Fasihi Andishi . Kf 202 Notes Zote 2

32
1 FASIHI ANDISHI ONYO KALI: HIZI NOTISI ZIMECHUKULIWA KATIKA MIHADHALA YA MWALIMU WA KF 202 NA SIYO NAKALA YAKE. NIMEZIANDIKA KATIKA MIHADHALA. KOSA LOLOTE LA NOTISI HIZI LISIELEKEZWE KWA MWALIMU WA SOMO BALI KWANGU LABDA KAMA NILIKOSEA KUANDIKA. KAMA UMEZIKUBALI USIWE MCHOYO NIPIGIE KWA 0786684062 __________________________________________________________________ I. USHAIRI Kuna mitazamo ya aina mbili katika kuelezea dhana ya ushairi. kuna wanamapokeo na mamboleo. Hata hivyo kabla ya kuendelea zaidi kuwachambua tuangalie wataalam mbalimbali wanavyofasili dhana hii . Dhana ya ushairi imejadiliwa na wataalamu mbalimbali huku kila mmoja akitoa fasili yake. Baadhi ya wataalam hao ni kama ifuatavyo: MAPOKEO Mssamba, (2003) akimnukuu Shaban Robert, anasema; “ushairi ni sanaa ya vina inayopambanuliwa kama nyimbo, mashairi na tenzi zaidi ya kuwa na sanaa ya vina ushairi unaufasaha wa maneno machache au muhtasari.” Mnyampala (1970) anasema kuwa “ushairi ni msingi wa maneno ya hekima tangu kale ndicho kitu kilichobora sana maongozo ya Dunia kwa kutumia maneno ya mkato na lugha nzito yenye kunata iliyopangwa kwa urari wa mizani na vina maalum.” Amri Abeid (1954:1) anasema kuwa “ushairi au utenzi ni wimbo, hivyo kama shairi haliimbiki halina maana.”

description

kiswahili

Transcript of Fasihi Andishi . Kf 202 Notes Zote 2

  • 1

    FASIHI ANDISHI

    ONYO KALI: HIZI NOTISI ZIMECHUKULIWA KATIKA MIHADHALA YA MWALIMU WA KF 202 NA SIYO NAKALA YAKE. NIMEZIANDIKA KATIKA MIHADHALA. KOSA LOLOTE LA NOTISI

    HIZI LISIELEKEZWE KWA MWALIMU WA SOMO BALI KWANGU LABDA KAMA NILIKOSEA

    KUANDIKA. KAMA UMEZIKUBALI USIWE MCHOYO NIPIGIE KWA 0786684062

    __________________________________________________________________

    I. USHAIRI

    Kuna mitazamo ya aina mbili katika kuelezea dhana ya

    ushairi. kuna wanamapokeo na mamboleo. Hata hivyo kabla ya

    kuendelea zaidi kuwachambua tuangalie wataalam mbalimbali

    wanavyofasili dhana hii . Dhana ya ushairi imejadiliwa na

    wataalamu mbalimbali huku kila mmoja akitoa fasili yake.

    Baadhi ya wataalam hao ni kama ifuatavyo:

    MAPOKEO

    Mssamba, (2003) akimnukuu Shaban Robert, anasema;

    ushairi ni sanaa ya vina inayopambanuliwa kama nyimbo, mashairi na tenzi zaidi ya kuwa na sanaa ya vina ushairi

    unaufasaha wa maneno machache au muhtasari.

    Mnyampala (1970) anasema kuwa ushairi ni msingi wa maneno ya hekima tangu kale ndicho kitu kilichobora sana

    maongozo ya Dunia kwa kutumia maneno ya mkato na lugha

    nzito yenye kunata iliyopangwa kwa urari wa mizani na vina

    maalum.

    Amri Abeid (1954:1) anasema kuwa ushairi au utenzi ni wimbo, hivyo kama shairi haliimbiki halina maana.

  • 2

    Abdulatifu anasema kwamba ushairi ni ule ulio na sifa ya

    ulinganifu wa vina na mizani, lugha laini (lugha tamu) na lugha

    hii iweze kugusa moja kama ilivyokusudiwa.

    Encyclopedia American (EA) inaeleza kuwa ushairi ni kauli

    zenye hisia na ubunifu, mpangilio fulani wenye urari,

    uwasilishaji wa tajiriba au mawazo ya mtunzi kwa maana

    ambayo huibua tajiriba kama hiyo katika nyayo za wasomaji au

    wasikilizaji na kutumia lugha ya picha yenye wizani wa sauti.

    MAMBOLEO

    Kezilahabi ( )anasema kuwa ushairi ni tukio hai au wazo ambalo limeonywa kwetu kutokana na upangaji uzuri wa

    maneno fasaha yenye mizani Fulani ili kuonyesha ukweli

    Topan (1996) anasema kuwa shairi ni unaoeleza hisia za ndani za binadamu kwa mpangilio Fulani wa maneno hivyo kwa mujibu wa Topan ushairi lazima uguse hisia za ndani ya moyo

    wa binadamu.

    Njogu na Chimerah (1999) wanasema ushairi ni sanaa ya lugha inayoeleza jambo kwa njia ya mkato na kwa namna

    inavyoteka hisia za msomaji au msikilizaji

    Mulokozi na Kahigi (1982:25) wanasema ushairi ni sanaa inayopambanuliwa kwa mpangilio maalum na fasaha na wenye

    muwala, kwa lugha ya picha, sitiari au ishara katika usemi,

    maandishi au mahadhi ya wimbo ili kuleta wazo au mawazo,

    kufunza au kueleza tukio au hisia fulani kuhusu maisha au

    mazingira ya binadamu kwa njia inayogusa moyo.

    Hivyo basi tunaweza kusema kuwa ushairi ni kazi ya sanaa

    yenye kuandikwa au kuimbwa kwa kufuata kanuni za ushairi au

  • 3

    kutofuata kanuni za ushairi ikiwa na maana kuwa ushairi

    waweza kuwa wa kimapokeo au wa kisasa ilimradi ushairi huo

    uwe na ujumbe.

    Katika ushairi FANI na MAUDHUI ni muhimu sana, mawazo

    fikra au sihi za ndani ni vitu muhimu sana katika ushairi

    CHANZO/CHIMBUKO LA USHAIRI

    Dhana ya chimbuko inafasiliwa na TUKI (2004) kuwa ni

    mwazo au asili ya kitu.

    Baadhi ya wataalamu wameweza kuelezea chimbuko la

    ushairi wa Kiswahili kwa kuzingatia mitazamo au nadharia

    mbili ambazo ni kama ifuatavyo:

    1. Nadharia ya kwanza inadai kuwa; Chimbuko la ushairi wa Kiswahili ulitokana na ujio wa Waarabu.

    2. Na nadharia ya pili inasema kuwa; Chimbuko la ushairi wa Kiswahili ni zao la jamii ya waswahili

    wenyewe.

    Hapa tunaenda kuzielezea nadharia hizi kila moja na kujaribu

    kuona ubora wake na udhaifu wake katika kuelezea chimbuko la

    ushairi

    1.Na nadharia ya pili inasema kuwa; Chimbuko la ushairi wa

    Kiswahili ni zao la jamii ya waswahili wenyewe.

    Kwa kuanza na Lyndon (1962) Swahili Poetry anatoa hoja tatu ambazo ni:

    ushairi wa Kiswahili umetokana na Uislamu,

    ushairi ulianzia kwenye upwa wa kaskazini mwa Kenya hususani Lamu.

  • 4

    Na maudhui ya ushairi wa Kiswahili yalitokana na ushairi wa Kiarabu. Utungo wa kwanza wa ushairi

    andishi wa Kiswahili ni Tambuka, Mwengo bin

    Athmani (1728)

    Ubora wa Nadharia hii

    Ubora wa nadharia hii au mtazamo wa Harries kuhusu chimbuko la ushairi wa Kiswahili ni kwamba umesaidia

    wengine kuendelea kuchunguza zaidi kuhusu chimbuko la

    ushairi wa Kiswahili.

    Udhaifu wa nadharia hii

    Udhaifu wa nadharia hii ni kuwa si kweli kwamba ushairi wa Kiswahili uliletwa na Uislamu bali ulikuwepo hata kabla

    ya ujio wa Uislamu, kwani ushairi hautenganishwi na

    jamii husika. Hivyo jamii za waswahili walitumia Nyanja

    mbalimbali za ushairi katika shughuli zao mbalimbali au

    shughuli zao za kila siku, kama vile; shughuli za kilimo na

    ufugaji.

    Pia ushairi wa Kiswahili ulianza karne ya 10BK na ushairi wa Kiswahili ulikuwa ukitungwa na kughanwa kwa ghibu

    bila kuandikwa. Wataalam wengi wanakubaliana kuwa

    asili ya ushairi wa Kiswahili ni tungo simulizi hasa ngoma

    na nyimbo.

    Udhaifu mwingine katika mtazamo wake wa kusema kuwa ushairi ulianzia pwani ya kaskazini ya Kenya si kweli kwa

    kuwa waswahili walikuwepo hata sehemu nyingine kama

    vile Kilwa na Bagamoyo ambapo ushairi wa Kiswahili

    ulitumika.

  • 5

    Hoja ya kusema ushairi wa Kiswahili ulitokana na Kiarabu haina mashiko kwa kuwa waswahili walikuwepo hata

    kabla ya waarabu na walikuwa na ushairi wao isipokuwa

    ujio wao ulileta athari kubwa kwa kuwa ulichanganya na

    mambo ya dini ya kiislamu na hati.

    Knappert (1979) Four centuries of Swahili verse anasema; Ushairi wa Kiswahili ulichipuka kwenye upwa wa Kenya kutokana na nyimbo na ngoma za waswahili na ulianza katika

    karne ya 17 na pia ni ushairi wa Kiislamu wenye kuchanganya

    sifa za tungo za kiafrika na za kiajemi.

    Ubora wa hoja hii ni kwamba, ni kweli Knappert amekubali

    kuwa,ushairi wa Kiswahili ulitokana na waswahili wenyewe.

    Hata hivyo hoja yake ina udhaifu kwa kuwa ushairi wa

    Kiswahili ulianza kabla ya karne ya 10 BK na pia amejikita

    katika maudhui ya mambo mengine kama vile siasa, uchumi na

    kijamii. Vilevile amechanganya chimbuko la ushairi wa

    Kiswahili na Uarabu.

    2. Nadharia ya pili inasema kuwa ushairi ni zao la waswahili

    wenyewe.

    Nadharia hii imejadiliwa na wataalam mbalimbali akiwemo

    Shaban Robert, Jumanne Mayoka (1993) na Senkoro, Mulokozi

    na Sengo.

    Jumanne, M. Mayoka (1993) anasema ushairi umetokana na

    jamii ya wanadamu wenyewe na umesheheneza ukwasi mkubwa

    wa lugha ambayo imekuwa ikitumika katika hatua zote za

    kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni katika historia ambayo

    mwanadamu amepitia, Kwa mfano kuwa msamiati uliotumika

    tangu enzi za kuishi mapangoni, enzi za uwindaji, ujima,

  • 6

    utumwa, vita vya makabila, uvamizi wa wageni, ukoloni na

    harakati za kupambana na ukoloni hadi kupata uhuru na

    maendeleo yake.

    Ubora wa hoja

    Ubora wa hoja hii ni kwamba ina mashiko ndani yake kwa

    sababu, kila jamii ina sanaa yake na ushairi ni moja kati ya

    sanaa hizo ingawa inaweza ikaathiriwa na sanaa ya jamii

    nyingine. Pia ushairi umekuwa ukikua na kuendelea kadri jamii

    inavyokuwa na kuendelea.

    Udhaifu wa hoja.

    Udhaifu wa hoja hii ni kwamba si kweli kuwa katika kipindi

    hicho ushairi ulikuwa tayari umesheheni ukwasi mkubwa wa

    lugha, na kama ulikuwa kweli umesheheni huu ukwasi wa lugha

    alipaswa kutuonesha huo utajiri wa lugha anaouzungumzia

    katika ushairi.

    Senkoro (1988) anasema kuwa ushairi uliibuka pale lugha

    ilipoanza katika kipindi cha uhayawani (kipindi ambacho

    mwanadamu alipoanza kupambana na mazingira yake) kwenda

    katika kipindi cha urazini (maana) ili kumwezesha binadamu na

    mazingira yake kwa mfano, zana za kazi zilizotumika

    ziliwafanya waimbe kwa kufuata mdundo wa zana hizo.

    Masamba anasema kwamba kimsingi chimbuko la ushairi wa

    Kiswahili ni waswahili wenyewe katika nyimbo, ngoma nk

    ambazo ziliimbwa katika masuala ya kilimo, jando na unyago

    n.k. Massamba anaendelea kusema kwamba nyimbo hizi

    zilikuwa zikiimbwa bila kufuata vina na mizani lakini kwa kadri

    muda ulivyoenda walizidi kuziendeleza na kuziboresha. Hivyo

  • 7

    suala la vina na mizani lililetwa na wageni sio kiini cha ushairi

    wa kiswahili

    Mulokozi fasili ya fasihi haiwezi kutenganishwa na utamaduni

    wa maisha ya watu. Anaelezea kuwa ushairi wa Kiswahili

    hutumia lugha ya Kiswahili, hivyo ili kujua chimbuko la ushairi

    wa Kiswahili ni lazima ujue juu ya waswahili wenyewe

    Pamoja na kuwa nadharia hii imeonesha kukubalika na

    wataalamu mbalimbali kama vile Senkoro, Mayoka na Shekhe

    Amri Abeid, lakini bado ina mapungufu. Hii ni kwa sababu

    imeshindwa kuonesha muda maalumu ambapo ushairi wa

    Kiswahili ulianza na ni wapi ulianza kutumika. Hili ni suala

    ambalo linaumiza vichwa vya wataalamu mbalimbali hadi hivi

    sasa, kwani hakuna mtaalamu yoyote aliyefanikiwa kuonesha ni

    wapi na ni lini ushairi wa Kiswahili ulianza.

    Hivyo basi, kutokana na nadharia hizo mbili tunaungana na

    nadharia inayosema kuwa, chimbuko la ushairi wa Kiswahili ni

    zao la waswahili wenyewe, kwa sababu waswahili wana

    utamaduni wao ambao ulikuwepo kabla ya ujio wa Waarabu. Na

    waliutumia ushairi huo katika shughuli mbalimbali za kijamii,

    kwa mfano katika harusi, jando na unyago.

    AINA ZA USHAIRI/BAHARI ZA USHAIRI

    Kwa ujumla ushairi upo katika makundi mbalimbali. Uainishaji

    wa ushairi unategemea wataalam. Mlokozi (1996) anadai kuna

    bahari 13 za ushairi ambazo kwa mujibu wa tapo la wataalamu

    wa Mombassa

    1. Wimbo/Tathilitha

  • 8

    Shairi la aina ya wimbo lina mishororo 3 inayoweza kuwa na mikondo tofauti, unaweza kuwa na kina kimoja

    mwishoni

    Mara nyingi wimbo huwa na vipande viwili 2. Shairi/Tarbia

    Utungo ambao una mishororo 4 katika kila beti na kila mshororo una vipande 2

    Shairi huweza kuwa na maudhui ya namna yoyote ile 3. Utenzi/utendi

    Ni ushairi wenye mizani michache kuliko 12

    Una vina vinavyobadilikabadilika isipokuwa cha mwisho

    Kwa kawaida husimulia visa virefu vya kihistoria.mfn vita nk

    4. Zivindo

    Ni shairi linalofafanua maana ya maneno

    Lengo kuu ni kufunza lugha. Mfn shairi la Kihindi. 5. Tumbuizo

    Hauna idadi kamili ya mizani na mishororo

    Nia yake ni kutoa hisia ambazo zimembana mtu. Mfn Mbolezi-nyimbo za misibani, nyimbo za kubembelezea

    watoto

    6. Hamziyya

    Una mishororo miwili miwili na vina vyake viko mwisho tu wa beti

    Ulitungwa na Sharif Aidarus bin Uthman

    Ulikuwa ni wa kumsifu mtume Mohamadi S.W.A 7. Dura Mandhuma au Inkishafi

    Unatokana na utenzi wa mtu aliyeitwa Inkishafi

    Una mambo ya kuonya, kufuata mambo ya kidini na kuelekeza

  • 9

    8. Ukawafi

    Una mstari mmoja wenye vipande vitatu

    Ukwapi-silabi 6

    Utao-silabi 4

    Mwandamizi 5

    Zinahusu maudhui ya kidini 9. Wajiwaji

    Ni utungo ambao una mishororo 5 kila ubeti wenye mizani 5

    Zinahusiana na mambo ya kidini, kumsifu mtu shujaa na bingwa

    10. Wawe au Vave

    Asili yake ni kaskazini ya mwambao wa Pwani hasa sehemu za Amu na Pate

    Unahusu kilimo, ziliimbwa wakati wa kufyeka mistu, kuchoma pori nk

    11. Kimai

    Ni utungo unaohusu mambo ya baharini au wakati wavuvi wanapomtafuta mwenzao ambaye amepotea

    Ni utungo unaohusu ubaharia

    Idadi ya mizani hubadilika badilika na vina si vya lazima 12. Ngonjera

    ni mazungumzo au mabishano ya kishairi kuhusu mada Fulani

    huundwa kwa kulumbana pande mbili

    suluhisho la kile kinachojadiliwa hupatikana mwishoni 13. Kikwamba

    Ni utungo ambao neno moja hutumiwa kila mwanzo wa ubeti na neno hilo hufululizwa na mabadiliko

    mbalimbali.

  • 10

    MABADILIKO NA MAENDELEO YA USHAIRI

    WA KISWAHILI

    MAENDELEO YA KIHISTORIA:

    Wataalamu ambao wanajaribu kutupa taarifa kuhusu maendeleo ya ushairi wa Kiswahili ni pamoja na M.M.

    Mulokozi (1996) ambaye anatuambia kwamba ulianza

    karne ya 10BK

    Katika kipindi hiki hakukuwa na ushairi ambao ulikuwa umeandikwa kwa utamaduni wa Waswahili bali kulikuwa

    na ushairi simulizi uliganwa kwa ghibu

    Kuanzia miaka ya 1000BK wakati wa ukoloni kulitokea athari kubwa katika ushairi wa Kiswahili k.v hati ya

    maandishi na dini ya kiislamu

    Ushari uliwaunganisha Waswahili na duni pana ya umma na taaluma ya uandishi kwa hati ya Kiarabu uliwapa

    wenyeji ujuzi wa kusoma na tabia ya kuandika

    1000-1500BK

    Katika kipindi hiki kulikuwa na ustawi na ustaarabu wa kimji wa waswahili katika miji yote ya Pwani na

    biashara ilistawi kati ya wageni na wenyeji

    Katika kipindi hiki fasihi pia ilistawi Mashujaa wanaosimuliwa katika tendi k.v Fumo Lyongo

    waliishi kipindi hiki

    Ushairi uliendelea kuwa simulizi Ushairi wa mwanzo uliitwa SWIFA

    1500-1750BK

  • 11

    Hiki ni kipindi cha tatu na kilikuwa kipindi cha misukosuko ya wenyeji na Wareno

    Kulikuwa na tungo zilizohidhiwa zilizowahusu Wareno, Migeni, Poatugei afila

    Tungo nyingine zilikuwa ni utendi wa Hamziyya, Siri Lasinari, Utendi wa Tambuka 1723 nyingi zilikuwa

    zikiwapa moyo Waswahili

    Waswahili walifanikiwa kuwaondoa wareno.

    1750-1900

    Hiki kilikuwa ni kipindi cha nne, na kilikuwa ni kipindi cha utawala wa Waarabu

    Kulikuwa na migogoro mingi ya kivita katika utawala wa Waarabu

    Tabia za Mamwinyi, wafanya biashara, matajiri na wamisionari vilistawi

    Kipindi hiki kilitawaliwa na fasihi ya kidini ambayo ilitafakari theologia na falsafa ya maisha

    Kulikuwa na tendi nyingi zilizoibuka kuko Arabuni wakati wa mtume Muhamed. Mfn Shutaki, Angamia, Nakaa,

    Masahibu nk

    Pia kulikuwa na tungo za kitamaduni, mawaidha na tumbuizo. Mfn utendi wa Mwanakupona

    Washairi walijitokeza kuhusu mashairi ya kisiasa ambao ni Myaka bin Haji (1776-1840), huyu aliishi Mombassa.

    KARNE YA ISHIRINI (20)

  • 12

    Katika kipindi hiki uchapishaji wa magazeti na vitabu ulijitokeza. Kulikuwa na Asasi za kudai uhuru. Waandishi

    waliandika sana kuhusu kudai uhuru. Mfn Saada Kandoro

    Baada ya uhuru ushairi wa kisiasa ulienea zaidi kama vile Ngonjera na makue.

    MAJARIBIO NA MABADILIKO KATIKA USHAIRI

    WA KISWAHILI

    Senko ( ) anasema baada ya fahamu zake kufunguliwa alianza

    kuangalia mabadiliko katika ushairi.alidai kuwa kuwa kuwa

    dunia inabadilika hivyo na ushairi hauna budi kubadilika.

    Wangai Mwai (2008:73) fasihi hubadilika badilika katika kumbo na maudhui kwa hiyo ushairi wa Kiswahili sharti

    uruhusu mabadiliko yanapotokea.

    MGOGORO WA USHAIRI WA KISWAHILI

    Baadhi ya washairi kama vile E.Kezilahabi, M.M Mulokozi, K.K Kahigi na wengineo walinza kuandika kazi

    za ushairi zisizo na urari wa vina na mizani

    Wengi walichukulia na kurudi nyuma kwa ushairi lakini waandishi hao waliona ni hatua ya maendeleo

    Hivyo mashairi yaliyotungwa kwa mfumo huo yalipata majina mbalimbali kama vile Makue, Mtiririko, Mapingiti.

    Nk

    Na hivyo watungaji wa mashairi haya waliwaita wanamapinduzi na wengine wakawaita wachochezi

    Ibrahim Noor Shariff (1988:183) amedai kuwa mzozo uliibuka pale wanamabadiliko walipodai mambo matatu:

    1) Mbinu za kutunga mashairi zilikuwa chache mno

  • 13

    2) Sharia za kutunga mashairi ziliwanyima uhuru wa kutunga

    3) Muundo wa tungo za kishairi uliokuwa wa Kiswahili hapo awali haukuwa na vina wala mizani, hivyo sharia

    si za lazima.

    Kauli hizi za wanamabadiliko zilipingwa sana na wanamapokeo ambao waliamini kwamba urari wa vina na

    mizani ndiyo roho ya ushairi, ruwaza ya vina na mizani

    ndizo zinazoufanya ushairi wa Kiswahili ujitambulishe.

    Njogu na Chimerah (1999:113) wanadai kwamba mgogoro

    huu ulikuwa baina ya vijana na wazee waliokuwa

    wamekulia katika mazingira ya tungo za vina na mizani

    Mawazo yao kwa ujumla yalipingana kwa kiasi kikubwa na

    mawazo ya wanamapokeo japo kuna mazingira Fulani

    walifanana. Wanamabadiliko waliamini kuwa

    Hakuna sheria za kutunga mashairi (Kezilahabi 1977:60), kila shairi lina njia yake ya kutunga na njia yake ya kutoa

    mawazo.

    Dhamira/maudhui, mawazo, maadili na falsafa zitawale fani ya ushairi

    Walidai kuwa mabadiliko ya umbo la ushairi yamefungamana na maendeleo ya historia ya jamii zetu, ni

    sehemu ya jamii yetu,hivyo kubadilika kwa ushairi wa

    Kiswahili si kitu cha kigeni

    Vina na mizani ni kunga za utungaji zilizozuia ushairi wa Kiswahili kukua na kusambaa kwa mapana yake na marefu

    yake.

    Soma Njogu na Chimerah (1999) ufundishaji wa fasihi.

  • 14

    II. RIWAYA

    Riwaya sio utanzu wa muda mrefu sana bali ni utanzu ambao

    umeanza kushika mashiko hivi karibuni kuanzia karne ya 19

    huko Ulaya

    Encloypedia hudai kuwa riwaya ni ubunilizi ya kinathari1

    inayotosha kuwa kitabu (kitabu kwa mujibu wa UNESCO ni

    chapisho lolote lenye kuanzia kurasa 48 na kuendelea.) bunilizi

    ya kifasihi ni ambapo matukio mengi yamebuniwa

    Enclopedia Bratanica wanasema riwaya ni masimulizi marefu ya kubuni ya kinathari yaliyochangamana kiasi na yenye

    kuzungumzia tajiriba2 ya binadamu. Wanaendelea kusema

    kwamba kwa kawaida riwaya huwa na mfululizo wa matukio

    yanahusiana na yenye kulihusu kundi Fulani la watu kaka

    manthari mahususi

    Mphahlele (1976) anasema kwamba riwaya fupi huwa na

    kati ya maneno thelathini na tano elfu (35,000) na hamsini elfu

    (50,000) na riwaya ndefu zaidi inaweza kuwa na maneno zaidi

    ya sabini na tano elfu (75,000)

    Mhando na Balsidya wanadai kwamba katika riwaya

    lazima kuwe na mchanganyiko wa matukio na ujenzi wa

    wahusika naye Foaster (1949) anachangia kwa kusema kwamba

    riwaya lazima iwe na wakati.

    SIFA ZA RIWAYA

    Ni masimulizi ya kubuni Ni hadithi ya nathari katika masimulizi

    1 nadhari-ni maelezo ya kina yanayoelezea jambo kwa mapana (hii inafanya itofautiane na ushairi na tamthiliya

    2 Tajiriba ni uzoefu alio nao mtu. Uwe mbaya au mzuri

  • 15

    Ni ya mpangilio au hakuna mpangilio Inafungamana na wakati (yaani yale yanayotendeka katika

    jamii hiyo)

    Ina sifa ya urefu kama tulivyoona hapo juu Ina mawanda mapana (yaani inaweza kuzungumzia mambo

    kwa upana sana)

    Lazima kuwe na mchangamano wa visa mfano; katika riwaya ya Janga Sugu la Wazawa ina visa kama, ushirikina,

    vifo, mapenzi ya kweli na ya uongo,ndoa, mila nk

    Ina wahusika wengi

    CHIMBUKO LA RIWAYA

    Riwaya imejazwa na mambo makubwa mawili:

    1) Fani za kijadi za fasihi 2) Mazingira ya kijamii

    a) Ngano-hadithi za kubuni zinazohusu wanyama, watunzi wengi wameathiriwa na ngano kw wasababu wanachota

    visa, mbinu za kifani , dhamira katika ngano (zinaonekana

    kwamba ni za kingano zaidi)

    b) Visasili-masimulizi ya kubuni ambayo yanaeleza juu ya maisha, asili, ya vitu na hatima yake. Kwa kawaida visasili

    huaminiwa kuwa ni hadithi za kweli

    c) Visakale-ni hadithi za kale zinazohusu kabila la kale, udini nk. M.M.Mulokozi anasema kuwa kila kabila lina visakale

    vyake. Katika riwaya visakale vinajitokeza katika riwaya

    ya Kisima cha Giningi

  • 16

    d) Hekaya-ni hadithi za kusisimua kuhusu masaibu na matukio ya ajabu yasiyo ya kawaida, mara nyingi masaibu

    yanasababishwa na mapenzi, huwa ni ndefu kuliko hadithi

    nyingine lakini si ndefu kuliko riwaya. Katika taaluma ya

    Kiswahili ni riwaya ya Adili na Nduguze-Shaaban Robert,

    Riwaya ya Ubeberu Umeshindwa ya KIIMBILA( 1971) e) Tendi-ni hadithi ya kishairi kuhusu mashujaa wa kihistoria

    na wakubuni wa jamii au taifa.mfano Utendi wa Fumo

    Lyongo, kuna baadhi ya riwaya zimeiga mbinu za kiutendi.

    Mfano huko Ulaya Illiad Odyssey, Don Tuliv 1928, Toistoi

    (1828-1910). Mfano katika Afrika ni riwaya ya Ngugi wa

    Thiongo ya Matigali. f) Masimulizi ya wasafiri-ilihusu masaibu waliyopata wasafiri

    mbalimbali. Mfano Riwaya ya kiingereza ya kwanza ni

    Robinson Kruso ilihusu habari ya mhusika mkuu ambaye

    alikuwamo katika merikebu iliyozama na akaokoka na

    kuamua kuiishi katika kisiwa peke yake. Katika Kiswahili

    kuna riwaya kama vile utumwa Kwa Heri Iselamagazi hizi zote ziko katika muundo huu.

    Katika karne ya 16 fani nyingi ziliendelea. Na mojawapo ya

    sababu ya kuendelea kwa riwaya ilikuwa ni:

    1) Ukuaji mkubwa wa shughuli za kiuchumi huko Ulaya baada mapinduzi ya kiviwanda

    2) Mageuzi ya kijamii na kisiasa yaliyofungamana na mabadiliko ya kiuchumi

    3) Ugunduzi wa teknolojia ya upigaji chapa

  • 17

    Mpaka sasa hakuna vigezo maalumu vya uainishaji wa

    riwaya, kila mtaalamu huangalia kwa jinsi anavyoona yeye.

    Wengine wanaangalia muundo, mtindo, umbo,

    lengo/shabaha/historia. Madumula (2009:61 anasema

    riwaya inaweza kuainishwa kifani, kidhamira, kihistoria na kiitikadi

    Naye Mulokozi M.M (1996) anaonyesha michepuo miwili ya

    riwaya:

    1) Riwaya ya dhati 2) Riwaya pendwa

    Katika mhadhara huu tutaangalia riwaya kama alivyoainisha

    Madumula

    Inahusu maisha ya mtu binafsi, yaani mwandishi mwenyewe, tatizo hapa ni uaminifu wa mwandishi, si rahisi

    kuandika kweli yote.

    Mfano katika Kiswahili ni Riwaya Maisha yangu baada ya miaka 50 ya Shaaban Robert

    Inahusu mtu mwingine na siyo mwandishi mwenyewe Pia inahusu maisha ya mtu binafsi lakini ni maisha ya mtu

    mwingine na siyo ya mwandishi mwenyewe

    Ni matukio ya kusisimua ambayo hayajawatokea watu wengine

    Lengo kuu ni kueleza ugumu wa maisha ya maisha ya mhusika mkuu jinsi anavyopambana na maisha. Mfano

    Wasifu wa Siti Binti Saadi ya Shaaban Robert

  • 18

    Ina lengo la kufundisha maadili mema ambayo ndiyo msingi katika maisha

    Inahusu: mateso na uvumilivu, majuto baada ya kutambua kosa. Mfano katia Kiswahili ni Adili na Nduguze,

    Kusadikika, Kufikirika-zote za Shaaban Robert

    Huchanganya historia halisi na sanaa ili kuleta maudhui Fulani

    Hazielezi matukio yote ya kihistoria bali yale ya muhimu tu, yaliyoathiri mwelekeo na mwenendo wa jamii Fulani

    Maudhui yake ni kumbukumbu ya mambo yaliyopita na dhamira zake huwagusa watu wengi. Mfano katika

    Kiswahili ni Riwaya ya Uhuru wa Watumwa ya J. Botela,

    Kwa Heri Iselamagazi ya J Mapalala, Zawadi ya Ushindi

    ya Beni Mtobwa, na Njozi iliyopotea ya Mungongo

    Inahusu maisha ya watu na msisitizo wake ni katika mila, desturi na mabadiliko ya kijamii

    Dhamira huanzia ngazi ya familia hadi kitaifa na hata kiulimwengu

    Husawiri matatizo yaliyo katika jamii kwa kuonyesha chanzo chake. Mfano katika Kiswahili ni Dunia Uwanja

    wa Fujo ya Kezilahabi, Siku ya Watenzi Wote ya

    Shaaban Robert na Harusi ya J.Safari

    Aina hii inaweka mkazo juu ya mikinzano ya ndani ya binadamu, kiakili, kinafsi na kijinsia

    Huonyesha uwezo na udhaifu wa binadamu katika kuzikabili hali ngumu za maisha

  • 19

    Mhusika mkuu husukumwa katika ukingo wa aidha kufa ili ayaepuke matatizo au aishi na hayo matatizo. Mfano katika

    Kiswahili ni riwaya ya KIU ya Muhamedi S.Abdalah,

    Nyota ya Rehema ya huyu huyu Muhamed, Rosa Misitika

    ya Kezilahabi na Kichwa Maji ya Kezilahabi

    Ni riwaya ambayo inajadili matatizo ya kisiasa Inalenga kuleta mabadiliko ya kisiasa na kijamii Mara nyingi riwaya za kimapinduzi zina mwelekeo wa

    kisosholisti ambapo mlengwa mkuu ni umma kushika

    hatamu

    Mkazo upo katika ITIKADI kama msingi na dira ya kuongoza jamii

    Wahusika wake wanatoka katika matabaka mbalimbali Mfano katika Kiswahili ni riwaya ya KULI ya Adamu

    Shafi, Utengano ya Saidi A Mohamed, Dunia Mti Mkavu

    ya S.A.Muhamedina KASRI MWINYIFUAD ya Shafi A

    Shafi

    Inajadili migogoro na maisha ya binadamu kwa kutafakari kwa mantiki na kwa kina kuhusu mambo yanayohusu

    maisha

    Inajadili maswali kama vile: maana ya maisha nini? Hatima ya binadamu nini? Uhusiano wa binadamu na malaika

    ukoje?

    Mifano ya riwaya ya kifalsafa ni: Mzingire, dunia uwanja wa fujo, Nagona, babu alivyokumbuka ya S.A Muhamedi,

    Riwaya ya Binadamu-ya K.w Wamitila. Riwaya hizi ni

    ngumu sana kuelewa zinaelezea, hata wahusika wake ni wa

    kufikirika zaidi, mfn wanyama nk

  • 20

    Ni riwaya ambazo hujishughulisha na masuala ya upelelezi, mapenzi na ujasusi, mara nyingine zinahusisha

    mapigano ya kimwili na ya kiakili kati ya mtu mmoja na

    watu wengi. Na mara nyingi huyu mtu mmoja

    huwashinda watu wengi

    Riwaya hii inakuwa na mhusika mkuu mkweli (ambaye anapewa sifa ambazo zinazidi uwezo wa mwanadamu

    wa kawaida-yaani huwezi kumshinda kuanzia mwanzo

    hadi mwisho). Riwaya za namna hii zina chumvi nyingi.

    Mfano Riwaya ya Kifo ni haki yangu mhusika wake mkuu Camila anayekata nyeti za wanaume. Mfano

    mwingine ni Simu ya kifa ya Faraji Katambula, Kikosi

    cha Kisasi ya E.Musiba. Mzimu wa watu wa kale, Kosa

    la Bwana Msa-vya Muhamedi S.Abdula-mhusika wake

    mkuu ni Msa

    Utanzu wa riwaya umekuja baada ya utanzu wa ushairi na tamthiliya lakini ukuaji wake umekuwa kwa kasi

    kubwa. Inasemekana kwamba riwaya ya Kiswahili

    ilianza kujitokeza katika mwisho mwa karne ya kumi na

    tisa. Kwa nini ilichelewa sana hapa Afrika? Sababu yake

    ni kwamba

    1. Hadhira kubwa ya watu haikujua kusoma na kuandika

    2. Hadhira kubwa ya watu haikuweza kununua vitabu

    3. Jamii ya waswahili haikuwa na mitambo ya kupigia chapa

    na pia haikuwa na mfumo mzuri wa usambazaji

    vitabu(hapakuwa na printers nk)

  • 21

    Hivyo tunaona kwamba wakati wa ujio wa wakoloni

    ulisababisha kuanzishwa kwa baadhi ya vituo vya kupigia

    chapa, kwa mujibu wa Mulokozi ( ) anasema ukoloni uliweka

    mazingira ambayo yameweza kuilea riwaya. Mfano: hati ya

    maandishi ya Kirumi, mfumo wa usambaji wa vitabu

    Mwanzo riwaya ya Kiswahili ilianza kujitokeza kwanza kama

    tafsiri ya kazi za nje, hivyo tafsiri nayo ilisaidia sana

    kuchipuka kwa riwaya. Kwa kadri tafsiri zilivyokuwa

    zikifanywa, waswahili walianza kuiga vitabu hivyo.

    Kamati hii ilihimiza uandishi katika lugha ya Kiswahili kwa

    njia ya kushindana. Hivyo ilianzisha mashindano ya uandishi

    wa Kiswahili. Riwaya ya kwanza ya Kiswahili ilikuwa Uhuru

    wa Watumwa ya MBOTELA Ilichapwa mwaka 1934, riwaya

    nyingine ni riwaya ya Mzimu wa watu wa kalena Simu ya Kifo

    Kulijitokeza riwaya ambazo zilikuwa zikifuata mkondo wa

    kingano.Njogu na Chimerah (2008) wanaeleza

    kuwakimaudhui riwaya nyingi zilikuwa na mambo ya kimila na tabia kama njia ya kutunza maadili. Miongoni mwa riwaya

    hizo ni Utu bora mkulima, Kufikirika, Kusaidikika, Adili na

    Nduguze na Siku za watenzi wote zote za Shaaban Roberti.

    Kulikuwa na mambo yafuatayo:

    Ukombozi wa bara la Afrika na ujenzi wa jamii mpya, hivyo

    maudhui yake yalikuwa ni ujenzi wa jamii mpya na:

  • 22

    Kusuta ubinafsi na ukandamizaji

    Zilikuwa zikihakiki unyama wa maisha ya kimiji

    Zilikuwa zikiielekeza jamii katika mkondo wa kibinadamu katika usawa na ustawi. Mfano riwaya hizo ni LILA NA FILA,

    KABURI BILA MSALABA-iliandikwa na KAREITHI

    Katika kipindi hiki pia kulijitokeza kundi la Riwaya Pendwa

    zilizohusu upelelezi na uharifu mfano Mzimu wa watu wa

    kale, Kisima cha Giningi, Simu ya Kifo

    Zile za uharifu ni MTAKA YOTE HUKOSA YOTE ya Leo

    Odera Omera, Tatizo Kisauni ya CHADHORO

    Ni kipindi cha kupevuka na kushamiri kwa riwaya ya Kiswahili, katika kipindi hiki riwaya nyingi zilianza

    kujishughulisha na uongozi na usaliti wa kisiasa.

    Njogu na Chimerah (2008) wanadai wasanii walianza kutafakari jinsi ukoloni ulivyoanza kufungua milango

    kwa watu wachache na kutumia mali kwa manufaa yao

    wenyewe

    Katika kipindi hiki kuliibuka riwaya za kihistoria kwa mfano KWA HERI ISELAMAGAZI iliyoandikwa na

    Mapalala. Miradi Babu ya wazalendo.

    Katika kipindi hiki kulizuka riwaya ya kifalsafa na ya majaribio. Mfano Nagona 1987, Mzingile(1991)-

    Kezilahabi. Riwaya ya Zilahiri na Zirani ya William

    Katika kipindi hiki kulikuwa na ongezeko la riwaya ya vijana na watoto. Mfano wa riwaya hizo ni Mashujaa wa

    Kaza kamba-ya Shija (1980) wimbo wa Sokomoko

    (1990), Ngome ya Mianzi (1990), Ngoma ya

  • 23

    Mianzi(1991) Moto wa Mianzi (1995) zote hizi ni za

    Mulokozi.

    Fasihi huithamini jamii kihistoria, kiitikadi, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni na kijamii, na kwa kuwa jamii

    imekuwa ikibadilika badilika kimtazamo, fasihi nayo

    imekuwa ikibadilika kwa sababu jamii inabadilia. Na hivyo

    fasihi nayo inahitaji kupokea mabadiliko hayo ili kwendana

    na jamii husika.

    Mabadiliko katika riwaya (fasihi) yanatokea kwa sababu ya wasanii kutumia vionjo vipya katika kuziumba kazi

    zao. Kama anavyosema Khamisi (2007) anasema,mara moja

    tunaona neno kionjo linajisemea lenyewe kimya kimya juu ya

    mabadiliko ya utanzu wa fasihi. Lengo la mabadiliko hayo ni

    kwamba chenye mwanzo hakikosi kuwa na mwisho

    Utanzu wa riwaya ya Kiswahili haukuepuka mabadiliko. Sababu zilizobadilisha mabadiliko haya ni makali

    ya wembe wa kisiasa, mfano nchini Kenya makali ya kisiasa

    yalikuwa dhidi ya Masosholisti. Mfano wa riwaya ni Gamba

    la Nyoka,

    Majaribio na mabadiliko ya riwaya ya Kiswahili yalianza pale ambapo waandishi wengi wa Kenya na

    Tanzania walipoanza kukataa kukubali kila kitu

    walichokisikia. Walipoanzaa kukataa kanuni za jamii za

    ughunaji, hivyo wakaanza kuandika riwaya tofauti na za

    mwanzo.

  • 24

    Madumula anawanukuu SCHOLES na APLLOE riwaya huweza kubadiliko kutokana na utanzu wenyewe

    kuwa hauna mashiko legelege na tepetepe, hubadilika badilika

    Hivyo kutokana na majaribio na mabadiliko katika riwaya ya Kiswahili tunaona upywa katika kazi za riwaya

    katika fani na maudhui yake. Kisanaa riwaya hizi

    zinachanganya uhalisia na falsafia. Mfano wa riwaya ya

    Kufikirika. Mfano mwingine ni UKIUSHI-Mtiririko

    haueleweki, na riwaya hizi zinakuwa na mwingiliano matini

    yaani kuchanganya kazi nyingi katika kazi moja.kisanaa pia

    zina wahusika wa kidhani

    Pia riwaya hizi zina mazingaombwe sana, kwa mfano katika Nagona lugha yake ni ya mafumbo, visasili, pia ni

    lugha inayoelekeza, haifafanui sana.kimaudhui riwaya hizi za

    majaribio inatazama matatizo kwa mtazamo wa ndani.

    Inashughulikia masuala ya ulimwengu wote, riwaya hizi pia

    kimaudhui zinaitetea dunia dhidi ya maangamizi ya uovu

    mkubwa.

    3. TAMTHILIYA NA DRAMA

    Kumekuwa na mkanganyiko kati ya dhana hizi mbili, watu

    wamekuwa wakizichanganya sana.

    Tamthiliya ni drama na kinyume chake

    Tamthiliya ni drama lakini si drama zote ni tamthiliya

    A. TAMTHILIYA

    Mulokozi (1999:88) tamthiliya ni kazi iliyokusudiwa kutendwa jukwaani kwa ajili ya hadhira fulani

  • 25

    Tamthiliya huitwa mchezo wa kuigiza. Istilahi hii tamthiliya imetokana na neno methali lenye maana ya

    mfano/ishara ya kitu

    Wamitila (2003)tamthiliya ni kazi ya kidrama na ya kimaongezi ambayo huigizwa mbele ya hadhira/kazi

    iliyoandikwa ili kusomwa

    Kimuundo tamthiliya hudhihilika katika:

    matendo na maonyesho, mazungumzo huchukua sehemu kubwa katika uwasilishwaji wake wa maudhui (huwa

    katika diolojia)

    haiweki msisitizo mkubwa katika uwasilishwaji wake jukwaani wakati drama inaweka msisitizo mkubwa katika

    uwasilishwaji wake

    Penina Mhando anadai kuwa Tamthiliya ni ule utungo unaoweza kuwa umeandikwa au haukuandikwa ambao

    ambao unaliweka wazo linalotaka kuwasilishwa katika

    umbo la tukio la kiliwezesha kutendeka mbele ya hadhira

    Kutokana na sifa hii ya kutendeka jukwaani tamthiliya inawekwa kwenye kundi la sanaa za maonyesho(Mulokozi)

    SANAA ZA MAONYESHO

    Mohamedi na Balysidya wanasema kuwa sanaa za maonyesho

    ni kitendo chochote chenye sifa 4

    a) Mchezo b) Mchezaji c) Uwanja wa kutendea d) Watazamaji

    tamthiliya ni andiko la kiuigizaji linalotoa simulio kwa

    kuonyesha maneno na matendo

  • 26

    B. DRAMA

    Wamitila (2003) anasema ni aina ya utanzu wa fasihi ambao kimsingi hudhamiriwa kuigizwa mbele ya hadhira inaweza kuwa imeandikwa au haikuandikwa lakini msisitizo wake ni

    kuigizwa

    Msingi mkuu wa drama ni utendaji na utanzu huu umebuniwa kwa ajili ya thieta

    Wahusika hupewa majina ya kuigiza mbele ya hadhira

    Iwochukuu (2000) anasema drama ni mabadiliko, ubunifu na usawiri wa uhalisi jukwaani. Msingi mkuu wa drama ni

    matendo. Hoja hii imeungwa mkono na Aristotle anayeifafanua

    drama kama uigaji wa matendo

    Bretcht anasisitiza kuwa drama si uigaji wa matendo pekee pia ni chombo cha ufafanuzi wa hali za kijamii, chombo

    cha mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi

    Kitendo huitwa drama endapo kitendo hicho ni mwigo wa kitendo cha kilichokwishatangulia.

    DRAMA ZA KIJADI

    Jamii ya waafrika ikiwemo ambayo utamaduni wake ulikuwa

    haujaingiliwa na wakoloni ilikuwa na sanaa ya maonyesho

    zilizogawanyika katika makundi mbalimbali. Balisdya na

    Mhando walianisha aina mbalimbali za drama hizo

    1. SHEREHE

    Zilihusishwa na kundi moja kwenda kundi jingine mfano. Jando na unyago, jina kwa mtoto, kuota meno nk

    Ziliambatana na madaraka kwa mwanajamaii ya mwanajamii aliyeingia katika kundi jipya. sherehe

  • 27

    ziliwekwa katika katika umbo la vitendo na vikapewa uzuri

    wa kisanaa

    2. NGOMA

    Mhando na Balisdya wanasema ni chombo, sherehe au uchezeshaji wa viungo vya mwili. Malengo yake ni

    kuburudisha

    3. MASIMULIZI YA HADITHI

    Katika usimuliaji wa hadithi kuna vipengele vya kidrama vinavyojitokeza. Yaani:

    Usimuliaji Uigizaji Uimbaji Muziki

    4. KUSALIA MIUNGU

    Jamii fulani inapopata mafanikio au matatizo fulani ndipo huenda kutambikia miungu yao kwa kushukuru au

    kuomba kutatuliwa matatizo yao

    5. MAJIGAMBO

    Masimulizi ya kujigamba ya mtu kuhusu mambo ya kishujaa aliyopata kuyatenda maishani mwake

    Kwa kawaida hutumia lugha ya kishairi na masimulizi huambatana na vitendo vya majigambo yenyewe.

    Pia yaliambatana na matumizi ya maleba

    AINA ZA TAMTHILIYA

    1. TANZIA

    Ni tamthiliya yenye huzuni inayogusa hisia za wasomaji kiasi cha kuogopesha na kumuonea huruma mhusika mkuu ambaye

    hupatwa na masahibu/matatizo/majanga hayo

  • 28

    Msingi mkuu inalenga msomaji kupata hisia

    Mhusika mkuu huwa ni maarufu

    Aristotle anasema kuwa mhusika mkuu lazima atoke katika familia yenye nasaba bora/tabaka la juu

    Si tanzia zote mhusika anatoka tabaka la juu. Mfano KIFO KISIMANI-mhusika mkuu hapa anatokea katika tabaka la

    chini kabisa

    Misingi ya utokeaji wa tanzia

    Iamushe hisia za woga na huruma miongoni mwa hadhira

    Shujaa lazima awe mtu mwema, sura nzuri,umbo zuri, ili yanayomtokea yasitarajiwe

    Mhusika huonyesha kuumia kadri mtu anavyoonekana kuwa ni mwema na ana umbo zuri.

    Anguko la shujaa huja kutokana na uamuzi wake ama kosa lake mwenyewe

    Katika tanzia ya kirasimi shujaa hutoka katika nasaba bora 2. RAMSA/KOMEDI

    Ni tamthiliya ambayo inachangamsha na huishia kwa kufurahisha/ni tamthiliya ya vichekesho, hii haina maana

    kwamba haina maudhui mazito ndani yake.

    Inashughulikia mambo yale yale yanayoweza kushughulikiwa na tanzia. Mfano masuala ya unafiki,uzembe, wivu nk, hata

    hivyo inayashughulikia kwa namna tofauti na tanzia

    Kwa kawaida wahusika wa Ramsa huumbwa vibaya kuliko walivyo

    Udhati wa ramsa si kwamba usanii humalizika katika kicheko/furaha zaidi ni kuishia mhusika mkuu kufanikiwa

    shujaa wa kiramsa

  • 29

    Si lazima awe mtu maalum/mbabe au shujaa, anaweza kuwa mtu wa kawaida

    Kwa mujibu wa Aristotle anasema mhusika wa ramsa lazima awe mtu wa wastani chini ya wastani, awe ni mtu ambaye

    hatarajiwi kujitokeza na mtu wa nasaba duni na matendo yake

    yawe ya ucheshi

    Ni lazima awe mtu ambaye akifanikiwa wasomaji au watazamaji watafurahi

    uhusika wa wahusika wa ramsa

    Ramsa inawahusu watu wa kawaida kuliko ilivyo tanzia

    Inawahusu watu wa kipato cha kati na cha chini

    Na dhamira zote huelekezwa kwa watu wa kipato cha chini na duni. Mfano walalahoi

    AINA ZA RAMSA

    a) UTANI

    Ni aina ya ramsa ambayo mambo inayozungumzia yanaokana kuwa ya kipuuzi

    Mambo hugeuzwa kuwa kinyume kabisa na jinsi yalivyo

    Kwa kawaida sura za wahusika hubadilishwa kuwa kama vinyago

    Lengo kuu ni kuchekesha-ambalo ndilo haswaa, lengo la tamthiliya ya ramsa

    b) RAMSA ZA MAPENZI/MAHABA

  • 30

    Hizi zinahusu mapenzi ambapo wapendanao huwekewa vikwazo kama vile fedha, elimu, din,

    kabila nk

    Wahusika hawa hushinda vikwazo hivyo c) TASHTITI/DHIHAKA

    Zinalenga kwa viongozi wa kisiasa au dini

    Zinawahusu matapeli, wanafiki, wala rushwa, ni

    Mhusika mkuu anakuwa na sifa za utapeli nk

    Lengo kuu ni kumdhihaki huyu kiongozi ili aachane na tabia hizo

    ni njia ya walalahoi kupeleka malalamiko yao kwa viongozi

    SIFA ZA RAMSA

    Sharti ivutie akili na siyo hisia

    Ni lazima kuwa na matendo bila kufikiria hii itapelekea msomaji au mtazamaji kujua kwamba

    wahusika hawa hawana akili

    lazima iwe na hali ya utu (ikitukumbusha ubinadamu wetu)

    sharti iwe na mila na desturi ambazo hadhira inazifahamu toka katika jamii yake

    Hadhira isiogope au kupata uchungu kwa sababu hii sio lengo lengo la ramsa

    Wahusika wa ramsa hujaribu kuepuka vikwazo ambavyo vimewekwa

    Inaonyesha haja ya kuikomboa nafsi Mfano wa ramsa ni kama vile MFALME JUHA

    d) TANZIA-RAMSA

  • 31

    Hii ni tamthiliya ambayo inaonyesha mabaliko ya aina fulani yanayogeuza matukio ya tanzia kuwa ya ramsa

    Ni tamthiliya inayochanganya vipengele vya tanzia na ramsa

    Hutumiwa sawa na tamthiliya ya kibwege-hii ni

    tamthiliya ambayo inaonyesha kwamba kicheko au

    furaha ndiyo jibu pekee la maisha kwa watu ambao

    hawana imani na maisha ambao kwao misingi

    dhabiti ya maisha imeondoleo. Mfano tamthiliya ya

    AMEZIDI ya S.A Mohamedi

    e) MELO-DRAMA

    CHIMBUKO , MABADILIKO NA MAENDELEO YA

    TAMTHILIYA YA KISWAHILI

    CHIMBUKO: Tamthiliya chimbuko lake duniani kote

    linashahibiana/zinapatikana duniani kote na kuonekana

    katika maumbo tofauti tofauti. Tamthiliya inahusishwa

    sana na visakale na matendo ya kidini. Katika bara la Ulaya

    tamthiliya inahusishwa na miviga ya kidini katika jamii ya

    Wayunani/Wagiriki wa zamani/ancient Greek. Miviga hii

    katika jamii ya wayunani iliambatana na dua ya

    kuzaliwa..mpaka kufa na kuoza na kuwa binadamu tena

    Huko India tamthiliya zilitokana na tenzi zilizoitwa

    Mahabharata na pia zilitokana na miviga zilizoendana na utendi wa tendi hizo kutika mahekalu ya

    kidini

    Kule Japani na China-drama inatokana na dansi na

    miviga ya kidini baadaye miviga hii ilijitenga na dini na

    kuanza kujishughulisha na sanaa

    Katika Afrika-maigizo ya tamthiliya yalikuwa

    yanapatikana huko Misiri na maigizo haya yalikuwa

  • 32

    yanahusu kufa na kufufuka kwa mungu wa wamisiri

    aliyeitwa osiais. Miviga hii ilikuwa inaigizwa kila mwaka

    kwa miaka kama elfu mbili. Pia katika Afrika kulikuwa na

    maigizo ambayo hayakuwa yameandikwa lakini yalikuwa

    ni sehemu ya matendo ya kijamii yaani miviga na ngoma.

    Kulikuwa na tamthiliya bubu, maigizo ya watoto na

    maigizo ya watani. Drama hizi zilikuwa

    zikifungamanishwa na fasihi simulizi

    Hivyo tamthiliya inatokana na mambo makuu matatu

    a. Miviga na viviga vya kijamii, na dini pamoja na tendi b. Usawilishaji wa maisha ya kawaida kwa ajili ya burudani,

    elimu nk

    c. Sanaa za maonyesho za kijadi; ngoma na dansi

    BWANA YESU ASIFIWE SANA

    0786 684062 0715684062

    PASTOR: SENI DANIEL JOHN

    B.A KISWAHILI