Harakati za kisiasa tanzania na athari zake kwa waislamu wa tanzania

57
HARAKATI ZA KISIASA TANZANIA, ATHARI ZAKE KWA WAISLAMU WA TANZANIA NA JINSI YA KUPAMBANA NAZO MTOA MADA Sh Mohammed Issa HAY-ATUL ULAMAA TANZANIA DODOMA, 24.04.2011 1

description

DARSA HILI LILTOLEWA APRIL 2011 NA MOHAMED ISSA -UNIVERSITY OF DODOMA MUSLI FORUM.

Transcript of Harakati za kisiasa tanzania na athari zake kwa waislamu wa tanzania

Page 1: Harakati za kisiasa tanzania na athari zake kwa waislamu wa tanzania

1

HARAKATI ZA KISIASA TANZANIA, ATHARI

ZAKE KWA WAISLAMU WA TANZANIA NA JINSI YA KUPAMBANA NAZO

MTOA MADASh Mohammed Issa

HAY-ATUL ULAMAA TANZANIA

DODOMA, 24.04.2011

Page 2: Harakati za kisiasa tanzania na athari zake kwa waislamu wa tanzania

2

UTANGULIZI

Harakati za kisiasa nchini Tanzania zinaanzia na Mkutano wa Berlin mwaka 1884.

Katika makubaliano ya jumla ya mkutano huo, kifungu cha VI kiliweka wazi wajibu wa Serikali zote za kikoloni barani Afrika kutoa ulinzi maalum na kuusaidia Ukristo katika makoloni yao.

“Christian missionaries, scientists and explorers, with their followers, property and collections, shall likewise be the objects of especial protection”.(The Berlin Conference, General Act, article VI)

Page 3: Harakati za kisiasa tanzania na athari zake kwa waislamu wa tanzania

3

CONTD………

Matokeo yake, sera za serikali za kikoloni za Kijerumani na Kiingereza nchini Tanzania, zilikuwa kuwapendelea wakristo katika elimu, ajira na huduma za jamii.

Kanisa lilijiimarisha kwa kutumia upendeleo huu na kuitumia serikali kuwakandamiza waislamu. Waislamu wakawa tabaka la wanyonge kielimu, ajira na huduma za jamii.

Uhusiano huu wa Kanisa na serikali ulianza tangu enzi ya ukoloni wa Wajerumani mwaka 1905 pale Askofu Thomas Spreiter wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam alipoingia Mkataba wa Maridhiano (MoU) na Gavana wa wakati huo.

Page 4: Harakati za kisiasa tanzania na athari zake kwa waislamu wa tanzania

4

CONTD……

Katika kitabu Historia ya Jimbo Kuu la Dar es Salaam, tunanukuu;-

“Askofu alisisitiza kwamba haitoshi kufungua mashule tu na kufundisha watoto dini, bali ni lazima pia kuinua hali nzima ya shule zetu …kusudi hali ilingane au iwe bora zaidi kuliko hali ya shule za serikali” (D.H.Mbiku, Historia ya Jimbo Kuu la Dar es Salaam, uk. 73)

Ili kutimiza lengo hili, Askofu Spreiter alionana na Gavana wa Kijerumani wakati huo na kukubaliana nae kama ifuatavyo;-.

Page 5: Harakati za kisiasa tanzania na athari zake kwa waislamu wa tanzania

5

CONTD…..

“Alikutana pia na Gavana, akapana nae kujenga uhusiano bora kati ya misioni na serikali. Isitoshe, walikubaliana kwamba hata mashule ya misioni yanastahili kupata misaada ya serikali na wanafunzi waliopita kutonyimwa nafasi za kazi”.(ibid, uk.73)

Page 6: Harakati za kisiasa tanzania na athari zake kwa waislamu wa tanzania

6

MFUMO WA ELIMU WA KANISA

Mwaka 1945-Mfumo wa Elimu Tanganyika

Shule Shule zaSerikali na Shule za Makanisa

Msingi 200 300 Govnt Aided200 Unaided

Sekondari 8 10TTC 8 16Chuo Kikuu 1 (Makerere )

Source : Dr John Sivalon- uk. 10 -

Page 7: Harakati za kisiasa tanzania na athari zake kwa waislamu wa tanzania

7

CONTD….

Uhusiano huu kati ya Kanisa na Serikali uliendelea hata baada ya Wajerumani kuondoka nchini kufuatia Vita Kuu ya I ya Dunia na hata baada ya uhuru.

1.0 HARAKATI ZA KISIASA WAKATI WA UKOLONIKwa kuwa waislamu walikuwa ndiyo tabaka la wadhulumiwa wakati wa ukoloni, wao ndio walioanzisha harakati za kisiasa nchini.

Page 8: Harakati za kisiasa tanzania na athari zake kwa waislamu wa tanzania

8

CONTD…

Mwaka 1929, waislamu wakaanzisha chama cha ustawi wa waafrika -African Association (AA).

Mwaka 1933, wakakibadili jina na kukiita TAA-Tanganyika African Association.

Chama hiki kiliongozwa na waislamu ambao pia walikuwa viongozi wa Aljaamiatul Islamiya Fii Tanganyika hadi mwaka 1953 Nyerere alipochaguliwa kuwa Raisi wa TAA baada ya Abdulwahid Sykes.

Mwaka 1954, TAA ikabadilishwa jina na kuwa TANU-Tanganyika African Union- ili kupigania haki ya watangayika kujitawala.

Page 9: Harakati za kisiasa tanzania na athari zake kwa waislamu wa tanzania

9

CONTD….

Wakati wote wa harakati hizi za waislamu kuanzia AA na TAA, wakristo walijiweka mbali na siasa kwa sababu Ukristo uliokuwa ndiyo dini rasmi ya Dola.

Lakini kuanzia mwaka 1954 ushiriki wa wakristo katika siasa ukachukua sura mpya kwa kuingia Nyerere katika uongozi wa TANU.

Page 10: Harakati za kisiasa tanzania na athari zake kwa waislamu wa tanzania

10

CONTD….

Kupitia Nyerere, wakristo wakajiandaa kuitawala Tanganyika huru pasina waislamu kujua kwamba Nyerere kuingia katika siasa ni mpango makhsusi wa Kanisa.

John Sivalon anasema “Nyerere ambaye mwenyewe alikuwa mkatoliki alikuwa na uhusiano wa karibu sana na viongozi fulani wa Kanisa na hivyo alionekana kuwa ni kiungo kati ya Kanisa na Serikali.” (Kanisa Katoliki na Siasa ya Tanzania Bara 1953-1985)

Page 11: Harakati za kisiasa tanzania na athari zake kwa waislamu wa tanzania

11

NYERERE ALIANDALIWA NA KANISA

Hatuwezi kuzungumza harakati za kisiasa Tanzania na athari zake kwa waislamu pasina kumzungumzia Julius Nyerere.

Tumekwishaona kuwa “Nyerere alikuwa na uhusiano na viongozi fulani wa Kanisa” (Sivalon).

Maana yake ni kwamba Kanisa lilijiandaa kushika hatamu za siasa na serikali Tanzania.

Page 12: Harakati za kisiasa tanzania na athari zake kwa waislamu wa tanzania

12

CONTD…

Hao “viongozi fulani” mmoja wao ni Padri Walsh –Katibu Mtendaji wa Idara ya Elimu ya Kanisa ambaye ndiye aliyekuwa mkufunzi wa Nyerere (mentor) kuhusu siasa.

John Sivalon anasema “Wawili hawa walikuwa marafiki na mara nyingi, inasemekana walikuwa wakizungumza katika jumba la ‘White Fathers’. Moja ya mazungumzo yao bila shaka yalikuwa juu ya Nyerere kujihusisha kikamilifu na siasa ya kutetea uhuru”. (Sivalon, uk. 17)

Page 13: Harakati za kisiasa tanzania na athari zake kwa waislamu wa tanzania

13

CONTD..

Katika barua yake kwenda Makao Makuu ya Kanisa Vatican kwa idara iitwayo Propaganda Fidei, Padri William Collins Katibu Mkuu wa Shirika la watawa la Maryknoll Fathers aliandika;-

“Shirika la Maryknoll limekubali kulipia tiketi ya kwenda Marekani na kurudi Uingereza kwa vile huyu ni kiongozi mkatoliki..Kwa vile ni nia ya serikali ya Waingereza kuwaandaa wenyeji kwa madaraka, Shirika la Maryknoll limeona kuwa msaada wowote linaoweza kuwapatia viongozi wakatoliki ni kulisaidia kanisa”. (William Collins, Report on Julius Nerere, Maryknoll Fathers Central Archives).

Page 14: Harakati za kisiasa tanzania na athari zake kwa waislamu wa tanzania

14

CONTD…

Huu ndio ulikuwa mkakati rasmi wa kanisa Katoliki kama unavyosisitizwa tena katika nukuu ifuatayo;-“Kuna hatari ya TANU kusambaratishwa na tofauti za kidini. Pia upo uwezekano wa TANU kutodumu katika udhibiti wa madhumuni, malengo na sera zake kama ilivyokuwa hadi sasa. Hatima yake inategemea uwezo wa wale watakaoshika madaraka miaka michache ijayo…kwa umuhimu huo, upo umuhimu wa hali ya juu wa kuwahimiza Wakatoliki waadilifu kujihusisha ipasavyo katika TANU ikiwa ndiyo njia pekee ya kudumisha uzalendo wa kiafrika ili usiangukie katika mawakala wapotovu” (Confidential Diary-Tanganyika” Maryknoll Central Archives, New York)

Page 15: Harakati za kisiasa tanzania na athari zake kwa waislamu wa tanzania

15

CONTD…

Ukweli huu unatufanya tuelewe kwa nini mara baada ya Nyerere kuingia katika TAA upepo wa kisiasa ghafla ukabadili mwelekeo na kuwa ‘harakati za kisiasa za Kanisa’.

Kanisa likahakikisha linatumia kila liwezalo ikiwemo vyombo vyake vya habari kama vile gazeti la Kanisa la ‘Kiongozi’ kuijenga TANU ili kujihakikishia nguvu ya kisiasa na kiutawala katika Tanganyika huru.

Page 16: Harakati za kisiasa tanzania na athari zake kwa waislamu wa tanzania

16

CONTD…

Athari za harakati hizi za siasa za Kanisa wakati wa kudai uhuru ni waislamu kuenguliwa kutoka katika siasa kupitia Uamuzi wa Busara 1958 kuhusu TANU kushiriki katika uchaguzi wa kura tatu.

Ukichanganya na propaganda za “Kutokuchanganya dini na Siasa” zilizoanza mwaka 1958 mara baada ya Mkutano wa Tabora, kuathirika kwa waislamu kisiasa kulikuja kuwafanya waathirike zaidi kiuchumi, kijamii na kidini katika Tanganyika huru.

Pamoja na mkakati wa Kanisa kumiliki siasa, harakati hizi zisingefanikiwa kamwe kama waislamu wangekuwa wanajitambua na kama wangeingia katika siasa kama kundi jamii lenye maslahi yake.

Page 17: Harakati za kisiasa tanzania na athari zake kwa waislamu wa tanzania

17

2.0 HARAKATI ZA KISIASA BAADA YA UHURU

Baada ya uhuru, Kanisa lilijiandaa kujilimbikizia zaidi nguvu kubwa kisiasa, kiuchumi na kiutawala.

“Sisi Maaskofu wenu, tunaona haja ya kueleza wazi kuwa kuenea kwa mafundisho rasmi ya Kanisa kuhusu siasa, jamii na uchumi hapa Tanganyika, kwa wakati huu ni muhimu zaidi kuliko kazi nyingine yoyote ile ya kujitolea” (Message of Tanganyika’s Bishops, Newsletter TEC, 1962, uk.2)

Page 18: Harakati za kisiasa tanzania na athari zake kwa waislamu wa tanzania

18

CONTD…

Katika juhudi hizi mpya za Kanisa, Uislamu ukaorodheshwa katika maadui wakubwa wa Kanisa pamoja na Ukomunisti ambao wanatakiwa kushughulikiwa ipasavyo.“Uislamu na ukomunisti ulikuwa unashughulikiwa na idara ya dini ya Baraza la Maaskofu” (Sivalon, uk. 31).

Mwaka 1963, waislamu wakaamua kujizatiti kielimu ili kujikomboa kwa kujenga shule yao na kuimarisha umoja ili kujihami na siasa za Kanisa.

Page 19: Harakati za kisiasa tanzania na athari zake kwa waislamu wa tanzania

19

SHULE ZA EAMS HADI MWAKA 1968

Uganda TanzaniaKenya

Shule/Msingi 77 70 28Vyuo vya Ufundi 3 -

-Hosteli 1 -

-

Source: Research data, (Warsha ya Waandishi Habari wa

Kiislamu)

Page 20: Harakati za kisiasa tanzania na athari zake kwa waislamu wa tanzania

20

CONTD… Mwaka 1961 Makao Makuu ya EAMWS yalihamishiwa

Dar es Salaam, kitendo hiki kikaonekana tishio kwa Kanisa.

“Hivyo, kutokana na kazi ya idara ya mambo ya dini ya TEC kwa wastani watendaji wote katika Kanisa Katoliki na jumuiya zake walielimishwa juu ya hatari za Ukomunisti na Uislamu kama zilivyodhaminiwa na viongozi wa Kanisa”.

Matokeo yake, maamuzi yote ya kisiasa na kiutawala yalikuwa yanatolewa na Nyerere na mawakala wengine wa Kanisa ndani ya TANU na serikali yalikuwa yakitolewa kulingana na mkakati rasmi wa Kanisa.

Page 21: Harakati za kisiasa tanzania na athari zake kwa waislamu wa tanzania

21

CONTD…

Sivalon anathibitisha hilo alipoandika kwamba;-

“..viongozi wa ngazi za juu waliohusika na utume wa Kanisa wa kijamii kitaifa walijaribu kutumia utume huo kama mkakati wa kupambana na waliodhaniwa kuwa maadui wa Kanisa: Ukomunisti na Uislamu” (Sivalon, uk. 34).

Wakati waislamu wajiiandaa kujikomboa kielimu na kijamii kutoka katika hali duni, wakristo walikuwa wanajiandaa kupiga pigo lao mwisho.

Page 22: Harakati za kisiasa tanzania na athari zake kwa waislamu wa tanzania

22

CONTD…

Matokeo yake ni kujengeka kwa Mfumo Kristo uliotawala kila kitu kuanzia siasa, dola, elimu, ajira, uchumi, huduma za kijamaii n.k.

Sera mbali mbali za kisiasa na kitaifa ziliakisi mafundisho ya Kanisa. Azimio la Arusha lililoanzisha Siasa ya Ujamaa na hatimaye vijiji vya ujamaa ni moja kati ya mikakati ya kisiasa ya Kanisa kuwashughulikia waislamu.

Page 23: Harakati za kisiasa tanzania na athari zake kwa waislamu wa tanzania

23

CONTD…

Kwanza walianza kwa kupiga maarufuku Mahakama ya Kadhi mwaka 1963 na kuleta Sheria moja ya kisekula.

Lengo ni kuwaondolea waislamu baadhi ya utambulisho wao (Muslim Identity) na kuwachanganya na wakristo (Assimilation of Muslims) hivyo kuwafanya wasijitambue kuwa wao ni kundi jamii.

Kisha wakapiga marufuku vyama vingi mwaka 1965 na kuweka mfumo wa chama kimoja kwa sababu walikhofia waislamu wasijijenge tena kisiasa kupitia chama kingine.

Page 24: Harakati za kisiasa tanzania na athari zake kwa waislamu wa tanzania

24

CONTD…

Kisha wakaja na Azimio la Arusha na Siasa ya Ujamaa mwaka 1967, hiyo ilikuwa sera ya Kanisa tangu mwaka 1905-1910 walipoanzisha vijiji vya ujamaa chini ya Askofu Spreiter.

“Kwa namna fulani, vijiji vile vilifanana na vijiji vya ujamaa vilivyokamilika. Kwa kawaida vijana walijenga nyumba zao kwa pamoja kusaidiana. Siku tatu hata tano walifanya kazi katika shamba la umma. Nidhamu na tabia ya kila mmoja ziliangaliwa na kulindwa na viongozi wa kijiji pamoja na wamisionari” (D.H.Mbiku, Historia ya Jimbo Kuu la Dar es Salaam, uk. 84)

Azimio la Arusha lilitaifisha njia kuu za uchumi ambazo kwa kiasi kikubwa zilikuwa mikononi mwa waislamu husuusan viwanda na majumba ambayo yalimilikiwa na Msajili wa Majumba (Shirika la Nyumba la Taifa).

Page 25: Harakati za kisiasa tanzania na athari zake kwa waislamu wa tanzania

25

MADHARA YA SERA YA MFUMO WA CHAMA KIMOJA, AZIMIO LA ARUSHA NA SIASA YA UJAMAA KWA WAISLAMU WA TANZANIA

Uamuzi wa kufuta Mahakama za Kadhi uliwaathiri waislamu katika utekelzaji wa mafundisho ya dini yao na kuwaathiri kiuchumi-mirathi, ndoa, talaka n.k.

Uamuzi wa kufuta mfumo wa vyama vingi uliwanyima waislamu fursa ya chama mbadala hivyo kuwafanya ima watumwa kisiasa au kukosa kabisa fursa ya kushiriki katika harakati za kisiasa.

Sera ya utaifishaji (Nationalization) ilisababisha wawekezaji waislamu hasa wahindi kuhama nchini hivyo kuua nguvu za waislamu kiuchumi.

Siasa za utaifa na uzalendo (Nationalism) ziliua umoja wa waislamu chini ya EAMWS na kuathiri mipango ya maendeleo ya waislamu kielimu.

Page 26: Harakati za kisiasa tanzania na athari zake kwa waislamu wa tanzania

26

CONTD…

Sera ya vijiji vya ujamaa ilimaliza kabisa mfumo wa kijamii wa waislamu na kuwaathiri kiuchumi kwa kuwatoa katika ardhi zenye rutuba na makazi yao tangu babu zao.

Vijiji vya ujamaa viliwapa wakristo fursa nzuri ya kuwaritadhisha waislamu au kuharibu maadili yao kwa kuwarundika mahali pamoja.

“Makatekista hao lazima wafanye kazi katika idara za maendeleo ya jamii vijijini, iwe ni katika kilimo au katika shuguhuli nyingine za maendeleo kama vile ujenzi wa nyumba, barabara n.k.” (Religious Affairs Department, “Some Pointers about Islam in Tanganyika” 1963)

Page 27: Harakati za kisiasa tanzania na athari zake kwa waislamu wa tanzania

27

CONTD…

Maaskofu mbali mbali waliwahimiza wakristo kwenda katika vijiji vya ujamaa kwa sababu kwao ilikuwa fursa ya kipekee kama Askofu Christopher Mwoleka alivyonukuliwa akisema;-

“Katika historia, Kanisa halijapata nafasi kama hii ya kuonyesha kwa vitendo yale ambayo limekuwa likuhubiri kwa karne nyingi.. Kijiji ambacho watu wake wanahimizwa kuwa sehemu ya mwili mmoja nii mahali pazuri kwa Ukristo kufanikiwa. Hapa Tanzania uwanja umekwisha tayarishwa, kinachobaki ni kueneza na kukuza injili…hivyo, vijijini wakristo waanzishe jumuiya ziwe kama sumaku kuwavuta wengine” (C. Mwoleka and J. Healey eds.., “Ujamaa and Christian Communities,” Spearhead No. 45).

Page 28: Harakati za kisiasa tanzania na athari zake kwa waislamu wa tanzania

28

CONTD….

Nyerere mwenyewe kama mlei aliwahimiza mapadri kuishi vijijini. Sivalon anasema;-“Baada ya Mwalimu Nyerere kuwataka mapadri kuishi vijini viongozi wa Kanisa kwa pamoja walitafuta njia ya kuitikia mwito huo. Ilikuwa dhahiri kwamba idadi ya mapadri waliohitajika kama alivyotaka Nyerere haikuwepo”. Hivyo katika mkutano wao wa mwaka 1970, maaskofu waliamua kwamba “makatekista moja kwa moja wawe ndio watakaoishi kwa kudumu vijijini..na hao makatekista wapewe mafunzo maalum kwa kazi hii” (Sivalon, uk. 41)

Page 29: Harakati za kisiasa tanzania na athari zake kwa waislamu wa tanzania

29

CONTD…

Mwaka huo huo wa 1970, Nyerere alikuwa ameshawaambia Maaskofu kuwa anataka kulipa Kanisa nafasi ya kipekee.

Akizungumza na Katibu Mkuu wa TEC, Padri Rweyemamu aliyekuwa amemtembelea Ikulu, Nyerere alisema;-“I am just a lay man but tell the Bishops that I am trying to do whatever I can to give my church a better chance so that it will not be blamed as it is in Latin America” (Van Bergen, Religion and Development in Tanzania).

Page 30: Harakati za kisiasa tanzania na athari zake kwa waislamu wa tanzania

30

CONTD…

Sivalon anasema Azimio la Arusha linasisitiza maadili ya Kikristo na ananukuu;-“Hakuna atakayetilia mashaka miongozo iliyo katika ‘Azimio la Arusha’. Tunapotafakari ‘Azimio la Arusha’, tunakumbuka ari ya wakristo wa kwanza kama ilivyoandikwa katika Matendo ya Mitume..(Ibid, uk.2).

Kwa hiyo kwa muda wote wa serikali ya awamu ya kwanza na mfumo wa chama kimoja, harakati za kisiasa zilikuwa ni Kanisa kupambana na Uislamu na Waislamu katika kila nyanja na kujenga Mfumo Kristo.

Page 31: Harakati za kisiasa tanzania na athari zake kwa waislamu wa tanzania

31

CONTD…

John Sivalon anasema mwaka 1969 uliitwa “Mwaka wa Semina za Mafunzo” na ananukuu azimio la Mkutano uliofanyika Chuo Kikuu Dar es Salaam;-“Viongozi wa Kanisa wanaombwa kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya vijijini kwa uwezo wao wote na kufuata mipango ya serikali. Kanisa linaombwa kusaidia kuwaelimisha watu kwa mtazamo mpya na maadili ya Kikristo yaliyomo katika siasa ya ujamaa ambayo hutegemewa sana na maendeleo ya kisiasa” (Sivalon, uk.45)

Page 32: Harakati za kisiasa tanzania na athari zake kwa waislamu wa tanzania

32

CONTD…

Hadi kufikia mwaka 1970, siasa za Tanzania zilikuwa mikononi mwa Kanisa kwa asilimia kubwa na kuwawezesha kuamua wanachotaka kukidhi maslahi ya Kanisa.

Semina ile ya “Mwaka wa Mafunzo” (SSY) ilikuwa na athari kubwa sana katika siasa za Tanzania.

“SSY na Baraza vimeleta msisimko huu ambao umewaamsha Wakatoliki kupigania viti katika uchaguzi wa wabunge na mimi nikiwa mmoja wao. Baadaye huko bungeni tulifanya utafiti usio rasmi na kugundua kwamba asilimia sabini na tano ya waliochaguliwa walikuwa wakristo, na kati ya hao, asilimia sabini walikuwa wakatoliki” (John Sivalon, uk. 46)

Page 33: Harakati za kisiasa tanzania na athari zake kwa waislamu wa tanzania

33

CONTD…

Kwa kutumia wingi wao bungeni, wakawa wanapitisha sheria mbali mbali za kuwakandamiza waislamu.

Sheria ya Ndoa na Talaka ya 1971 ni moja ya sheria hizo kandamizi kwa waislamu kwa sababu;- Inakataza msichana chini ya miaka 18 kuolewa. Inaruhusu uzinzi kwa kutambua mwanamume na mwanamke

waliokaa katika ukimada kuwa mke na mume. Inaruhusu ndo za mchanganyiko watu wa dini mbili tofauti (ndoa

ya kiserikali/Bomani). Haitambui talaka ya mume kwa mkewe hadi ithibitishwe na

mahakama. Inamtambua mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa kuwa mtoto halali na

anarithi.

Page 34: Harakati za kisiasa tanzania na athari zake kwa waislamu wa tanzania

34

3.0 HARAKATI ZA KISIASA KATIKA MFUMO WA VYAMA VINGI (1992 TODATE)

Hatimaye sera ya Mwalimu Nyerere na Kanisa ya Ujamaa na Kujitegemea ikafeli vibaya. Ukichangia na Vita vya Kagera ambavyo pia vilianzishwa na Mfumo Kristo, uchumi wa Tanzania ukaporomoka na nchi kuingia katika kipindi kigumu cha hali ya maisha.

Profesa Ali Mazrui alikuita kufeli huku kwa Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea “Nyerere’s policy of Socialism seemed a heroic failure”. (Prof. Ali Mazrui, The Africans, A Triple Heritage, BBC Documentary).

Ndiyo, ingawa alifeli vibaya, kwa Kanisa Katoliki Nyerere ni “Hero” ndiyo maana wamemtangaza kuwa “Mwenye Heri” akielekea katika “Utakatifu”.

Page 35: Harakati za kisiasa tanzania na athari zake kwa waislamu wa tanzania

35

CONTD…

Akikabiliwa na hali mbaya ya uchumi, Nyerere akalazimika kung’atuka na kumkabidhi nchi Ali Hassan Mwinyi mnamo mwaka 1985.

Kipindi chote cha Rais Mwinyi kilitawaliwa na upinzani mkubwa wa Kanisa huku Kanisa likijipanga upya kwa kurejesha mfumo wa siasa wa Vyama Vingi mwaka 1992.

Julius Nyerere akawa mwongozaji mkubwa wa ujenzi wa mfumo wa vyama vingi kwa maslahi ya kanisa akihofia kuibuka kwa vyama au chama cha Kiislamu.

Page 36: Harakati za kisiasa tanzania na athari zake kwa waislamu wa tanzania

36

CONTD…

Katiba ya Jamhuri ya Muungano Sura ya Kwanza Kifungu cha 3.-(1) inasema;- “The United Republic is a democratic and Socialist State which adheres to multi-party democracy”.

Pamoja na kurejesha mfumo wa vyama vingi, katiba inakataza kuundwa kwa vyama vya kidini, kikabila au kikanda.(Katiba 20 - (2))

Page 37: Harakati za kisiasa tanzania na athari zake kwa waislamu wa tanzania

37

CONTD…

Wakati mfumo wa vyama vingi inaanza tena, waislamu wengi walishapoteza hamu kuhusu siasa kwa kuona kuwa haina maslahi na dini yao.

Matokeo yake, kwa mara nyingine ni wakristo ndio waliokuwa kwenye nafasi nzuri zaidi kisiasa kujipanga kwa maslahi yao na waislamu wameendelea kuwa nguvu kazi ya wengine.

Page 38: Harakati za kisiasa tanzania na athari zake kwa waislamu wa tanzania

38

CONTD…

Kwa muda mfupi, waislamu walipata matumaini kisiasa kupitia Prof. Kighoma Ali Malima alipojiunga na NRA (National Reconciliation Alliance) na kutangaza kugombea Uraisi uchaguzi mwa kwanza wa vyama vingi mwaka 1995.

Hakuna aliyekuwa tayari kuona hilo likitokea hivyo Prof. Malima akafariki dunia katika mzingira ya kutatanisha jijini London mwaka mmoja kabla ya uchaguzi huo.

Page 39: Harakati za kisiasa tanzania na athari zake kwa waislamu wa tanzania

39

CONTD…

Katika uchaguzi wa mwaka 1995, waislamu waliokuwa wamezinduka kisiasa wakajiunga kwa wingi na CUF chini ya mgombea Uraisi Prof. Lipumba.

Mawakala wa Kanisa wakaeneza propaganda kuwa CUF ni chama cha waislamu tena wenye msimamo mkali kujaribu kudhibiti waislamu kujikomboa kisiasa na kwa kiasi kikubwa wakafanikiwa.

Page 40: Harakati za kisiasa tanzania na athari zake kwa waislamu wa tanzania

40

CONTD…

Angalau kipindi cha awamu ya pili, waislamu walipata ahueni kidogo dhidi ya ukandamizaji na hivyo kupata fursa za kujiendeleza kielimu kijamii na hata kiuchumi.

Pamoja na hayo, hakukuwa na mkakati wa kuitumia fursa hiyo adhimu kujipanga kisiasa kwa ajili ya siku za mbeleni.

Page 41: Harakati za kisiasa tanzania na athari zake kwa waislamu wa tanzania

41

CONTD…

Badala yake ni wakristo ndio walioitumia vema fursa ya Rais muislamu kuweka Makubaliano ya Maridhiano (Memorandum of Understanding-MoU) kati ya Makanisa ya Kikristo na serikali kwa maslahi yao.

Waislamu walipotaka kurejeshwa kwa Mahakama ya kadhi na Tanzania kujiunga na Umoja wa Nchi za Waislamu Duniani (OIC), Maaskofu na bunge linalodhibitiwa na wakristo likapinga kwa nguvu zote.

Page 42: Harakati za kisiasa tanzania na athari zake kwa waislamu wa tanzania

42

CONTD…

Uchaguzi wa 1995 ulionesha kuwa waislamu bado wako nyuma sana kisiasa kulinganisha na wakristo kwani wakristo walitumia hamasa ya waislamu juu ya CUF hata kuwaangusha wabunge waislamu waliokuwa CCM na kuwaweka wabunge wakristo. (Jimbo la Kigamboni – DSM).

Uchaguzi wa 2000 na 2005, waislamu walikuwa wasindikizaji tu kwani hakukuwa na mkakati wowote ule madhubuti kisiasa kushiriki kama kundi jamii lenye maslahi yake.

Page 43: Harakati za kisiasa tanzania na athari zake kwa waislamu wa tanzania

43

CONTD…

Kipindi chote cha awamu ya tatu, waislamu walijikuta wakipata madhila makubwa kisiasa na kiimani. (Mauaji Mwembechai, Zanzibar, Pemba, Morogoro, masheikh kuswekwa ndani, wahadhiri kufungwa n.k.).

Hali hii imechangia kwa kiasi fulani mwamko wa waislamu kisiasa ingawa bado hakuna umoja na mwelekeo maalum hivyo kuendelea kukosa mafanikio makubwa kisiasa kulinganisha na wakristo.

Page 44: Harakati za kisiasa tanzania na athari zake kwa waislamu wa tanzania

44

CONTD…

Uchaguzi wa mwaka 2010, harakati za kisiasa nchini ziligubikwa na mambo mawili makubwa;- Mkakati mpya wa Mfumo Kristo kutaka kuwa na

chama chake. Muafaka wa kisiasa Zanzibar uliopelekea kuundwa

kwa serikali ya umoja wa kitaifa katika ya CCM na CUF.

Matukio haya mawili yamebadili upepo wa harakati za kisiasa huku athari zake zikisabisha mabadiliko mubwa katika medani za kisiasa.

Page 45: Harakati za kisiasa tanzania na athari zake kwa waislamu wa tanzania

45

CONTD…

Muafaka wa Zanzibar, umeleta hali ya amani, udugu na mshikamano kiasi fulani Zanzibar na kupunguza hali ya uhasama kati ya wapemba na waunguja waliyojengewa kwa muda mrefu.

Matokeo ya muafaka ni kufanyika kwa mabadiliko ya katiba ya Zanzibar ambapo Zanzibar imejitambulisha kuwa ni dola kwa mara nyingine.

Aidha hali ya utaifa wa wazanzibari inazidi kujitokeza wakihiji muundo wa muungano, kunufaika na rasilimali zao na pato la taifa na hata kuhoji kuhusu Muungano.

Page 46: Harakati za kisiasa tanzania na athari zake kwa waislamu wa tanzania

46

CONTD…

Kwa upande wa Tanzania Bara, matukio ya muafaka wa Zanzibar yameleta kuzorota kwa nguvu za kisiasa za waislamu.

Wakikhofia Raisi ajae kutoka Zanzibar, wakristo wakaja na harakati za kukitia nguvu chama cha Chadema ili kiwe chama kikuu cha upinzani na ikiwezekana kuiondoa madarakani CCM inayotuhumiwa kuwalea waislamu.

Page 47: Harakati za kisiasa tanzania na athari zake kwa waislamu wa tanzania

47

CONTD…

Ingawa wakristo wameitumia CCM kujijenga, sasa wanataka kuondokana na chama chenye historia na waislamu na kuwa na chama ambacho hakina historia na waislamu.

Mpango wa Kichungaji wa Kuhamasisha Jamii Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2010 na Ilani na Vipaumbele vya Kanisa vililenga katika mwelekeo huo.

Wakristo wamejizatiti pia katika chama cha CUF upande wa bara wakisimamisha hata wachungaji kugombea nafasi mbali mbali. Kwa tiketi ya CUF.

Page 48: Harakati za kisiasa tanzania na athari zake kwa waislamu wa tanzania

48

CONTD…

Mgombea wa Chadema kuwa Padri haikuwa bahati mbaya hata kidogo. Kampeni zikapigwa wazi wazi makanisani na katika vyombo vyao vya habari ikiwemo TBC na TBC Taifa.

Harakati hizi za Kanisa zikawazindua waislamu wengi kuiona hatari inayowakabili na kuwalazimisha kujihami kwa kuunganisha nguvu zao kumhami mgombea Urais wa CCM ili kuzuia mgombea wa Chadema kushinda.

Page 49: Harakati za kisiasa tanzania na athari zake kwa waislamu wa tanzania

49

CONTD…

Kwa mara ya kwanza, masheikh wakashiriki katika siasa pasina kificho kama wafanyavyo Mapadri, Wachungaji na Maaskofu jambo ambalo linaashiria mwamko mpya kwa viongozi hawa wa waislamu.

Kilichokosekana ni stratejia ya pamoja kuweka wagombea wao katika ngazi mbali mbali hivyo kukosa ushindi kisiasa kama kundi jamii.

Bado waislamu wamegwanyika katika vyama mbali mbali jambo ambalo linawaathiri sana kwa kukosa nguvu ya pamoja kisiasa.

Page 50: Harakati za kisiasa tanzania na athari zake kwa waislamu wa tanzania

50

BAADA YA UCHAGUZI 2010

Mambo yanayojitokeza baada ya uchaguzi wa 2010 yanaashiria mkakati wa Mfumo Kristo kubadili mazingira ya kisiasa Tanzania.

Uongozi wa awamu ya nne umeonesha kwamba maslahi ya Kanisa yanaweza kuguswa (Muswada wa kufuta misamaha ya kodi, kushindwa kwa mgombea wao 2010, kushikwa nafasi nyeti na waislamu, kuongezeka idadi ya mawiziri waislamu kufikia 40%) n.k.

Page 51: Harakati za kisiasa tanzania na athari zake kwa waislamu wa tanzania

51

CONTD…

Mkakati mpya ni kuhakikisha kuwa nchi haitawaliki ili kuzidi kujenga chama chao tayari kwa uchaguzi wa 2015.

Madai ya katiba mpya ni njia ya kufikia malengo ya Mfumo Kristo kuweza kudhibiti siasa na dola katika karne ya 21 kwa kupunguza madaraka ya Urais na kulipa nguvu bunge.

Hii ni kutokana na ukweli kuwa ingawa wanaweza kudhibiti bunge kirahisi katika mazingira yaliyopo, lakini upo uwezekano wa Raisi kuwa Muislamu.

Page 52: Harakati za kisiasa tanzania na athari zake kwa waislamu wa tanzania

52

CONTD…

Kwa hiyo madaraka ya Raisi yapunguzwe na bunge liruhusiwe hata kupiga kura kumuondoa Raisi madarakani.

Katika mazingira haya, waislamu tunapaswa kutafakari kwa makini ni lipi jema kwetu? Raisi mwenye mamlaka makubwa kuliko bunge au bunge lenye malaka makubw akuliko Raisi?

Wakati ni rahisi kumkabili mtu mmoja, ni vigumu kulikabili bunge lenye idadi kubwa ya wakristo na hakuna matumaini ya idadi hiyo kupungua siku za karibuni.

Page 53: Harakati za kisiasa tanzania na athari zake kwa waislamu wa tanzania

53

CONTD…

Ingawa harakati za kudai katiba mpya ni fursa kwa kila kundi jamii kuhakikisha maslahi yake yanazingatiwa na katiba, kwa mkao wa waislamu harakati hizi zinaweza zisiwasaidie kutimiza lengo hilo. Hatuna umoja na mshikamano. Hatuna mkakati wa pamoja. Hatuna Uongozi ulio katika mfumo (central

control). Hatuna ushirikiano wa pamoja (co-ordination). Hatuna NGO’s na CBO’s za kutetea haki zetu.

Page 54: Harakati za kisiasa tanzania na athari zake kwa waislamu wa tanzania

54

NINI CHA KUFANYA?

Kung’amua mbinu za maadui wa Uislamu na kuwatahadharisha waislamu ipasavyo.

Kuweka mbele maslahi ya Uislamu na Waislamu katika harakati zetu za kisiasa.

Kuwaamsha waislamu wa kada mbali mbali ili wajitambue na kuweka mbele maslahi ya waislamu na Uislamu nchini kwa kutumia uwezo na nafasi walizonazo.

Page 55: Harakati za kisiasa tanzania na athari zake kwa waislamu wa tanzania

55

CONTD…

Kuendesha mihadhara, semina, makongamano n.k. Kuandaa machapisho mbali mbali VCD’s na DVD’s na

kuzisambaza. Kutumia vyombo vyetu vya habari.

Kujenga mtandao (network) wa waislamu nchini. Wanafunzi mashuleni na vyuoni (vyama wa

wanafunzi waislamu). Wafanyakazi maofisini. Viongozi wa taasisi za kiislamu. Vyombo vya habari.

Page 56: Harakati za kisiasa tanzania na athari zake kwa waislamu wa tanzania

56

CONTD…

Kufahamu lengo ni nini na kuwa na stratejia ya kulifikia lengo hilo kwa maslahi ya waislamu. Kuandaa mpango mkakati na mpango kazi wa

ummah. Kujiunga na vyama vya siasa kistratejia. Kuandaa wagombea wa nafasi mbali mbali za

uongozi katika serikali za mitaa na taifa. Kutoa mafunzo elekezi kwa wagombea watarajiwa. Kuandaa waraghibishi na washawishi (lobbying and

advocacy groups-wanastratejia).

Page 57: Harakati za kisiasa tanzania na athari zake kwa waislamu wa tanzania

57

CONTD…

Kushambulia badala ya kujilinda tu. Propaganda war (vyombo vya habari,

strategists etc). Research and outreach.

MWISHO