Gazeti la ANNUR

12
ISSN 0856 - 3861 Na. 1042 DHUL-HIJJA 1433, JUMANNE OCTOBA 30 Nov 1, 2012 BEI TShs 500/=, Kshs 50/= Walionajisi Qur’an umewafanya nini? Kama kosa ni kiwanja cha Chang’ombe... Aliyeuziwa aende Mahakama ya Ardhi Kumnyima dhamana ni kuchochea vurugu Watauwa, watachoma makanisa Ili muwadhuduru watu wasio na hatia Waislamu Dar waige Uamsho Zanzibar ITV mnatamani ya Parokia ya Nyamata? Kova: Usimsingizie Ponda Vikosi SMZ vyadaiwa kuuwa siku ya Idd DKT. Emmanuel Nchimbi, Waziri wa Mambo ya Ndani. KAMANDA wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova. Fikra za Kimaskani zitaiangamiza Zanzibar Uk. 6

description

Soma gazeti la ANNUR kila wiki Mara Mbili

Transcript of Gazeti la ANNUR

Page 1: Gazeti la ANNUR

ISSN 0856 - 3861 Na. 1042 DHUL-HIJJA 1433, JUMANNE OCTOBA 30 Nov 1, 2012 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

Walionajisi Qur’an umewafanya nini?Kama kosa ni kiwanja cha Chang’ombe...Aliyeuziwa aende Mahakama ya ArdhiKumnyima dhamana ni kuchochea vurugu

Watauwa, watachoma makanisaIli muwadhuduru watu wasio na hatiaWaislamu Dar waige Uamsho ZanzibarITV mnatamani ya Parokia ya Nyamata?

Kova: Usimsingizie Ponda

Vikosi SMZ vyadaiwa kuuwa siku ya Idd

DKT. Emmanuel Nchimbi, Waziri wa Mambo ya Ndani.KAMANDA wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova.

Fikra za Kimaskani

zitaiangamiza Zanzibar

Uk. 6

Page 2: Gazeti la ANNUR

2 DHUL-HIJJA 1434, JUMANNE OKTOBA 30 Nov 1, 2012 AN-NUUR

YAPO mafundisho kuwa ukimlani mtu, laana ile huzunguka k u m t a f u t a a l i y e l a a n i w a . I k i m p a t a b a s i , hufanya kazi yake. Na inampata iwapo kweli aliyerushiwa laana hiyo ni mkosa au amedhulumu. Lakini ikimkosa, kwa maana kuwa kaonewa, hana kosa, laana hiyo haianguki c h i n i i k a p o t e a . Hurudi ikamvamia yule yule aliyeituma. K w a m a a n a humrudia aliyetoa laana kumlani mtu ambaye hajamkosea wala kumdhulumu kwa lolote.

Toka atekwe Sheikh Farid na toka akamatwe Sheikh Ponda Issa Ponda, ukisikiliza kauli za viongozi wa kisiasa, makamanda wa Polisi, viongozi wa makanisa na t aa r i f a ka t i ka vyombo vya habari, utaona kuwa wote hao wameungana katika jambo moja: Kupiga propaganda kuwa nchi hii inakabiliwa na kitisho cha uharamia na ugaidi wa Kiislamu.

Tumes ik i a j i n s i ambavyo matukio ya kuharibiwa makanisa yanavyopigiwa zumari huku lile la kunajisiwa Qur’an mara mbili l i k ionekana kana kwamba hakijatokea kitu au kama kilitokea, basi si ajabu wala hakuna kosa.

Tukishajua kuwa hilo ndio lengo, busara i n a e l e k e z a k u w a tusifanye jambo lolote ambalo litawasaidia wanaopanga njama

h iz i . Kwa agenda yao hii, wanachotaka w a o n i k u o n a makanisa yakiendelea kuchomwa, Waislamu kutoka mitaani kwa maandamano maana hiyo ndiyo itatoa fursa hata kutuma vijana w a o w a k u p a n g a wakachome makanisa ili wapate kuwasingizia Waislamu.

Tuliwasikia Ijumaa ile walipopeleka Jeshi Kariakoo wakisema k u w a Wa i s l a m u walikuwa wamepanga k w e n d a k u m t o a Ponda kwa nguvu. Tuliwasikia pia siku ile baadhi ya Waislamu walipokwenda kituo cha Polisi kujua nini kimemsibu Sheikh P o n d a a m b a p o walidai pia kuwa watu walikwenda kutaka kumtoa Ponda kwa nguvu.

Na wanayasema yote hayo wakijua kuwa Waislamu hawana silaha za kuweza kupambana na mabomu na risasi za moto za Askari mpaka wakapenya wakamtoa Ponda. Ila wanasema ili kukoleza hofu na kitisho kwamba Waislamu ni watu hatari sana. Ni makomandoo wa ki-Boko Haram na Al Qaida!!!

Ukiwasikia wanatoa kauli za onyo, ni za kinafiki tu au kama njia moja wapo ya kuwachochea Waislamu waseme hatukubali. Wa n a w a t u m i a p i a M a s h e i k h a m b a o wanajua fika kuwa h a w a n a u s o w a kusimama mbele ya Waislamu na kusema jambo wakasikilizwa.

Mahesabu yao ni kuwa iwapo Masheikh hao wasiotambulika na umma wa Waislamu, watakataza jambo, kwa hoja yoyote ile, hata yenye mantiki, bas i Wais lamu na ‘ W a n a h a r a k a t i ’ watafanya kinyume chake.

Kwa hiyo kat ika nafsi zao watakuwa w a n a f u r a h i s a n a wakisikia Waislamu w a k i h a m a s i s h a n a kwenda mahakamani kwa maelfu maana watapata fursa ya kuwapiga mabomu, k u w a d h a l i l i s h a w a n a w a k e w a Kiislamu, kuongeza idadi ya Waislamu rumande na kubwa zaidi kuhakikisha kuwa ghasia zinasambaa mitaani huku wakitumia vyombo vya habari kusambaza uwongo na p ropaganda za kukoleza kitisho cha Boko Haram.

Ikitokea Waislamu w a k i p a n g a k u a n d a m a n a n d i o kabisa watasherehekea na kunywa ‘waini’. Ila watanuna wakisikia hakuna maandamano. Japo watakuwa wanatoa vitisho kuwa asithubutu mtu kuandamana, lakini ni katika namna ya kuchochea tu.

N i j a m b o l a kushukuru Mungu kwamba Masheikh Zanzibar, Waislamu na Wazanzibari kwa ujumla, wameigundua njama hii. Wametulizana M i s i k i t i n i n a majumbani mwao. Ha ta Mahakamani w a n a p a n g a i d a d i ya watu kwenda ili kuondoa wingi wa kuwapa sababu FFU.

Kwa hakika busara hii ambayo inathibitisha ile kauli ya Qur’an kuwa waumini ndio Uli l Albaab, yaani wenye ndio wenye akili, ndiyo imeifanya Zanzibar mpaka sasa ipo katika salama. Na huenda ndiyo itakayoisalimisha ile hali ya maelewano baada ya kupitia katika

kipindi kirefu cha fitna, farka na uhasama.

Ukitizama lile zoezi zima la kutekwa Sheikh Farid hutakosa kuona kuwa lengo kubwa lilikuwa ni kutengeneza mazingira ya fujo na kuhalalisha matumizi ya nguvu, ghasia na uvunjwaji wa haki za binaadamu.

H i l o l i k i t o k e a ipatikane sababu ya kuivunjilia kwa mbali serikali ya Umoja wa Kitaifa na Maridhiano na wakati huo huo kuhakikisha kwamba ajenda ya Wazanzibari kudai mamlaka kamili k u p i t i a m c h a k a t o w a K a t i b a M p y a inashindwa.

Kat ika jumla ya habari ambazo zilipewa kipaumbele na nafasi kubwa katika vyombo vya habari Tanzania, Afrika na dunia toka juzi na jana, ni lile la kushambuliwa Kanisa kule Kaduna, Nigeria na kuuliwa watu saba.

Kwa mujibu wa tarifa za vyombo vya habari ambavyo kama kawaida yao, walizipamba sana, ilidaiwa kuwa Muislamu m m o j a a l i f a n y a shambulio la kujitoa muhanga aka l ipua Kanisa Katoliki huku waumini wa Kanisa hilo wakiwa ndani wakifanya ibada.

Baadhi ya vyombo vya habari vilidai kuwa mtu huyo alindesha gari alilolijaza mabomu na kuja kuliegesha karibu na Kanisa hilo Katoliki na kulilipua.

Ha ta h ivyo kwa wanaofuatilia habari za Nigeria watakumbuka kwamba shambulio kama hilo lilidaiwa kufanyika Februari 21, 2012 nje ya Kanisa la Christ Embassy Church (CEC), Barabara ya M o r o c c o , S u l e j a , Jimbo la Niger. Katika shambulio hilo ilidaiwa kuwa Waislamu Boko H a r a m w a l i t e g a mabomu katika gari halafu wakaliegesha jirani na Kanisa hilo.

Hata hivyo, haukupita

muda uchunguzi wa kipolisi ukagundua kuwa gari hilo lilikuwa la mmoja wa waumini wa Kanisa hilo na ndiye aliyelipaki likiwa na milipuko akaondoka akiliacha likilipuka huku nyuma.

P r o p a g a n d a inayopigwa hivi sasa ni kuwa Waislamu wanapanga kulipua m a k a n i s a . A i d h a , washaanza kuambiwa kuwa wana tawi la Boko Haram. Yakiwemo mazingira ya fujo na zogo l i takalotokea FFU wakikabiliana n a W a i s l a m u w a n a o a n d a m a n a , inaweza kuwa fursa n z u r i k w a w e n y e mipango hii miovu ku l ipua Makan i sa n a k u w a s i n g i z i a Waislamu.

Lakini katika hali ya utulivu, inaweza kuwa rahisi kuwaona n a k u w a u m b u a wanaopanga kulipua makanisa yao kama walivyoumbuliwa wale waliolipua Kanisa la (CEC), Nigeria.

U t u l i v u w a Waislamu Zanzibar umesababisha sasa laana wanayowarushia M a s h e i k h w a Uamsho kuwarudia wao wenyewe. Ni vikosi vya SMZ sasa v i n a v y o o n e k a n a k u b u g h u d h i w a t u mitaani.

Na uzuri wa mambo ni kuwa Wazanzibari wote wenye mapenzi na nchi yao wametambua k u w a v i p i g o v i n a v y o t e m b e z w a n a v i k o s i h i v y o , ni namna nyingine y a k u w a c h o c h e a na kuwachokonoa wakasirike waamue kulipa kisasi. Wanazidi kuusiana na kumeza hasira na kuwa na subra.

Itakuwa vyema kama Waislamu wa Tanzania Bara na hasa Dar es Salaam watakuwa na ujasiri huu wa kumeza hasira na kusubiri katika kipindi hiki kigumu.

TAHARIRI

AN-NUUR S.L.P. 55105, Simu: Simu: +022 2400786

Cel: 0784 370 208, 0713 110148, 0755 260 087, DSM. www.ipctz.org E-mail: [email protected]

Ofisi zetu zipo: Manzese Tip TopUsangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro,

D'Salaam

MAONI YETU

Tusicheze ngoma yao

Page 3: Gazeti la ANNUR

3DHUL-HIJJA 1434, JUMANNE OKTOBA 30 Nov 1, 2012AN-NUUR

“DAMU zi l izotapakaa kwenye makanisa bado zinaonekana na hasa sehemu ambapo watoto wadogo walikuwa wakibamizwa hadi vichwa vinapasuka. Damu iliyokauka inaonekana kwenye ukuta kuashiria kwamba watoto wengi walikufa kwa kubamizwa kwenye ukuta.”

“Mwili wa mwanamke aliyebakwa na baadaye kuteswa hadi kufa kwa kuwekewa kijiti sehemu za siri umetunzwa kwenye kanisa la Nyamata. Mauaji na mateso ya kutisha yalitokea kanisani na kuna ushahidi kwamba watu wengi waliuawa juu ya altare, meza ambayo kila Jumapili Padri wao alikuwa akisimama na kugeuza mkate kuwa mwili wa Bwana (Yesu), na divai kuwa damu ya Yesu; watu wote wa Nyamata, waliouawa na walioua walikuwa kila Jumapili wakikutana kwenye kanisa hilo kusali pamoja.”

(Maka la ya Pr iva tus Karugendo, aliyoipa jina: Maua j i ya Kimbar i ya Rwanda, nani wa kujifunza? Kama ilivyochapishwa katika gazeti la RAIA MWEMA Toleo la 211 la Novemba 9, 2011)

Mara baada ya taarifa ya habari ya saa mbili usiku Ijumaa iliyopita, ITV walionyesha kibonzo kinachoandaliwa na Nathan Mpangala kama ilivyo ada yao. Kwa siku hiyo kibonzo kilikuwa kinaonyesha nyumba ambayo ni nchi ya Tanzania ikiwa inakaribia kuangamizwa na Uamsho na Boko Haram.

Ufupi wa maneno ujumbe uliobebwa na kibonzo hicho ni kuwa hivi sasa Tanzania ipo hatarini kuangamizwa na manunda mawaili: Uamsho na Boko Haram. (Magaidi wa) Uamsho wakishambulia kutokea Zanzibar, Boko Haram wamepiga kambi Dar es Salaam.

ITV wamechagua kutumia Boko Haram wakiamini kuwa ujumbe wanaokusudia kuufikisha utafika ukiwa na nguvu. Hii ni kutokana na ukweli kuwa propaganda i l i y o k w i s h a p i g w a , i m e w a f i k i s h a m a h a l i walimwengu kuamini kuwa Boko Haram ni magaidi katili wenye agenda ya kuchoma makanisa na kuuwa Wakristo nchini Nigeria.

K u l e N i g e r i a , k a m a n i t a k a v y o o n y e s h a , propaganda hiyo imekuwa iki tumika kuwachochea

Na Omar Msangi vijana wa Kikristo kuvamia vijiji vya Waislamu kuwauwa kikatili na kuharibu mali. Kwa upande mwingine, propaganda hiyo imekuwa ikitumika pia ‘kuvilazimisha’ vyombo vya dola kuwashukia Waislamu kwa hasira na hata kuuwa wakidai kuwa wameuwa magaidi.

Kwa hiyo, kutokana na haya matukio yaliyotokea hivi karibuni ya kuharibiwa makanisa baada ya lile tukio la kukojolewa Qur’an na kutekwa Sheikh Farid Hadi, mahesabu ya ITV ni kuwa ukionyesha kuwa waliofanya hivyo ni Boko Haram, basi kama ilivyo Nigeria, utakoleza chuki ya Wakris to kwa Waislamu na kuwachochea kulipa kisasi lakini pia utakuwa umeichagiza serikali iwaangukie Waislamu kwa hasira kali na kwa nguvu zote za Dola. Ukisikiliza kauli ya Rais wa Zanzibar na zile zilizotangulia ikiwemo ile ya Waziri wa Mambo ya ndani na ya Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum, Dar es Salaam, Afande Suleiman Kova, ukisikiliza pia ile ya Makamu wa Rais, Mheshimiwa Dr. Bilal katika Baraza la Idd na pia zile za akina Soraga na Masheikh wengine ambao katika jamii hawakosekani watu kama hao; utaona jinsi waliobuni agenda ya propaganda hii ya Al Qaida na Boko Haram walivyofanikiwa.

H a t a h i v y o , w a k a t i tunazingatia ujumbe huu wa ITV na Boko Haram yake, lipo jambo moja linapasa tul iangalie ambalo ITV hawakutaka kulisema na wasingependa lisemwe. Mwezi Februari mwaka huu, vijana 9 wa Kikristo walikamatwa wakitaka kulipua Kanisa moja katika Jimbo la Bauchi, Nigeria. Ikaelezwa kuwa hilo ni moja katika matukio mengi ambapo vijana wa Kikristo wamekuwa wak ichoma makanisa na kusambaza habari katika vyombo vya habari kwamba ni Boko Haram. Wakishafanya hivyo, hupata sababu ya kuvamia Waislamu na kuwauwa, kuchoma Misikiti na kuharibu mali.

“ C h r i s t i a n s C a u g h t Attempting To Bomb Own Church In Bauchi”, ilikuwa moja ya vichwa vya habari katika baadhi ya magazeti hapo Februari 26, 2012 katika kuelezea tukio hilo.

Waliokamatwa katika tukio hilo na kuonyeshwa hadharani walitajwa kuwa ni Lamba Goma, Filibus Danasa, Joshua

Ali, Danjuma Sabo, Joseph Audu, Simon Gabriel, Bulus Haruna, Yohanna Ishaya na Daniel Ayuba.

Hata hivyo, hilo halikuwa tukio la mwanzo na la mwisho, yalitajwa matukio mengine kadhaa ambapo watu waliovalia mavazi ya Kiislamu w a l i k w e n d a k u c h o m a makanisa na kisha kupeleka habari katika vyombo vya habari kwamba wao ni Boko Haram.

Mfano mwingine uliotajwa

ni ule wa tukio la Kanisa la Yenagoa, Bayelsa State ambapo Mkristo mwenye kuvalia kanzu na kofia alikamtwa akichoma kanisa. Upo pia mfano wa pale Adamawa Yola, ambapo watu watatu waliuliwa ndani ya Kanisa na ikadaiwa kuwa ni Waislamu walioshambulia. Lakini uchunguzi wa Polisi ukaonyesha kuwa waliohusika walikuwa Wakristo. Nitaje pia hapa tukio la yule mwanamke wa Kikristo, Lydia Joseph,

aliyetaka kuchoma Kanisa Bauchi akisema anafanya kazi ya Kanisa.

Mifano ni mingi, lakini la kusikitisha ni kuwa kwa vile matukio haya yamepangwa, kuratibiwa na kusimamiwa kwa malengo ya kukoleza kitisho cha Boko Haram i l i ipat ikane sababu ya kuwahujumu Waislamu, habari za matukio haya hazipewi nafasi katika vyombo vya habari wala kupewa uzito na wanasiasa ndani na nje ya Nigeria.

Chuki (prejudice) inatiaupofu wa macho na akili

“ W h e n B o k o H a r a m Became Chris t ians….”, liliandika gazeti moja na katika habari likishangaa na kuonyesha jinsi ilivyo hatari mtu kuwa na chuki isiyo na sababu. Mwandishi wa makala hiyo alionyesha kushangazwa kwake j ins i tuk io h i lo muhimu lilivofukiwa na watu kuendelea na propaganda zao za Boko Haram.

Katika kushangaa akasema, “Indeed wonders shall never end, at least not in Nigeria. There is an old saying that says that “it is easier to convince a man to burn his own house

than to convince him to give up his prejudice”.

K i l i c h o m s h a n g a z a mwandishi ni kuwa pamoja n a k u w a w a l i o h u s i k a katika jaribio la kuchoma kanisa walikamtwa na kosa kuthibiti, lakini hapakuwa na umakini wowote wala kujali kulikoonyeshwa katika kuona tatizo hilo.

B a a d h i y a w a h a r i r i wanapoulizwa ni kwa nini habari kama hizo wanazifukia, majibu yao yamekuwa kwamba habari za Wakristo kulipua makanisa ili kuwasingizia Waislamu” does not fit into

their propaganda against Muslims and the religion of Islam.”

Wanachosema bila ya kutamka ni kuwa, “Christians cannot be terrorist, terrorism is a Muslim thing.” (Wakristo hawawezi kuwa magaidi, ugaidi ni bidhaa yenye hati miliki ya Waislamu tu.)

Pengine swali la kujiuliza hapa ni je, kama watu hawa wanaweza kupanga wakaenda kushambulia Makanisa yao wenyewe na hata ikibidi kuuwa watu wao ilimuradi tu wapate kisingizio cha

Inaendelea Uk. 5

“NYAMATA, ilikuwa ni parokia ya Kanisa Katoliki na Ntarama kilikuwa ni kigango cha Parokia ya Nyamata. Ndani ya kanisa la Nyamata, waliuawa watu 10,000 na miili ya watu hawa imetunzwa kwenye kanisa hili. Katika Kigango cha Ntarama waliuawa watu 5000 na miili ya watu hawa na vitu vyao kama vile nguo, viatu, magodoro, vifaa vya maji bado vinatunzwa kwenye kanisa hili dogo.

Vifaa vilivyotumika kwa mauaji, kama mapanga, nyundo na vijiti wal ivyokuwa wakiwaingiz ia wanawake sehemu za siri bado vimetunzwa. Damu zilizotapakaa kwenye makanisa hayo bado zinaonekana na hasa sehemu ambapo watoto wadogo walikuwa w a k i b a m i z w a h a d i v i c h w a vinapasuka, damu iliyokauka inaonekana kwenye ukuta na kuashiria kwamba watoto wengi walikufa kwa kubamizwa kwenye ukuta.

Makanisa haya mawili hayatumiki tena kwa ibada. Yamebaki kama vituo vya makumbusho ya mauaji ya kimbari. Wamejitahidi kuacha kila kitu kilivyokuwa mwaka 1994, ingawa kwenye kanisa la Nyamata, wamejenga kaburi kubwa chini ya kanisa, kutunzia mabaki ya miili ya

Mauwaji ya Kimbariwahanga wa mauaji ya kimbari. Nje ya kanisa hilo wamejenga kaburi kubwa ambalo mtu unaweza kuingia na kushuhudia mwenyewe mabaki ya miili ya marehemu.

Mwili wa mwanamke aliyebakwa na na baadaye kuteswa ahadi kufa kwa kuwekewa kijiti sehemu za siri umetunzwa kwenye kanisa la Nyamata. Mauaji na mateso ya kutisha yalitokea kanisani na kuna ushahidi kwamba watu wengi waliuawa juu ya altare, meza ambayo kila Jumapili padri wao alikuwa akisimama na kugeuza mkate kuwa mwili wa Bwana, na divai kuwa damu ya Yesu; watu wote wa Nyamata, waliouawa na walioua walikuwa kila Jumapili wakikutana kwenye kanisa hilo kusali pamoja.

Watu walikimbilia kanisa kupata ulinzi. Miaka ya nyuma makanisa ndiyo yalikuwa kimbilio. Waliamini hakuna baya linaweza kutokea kanisani. Wauaji walitumia mbinu hiyo kuwahadaa Watutsi kukimbilia kanisani, ili wapate njia nzuri ya kutekeleza mauaji yao. Baada ya kuhakikisha idadi kubwa imeingia kanisani, walitoa taarifa kwa jeshi. Hivyo kwa kiasi kikubwa mauaji ya Nyamata na Ntarama, yalifanywa na

jeshi. Mabaki ya risasi na mabomu kwenye kanisa la Nyamata, matundu ya risasi kwenye kuta, milango na paa la kanisa hilo ni ushahidi wa kutosha kwamba mauaji hayo hayakutekelezwa kwa mapanga na nyundo tu bali hata kwa risasi na mabomu.

Risasi hazikuangalia mwili wa Kristu, maana kwenye kanisa hilo la Nyamata, kisanduku (Tabenakulo) kinachotumika kuhifadhi mwili wa Kristu, kilicharazwa risasi, na ni wazi hostia (Mwili wa Kristu) zilimwagika chini.

Bwana Yesu, akawaacha watu wake kuchinjana mbele yake!

Sanamu ya Bikira Maria, mama wa shauri jema, mama wa huruma na upendo, kwenye kanisa hilo nayo ilicharazwa risasi! Sanamu hiyo bado ipo kanisani na “majeraha” yake! Hapana shaka kwamba ukatili wa kutisha ulifanywa kwenye kanisa hilo. “

(Hii ni sehemu ya Makala ya Privatus Karugendo aliyoipa jina: Mauaji ya kimbari ya Rwanda, nani wa kujifunza? Makala hii ilichapishwa na gazeti la RAIA MWEMA Toleo namba 211 la Novemba 9, 2011)

HABARI

Watauwa, watachoma makanisa

Page 4: Gazeti la ANNUR

4 DHUL-HIJJA 1434, JUMANNE OKTOBA 30 Nov 1, 2012 AN-NUUR MAKALA

Kova: Usimsingizie Ponda NCHI yetu imeingia kat ika mgogoro na mtafaruku mkubwa baada ya kijana mmoja kukojolea kitabu cha Qur’an tukufu maeneo ya Mbagala na kufuatiwa na baadhi ya makanisa hapa nchini kuharibiwa na kuchomwa moto. Kwa Waislamu kitendo cha kuinajisi Qur’an ni udhalilishaji wa hali ya juu na vyombo vya dola vinapaswa kuelewa kuwa hisia za Waislamu wengi z inaathi r iwa sana na kitendo hicho. Hatua za haraka za kumkamata na kumuhoji kijana aliyehusika na kutoa maelezo kwa u m m a k u w a s u a l a hili linashughulikiwa ipasavyo, kungewatuliza w a n a n c h i w e n g i . Kuchelewa kuchukua h a t u a k u l i t o a mwanya kwa watu wengine na v ibaka kuvamia Makan i sa kupora, kuyaharibu n a k u y a c h o m a moto. Kitendo hiki k i m e w a u m i z a , k u w a k a s i r i s h a n a kuwafadhaisha Waumini wa Makanisa hayo na Watanzania kwa ujumla.

CUF Chama Cha Wananchi kinalaani v i k a l i k i t e n d o kilichofanywa na kijana kunajisi Qur’an tukufu. Huku ni kuporomoka kukubwa kwa maadili ya vijana wetu. Kitendo cha kijana huyu kilipaswa kuchukuliwa hatua mara moja baada ya taarifa kufikishwa kwenye vyombo vya dola.

Kitendo cha kijana huyu hak iha la l i sh i kwa namna yeyote ile kuvamia makanisa , kuyapora, kuyaharibu na kuyachoma moto. CUF Chama Cha Wananchi kinalaani vikali vitendo vya kihalifu na vya kuchochea mfarakano n d a n i y a j a m i i vilivyofanywa na watu na vibaka waliovamia m a k a n i s a h a y a . Tunawapa pole Waumini wote walioathirika na matukio haya.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI: WATANZANIA TUSIKUBALI KUINGIZWA KATIKA MAPAMBANO YA KIIMANI

Baada ya matukio ya kuharibu makanisa, p o l i s i w a l i e l e z a w a m e w a k a m a t a w a t u w a l i o h u s i k a na vitendo hivyo na kuwa watawafikisha M a h a k a m a n i . R a i s Kikwete alienda kukagua makanisa yaliyoathirika na kuwapa pole waumini wa makanisa hayo. Hii ilikuwa hatua ya mwanzo yakulirudisha taifa katika maelewano.

KUSHIKWA KWA SHEIKH PONDA

Katika hali hii ya kuvurugika kwa amani ku l ikochang iwa na v y o m b o v y a d o l a kutochukua hatua za haraka dhidi ya kijana al iyeinajisi Qur ’an, pol is i walimkamata Sheikh Ponda. Vyombo vya Habari vimemnukuu Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova akieleza pamoja na mambo mengine kuwa Sheikh Ponda “Amekuwa akifanya maandamano kinyume cha sheria na

hata kutishia umwagaji damu Dar es Salaam, kipindi chote tulikuwa katika uvumilivu wa kufuatilia nyendo zake kila kukicha,. . . l icha ya hali hii, Oktoba 12, mwaka huu , Ponda pamoja na wafuasi wake, walisababisha kuvunjwa makanisa us iku wa m a n a n e , u h a r i b i f u wa magari na wizi na upotevu wa vifaa katika makanisa… haya yote yameongozwa na Ponda na madhara yake ni makubwa.” (Mtanzania ALHAMISI, OCTOBA 18, 2012 05:06)

Unaweza usikubaliane na Sheikh Ponda katika maelezo na msimamo wake kuhusu dhulma dhidi ya Waislamu, lakini ni makosa makubwa kumsingizia mambo ambayo hakuyatenda. Kwa jeshi la polisi kutoa shutuma hizi ambazo hazina msingi wowote kunaongeza mfarakano ndani ya jamii.

Ha ta h ivyo , ke s i aliyoshitakiwa Sheikh

Ponda ni ya kuvamia kiwanja kisochokua c h a k e . K i w a n j a ambacho Sheikh Ponda anadaiwa kukivamia ni kiwanja kilichokuwa kinamilikiwa na East African Muslim Welfare Society kwa madhumuni ya kujenga Chuo Kikuu cha Kiislamu. Baada ya serikali kuivunja East African Muslim Welfare Society na kuanzisha BAKWATA, mali zake zilikabidhiwa BAKWATA. Anachodai Sheikh Ponda ni kuwa k iwan ja h i cho cha Waislamu kimeuzwa kinyume cha utaratibu na sheria zinazolinda mali ya Waqfu.

Kesi ya viwanja ni ya Mahakama ya Ardhi. M w e n y e k i w a n j a a l i s t a h i k i k w e n d a Mahakama ya Ardhi na kueleza kuwa kiwanja chake kimevamiwa. Kutumia polisi wa FFU kumkamata She ikh Ponda kwa tuhuma za kuvamia kiwanja ni kitendo ambacho

kimechochea vurugu. Matamshi ya Kamanda Kova yakumuhusisha S h e i k h P o n d a n a uchomaji wa Makanisa jambo ambalo hakuhusika nalo na kutoa wito kwa wafuas i wa Sheikh Ponda kujisalimisha polisi ndilo lililochochea maandamano ya Ijumaa tarehe 19 Oktoba 2012.

Jeshi la Wananchi ni la kulinda mipaka yetu siyo la kwenda kupiga raia wanaoandamana. Kitendo cha kuwaingiza barabarani wanajeshi kupambana na raia, ni kitendo cha aibu na cha kusikitisha. Serikali iepuke kujenga uhasama kati ya Jeshi la Wananchi na raia.

Kitendo cha kumnyima dhamana Sheikh Ponda na wenzake siyo cha haki.

Kuinusuru nchi isingie katika mgogoro, Sheikh Ponda na wenzake wapewe dhamana. Hiyo ni haki yao ya msingi. Mwenye kiwanja apeleke malalamiko yake Mahakama ya Ardhi na kesi hiyo ya kiwanja ihamishiwe huko.

Baada ya uchaguzi mkuu wa 2010, Rais Kikwete alizungumzia mgawanyiko wa kidini uliotokea wakati wa uchaguzi. Hata hivyo hajachukua hatua zozote za kuleta maelewano ya kujenga utamaduni wa kuvumiliana baina ya Watanzania wenye imani tofauti. CUF, Chama Cha Wananchi kinatoa wito kwa Watanzania kuwa na mjadala wa kujenga mahusiano mazuri na kuvumiliana baina ya dini na madhehebu hapa nchini. Mijadala hii ifanyike katika ngazi ya ki ta i fa na kat ika maeneo ya wananchi na yahusishe viongozi wa dini wa taasisi zote, vyama vya siasa na vyama vya kijamii kwa lengo la kujenga na kuimarisha utamaduni wa kuvumiliana n a k u h e s h i m i a n a . Wa t a n z a n i a w o t e wajisikie kuwa ni raia wa daraja la kwanza katika nchi yao.

P r o f . I b r a h i m Haruna Lipumba

Mwenyekiti - CUF

Prof. Ibrahim Haruna Lipumba Mwenyekiti - CUF

Page 5: Gazeti la ANNUR

5DHUL-HIJJA 1434, JUMANNE OKTOBA 30 Nov 1, 2012AN-NUUR

Chuki (prejudice) inatiaupofu wa macho na akili

k u w a b a m b i k i z i a u o v u Waislamu, wakijengewa maz ing i r a ya ku fanya kazi hiyo bila kufahamika wataitumia kwa kiwango gani? Wakipata fursa pale wanapokuwa miongoni mwa FFU wanaotumwa kusambaratisha maandamano ya Waislamu, wanapiga watu kiasi gani? Je, wakiwa na silaha za moto wataona vibaya kuzitumia? Ukiwa na Askari Magereza walio na chuki ya kiwango hicho, ufedhuli gani wanawafanyia Wa i s l a m u w a l i o i n g i a mahabusi kwa tuhuma za kuchoma makanisa?

Inapotokea kwa mfano maandamano na hali ya ghasia kama ilivyotokea ‘alipotekwa’ Sheikh Farid, ambapo vijana walikuwa wakiharibu na kupora mali ovyo, unafikiri walio na agenda kama hizi za Wakristo wa Nigeria watafanya nini? Si watachoma makanisa na baa halafu isemwe kuwa ni Waislamu?

Na hapa nichukue fursa hii kuwapongeza Masheikh wa Uamsho kwa juhudi kubwa waliyofanya kuwatuliza watu wasitoke barabarani kuandamana. Lakini pia niwapongeze Waislamu wa Zanzibar waliosikia na kuwatii viongozi wao wakazuiya hasira zao hata walipoona Sheikh wao kadhalilishwa kwa kunyolewa ndevu na kuachwa sharubu kama Yahudi.

Kujizuiya kwao ndio k u m e l e t a s a l a m a k w a Waislamu na kwa wananchi wa Zanzibar. Kujizuiya kwao kunawaumbua wenye nia mbaya na Zanzibar. Sasa wanajikuta wakivamia watu ovyo majumbani mwao na kuwapiga bila ya sababu. Wamekasirika kwa sababu wamekosa kisingizio. Na hiyo ndiyo dawa yao. Ulimwengu mzima sasa unashuhudia kuwa kama wapo watu wanaovuruga amani, kama wapo watu wanaleta fujo na kuharimu mali za watu, basi sio taasisi za Kiislamu na viongozi wao.

Hapana shaka inaweza isionekane kuwa agenda ya Zanzibar ni hii hii ya Kanisa. Lakini kama ukijenga mazingira ya kuvuruga maridhiano yaliyofikiwa na kuwapa watu uhuru wa kudai aina ya muungano wenye masilahi nao, si ndio vile vile unavunja nguvu ya Kanisa Zanzibar? Hawatakubali. Lakini na wenye uchungu na Uislamu, nao wasiwape sababu.

Pengine ili kuona hatari ya propaganda hii ya Boko Haram inayopigwa nchini, tuangalie yanayojiri Nigeria

Inatoka Uk. 3

baada ya wanaodaiwa magaidi kushambulia Kanisa. Mara baada ya kulipuka bomu Jos lililouwa watu watatu, ambapo baadae mtuhumiwa mkubwa alikuwa Kasisi wa Kanisa (COCIN Church), Ishaya Izam, Vijana wa Kikristo waliodaiwa kuwa na hasira walivamia nyumba za Waislamu na kuanza kuuwa. Shirika la habari la AFP, liliripoti tukio moja ambapo mwandishi wake alishuhudia Waislamu kadhaa wakiuliwa na vijana hao.

“The attack sparked a riot by Christian youths who went on a killing spray. At least two (2) Muslims were killed by the rampaging agreed Christian Youths. The two men were dragged off their bikes after being stopped at a roadblock set up by the Christian Youths. Also, a row of Muslim-owned shops was also burned.”

Mwandishi huyo wa AFP anasema kuwa Waislamu wawili walipachuliwa kutoka katika pikipiki waliyokuwa wamepanda wakapigwa na vijana wa Kikristo hadi kuuliwa. Na katika sehemu nyingine wakawa wanavamia maduka ya Waislamu na kuyachoma moto.

“Kaduna Bomb blast: Rampaging Christian Youths Kill Over 40 people.”

“100 Dead: Boko Bombs Church; Christians Kill Innocent Muslims in Nigeria; Media Spins Story.”

“Murdering Innocent Peop le i s Te r ro r, No t

Reprisal!”Hivi ni baadhi ya vichwa

vya habari katika magazeti ya Nigeria vinavoonyesha hatari na hasara inayoletwa na wendawazimu huu wa propaganda za Boko Haram.

Kwamba ikisharipotiwa k w a m b a B o k o H a r a m wamelipua Kanisa, iwe ni

tukio la kweli au la kupanga (false terror attacks), vijana wa Kikristo waliojazwa chuki kama wale Wakatoliki waliowachinja Wakatoliki wenzao wa Kitutsi ndani ya Kanisa, huvamia mitaa ya Waislamu na kufanya mauwaji pamoja na kuchoma Misikiti.

K a t i k a t u k i o m o j a Kaduna Waislamu wapatao 40 waliuliwa wengine kwa kuchomwa moto akiwemo Afisa wa Polisi Mkristo na mwanajeshi waliojaribu kuwazu iya v i j ana hao kuacha mauwaji holela. Maofisa hao wa Polisi na Jeshi walichinjwa kikatili na vijana hao wa Kikirsto katika eneo la Nassawa, Kaduna kama il ivyoripotiwa na vyombo vya habari. “Brutally slaughtered”, ndiyo maneno yaliyotumiwa na baadhi ya magazeti kuelezea ukatili waliofanyiwa askari hao.

Ukizingatia kiwango hiki cha ukatili kinachofanywa na vijana wa Kikristo Nigeria waliojazwa chuki dhidi ya Waislamu, sasa jiulize, hali itakuwa vipi kama utakuwa na vijana kama hao katika FFU, Vikosi vya SMZ na hata JWTZ halafu uwape fursa ambapo watafanya ukatili wao bila kujulikana!

Kama utayatafakari haya na ukirejea nyuma na kuzingatia zile kauli za baadhi ya askari wa l iokuwa wak i t amba kwa ubaya waliowafanyia wanawake na mabinti wa Kiislamu Pemba wakati wa chaguzi zilizopita, ukizingatia pia yale wanayofanyiwa wanawake wa Kiislamu na wanajeshi wa Marekani kule Iraq na Afghanistan; hapana shaka utaona busara ya hali ya juu waliyokuwa nayo viongozi wa Uamsho waliowatuliza Wazanzibari wasitoke mitaani.

Kumeza hasira si woga tuangalieyaliko masilahi makubwa zaidiJAMBO ambalo Waislamu w a D a r e s S a l a a m wanatakiwa wajiulize ni hili: kama kuna watu kwa chuki za kikabila walizojazwa waliweza kuwakusanya Wakatoliki wenzao ndani ya Kanisa wakawauwa, wakibamiza vichwa vya vitoto vichanga ukutani a m b a p o t u n a a m b i w a kuwa mpaka leo damu ipo ukutani; hivi tunatarajia hali itakuwaje Tanzania kama propaganda hi i inayojengwa ya Boko H a r a m u i t a f a n i k i w a kuwaingia na kuwakolea Wakristo wa mitaani mpaka wale walioko katika FFU na JWTZ? Je, hatuoni kuwa Jihad kubwa kwetu hivi sasa itakuwa kufanya lolote la kuwafanya wanaopika fitna hii waumbuke?

Alizungumza kwa uchungu sana Khatib katika hotuba ya Idd pale Msikiti wa Mwenge

ambapo nami niliswalia Idd el Adh’ha Ijumaa iliyopita. Kwa hakika nampongeza kwa jinsi alivyowarejesha waliokuwepo katika moyo wa kuupenda Uislamu na kuwa tayari kuupigania na kuwahami Waislamu.

Nadhani katika hali kama hii na katika mazingira tuliyo nayo Waislamu hivi sasa, jambo muhimu ni kuangalia lipi litakuwa na masilahi zaidi na Uislamu na Waislamu.

Kama Waislamu wataweza kujitolea kuhakikisha kuwa mawakili wa kuwatetea w e n z e t u w a l i o n d a n i wana l ipwa, fami l ia za walioko ndani hawakosi chakula na huduma nyingine muhimu na tunawatembelea walioko ndani kuwafariji na kuwapa mahitaji muhimu, huku tukijizuiya hasira zetu tusifanye jambo la kuongeza idadi ya walioko ndani au

kuwaletea madhara makubwa zaidi Waislamu na wananchi wasio na hatia mitaani, hilo nadhani itakuwa tumefanya jambo kubwa kwa Uislamu, Waislamu na nchi.

Ile Sheikh Farid, Sheikh Msellem na viongozi wenzao wa Uamsho kuwatangazia Waislamu wa Zanzibar kuwa watulie, wasiandamane, sio kuwa ilikuwa ni woga. I le kuwa Waislamu wa Unguja wamesikia na kutii maagizo ya viongozi wao kuwa wasiandamane hata kama Masheikh wa Uamsho watanyimwa dhamana, haina maana kuwa Waislamu hao ni waoga au wamewatelekeza viongozi wao. Lakini hiyo inaonyesha ujasiri mkubwa wa kumeza hasira kwa masilahi makubwa zaidi ya Uislamu.

Inaendelea Uk. 8

Makala

VIONGOZI wa Taasisi ya UAMSHO kabla ya kukamatwa.

Page 6: Gazeti la ANNUR

6 DHUL-HIJJA 1434, JUMANNE OKTOBA 30 Nov 1, 2012 AN-NUUR MAKALA

M A S K A N I z a C C M zinafahamika na ki la mwenye kufuatilia siasa za Zanzibar. Ni genge la watu ambao wengi wao hawakupata bahati ya kwenda skuli ambao walikusanywa na utawala wa Dr. Salmin Amour na kujengewa majengo kwa ajili ya kupotezea muda na kushiriki shughuli za siasa za chama hicho. Maskani kuu n i i l e inayo i twa KISONGE iliyopo katika eneo la Michenzani round about.

Fikra za kimaskani zote na malengo yake ni sawa na maskani hii kaka ya KISONGE. Lengo ilikuwa ni kuwatumia wanamaskani kama hazina ya kuzalishia nguvu kazi inayohitajika katika hujuma mbali mbali zinazokilenga chama cha CUF, wafuasi wa CUF, Wazanzibari wanaoipenda nchi yao, viongozi wa CUF na Wazanzibari wenye asili ya Pemba.

Genge h i lo l i l i pewa maa r i f a , u juz i , mb inu na uwezo wa kutosha ili kutekeleza kwa ufanisi hujuma dhidi ya walengwa. Kwanza kabisa walikusanywa vyema na kufundishwa hadithi za uongo na propaganda za chuk i z i l i zo tungwa na akina Mrina, Mattoke na Maliamkono kwamba Waarabu, Wazanzibari wenye ngozi nyeupe na Wapemba, si Wazanzibari halisi. Ni wageni waishio kwa ihsani hapa Zanzibar. Elimu hiyo i l iyokuwa ikisimamiwa na viongozi wakubwa wa serikali kwa wakati huo, iliwafundisha wana-Kisonge maarifa kwamba wenyeji halisi wa Zanzibar ni wale Wazanzibari wenye ngozi nyeusi na wenye asili ya Kibantu (Kibara).

Ni vyema hapa tuwekane s awa kwanza kwamba kutokana na sababu za kihistoria za kiuchumi (si za kisiasa) za enzi hizo, sura ya mjengeko wa kiasili na kikabila watu katika jamii za visiwa viwili vya Unguja na Pemba i l i tofaut iana sana. Kisiwa cha Pemba kilichokuwa zaidi ni kwa ajili ya kilimo cha karafuu ni mjengeko wa jamii yake ulikuwa Washirazi (watu wenye asili ya Iran) na Waarabu wanafanya asilimia kubwa ukilinganisha na Wabantu (wenye asili ya bara) wachache. Kisiwa cha Unguja ambacho kilikuwa zaidi ni cha kibiashara na maofisi ya serikali na makao makuu ya utawala, kinaonyesha kuwa na mjengeko wa idadi kubwa

Fikra za Kimaskani zitaiangamiza Zanzibar

Tunachotaka ni nchi yetu yenye mamlaka kamiliWazanzibari tumeapa hatuondoki katika mstari huo

Na Ahmed Omar Khamis

ya Washirazi na Wabantu ik i fuat iwa na Waarabu na wachache kutoka asili nyenginezo.

Mjengeko huu ulitumiwa vibaya na wakoloni wa Kiingereza katika siasa za miaka ya 1960 ya kupigania uhuru kuwagawa Wazanzibari wa Unguja na Pemba katika siasa zinazopingana kikabila. Wingi wa watu wenye asili ya Kibantu Unguja uliwafanya wanasiasa na watawala wa Zanzibar wa baada ya mapinduzi kuihesabu Unguja kuwa ndio Afika ya kweli na iliyonasibika na mapinduzi ya 1964. Kinyume chake, Pemba kwa kuwa na watu wachache wenye asili ya Kibantu ikazingatiwa kuwa mapinduzi ya 1964 hayakuwa yao. Wakati ukweli ni kwamba Wazanzibari katika siasa za miaka ya 1960 waligawanyika kwa misingi ya makabila yao na sio kisiwa gani anaishi. Afroshirazi ilikuwepo Pemba na Unguja kama ilivyokuwa kwa ZNP na ZPPP.

Kilichofanywa na kina Mrina, Mattoke, Maliamkona na Mapuri ni kuwapa wana-Kisonge picha ya uongo ya Pemba kutokunasibika na ASP na Mapinduzi badala

yake kuinasibisha na ZNP (HIZBU) na ZPPP na hivyo kuwajenga wana-Kisonge waone Pemba na Wapemba ni maadui wa Unguja na serikali ya mapinduzi inayotawala hivi sasa.

Hata h ivyo , h i s tor ia ya ASP na mizizi yake inaonekana kutokukubaliana na uongo huo kwani Pemba ina mchango mkubwa katika uanzishwaji wa ASP pamoja uendelezaji wa chama hicho. Pemba ndio iliyokuwa ngome kuu ya Ushirazi. Jumuiya ya Wash i r az i (Sh i r az i Association) ambayo ni mmoja ya wazazi wa ASP haikuwepo hapo kabla. Kuzuka kwa Jumuiya ya Washirazi ni pale Washirazi wa Pemba walipokwenda k w a w a k o l o n i k u d a i uwakilishi wao baada ya kuona Jumuiya ya Waafrika ( A f r i c a n A s s o c i a t i o n ) i l ikuwa ikiwawakil isha Waafrika wenye asili ya kibantu peke yao. Kama ishavyoelezwa pia hapo kabla kuwa Waafrika kutoka bara walikuwa wamejikita zaidi katika kisiwa cha Unguja kuliko Pemba na Washirazi wal ionekana wal i j ik i ta zaidi Pemba kuliko Unguja, hivyo Jumuiya ya Waafrika

kuonekana kutokuwa na nguvu za kuwawakilisha Washirazi ambao ndio wengi katika kisiwa cha Pemba.

Hivyo Washirazi walianza kujikusanya na kuunda jumuiya yao iliyojulikana Jumuiya ya Washirazi, au Shirazi Association. Jumuiya hi i i l ianzishwa mnamo mwaka 1940 na Washirazi huko Pemba. Muasisi wa Jumuiya hii alikuwa Bwana Ali Sharif wa Pandani. Wakati akitoa hoja ya kuanzisha jumuiya hii, Bwana Ali Sharif alimuandikia barua Mkuu wa Wilaya wa serikali ya kikoloni huko Pemba kwamba kati ya wenyeji 73,000 wa Pemba asilimia kubwa yao walikuwa Washirazi. Hivyo basi alifafanua kwamba jumuiya yao ina malengo ya kujaribu kupata uwakilishi wa kitaifa kwa kuwa jumuiya ya Waafrika inayotetea maslahi ya watu wenye asili ya kibantu ilikuwa haiwawakilishi watu wa Pemba kwa kuwa watu wa asili hiyo walikuwa wachache huko Pemba.

Jumuiya ya Washirazi iliundwa huko Unguja katika mwaka wa 1941 mwaka mmoja baada ya kwisha kuundwa huko Pemba. She ikh Thab i t Kombo

muanzilishi wa jumuiya hiyo huko Unguja alimuandikia ka t ibu wa Jumuiya ya Washirazi Pemba kujiunga na jumuiya yao. Barua hii mpaka leo ipo pale nyaraka za Taifa Kilimani. Maombi hayo yaliambatanishwa na orodha ya wanachama 54 wakiongozwa na Sheikh Ameir Tajo. Hapo baadae baada ya siasa kuanza viongozi wa African Association na Shirazi Associat ion kwa upande wa Unguja walikubaliana na viongozi wa Shirazi Associat ion wa Pemba kuunda chama cha ASP. Hivyo basi akina Sheikh Ali Sharif (mwasisi wa Shirazi Associataion) na Sheikh Mohamed Shamte (Mwenyekiti wa Shirazi Associataion) ndio watu muhimu waliokikaribisha chama cha ASP Pemba na kuitafutia uungwaji mkono. Kwa kiasi kikubwa kutokana na jitihada za watu hao chama cha ASP kilijipatia umaarufu na uungwaji mkono na umma wa Wapemba. Haikuwa rahisi kwa Africa Association kufanya siasa bila ya kuugana na Shirazi Associat ion kwani kwa Zanzibar nzima Wazanzibari wenye asili kutoka bara walikuwa 19%, Waarabu 17% na Washirazi 53%.

Takwimu za uchanguzi mwisho wa mwaka 1963 kabla ya mapinduzi zinaonyesha kuwa ASP ilishinda kwa 44.39 (wakati hivi sasa CCM inapata ushindi wa chini ya asilimia 10) huko Pemba wakati ZNP/ZPPP ilishinda kwa 45.79 huko Unguja. Hii inadhihirisha kuwa ushindi wa ASP ulisababishwa na mjengeko wa makabila katika visiwa viwili hivi na sio Upemba na Uunguja. Mwarabu, Mshirazi, Mbantu wote walikuwa na misimamo yao ya kisiasa isiyobadilika bila ya kujali walikuwa Unguja au Pemba.

Uunguja na Upemba uliletwa na watawala baada ya kukidharau kisiwa cha Pemba na kukiweka nyuma kimaendeleo kwa miaka mingi tokea mapinduzi ya 1964. Ndio maana ASP ilishinda kwa 44.39 katika mwaka 1963, lakini CCM ilishinda kwa 10% katika uchaguzi wa 2010 kwa sababu Wapemba wote waliuchukia u tawala b i la ya kuja l i Ubantu, Uarabu au Ushirazi wal ionao. Hata mzal ia cha kibantu kindakindaki ambae anatokana na mizizi ya ki-Afroshirazi huko Pemba hutamkuta akiunga mkono CCM kwa kuwa nae pia amedharauliwa bila kujali ubantu wake. Baada kupindishwa kwa ukweli

Inaendelea Uk. 7

POLISI wakiwa kwenye doria, Zanzibar hivi karibuni.

Page 7: Gazeti la ANNUR

7DHUL-HIJJA 1434, JUMANNE OKTOBA 30 Nov 1, 2012AN-NUUR MAKALA/HABARI

Fikra za Kimaskani zitaiangamiza Zanzibar

Inatoka Uk. 6

huo na kufundishwa hadithi za uongo wana-Kisonge walijazwa chuki dhidi ya Wapemba na Wazanzibari wenye asili zisizokuwa za kibantu.

Mabango maalum ya KISONGE yakatengezwa a m b a y o k a z i y a k e n i kuwatukana wafuasi wa CUF, viongozi wao na watu wenye asili ya kisiwa cha Pemba. Ujumbe wa kila aina wa kuwambia watu hao si wazawa, ni vijukuu vya Sultani, ni watoto wa wakoloni, ni Mahizbu n.k ulikuwa ukichapishwa katika mabango hayo huku vitendo hivyo vikisherehekewa na SMZ/CCM.

Maskani ya Kisonge na nyenginezo, ndizo zilikuwa ndio hazina ya kuchagua watu kwa ajili ya askari polisi, jeshi na vikosi vya SMZ. Ajira nyingi za kiaskari zilitolewa kwa wanamaskani ili kuhakikisha nidhamu ya utiifu kwa dola/CCM na chuki dhidi ya wapinzani wa serikali na Wapemba inajengewa misingi imara ndani ya idara hiyo.

Hapa ndipo askari polisi na askari wa vikosi vyote vya SMZ walipopata nidhamu yao walionayo sasa ya kufanya majukumu yao ya kiaskari kwa kuongozwa na misingi ya chuki na uonevu. Askari polisi au askari wa kikosi anaona fakhari kumshambulia raia bila ya kosa na hata

kumuua akigundua tu ndie yule aliyefunzwa kuwa ni adui yake. Utashangaa kama tulivyoshangaa kuona askari anapiga teke hata baiskeli au vespa ilimuradi anadhani ni ya Mpemba au CUF. Askari hawa ndio hao hao tulionao leo eti wanatulinda.

Walidhibitiwa kidogo na nguvu ya mar idh iano , lakini sasa kwa kasi kubwa wanarejea katika misingi yao ya awali baada ya Dr Shein kuanza kuupoteza muelekeo na misingi ya maridhiano hayo.

Baadhi ya Maskani ndizo

zilikuwa hazina ya kuwaajiri maharamia wajulikanao kama MAJANJAWIRI . Majanjawiri si askari rasmi. Hii ni hatua ya awali kabla hawajawa askari kamili anaevaa sare na kukabidhiwa s i laha . Manjawir i wao hutumika kuwavamia watu,

kuwapiga kwa kutumia marungu na mapanga ili ionekane sio chombo cha dola kilichotumika kufanya hujuma hizo. Majanjawri wakifanya maonevu zaidi kuliko askari polisi kwani hata askari polisi na askari vikosi baadhi ya wakati huvua sare na kubeba silaha zao na kujiunga na vikosi vya majanjawiri, kushambulia watu. Hizi ndio Maskani na kazi zake katika siasa na utawala wa Zanzibar ilivyokua. Katika enzi hizo hazina kubwa ya serikali ilitumika kugharamia shughuli za uharamia za watu hawa kwa kulipwa pesa nyingi, vyakula na starehe kadhaa wa kadhaa. Wakati huo huo maeneo mbali mbali yakinyimwa mgao wa huduma za maendeleo kwa fedha nyingi kupotelea katika uharamia huu.

Maskani ndio hazina ya wapiga kura mamluki siku za chaguzi zinapofika. Mbinu na mafunzo ya kuvuruga uchaguzi kwa kujiandikisha mara nyingi na kupiga kura nyingi hutolewa hapo. Hapa huambiwa kuwa kura zenu kumi kumi zinakwenda kuzuia usultani usirejee Zanzibar na Waarabu (Wapemba) wasichukue serikali watakuja kuwafagilisha tena Waafrika kwa kutumia maziwa (matiti) yao. Huambiwa kura zenu kumi kumi zitazuia Waarabu wasichukue dola wakaja wakawalipizia kisasi kwa kuwachinja na kuwatia katika matanuri ya mbata kama walivyowafanya wao babu zenu huko nyuma.

ALICHOKIFANYA Amani Karume na Maalim Seif Novemba 9, 2009 kupitia Maridhiano na kuunda serikali ya umoja wa kitaifa ni pamoja na kulidhibiti kundi la wahafidhina lenye fikra potofu na misingi miovu ya Kimaskani. Azma kubwa ya hili ni kuwafanya Wazanzibari waongozwe na Uzanzibari wao katika kuishi kwa amani na utulivu katika nchi yao na kuyatafuta maslahi yao. Kuondoka kwa utawala wa Mheshimiwa Amani Abeid Karume imechukuliwa na wahafidhina kua ni sawa na kuirejesha Zanzibar katika mikono yao na mtandao wao ndani ya sura mpya kabisa ya kuwateka nyara washirika wa maridhiano hayo na serikali ya umoja huo wa kitaifa.

Ta y a r i w a m e j a r i b u kumchimba Dr Ali Mohamed Shein a iwachie kamba ya maridhiano ambayo Amani Karume na Maalim Seif waliishika na baadae kumkabidhi Dr. Shein aienzi. Amekuwa kwa muda mrefu akishawishiwa kuwaweka kando viongozi wa CUF

Shujaa Amani KarumeAliamua kubakia kwao Zanzibar kuliko Dodoma

serikalini na kuwawacha kama wageni waalikwa wa GNU. Lengo ni kuwa viongozi hao wa CUF serikali wabakie hawana sauti yoyote yenye nguvu, si kimaamuzi wala kiushauri.

K u n d i l i l i l o a s i s i maridhiano ikiwemo kamati ya watu sita (six comandos), tayari limeshatangaza wazi msimamo wake wa kutaka mabadiliko ya muungano kutoka mfumo na muundo uliopo sasa wa serikali 2 kwenda katika muungano wa MKATABA. Katika waasisi wa maridhiano na serikali ya umoja wa kitaifa, ambae hajaweka hadharani msimamo wake huo ni Mheshimiwa Amani Karume peke yake.

Baada ya hilo kufanyika, wana maskani na wahafidhina wamejaribu kumteka Dr Shein na kumfanya aamini kuwa wana CCM hawana

haki ya kuweka msimamo wa mabadiliko ya mfumo na muundo wa muungano kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na sera ya chama chao. Akina Mhe Mansoor na Mzee Moyo ambao ni machampioni wa maridhiano ndani ya CCM wanaendelea kutishwa kwa kauli kali kali, kutukanwa, kufanyiwa vitendo vya kuwakatisha tamaa, na kudharauliwa kutokana na misimamo yao ya kudai mabadiliko ya mfumo wa muungano. Lengo ni kuwatisha na kuwafanya waamini kwamba fikra, misingi, ushawishi na nguvu za KISONGE zimerejea katika safu yake ya awali na zimeshika hatamu upya. Wanavyoamini wahafidhina akina Mhe Mansoor na wenzao watamini kwamba misingi, fikra na nguvu za maridhianao na serikali ya umoja wa kitaifa iliyotandikwa na Amani Karue na Maali Seif bila shaka ishapigwa teke na wao watakuwa woga wa kusimamia misimamo yao ya mabadiliko.

Vitimbi kadhaa wa kadhaa DKT. Amani Abeid Karume, Rais Mstaafu SMZ. Inaendelea Uk. 9

RAIS wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein.

Page 8: Gazeti la ANNUR

8 DHUL-HIJJA 1434, JUMANNE OKTOBA 30 Nov 1, 2012 AN-NUUR

Yuko mtengeneza filamu mmoja ambaye baada ya kukamilika kazi yake, ilibidi aingie hasara ya kurudia kuipiga upya. Sababu ya kufanya hivyo ni kuwa alikosea kuchagua makazi ya mmoja wa wachezaji. Mchezaji huyo akiwa mitaani alionyeshwa kama mlevi wa kupindukia wa pombe za kienyeji, anayevaa hovyo, nguo chafu, zilizochanika, k a n d a m b i l i m i g u u n i zikiwa za rangi tofauti na zilizofungwa kwa kamba kwa kukatika. Haangalii familia kwa hiyo inabidi watoto wa kike pamoja na mama yao wapite kwa washikaji wao kujiuza ili wapate chakula. Hata hivyo, mtu huyo akiwa nyumbani ikaonyeshwa nyumba yake ikiwa nzuri yenye makochi mazuri, kabati zuri la vyombo, yenye taili, almuradi safi kabisa ya mtu mstaarabu mwenye mshahara mkubwa au mfanyabiashara aliyefanikiwa kiasi. Kwa hiyo ukiangalia nyumba inamkataa mtu huyo. Hailingani naye. Nyumba inaonekana kuwa ni ya mtu mstaarabu, sio ya ‘Chapombe’ asiyejitambua anayeshinda kilabuni kupiga masanga ambaye hata nguo zinamshinda kufua.

Wakati wa Baraza la Idd, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dr. Ali Mohamed Shein, ametoa kauli kali kama walivyotoa viongozi wengine wa kisiasa na vyombo vya Dola wakionyesha kuwa nchini kuna hali ya hatari. Na ha ta r i yenyewe n i kuwa Waislamu wanaleta vurugu mitaani, wanachoma Makanisa na kufanya vitendo vya kiharamia.

Hal i i l ivyo Zanzibar hivi sasa inaikataa kauli ya Rais Shein. Zile nasaha za Sheikh Farid na Viongozi wa Uamsho kwa Waislamu n a Wa z a n z i b a r i k u w a wasihamaki, watunze amani ya nchi, na jinsi Waislamu walivyotii na kutulizana, inafanya makemeo ya Rais Shein yakose mashiko na kubaki yakielea hewani. Imekuwa kama lile onyo katika Uislamu kwamba ukimlaani mtu kama hilo unalomlani kwalo hanalo, kwa maana kuwa umenuonea, laana hiyo inakurudia.

Hivi sasa laana inairudia serikali na vikosi vyake. Ndio wanaoonekana wakipita mitaani kupiga watu wasio na hatia. Na maadhali Waislamu wataendelea kuwatii viongozi wao wakaongeza ujasiri wao katika kuzuiya hasira zao, hautapita muda, maadui wa Uislamu na wasio itakia

Tuangalie silaha yenyekufaa kwa kipindi hiki

mema nchi hii wataumbuka. Ile dhamira yao ya kuvuruga maelewano yaliyopo Zanzibar hivi sasa itafeli. Kwa Bara ile agenda yao ya kuizamisha nchi hii katika ule ukatili waliofanyiana Wakatoliki ndani ya Makanisa ya Rwanda itafeli pia.

Wiki iliyopita tumemsikia yule mchungaji kule Tanga akidai kuwa kuna watu (Waislamu) waliwasha moto katika makanisa mawili, lakini kwa nguvu za Yesu moto huo ukazimika kimaajabu kabla ya kuleta madhara. Halafu baada ya kutoa madai hayo, katika staili ile ya Paroko Lwambano, anaichagiza

serikali kuchukua hatua.Tufanye subra, hatutapoteza

kitu. Na subra ni katika mwanzo wake. Punde tu Allah atawaumbua kama alivyowaumbua wafadhili wao kat ika “Operat ion Cyanide” na “Lavon Affair”.

Ila tu tufahamu kuwa watu hawa wanapotaka lao hawaoni vibaya wala kuchoka. Sasa tusije kudhani kuwa tutasalimika kwa harakati za moto wa kifuu.

Iraq na Pakistan kwa vile wote ni Waislamu, walilipua Misikiti ya pande zote mbili kwa zamu. Unalipuliwa M s i k i t i w a S h i a k w a shambulio la kupanga, kisha wanatangaza katika vyombo

vya habari kuwa waliohusika ni Sunni. Shia wanakasirika. Wakitoka hapo, wanalipua Msikiti wa Sunni, wanauwa dazeni ya Wasuni, wanadai ni Shia wanalipa kisasi. Sunni wanakasirika. Matokeo ni kuwagawa na kujenga uhasama mkubwa kati ya Sunni na Shia. Kwanza wote Waislamu, wote Wairaq (Pakistan), lakini wanajiona maadui wao kwa wao na kumwacha adui kando akiwahujumu wote.

Hapa Tanzania maadhali ni Waislamu na Wakristo, yatal ipul iwa makanisa. Wakris to watakasir ika . Msikiti utalipuliwa, Waislamu w a t a k a s i r i k a . M w i s h o

wake inakuwa uadui baina ya Waislamu na Wakristo. Ikifikia hapo hakuna nchi tena.

Kwa sasa inaonekana kuwa Wakristo hawaoni hatari hii maadhali wakisema serikali inawabamiza Waislamu bila kujua kuwa fitna ikikolea hatasalimika mchungaji wala Polisi. Au hatusikii vituo vya Polisi vinavyolipuliwa Pakistan na mamia ya Polisi kuuliwa?

Maadhali Waislamu ndio wamebaki na akili zao timilifu na busara ya kuona hatari ya mchezo huu hatari wa propaganda za Boko Haram, basi wajue kuwa ndio wenye dhima ya kuinusuru nchi hii.

Kama ambavyo mababu zao Sheikh Suleiman Takadir, Sheikh Hassan Bin Ameir, Mshume Kiate, Dossa Aziz, Sheikh Mohamed Ramiya na wengine; walivyofanya harakati makini zilizotupatia uhuru, ndivyo wajukuu zao hivi leo wanavyotakiwa kufanya harakati zilizopangwa vyema ili kuinusuru nchi hii na machafuko ya kidini yanayochochewa kila uchao. Lakini pia kuiepusha nchi hii katika balaa la kutumiwa na mabeberu kama uwanja wa Vita Kichaa ya Ugaidi. Vita ambayo ikiingia, hasalimiki Padiri, Sheikh wala Polisi.

Kwa Zanzibar wana hiyari, kukubali kufarakanishwa kati ya “wanaotaka kupumua na wasiotaka” warejee kwa Bamkwe, Janjawid na kero zao za muungano; au wazindukane wachukue mwelekeo mpya utakaowapa heshma kama watu wenye fikra huru na pevu.

The USS Liberty was attacked by unmarked planes and torpedo boats in international waters during the Six Day War between Israel and the Arab States.

T h e a t t a c k o n t h e surveillance ship lasted 75 minutes -- 34 men died and 172 were injured. Initially it was thought that either Egypt or the U.S.S.R. was responsible, but astonishingly Israel, the U.S.’s closest ally, said that the planes and boats belonged to them, and that they mistook the ship for an Egyptian vessel -- despite the prominently displayed Stars and Stripes.

T h i s h a r d - h i t t i n g investigation shows that on

Operation Cyanidethat day in 1967, the world came closer to all-out nuclear war than ever before -- this incident made the Cuban Missile Crisis seem tame by comparison.

Peter Hounam reveals that the attack was part of a clandestine plan between the US and Israel known as “Operation Cyanide,” designed to ensure victory for Israel in the Middle East. By blaming the attack on the Arab world, retaliation on a grand scale would be justified.

The Lavon AffairThe Lavon Affair refers to a

failed Israeli covert operation, code named Opera t ion Susannah, conducted in Egypt

in the Summer of 1954. As part of the false flag

operation, a group of Egyptian Jews were recruited by Israeli military intelligence for plans to plant bombs inside Egyptian, American and British-owned targets. The attacks were to be blamed on the Muslim Brotherhood, Egypt ian Communis t s , “unspecified malcontents” or “local nationalists” with the aim of creating a climate of sufficient violence and instability to induce the British government to retain its occupying troops in Egypt’s Suez Canal zone.

The operation caused no casualties, except for those members of the cell who committed suicide after being

captured.The operation ultimately

became known as the Lavon Affair af ter the Israel i defense minister Pinhas Lavon was forced to resign as a consequence of the incident.

B e f o r e L a v o n ’ s resignation, the incident had been euphemistically referred to in Israel as the “Unfortunate Affair” or “The Bad Business” (Hebrew: ה ע ס ק ה ב י ש ‎ , H a E s e k HaBish).

After Israel publicly denied any involvement in the incident for 51 years, the surviving agents were officially honored in 2005 by being awarded certificates of appreciation by Israeli President Moshe Katzav.

KUNDI la Boko-Haram la Nigeria

MAKALA

Inatoka Uk. 5

Page 9: Gazeti la ANNUR

9DHUL-HIJJA 1434, JUMANNE OKTOBA 30 Nov 1, 2012AN-NUUR MAKALA

Shujaa Amani KarumeInatoka Uk. 7

vinavyoendelea dhidi ya harakati zote zinazodai mabadiliko, CUF, UAMSHO, kamat i ya mar idhiano, a k i n a M a n s o o r, M z e e Moyo, Amani Karume nk ni suala moja tu, yaani ni vita dhidi ya umoja ambao Wazanzibari wanaringia hivi sasa. Hivyo vyote ni visu vinabadilishwa hiki na kile kuhakikisha kuwa kamba hii ya umoja iliyowaweka pamoja na kuwapa sauti moja Wazanzibari bila kujali vyama vyao, asili zao, rangi zao wala historia za babu na bibi zao inakatwa ili wasambaratike wasifikie lengo tulilolikusudia na badala yake nguvu ya KISONGE ichukue nafasi yake.

Amani Karume aliyapuuza m e n g i y a D o d o m a n a maa jen t i wao wa l iopo Zanzibar ndio umoja wa Wazanzibari ukapatikana na serikali ya umoja wa kitaifa ukaundwa. Aliamua kubakia

zaidi kwao Zanzibar kuliko Dodoma. Aliamua kubaki na Uzanzibari zaidi kuliko chama chake. Aliangalia maslahi ya Zanzibar na Wazanzibari zaidi kuliko maslahi binafsi. Alimpigia debe Dr Shein ili awe rais na amrithishe kiti cha serikali ya umoja wa kitaifa kwa misingi hiyo hiyo ya kuangalia zaidi Uzanzibari kuliko Dodoma kwenye chama chao.

Kitu cha kusikitisha sana ni kuona Dr Shein anaelekea kukubali pole pole kutolewa katika mstari wa Uzanzibari na kusogezwa zaidi Dodoma ambako wahafidhina ndiko wanakokuangalia zaidi, ndiko wanakokutegemea na ndiko kuliko na ushawishi na nguvu zao zote. Salama ya Zanzibar na Wazanzibari, haiwezi kupatikana kwa kupokea

ushauri na maelekezo ya wahafidhina. Yao ni ya kuwaondoa Wazanzibari katika agenda yao.

Kinachoonekana hivi sasa serikali inajaribu tena kubariki vitendo vya chaguzi za KISONGE, za upigaji kura wa kimamluki, enzi za kuunga mkono tena vita ya kuzuia mabadiliko ambayo Wazanzibari wanayadai. Aidha inajaribu kubariki tena uundwaji wa vikundi vya uharamia na kufanywa vitendo vya uharamia na kuwasingizia wanaharakati wanaodai mabadiliko. Yale yale yaliofanywa Shengejuu Pemba enzi hizo eti wanakijiji waliwavamia askari watatu na kuwapora silaha. Matokeo yake ni kijiji kuvamiwa baada ya kuzuliwa uongo huo, wanakijiji kuteswa, mali

SIKU chache zilizopita, Naibu Waziri wa Elimu Tanzania (sio Tanganyika), Bwana Phillipo Mulugo a l i v u n j a m w i k o w a ule usemi wa Kiswahili usemao ‘Funika kombe mwanaharamu apite’! Mficha aibu huaibika za id i , na mdanganya kiaga hudanganya utupu wake. Huu ndio ukweli uliopelekea Waziri wetu huyu kulifunuwa kombe mbele ya mwanaharamu licha ya juhudi kubwa ya kujificha asifanye hivyo. Aibu iliibuka tu.

Sina haja kurudia sana alichokifanya Waziri Mulugo, lakini kwa kukumbushia tu ni kwamba Mheshimiwa Waziri alifanya manyanga ya kupigiwa mfano katika historia ya nchi hii mbele ya umati na mitandao ya kimataifa. Kizungu kibovu kabisa, hoja za jongoo bumbwi zisizo macho, papasio wala ndewe za masikio katika mawasilisho yake, sambamba na kufanya makosa makubwa ikiwemo lile baya zaidi la kuitangazia dunia kuwa Tanzania ni Muungano wa nchi mbili yaani Zimbabwe na Pemba.

Hakuna mtu anaweza kutegemea kwamba yupo Mtu, si Mtanzania tu, lakini hata Muafrika wa Congo, Eriterea au Togo, sembuse Waziri mwenye dhamana nzi to ya Elimu nchini ; anaweza kusema kuwa Tanzania ni muungano wa Pemba na Zimbabwe.

Mimi kama mwandishi sitaki nimhukumu Waziri Mulugo nitaitwa CUF au Uamsho. Lakini kama kuna

Hongera Waziri Mulugo

Naibu Waziri wa Elimu Tanzania (sio Tanganyika), Bwana Phillipo Mulugo.

Atakayekulaumu mwambie kama ana ubavu…Akamkabili Rais Kikwete aliyekuona unafaa

mtu aliwahi kuona katika Blogu kama vile Michuzi, ataona jinsi gani watu wa huko kwao Bara walivyokerwa na hutuba na upeo mdogo alionao Waziri Mulugo. Kule Youtube ndio kabisa, na laiti ingekuwa Video ile ingemhusu kiongozi au mtu maarufu wa nchi za Ulaya, basi ingekuwa balaa.Angekwishalazimishwa

ajiuzulu. Maana kwanza ni aibu kubwa kwa Rais aliyemchagua na kwa vyombo v inavyoda iwa kufanya kinachoitwa “vetting.”

Binafsi sishangai kwa watendaji wetu wakuu kuwa wabovu si kwa kuongea kimombo tu , bal i hata ule uwezo wa kujenga na kuwasilisha hoja, utashangaa.

Viongozi kadhaa yamewakuta haya ndio maana wanashindwa hata kuweka mikataba ya kuchimba madini yenye manufaa kwa nchi. Hivi kwa watu wa ‘uwezo huu wa Mulugo’, tunawatarajiwa w a t u w a k i l i s h e k a t i k a mazungumzo na makampuni ya kuchimba madini halafu watuletee kitu cha maana?

Aibu aliyotuletea Waziri Mulugo, inaweza kujenga picha na hoja kuwa Serikali zetu hazitafuti watu kwa mujibu wa uwezo wao. Bali kwa vigezo vingine binafsi na visivyozingatia masilahi ya nchi. Tabia hii inaiondolea heshima Serikali kwani huonekana ni kichaka kidugu cha watafuta kula badala ya watu wenye upeo mkubwa wa kuendesha nchi na kuleta maendeleo.

Tanzania hii ina watu wenye uwezo sana kiuongozi wa nafasi aliyonayo kama huyo Waziri Mdogo Mulugo. Nakumbuka Rais Kikwete ameshabadilisha Baraza la Mawaziri mara kadhaa, lakini kila uchao ndio hivyo hivyo. Bado tunao ‘Mulugo’ na tunataraji nchi iende mbele!

U p i g w a v y o n d i v y o uchezwavyo. Na sisi hatuna budi tuucheze hivi hivi wanavyoupiga, siku ikipasuka kila mtu atatafuta njia yake aende lakini swali linabakia kuwa Mustakabli wa Taifa hili. Nini hatma ya nchi hii?

Tutabakia kuwa vizuu na misukule ya kuuwana wenyewe huku wajanja wakihujumu uchumi wa nchi yetu tunaowaachia kwa hiari zetu. Na kwa mtindo huu hatufiki popote!

Hongera Waziri Mulugo! Huna lawama, na atakaye kulaumu mnyooshe kidole bosi wako aliyekuteuwa akiamini kuwa lawama zote za uteuzi wake ni zake yeye mwenyewe.

(Makala hii imenukuliwa na kuhaririwa kutoka mtandao wa Mzalendo)

kuibwa, wanawake kubakwa na wanaume kukimbilia msituni kwa miezi kadhaa wakiziwacha familia zao na njaa.

Mheshimiwa Rais wetu Dr. Shein anasema kuwa muda wote huo alikua anastahamili tu, ila sasa ustahmilivu wake umefika mwisho. Hii ni kweli kwani mahafidhina kila walipoona wimbi la kudai Zanzibar linakuwa kali humlilia Dr. Shein na kumuuliza unafanya nini? Mbona hivi lakini? Mwanzoni aliogopa serikali ya umoja wa kitaifa na kuheshimu sauti za wanaodai mabadiliko.

Kinachijitokeza hivi sasa ni kuwa wana-Maskani wanepata nguvu mpya ukianzia na hali ilivyokuwa katika uchaguzi wa Bububu. Kwa hali ilivyo, demokrasia na uhuru wa

kutoa maoni ni suala la muda tu. Unachimbiwa kaburi kwa kasi sana.

Mtu unajiuliza, inakuwaje serikali inashindwa kukemea na kuchukua hatua dhidi ya matusi wanayorushiwa Mheshimiwa Rais Mstaafu Amani Karume na dhidi ya Maalim Seif, ambaye ni Makamo wa Kwanza wa Rais?

Tumeugua sana maradhi ya farka, fitna, chuki na uhasama kwa miaka mingi na mwisho tuliyapatia dawa. Tumekuwa na serikali ya maridhiano na umoja wa kitaifa angalau kumekuwa na nafuu. Nchi imeanza kupata nuru.

Wengine, na kwa hakika walio wengo, hawana tamaa ya kupata nafasi yoyote ya kisiasa, Si urais wala uwaziri wa SMZ. Bali tunachotaka ni nchi yetu yenye mamlaka kamili. Wazanzibari tumeapa hatuondoki katika mstari huo.

Page 10: Gazeti la ANNUR

10 DHUL-HIJJA 1434, JUMANNE OKTOBA 30 Nov 1, 2012 AN-NUUR

IDD YENYE HUZUNIKalamu nimeishika,Ilahi namkumbukaWahadahu la sharika,Ni yeye alotukukaNinalo jambo hakika,daima nalikumbukaIngawa tunafurahi,donda tunalo moyoni

Sala tutumeimaliza,vichinjwa tunakamataSauti tumeipaza,Takbira kutamkaPilau tutamaliza,sururi tatukamataIngawa tunafurahi,donda tunalo moyoni

Ndugu zetu mahabusu,hivi twafikiria?Wale wanaotuhusu,na wote IslamiaTuwape hata sudusu,waweze kufurahiaIngawa tunafurahi,donda tunalo moyoni

Shekhe Ponda na wenzake,Jamani tuwakumbukeKula kisha upeleke,Segerea uwakuteWasijihisi upweke,sisi ndio ndugu zakeIngawa tunafurahi,donda tunalo moyoni

Shekhe Faridi Hadi,akiwa MwanakwerekweMselem namnadi,pia na viongozi woteTuzipeleke zawadi,na wao wafurahikeIngawa tunafurahi,donda tunalo moyoni

Tumalizapo Ibada,kunuti tuwapigieTuzitupe zetu shida,Allahu tumwelekeeSio kuimba nashida,halafu tujyondokeeIngawa tunafurahi,donda tunalo moyoni

Kwa kila mwenye uchungu,litamgusa moyoni Na wale wenye majungu,watafurahi kifaniKama mpango wa Mungu hawatakuwa shariniIngawa tunafurahi,donda tunalo moyon

Inabidi kusimama,na mikono kuinuaYa Ilahi Ya Rabana,dhulma imeeneaYote wewe wayaona,hukumu unavyojuaKama hii ni dhuluma,dhalilisha walotenda.

Mwl.Mohammed MakimuUITC-Dar es [email protected]

ZAWADI GANI?Nasomeka Gazetini, kuomba zenu hekimaSwali hili ni makini, laniumiza mtima Naitafuta yakini, nisije fanya hujuma Niwape zawadi gani, wazazi Baba na Mama

Mlipo maburuhani, mliye pewa Karama Nawaomba ihisani, nisije kwenda Mrama Niipate ahueni, moyo upate tuama Niwape zawadi gani, wazazi Baba na Mama

Wazazi ndiyo kiini, fika nilipo simama Miezi tisa tumboni, alipata tabu mama Baba yupo mashakani, mke kuvuka salama Niwape zawadi gani, wazazi Baba na Mama

Wazo lapita kichwani, niwapeleke Dodoma Wafike kule Bungeni, wabunge kuwatazama Wajifunze kitu gani, majibu yamenigoma Niwape zawadi gani, wazazi Baba na Mama

Ufisadi “namba wani”, wafanye tuso watuma Hadi miaka sitini, mafao kuja yachuma Nani ata tuauni, katika hii hujuma Niwape zawadi gani, wazazi Baba na Mama

Niwapeleke Mbugani, wanyama kuwatazama Twiga, Faru wa Kusini, wanasafirishwa wima Waziri madarakani, avuna asicholima Niwape zawadi gani, wazazi Baba na Mama

Ulaya na Marekani, wafike Baba na Mama Niwapandishe Ndegeni, wakamuone Obama Nime gutuka Bongoni, wazo hili sio jema Niwape zawadi gani, wazazi Baba na Mama

Kuwapeleka ni Shani, iliyo jaa AdhamaKule Hija ibadani, ni Makati MukaramaAwatakase Manani, Mola wetu ni Karima Niwape zawadi gani, wazazi Baba na Mama

Nikiwa msikitini, Duwa naiomba njemaNaonyesha shukurani, kwa malezi yao memaKunilea kiimani, mengi yame wasakamaNiwape zawadi gani, wazazi Baba na Mama

Mapengo wa Visiwani, wewe ni Bingwa DaimaNyamkomogi Bayani, kuwakilisha Mrima Mnitowe mashakani, majibu mkiyatuma Niwape zawadi gani, wazazi Baba na Mama

Hapa ndiyo kituoni, Mkutubi kaditamaNimeshafika mwishoni, hekima ni kusimamaKalamu naweka chini, ni mshukuru Karima Niwape zawadi gani, wazazi Baba na Mama

Is-haq Hemed Mzuzuri Morogoro

SHAIRI/HABARI

KIRINJIKO ISLAMIC TEACHERS’ COLLEGES.L.P. 62, Same – Kilimanjaro, Mob: 0787 188964 Tanzania

Sifa na masharti ya kujiunga

NAFASI ZA KUJIUNGA NA KOZI YA UALIMU WA SHULE ZA AWALI, MSINGI NA MADRASA 2013

Muombaji atimize sifa na masharti yafuatayo:(i) Awe Muislamu aliye tayari kuishi Kiislamu(ii) Awe anajua kusoma Qur’an kwa ufasaha.(iii) Awe amemaliza juzuu ya 1 na 2 ya Maarifa ya Uislamu, Darasa la Watu Wazima kabla ya

kujiunga.(iv) Awe amehitimu darasa la saba au kidato cha nne na awe anafundisha madrasa au kipindi cha

dini katika shule za Msingi au Sekondari.• Patakuwa na usaili siku ya tarehe 1/12/2012 saa 2:00 asubuhi katika vituo vilivyoainiashwa

kwenye fomu ya maombi.• Mwisho wa kuchukua fomu ni tarehe 30/11/2012.• Fomu italipiwa shilingi 5,000/- tu.

Fomu zinapatikana katika vituo vilivyoorodheshwa ukurasa wa 11MKUU WA CHUO

Ndugu Mhariri,Adui wa mti ni mti. Na hi i inadhihirika wazi hapa kwetu Zanzibar pale tunapooana Waislamu wenyewe kwa wenyewe wanafanyiana hujuma n a k u u m i z a n a h u k u wakitegemea Rehema na Baraka za Allah ziwashukie. Bwana Mtume Muhammad (s.a.w) alisema na kutuusia kuwa “Muislamu ndugu yake ni Muislamu”. Na akatuusia tena akisema kwamba tushikamane katika upendo baina yetu ili tupate kurehemewa na Allah subhananuhu walataala.

Zanzibar ni nchi inayotajwa kuwa ya Waislamu kwa asilimia 99 (Sina uhakika kama ni Waislamu kweli wote hao). Katika asilimia kubwa kama hii ya Waislamu nchini, ni wazi safu ya Uongozi wa juu yote ni ya Waislamu, na kwa hio kimaumbile kuhurumiana na kupendana ni jambo ambalo lilitarajiwa na kwamba lau lingekuwepo japo kwa asilimia ndogo kabisa, basi hakuna sababu ya Mola kutoishushia rehema na baraka nyingi. Lakini tazama ilivyo Zanzibar hivi leo na inakoelekea! Idhilali, shida na mashaka matupu ndiyo yaliyotawala.

Kinachosikitisha sana hapa ni kuona jinsi gani Waislamu wenzetu, hasa viongozi wetu wanavyotumiliwa na kuyatumia mamlaka waliyonayo kuwadhalilisha na kuwadunisha ndugu zao wa Kiislamu kwa sababu ambazo zinazungumzika, hazina mashiko, au hata

Hujuma dhidi ya Waislamu Zanzibarambazo ni za kuzushiwa tu. Kuna ndugu zetu wengi hapa waliuwawa kikatili wakati wa mapinduzi kwa kutiliwa fitina tu. Katika zama hizo, wapo wengi walio hai leo ambao waliponea tundu ya sindano.

Viongozi wetu hawawezi kubarikiwa wala kurehemewa na Allah kwa sababu moja kubwa ya uadilifu dhidi y a Wa i s l a m u w e n z a o inaowaongoza. Kwa mfano, viongozi wetu wa kidini ambapo mimi na wewe na viongozi wetu wote ni lazima kuwaheshimu na kuwalinda kwa gharama yoyote, leo ndio wamefanywa viroba vilivyojazwa mchanga vya vyombo vya dola kufanyia mazoezi.

N i s i s i Wa i s l a m u tuliotumiliwa huko nyuma kuwauwa Mashekhe na kuwadhalilisha kupindukia mipaka i lhal i tuki juwa kufanya hivyo ni laana kubwa kwa nchi yetu.

Hii leo tena tunarejea katika uovu ule ule, halafu tunatarajia nchi hii iwe na salama na ichanue kwa hali

nzuri ya kiuchumi na hali bora za wananchi. Tunayochuma h i v i s a s a , i t a k u w a n i kudhalilika kutoka viongozi wa juu mpaka mwananchi wa chini. Tusubiri!

Kule bara fitina ya Kanisa yanuka uvundo, na dunia nzima yajuwa ubaya ufanywao dhidi ya Waislamu na hata katika kuvuruga amani ya nchi. Lakini cha ajabu ulisikia wapi Viongozi wa huko wakiwachukulia hatua ya idhilali Maaskofu na Mapadre wanaotoa kauli za uchochezi na hata kutishia umwagaji damu? Au hamkuwasikia katika uchaguzi uliopita na jinsi walivyokuwa nyuma ya Chadema na lile zogo la Arusha hadi kuuliwa mtu?

Kwa hakika ukitizama historia ya Tanganyika na Zanzibar, ni viongozi tu wa kisiasa wenye majina ya Kiislamu wanaotumiliwa kuwahujumu viongozi wao wa Kiislamu. Kwa maana hiyo, amani haiwezi kupatikana kwa staili hii.

Mwananchi, MzalendoMji Mkongwe, Zanzibar

Ndugu Mhariri,Mi n a j iu l i za k a m a j e , tumo ndani ya Zanzibar au Ukanda wa Gaza huko Palest ina? Kwani haya maafa tunayoyashuhudia t u n a y o f a n y i w a s i s i Wazanzibari na Vikosi vya Dola, sikuyatarajia na wala sioni sababu yake.

J a m b o b a y a z a i d i , yanafanyika ndani ya Mwezi huu mtukufu ambao Waislamu wa dunia nzima wako kwenye

Hii ni Gaza au Unguja?ibada ya Hijja huko Makkah.

J e , w a n a o a m r i s h a n a kuyasimamia haya, watakwenda kujibu nini mbele ya Allah (S.W)?

Au wanadhani wataishi milele hawataingia kaburini wala kuulizwa na Allah aliye Hakimu Muadilifu na Maliki yaumiddiin? Au huku ndio kulinda amani ya Zanzibar kama wanavyotutangazia?

Maalim Yusuf HajiZanzibar

Page 11: Gazeti la ANNUR

11DHUL-HIJJA 1434, JUMANNE OKTOBA 30 Nov 1, 2012AN-NUUR TANGAZO

BAADA ya taarifa kutokea kuwa kijana mwingine, mwenye umri wa kuweza k u s h i t a k i w a k a t i k a mahakama ya kawaida ya jinai kwani ana umri wa miaka 20 , ambaye ametenda kosa li le l i le lililotokea Mbagala, ulazima wa makuhani wa Kikristo kuondoa chanzo cha hali hii sasa unakuwa dhahiri. Chanzo chenyewe ni kuwa hakuna fundisho lolote katika Ukristo linalosema kuwa Mtume Muhammad ametumwa na Mungu, hata kama Kanisa lingesema kuwa ujumbe wake haufanani na ule wa Kikristo kwa hiyo hawauamini kama msingi wa imani. Kutokuamini moja kwa moja ni tofauti na kudai hautokani na Mungu.

Unaweza kusema kuwa chanzo halisi cha mgogoro usioisha kati ya Uislamu na Ukristo ni hicho. Kuwa Ukristo kwa miaka yote umekuwa na kanuni ya kujihami kuhusu Uislamu, na kukataa siyo hoja zake kuwa haziendani na imani yao, ila chanzo chake. Ingekuwa Ukristo unakubali kuwa Uislamu umeinuliwa na Mungu, ila katika mazingira ambako Torati haijainuliwa, hivyo ikawa ndiyo msingi wa imani hiyo, na Injili ikapewa nafasi ndogo zaidi ya kuwa ‘mawaidha’ tu ya maisha, ushindani ungekuwa ‘wa kirafiki,’ kama vile madhehebu ya Kikristo yalivyoshindana. Ni kukubali kutofautiana si kupuuza.

Liko tat izo la msingi katika kushindwa kwa wakuu wa makuhani wa imani ya Kikristo kwa miaka yote (karne nyingi) kuhusiana na suala hilo, ambalo linatokana zaidi na jinsi Mtume Paulo alivyofundisha Ukristo, na hata kuuinua kama dini (kwani tofauti zao na Wayahudi zilikuwa kubwa mno, uadui wa Wayahudi wa Wakristo ulikuwa haupimiki). Ni pale Mtume Paulo anapoangalia Ukristo kama ni kifo cha Yesu msalabani, kuwa yeye alitumwa kwa kazi hiyo, na fundisho la maadili linapoishia katika ndoa ya mke mmoja - ambayo hata hivyo hakuiweka Yesu . A l ip inga t a l aka ; hakusema watu wasiongeze wake.

Ni moja ya masuala ambayo yanaibuka mara kwa mara katika Ukristo, kwani Mtume Paulo mwenyewe anakubali kuwa ‘jambo hili (la ndoa) sikulitoa kwa Bwana, bali kwa vile nadhani mimi pia ninaye Roho wa Mungu, naweza kuwapa amri,’ hivyo ni amri ya Mtume Paulo, na wakati huo ikiwalenga ‘maaskofu,’ v iongozi , wazee ka t ika Kanisa. Alisema awe ni ‘mtu mwadilifu, wa kuaminika, mume wa mke mmoja,’ amri ambayo baadaye Kanisa

Mjadala wa ‘Yesu si mwana wa Mungu’ si hoja ya kupuuza utume wa Muhammad SAW

Na Anil Kija

liliiweka kwa waumini wote, halafu mapadri wasioe kabisa, hali ambayo Mtume Paulo aliitaja tu kama rai, kuwa mtu akiweza ‘kuishi kama yeye.’ Hata hivyo zipo pia hadithi za wakati huo zinazosema Mtume Paulo alimwoa binti wa Maria Magdalena mwaka 55 AD (miaka 21 baada ya kuondoka Kristo); Kanisa linaita ni hadithi za uzushi.

Miezi kadhaa iliyopita Imam mmoja alinukuu aya moja ya Qurani katika hotuba (ni mikanda inayorudiwa Radio Imaan FM) kuwa inasema “ tu l iwainua manabi i na kuwapa wake”, akasema kuwa kwa kawaida kuna ukaribu kati ya Mtume Muhammad SAW na Yesu Kristo (Issa bin Mariam), hivyo aya hii inaashiria kuwa hata Issa AS alipewa mke kwa maana hiyo, lakini kwa vile jambo hilo halijafafanuliwa kokote, akaliachia hapo. Hii hadithi ambayo ilielezewa kwa undani na Wayahudi waliohamia Ulaya baada ya Warumi kuzima uasi wa Wayahudi na kuteketeza Yerusalemu mwaka 70 AD (miaka 36 bada ya kuondoka Kristo) inasema kuwa Maria alikuwa mke halali wa Kristo. Ziko chembe pia za alichosema Yesu kwa upande huo lakini hazifafanui, kama ilivyo ile aya ya Qurani, pale Yesu anaposema ‘amekuja Yohana Mbatizaji hali wala hanywi, wakasema ana pepo - sasa amekuja mwana wa Adamu anakula na kunywa, wanasema, anakula na wenye dhambi.’ Hivi ‘mwenye dhambi’ halisi hakuwa Maria Magdalena, mwandani wa karibu?

Eneo kubwa zaidi la ugomvi kati ya Uislamu na Ukristo, ambalo pia l inatufikisha katika kadhia hizi za vijana watovu wa nidhamu na wenye ufahamu potofu kuhusu dini (kuwa Uislamu ni mila tu ya Kiarabu inayofuatana na kufuga majini, si zaidi ya hapo), ni dhana ya uana wa Yesu kwa Mungu, ambayo pia huambatana na ile ya utatu mtakatifu (wa Baba, Mwana na Roho Mtakatifu). Cha msingi katika eneo hilo ni kuwa hakuna chembe ya kukubaliana katika Ukristo maana yake nini dhana hizo mbili, na kimsingi Mungu alitumia dhana hizo kuunganisha himaya ya Roma barani Ulaya ilipoelekea kuzorota, kwa kuwepo dini inayofanana nao, kuwa Mungu ana mwana, halafu kuigawa himaya mpya ya Kikristo wazozane, wapigane. Ni mwanzo wa kuundwa mataifa ya baadaye, kutokana na utii kwa wafalme tofauti katika eneo lote la himaya ya Kanisa, ambao kimsingi walitofautiana kuhusu ‘utatu mtakatifu,’ mashariki wakatengana na magharibi.

Baadaye wale wa magharibi wakahitilafiana kimsingi kuhusu mamlaka ya Papa (Askofu mkuu wa jiji la Roma) na pia baadhi ya sera zake, kama kulipa faini na kupata cheti cha msamaha wa dhambi, n.k. Ile sera ya mke mmoja ilijaziwa na Kanisa kuchukua wengi tu kati ya wanawake waliokosa waume wa kuwaoa, na kuwaweka katika nyumba za utawa watumikie Kanisa, hali ambayo haipo katika makanisa yasiyo ya Kikatoliki, na Kanisa

hilo pia halichukui idadi hiyo ya wanawake kama ilivyokuwa zamani. Unajiuliza kama kuna mfumo halisi wa Kikristo wa jinsi jamii inavyotakiwa iwe, au ni kubuni mfumo unaofaa, halafu kupuuzia ufunuo mwingine kuhusu suala hilo, bila kuhitaji tafakuri.

Kimsingi inabidi wakuu wa makuhani wa Kikristo wakubali kuwa yako maeneo mengi ambako mapokeo yao hayana majibu. Na katika maeneo hayo kuna ufunuo mwingine ambao umejibu kwa njia tofauti maeneo hayo ya fikra. Wanahitaji kuutambua kama njia mbadala ya masuala hayo (nini mfumo unaofaa wa kuishi kinyumba katika jamii, pale wanapokuwepo wanaume wengi wasio na uwezo kitabia au kisaikolojia kumchukua mwanamke na kumlinda, amtegemee maisha yake yote), na hata masuala mengine.

Jambo lingine linalofuatana nalo ni kuwa inabidi kukiri kuwa hakuna ufunuo wenye majibu yote, kwani kila ufunuo una maeneo kinzani, kwani binadamu ana udhaifu mwingi katika kila chembe ya maisha yake, hivyo kila upande mmoja unapopewa kipaumbele , mengine yanaporomoka. Kwa mfano katika hizi dini nne kuu za dunia, kila mmoja ina chembe yake maalum inayoulinda utakatifu au utukufu wake, na ni maeneo tofauti ya maisha ya binadamu ambayo waanzilishi wa dini hizi walipewa vipaumbele tofauti, kila mmoja atetee kimojawapo, na kiwe msingi wa maadili katika umma ambao atauinua.

Kubisha ni ufunuo upi unatoka kwa Mungu ni kumzuia Mungu asitoe ufunuo.

Kwa mfano utukufu wa Ukristo umejikita kimaadili katika ndoa ya mke mmoja ambayo kimsingi haivunjiki; watu wanavunja ndoa kwa vile si Kanisa bali Kaisari ndiye mwenye mamlaka, na kwa vile Kristo aliwaambia wafuasi wake (na umma wa Israeli) kumtii Kaisari kwani amewekwa na Mungu, imekuwa rahisi (baada ya mifarakano mirefu) kutenga eneo la Kanisa (imani inayotajwa katika ibada) na maisha binafsi, yaani uhuru wa mtu kujipangia maisha. Dhana hiyo sasa inaingia katika Uislamu; kama ilivyokuwa barani Ulaya, walinzi wa imani, mapokeo ya dini, hawasalimu amri haraka kwa uliberali.

Hata hivyo inabidi Kanisa l ianze kuangalia ni nini linaweza kuchota kutoka Uislamu ili kuanza kuiokoa jamii ya Ulaya na kote ambako Ukristo ndiyo utamaduni wa jadi, kwani ni maeneo ambayo uwezo wa kuzaa na kulea unapungua, jamii zinazeeka, na baadhi (kama Japan) zinatishiwa kupotea. Takwimu za miezi ya karibuni zinasema kuwa idadi ya watu itapungua nchini Japan kutoka wakazi milioni 120 takriban hivi sasa na kufikia milioni 47 ifikapo mwaka 2050, kutokana na Wajapani kutaka tu kupata kisomo cha hali ya juu na kufanya kazi nzuri maisha yao yote. Kuzaa na kulea kunavuruga matazamio katika eneo la kazi la mwanamke; wanaume hutaka maisha ya juu, si gharama za mtoto.

Matokeo yake ni kuwa Wa j a p a n i w a n a p o o a n a wakiwa vijana, wanatafuta kichanga cha mbwa na kuanza kukilea, halafu uhusiano wao unakuwa na jambo muhimu la kuongea nyumbani jinsi mbwa anavyokua, na si mtoto anavyokua. Kwa maana hiyo licha ya kuwa utamaduni wa Japan hautaki wageni wakaingia na kukaa, itafika mahali mwiko huo utaanza kuvunjwa wazee wakiwa ni wengi mno - kwani dawa ya ujana miaka 100 au zaidi haijagunduliwa bado - na wakiingia Japan itaanza kubadilika sura, ipoteze haiba yake ya asili. Ni marudio ya Mungu kuitoa Kanaani kutoka kwa Waamori, Wafilisti na wengine na kuwapa wana wa Yakobo; Japan, Ulaya, hata Marekani wanapewa wengine.

Kr i s to anasema ‘her i wanyenyekevu maana hao watairithi nchi.’ Na katika dunia bado ni Uislamu ambao una unyenyekevu zaidi kwa wanawake kwa kile ambacho Mungu ametaka wafanye, yaani kazi ya kuzaa na kulea, kutokana na malezi ya msingi wa imani. Katika maeneo mengine unyenyekevu huu unapotea, na licha ya kuwa haihitajiki kufuata sharia yote ili wanawake waendelee kutii amri hii ya Mungu, maadili ya Uislamu hayakwepeki.

Page 12: Gazeti la ANNUR

DHUL-HIJJA 1434, JUMANNE OKTOBA 30 NOV 1, 2012

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagaration Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.

AN-NUUR Soma AN-NUUR

kila Ijumaana Jumanne

Vikosi SMZ vyadaiwa kuuwa siku ya IddVIKOSI vya SMZ vidaiwa kumuuwa kijana Hamadi Ali Kaimu siku ya Idd el Haj.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Chama cha CUF jana, Hamad alipigwa siku ya Idd Mosi hadi kupoteza maisha.

C h a m a c h a C U F “kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kijana aitwae Hamadi Ali Kaimu, mwenye umri wa miaka 22, mkaazi wa Nyerere. Kijana huyu akiwa yuko katika shughuli za kulisha ng’ombe wake huko kwao Nyerere alivamiwa siku ya Ijumaa ya tarehe 26/10/2012 siku ya Idi Mosi na vikosi hivyo vya ulinzi na usalama wakiendeleza zoezi lao la kusaka wahalifu. Kijana Hamadi alipigwa vibaya sana hadi kupoteza maisha. Baada ya wazee wake kumtafuta katika vituo mbali mbali vya polisi hawakufanikiwa kumpata n d i p o w a l i p o k w e n d a kumtafuta katika hospitali kuu ya Mnazi mmoja.”

Imeeleza taarifa ya CUF na kuongeza kuwa “baada ya kukosa taarifa zake sehemu ya mapokezi walielekezwa wende chumba cha maiti na ndipo walipogundua kijana wao, Hamad Ali Kaimu ameshafariki huku mwili wake ukiwa na majeraha sehemu mbali mbali.”

Taarifa hiyo ambayo ilisomwa na Salim Bimani ambaye ni Mkurugenzi wa Haki za Binadamu, Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma imesema kuwa katika operesheni inayofanywa h i v i s a s a n a v i k o s i , “majumba yanavunjwa na waliomo ndani kuvamiwa na kuteswa.”

Ametajwa kuwa miongoni mwa wal iovamiwa na kupigwa ni pamoja na wato to ya t ima ka t ika “Kituo cha ushoni cha kuwaendeleza mayatima B u b u b u ( J U D A M A ) ambacho kilivamiwa na watoto wa kike mayatima kupigwa vibaya.”

Wengine waliopigwa na kuchukuliwa katika tukio hilo, wametajwa kuwa ni

Na Mwandishi Wetu

Khalid Shindano na Suleiman Kichwa.

Taarifa ya Bimani ikadai pia kuwa wapo waliopigwa na “kunyo lewa ndevu zao hadharani”, ambao amewataja kuwa ni ”Khamis Khatibu na Mohamed Omar wote wa Fuoni.”

Imeelezwa katika taarifa hiyo kuwa japo inadaiwa kuwa kinachofanyika ni kusaka wahalifu hasa baada ya tukio la kuuliwa Polisi wa Kikosi cha FFU…, lakini CUF wanasema kuwa ilitarajiwa vyombo vya usalama kutumia taratibu za kitaalamu na kipolisi kuwasaka wahalifu hao, sio kupiga watu ovyo mitaani majumbani mwao.

“Matukio ya Zanzibar hayana tofauti kubwa na matukio ya kule Mwanza na Dar es Salaam. Kule Mwanza Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo Libertus Barlow aliuliwa kwa kupigwa risasi siku ya tarehe 13, Oktoba 2012 na hatukuona serikali

ikiwaamuru askari wake kufanya uvamizi wa vijiji, uvunjaji majumba, upigaji kiholela wa watu, maonevu ya wanawake, wizi na uharibifu wa mali na mauwaji kama inavyofanyika hivi sasa hapa Zanzibar.”

I m e s e m a t a a r i f a y a Bimani na kuongeza kuwa “kilichofanyika Mwanza ni msako uliofanyika kitaalamu kwa taratibu za kiupelelezi na kiasi cha watu watano tayari wamekamatwa kwa lengo la kufikishwa katika vyombo vya sheria na kuripotiwa katika vyomba vya habari.”

“ H a t u s e m i s e r i k a l i isiwasake waliofanya fujo na wahalifu waliomuua Coplo Said Abdulrahman, iwasake na iwafikishe wahusika wote katika vyombo vya sharia, lakini sio watumie kisingizio hicho kufanya hujuma, mateso, unyanyasaji na mauwaji kwa wasio na hatia ambao wengi ni wafuasi wetu wa CUF.” Imesema na

kusisitiza taarifa hiyo. Maeneo yaliyokumbwa

na zahama ya Vikosi tokea tarehe 25 Oktoba 2012 yametajwa kuwa ni Amani, Magogoni, Daraja-bovu, Mwanakwerekwe, Mtoni, K i n u n i , K w a m t i p u r a , Mboriborini, Kilimahewa, Mpendae , Mikungun i , Nyerere, Kwarara, Tomondo na Nyarugusu.

Katika maeneo hayo imedaiwa kuwa hufanywa “msako nyumba hadi nyumba, na barabarani, kuwapiga, kuwatesa, na kuwakamata raia wasiokuwa na hatia bila ya kujali na kuiheshimu Sikukuu ya Iddi.”

A k i m a l i z i a k u s o m a taarifa yake ndefu kiasi, Salim Bimani alisema kuwa “Chama Cha wananchi CUF, kinamtaka Kamishna wa Jeshi la polisi Zanzibar, Bwana Mussa Ali Mussa kuhakikisha anakomesha v i t e n d o v y o t e v y a unyanyasaji vinavyofanywa

na vyombo vya dola dhidi ya raia wasio na hatia na hapo hapo kuwachukulia hatua wale wote wanaotenda unyanyasaji huo.”

Kwa upande mwingine alisema kuwa Chama cha wananchi CUF kinamtaka Waziri wa nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais, Mhe Mohammed Aboud Mohammed kuhakikisha serikali inaheshimu haki za raia wake chini ya misingi ya utawala bora.

“Pamoja na kuiwacha Sheria ichukue mkondo wake, ni vyema Serikali na Vyombo vyake vya Dola kutekeleza wajibu na majukumu yao kwa kuzingatia sheria, haki, hikma na uadilifu, bila kuwahujumu na kuwasumbua Wananchi wasi na hatia, ikieleweka kuwa wao ni sehemu muhimu ya maisha na raia halali wa Nchi hii.” Taarifa hiyo ilihitimisha.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Dkt. Emmanuel Nchimbi akiwa na Kamishna wa Jeshi la polisi Zanzibar, Bwana Mussa Ali Mussa.