vile baa, vibanda vya mboga mboga na maduka ya sanaa. Wanavijiji wengine pia hupata kazi kwenye kampuni za watalii ndani ya hifadhi ya Ruaha. Baadhi ya hoteli na kambi za watalii ndani ya hifadhi ya Ruaha pia husaidia uchumi wa wenyeji kupitia ununuzi wa vifaa vya ujenzi kama nyasi za kuezekea na miti na mawe.

Maboresho ya miundombinu na ustawi wa jamii

Mapato yanayozalishwa kutokana na shughuli za uwindaji wa kitalli na ule wa picha kwenye eneo la jumuiya yanabadilika kila mwaka.,Baadhi ya mapato hukusanywa kutokana na faini mbalimbali ambazo watu hulipishwa na jumuiya pale inapotokea wamekiuka sheria na taratibu zilizowekwa. Mwanamke mmoja kutoka kijiji wanachama cha Mahuninga alijitokeza na kusema mapato yanayopatikana yanatumika zaidi katika shughuli za jumuiya kuliko zile za jamii. Wanajamii hujitafutia pesa zao wenyewe na kulipia chakula, mafuta ya taa, matibabu na na mahitaji mbalimbali ya shule kwa ajili ya watoto wao.

Vijiji vinatumia faida inayotokana na jumuiya katika ujenzi wa miundombinu Mfano shule ya sekondari Idodi ilijengwa na kusababisha idadi kubwa ya watoto kujiunga na elimu ya sekondari. Katika kipindi cha mwaka 2008 na 2011, MBOMIPA Ilikuwa na uwezo wa wa kutoa ufadhili kwa watoto yatima 42 kutoka kwenye vijiji wanachama. Uboreshaji wa miundombinu ya barabara katika vijiji husika kumeasaidia wakulima kupeleka bidhaa zao sokoni. Baadhi ya faida ni pamoja na kupata huduma ya maji bomba pamoja na visima. Pia faida hiyo imetumika katika kufadhili zahanati na kujenga

kituo cha afya Kimande. Kituo cha afya kimeongeza upatikanaji wa huduma za afya na kusababisha upungufu wa vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga.

Kubadilisha mitazamo na mazoea

Utoaji wa ajira za muda mfupi na kupatikana kwa faida kutokana na shughuli za utalii kumesababisha kubadilika kwa mitazamo ya jamii katika eneo hili kuhusu uhifadhi wanyamapori. Kwa mujibu wa maafisa wa MBOMIPA, wanakijiji sasa wanazungumza kuhusu “haki za wanyampori” dhana iliyokuwa ya kigeni hapo awali. Katika mwaka wa 2014, mradi wa Strengthening the Protected Area Network in Southern Tanzania (SPANEST, Kuimarisha Mtandao wa maeneotengefu Kusini mwa Tanzania) ulizindua mashindano ya soka, yaliyoitwa Kombe la SPANEST, katika vijiji vya MBOMIPA kama njia ya kuongeza uelewa wa mambo ya ujangili kwa vijana. Mashindano ni sehemu ya mpango mpana unaoshugulikia uhalifu wa wanyamapori ikiwa ni pamoja na mikutano, warsha, programu za vyombo vya habari vya mahali hapo na machapisho mbalimbali, na hutoa fursa kwa vijana na jamii kushiriki maoni yao kuhusu jinsi ya kukabiliana na ujangili. Zaidi ya vijana 250 walishindana katika kombe la SPANEST na timu nane ambazo zilifika robo fainali zilipewa jezi zilizoonyesha kauli ya mbiu ya kampeni, “Acha ujangili dhidi ya tembo, linda tembo, cheza soka.”

Aidha wanavijiji wamebadilisha mazoea yao ya usimamizi wa ardhi katika juhudi za kuepuka migogoro ya binadamu na wanyamapori. Kwa mfano, wanavijiji wameanza kupanda pilipili na kutumia uzio ulio na mafuta ya pilipili kulinda mashamba kutokana na uvamizi wa wanyamapori. Wanavijiji pia wanapanda mimea ambayo haivutii wanyamapori lakini bado wanazalisha mazao yanayoweza kuuzwa na kuwa na usalama wa chakula.

JINSIAKatiba ya MBOMIPA huonyesha umuhimu wa kuwahusisha wanawake kwenye uongozi na nafasi za kufanya maamuzi katika jumuiya. Kwa sasa, wanawake watatu wanatumikia kama viongozi wa kamati tendaji, na wanawake wanashikilia nafasi katika kamati zote nne tendaji za jumuiya. Wanawake pia wamekuwa na nafasi za uenyekiti na maafisa watendaji wa wa baadhi ya vijiji wananchama. Kwa mujibu wa mwanamke kutoka kijiji cha Mahuninga, anasema uundaji wa WMA umekuwa wa manufaa kwa wanawake. “Hapo awali, wanaume waliwinda, wakauza nyama na kuweka pesa katika mifuko yao,” alisema. “Sasa tunapata pesa kutokana na mauzo ya uwindaji wa kitalii na kila mtu ananufaika, ikiwa ni pamoja na wanawake na watoto. Kwasababu ushuru wa kijiji umeshuka, tuna elimu bora, shule ya sekondari, barabara na zahanati bora zaidi.” Utalii

“Mara tu jamii zinapowezeshwa zinaweza kufaidika kutokana na maliasili katika maeneo yao. Uwezeshaji huhakikisha matumizi endelevu ya maliasili hii kwa faida ya vizazi vya sasa na

vizazi vijavyo.” Josephat Kisanyage, Katibu wa MBOMIPA WMA

Page 9: MATUMIZI BORA YA MALIASILI IDODI NA PAWAGA (MBOMIPA); JUMUIYA YA … · 2018-06-12 · za wanyamapori na kupewa mamlaka na faida ya moja kwa moja kutoka kwa rasilimali hiyo, vinginevyo

9

wa mazingira umewapa wanawake wa MBOMIPA fursa kubwa zaidi za kuzalisha mapato, hasa katika uzalishaji wa kazi za mikono. Uwezo wa wanawake kuzalisha mapato yao wenyewe unawapa uwezo kwani unaongeza kujiamini, kujitegemea, ujuzi na hadhi ya kijamii.

ATHARI ZA KISERAJumuiya hii iliundwa kutokana na Mradi wa Usimamizi wa Mazingira ya Wanyamapori na kufadhiliwa na United Kingdom’s Department

for International Development (DFID) kutoka mwaka wa 1992 hadi 1996. Mojawapo ya malengo ya mradi huu yalikuwa utekelezaji wa shughuli za jumuiya kwa ufanisi wa sera mpya ya wanyamapori. Lengo hili lilitimizwa katika miaka miwili:Idara ya Wanyamapori Tanzania ilitumia MBOMIPA kama jumuiya ya mfano na kuwatia moyo kwa kuwashilikisha katika katika warsha, na hatimaye kuitimiza malengo ya sera ya mwaka 1998 ya wanyamapori .

“Usimamizi endelevu wa ardhi ni muhimu kwa kudumisha hali nzuri ya hewa kwa maisha ya binadamu na maendeleo na kuhakikisha upatikanaji wa mahitaji muhimu ya binadamu kama

vile hewa, chakula, makazi, maji nk.” Josephat Kisanyage, Katibu wa MBOMIPA WMA

Page 10: MATUMIZI BORA YA MALIASILI IDODI NA PAWAGA (MBOMIPA); JUMUIYA YA … · 2018-06-12 · za wanyamapori na kupewa mamlaka na faida ya moja kwa moja kutoka kwa rasilimali hiyo, vinginevyo

10

UENDELEZAJIMBOMIPA ni WMA inayotambulika kisheria na inayofanya kazi kwa ushirkiano na Idara ya Wanyamapori na Hifadhi za Taifa chini ya uongozi ulioelezwa katika Sera ya Wanyamapori ya Tanzania. Mfumo wa kisheria hutoa muongozo wa kukua na kuendelea kwa jumuiya Ushirikiano baina ya MBOMIPA na serikali za mtaa na mashirika yasiyo ya kiserikali umeimarisha uwezo wake wa kujiendeleza. Hata hivyo, uwekaji saini wa mikataba ya muda mrefu kati ya MBOMIPA na sekta binafsi, hasa kampuni za uwindaji na utalii wa picha, unaweza kuimarisha kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa pesa za jumuiya. Utafiti wa kuongeza kipato kutokana na utalii wa kitamaduni unahitajika zaidi ili kuona ufanisi wake. Vivile viongozi wa jumuiya kujengewa uwezo juu ya maswala ya utawala, fedha na usimamizi wa jumuiya unahitaji zaidi ili kuifanya WMA izidi kukua.

UTOAJI NAKALAMaeneo tengefu ni muhimu katika uhifadhi wa wanyamapori na mazingira yake, lakini kuna mipaka ya uwezo wao wa kusaidia kikamilifu uhifadhi mazingira. Kuna ongezeko la uelewa ambapo jamii wanaweza kuwa mawakili katika kulinda rasilimali za asili katika maeneo haya. Maeneo ya usimamizi wa Wanyamapori hutoa mfano wa usimamizi wa maliasili yanayozunguka jamii ambao unaweza kuigwa duniani kote. MBOMIPA imekuwa mwenyeji wa mashirika yasiyo ya serikali kadhaa ambayo yameonyesha nia ya kuanzisha maeneo ya usimamizi wa wanyamapori katika Tanzania na mbali zaidi Afrika mashariki. Katika mashirika ya Uhifadhi wa Wanyamapori yamesaidia sana uanzishwaji wa maeneo mawili mapya ya usimamizi wa wanyamapori (WAGA na UMEMARUWA) katika kanda muhimu za wanyamapori kusini na mashariki mwa Hifadhi ya Ruaha.

WABIADFID ilitoa ufadhili muhimu na usaidizi wa kiufundi kwa MBOMIPA katika miaka ya mwanzo ya maendeleo yake (1992-2003). Msaada wa baadaye kwa maendeleo ya kitaasisi ya MBOMIPA ulitolewa na World Wildlife Fund - WWF (Mfuko wa Dunia wa Wanyamapori na kutekelezwa kupitia Shirika la Uhifadhi wa Wanyamapori yaani Wildlife Conservation Society (WCS), Shirika hili limetoa ushauri na utaalamu wa kiufundi kwa MBOMIPA katika mambo mengi kama vile kupanga matumizi shirikishi ya ardhi, mpango usimamizi wa rasilimali. Wafanyakazi wa WCS wametumika kama wapatanishi kati ya MBOMIPA na wawekezaji na kusuluhisha migogoro ndani ya MBOMIPA (kwa mfano, migogoro kati ya wakulima na wafugaji). Shirika la msaada la kimarekani la USAID ilifadhili mpango wa kazi kwa pesa ili kuboresha miundombinu ndani ya WMA na kuendelea kutoa usaidizi wa kifedha kwa MBOMIPA. Shirika lisilo la kiserikali la Kitanzania la Marafiki wa Ruaha (Friends of Ruaha), lilianzisha mpango wa elimu ya mazingira katika shule za msingi kwenye vijiji wanachama. Wabia wa MBOMIPA ni pamoja na Wizara ya Maliasili

Uendelezaji na Utoaji nakala

admin
Highlight
Page 11: MATUMIZI BORA YA MALIASILI IDODI NA PAWAGA (MBOMIPA); JUMUIYA YA … · 2018-06-12 · za wanyamapori na kupewa mamlaka na faida ya moja kwa moja kutoka kwa rasilimali hiyo, vinginevyo

1111

na Utalii, Idara ya Wanyamapori na Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA). Washirika wengine ni pamoja na serikali kuu na serikali za mtaa kama vile mkoa wa Iringa, Ofisi ya maji Bonde Rujifi ambao walihuisha usajili wa kisheria wa jumuiya na kuwezesha utoaji wa vibali kwa matumizi ya rasilimali.

“Mafanikio kufanya kazi katika maeneo kame yanatokana na elimu na juhudi za kuimarisha uhamasishaji, utoaji wa faida za moja kwa moja kwa jamii na kutokana na kufanya kazi kwa

ushirikiano na jamii na mashirika mengine ya uhifadhi.” Josephat Kisanyage, Katibu wa MBOMIPA WMA

Page 12: MATUMIZI BORA YA MALIASILI IDODI NA PAWAGA (MBOMIPA); JUMUIYA YA … · 2018-06-12 · za wanyamapori na kupewa mamlaka na faida ya moja kwa moja kutoka kwa rasilimali hiyo, vinginevyo

REJEA ZAIDI ■ Tovuti ya eneo la Usimamizi wa Wanyamapori MBOMIPA. Inapatikana kwenye mtandao hapa.

■ Eneo lililopendekezwa la Usimamizi wa Wanyamapori la Pawaga-Idodi. Inapatikana kwenye mtandao hapa.

■ Tovuti ya Hifadhi za Taifa Tanzania Inapatikana kwenye mtandao hapa.

■ Walsh, M, MBOMIPA: Kutoka Mradi hadi jumuiya na Kutoka Uhifadhi hadi Kupunguza Umaskini. Ripoti ya mradi wa mwisho, 2003. Wizara ya Maliasili kitengo cha Utalii na Wanyamapori na Hifadhi za Taifa Tanzania. Inapatikana kwenye mtandao hapa.

■ Wizara ya Maliasili na Utalii ya Tanzania, ‘Sera ya Wanyamapori ya mwaka 1998. Inapatikana kwenye mtandao hapa.

Equator InitiativeSustainable Development ClusterUnited Nations Development Programme (UNDP)304 East 45th Street, 6th Floor New York, NY 10017Tel: +1 646 781-4023 www.equatorinitiative.org

UNDP hushiriki na watu katika ngazi zote za jamii kusaidia kujenga mataifa yanayoweza kuhimili migogoro, na kuendesha na kuendeleza ukuaji unaoboresha maisha kwa kila mtu. Kwa uhalisi zaidi ya nchi na maeneo 170, tunatoa mtazamo wa kimataifa na ufahamu wa ndani ili kusaidia kuwezesha maisha na kujenga mataifa thabiti.

Uanzishwaji wa Ikweta unaleta pamoja Umoja wa Mataifa, Serikali, asasi za kiraia, biashara na mashirika ya kiraia kutambua na kuendeleza suluhisho za ndani za maendeleo endelevu, asili na jamii thabiti.

©2016 Equator Initiative Haki zote zimehifadhiwa

WABIA WA MRADI

WABIA WA UANZISHWAJI WA IKWETA

Empowered lives. Resilient nations.

Empowered lives. Resilient nations.