KUITANGAZA - Decade of Pentecost · 2012. 12. 4. · 47. Agizo Kuu Na Ubatizo Kwa Roho Mtakatifu...

242

Transcript of KUITANGAZA - Decade of Pentecost · 2012. 12. 4. · 47. Agizo Kuu Na Ubatizo Kwa Roho Mtakatifu...

  • KUITANGAZA PENTEKOSTE

    MIHUTASARI 100

    YA MAHUBIRI KUHUSU NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU

    MARK R. TURNEY

    MHARIRI

    DENZIL R. MILLER

    MHARIRI MWENZA

    Chapisho La Miaka Kumi Ya Pentekoste

  • Kuitangaza Pentekoste: Mihutasari 100 Ya Maubiri Kuhusu Nguvu Za Roho Mtakatifu. © 2012, AIA Publications. Haki Zote Zimehifadhiwa. Hairuhusiwi sehemu yoyote ya kitabu hiki kunakiliwa, kutunzwa katika mfumo wa uhifadhi, wala kutumwa kwa namna yoyote au kwa njia yoyote – kielektroniki, kikawaida, kwa kurudufu, kwa kurekodi au vinginevyo – pasipo kibali kwanza kutolewa na msimamizi wa haki miliki kwa njia ya maandishi. Ila, nakili fupi fupi zinaruhusiwa kutumiwa kwa ajili ya marejeo katika majarida au magazeti. Maandiko yote yatumikayo katika kitabu hiki yanatoka katika BIBLIA – MAANDIKO MATAKATIFU. Toleo la Kiswahili la UNION VERSION. © 1952, BFBS, © 1997, BST, BSK (Vyama Vya Biblia Tanzania na Kenya). Wakati mwingine mfasiri atafanya tafsiri ya moja kwa moja kwa lugha rahisi ili kusaidia kifungu kueleweka vizuri zaidi, na hiyo itaonyeshwa kwa herufi hizi: TLR (yaani, Tafsiri Ya Lugha Rahisi). Translated from English into Swahili by Simon Joel Vomo Kimetafsiriwa kwa Kiswahili na Simon Joel Vomo yoka Kiingereza Library of Congress Cataloging-in-Publication Data Turney, Mark R., 1968– Miller, Denzil R., 1946– Translated from Proclaiming Pentecost: 100 Sermon Outlines on the Power of the Holy Spirit / Mark R. Turney / Denzil R. Miller ISBN: 000-0-0000-0000-0 1. Bible. 2. Practical Theology: Homiletics. 4. Pentecostal. 5. Holy Spirit. 6. Missions Printed in the United States of America AIA Publications, Springfield, MO, USA 2011 A Decade of Pentecost Publication Websites: www.DecadeofPentecost.org www.ActsinAfrica.org

  • Yaliyomo

    Yaliyomo 3

    Orodha Ya Walioandika Mahubiri 7

    Fahirisi 10

    Utangulizi 12

    Sehemu Ya 1: Ubatizo Katika Roho Mtakatifu 15 1. Ahadi Ya Yesu Katika Matendo 1:8 16

    2. Ubatizo Katika Roho Mtakatifu 18

    3. Ubatizo Katika Roho Mtakatifu Ndiyo Hitaji Letu 20

    4. Mfululizo Kuhusu Ubatizo Katika Roho Mtakatifu 22

    5. Mfululizo Kuhusu Ubatizo Katika Roho Mtakatifu 24

    6. Mfululizo Kuhusu Ubatizo Katika Roho Mtakatifu 26

    7. Mfululizo Kuhusu Ubatizo Katika Roho Mtakatifu 28

    8. Mfariji Amekuja 30

    9. Maswali Ya Kawaida Kuhusu Ubatizo Katika Roho

    Mtakatifu 32

    10. Ile Siku Ya Pentekoste 34

    11. Je, Ulimpokea Roho Ulipoamini? 36

    12. Usiondoke Nyumbani Bila Hii 38

    13. Chochea Karama Ya Mungu 40

    14. Je, Tangu Ulipoamini, Umepokea? 42

    15. Roho Mtakatifu Huwezesha 44

    16. Maagizo Binafsi Ya Yesu Kuhusu Kumpokea Roho 46

    17. Yesu, Abatizaye Kwa Roho Mtakatifu 47

    18. Yesu: Mwokozi Na Abatizaye 48

    19. Yesu Atakujaza Na Roho Mtakatifu Ili Uweze Kushuhudia 50

    20. Maji Yaliyo Hai 52

    21. Kitu Muhimu Zaidi Katika Kanisa Leo 54

    22. Mungu Wetu Mkarimu 56

    23. Nguvu Za Ahadi 58

  • 24. Maombi Yenye Kumfanya Roho Ashuke 60

    25. Ahadi Imetimizwa 62

    26. Ahadi Ya Pentekoste 64

    27. Ahadi Ya Roho Mtakatifu 66

    28. Kusudi La Pentekoste 68

    29. Mpokee Roho Mtakatifu 70

    30. Kupokea Ukamilifu Wa Roho 72

    31. Roho Juu Ya Wote Wenye Mwili 74

    32. Mito Ya Maji Yaliyo Hai 76

    33. Mara Kutoka Mbinguni 78

    34. Nyakati Za Kuburudisha Kutoka Katika Uwepo Wa Bwana 80

    35. Kujazwa Mara Mbili Kwa Pentekoste 82

    36. Nini Maana Ya Kujazwa Na Roho Mtakatifu? 84

    37. Unaweza Kupata Ubatizo Wa Kweli Wa Roho Mtakatifu 86

    Sehemu Ya 2: Utume Unaowezeshwa Na Roho Na Huduma 89 38. Kuendeleza Ufalme Wa Mungu 90

    39. Watu Wote Wa Mungu Ni Manabii 92

    40. Upako Unaovunja Nira 94

    41. Watumishi Bora Wa Roho 96

    42. Dunamis Na Martus 98

    43. Kuwezeshwa Kwa Ajili Ya Siku Za Mwisho 100

    44. Uwezesho Wa Roho Na Agizo Kuu 102

    45. Mungu Amewachagua Walio Wanyonge 104

    46. Mungu Wa Hali Zote 106

    47. Agizo Kuu Na Ubatizo Kwa Roho Mtakatifu 108

    48. Kazi Kubwa Kuliko Hizi 110

    49. Roho Mtakatifu Na Kuleta Watu Kwa Yesu 112

    50. Roho Mtakatifu Na Huduma Ya Kanisa 114

    51. Ramani Ya Yesu Ya Kujenga Kanisa La Kipentekoste 116

    52. Maneno Ya Mwisho Ya Yesu Ambayo Si Maarufu Sana 118

    53. Masomo Kutoka Matendo 2 120

  • 54. Watu Wakihubiri Kote Kote 122

    55. Kusudi La Kimishenari La Pentekoste 124

    56. Kuhamasisha Makanisa Yenye Kuwezeshwa Na Roho 126

    57. Si Kwa Nguvu, Wala Uwezo, Bali Kwa Roho Wangu 128

    58. Pentekoste Na Kushuhudia Ulimwengu 130

    59. Nguvu Ya Pentekoste 132

    60. Nguvu Yenye Kusudi 134

    61. Shauku Ya Roho Kwa Ajili Ya Mataifa 136

    62. Hatupaswi Kusahau 138

    63. Nilicho Nacho Ninakupa 140

    64. Kushuhudia Katika Roho 142

    65. Ni Lazima Tudumishe Mtazamo Wa Kimishenari 144

    66. Sababu Ya Roho Mtakatifu Kuja 146

    67. Binti Zenu Watatabiri 148

    Sehemu Ya 3: Maisha Katika Roho 151 68. Sababu Nane Za Kuomba Kwa Lugha 152

    69. Moto, Upepo, Na Hua (Njiwa) 154

    70. Kumjua Kiongozi Wetu 156

    71. Zawadi Ya Lugha 158

    72. Msaidizi Wetu 160

    73. Kuenenda Katika Roho 162

    74. Maisha Katika Roho 164

    75. Kuishi Kwa Msukumo 166

    76. Kwa Kuwa Sasa Umejazwa Na Roho 168

    77. Kuitii Sauti Ya Roho 170

    78. Matokeo Ya Upentekoste Halisi 172

    79. Kunena Kwa Lugha Na Ubatizo Wa Roho Mtakatifu 174

    80. Maana Ya Kunena Kwa Lugha 176

    Sehemu Ya 4: Umuhimu Wa Pentekoste 179 81. Kanisa La Matendo 1:8 180

    82. Kipaumbele Cha Kristo Kwa Ajili Ya Kanisa 182

  • 83. Usitupe Mtoto Pamoja Na Maji Uliyomwogeshea 184

    84. Jibu la Mungu Huja Kwa Moto 186

    85. Ni Dunia Ya Mambo Yasiyokuwa Ya Kawaida 188

    86. Wanahitajika Watu Wanaowezeshwa Na Roho 190

    87. Shauku Na Nguvu: Zawadi Ya Roho Kwa Kanisa 192

    88. Ukuu Wa Pentekoste 194

    89. Kwa Nini Kumpokea Roho Mtakatifu? 196

    90. Kuimarisha Urithi Wetu Wa KiPentekoste 198

    Sehemu Ya 5: Masomo Ya Kongamano 201 91. Roho Mtakatifu Na Utume Wa Mungu 202

    92. Ubatizo Wa Roho Unarejewa 204

    93. Maana Ya Kuwa Mpentekoste 206

    94. Pentekoste Na Kizazi Kijacho 208

    95. Wanawake Na Uamsho Wa Kipentekoste 210

    96. Shule Ya Biblia Ya Kipentekoste 212

    97. Jinsi Ya Kuhubiri Juu Ya Ubatizo Wa Roho Mtakatifu 214

    98. Kuomba Na Waaminio Wampokee Roho 216

    99. Kupanda Makanisa Ya Kiroho Ya Umisheni 218

    100. Kuongoza Kanisa La Mahali Katika Uamsho Wa

    Kipentekoste 220

    Orodha Ya Maandiko Yaliyotumiwa Katika Mahubiri 222

  • 7

    Orodha Ya Walioandika Mahubiri BN Mch. Brett Nelson, Mishenari wa Assemblies of God World

    Missions Marekani katika Afrika. (Mahubiri Namba 77) CO Mch. Dkt Charles O. Osueke, Askofu Mkuu, Assemblies of

    God ya Nigeria, 1988-2010. (Mahubiri Namba 50) DC Doug Clay, Mtunza Hazina Mkuu, Assemblies of God ya

    Marekani. (Mahubiri Namba 36) DG Dean Galyen, Mishenari wa Assemblies of God World

    Missions Marekani katika Afrika. (Mahubiri Namba 51) DJ Darius Johnston, Mchungaji Kiongozi, Kanisa la Assemblies

    of God la Christ Church huko Ft. Worth Texas, Marekani. (Mahubiri Namba 70)

    DM David Mensah, Askofu Mkuu, Assemblies of God ya Benin.

    (Mahubiri Namba 25) DN Don Nordin, Mchungaji Kiongozi, Kanisa la Assemblies of

    God la Christian Temple huko Houston, Texas; Makamu Askofu wa Jimbo la Texas Kusini, Assemblies of God ya Marekani. (Mahubiri Namba 78, 89)

    DRM Denzil R. Miller, Mkurugenzi wa Acts in Africa Initiative;

    Mishenari wa Assemblies of God World Missions Marekani katika Afrika. (Mahubiri Namba 1, 2, 4-7, 16, 18, 21, 24, 29, 30, 32-35, 39, 41, 43-45, 47, 52-55, 60, 62-64, 67, 68, 73, 76, 88, 91, 93, 97-99)

    DT Don Tucker, Mkurugenzi wa Africa AG Care; Mishenari wa

    Assemblies of God World Missions Marekani katika Afrika. (Mahubiri Namba 42)

    DWC D. Wendell Cover, Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Word of

    Life International la Assemblies of God huko Springfield, Virginia, Marekani. (Mahubiri Namba 79)

    DWM Dennis W. Marquardt, Askofu wa Jimbo la New England

    Kaskazini, Assemblies of God ya Marekani. (Mahubiri Namba 15)

  • 8

    EC Edward Chitsonga, Katibu Mkuu wa Malawi Assemblies of God; Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Glorious Temple Assemblies of God, Lilongwe, Malawi. (Mahubiri Namba 49)

    EJ Elwyn Johnston, Mchungaji Kiongozi, Kanisa la Bethel

    Assembly of God la Temple, Texas, Marekani. (Mahubiri Namba 72)

    EL Enson Lwesya, Mkurugenzi wa All Nations Theological

    Seminary, Malawi; Mkurugenzi wa Kamisheni ya Umisheni Duniani ya Muungano wa Assemblies of God Afrika (AAGA World Missions Commission); Mwanatimu, Acts in Africa Initiative. (Mahubiri Namba 22, 46)

    FK Fredrick Kyereko, Mkuu wa Chuo cha Biblia cha Ghana

    Kusini cha Assemblies of God. (Mahubiri Namba 80) GRC G. Raymond Carlson, Askofu Mkuu wa Assemblies

    of God Marekani, 1986-1993. (Mahubiri Namba 59) GW George O. Wood, Askofu Mkuu wa Assemblies of God

    Marekani. (Mahubiri Namba 71) JE John Easter, Makamu wa Rais Mtendaji wa Pan-Africa

    Theological Seminary; Mwanatimu, Acts in Africa Initiative; Mishenari wa Assemblies of God World Missions Marekani katika Afrika. (Mahubiri Namba 61, 87, 96)

    JI John Ikoni, Katibu Mkuu wa Assemblies of God, Nigeria;

    Rais wa Pan-Africa Theological Seminary huko Lome, Togo. (Mahubiri Namba 3, 26, 40, 90)

    JK Jimmy Kuoh, Askofu Mkuu wa Assemblies of God, Liberia. (Mahubiri Namba 81) JL John Lindell, Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Assemblies

    of God James River, Springfield, MO, Marekani. (Mahubiri Namba 10)

    JWL Jimmie W. Lemons, Mwanatimu, Acts in Africa Initiative;

    Mishenari wa Assemblies of God World Missions huko Cameroon, Afrika. (Mahubiri Namba 17, 37)

    JP Jeff Peterson, Mchungaji Kiongozi, Kanisa la Central

    Assembly of God, Springfield, MO, Marekani. (Mahubiri Namba 83, 85)

  • 9

    KB Ken Benintendi, Mishenari wa Assemblies of God World

    Missions Marekani katika Asia Pacific. (Mahubiri Namba 8, 9)

    KK Ken Krucker, Mkurugenzi, Africa Financial Empowerment;

    Mwanatimu, Acts in Africa Initiative; Mishenari, Assemblies of God World Missions Marekani katika Afrika. (Mahubiri Namba 14, 23)

    LB Leroy Bartel, Msimamizi, Chuo cha Biblia na Huduma za

    Kanisa katika Southwestern Assemblies of God University. (Mahubiri Namba 75)

    LC Lazarus Chakwera, Askofu Mkuu wa Malawi Assemblies of

    God; Mwenyekiti, Muungano wa Assemblies of God katika Afrika (Africa Assemblies of God Alliance). (Mahubiri Namba 56, 65)

    MH Melvin Hodges, Mkurugenzi Kanda wa AGWM Marekani na

    Marekani ya Latin, 1954-1973. (Mahubiri Namba 31, 58, 66) MS Mel Surface, Mwenyekiti, Kitengo cha Huduma Kwa Watu

    Wazima katika Jimbo la Texas Kaskazini la Assemblies of God, Marekani. (Mahubiri Namba 27)

    MT Mark Turney, Mkurugenzi Mwenza wa Acts in Africa Initiative; Mishenari wa Assemblies of God World Missions Marekani katika Afrika. (Mahubiri Namba 11, 12, 13, 19, 20, 38, 48, 57, 82, 86, 92, 94, 100)

    NB Lindsay Blackburn, Askofu Mkuu wa Assemblies of God huko Mauritius. (Mahubiri Namba 69)

    NO Neubueze O. Oti., Mchungaji wa Assemblies of God,

    Nigeria. (Mahubiri Namba 3, 26) SE Scott Ennis, Mishenari wa Assemblies of God World

    Missions Marekani katika Afrika. (Mahubiri Namba 74) SM Sandy Miller, Mtumishi wa Acts in Africa Initiative; Mishenari

    wa Assemblies of God World Missions Marekani katika Afrika. (Mahubiri Namba 95)

    SOA Sebastian Obiang Abeso, Askofu Mkuu wa Assemblies of God huko Equatorial Guinea. (Mahubiri Namba 84)

    WC William Caldwell, Mwana-uamsho wa KiPentekoste.

    (Mahubiri Namba 28)

  • 10

    Dibaji

    Katika miaka kumi ya mwisho ya karne ya ishirini, Assemblies of God ya Afrika ilishiriki katika mkazo wa bara zima uliopewa jina la “Miaka Kumi Ya Mavuno”. Katika miaka kumi hiyo ya hali ya juu sana, na ile iliyofuata, ushirika wetu ulipata baraka kubwa na ukuaji wa hali ya juu sana. Idadi ya washirika katika makanisa yetu iliongezeka toka watu kama milioni 2 hadi zaidi ya milioni 16. Idadi ya makanisa ya mahali pamoja iliongezeka toka makanisa kama elfu 12 hadi makanisa elfu 65. Kweli tunamshukuru Mungu kwa baraka Zake za neema kubwa katika ushirika wetu. Hata hivyo, sisi kama ushirika wa makanisa shirika ya Assemblies of God Afrika hatukuamua kubakia katika siku zilizopita. Badala yake tuliamua kutazama mbele na baadaye kwa matarajio makubwa. Basi, mwezi Machi 2009, tarehe 3 hadi 6, Mkutano Mkuu wa Umoja wa Assemblies of God wa Afrika (AAGA) ulipitisha bila kupingwa azimio la kujitolea kwa pamoja na kila kanisa la nchi kuingia katika mkazo mwingine wa hali ya juu zaidi wa kimishenari. Huu mkazo tunauita “Miaka Kumi Ya Pentekoste” (2010 hadi 2020). Hii Miaka Kumi Ya Pentekoste inaonekana itakuwa kati ya miaka yenye kusisimua na matunda mengi sana katika historia ya kanisa la Afrika inayokaribia kuwa miaka mia moja.

    Katika kuitikia azimio hili, makanisa ya Assemblies of God katika bara zima yanajipanga na kuingia katika uinjilisti kwa uzito, upandaji wa makanisa, na mipenyo ya kimisheni. AAGA imeweka lengo la kuona waamini wapya milioni kumi wakiwa wamebatizwa kwa Roho Mtakatifu na kuhamasishwa kama washuhudiaji waliowezeshwa na Roho, wapanda makanisa, na wamishenari katika kipindi hicho cha miaka kumi. Malengo mengine ni pamoja na yafuatayo,

    Kuwahamasisha waombaji laki moja (100,000) watakao-omba kila siku kwa ajili ya umwagiko wa KiPentekoste juu ya makanisa yetu.

    Kupanda makumi elfu ya makanisa mapya katika Afrika na katika Bonde la Bahari Ya Hindi.

    Kutuma mamia ya wamishenari wa KiAfrika, wanaowezeshwa na Roho.

  • 11

    Kuingia katika juhudi za kufikia makundi zaidi ya 900 ya watu ambao hawajafikiwa katika Afrika.

    Ili hayo yatokee, ni lazima tuwe na umwagiko wa kweli wa KiPentekoste juu ya makanisa yetu, ambao unalenga kwenye kuwezeshwa na Roho ili tufanikishe na kutimiza utume wa Mungu (mission Dei) na kutimiza Agizo Kuu la Kristo. Basi, ni lazima tutangaze kwa ujasiri ujumbe wa Pentekoste na kwa mwamko mkubwa tuwaongoze watu wetu kuingia katika ubatizo wa Roho Mtakatifu. Na inabidi tufanye hivyo kila nafasi tunayopata. Hapo ndipo tutakapokuwa tayari kushughulika na mataifa kwa kuwapelekea Injili.

    Zaidi ya hayo, katika Miaka Kumi Ya Pentekoste, uongozi wa AAGA unamwomba kila mchungaji katika Afrika ahubiri ujumbe wa kitume kila Siku ya Pentekoste, wenye kutilia mkazo ubatizo katika Roho Mtakatifu. (Siku ya Pentekoste kila mwaka inaadhimishwa Jumapili ya saba baada ya Pasaka.) Vile vile tunawaomba wachungaji kuwaita watu wao kufika mbele na kuomba nao ili watiwe nguvu za Roho kwa ajili ya kuwashirikisha watu waliopotea Injili. Kitabu hiki kinaweza kuwa kama chanzo kizuri kwa ajili ya hayo, na ibada nyingine kama hizo, zenye mkazo wa Roho Mtakatifu.

    Basi, kwa moyo wangu wote ninapendekeza chapisho hili jipya la Miaka Kumi ya Pentekoste liitwalo Kuitangaza Pentekoste: Mihutasari 100 Ya Mahubiri Kuhusu Nguvu Za Roho Mtakatifu. Kimetolewa ili kuwasaidia wachungaji, waalimu, wainjilisti, wamishenari, na wahubiri wa kawaida barani Afrika na duniani kote, ili wahubiri na kufundisha kwa ufanisi zaidi ujumbe wa nguvu za Roho. Ninaamini kwamba utakitumia kitabu hiki mara nyingi, na kwamba utahubiri mara nyingi juu ya mada husika na kuwaombea waaminio wampokee Roho Mtakatifu.

    —Ni Mimi,

    Lazarus Chakwera Mwenyekiti

    Africa Assemblies of God Alliance

  • 12

    Utangulizi

    Ukuaji wa kushangaza sana wa Assemblies of God katika bara la Afrika katika kipindi cha miaka ishirini iliyopita ni ushuhuda wenye nguvu sana kwamba Mungu yuko kazini katika bara hili. Ongezeko ni kutoka kiasi cha watu milioni 2 hadi zaidi ya milioni 16. Pamoja na kwamba tunashangilia kwa sababu ya ukuaji huu mkubwa, tunaamini kwamba huo ni mwanzo tu wa kile ambacho Mungu anakikusudia kufanya ndani ya kanisa la KiAfrika, na kwa kupitia katika kanisa la KiAfrika.

    Bila shaka yoyote, ni mapenzi ya Mungu kwamba kanisa la Afrika liwe kanisa lenye nguvu sana katika eneo la utume. Lakini, ili hayo yatokee, lazima kanisa la Afrika liwezeshwe na Roho Mtakatifu, sawa tu na ilivyokuwa kwa kanisa la kwanza (Matendo 1:8). Kanisa la namna hiyo halitatiwa nguvu kufikia mamia ya makabila ya watu ambao hawajafikiwa tu, na mamilioni ya watu ambao hawajaokoka walioko barani humu, bali pia litawezeshwa kwenda kwa mataifa yote na kuyafikishia Injili ya Kristo, yenye kubadilisha maisha.

    Mkusanyiko huu wa mihutasari ya mahubiri kuhusu nguvu za Roho Mtakatifu umeandaliwa ili kuwasaidia wanaume na wanawake wenye ari ya kuliona kanisa la Afrika likiwa kanisa la kitume, lililotiwa nguvu na kuwezeshwa na Roho Mtakatifu. Ikiwa kanisa la Afrika linataka kutimiza utume wa Mungu, ni lazima wachungaji, viongozi wa kanisa na wanafunzi wengine waliojitolea wahubiri na kufundisha kila mara juu ya ubatizo katika Roho Mtakatifu na kuwapa wasikilizaji wao nafasi ya kumpokea huyo Roho. Kama tutakuwa waaminifu kutangaza ujumbe wa Pentekoste, Mungu atakuwa mwaminifu kutimiza ahadi Yake ya kutoa “nguvu kutoka juu”.

    Mahubiri haya yanatoka kwa watumishi na wamishenari waliochaguliwa watokao Afrika na Marekani, wenye shauku na msukumo kuhusu hitaji kuu la kanisa la Afrika kupata nguvu za Pentekoste. Pamoja na kwamba ujumbe mkuu wa kila mahubiri ni nguvu ya Roho Mtakatifu, utagundua kwamba mahubiri yenyewe yanaelekea kwenye utume au umisheni. Ni kweli kwamba uwepo na nguvu za Roho Mtakatifu huleta baraka nyingi binafsi katika maisha yetu. Lakini, hatupaswi kusahau ukweli kwamba zawadi hiyo ilitolewa kwa kusudi maalum. Tunatafuta nguvu za Roho ili zituwezeshe kufanikisha utume wa Mungu.

  • 13

    Jinsi Ya Kutumia Kitabu Hiki

    Kila mahubiri kati ya hayo mia moja ambayo yanapatikana kitabuni humu kwa namna ya muhtasari yamehaririwa ili yatoshe kurasa mbili. Kwa kufanya hivyo, tumejitahidi kuhakikisha kwamba kuna maudhui ya kutosha katika kila muhtasari ili kumpa msomaji onyesho la wazi la mfumo na mtiririko wa ujumbe. Wakati huo huo, tumejaribu kufanya kwa kifupi kiasi iwezekanavyo ili wahubiri na waalimu wapate nafasi ya kutosha kupanua na kutengeneza mahubiri yenyewe kulingana na uhitaji maalum wa wasilizaji wao. Unapojifunza, na kuomba na kuhubiri kutoka katika mihutasari hii, tunaamini kwamba Roho Mtakatifu atakuvuvia kwa mawazo mapya kuhusu jinsi ya kupanua mahubiri yako mwenyewe juu ya nguvu za Roho Mtakatifu na Utume wa Mungu.

    Basi, ili tuweze kuhubiri kwa ufanisi kuhusu ubatizo katika Roho Mtakatifu, ni lazima tuwe na muda wa kutosha katika kujifunza na maombi, tukimruhusu Roho Mwenyewe aijaze mioyo yetu ujumbe husika. Tuna imani kwamba Roho atakusaidia kuhubiri mahubiri haya kwa ubora kuliko ilivyowahi kutokea huko nyuma – na kwa matokeo makubwa zaidi. Unapojifunza na kujiandaa kuhubiri juu ya nguvu za Roho Mtakatifu, tunakuhimiza utumie muda mwingi katika maombi ukimwuliza Mungu akujaze kwa nguvu sana Roho Wake, ili akuwezeshe kulitangaza Neno Lake.

    Hiki kitabu kimegawanywa katika sehemu kuu tano. Zile nne za kwanza zimepangwa kwa kufuatana na mada, na ile ya mwisho ina mahubiri kama yalivyotolewa katika makongamano ya Matendo 1:8 yanayoendeshwa na timu ya Acts In Africa barani kote. Waweza kupenda kutumia hiyo sehemu ya mwisho kuendesha Kongamano lako binafsi la Matendo 1:8 ili kuhamasisha kanisa lako au kundi la makanisa, kuhusiana na utume unaowezeshwa na Roho Mtakatifu.

    Wachangiaji

    Mwishoni mwa kila muhtasari utakutana na herufi za jina la mwenye kuandaa mahubiri hayo, yakiwa yamewekwa kwenye mabano. Ukipenda, waweza kupata habari zaidi juu ya mhusika katika orodha ya Waandishi ipatikanayo ukurasa wa saba. Mwisho:

  • 14

    Napenda kumshukuru kila mchangiaji katika hao 36 kwa kusaidia kuhakikisha kwamba ujumbe wa Pentekoste utaendelea kutangazwa katika Afrika nzima na hata zaidi ya Afrika, mpaka Yesu atakaporudi tena.

    Ni Mimi, Mark R. Turney

    Mkurugenzi Mwenza Acts in Africa Initiative

  • 15

    SEHEMU YA 1

    UBATIZO KATIKA

    ROHO MTAKATIFU

  • 16

    Matendo 1:8 Ahadi Ya Yesu Mahubiri Yenyewe Kwa Sentensi Moja: Yesu aliahidi kuwatia

    nguvu wafuasi Wake wote, ili wawe mashahidi Wake. Kusudi La Mahubiri: Waamini wabatizwe katika Roho Mtakatifu na

    kutiwa nguvu kama mashahidi wa Kristo. Andiko: Matendo 1:4-8 Utangulizi 1. Ni mapenzi ya Mungu kila mwamini aliyeko hapa abatizwe kwa

    Roho Mtakatifu na kutiwa nguvu kwa ajili ya kazi ya uinjilisti na umisheni.

    2. Ahadi ya Yesu katika Matendo 1:8 ndiyo ya mwisho na muhimu sana aliyotoa kwa kanisa. a. Kwa mara ya kwanza aliitimiza Siku ya Pentekoste. b. Pentekoste ilianzisha wimbi lenye nguvu sana la umisheni

    katika karne ya kwanza. c. Maelezo ya Luka ni kama ifuatavyo: (Soma Matendo 2:1-4).

    3. Lakini, nini maana ya hayo yote? a. Ilimaanisha kwamba Yesu ameanza kutimiza ahadi Yake

    katika Matendo 1:8. b. Nguvu za KiMungu ziliingia katika hao wanafunzi. c. Walibadilishwa kwa ndani. d. Wakawa mashahidi wenye nguvu, waliowezeshwa na Roho.

    4. Ombi letu ni kwamba leo hii, Yesu atatimiza Ahadi Yake katika Matendo 1:8 miongoni mwetu.

    5. Kutokana na ahadi hii ya Yesu, tunajifunza kweli nne zenye nguvu sana, kama ifuatavyo:

    I. TUNAJIFUNZA JUU YA AHADI YA YESU KUHUSU NGUVU. (“Lakini mtapokea nguvu ...“)

    A. Yesu ametupa sisi kazi muhimu sana. 1. Nayo ni: Kuwa mashahidi Wake kuanzia nyumbani na

    kuendelea hadi duniani kote. 2. Kibinadamu, ni kazi isiyowezekana. 3. Hebu fikiri wanafunzi wale wa mwanzo walijisikiaje.

    B. Lakini, Yesu aliahidi kutoa nguvu za kusaidia kufanikisha kazi yenyewe. 1. Ingekuwa nguvu ya KiMungu. 2. Imeahidiwa kwa kila aaminiye.

    C. Swali: “mtapokea” wanaotajwa na Yesu katika Matendo 1:8 ni akina nani? 1. Kwanza: Ni Mitume Wake.

    a. Walikuwa wameokolewa, kuitwa na kuagizwa.

    1

  • 17

    b. Sisi ni kama wao kwa sehemu kubwa. Maana, hata sisi tumeokolewa, kuitwa na kuagizwa.

    2. “Yenu” pia inawahusisha waaminio wote kila mahali (Matendo 2:38-39).

    3. “Yenu” inamhusu pia kila mtu aliyeko hapa leo. 4. Ni pamoja na wewe! (Matendo 2:39).

    II. TUNAJIFUNZA KUHUSU CHANZO CHA NGUVU HIYO. (“... Roho Mtakatifu akiisha kuwajilia juu yenu”)

    A. Chanzo cha nguvu ni Roho Mtakatifu. B. Roho Mtakatifu hutoa uwezesho wa KiMungu:

    1. Ili kuwa shahidi wa Kristo. 2. Ili kuhubiri na kufundisha kwa nguvu. 3. Ili kuyatenda matendo ya Yesu. 4. Ili kuendeleza Ufalme wa Mungu.

    III. TUNAJIFUNZA KUHUSU KUSUDI LA NGUVU HIYO.

    (“... nanyi mtakuwa mashahidi Wangu, katika Yerusalemu, na Uyahudi wote, na Samaria, mpaka mwisho wa nchi.”) A. Roho anatupa sisi nguvu ya kulitii agizo la Kristo la kuihubiri

    Injili nyumbani kwetu mpaka mwisho wa nchi. B. Kwa bahati mbaya sana, WaPentekoste wengi

    wameshindwa kuupokea huu ukweli. C. Wote ni lazima tushiriki katika kuitangaza Injili.

    IV. TUNAJIFUNZA KITU KUHUSU JINSI YA KUPOKEA NGUVU

    HIYO, NA LINI TUNAIPOKEA. (“...akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu”).

    A. Hii nguvu ya kushuhudia haiji tu yenyewe wakati wa kuokoka au wa kubatizwa.

    1. Kuna kitu ambacho lazima tufanye ili kupokea nguvu hiyo.

    2. Ni lazima tumpokee Roho Mtakatifu kwa imani ili tuweze kuipokea nguvu hiyo (Wagalatia 3:2, 14).

    B. Yesu alitufundisha jinsi ya kupokea: (Soma: Luka 11:9-13) 1. Kwanza: Lazima uombe kwa imani (Luka 11:9, 13). 2. Pili: Ni lazima upokee kwa imani (Luka 11:10; Mk 11:24). 3. Kisha, Inakubidi unene kwa imani (Matendo 2:4; Yohana

    7:38) Hitimisho, Na Kuita Watu Waje Madhabahuni

    Hebu njoo sasa upokee Ahadi ya Yesu katika Matendo 1:8.

    [ DRM ]

  • 18

    Ubatizo Katika Roho Mtakatifu Mahubiri Yenyewe Kwa Sentensi Moja: Unaweza kubatizwa kwa

    Roho Mtakatifu leo hii. Kusudi La Mahubiri: Kuona waaminio wakibatizwa kwa Roho

    Mtakatifu Andiko: Matendo 1:8; 2:1-4 Utangulizi 1. Hakuna kilicho muhimu zaidi katika maisha ya Mkristo kuliko

    kubatizwa kwa Roho Mtakatifu. 2. Katika mahubiri haya, tutajibu maswali matatu juu ya ubatizo wa

    Roho Mtakatifu.

    I. UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU NI KITU GANI? A. Ni tukio toka kwa Mungu, lenye nguvu, linalobadilisha

    maisha, ambalo kwa hilo Mungu humvika na kumjaza aaminiye nguvu na uwepo Wake (Luka 24:49; Matendo 1:8; 2:1-4).

    B. Ni ahadi kwa ajili ya waaminio wote (Matendo 2:4; 2:14-17; 2:38-39).

    C. Ni agizo kwa waaminio wote (Matendo 1:4-5; Waefeso 5:18). II. MBONA UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU NI WA MUHIMU

    MNO KATIKA MAISHA YA KILA AAMINIYE? A. Kwa sababu ndiyo chanzo cha nguvu za Mkristo kwa ajili ya

    maisha na huduma (Matendo 1:8; 4:31-33). B. Kwa sababu, unapobatizwa kwa Roho Mtakatifu, utapokea

    nguvu za kushuhudia (Matendo 1:8). C. Kwa sababu, unapobatizwa kwa Roho Mtakatifu, utapokea

    nguvu pia za kufanya yafuatayo: 1. Nguvu za kushinda majaribu na kuishi maisha

    matakatifu (Warumi 1:4; 8:13). 2. Nguvu za kuomba kwa ufanisi zaidi (Luka 11:1-13;

    Warumi 8:26-28). 3. Nguvu za kupenda kwa bidii zaidi (Warumi 5:5). 4. Nguvu za kuelewa Neno la Mungu vizuri zaidi (1Wakor.

    2:14; Yohana 14:26; 16:13). 5. Nguvu za kuhubiri kwa ufanisi zaidi (Matendo 4:8, 31;

    1Wakor. 2:4). 6. Nguvu za kufanya matendo ya Yesu (Yohana 14:12,

    soma pamoja na Yohana 14:16; 16:7). 7. Nguvu za kutambua sauti ya Mungu kwa uwazi zaidi

    (Warumi 8:16). 8. Nguvu za kuabudu (Yohana 4:24).

    2

  • 19

    III. TUNAWEZAJE LEO KUJAZWA NA ROHO MTAKATIFU?

    A. Ni lazima ufanye mambo matatu kabla ya kujazwa na Roho Mtakatifu. 1. Lazima uwe umezaliwa mara ya pili kweli kweli

    (Matendo 2:38; Yohana 14:17). 2. Lazima uwe na njaa na kiu ya kumtaka Mungu (Mathayo

    5:6; Yohana 7:37). 3. Lazima uwe tayari kumtii Mungu na kuwa shahidi kwa

    ajili Yake (Matendo 5:32). B. Unampokea Roho Mtakatifu kwa imani.

    1. Imani ndicho kitu cha lazima ili uweze kupokea chochote kutoka kwa Mungu (Wagalatia 3:2, 5, 14).

    2. Lazima umwamini Mungu, kwamba atakupa Roho Mtakatifu (Yohana 7:38).

    C. Piga hizi hatua tatu za imani: 1. Omba kwa imani (Luka 11:9, 13). 2. Pokea kwa imani (Luka 11:10; Marko 11:24). 3. Kwa imani nena kutoka ndani ya moyo wako (Matendo

    2:4; Yohana 7:37). Hitimisho, Na Kuita Watu Waje Madhabahuni

    Njoo sana, ukabatizwe kwa Roho Mtakatifu.

    [ DRM ]

  • 20

    Ubatizo Wa Roho Mtakatifu Ndicho Kitu Tunachohitaji

    Mahubiri Yenyewe Kwa Sentensi Moja: Kama tunataka kupata

    nguvu za kupinga na kubadilisha mazingira yetu, lazima kila mmoja wetu abatizwe kwa Roho Mtakatifu.

    Kusudi La Mahubiri: Waamini wapate kuelewa hitaji lao la kuwezeshwa kwa Roho Mtakatifu na watafute na kupokea ubatizo wa Roho Mtakatifu.

    Maandiko: Luka 24:49; Matendo 1:4-8; 8:14-17; 19:1-7 Utangulizi 1. Kupokea ubatizo wa Roho Mtakatifu ndiyo ufumbuzi wa matatizo

    ya kupoa, udunia na imani ndogo katika kanisa, na katika maisha yetu wenyewe siku za leo.

    2. Hali ya kuabudu katika kanisa siku hizi inaonyesha kanisa lenye uhitaji mkubwa sana wa nguvu za Roho Mtakatifu.

    I. KANISA GONJWA

    A. Paulo alipofika Efeso, alikuta kanisa gonjwa. 1. Lilikuwa dogo, na dhaifu. 2. Halikuwa na uwezo wa kugusa mji na kuufikia kwa ajili

    ya Kristo. B. Kanisa lilikuwa linanyanyaswa na kubanwa na mazingira

    yake. 1. Kuabudiwa kwa Diana, mungu wa kike, kulitawala mji. 2. Ibada ya Diana ilihusisha uchawi, uganga, uaguzi na

    ulozi, pamoja na matendo ya ngono mbaya kinyume cha kawaida.

    3. Kanisa halikuwa na nguvu za kupambana na majeshi hayo ya pepo.

    C. Makanisa mengi siku hizi yako katika hali kama hiyo. 1. Yamebanwa na mazingira yake 2. Ni ya kimwili, madhaifu, na haya nguvu za kupambana

    na maovu katika mazingira yake. II. DAWA YA KUTIBU

    A. Paulo alijua dawa ya ugonjwa wa kanisa – ni kubatizwa kwa Roho Mtakatifu.

    B. Kanisa la Efeso lilihitaji dawa aina mbili: 1. Maarifa: Walihitaji kurekebishiwa mafundisho yao. 2. Uzoefu: Walihitaji nguvu za Roho Mtakatifu. 3. Paulo anashughulikia yote mawili, hivi:

    a. Alirekebisha maarifa yao (Matendo 19:1-4). b. Aliwasaidia kupata uzoefu (Matendo 19:5-6).

    3

  • 21

    C. Ni kweli hata kwa kanisa la leo. 1. Lazima tuelewe kinachofundishwa na Biblia kuhusu

    ubatizo wa Roho Mtakatifu, kwamba: a. Ni tofauti na wokovu. b. Ni kwa ajili ya waaminio wote. c. Ni kwa ajili ya kupata nguvu za kushuhudia na

    kumwakilisha Kristo. d. Uthibitisho wake ni kunena kwa lugha.

    2. Sawa na wale wanafunzi kumi na mbili wa Efeso, ni lazima kila mmoja wetu apate ubatizo wa Roho Mtakatifu.

    III. FAIDA ZA UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU

    A. Kuna faida nyingi zitokanazo na kumpokea Roho, ikiwa ni pamoja na hizi zifuatazo: 1. Uwepo binafsi wa Yesu hufanyika halisi zaidi (Yohana

    14:15-17; 16:14-15). 2. Tunawezeshwa kuishi maisha matakatifu (Warumi 8:2,

    13). 3. Tunasaidiwa katika kuomba kwetu (Warumi 8:26-27). 4. Tunafarijiwa katika nyakati za shida (Yohana 14:16, 26;

    15:26; 16:7; Matendo 18:9-11). B. Faida ya muhimu zaidi ni kwamba tunapokea nguvu za kuwa

    mashahidi wa Kristo (Matendo 1:8). IV. MPOKEE ROHO MTAKATIFU

    A. Tunampokea Roho kibinafsi (Matendo 9:17-18). B. Lazima tutamani kabisa kupokea (Mathayo 5:6; Yohana 7:37). C. Lazima tutubu, na kuomba tupewe Roho Mtakatifu (Matendo

    2:38). D. Lazima tuwe na imani (Yohana 7:38; Marko 11:24).

    Hitimisho, Na Kuita Watu Waje Madhabahuni

    1. Waamini watakapojazwa na Roho ndipo kanisa litakapokuwa na nguvu za kutosha kupingana na athari za mazingira yake.

    2. Hapo ndipo tutakapokuwa na nguvu za kugusa na kubadili miji yetu na vijiji kwa ajili ya Kristo.

    3. Sasa, njoo ujazwe na Roho.

    [ JI na NO ] Kutoka “Somo La 3: Hitaji La Ubatizo Katika Roho Mtakatifu” katika andishi liitwalo The Relevance of the Holy Spirit in Today’s Church la Mchgj. Dkt. John O. Ikoni na Mchgj. Neubueze O. Oti. (Aba, Nigeria: Assemblies of God Press, 2009).

  • 22

    Mfululizo Wa Mahubiri Kuhusu Ubatizo Katika Roho Mtakatifu

    Namba 1 Kati Ya 4 Ubatizo Katika Roho Mtakatifu Ni Kitu Gani?

    Mahubiri Yenyewe Kwa Sentensi Moja: Ubatizo katika Roho

    Mtakatifu ni tukio lenye nguvu sana kiroho, kwa ajili ya wote wanaomwamini Kristo.

    Kusudi La Mahubiri: Kila aaminiye afikie mahali pa kutaka na kupokea ubatizo wa Roho Mtakatifu.

    Andiko: Luka 3:16

    Utangulizi 1. Katika andiko letu, Yohana Mbatizaji alizungumzia juu ya tukio

    kwa ajili ya wafuasi wa Kristo linaloitwa ubatizo katika Roho Mtakatifu.

    2. Katika mahubiri haya, tutajibu swali muhimu lifuatalo: “Ubatizo katika Roho Mtakatifu ni kitu gani?”

    I. UBATIZO KATIKA ROHO MTAKATIFU NI AHADI NZURI

    SANA KUTOKA KWA MUNGU. A. Yesu aliuita ubatizo katika Roho Mtakatifu “Ahadi ya Baba”

    (Luka 24:49; Matendo 1:4). B. Yesu alitoa ahadi nzuri sana kuhusu zawadi ya Roho

    Mtakatifu (tazama Luka 11:9-13). C. Wanafunzi walipokea ahadi ya Roho Siku ile ya Pentekoste

    (Matendo 2:4, 33). II. UBATIZO KATIKA ROHO MTAKATIFU NI TUKIO LA SIKU

    HIZI, LENYE NGUVU SANA, LINALOBADILISHA MAISHA. A. Ni tukio lenye nguvu sana.

    1. Linaelezwa kuwa ni kitu kinacholeta nguvu (Luka 24:49; Matendo 1:8).

    2. Husababisha huduma yenye nguvu (Matendo 4:33). B. Ni tukio la siku hizi pia.

    1. Ni kwa ajili ya vizazi vyote vya Wakristo (Matendo 2:39). 2. Lilitokea tenana tena katika Kitabu cha Matendo (2:4;

    8:17-18; 9:18-10; 10:44-46; 19:6). C. Ni tukio linalobadilisha maisha.

    1. Lilibadilisha wanafunzi wakaacha kuwa waoga, na kuwa mashuhuda hodari wenye nguvu.

    2. Litakubadilisha na wewe pia!

    4

  • 23

    III. UBATIZO KATIKA ROHO MTAKATIFU NI UVAMIZI KUTOKA MBINGUNI. A. Siku ya Pentekoste, sauti “kutoka mbinguni” ilisikika.

    1. Tukio hilo hutoka mbinguni (yaani, kutoka kwa Mungu). 2. Wao “walivikwa uwezo kutoka juu” (yaani, kutoka kwa

    Mungu). B. Roho huja kama “uvamizi mtakatifu” kutoka mbinguni.

    1. Mifano katika Matendo: 1:8; 4:31; 10:44 2. Unaweza kutarajia Roho Mtakatifu aje juu yako kama

    vile umevamiwa kutoka mbinguni. IV. UBATIZO KATIKA ROHO MTAKATIFU PIA NI KUJAZWA

    KABISA NDANI (Yaani, Ni Kujazwa Kikamilifu Kabisa Kwa Kila Sehemu Ya Nafsi Ya Mtu). A. Maneno yale “kujazwa na Roho Mtakatifu” mara kwa mara

    hutumiwa kuelezea tukio tunalozungumzia. 1. Yanatumiwa mara sita katika Matendo. 2. Yanatumiwa kwa mara ya kwanza katika Matendo 2:4.

    B. Kubatizwa katika Roho hakuonekani kama uvamizi mtakatifu tu kwa nje, bali pia ni badiliko kubwa sana linalotokea ndani. 1. Mfano: Kama sifongo inavyojaa maji.

    C. Ili kupokea ukamilifu wa Roho, ni lazima tumfungulie Mungu maisha yetu kwa ukamilifu kabisa.

    V. UBATIZO KATIKA ROHO MTAKATIFU NI AGIZO LA BIBLIA.

    A. Tukio hili ni la lazima mno kwa ajili ya maisha ya Kikristo kiasi kwamba Biblia haisemi tuna hiari katika jambo hilo.

    B. Yesu pamoja na Paulo wanatuagiza tujazwe (Matendo 1:4-5; Waefeso 5:18).

    C. Tuna heri wakati tunapotii!

    VI. UBATIZO KATIKA ROHO MTAKATIFU NI TUKIO KWA AJILI YA WAAMINIO WOTE. A. Ona ni mara ngapi neno “wote” linatumika kusema juu ya

    ubatizo katika Roho Mtakatifu ndani ya Biblia (Hesabu 11:29; Yoeli 2:28; Matendo 2:4; 4:31)

    B. Katika Luka 11, Yesu anabadilisha lugha. Anaacha kusema “wote” na kusema “kila mmoja” (Luka 11:10; ling. Matendo 2:39).

    Hitimisho, Na Kuita Watu Waje Madhabahuni

    1. Je, uko tayari kumruhusu Roho abadilishe maisha yako? 2. Njoo ujazwe na Roho Mtakatifu leo.

    [ DRM ]

  • 24

    Mfululizo Wa Mahubiri Kuhusu Ubatizo Katika Roho Mtakatifu

    Namba 2 Kati Ya 4 Kwa Nini Ubatizo Wa Roho Mtakatifu Ni Lazima Kwa Kila Aaminiye?

    Mahubiri Yenyewe Kwa Sentensi Moja: Ni muhimu kila aaminiye

    abatizwe katika Roho Mtakatifu. Kusudi La Mahubiri: Kutia moyo na kuhakikisha kwamba waaminio

    wanabatizwa katika Roho Mtakatifu Maandiko: Matendo 1:4-5, Waefeso 5:18 Utangulizi 1. Mistari yetu ya Biblia ina maagizo mawili kwa waaminio kujazwa

    na Roho Mtakatifu. Agizo moja linatoka kwa Yesu, na lingine kwa Paulo.

    2. Hayo maagizo yanaonyesha umuhimu wa mtu kubatizwa katika Roho Mtakatifu.

    3. Tutazame ni kwa nini kila mmoja lazima ajazwe na Roho Mtakatifu leo.

    I. LAZIMA KILA MMOJA AJAZWE NA ROHO KWA SABABU

    KUNA MAISHA TUNAYOTAKIWA KUISHI AMBAYO NI ZAIDI YA UWEZO WETU. A. Hebu tazama maisha ambayo Mungu anataka tuishi:

    1. Maisha kama aliiyoishi Yesu (1Yohana 2:6). 2. Ni maisha ya usafi na utakatifu (1Petro 1:15-16). 3. Ni maisha ya upendo (Mathayo 5:43-44).

    B. Lakini sisi ni dhaifu na kwa nguvu zetu wenyewe hatuwezi kuishi maisha hayo. 1. Ni rahisi zaidi kwetu kuchukia, kuona wivu, na

    kunung’unika. 2. Ni rahisi zaidi kwetu kuishi kama dunia inavyoishi,

    badala ya kuishi kama Yesu. 3. Tunalia kama Paulo na kusema: “Ole wangu maskini

    mimi! Nani atakayeniokoa . . .?” (Warumi 7:24). 4. Jibu linakuja: “Usikate tamaa. Tuna msaada utokao juu!”

    (tazama Wagalatia 5:16) C. Swali muhimu ni hili: Tunaupataje msaada huo toka kwa

    Mungu? 1. Tunaanza kwa kuwa na njaa na kiu ya kumtaka Mungu

    zaidi (Mathayo 5:6). 2. Katika Matayo 5:6, ona sehemu ya kwetu na yake

    Mungu: a. Sehemu yetu: “kuwa na njaa na kiu . . .” b. Sehemu ya Mungu: “watajazwa . . .”

    5

  • 25

    II. NI LAZIMA KILA MMOJA AJAZWE NA ROHO KWA SABABU

    TUNA KAZI YA KUFANYA ILIYO KUU ZAIDI YA RASILMALI TULIYO NAYO. A. Yesu alituachia kazi kubwa sana.

    1. Inajulikana kama Agizo Kuu. 2. Mathayo 28:19-20 3. Mathayo 24:14

    B. Ila, rasilmali zetu binafsi hazitoshi kwa hiyo kazi. 1. Jinsi tulivyo kibinafsi hakutoshelezi. 2. Hali yetu kifedha haitoshelezi.

    C. Pamoja na hayo, Yesu ametuahidi nguvu za kufanikisha kazi yenyewe, kama ifuatavyo: 1. Katika Matendo 1, aliwapa wanafunzi Wake ahadi na

    amri: a. Ahadi ni hii (1:8): “Mtakuwa mashahidi wangu . . .

    mpaka mwisho wa nchi.” b. Amri ni hii (1:4-5): “Msiondoke Yerusalemu, bali

    ingojeni ile zawadi ambayo Baba yangu aliahidi . . .” 2. Hatuwezi kutimiza hiyo ahadi mpaka kwanza tutii amri

    yenyewe. Hitimisho, Na Kuita Watu Waje Madhabahuni

    1. Una maisha ya kuishi ambayo yanazidi uwezo wako. 2. Unayo kazi ya kufanya ambayo inazidi uwezo wako. 3. Unahitaji kupokea nguvu za Mungu. 4. Njoo ujazwe na Roho siku ya leo.

    [ DRM ]

  • 26

    Mfululizo Wa Mahubiri Kuhusu Ubatizo Katika Roho Mtakatifu

    Namba 3 Kati Ya 4 Jinsi Ya Kupokea Ubatizo Katika Roho Mtakatifu

    Mahubiri Yenyewe Kwa Sentensi Moja: Mruhusu Roho Mtakatifu

    akujaze leo na kubadilisha maisha yako. Kusudi La Mahubiri: Waaminio wapate kujazwa na Roho Mtakatifu,

    na waliojazwa wapate kujazwa upya Andiko: Luka 11:9-13 Utangulizi 1. Katika fungu hili, Yesu anawafundisha wanafunzi Wake jinsi ya

    kuipokea zawadi ya Roho Mtakatifu. 2. Katika mahubiri haya, tutatazama jinsi wewe unavyoweza

    kumpokea Roho Mtakatifu siku ya leo. I. MAZINGIRA YA KUMPOKEA ROHO MTAKATIFU

    A. Roho hupokelewa katika mazingira ya maombi. 1. Katika andiko letu, Yesu alikuwa anajibu swali la

    wanafunzi, waliposema, “Bwana! Tufundishe na sisi jinsi ya kuomba” (ms. 1).

    2. Yesu alipopokea Roho, alikuwa kwenye maombi (Luka 3:21-22).

    3. Paulo alikuwa anaomba wakati alipojazwa (Matendo 9:11-12, 17).

    4. Maombi ni muhimu. B. Roho hupokelewa katika mazingira ya utii kwa habari ya

    kuhubiri Injili (Matendo 5:32). C. Roho hupokelewa katika mazingira ya unyenyekevu (1Petro

    5:6). D. Roho hupokelewa katika mazingira ya imani (Wagalatia 3:2,

    5, 14). 1. Yesu alisema hivi: "Yeyote aniaminiye mimi kama

    Maandiko yasemavyo, mito ya maji yaliyo hai itabubujika kutokea ndani mwake" (Yohana 7:38).

    II. ILI KUMPOKEA ROHO MTAKATIFU, FANYA HIVI:

    A. Kiendee kiti cha Mungu cha rehema kwa ujasiri, ukijua kwamba uko katika mapenzi kamilifu ya Mungu (Waebrania 4:16; 1Yohana 5:14-15).

    B. Omba kwa imani yenye ujasiri. 1. Dai ahadi Zake (Luka 11:9-13). 2. Tazamia Mungu akujaze (Marko 11:24). 3. Tazamia kunena kwa lugha (Matendo 2:4).

    6

  • 27

    4. Jitayarishe kuwa shahidi wa Kristo (Matendo 1:8). C. Mpokee Roho kwa tendo la imani.

    1. Roho hapokelewi bila wewe kufanya chochote. 2. MFANO: Kama Petro alivyojitokeza kwa imani kutoka

    kwenye mtumbwi ili atembee juu ya maji, ndivyo na sisi tunavyopaswa kujitokeza kwa imani ili Mungu atujaze (tazama Mathayo 14:25-29).

    D. Jisikie uwepo wa Mungu ndani yako. 1. Mwelekee Mungu zaidi, na kile anachofanya moyoni

    mwako. 2. Hisi uwepo Wake juu yako na ndani yako.

    E. Nena kwa imani (Matendo 2:4). 1. Ruhusu nguvu na uwepo huo kububujika (Yohana 7:37-

    38). 2. Nena kadiri Roho anavyokupa maneno ya kutamka.

    Hitimisho, Na Kuita Watu Waje Madhabahuni

    Njoo sasa ujazwe na Roho

    [ DRM ]

  • 28

    Mfululizo Wa Mahubiri Kuhusu Ubatizo Katika Roho Mtakatifu

    Namba 4 Kati Ya 4 Wajibu Wetu Kuhusu Kubatizwa Katika Roho Mtakatifu

    Mahubiri Yenyewe Kwa Sentensi Moja: Ukisha batizwa kwa Roho

    Mtakatifu, una majukumu Fulani ya kutekeleza. Kusudi La Mahubiri: Khamasisha watu wabatizwa kwa Roho, na

    kuwatia moyo wale waliobatizwa, kuanza kufanya huduma katika Roho

    Andiko: 2Wakorintho 3:7-10: (tazama sana maneno yafuatayo: “huduma ya Roho”)

    Utangulizi 1. Katika andiko letu, Paulo analinganisha aina mbili za huduma:

    a. Mfano: Huduma chini ya Torati, na huduma katika Roho. b. Moja huleta mauti, nyingine huleta haki. c. Moja ni yenye utukufu, na nyingine ni yenye utukufu zaidi

    sana. 2. Huduma ya Agano Jipya inaelezwa kwamba ni “huduma ya

    Roho.” a. Huduma ya Roho ni huduma “inayowezeshwa na Roho, na

    matokeo ni wengine kumpokea Roho” (Gordon D. Fee). b. Mahubiri haya yatalenga kwenye majukumu yetu katika

    kuwaongoza wengine kupokea ubatizo wa Roho Mtakatifu. 3. Biblia inafundisha majukumu matano ya waaminni kuhusu

    ubatizo wa Roho Mtakatifu, kama ifuatavyo: I. NI LAZIMA TUUPATE KIBINAFSI.

    A. Wote tumeagizwa kujazwa na Roho (Matendo 1:4-5; Waefeso 5:18). 1. Yesu alijazwa na Roho (Luka 3:26; Matendo 10:38). 2. Wanafunzi walijazwa na Roho (Matendo 2:4; 4:31, 33).

    B. Je, wewe umeupata ubatizo wa Roho Mtakatifu? II. NI LAZIMA TUENENDE NDANI YAKE KILA SIKU.

    A. Biblia inatuagiza “tuenende katika Roho.” 1. Warumi 8:1; Wagalatia 5:16, 25. 2. Wagalatia 3:3.

    B. Ni lazima “kuchochea” karama ya Roho ndani yetu (2Timotheo 1:6).

    C. Ewe kiongozi: Hitaji kuu la watu wako ni wewe mwenyewe kuenenda katika Roho.

    7

  • 29

    III. NI LAZIMA TUTANGAZE NA KUFUNDISHA JUU YAKE KWA UAMINIFU. A. Yesu alifundisha na kutangaza ujumbe wa ubatizo katika

    Roho Mtakatifu (Luka 11:9-13; Yohana 14–16; Matendo 1:4-8).

    B. Petro alihubiri kuhusu ubatizo wa Roho, kama ifuatavyo: 1. Katika mahubiri yake ya kwanza Siku ya Pentekoste

    (Matendo 2:14-17; 38-39). 2. Katika mahubiri yake ya pili (Matendo 3:19).

    C. Paulo alihubiri na kufundisha kuhusu ubatizo katika Roho Mtakatifu. 1. Huko Efeso (Matendo 19:1-7).

    2. Katika nyaraka zake (kwa mfano: Waefeso 5:18) D. Je, umekuwa ukihubiri kuhusu ubatizo katika Roho

    Mtakatifu? Utaanza sasa na kuendelea kufanya hivyo? IV. NI LAZIMA TUJUE JINSI YA KUWAONGOZA WENGINE

    KUPOKEA. A. Huu ni wajibu wa msingi kwa kila mhubiri wa KiPentekoste. B. Yesu na mitume walimaanisha katika jambo hili la

    kuwaongoza wengine kumpokea Roho Mtakatifu, kama ifuatavyo: 1. Kabla Yesu hajarudi mbinguni (Luka 24:45-49). 2. Mitume huko Samaria (Matendo 8:15-17). 3. Paulo huko Efeso (Matendo 19:1-7).

    C. Ni lazima tumwige Yesu na mitume Wake. V. NI LAZIMA TUTOE NAFASI KWA WATU WETU KUPOKEA.

    A. Ni lazima tutengeneze mazingira yanayofaa kanisani kwa ajili ya jambo hilo.

    B. Ni lazima tuhubiri mara kwa mara juu ya mada hii. C. Ni lazima kuomba na waaminio ili wapokee. D. Ni lazima tuwafundishe wengine jinsi ya kuwaombea

    wengine wapokee. Hitimisho, Na Kuita Watu Waje Madhabahuni

    1. Usipuuzie zawadi hii ya thamani kuu. 2. Sasa, njoo ujazwe na kujazwa upya na Roho.

    [ DRM ]

  • 30

    Mfariji Amekuja Mahubiri Yenyewe Kwa Sentensi Moja: Yesu aliahidi uwepo na

    nguvu za Roho ili kutuwezesha sisi sote kuishi na kumshuhudia Yeye.

    Kusudi La Mahubiri: Kuona watu wakijazwa na Roho, na kushuhudia

    Andiko: Yohana 14:12-20; 16:7; Matendo 1:8 Utangulizi 1. Ukristo una mizizi katika matukio manne makubwa.

    a. Krismasi: Mungu, kwa njia ya Mwana Wake, kuingia kibinafsi katika maisha ya mwanadamu.

    b. Ijumaa Kuu: Kazi ya Kristo ya ufunuo, upatanisho na ukombozi.

    c. Pasaka: Ushindi wa Mungu kwa njia ya Yesu Kristo juu ya nguvu za dhambi na kifo

    d. Pentekoste: Kutiwa nguvu kwa watu wa Mungu kwa uwezo ule ule uliokuwemo ndani ya Kristo, kwa njia ya Roho Mtakatifu.

    2. Pentekoste huzungumza nasi kuhusu “kuja kwa Roho Mtakatifu juu ya kanisa”

    a. Mfariji amekuja! I. TUTAFAKARI AHADI YA ROHO MTAKATIFU.

    A. Mara kadhaa Yesu alizungumzia ahadi hiyo. 1. Yesu aliahidi kwamba kila mtu aliyemwamini angepokea

    Roho kama mto wa maji yaliyo hai ndani ya maisha yake (Yohana 7:37-39).

    2. Yesu aliwaambia wanafunzi kwamba alikuwa karibu kuwaacha, ila, angemtuma Roho Mtakatifu kuchukua mahali pake (Yohana 14:16-17 na 16:7).

    3. Kabla hajapaa kwenda mbinguni, aliwaambia wanafunzi kungojea hadi wapokee ahadi ya Roho (Matendo 1:4-5).

    B. Wakati wa Pentekoste, Yesu alitimiza hiyo ahadi kwa mara ya kwanza (Matendo 2:1-4).

    C. Kisha, chini ya upako wa Roho, Petro aliwatangazia watu kwamba ahadi ya Roho ilikuwa kwa ajili ya wote (Matendo 2:38-39). 1. Basi, ahadi ya “masamaha ya dhambi” na “zawadi ya

    Roho Mtakatifu” haikuwa kwa ajili yao tu, bali inatufikia na sisi leo.

    II. TUTAFAKARI KUHUSU UWEPO WA ROHO MTAKATIFU. A. Kwanza: Yesu aliahidi kwamba Mfariji angekuwa pamoja

    nasi milele (Yohana 14:16,18).

    8

  • 31

    1. Hatatuacha sisi kama yatima (ms. 18). 2. Yesu alikuwa anawaambia wanafunzi hivi: “Siwatelekezi.

    Nina mpango wa muda mrefu. Naondoka, ili Roho Mtakatifu aweze kuja.”

    3. Vile vile alikuwa anasema, hii si hatua ya kurudi nyuma (Yohana 16:7). a. Hii ni sehemu ya mpango Wangu mkuu wa kueneza

    Injili mpaka mwisho wa nchi. b. Aliwataka watambue kwamba ilikuwa bora kwao

    Yeye kuondoka. c. Kama angebakia duniani 1) huduma ingekuwa ya mahali pamoja tu. 2) isingewezekana Kwake kuwasiliana na

    wanafunzi Wake wote sawasawa kwa wakati wote na katika maeneo yote.

    B. Pili: Yesu aliahidi kwamba Roho Mtakatifu asingekuwa pamoja nasi tu, bali angekuwa ndani yetu pia (Yohana 14:17). 1. Ni ahadi ya ajabu sana hiyo: Mungu atakuja kukaa ndani

    yetu na kutupa ujuzi usioweza kukanushwa wa Yeye kuwepo

    2. Itatuthibitishia sisi kwamba Kristo yu ndani yetu (Yohana 14:20).

    III. TUTAFAKARI KUHUSU NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU.

    A. Yesu alifundisha kwamba, wakati Roho Mtakatifu atakapokuja juu yetu, tunapewa nguvu za kushuhudia (Matendo 1:8). 1. Alitaka wanafunzi Wake wajue kwamba kuja kwa

    “Mshauri” kungewawezesha kupata huduma pana na yenye nguvu zaidi (Yohana 14:12).

    2. Angewajaza kwa nguvu nyingi kiasi kwamba huduma yao ingekuwa na mguso mpana zaidi kuliko hata Yake Mwenyewe.

    B. Roho Mtakatifu ni Roho anayeshuhudia. 1. Anapotujaza kwa nguvu Zake, anafanya hivyo ili

    tuwezeseshwe kuwa mashahidi wenye nguvu kwa ajili ya Kristo (Yohana 15:26-27).

    C. Leo hii, kama tuonavyo katika Kitabu cha Matendo, nguvu ya Roho itatuongoza, itatuwezesha kuishi maisha matakatifu, na kutupa nguvu za kushirikisha watu imani yetu kwa mafanikio makubwa.

    Hitimisho, Na Kuita Watu Waje Madhabahuni Sasa njoo upokee zawadi ya Roho Mtakatifu katika maisha yako

    [ KB ]

  • 32

    Maswali Ya Kawaida Kuhusu Ubatizo Katika Roho Mtakatifu

    Mahubiri Yenyewe Kwa Sentensi Moja: Biblia inajibu maswali

    mengi ya kawaida, kuhusu Ubatizo katika Roho Mtakatifu. Kusudi La Mahubiri: Kuwasaidia waaminio kutamani kuwezeshwa

    na Roho Mtakatifu kama mashahidi wa Kristo. Utangulizi Hebu tutafakari baadhi ya maswali ambayo kwa kawaida huulizwa na watu, kuhusu ubatizo katika Roho Mtakatifu: I. JE, WAKRISTO HUMPOKEA ROHO MTAKATIFU WANAPO-

    OKOLEWA? A. Hakika, ulipompokea Kristo, Roho Mtakatifu alikuwa kazini

    (Warumi 8:9). B. Kila mmoja wetu aliyekuja kwa Kristo amekutana na kazi ya

    neema ya Roho Mtakatifu katika kuzaliwa mara ya pili (Yohana 3:3-6).

    II. KAMA NI HIVYO, UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU

    UNATOFAUTIANAJE NA WOKOVU? A. Ipo huduma ya ziada ya kipekee kabisa ya Roho Mtakatifu,

    iitwayo ubatizo katika Roho Mtakatifu (Matendo 1:4-5,8). 1. Hii ni zawadi yenye kutia nguvu itokayo kwa Mungu

    Baba, iliiyo kwa ajili ya kila aaminiye. 2. Ubatizo wa Roho Mtakatifu hutusaidia kuishi maisha

    matakatifu na kutuwezesha kujitoa kwa Bwana Yesu kwa moyo wa dhati kabisa na kwa kumaanisha.

    B. Pamoja na hayo, kusudi la msingi la ubatizo wa Roho Mtakatifu ni kutupa nguvu na ujasiri wa kuwashuhudia wengine imani yetu (Matendo 1:8).

    C. Wote tunahitaji hii “Zawadi Ya Kutia Nguvu” itokayo kwa Mungu ili tuishi maisha ya ushindi na tuweze kuwashirikisha wengine imani yetu, kwa ufanisi mkubwa. 1. Ujuzi huu ni wa muhimu mno kiasi cha Yesu kuwaambia

    wanafunzi Wake wasiondoke Yerusalemu mpaka wapokee (Matendo 1:4-5).

    III. JE, MTU ANAWEZA KUJAZWA ROHO MTAKATIFU BILA YA

    KUNENA KWA LUGHA? A. Ili kujibu swali hili, lazima tukae kwenye mfano unaotolewa

    na Biblia.

    9

  • 33

    1. Siku ya Pentekoste, “wote wakajazwa na Roho Mtakatifu, wakaanza kunena kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowawezesha” (Matendo 2:4, TLR)

    2. Nyumbani kwa Kornelio, “Roho Mtakatifu aliwashukia wale wote waliosikia mahubiri” na “waliwasikia wakinena kwa lugha, wakimtukuza Mungu” (Matendo 10:46, TLR).

    3. Huko Efeso, “wakati Paulo alipowawekea mikono, Roho Mtakatifu alikuja juu yao, nao wakanena kwa lugha na kutabiri” (Matendo 19:6, TLR).

    B. Mistari hiyo inaonyesha kwamba “ushahidi wa mwanzo, wa kuonekana” wenye kuonyesha kwamba mtu amebatizwa kwa Roho Mtakatifu, ni kunena kwa lugha.

    IV. NINI FAIDA YA KUOMBA KWA LUGHA KATIKA MAISHA YA

    MAOMBI YA MTU BINAFSI? A. Husaidia kuthibitisha kwamba umempokea Roho. B. Utajengwa katika maisha yako ya kiroho na katika kutembea

    kwako na Mungu (1Wakor. 14:2,4; Yuda mstari wa 20). C. Tunapo-omba katika lugha, Roho Mtakatifu hutusaidia

    kuomba (Warumi 8:26). 1. Wakati mwingine, lugha yetu ya kawaida huonekana

    haitoshi kujieleza jinsi tunavyojisikia moyoni mbele za Mungu. Maombi katika lugha hutupeleka zaidi ya mipaka ya ufahamu wa kawaida, wakati Roho anapo-omba kupitia kwetu.

    V. MANENO YA KUTIA MOYO KWA WALE AMBAO BADO

    HAWAJABATIZWA NA ROHO MTAKATIFU: A. Kama mambo haya bado hayako wazi kwako, jifunze Neno

    la Mungu na kumtafuta ili upate ufahamu. 1. Kumbuka kwamba Mungu anatupenda sisi sote

    sawasawa. 2. Roho Mtakatifu huja kutufariji, kutuongoza katika kweli

    yote, na kututia nguvu ili tushuhudie. 3. Tafuta kumpokea Roho Mtakatifu, si kunena kwa lugha

    tu. B. Kujazwa na Roho ni mwanzo tu. 1. Baada ya hapo, ni wajibu wako kudumisha upya wa hali

    hiyo na uhai wake kila siku. Hitimisho, Na Kuita Watu Waje Madhabahuni

    1. Daima ombi letu liwe hili: “Uje, Roho Mtakatifu. Ninakuhitaji!” 2. Hebu tujiunge pamoja kumkaribisha Roho Mtakatifu katika

    maisha yako. 3. Naomba ujipatie Pentekoste yako binafsi!

    [ KB ]

  • 34

    Siku Ya Pentekoste Mahubiri Yenyewe Kwa Sentensi Moja: Kuielewa Siku ya Pentekoste

    hutuongoza kuamini na kutafuta kujazwa Roho Mtakatifu. Kusudi La Mahubiri: Watu wajazwe na Roho, na kuwa washuhudiaji wenye

    ufanisi. Andiko: Matendo 2:1-12 I. MAELEZO KUHUSU UJIO WA ROHO (Matendo 2:1a).

    A. Kwa Kiyunani, maana ya Pentekoste ni “hamsini”. 1. Wayahudi wanaiita “Sikukuu Ya Majuma” (Walawi 23:15-21). 2. Sheria za Agano la Kale zilizohusu sikukuu zilikuwa mfano wa

    Kristo na kazi Yake (Wagalatia 3:24; Wakolosai 2:16,17). B. Picha Ya Kwanza: Pasaka (Walawi 23:5, 1Wakor. 5:7).

    1. Pasaka iliwakumbusha watu jinsi Mungu alivyowaokoa Waisraeli kutoka utumwani huko Misri.

    2. Mwanakondoo wa Pasaka ni picha ya kazi aliyofanya Kristo kwa ajili yetu, alipokufa msalabani ili kutuokoa kutoka dhambini.

    C. Picha Ya Pili: Sikukuu Ya Malimbuko (Walawi 23:9-10). 1. Hii ilisherhekewa siku ya kwanza ya juma, baada ya Pasaka. 2. Watu walimtolea Mungu sehemu ya mavuno yao ya zao la

    shayiri. 3. Hii sikukuu iliitwa “malimbuko” kwa sababu ilikuwa ni mfano wa

    mavuno yaliyosalia, ambayo yangevunwa. 4. Ni picha ya kufufuka kwa Kristo, siku ya kwanza ya juma

    baada ya Pasaka (1Wakor. 15:20-23). D. Picha Ya Tatu: Sikukuu Ya Majuma, au Pentekoste (Walawi 23:15-

    17, Matendo 2:1). ONA: Kuna mambo mawili yanayoambatana na sherehe hii: 1. Ilisherehekea mavuno yajayo, ya nafaka:

    a. Pentekoste inahusu mavuno! (Matendo 2:14, 16-17, 21). b. Kusudi la kujazwa na Roho ni kutiwa nguvu za kuwa

    washuhudiaji kwa ajili ya Bwana, ili kuleta wengi waliopotea kama mavuno kwa Yesu (Matendo 1:8).

    2. Ilisherehekea agano jipya katika Kristo. a. Mungu alifanya agano na Ibrahimu, na aliahidi kuibariki

    dunia nzima kupitia kwake (Mwanzo 12:3). b. Mungu alipanga kutumia taifa la Kiyahudi kuwaongoza

    watu kumwamini Masiya (Kutoka 19:5-6). c. Marabi walifundisha kwamba, siku 50 baada ya Pasaka,

    Mungu alishuka juu ya Mlima Sinai na kufanya maagano. d. Lakini, Israeli walishindwa kulishika agano. Basi, Mungu

    aliahidi kufanya agano jipya (Yeremia 31:31-34). e. Tunasoma sasa katika Matendo 2:1 kwamba, siku 50

    baada ya Pasaka, Mungu kwa mara nyingine tena alishuka ili kuanzisha agano jipya.

    II. USHAHIDI WA KUJA KWA ROHO (Matendo 2:1b-4).

    A. Upepo (ms.2).

    10

  • 35

    1. Yesu alimfananisha Roho Mtakatifu na upepo (Yohana 3:8). 2. Siku ya Pentekoste, upepo huu hautajwi kuwa mwanana, bali

    unaelezwa kuwa upepo mkali wenye nguvu, kana kwamba ni pumzi ya Mungu Mwenyewe.

    3. Sauti hii iliwafanya watu kukusanyika (Matendo 2:6a). B. Moto (ms.3).

    1. Haukuwa moto kweli, bali ulionekana kama moto. 2. Ulikuwa dhihirisho lenye kuonekana la uwepo wa Roho

    Mtakatifu. C. Wote wakajazwa na Roho Mtakatifu (ms. 4a).

    1. Neno kujazwa kwa Kiyunani ni pleroo, ambalo linaeleza jinsi upepo unavyojaa katika tanga la meli illi iendeshwe kwa upepo.

    2. Maana yake ni kwamba wanafunzi walijitolea kutawliwa na Roho, Naye alikuwa anawafanya watende walichotenda.

    3. Tunaambiwa na kitabu cha Matendo kwamba hayo ndiyo yaliyotokea tena na tena katika maisha ya wanafunzi hao (Matendo 4:8, 31).

    D. Wakanena kwa lugha kadiri Roho alivyowawezesha (ms. 4b). 1. Walikuwa wanazungumza lugha ambazo hawakuzijua. 2. Huu ulikuwa muujiza ambao Roho aliwawezesha kufanya.

    III. MATOKEO YA KUJA KWA ROHO (Matendo 2:5-12).

    A. Lile kundi kubwa lilikuwa na watu kutoka mataifa mbalimbali (mis. 5, 9-11).

    B. Hitimisho (mis. 6-8,12). 1. Lile kundi kubwa liliwasikia watu ambao hawakuwa na elimu

    wakitangaza maajabu ya Mungu kwa lugha mbalimbali toka duniani kote.

    2. Bila shaka walifikiri hivi: “Hayo yamewezekanaje? Huu ni muujiza! Nini maana yake?”

    C. Kilele Chake (Matendo 2:41). 1. Hii ilikuwa kazi ya Mungu akiandaa mazingira kwa ajili ya

    kutangazwa kwa Injili na kazi ya kuleta wokovu na baraka kwa mataifa.

    D. Tunafikia hatima nne, kama ifuatavyo: 1. Muda wa Mungu ni mkamilifu, na Neno Lake litatimizwa. 2. Sisi pia tutapokea nguvu Zake, tukitii mapenzi Yake.

    a. Wale 120 walijazwa na Roho kwa sababu walimtii Kristo (Matendo 1:4,13-14; 2:1).

    3. Hii zawadi ya Roho ni kwa ajili ya kila mmoja (Matendo 2:17, 39).

    4. Mungu amefanya hayo yote ili tuwezeshwe kuwashirikisha wengine habari za Kristo kwa ufanisi mkubwa na kuwaongoza kuokoka

    Hitimisho, Na Kuita Watu Waje Madhabahuni

    Hebu tuje mbele na kumwomba Mungu atujaze Roho na kututia nguvu ili tuwe mashahidi Wake.

    [ JL ]

  • 36

    Je, Ulimpokea Roho Ulipoamini? Mahubiri Yenyewe Kwa Sentensi Moja: Ubatizo wa Roho Mtakatifu ni

    swala muhimu kwa sababu kusudi la Mungu ni kumpa kila aaminiye nguvu za kuwa shahidi.

    Kusudi La Mahubiri: Kuwashawishi waamini waone kwamba wanahitaji ubatizo wa Roho Mtakatifu, na kuwasaidia kujiandaa kuupokea.

    Andiko: Matendo 19:1-12 I. UMUHIMU WA UBATIZO KATIKA ROHO MTAKATIFU

    A. Swali la Paulo: Je, mlimpokea Roho Mtakatifu mlipoamini? 1. Swali hili linaonyesha uwezekano wa kuwa mwanafunzi

    lakini usiwe umejazwa na Roho Mtakatifu. 2. Vile vile linaonyesha kwamba hili ni swala muhimu sana

    kwa Wakristo. 3. Paulo alitaka kujua kwa uhakika kama walikuwa

    wamejazwa na Roho, kwa sababu alikuwa anataka kanisa lile jipya la Efeso liwe la KiPentekoste kweli.

    B. Umuhimu huu kuhusu ubatizo wa Roho unaonekana hata huko Samaria (Matendo 8:14-17).

    C. Ubatizo wa Roho ni wa muhimu mno kiasi kwamba haupaswi kuwa kitu cha mara moja, bali kitu endelevu. 1. Miaka mingi baadaye Paulo aliliandikia kanisa la Efeso na

    kuwahimiza kujazwa na Roho na kuendelea kujazwa (Waefeso 5:18).

    2. “Mjazwe Roho”. Katika Kiyunani, ni agizo la kudumisha hali ya kujazwa, au, kuendelea kujazwa wakati wote.

    D. Kanisa la kwanza lilifanya swala hilo kuwa la muhimu sana. Basi, na kwetu inatakiwa iwe vivyo hivyo.

    II. KUSUDI LA UBATIZO KATIKA ROHO MTAKATIFU: USHUHUDA

    WENYE NGUVU. A. Paulo alitaka sana watu hao wajazwe Roho kwa sababu ya

    kusudi la Mungu kwa ajili ya ubatizo katika Roho. 1. Yesu alifafanua kusudi la ubatizo katika Roho (Matendo

    1:8). 2. Ubatizo katika Roho si kwa faida ya mtu binafsi na baraka

    zake, bali ni ili kupata nguvu za kumtumikia Mungu katika utume Wake.

    3. Paulo alijua kwamba hao wanafunzi 12 walihitaji nguvu kwa ajili ya kushuhudia.

    B. Matokeo ya hao watu 12 kujazwa na Roho: 1. Walijazwa na Roho, wakaanza kunena kwa lugha na

    kutabiri, kwa nguvu za Roho (Matendo 19:6). 2. Basi, ushuhuda wenye nguvu sana ukatoka na kuenea

    katika sehemu yote ile (Matendo 19:8-10). C. Mpango wa Paulo ulikuwa kueneza Injili katika Asia nzima.

    11

  • 37

    1. Tunaona katika Matendo 19:9-10 kwamba si Paulo peke yake aliyekuwa anahubiri na kutumiwa na Mungu.

    2. Sababu ya Paulo kufanya swala la ubatizo wa Roho Mtakatifu kuwa la muhimu sana huko Efeso ilitokana naye kupanga kuifikia Asia yote kupitia ushuhuda wa waaminio waliojazwa na Roho.

    3. Makanisa mengine ya huko Asian yanatajwa katika Agano Jipya ambayo huenda yalianzishwa kama matokeo ya huduma ya Paulo huko Efeso.

    4. Paulo alikuwa anafuta mpango ambao Kristo alitoa kwa Kanisa: Mjazwe Roho na kuwa mashahidi (Matendo 1:8).

    D. Mpango wa Mungu haujabadilika. Bado anawaita watu watafute nguvu za Roho Wake ili wawe mashahidi.

    III. MATAYARISHO KWA AJILI YA KUMPOKEA ROHO MTAKATIFU

    A. Hatua ya Kwanza: Kutubu dhambi. 1. Wale watu wa Efeso walikuwa wamekubali ujumbe wa

    Yohana Mbatizaji kwamba watubu na kuziacha dhambi zao. B. Hatua ya Pili: Kumwamini Kristo kama Bwana na Mwokozi.

    1. Paulo alipotambua kwamba watu wa Efeso walikuwa wamesikia ujumbe wa Yohana tu, aliwafafanulia kwamba Yohana Mbatizaji alikuwa ametumwa kuandaa watu kwa ajili ya ujio wa Yesu.

    2. Yohana Mbatizaji alihubiri mambo mawili: a. Tubuni kwa sababu Ufalme wa mbinguni umekaribia

    (Mathayo 3:2). b. Yupo anayekuja, ambaye ataondoa dhambi za dunia.

    (Ni Yesu, Yohana 1:29) 3. Walipoelewa, walimpokea Kristo (Matendo 19:5).

    C. Hatua ya Tatu: Amini kwamba Kristo atakujaza na Roho. 1. Mahubiri ya Yohana yalikuwa na ahadi kwamba Yesu

    angebatiza watu kwa Roho Mtakatifu (Luka 3:16). D. Hatua ya Nne: Mwombe Mungu akujaze Roho Mtakatifu.

    1. Wale watu waliamini, na wakati Paulo alipoweka mikono yake juu yao, walianza kuomba, nao wakajazwa na Roho (Matendo 19:6).

    2. Wewe pia waweza kumpokea Roho, ukimtaka kwa maombi.

    Hitimisho, Na Kuita Watu Waje Madhabahuni 1. Sawa na wale wanafunzi huko Efeso, jiandae kumpokea Roho

    Mtakatifu. 2. Fungua moyo wako uwe wazi kwa Mungu na uamini kwamba

    hayo ndiyo Mungu anayotaka kukutendea. 3. Mwombe Mungu akutendee.

    [ MT ]

  • 38

    Usiondoke Nyumbani Bila Hii Mahubiri Yenyewe Kwa Sentensi Moja: Amri ya mwisho ya Kristo

    kwa wanafunzi Wake ilikuwa wapokee nguvu za Roho Mtakatifu ili waweze kufanikisha Agizo Kuu.

    Kusudi La Mahubiri: Kuona waamini wakitii amri ya mwisho ya Kristo ya kubatizwa kwa Roho Mtakatifu na kupokea nguvu za kuwa mashahidi Wake.

    Andiko: Matendo 1:4-5, 8 Utangulizi 1. Kwa kawaida, maneno ya mwisho ya mtu ni ya muhimu sana

    kwake. 2. Maneno ya mwisho ya Yesu kwa kanisa, kabla hajapaa kwenda

    mbinguni, ni amri kwa kila aaminiye. 3. Katika amri hii, Yesu aliweka wazi kabisa kwamba ubatizo katika

    Roho Mtakatifu lazima upewe kipaumbele katika maisha ya kila Mkristo.

    I. AMRI YA MWISHO YA KRISTO (Matendo 1:4a,5).

    A. Msiende popote bila zawadi yenyewe: “msiondoke Yerusalemu. Ngojeeni” (ms. 4a).

    B. Hiyo zawadi tunayotakiwa kuingojea ni ipi? “Mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu” (ms. 5).

    C. Yesu alitoa hiyo amri ya kungojea ubatizo zaidi ya mara moja (Luka 24:49).

    D. Nini maana ya kubatizwa kwa Roho Mtakatifu? 1. Maana yake ni kuvikwa nguvu na kujazwa nguvu za

    Roho wa Mungu (Luka 24:49; Matendo 1:8). II. SABABU YA AMRI YA MWISHO YA KRISTO (Matendo

    1:4,5,8). A. Baba alikuwa ameahidi zawadi hii 1. kupitia nabii (Yoeli 2:28-29).

    2. kupitia kwa Yohana Mbatizaji (Marko 1:7-8). B. Zawadi ya Roho Mtakatifu ilikuwa lengo la msingi sana la

    huduma ya Yesu. 1. Yohana Mbatizaji alisema kwamba, Yesu atakapokuja,

    “atabatiza watu kwa Roho Mtakatifu.” (Marko 1:7-8) 2. Mara nyingi Yesu alizungumzia hilo akiwa na wanafunzi

    Wake (Matendo 1:4) “ambayo mlinisikia nikisema habari zake.”

    3. Maandiko ya Yohana 7:37-39 yanataja wakati mmoja tu ambapo Yesu alizungumzia hilo.

    12

  • 39

    C. Hiyo zawadi ni njia ya Mungu kuwatia nguvu Wakristo ili wawe mashahidi Wake (Matendo 1:8). 1. Yesu aliwaamuru wanafunzi Wake kwenda duniani kote

    na kujipatia wanafunzi katika mataifa yote (Mathayo 28:18-20).

    2. Yesu aliwaamuru wanafunzi watafute kujazwa na Roho Mtakatifu, kwa sababu walihitaji nguvu Yake ili kutimiza na kufanikisha Agizo Kuu.

    3. Agizo la Mungu kwa kanisa halijabadilika. Basi, bado tunahitaji nguvu ya Roho Mtakatifu ili tulifanikishe.

    III. JE, UTATII AMRI YA KRISTO YA MWISHO?

    A. Kwa sababu Roho amekuja, tuaamriwa kuwa mashahidi wa Kristo (Yohana 15:26-27).

    B. Kama tunampenda, tutamtii, Naye atatupa Roho akae ndani yetu na kutujaza nguvu (Yohana 14:15-17).

    C. Mungu humtoa Roho Wake kwa wale wanaomtii (Matendo 5:32). 1. Mitume walikuwa wanazungumza juu ya kumtii Kristo na

    kwenda kushuhudia. Hitimisho, Na Kuita Watu Waje Madhabahuni

    Njoo katika hali ya kutii amri ya Kristo, upokee nguvu zile anazotaka kukupa ili uweze kumtumikia na kuwa shahidi mwenye ufanisi.

    [ MT ]

  • 40

    Chochea Zawadi Ya Mungu Mpaka Iwake Mahubiri Yenyewe Kwa Sentensi Moja: Lazima kila mmoja wetu

    aendelee katika uamsho binafsi wa KiPentekoste, wa kudumu na endelevu, kama tunataka kuwa Wakristo wenye ufanisi na mvuto.

    Kusudi La Mahubiri: Watu waweze kuelewa jinsi wanavyoweza kuendelea kujazwa na Roho na kujazwa tena na tena, na itokee hata leo hii.

    Andiko: 2Timotheo 1:6-8, 11-12, 14 Utangulizi 1. Katika andiko letu, Paulo anamwambia Timotheo jinsi anavyoweza

    kuwa na uamsho binafsi wa Pentekoste, na sababu ya kuutafuta. 2. Anamkumbusha Timotheo “kuchochea mpaka iwake” ile zawadi ya

    Mungu iliyokuwa ndani yake, aliyopokea kwa mara ya kwanza wakati Paulo alipomwekea mikono.

    3. Hapa, Paulo anazungumzia ile zawadi ya Roho Mtakatifu aliyopokea Timotheo alipobatizwa kwa Roho Mtakatifu.

    4. Zawadi hiyo ni lazima ifanywe upya kila wakati. 5. Ni lazima tufanye mambo Fulani ili tupate uamsho binafsi wa

    Pentekoste. 6. Lakini kwanza hebu tuone jinsi Paulo anavyofafanua mistari hii. I. KWA MUJIBU WA ANDIKO HILI, KUPATA UAMSHO BINAFSI

    WA KIPENTEKOSTE KUNAMAANISHA MAMBO MATATU: A. Maana yake ni kujazwa Roho kibinafsi (2Timotheo 1:6b).

    1. Ile “zawadi ya Mungu” inayosemwa katika andiko hili ni ubatizo wa Roho Mtakatifu (Matendo 1:4, 8:20, 11:17). a. Kwa mantiki hii, si karama ya huduma. b. Paulo vile vile alijiweka mwenyewe katika kundi la

    waliokwisha pokea zawadi hiyo. (“Mungu ametupa sisi roho …”)

    2. Bila shaka Timotheo alijazwa na Roho wakati Paulo alipomwekea mikono na kumwombea a. Yawezekana hili lilitokea katika lile kanisa ambalo

    Paulo alianzisha huko Listra (Matendo 14:8-20, 16:1-3). 3. Kubatizwa na Roho baada ya wokovu ulikuwa ndiyo mtindo

    wa kanisa la Agano Jipya (Matendo 8:15-17; 9:17; 19:6). B. Maana yake ni kumruhusu kwa makusudi kabisa Roho afanye

    kazi katika maisha ya mtu (2Timotheo 1:7). 1. Uwepo na kazi ya Roho huleta mabadiliko katika maisha

    yetu. 2. Mahali pa hofu Yeye huleta nguvu (Matendo 1:8). 3. Huleta upendo (Warumi 5:5). 4. Huleta kujitawala (au kiasi) (Wagalatia 5:16).

    C. Maana yake ni kuhusika katika kumshuhudia Kristo kwa bidii. 1. “Usione aibu kumshuhudia Bwana wetu” (2Timotheo 1:8). 2. Hii hutukumbusha maneno ya Kristo katika Matendo 1:8.

    13

  • 41

    II. SABABU TATU REASONS ZA SISI KUHITAJI UAMSHO

    BINAFSI. A. Tutakutana na upinzani tutakapohubiri Injili (2Timotheo 1:8, 11-

    12). B. Tunahitaji msaada wa Roho ili kusimamia ujumbe wa Injili na

    mafundisho sahihi ya kweli (2Timotheo 1:14). C. Tunayo kawaida ya kupoteza shauku (ari, bidii) ya kumtumikia

    Kristo (2Timotheo 1:6a). 1. Paulo anamwambia Timotheo “achochee hadi iwake” ile

    zawadi ya Mungu iliyokuwa ndani mwake. 2. Ni lazima moto uchochewe na kutiwa kuni, la sivyo

    utazimika. 3. Wengi walikuwa wamemtelekeza na kumwacha Paulo, na

    kurudi nyuma (2Timotheo 1:15; 4:10a). 4. Paulo alitaka sana Timotheo abakie kwenye msimamo. 5. Sisi pia lazima tuwe macho na kudumisha msimamo wetu

    kwa Kristo na utume Wake kwa kuhakikisha kwamba uwepo wa Roho unadumu maishani mwetu.

    III. ILI KUPATA UAMSHO BINAFSI WA KIPENTEKOSTE, LAZIMA

    TUFANYE KITU. A. Sawa na Timotheo, ni lazima tuanze kwa kumwamini Kristo

    kiukweli (2Timotheo 1:5). B. Lazima tutambue kwamba Roho Mtakatifu huleta uamsho

    tunapotafuta kujazwa uwepo Wake. C. Lazima tuanze kwa kuhakikisha kwamba tumejazwa.

    1. Unaweza kujazwa hata leo. D. Halafu, lazima tudumu kuchochea moto wa ile zawadi ya

    Mungu. 1. Kwa kuiamini ahadi yenyewe (Yohana 7:37-39). 2. Kwa kupiga hatua ya imani na kumshuhudia Kristo

    (Matendo 5:32). 3. Kwa kuendelea kumtafuta Mungu na kuomba tujazwe (Luka

    11:9-10, 13). Hitimisho, Na Kuita Watu Waje Madhabahuni

    1. Hebu tuje mbele na k uomba ili Mungu atujaze Roho Mtakatifu. 2. Kama hujawahi kujazwa hata mara moja, ahadi hii ni kwa ajili

    yako. Njoo mbele ili moto uwashwe maishani mwako. 3. Ikiwa umekwisha pokea ubatizo katika Roho Mtakatifu, njoo

    uchochee moto kwa kujazwa kwa mara nyingine tena ili uweze kuendelea kumtumikia Kristo na kushuhudia katika nguvu za Roho Mtakatifu.

    [ MT ]

  • 42

    Je, Tokea Ulipoamini Umewahi Kupokea?

    Mahubiri Yenyewe Kwa Sentensi Moja: Unaweza kumpokea Roho Mtakatifu kama ilivyotokea kwa wale wanafunzi kumi na mbili huko Efeso.

    Kusudi La Mahubiri: Waamini wasiojazwa wajazwe na waliojazwa wajazwe tena na Roho Mtakatifu.

    Andiko: Matendo 19:1-7 Utangulizi 1. Paulo alipofika Efeso alikuta mji uliojaa uasherati na ibada ya

    sanamu. (Huko walikuwa wanamwabudu Diana au Artemi, mungu wa kike wa uzazi, aliyekuwa na matiti mengi kwenye sanamu yake.)

    2. Mpango wa Paulo ulikuwa kuifikishia Efeso na Asia Ndogo yote ujumbe wa Injili (tazama Matendo 19:10).

    3. Alianza kwa kuuliza swali: I. SWALI LA PAULO

    A. Aliuliza hivi: “Je, mmempokea Roho Mtakatifu tangu mlipoamini?”

    B. Mbona akauliza swali hili? Nini kilichomfanya afikiri kwamba hawakupokea zawadi hiyo iliyokuwa ahadi? Walikuwa wanafanya nini mpaka swali hilo likaulizwa? 1. Pengine tabia yao au jinsi walivyozungumza. 2. Labda ni jinsi walivyoabudu. 3. Pengine Paulo alijisikia hivyo katika roho yake. 4. Ingawa Paulo aliwahesabu kama waaminio wa kweli,

    alijua kwamba kuna kitu cha zaidi kilichohitajika maishani mwao.

    5. Uelewa wao na ujuzi kuhusu Roho Mtakatifu ulikuwa umepungua mahali.

    C. Je, mtu anaweza kutambua kwamba Roho yuko katika maisha yako?

    II. JIBU LA WALE WANAFUNZI KUMI NA MBILI

    A. Walijibu hivi: “Sisi hatujawahi hata kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu!” 1. Hawakujua kuhusu nguvu ambazo Roho alikuwa nazo

    kwa ajili ya kuwasaidia. 2. Au kuhusu zawadi alizotaka kuwapa. 3. Au hata kuhusu mwongozo aliokuwa nao kwa ajili ya

    kuwasaidia. 4. Hata hawakujua kwamba anapatikana, au yupo!

    B. Wewe ungejibuje swali la Paulo?

    14

  • 43

    1. Je, ungejibu kama Waefeso walivyojibu? 2. Je, matendo yako yangewafanya watu waulize:

    “Umewahi kupokea tangu ulipoamini?” 3. Je, sisi tunaojiita WaPentekoste tumepokea kabisa

    huduma ya Roho Mtakatifu? C. Je, uko tayari kupokea nguvu Zake leo kwa ajili ya

    kukusaidia kuishi?

    III. ALICHOFANYA PAULO A. Aliomba pamoja nao ili wapokee Roho Mtakatifu (Matendo

    19:6). B. Walimpokea Roho Mtakatifu, kama ilivyokuwa kwa wale

    wanafunzi 120 ile Siku ya Pentekoste (Matendo 2:1-4). 1. Hii ilikuwa miaka 25 baada ya Pentekoste.

    IV. ITIKIO LETU LEO

    A. Sisi pia tunaweza kupata ujuzi huo huo leo! 1. Kwa njia ile ile (Matendo 2:38-39). 2. Kwa ishara ile ile (Matendo 2:4; 19:6). 3. Kwa kusudi lile lile (Matendo 1:8).

    B. Lakini: Kwa nini tunahitaji ujuzi huu? 1. Tunaishi katika jamii iliyopotoka, kama ile ya Efeso. 2. Lazima tuwe na nguvu za Roho ili tuwe mashahidi wa

    Kristo wenye ufanisi. 3. Tena, tunahitaji nguvu za Roho ili tuweze kuwa na

    mahusiano binafsi na Kristo, yenye kina – ili Kristo aweze kujulikana na kutukuzwa maishani mwetu.

    C. Hakuna hata moja katika hayo litakalotokea, mpaka kwanza tubatizwe kwa Roho Mtakatifu (Luka 24:49; Matendo 1:4-8). 1. Ilitokea kwa wanafunzi Siku ya Pentekoste. 2. Ilitokea kwa wale wanafunzi kumi na mbili huko Efeso. 3. Inaweza kutoka kwako wewe leo.

    Hitimisho, Na Kuita Watu Waje Madhabahuni

    1. Tayarisha moyo wako mbele za Mungu. 2. Njoo kwa imani na ukiwa na matarajio. 3. Mwombe Mungu akujaze (Luka 11:13).

    [ KK ]

  • 44

    Roho Mtakatifu Hutia Nguvu Mahubiri Yenyewe Kwa Sentensi Moja: Ukikubali kubatizwa kwa Roho

    Mtakatifu, utapokea nguvu za kuwa shahidi wa Kristo. Kusudi La Mahubiri: Waamini waweze kuelewa na kupokea nguvu za

    Roho Mtakatifu zinazobadilisha. Andiko: Matendo 1:8 Utangulizi 1. Kama ilivyokuwa katika Kitabu cha Matendo, nguvu ya Pentekoste

    huhusika sana kusababisha kuenea kwa Injili leo, kuliko kitu kingine chochote. a. Si bahati mbaya kwamba shughuli kuu ya umishenari katika

    dunia ya leo inatoka kwa WaPentekoste. b. Pamoja na hilo, wengi hawaelewi vizuri asili ya tukio hili. c. Huku kueleweka vibaya huzuia ushuhuda wetu kwa dunia.

    2. Katika mhubiri haya, tunatafuta kuelewa asili na kusudi la nguvu za Pentekoste.

    3. Hebu tutazame mambo matatu yafuatayo, ambayo Yesu alifundisha kuhusu nguvu za Roho katika Matendo 1:8.

    I. YESU ALIAHIDI KUTOLEWA KWA ROHO

    A. Je, Yesu aliahidi nguvu aina gani katika mstari wa 8? 1. Hakusema juu ya mamlaka (kwa Kiyunani: exousia, neno

    litumikalo katika ms. 7), bali juu ya uwezo (kwa Kiyunani: dunamis, ms. 8).

    2. Yesu alikuwa anaahidi nguvu ili kazi itendeke. B. Yesu alijua kwamba hao waamini hawakuwa tayari kwenda

    duniani kwa uweza au nguvu zao wenyewe. 1. Alikwisha wapa mamlaka Yake tayari (Luka 9:1); sasa

    walihitaji nguvu ambazo zingewabadilisha. 2. Hii nguvu ingewawezesha kadiri ya uhitaji wao, ili watende

    kazi ambayo Yesu aliwaita kuitenda. 3. Hata sisi tunaihitaji nguvu hiyo hiyo siku za leo.

    C. Ubatizo wa Roho ni tukio halisi, lenye kuonekana. 1. Ni tofauti na wokovu.

    2. Watu hawa walikwisha mpokea Roho Mtakatifu walipozaliwa mara ya pili (Yohana 20:22).

    3. Walikuwa na Roho Mtakatifu tayari. Baada ya muda mfupi, Roho Mtakatifu angewamiliki.

    4. Hata sisi tunahitaji huo mguso wa Roho siku hizi.

    II. YESU ALIFAFANUA NAFASI MPYA YA WANAFUNZI.

    A. Yesu alikuwa anaahidi mabadiliko. 1. Ni hivi: Yesu alisema, wangekuwa mashahidi Wake.

    a. Mkazo hauko kwenye kutenda tu, bali kuwa inavyotakiwa.

    15

  • 45

    b. Hii ni pamoja na kubadilishwa kwa tabia. 2. Katika Matendo, watu walihudumu kutokana na maisha

    yaliyobadilishwa. a. Petro ni mfano mzuri (Fananisha Mathayo 26:69-75 na

    Matendo 2:14 kuendelea). b. Mtu anabadilika ... siyo ulimi tu.

    3. Kazi ya kwanza ya Roho ni kutubadilisha sisi. a. Hii ndiyo sababu ubatizo wa Roho Mtakatifu ni wa

    maana sana kwa waaminio! B. Yesu pia alijali sana kuhusu ushuhuda.

    1. Ubatizo wa wanafunzi ulisababisha ushuhuda wenye nguvu sana.

    2. Huo ushuhuda ulikuwa pamoja na a. Mahubiri yenye nguvu (Matendo 2:14-40). b. Ishara na maajabu vyenye nguvu (Matendo 2:43). c. Jamaa yenye nguvu (Matendo 2:44-47).

    3. Yote hayo yalikuwa ushuhuda wenye nguvu kwa waliopotea.

    III. YESU ALIDHIHIRISHA MAHALI PA ROHO MTAKATIFU.

    A. Nguvu hii itapata mahali pa kutokea ambapo ndiyo penyewe. 1. Kuna mahali, na kuna utendaji. 2. Nguvu ya Roho inapaswa kuonekana au kusikika katika

    maeneo manne nyeti sana ya ushuhuda: a. Katika nyumba zetu. b. Katika kijiji au mji wetu (“Yerusalemu”). c. Katika miji na vijiji jirani (“Uyahudi na Samaria”). d. Katika dunia yote (“mpaka mwisho wa nchi”).

    3. Mungu huwachukua watu Wake, na kuwajaza kwa Roho Wake, kisha kuwasambaza katika dunia yenye kuwahitaji sana sana.

    B. Nguvu hii inahusiana pia na wakati. 1. Agizo Kuu, halifiki “mpaka mwisho wa nchi” (Matendo 1:8)

    tu, bali mpaka “utimilifu wa dahari” (Mathayo 28:20). 2 Ubatizo huu wa Roho Mtakatifu haukuwa kwa ajili ya

    watakatifu wa karne ya kwanza tu. Ni kwa ajili ya waamini wote, wa wakati wote, mpaka Yesu atakaporudi tena! (Matendo 1:11; 3:19-20).

    3. Ni kwa ajili yetu sisi leo! C. Siku ya Pentekoste “wote wakajazwa na Roho Mtakatifu.”

    1. Wote waliambiwa wangoje mpaka ahadi ije. 2. Sisi pia lazima “tungojee mpaka tutakapovikwa uwezo

    utokao juu” (Luka 24:49). Hitimisho, Na Kuita Watu Waje Madhabahuni

    1. Roho atakubadilisha uwe shahidi kwa ajili ya Kristo. 2. Atakubadilisha ili na wewe ubadilishe dunia yako. 3. Njoo ujazwe sasa. [ DWM ]

  • 46

    Ushauri Binafsi Wa Yesu Kuhusu Kumpokea Roho

    Mahubiri Yenyewe Kwa Sentensi Moja: Yesu anatuambia jinsi ya

    kumpokea Roho Mtakatifu. Kusudi La Mahubiri: Waamini wampokee Roho Mtakatifu. Andiko: Luka 11:9-13 Utangulizi 1. Yesu anawaambia wanafunzi Wake jinsi wanavyoweza kumpokea

    Roho Mtakatifu. 2. Ona kwamba anaelekeza mafundisho Yake kwa wanafunzi, si kwa

    wenye dhambi. a. Ms. 1 - “wanafunzi” b. Ms. 13 - “wana”

    3. Yesu anatupa maelekezo matatu kuhusu kumpokea Roho Mtakatifu, kama ifuatavyo:

    I. NI LAZIMA TUOMBE.

    A. Tunashauriwa mara tatu “kuomba” (ms. 9, 10, 13) B. Kuomba kwetu lazima kuwe kwa imani (Marko 11:24). C. Tunaomba, Yeye anatoa, sisi tunapokea, kwa imani (ms. 9-10).

    II. NI LAZIMA TUMAANISHE.

    A. Zaidi ya kuomba, lazima “kutafuta” na “kubisha” (ms. 9). 1. Hii huonyesha kwamba tunamaanisha.

    B. Lazima tuwe na njaa na kiu ya Mungu (Mathayo 5:6; Yohana 3:37).

    C. MFANO: Simulia habari za yule rafiki mwenye bidii (ms. 5-8). III. HATUPASWI KUOGOPA.

    A. Kuna wanao-ogopa … 1. … kwamba Mungu hatawapokea. 2. … kwamba watapata tukio bandia, au la kipepo. 3. Hapa Yesu anatuliza hofu zote.

    B. Usimwogpe Mungu. 1. Kwa sababu Yeye ni Baba wa Mbinguni mwenye upendo.

    C. Usiogope kwamba kutakuwa na tukio bandia, kwa sababu Mungu … 1. … hatakupa nyoka ukiomba samaki. 2. … hatakupa nge ukiomba yai. 3. … hatakupa kitu bandia.

    Hitimisho, Na Kuita Watu Waje Madhabahuni

    Njoo leo umpokee Roho. Omba nawe utapewa. Tafuta nawe utaona. Bisha na mlango utafunguliwa. [ DRM ]

    16

  • 47

    Yesu, Abatizaye Kwa Roho Mtakatifu Mahubiri Yenyewe Kwa Sentensi Moja: Mtazame Yesu ili ubatizwe

    kwa Roho Mtakatifu. Kusudi La Mahubiri: Waamini waje kwa Yesu na kubatizwa kwa Roho

    Mtakatifu. Andiko: Luka 3:16 I. YESU NDIYE ABATIZAYE KWA ROHO MTAKATIFU.

    A. Tunatakiwa kumwangalia Yesu, si kama Mwokozi na Mponyaji wetu tu, bali pia kama Anayebatiza kwa Roho Mtakatifu.

    B. Ishara pekee ya Masiya inayotajwa katika Injili zote nne ni kwamba, Yeye anabatiza kwa Roho Mtakatifu (Mathayo 3:11; Marko 1:8; Luka 3:16; Yohana 1:33).

    C. Leo hii mtazame Yesu kama Mbatizaji wako katika Roho Mtakatifu!

    II. LAZIMA TUJIANDAE KUPOKEA UBATIZO HUO KUTOKA KWA

    YESU. A. Ni lazima tujiandae kiroho (Matendo 2:38).

    1. Lazima tuzaliwe mara ya pili. 2. Lazima tutubu na kuacha dhambi zozote zilizo zoeleka na

    ambazo zimekuwa kawaida. B. Ni lazima tujiandae kiakili.

    1. Tusiruhusu yasiyo kweli yatuchanganye akili. 2. Badala yake, tuamini kinachofundishwa na Biblia, kama

    ifuatavyo: a. Ubatizo katika Roho Mtakatifu unapatikana leo

    (Matendo 2:14-17). b. Ubatizo katika Roho Mtakatifu ni kwa ajili ya waaminio

    wote (Matendo 3:38-39). c. Kunena kwa lugha kama Roho anavyojalia ndiyo ishara

    ya kwanza ya kubatizwa katika Roho Mtakatifu (Matendo 2:4).

    d. Matokeo mengine mazuri sana yatafuata (MFANO: nguvu za kushuhudia, ukaribu katika mahusiano na Mungu, karama za Roho, nguvu juu ya mapepo, na kadhalika.).

    e. Huo ujazo lazima udumishwe (Waefeso 5:18). C. Ni lazima tujiandae kihisia.

    1. Mioyo yetu lazima iwe tayari kupokea. 2. Lazima tutake kubatizwa katika Roho Mtakatifu (Mathayo

    5:6; 6:33; Yohana 7:37-39). 3. Lazima tuamini kwamba Yesu atatubatiza kwa Roho

    Mtakatifu (Matendo 1:4-5; Marko 11:24). Hitimisho, Na Kuita Watu Waje Madhabahuni

    Njoo kwa Yesu, na umruhusu akubatize leo. [ JWL ]

    17

  • 48

    Yesu: Mwokozi Na Abatizaye Mahubiri Yenyewe Kwa Sentensi Moja: Leo unaweza kumjua

    Yesu kama Mwokozi wako na Anayebatiza katika Roho Mtakatifu.

    Kusudi La Mahubiri: Wewenye dhambi wamjie Kristo na kuokolewa, na waaminio wamjie Kristo na kuwezeshwa kushuhudia.

    Andiko: Yohana 1:29-34 Utangulizi 1. Katika andiko letu, Yohana Mbatizaji alitangaza kazi mbili kuu za

    Yesu za ukombozi, kama ifuatavyo: (Yeye ni …) a. “Mwanakndoo wa Mungu aziondoaye dhambi za dunia” (ms.

    29). b. “Anayebatiza kwa Roho Mtakatifu” (ms. 33).

    2 Leo unatakiwa umjue kama Mwokozi na Mbatizaji! a. Msalabani alifanyika Mwokozi wetu … alipojitoa kama kafara

    kwa ajili ya dhambi zote za binadamu. b. Siku ya Pentekoste akawa Mbatizaji kwa Roho ...

    alipomwaga Roho Wake juu ya kanisa Lake ili kulitia nguvu kwa ajili ya kupeleka ujumbe wa msalaba kwa binadamu wote.

    3. Mahubiri haya yatatazama hizo kazi zote mbili za Yesu, na maana yake kwetu sisi leo.

    I. KUTANA NA YESU, MWOKOZI WA DUNIA.

    A. Yeye ndiye Mwanakondoo wa Mungu. 1. Tangazo la Yohana: “Tazameni, huyo ni Mwanakondoo

    wa Mungu …” (Yohana 1:29). 2. Kama Mwanakondoo wa Mungu, Yesu ni toleo la Mungu

    kwa ajili ya dhambi zetu (1Yohana 2:2; Yohana 3:16). 3. Anataka wote waokolewe (2Petro 3:9).

    B. Alikufa ili tuwe na uzima. 1. Alikufa badala yetu (kwa niaba yetu) (2Wakor. 5:21). 2. Alikufa kwa ajili yetu wote (1Yohana 2:2).

    C. Mpokee leo kama Mwokozi (Kwa namna gani?) 1. Kwa njia ya toba na imani (Marko 1:15; Matendo 20:21). 2. Tubu dhambi zako (Matendo 3:19; 17:30). 3. Mwamini Kristo tu ili uokolewe (Matendo 16:31).

    II. KUTANA NA YESU, ABATIZAYE KWA ROHO MTAKATIFU. A. Yeye ndiye amtoaye Roho.

    1. Tangazo la Yohana: ms. 33 “Yeye atawabatiza kwa …”

    18

  • 49

    2. Kama Abatizaye kwa Roho Mtakatifu, anawatia nguvu watu Wake kuhubiri ujumbe wa wokovu. a. Kabla ya Pentekoste (Matendo 1:8). b. Siku ya Pentekoste (Matendo 2:4, 41, 47). c. Baada ya Pentekoste (Matendo 4:31, 33).

    3. Anataka wote wasikie (Luka 24:47). B. Alimtoa Roho Wake ili sisi tuwe na nguvu.

    1. Wote walio-okoka wameagizwa kuwa mashahidi Wake (Luka 24:48).

    2. Hivyo, wote walio-okoka wanahitaji nguvu Zake (Luka 24:49). 3. Basi amewaamuru wote wampokee Roho Wake

    (Matendo 1:4-5). C. Mpokee kama Mbatizaji leo. (Kwa njia gani?)

    1. Omba kwa imani (Luka 11:9, 13). 2. Pokea kwa imani (Luka 11:10; Marko 11:24). 3. Nena kwa imani (Matendo 2:4; Yohana 7:37-39).

    Hitimisho, Na Kuita Watu Waje Madhabahuni

    Njoo kwa Yesu sasa kama Mwokozi wako na Mbatizaji kwa Roho Mtakatifu!

    [ DRM ]

  • 50

    Yesu Atakujaza Na Roho Mtakatifu Ili Ushuhudie

    Mahubiri Yenyewe Kwa Sentensi Moja: Kipaumbele cha Kristo kwa

    ajili ya kila aaminiye ni kwamba ajazwe Roho na kuwezeshwa kushuhudia kwa ajili Yake.

    Kusudi La Mahubiri: Waaminio wajazwe na nguvu za kushuhudia Andiko: Matendo 1:8 Utangulizi 1. Yesu alikuja hapa duniani kwa makusudi makuu mawili. Yohana

    Mbatizaji aliyatangaza (Yohana 1:29-34): a. Kutoa wokovu na msamaha wa dhambi. b. Kutujaza kwa Roho Mtakatifu ili tuweze kuhubiri Injili.

    2. Kwa mujibu wa Matendo 1:8, kusudi la ubatizo kwa Roho Mtakatifu ni kuwapa waamini nguvu ili kuwa mashahidi wa Kristo.

    3. Kila aaminiye aliyezaliwa mara ya pili anahitaji kuwa shahidi kwa ajili ya Kristo. Basi, anahitaji kujazwa na kudumu akiwa amejazwa na Roho Mtakatifu.

    4. Mwisho kabisa wa muda wa Yesu kuwa hapa duniani, alisisitiza tena na tena kipaumbele cha kupokea nguvu za Roho Mtakatifu na kuwa mashahidi Wake.

    5. Tutazame kweli tatu zenye nguvu sana zinazothibitisha kwamba kipaumbele cha Yesu kwa ajili ya kila aaminiye ni kujazwa na Roho Mtakatifu na kuanza kumshuhudia.

    I. USIKU KABLA YA KUSULUBIWA KWAKE, YESU

    ALIZUNGUMZIA UJIO WA ROHO NA JINSI MITUME WANAVYOPASWA KUSHUHUDIA KWA AJILI YAKE. A. Usiku ule Yesu aliposalitiwa, alizungumza mara kadhaa na

    wanafunzi Wake kuhusu kuja kwa Roho Mtakatifu, na kazi ambayo Roho angefanya ndani yao (Yohana sura 13-17).

    B. Akasema, wao wangefanya kazi zile zile kama Yeye, na hata kuu kuliko hizo (yaani, nyingi zaidi) kwa kuwa anakwenda kwa Baba (Yohana 14:12). 1. Maana ni kwamba, Yeye alikuwa anakwenda kwa Baba ili

    Roho aje kuchukua nafasi Yake (Yohana 16:7-8). C. Aliahidi kuwatumia Roho Mtakatifu kama wangetii amri Yake

    (Yohana 14:15-20). 1. Agizo kwamba wangojee Yerusalemu lingekuja baadaye,

    baada ya kufufuka Kwake. 2. Alisema, Roho aliyekuwa pamoja nao kwa wakati huo,

    angeingia ndani mwao (ms. 17).

    D. Baadaye katika maandiko hayo, Yesu alirudia tena kuzungumza kuhusu kuja kwa Roho. Safari hii anawaambia wanafunzi

    19

  • 51

    kwamba, matokeo ya ujio huo ingekuwa kuanza kushuhudia (Yohana 15:26).

    II. JIONI YA UFUFUO WAKE YESU ALIWAAMURU WANAFUNZI

    KUJAZWA NA ROHO NA KUSHUHUDIA (Yohana 20:19-22). A. Siku Yesu alipofufuka, aliwatokea mitume, na kitu cha kwanza

    alichowaambia ni agizo la kuwa mashahidi Wake (ms. 21). B. Aliwavuvia na sema, “Mpokeeni Roho Mtakatifu.” (ms. 22). C. Tuliona jinsi ambavyo kabla ya kufa Kwake, Yesu alizungumza

    na wanafunzi kuhusu kujazwa na Roho Mtakatifu, na kushuhudia. Mara tu baada ya kufufuka Kwake, anarudia hilo hilo.

    III. KABLA HAJAPAA MBINGUNI, YESU ALIWAAGIZA WANAFUNZI

    WAKE MARA MBILI WASIONDOKE YERUSALEMU MPAKA WATAKAPOKUWA WAMEBATIZWA KWA ROHO MTAKATIFU NA KUWEZESHWA KWA AJILI YA KUSHUHUDIA (Luka 24:46-49; Matendo 1:4-5). A. Luka anaandika kuhusu matukio hayo yote mawili, wakati Yesu

    alipotoa agizo hili kwa wanafunzi Wake. Hayo yalikuwa maneno ya mwisho ya Yesu, na huonyesha kitu anachokipa umuhimu zaidi (kipaumbele) kwa wafuasi Wake. 1. Kusudi la Yesu kwa ajili ya waaminio ni wao kuwa

    mashahidi Wake. 2. Ndiyo sababu kipaumbele Chake kwa ajili yetu ni sisi

    kujazwa na Roho, ili tuwe na nguvu za kutimiza utume Wake.

    B. Tukimpenda Bwana wetu, tutamsikiliza na kutii amri Yake kwamba tutafute ubatizo wa Roho Mtakatifu.

    C. Wale wanafunzi wa kwanza waliomsikia Yesu akikazia mara kwa mara juu ya uhitaji wao kupokea utimilifu wa Roho, walitii agizo Lake, na walingojea pale Yerusalemu (Matendo 1:12, 14).

    D. Siku 10 baadaye, Siku ile ya Pentekoste, ahadi ilitimizwa, na Mungu alimimina Roho Mtakatifu juu ya wale wote waliotii na waliokuwa wanatafuta nguvu za Roho.

    E. Baada ya wanafunzi kujazwa na Roho Siku ya Pentekoste, Petro alitangaza kwamba hiyo zawadi ya Roho sasa inapatikana kwa wote watakaotubu na kumwamini Kristo (Matendo 2:38-39).

    Hitimisho, Na Kuita Watu Waje Madhabahuni

    1. Tangu wakati huo, Yesu amekuwa akitafuta watu watakaoamini na kupokea zawadi Yake ya Roho Mtakatifu.

    2. Ukiamini, na uwe tayari kutoa maisha yako kwa ajili ya kumshuhudia Kristo, hata wewe utajazwa na Roho Mtakatifu.

    3. Njoo sasa kwa imani na uanze kumwomba Yesu akujaze Roho Mtakatifu.

    [ MT ]

  • 52

    Maji Yaliyo Hai Mahubiri Yenyewe Kwa Sentensi Moja: Kristo amewaalika wote wenye kiu

    ya nguvu za Mungu na uwepo Wake waje wajazwe na Roho Wake Kusudi La Mahubiri: Kuona watu wakibatizwa kwa Roho Mtakatifu Andiko: Yohana 7:37-39 Utangulizi 1. Watu wengi hutamani ujuzi halisi wa kiroho, ambao utatosheleza mioyo

    yao na kuwajaza nguvu, kusudi na amani. 2. Katika jitihada za kutosheleza shauku hiyo, wanatafuta mahali pengi. 3. Katika Yohana y, Yesu anawaaalika wote wanaotafuta kitu cha kujazia

    hiyo shauku isiyotoshelezwa maishani mwao, kwamba wamwendee Yeye na kupokea hiyo zawadi, itakayowatosheleza kweli kweli.

    4. Hebu tutazame mwaliko huu ambao Yesu ameutoa (Yohana 7:37-39): I. YESU ALITOA ZAWADI YA MAJI YALIYO HAI.

    A. Zawadi yenyewe ni ipi? 1. Maji yaliyo hai ni mfano wa Roho Mtakatifu (ms. 39). 2. Hapa, Yesu anazungumzia umwagiko wa Roho Mtakatifu wa

    ile Siku ya Pentekoste (ms. 39). 3. Anatualika tuke na kunywa (yaani, kupokea uwepo na nguvu

    za Roho ndani yetu.) 4. Mungu alikwisha ahidi kuhusu zawadi hii, kama ifuatavyo:

    “Mimi nitamimina Roho Wangu” (Yoeli 2:28-29) 5. Kabla Yesu hajapaa mbinguni, alithibitisha kwamba hiyo ahadi

    ingetimizwa siku za karibuni. (Matendo 1:4-5). 6. Zawadi ya maji yaliyo hai nit oleo la nguvu za Mungu ili wale

    wanaolipokea waweze kufanikisha mpango wa Mungu wa kujenga Ufalme Wake (Matendo 1:8).

    7. Siku ya Pentekoste hayo maji yaliyo hai yalimiminwa (Matendo 2:1-4).

    B. Zawadi yenyewe ni kwa ajili ya nani? 1. Zawadi ya Roho Mtakatifu ni kwa ajili ya watu wote kila mahali. 2. Yesu alisema, “Kama mtu yeyote ana kiu, na aje”, halafu tena

    akasema, “yeyote aniaminiye Mimi”. 3. Siku ile ya Pentekoste, wote waliokuwa wamekutanika

    walijazwa. Baadaye Petro alitangaza kwamba zawadi hiiyo ilikuwa “kwa ajili ya wote ambao Bwana Mungu wetu atawaita” (Matendo 2:39).

    4. Zawadi ya Roho ni kwa ajili yako. Ipokee leo. II. MATOKEO YA KUPOKEA ZAWADI HIYO YA MAJI YALIYO HAI

    A. Maji yaliyo hai hutosheleza kiu ya nafsi. 1. Maji ambayo Yesu anatoa ni hai. Ni zawadi ya Roho wa

    Mungu Mwenyewe, anayetujaza kwa uzima na nguvu za Kristo.

    2. Uwepo na kazi ya Roho ndani yetu italeta matokeo yafuatayo … a. … tunda la Roho (Wagalatia 5:22-23).

    20

  • 53

    b. … nguvu za kushinda dhambi (Wagalatia 5:16). c. … uhakikisho kwamba wewe ni mtoto wa Mungu (Warumi

    8:15-16). d. … uthibitisho kuhusu ukombozi wetu ujao (Waefeso

    1:13nk). B. Maji yaliyo hai hutujaza nguvu za kuwabariki wengine (Yohana

    7:38). 1. Mito ya maji yaliyo hai itabubujika kutoka ndani yetu. 2. Kusudi la Mungu kutujaza ni ili nguvu za Roho zifurike kutoka

    ndani yetu, na kuleta uzima kwa wengine. 3. Ndicho Yesu alikuwa anakisema, katika Matendo 1:8. 4. Kristo anataka maisha yako yawe mfereji wa Roho kupitia ili

    kupeleka uzima kwa wale walio wafu katika dhambi. C. Mpango wa Mungu ni kwamba, maji yaliyo hai kiwe ni kitu endelevu

    (Yohana 7:38). 1. Uwepo wa Roho unatakiwa kuwa mto unaoendelea

    kububujika. 2. Ndiyo sababu wakati wote tunatiwa moyo na Agano Jipya

    kuenenda katika Roho na kuishi katika Roho. (Wagalatia 5:25: “Kwa kuwa tunai