YALIYOMO · 2 mstari huu hata wewe unayesoma unaona wazi kuwa Mstari hausemi kuwa Mungu ananafsi...
Transcript of YALIYOMO · 2 mstari huu hata wewe unayesoma unaona wazi kuwa Mstari hausemi kuwa Mungu ananafsi...
YALIYOMO
SOMO LA KWANZA ................................................................ 1
1 YOHANA 5:8. .................................................................... 1
SOMO LA PILI .......................................................................... 5
MUNGU NI NAFSI NGAPI? ................................................ 5
SOMO LA TATU ..................................................................... 11
UUNGU WA MWANA WA MUNGU ................................ 11
SOMO LA NNE ....................................................................... 23
ROHO MTAKATIFU NI NANI? ....................................... 23
1
SOMO LA KWANZA
1 YOHANA 5:8.
Habari za muda huu mpendwa
katika Bwana. Binafsi huwa
sipendi kuingia katika mabishano
kwa maana naona kuwa hayaleti
umoja katika imani. Pia nimeona
kuwa Whatsapp au mitandao ya
kijamii sio njia nzuri sana ya
kuweza kuongea kwa kina kuhusu
kile ambacho nataka kusema. Kwa
kuona hivyo nimeona niandike
kwa ufupi yote ambayo nataka
kusema wenda unaweza
ukanielewa kwa kina na nikuache
ukitafakari.
Kama jinsi ilivyo mtu yoyote yule
ambaye anaamini katika fundisho
la utatu, unaamini kuwa kuna
Mungu mmoja Baba, mwana na
Roho mtakatifu. Unaamini kuwa
Baba ni nafsi ya kwanza, mwana ni
nafsi ya Pili, Roho mtakatifu ni
nafsi ya tatu. Ninajua kuwa wewe
ni mwanafunzi wa Biblia na
unapenda kufundisha kile
ambacho wewe unaona ni sahihi.
Na pia unapenda kujifunza Biblia.
Na Mungu akubariki kwa hilo.
Katika mazungumzo yetu tulikuwa
tunaongelea mambo mengi kwa
wakati mmoja na nimeona kwa
mtu wa wakaida ni vigumu sana
kunielewa kile ninachotaka
kusema. Kwanini inakuwa ni
ngumu kunielewa? Nikwasababu
kila hoja niliyokuwa naleta
hakukuwa na mtiririko mzuri ili
kwamba hata anayefatilia aweze
kuelewa vyema. Kwa kuona hivyo
nimeona sio jambo jema niliache
swala hili hewani na ukaondoka
hali hujanielewa. Kwa vile kila
kitu lazima kilinganishwe na jinsi
Biblia inavyosema, katika kitabu
hiki kidogo sitotumia kitabu
chochote kile ila Biblia.Kwa
kuanza naomba nianze na mstari
mkuu ambao tulikuwa tunaujadili,
mstari huu ni,
1 Yohana 5
8 Kwa maana wako watatu
washuhudiao [mbinguni, Baba, na
Neno, na Roho Mtakatifu, na
watatu hawa ni umoja
Huu ni moja kati ya mistari
ambayo inatumika kuthibitisha
kuwa Mungu ananafsi tatu. Katika
mstari huu kuna jambo ambalo
hata wewe unaweza kuligundua
kama ukisoma vizuri, utagundua
mambo haya,
1. Kuna Ushuhuda
2. Kuna Baba mwana na Roho
3. Kuna umoja kati ya Baba
mwana na Roho
Haya mambo matatu unaweza
kuyaona wazi kabisa. Katika
2
mstari huu hata wewe unayesoma
unaona wazi kuwa Mstari hausemi
kuwa Mungu ananafsi tatu. Sio
lengo langu nikuelewe vibaya
lakini nataka kukuonesha kuwa
mstari hausemi kuwa Baba mwana
na Roho ni nafsi tatu za Mungu.
Kwa vile sisi kama wakristo
tunatakiwa kutumia neno
“Imeandikwa” kama ndio msingi
katika kutafsiri maandiko na
kuelewa vyema maandiko,
tunaona wazi kuwa hakuna
ushahidi wa kile tunachotaka
kukizungumzia. Kwa macho
yangu na kwa macho yako wote
wawili tunaona kuwa mstari
haujasema kuwa Baba, mwana na
Roho mtakatifu ni nafsi za Mungu.
Sasa tutizame maana na neno
“umoja”. Nafikiri tumetumia hili
neno mara nyingi sana. Na pale
tunapolitumia tunawasilisha kile
ambacho tunataka wengine
wakielewe. Mara nyingi huwa tuna
tumia maneno kama vile “umoja ni
nguvu” hakuna hata mmoja
ambaye ataelewa vibaya kile
ambacho tunataka kumaanisha
katika kauli hiyo. Kila mmoja
ataelewa kuwa maana ya neno
“umoja” ni ushirikiano katika
chochote kile ambacho tutakuwa
tunafanya.
Napenda kukuuliza swali, je
nikisema Dani, Peter na David
wanaumoja, je maana itakayokuja
kichwani mwako ni kuwa Hawa
watatu wanaushirikiano, au hawa
watatu ni mtu mmoja katika nafsi
tatu?
Swali hili nimeuliza ili uweze
kutafakari kwa kina kuhusu maana
halisi ya umoja katika mstari huu.
Yesu alikuwa na mitume 12. Na
hawa mitume walikuwa na umoja.
Je umoja wao uliwafanya wawe
mtume mmoja katika nafsi 12?
Sidhani kama hata wewe unaweza
kuelewa hivyo. Umoja wa watu
hauwafanyi waungane na kuwa
mwili mmoja katika nafsi
mbalimbali. Bali kila mmoja ni
nafsi huru.
Sasa turudi katika mstari huo
ambao nimetoka kuuonesha.
Katika mstari huo imeonesha wazi
nini chanzo cha Baba, mwana na
Roho kuwa na umoja. Chanzo cha
Baba, mwana na Roho kuwa na
umoja ni ushuhuda wanaoutoa. Ni
wazi kuwa hata wewe ukiwa na
marafiki zako kama kile
unachosema ni sawa na kile
ambacho marafiki zako wanasema
ni wazi kuwa wewe unaumoja na
marafiki zako. Ushuhuda wa Baba
ni sawa na ushuhuda wa Mwana na
ushuhuda wa Mwana ni sawa na
ushuhuda wa Roho mtakatifu.
Kutokana na ushuhuda huu ndio
mana hawa watatu ni umoja.
3
Tukumbuke kuwa Biblia imesema
kuwa hawa watatu ni “umoja” na
wala sio “Mungu mmoja” haya
maneno mawili hayapo sawa na
ndio maana watu wengi
wanashindwa kupata maana kamili
ya kile ambacho mstari unataka
kukisema. Kama ukisoma mstari
huu katika fikra kuwa hawa tatu ni
“Mungu mmoja” basi
utashawishika kuona Baba,
mwana na Roho ni nafsi tatu za
Mungu. Lakini ukweli ni kwamba
Mstari haujasema hivyo na wala
haujasema kuwa Baba, mwana na
Roho ni Mungu mmoja, bali
umesema kuwa Baba, mwana na
Roho ni umoja.
Nafikiri mpaka kufikia hapa
unaanza kuona utofauti na ule
mstari ambao umekuwa ukidhani
kuwa unaonesha kuwa Mungu ni
nafsi tatu sasa unaanza kuona
kuwa haoneshi hivyo. Kwa maana
kama kweli ni nafsi tatu basi Biblia
ingesema wazi kabisa kuwa Baba
mwana na Roho ni nafsi tatu za
Mungu mmoja. Hakuna mtu
yoyote ambaye angebishana na
Biblia. Lakini hata wewe
ukiangalia wazi mstari huo unaona
imesema,
1 Yohana 5:8
Kwa maana wako watatu
washuhudiao [mbinguni, Baba, na
Neno, na Roho Mtakatifu, na
watatu hawa ni umoja
Umoja wa Baba, Mwana na Roho
ni kutokana na ushuhuda
wanaoutoa. Hii inamaana kama
Baba anatoa ushuhuda tofauti na
Mwana basi ni wazi kuwa
hakutakuwa na umoja. Kile
ninachotaka kusema kimewekwa
wazi kabisa katika mstari unaofata,
1 Yohana 5:9
Kisha wako watatu washuhudiao
duniani], Roho, na maji, na damu;
na watatu hawa hupatana kwa
habari moja. Tukiupokea
ushuhuda wa wanadamu,
ushuhuda wa Mungu ni mkuu
zaidi; kwa maana ushuhuda wa
Mungu ndio huu, kwamba
amemshuhudia Mwanawe
Tunaona kuwa Roho, Maji na
damu hupatana katika habari moja.
Ni wazi kuwa ushuhuda wa Roho
ni sawa na ushuhuda wa Maji na
ushuhuda wa maji ni sawa na
ushuhuda wa damu. Hakuna mtu
yoyote ambaye anaweza kuelewa
kuwa umoja wa roho, maji na
damu yani washuhudiano duniani
unawafanya wawe mmoja katika
nafsi tatu. Hata wewe najua
hautaweza kukubali, bali utakubali
wazi kuwa watatu wanaoshuhudia
duniani hupatana katika habari
moja sawa na watatu wa mbinguni
4
ambao pia wanapatana katika
habari moja.
Tukumbuke kuwa Yesu
alimwambia Petro kuwa
litakalofungwa duniani litakuwa
limefungwa mbinguni. Na pia
Yesu alitufundisha,
Mathayo 6
10 Mapenzi yako yatimizwe, hapa
duniani kama huko mbinguni.
Inamaana kuwa Hata ushuhuda wa
watatu wa hapa duniani ni sawa na
ushuhuda wa watatu wa juu
mbinguni kwa maana Hapa
duniani ni kama huko mbinguni.
Hii inatosha kabisa kutufanya
tuelewe kuwa kama washuhudiao
Duniani wanapatana katika habari
mmoja, ni wazi kuwa hata
wanaoshuhudia mbinguni nao
wanapata katika habari moja.
Lakini mara nyingi tunaposoma
mstari huo tunashindwa kupata
maana kamili kile mstari unataka
kusema. Lakini naamini kuwa
maelezo kwa ufupi niliyoyatoa
kuhusu mstari huu yanatosha
kukupa mwangaza kuwa Biblia
haijasema kuwa Mungu ana nafsi
tatu. Na wala mstari haujasema
kuwa Baba, mwana na roho ni
nafsi za Mungu mmoja. Kama
umenielewa vyema hapa basi
nakukaribisha tena sehemu
nyingine. Kwa maana nataka kuwe
na matiririko mzuri wa hoja ili
uweze kunielewa. Kabla
sijazungumzia jambo lingine
napenda turudi tena kusoma ule
mstari kuhakikisha kuwa
tunauelewa vyema.
1 Yohana 5:8
Kwa maana wako watatu
washuhudiao [mbinguni, Baba, na
Neno, na Roho Mtakatifu, na
watatu hawa ni umoja
Ni wazi kabisa kuwa Biblia ipo
kimya kuhusu Baba, mwana na
Roho kuwa nafsi tatu za Mungu.
Kwa vile ipo kimya Baba, mwana
na Roho hizi sio nafsi za Mungu
mmoja. Katika mstari huu hata
wewe unaona wazi kabisa
Hausemi kuwa Baba, mwana, na
Roho ni nafsi za Mungu. Kama
Mstari hausemi kwanini sisi
tuseme kuwa Baba mwana na
Roho ni nafsi tatu za Mungu? Na
tunaenda mbali zaidi na kusema
Baba ni nafsi ya Kwanza, Mwana
ni nafsi ya Pili, na Roho ni nafsi ya
tatu wakati haya yote hayapo
katika mstari huu? Nafikiri muda
umefika inabidi tuisome Biblia na
tusiongezee mambo ambayo
hayapo katika Biblia.
5
SOMO LA PILI
MUNGU NI NAFSI NGAPI?
Kwa vile nimesema kuwa Mungu
sio nafsi tatu, ni wazi kuwa swali
utakalotaka kuniuliza ni je Mungu
ananafsi ngapi? Kwa kuona hivyo
nimeona niwahi kutoa maelezo.
Mimi nataka kukupa mistari ya
Biblia kukuonesha kile ambacho
Biblia inasema kuhusu Mungu.
Naamini hata wewe unaamini
kuwa Mungu habadiliki. Kuwa
yeye sio kigeugeu kuwa
anabadilika. Kwa mantiki hiyo
najua utakuwa katika nafasi nzuri
ya kuelewa kile ninachotaka
kusema,
Kwanza nianze kwa kutoa mistari
hii.
Amosi 6:8
"Bwana MUNGU ameapa KWA
NAFSI YAKE asema BWANA
Mungu wa majeshi Naizira Fahari
ya yakobo, nachukizwa na
majumba yake kwasababu hiyo
nitautoa huo mji pamoja na wote
waliomo ndani yake"
Yeremia 51
14 BWANA wa majeshi ameapa
KWA NAFSI YAKE akisema
Hakika Nitakujaza watu kama
Nzige nao watapiga kelele juu
yako"
Isaya 42:1
"Tazama mtumishi wangu
nimtegemezaye mteule wangu,
ambaye NAFSI YANGU
imependezwa Naye nimetia roho
YANGU juu yake naye atawatolea
mataifa hukumu"
Isaya 42: 6
"MIMI BWANA nimekuita katika
haki nami nitakushika mkono na
kukulinda na kukutoa uwe agano
la watu na nuru ya mataifa
Isaya 45: 5
"MIMI NI BWANA wala Hapana
mwingine zaidi yangu MIMI
hapana Mungu, nitakufunga
mshipi ijapokuwa hukunijua
Hii ni mistari michache ambayo
najua inatosha kukuacha
ukitafakari. Mungu ni nafsi ngapi?
Jibu tunalolipata katika mistari hii
ya Biblia ni kwamba Mungu ni
nafsi moja tu. Ndio maana Mungu
anasema “Nafsi yangu” au
“Mimi”. Kwa maana Mungu
mwenyewe anayejifunua anasema
wazi kuwa yeye ni Nafsi moja.
Nafuta kokote katika Biblia kama
utaona sehemu ambayo Mungu
anasema yeye ni zaidi ya nafsi
moja kama jinsi alivyosema katika
mistari hii.
6
Katika vitabu vinavyojulikana
kama vitabu vya agano jipya pia
havipo mbali kusema kuwa Kuna
Mungu mmoja. Na kama kuna
Mungu mmoja ni wazi kuwa
Mungu ni nafsi moja.
Wakolosai 1:3
TWAMSHUKURU MUNGU,
BABA YAKE BWANA WETU
YESU KRISTO siku zote
tukiwaombea"
Waefeso 1: 3
"ATUKUZWE MUNGU, BABA
WA BWANA WETU YESU
KRISTO aliyetubariki kwa baraka
zote za rohoni katika ulimwengu
wa roho ndani yake Kristo"
2wakoritho 1:3
"NA AHIMIDIWE MUNGU,
BABA WA BWANA WETU YESU
KRISTO, Baba wa Rehema,
Mungu wa faraja yote"
Katika Mistari hii michache
tunaona kuwa Paulo anasema wazi
kuwa MUNGU NI BABA YAKE
YESU KRISTO. Hakuna hata
mmoja ambaye anashindwa
kuelewa kuwa Baba wa Yesu
Kristo ni Baba mmoja. Na kama ni
Baba mmoja basi ni Mungu
mmoja. Paulo anaendelea kusema
kuwa,
1 Wakorintho 8:6
"Lakini kwetu sisi MUNGU NI
MMOJA TU, ALIYE BABA
ambaye vitu vyote vimetoka kwake
nasi tunaishi kwake, yuko na
Bwana mmoja Yesu Kristo ambaye
kwake vitu vyote vimekuwapo na
sisi kwa yeye huyo"
Paulo anaendelea kutuambia wazi
kuwa Kuna Mungu mmoja
ambaye ndiye Baba wa Bwana
wetu Yesu Kristo. Kuna Baba
mmoja, na Huyu ndiye Mungu
ambaye kama jinsi tulivyoona
alikuwa anaapa kwa nafsi yake.
Isaya 42:1
"Tazama mtumishi wangu
nimtegemezaye mteule wangu,
ambaye NAFSI YANGU
imependezwa Naye nimetia roho
YANGU juu yake naye atawatolea
mataifa hukumu
Huyu ndiye Mungu mmoja
ambaye ndiye Baba wa Bwana
wetu Yesu Kristo. Mpaka Mungu
aseme kuwa “NAFSI YANGU” ni
wazi kuwa Mungu ni nafsi moja tu.
Na Paulo akasema mara nyingi
kuwa Baba yake Yesu Kristo ndiye
Mungu. Yesu ana Baba mmoja
hivyo kuna Mungu mmoja. Na
Yesu anatusaidia kuelewa wazi
kuwa Baba yake ndiye Mungu wa
kweli,
7
Yohana 17:3
"Na uzima wa Milele ndio huu
wakujue wewe MUNGU WA
PEKEE WA KWELI na Yesu
kristo uliyemtuma"
Yesu anaposema kuwa watu
wamjue Mungu wa kweli
haimaanishi kuwa yeye ni wa
uongo. Lakini anamaanisha wazi
Baba yake ndiye Mungu mkuu na
ambaye anatakiwa ajulikane
rasmi. Mwana siku zote anatafuta
kufanya mapenzi ya Baba. Hata
kiti cha enzi kile ambacho mwana
aliketi baada ya kushinda ni kiti
cha enzi cha Baba yake.
Ufunuo 3:21
Yeye ashindaye, nitampa kuketi
pamoja nami katika kiti changu
cha enzi, kama mimi nilivyoshinda
nikaketi pamoja na Baba yangu
katika kiti chake cha enzi.
Ni wazi kuwa Mwana
anamtegemea Baba. Na Baba
ndiye aliyempa mamlaka yote
mbinguni na duniani. Ni Baba
ndiye aliyeona vyema kumfanya
mwanae awe kama yeye.
Mpaka hapa tulipofikia naamini
umeweza kuona wazi kuwa
Mungu ni nafsi moja. Ni Mungu
ambaye akiapa huwa anaapa kwa
nafsi yake. Kama Mungu
angekuwa ni nafsi tatu basi ni wazi
kuwa isinge kuwa Mungu anaapa
kwa nafsi yake bali ingekuwa
anaapa kwa nafsi “zake”. Najua
kuna sehemu katika Mwanzo
Mungu alitumia neno “wetu”
lakini hayo yote utaelewa katika
somo lijalo lakini kwa sasa elewa
kuwa Kuna Baba mmoja basi kuna
Mungu mmoja.
Biblia imesema wazi kuwa Mungu
ni Mungu mwenye Nafsi moja. Na
Mungu huyo mmoja ana mwanae
ambaye Jina lake ni Yesu Kristo.
Yesu alisema wazi kuwa,
Yohana 14:28
Mlisikia ya kwamba mimi
naliwaambia, Naenda zangu, tena
naja kwenu. Kama mngalinipenda,
mngalifurahi kwa sababu naenda
kwa baba, KWA MAANA BABA NI
MKUU KULIKO MIMI
Na pia sehemu nyingine Yesu
anasema wazi kuwa Baba yake
ndiye Mungu mmoja, nani Mungu
wake pia
Yohana 20:17
"Yesu akamwambia usinishike kwa
maana sijapaa kwenda kwa Baba,
Lakini enenda kwa Ndugu zangu
ukawaambie Ninapaa Kwenda
kwa BABA YANGU NAYE NI
BABA YENU, KWA MUNGU
WANGU NAYE NI MUNGU
WENU"
8
Yesu Kristo anasema kuwa Baba
yake ndiye Mungu mmoja ambaye
sisi tunatakiwa kumwabudu.
Anasema wazi kuwa Baba yake ni
ndiye Mungu wetu. Na pia Baba
yake ni Mungu wake pia. Hakuna
lugha nyepesi ambayo tunaweza
kujifunza kuliko hii. Ya kwamba
kuna Mungu mmoja ambaye ndiye
Baba yake Mwana wa Mungu
Yesu Kristo. Hii ndio injili
ambayo Paulo alikuwa
anafundisha. Kwamba Mungu ni
Baba yake Yesu Kristo. Katika
mantiki hii tunaelewa kuwa
Mungu ni nafsi moja tu. Na huyo
ndiye Baba yake Yesu Kristo.
Labda nikuulize swali na wewe, je
kokote uliposoma katika maandiko
matakatifu, kuna sehemu yoyote
ulipoona Yesu anasema yeye ni
nafsi ya Pili ya Mungu?
Hakuna sehemu yoyote katika
Biblia ambayo Yesu alisema kuna
zaidi ya Mungu mmoja. Bali
alisema, wazi kuwa kuna Mungu
mmoja,
Marko 12
29 Yesu akamjibu, Ya kwanza
ndiyo hii, Sikia, Israeli, BWANA
MUNGU WETU NI BWANA
MMOJA.
Yesu hakuwahi kusema kuwa
kuna Mungu zaidi ya mmoja.
Kama jinsi alivyosema kuwa Baba
ni nafsi moja, basi Mungu ni nafsi
moja. Kwa maana tuna Baba
mmoja tu. Paulo alisema pia,
Wafilipi 4
6 MUNGU MMOJA, NAYE NI
BABA WA WOTE, aliye juu ya yote
na katika yote na ndani ya yote
Kuna Baba mmoja tu na huyo ni
Baba wa Yesu Kristo. Baba wa
Yesu Kristo ndiye kama
tulivyoona pia ni Mungu wa Yesu
Kristo kama jinsi tulivyo sisi.
Paulo anaendelea kusema kuwa,
1 Timotheo 2
5 KWA SABABU MUNGU NI
MMOJA, na mpatanishi kati ya
Mungu na wanadamu ni mmoja,
Mwanadamu Kristo Yesu.
Kuna Mungu na Baba mmoja. Na
tuna mpatanishi mmoja. Hakuna
Mungu zaidi ya mmoja, ndio na
huyo ndiye Baba mmoja.
Yakobo 2
19 WEWE WAAMINI YA KUWA
MUNGU NI MMOJA; watenda
vema. Mashetani nao waamini na
kutetemeka
Tukumbuke kuwa Bila kumjua
Mungu wa kweli hatuwezi kupata
uzima wa milele, kwa maana Yesu
alisema hilo wazi kabisa, na Yesu
alisema wazi kuwa Baba yake
ndiye Mungu wa Kweli. Na kwa
9
kusema hivyo alikuwa
anamuonesha Baba yake kama
ndiye Mungu rasmi ambaye sisi
tunapaswa kumwabudu.
Yohana 8
41 Ninyi mnazitenda kazi za baba
yenu. Ndipo walipomwambia, Sisi
hatukuzaliwa kwa zinaa; sisi
tunaye Baba mmoja, yaani,
Mungu. 42 Yesu akawaambia,
Kama Mungu angekuwa baba
yenu, mngenipenda mimi; kwa
maana nalitoka kwa Mungu, nami
nimekuja; wala sikuja kwa nafsi
yangu, bali yeye ndiye aliyenituma
Wayahudi walikuwa wanajua
kuwa kuna Baba mmoja ambaye
ndiye Mungu. Lakini walikuwa
hawataki kukubali kuwa Yesu
alikuwa ndiye Mwana wa Huyo
Baba mmoja ambaye walikuwa
wanasema wanamuamini.
Mistari hii mingi niliyotoa
nimejaribu kukuelewesha kuwa
kuna Baba mmoja hivyo Kuna
Mungu mmoja. Huyu ndiye
Mungu ambaye anaapa kwa nafsi
yake. Yeye ndiye Mungu wa
Kweli ambaye amempa mamlaka
yake Mwana wake Yesu Kristo
kwasababu anampenda sana
mwanae.
Yohana 3
35 Baba ampenda Mwana, naye
amempa vyote mkononi mwake.
Ukuu wa mwana unatokana na
Baba. Ni kweli kuwa Baba
amemnyanyua sana Mwana na
kwa Mwana kila goti litapigwa.
Lakini japokuwa na haya yote
Mwana anatuelekeza kwa Baba
kama huyo ndiye Mungu wetu
ambaye tunatakiwa kumwabudu
na kumuomba. Japokuwa na
uungu wake lakini Yesu hataki
tuelewe kuwa kuna Mungu zaidi
ya mmoja, bali anataka tuelewe
kuwa kuna Mungu mmoja na huyo
ni Baba yake.
Hata hapa duniani Mwana wa
mfalme anaweza kuwa na heshima
na mamlaka kama ya mfalme
lakini sikuzote atawaelekeza watu
kwa mfalme wa kweli ambaye ni
Baba yake.
10
lakini kwetu sisi Mungu ni mmoja tu,
aliye Baba, ambaye vitu vyote vimetoka
kwake, nasi tunaishi kwake; yuko na
Bwana mmoja Yesu Kristo, ambaye
kwake vitu vyote vimekuwapo, na sisi kwa
yeye huyo (1wakorintho 8:6)
11
SOMO LA TATU
UUNGU WA MWANA WA
MUNGU
Katika uumbaji
Kama jinsi tulivyo kwisha ona
katika somo lililopita kuwa Kuna
Mungu mmoja na huyo Mungu
anamwana wake ambaye ni
Mwana wa Mungu Yesu Kristo.
Tukumbuke kuwa Yesu alisema,
Yohana 17
5 Na sasa, Baba, unitukuze mimi
pamoja nawe, kwa utukufu ule
niliokuwa nao pamoja nawe kabla
ya ulimwengu kuwako
Kwamba mwana wa Mungu
alikuwepo hata kabla ya kuumbwa
kwa ulimwengu. Hakuna ambaye
atasoma huu mstari atashindwa
kuelewa kile ambacho mstari
unataka kusema, hata wewe
ukisoma najua kuwa hauwezi kosa
maana ile ambayo mstari
unazungumzia. Kwa mantiki hiyo,
tukisema kuwa Yesu Kristo
alianza kuwa mwana wa Mungu
alipobatizwa na yohana mbatizaji
kwasababu Mungu alisema
hadharani kuwa Yesu ni mwana
wake, tunashindwa kuelewa kuwa
kumbe wana wa Mungu alikuwepo
hata kabla ya ulimwengu kuwako.
Yesu anasema mara nyingi sana
kuwa yeye alikuwako hata kabla
Ibrahimu alikuwepo,
Yohana 8
58 Yesu akawaambia, Amin, amin,
nawaambia, Yeye Ibrahimu
asijakuwako, mimi niko
Wayahudi walitaka kumpiga
mawe kwa maana walijua kuwa
Yesu anajifanya ni Mungu hata
kusema kuwa yeye ni
“NIKO”ambaye wanajua kuwa
Mungu alipomtokea Musa alisema
yeye ni “NIKO.”
Kwa maana hiyo tunaendelea
kujifunza kuwa Yesu Kristo
mwana wa Mungu hakuanza kuwa
mwana wa Mungu alipobatizwa na
Yohana mbatizaji wala
alipozaliwa Bethlehemu kwa
maana alikuwa tayari mwana wa
Mungu hata kabla ya Ulimwengu
kuwako.
Waebrania 1
2 mwisho wa siku hizi amesema na
sisi katika Mwana, aliyemweka
kuwa mrithi wa yote, tena kwa
yeye aliufanya ulimwengu
Tunaona kuwa ni kwa kupitia
mwana Baba aliumba Ulimwengu
na Vyote ambavyo vipo. Yesu
anasema katika,
12
Mithali 8
22 Bwana alikuwa nami katika
mwanzo wa njia yake, Kabla ya
matendo yake ya kale. 23
Nalitukuka tokea milele, tangu
awali, Kabla haijawako dunia. 24
Wakati visipokuwako vilindi
nalizaliwa, Wakati zisipokuwako
chemchemi zilizojaa maji. 25
Kabla milima haijawekwa imara,
Kabla ya vilima nalizaliwa. 26
Alipokuwa hajaiumba dunia, wala
makonde Wala chanzo cha
mavumbi ya dunia; 27
Alipozithibitisha mbingu
nalikuwako; Alipopiga duara
katika uso wa bahari; 28
Alipofanya imara mawingu yaliyo
juu; Chemchemi za bahari
zilipopata nguvu; 29 Alipoipa
bahari mpaka wake, Kwamba maji
yake yasiasi amri yake;
Alipoiagiza misingi ya nchi; 30
Ndipo nilipokuwa pamoja naye,
kama stadi wa kazi; Nikawa
furaha yake kila siku; Nikifurahi
daima mbele zake;
Katika mistari hii kuna jambo
ambalo utagundua kuwa Mwana
wa Mungu alikuwa pamoja na
Baba kabla kitu chochote
hakijaumbwa. Yesu anasema wazi
kuwa alizaliwa kipindi ambacho
kabla ya uumbaji. Hatujui ni muda
gani huo lakini tunachojua ni
kwamba alizaliwa kabla ya
uumbaji. Kabla ya dunia na kabla
ya malaika hawajaumbwa, kabla
ya vilindi vya maji, mwana wa
Mungu alizaliwa.
Na kwavile amezaliwa na Mungu,
tunaelewa kile ambacho Paulo
alisema kuwa,
Waebrania 1:3
Yeye kwa kuwa ni mng'ao wa
utukufu wake na chapa ya nafsi
yake, akivichukua vyote kwa amri
ya uweza wake, akiisha kufanya
utakaso wa dhambi, aliketi mkono
wa kuume wa Ukuu huko juu;
Yeye ni m’ngao wa utukufu wake
na chapa ya “nafsi yake”. Katika
kauli hii tu inatosha kutuelewesha
kuwa kumbe Mungu ni nafsi moja.
Kwa maana Mwana wa Mungu ni
chapa ya “NAFSI” ya Mungu.
Hivyo Mungu hawezi kuwa ni
zaidi ya nafsi moja. Katika Mithali
tunagundua kuwa Baba na Mwana
ndio walioshirikiana kuumba
mbingu na dunia. Kwa maana
Yesu anasema wazi kuwa alikuwa
pamoja na Baba kama stadi wake
wa kazi.
Katika mantiki hiyo sasa turudi
katika kitabu cha mwanzo wakati
wa uumbaji,
Mwanzo 3:3
Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa
nuru
13
Tukisoma sura yote ya kitabu cha
mwanzo tunaona kuwa ni Mungu
ndiye aliyekuwa naongea.
Tukumbuke kuwa Biblia imesema
wazi kuwa mwana wa Mungu
alikuwepo wakati Mungu
anaumba mbingu na nchi. Sasa
Mungu anasema, , Iwe nuru, Je
Mungu alikuwa anamwambia
nani? Bila shaka alikuwa
anamwambia yule ambaye yupo
pembeni yake kama stadi wake wa
kazi yani Mwana wa Mungu Yesu
Kristo.
Mithali 8
29 Alipoipa bahari mpaka wake,
Kwamba maji yake yasiasi amri
yake; Alipoiagiza misingi ya nchi;
30 Ndipo nilipokuwa pamoja naye,
kama stadi wa kazi; Nikawa
furaha yake kila siku; Nikifurahi
daima mbele zake;
Wenda umeanza kuelewa kile
ambacho anataka kukisema.
Kwamba Mungu alikuwa
anaongea na mwana wake ambaye
huyo ni chapa ya “nafsi yake”.
Aliyekuwa anasema “iwe nuru”
alikuwa ni Baba. Na alikuwa
anamwambia stadi wake wa Kazi
Mwana wake. Sasa tuje katika
mstari wa 26 wa kitabu cha
mwanzo,
Mwanzo 1
26 Mungu akasema, Na tumfanye
mtu kwa mfano wetu, kwa sura
yetu; wakatawale samaki wa
baharini, na ndege wa angani, na
wanyama, na nchi yote pia, na kila
chenye kutambaa kitambaacho juu
ya nchi
Tunaona kuwa Mungu anasema
tumfanye Mtu “kwa mfano wetu.”
Wengi wanapofika katika mstari
huu wanadhani kuwa Nafsi tatu za
Mungu ndizo zinafanya mjadala .
Lakini kama jinsi tulivyoona
katika somo lililopita kuwa Kuna
Baba mmoja na huyo ndiye
Mungu. Kama umeelewa vyema
katika somo lililopita itakuwa ni
rahisi kuelewa mstari huu. Kwanza
kabisa Mstari unaonesha wazi
kuwa Baba hakuwa mwenyewe
wakati anaumba Mbingu na nchi
alikuwa na mtu pembeni yake.
Kwa vile Baba anamwambia mtu
huyo tumfanye mtu “kwa mfano
wetu” ni wazi kuwa aliyepembeni
yake alikuwa anafanana na Baba.
Ni mmoja tu ambaye alikuwa na
Baba tangia siku ya kwanza ya
uumbaji ambaye ndiye alikuwa ni
chapa ya nafsi yake. Huyu ni
Mwana wake Yesu Kristo. Hivyo
tunaelewa kuwa Baba alikuwa
namwambia mwana wake kuwa
“tumfanye mtu kwa mfano wetu”
14
Ni Baba ndiye aliyekuwa
anaongea na mwana kuhusu
kumfanya mtu kwa mfano wao.
“29 Alipoipa bahari mpaka wake,
Kwamba maji yake yasiasi amri yake;
Alipoiagiza misingi ya nchi; 30 Ndipo
nilipokuwa pamoja naye, kama stadi wa
kazi; Nikawa furaha yake kila siku;
Nikifurahi daima mbele zake”—Mithali
8:29-30
Je Yesu ni Melkizedeki?
Ili tujubu swali hili inabidi kusome
kitabu cha mwanzo tena,
Mwanzo 14: 17
7 Abramu aliporudi kutoka
kumpiga Kedorlaoma na wale
wafalme waliokuwa pamoja naye,
mfalme wa Sodoma akatoka
amlaki katika bonde la Shawe,
nalo ni Bonde la Mfalme. 18 Na
Melkizedeki mfalme wa Salemu
akaleta mkate na divai, naye
alikuwa kuhani wa Mungu Aliye
juu sana. 19 Akambariki,
akasema, Abramu na abarikiwe na
Mungu Aliye juu sana, Muumba
mbingu na nchi. 20 Ahimidiwe
Mungu Aliye juu sana, aliyewatia
adui zako mikononi mwako.
Abramu akampa fungu la kumi la
vitu vyote.
Melkizedek alikuwa ni mfalme wa
Salemu napia alikuwa ni Kuhani
wa Mungu. Kuna jambo ambalo
kila mmoja atagundua kuwa
Kipindi ambacho Abram na
Melkizedek wanakutana, tayari
Melkizedeki alikuwa ni Kuhani na
pia alikuwa tayari ni Mfalme.
Paulo pia anasema,
Waebrania 7:1-3
Kwa maana Melkizedeki huyo,
mfalme wa Salemu, kuhani wa
Mungu aliye juu, aliyekutana na
Ibrahimu alipokuwa akirudi katika
kuwapiga hao wafalme,
akambariki; 2 ambaye Ibrahimu
alimgawia sehemu ya kumi ya vitu
vyote; (tafsiri ya jina lake kwanza
ni mfalme wa haki, tena, mfalme
wa Salemu, maana yake, mfalme
wa amani; 3 hana baba, hana
mama, hana wazazi, hana mwanzo
wa siku zake, wala mwisho wa
uhai wake, bali amefananishwa na
Mwana wa Mungu); huyo adumu
kuhani milele.
Kitendo cha kwamba Melkizedek
anafananishwa na mwana wa
15
Mungu Yesu Kristo inatosha
kutuambia kuwa Melkizedeki
hakuwa mwana wa Mungu. Bali
alifananishwa na mwana wa
Mungu, kwasababu mwana wa
Mungu ni Mfalme na pia ni
kuhani.
Lakini pia tunaona kuwa Mwana
wa Mungu Yesu Kristo hakuwa
Kuhani kabla ya msalaba bali
baada ya kufa msalabani.
Tukisoma vitabu vyote vya Agano
la kale tunaona kuwa kulikuwa na
makuhani na hao ndio waliokuwa
wanafanya kazi ya kupatanisha
watu wa Mungu kwa Mungu. Yesu
hakuwa Kuhani kabla ya kuja
kwake hapa duniani, bali baada ya
kufa msalabani. Paulo anasema,
Waebrania 9
11 Lakini Kristo akiisha kuja, aliye
kuhani mkuu wa mambo mema
yatakayokuwapo, kwa hema iliyo
kubwa na kamilifu zaidi,
isiyofanyika kwa mikono, maana
yake, isiyo ya ulimwengu huu, 12
wala si kwa damu ya mbuzi na
ndama, bali kwa damu yake
mwenyewe aliingia mara moja tu
katika Patakatifu, akiisha kupata
ukombozi wa milele. 13 Kwa
maana, ikiwa damu ya mbuzi na
mafahali na majivu ya ndama ya
ng'ombe waliyonyunyiziwa wenye
uchafu hutakasa hata kuusafisha
mwili; 14 basi si zaidi damu yake
Kristo, ambaye kwamba kwa Roho
wa milele alijitoa nafsi yake kwa
Mungu kuwa sadaka isiyo na
mawaa, itawasafisha dhamiri zenu
na matendo mafu, mpate
kumwabudu Mungu aliye hai?
Tunaona kuwa ukuhani wa Yesu
sio ukuhani wa hapa duniani bali
ni ukuhani katika hekalu la juu
mbinguni. Kristo alipokuja na
akafa msalabani anatumia damu
yake iliyomwagika pale msalabani
na kuingia nayo katika hekalu la
mbinguni kutoa upatanisho
kwaajili ya dhambi za ulimwengu.
Lakini Melkizedek alikuwa ni
kuhani wa hapa duniani. Ni wazi
kuwa Melkizedeki hakuwa Yesu
Kristo mwana wa Mungu.
Ukuhani wa Kristo haitumii damu
ya wanyama, bali unatumia damu
yake iliyobora kuliko damu za
wanyama, wakati ukuhani wa hapa
duniani ulikuwa unatumia damu
ya wanyama ukisubiri ujio wa
damu ya Kristo. Kwa vile
Melkizedeki alikuwa ni kuhani
tayari. Hii inamaana kuwa ukuhani
wa Melkizedeki ulitegemea damu
za wanyama.
Pia tunaona kuwa Melkizedeki
alikuwa ni mfalme wa Salem.
Lakini Ufalme wa Kristo ulikuwa
bado haujaja hivyo rasmi Kristo
alikuwa bado sio mfalme mpaka
wakati ambapo ufalme utakuja,
16
Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa
mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale
samaki wa baharini, na ndege wa angani,
na wanyama, na nchi yote pia, na kila
chenye kutambaa kitambaacho juu ya
nchi (Mwanzo 1:26)
Mathayo 6:9
Basi ninyi salini hivi; Baba yetu
uliye mbinguni, Jina lako
litukuzwe, Ufalme wako uje,
Katika Sala ambayo Kristo
aliwafundisha wanafunzi wake
inaonesha wazi kuwa ufalme wa
Mungu ulikuwa bado haujaja ndio
maana Kristo alitufundisha
kuomba kuwa ufalme wake uje.
Lakini Melkizedeki alikuwa tayari
ni mfalme wa Salem alikuwa
tayari anaufalme. Wakati ufalme
wa Kristo ulikuwa bado haujaja.
Hata sasa bado ufalme wa Kristo
haujaja kwa maana ufalme wa
Kristo utakuwa hapa duniani na
ambao watakaokuwa katika
Ufalme huo ni wale ambao
wamefua mavazi yao na
wamemfata Bwana wao kwa
kuikana nafsi zao. Kitabu cha
Ufunuo kinatupa uelewa kuwa
makao makuu ya ufalme wa
Mungu itakuwa ni Yerusalem
mpya na makao hayo makuu
yatashushwa hapa duniani yaani
Mungu na mwana wa Mungu
watakuwa hapa duniani.
Ufunuo 21:10-14
Akanichukua katika Roho mpaka
mlima mkubwa, mrefu,
akanionyesha ule mji mtakatifu,
Yerusalemu, ukishuka kutoka
mbinguni kwa Mwenyezi Mungu;
11 wenye utukufu wa Mungu, na
mwangaza wake ulikuwa mfano
wa kito chenye thamani nyingi
kama kito cha yaspi, safi kama
bilauri; 12 ulikuwa na ukuta
mkubwa, mrefu, wenye milango
kumi na miwili, na katika ile
milango malaika kumi na wawili;
na majina yameandikwa ambayo
ni majina ya kabila kumi na mbili
za Waisraeli. 13 Upande wa
mashariki milango mitatu; na
upande wa kaskazini milango
mitatu; na upande wa kusini
milango mitatu; na upande wa
magharibi milango mitatu. 14 Na
ukuta wa mji ulikuwa na misingi
kumi na miwili, na katika ile
17
misingi majina kumi na mawili ya
wale mitume kumi na wawili wa
Mwana-Kondoo.
Wakati tayari Melkizedeki
alikuwa ni mfalme wa Salemu,
Kristo alikuwa anasubiri ufalme
utakaokuja katika wakati ujao kwa
maana wale watakao kuwa katika
ufalme huo ni wale ambao
wameamua kumuamini Yesu
Kristo. Ndio maana Paulo hasemi
kuwa Melkizedeki ni Yesu Kristo
bali anasema kuwa Ukuhani na
ufalme wa Yesu Kristo ni kama ule
wa Melkizedeki lakini
Melkizedeki na Yesu Kristo ni
wawili tofauti.
Je Yesu Kristo ndiye Baba?
Najua unaweza kuniuliza Mbona
Isaya 9:6 imesema kuwa Kristo ni
Baba wa milele inamaana kuwa
Baba sio mwingine ila Kristo. Kwa
kuanza naomba tusome tena kitabu
cha,
Isaya 9
6 Maana kwa ajili yetu mtoto
amezaliwa, Tumepewa mtoto
mwanamume; Na uweza wa
kifalme utakuwa begani mwake;
Naye ataitwa jina lake, Mshauri
wa ajabu, Mungu mwenye nguvu,
Baba wa milele, Mfalme wa amani
Katika Mstari kuna mambo
ambayo napenda uelewe. Kuwa
katika mstari huu kuna mambo
ambayo yalitimia wakati Yesu
alipokuja na kuna mambo ambayo
yatatimia katika mbingu mpya na
nchi mpya. Ngoja nianze
kukuonesha
“Maana kwa ajili yetu mtoto
amezaliwa, Tumepewa mtoto
mwanamume; Na uweza wa
kifalme utakuwa begani mwake”
Maneno haya yalitimia wakati
Yesu amekuja hapa duniani. Yesu
alipokuja hapa duniani alikuja
kama mwanakondoo wa Mungu
achukuaye dhambi za ulimwengu.
Japokuwa uweza wa kifalme
ulikuwa katika mabega yake lakini
alikuwa rasmi bado sio mfalme
bali alikuja kama mwanakondoo
wa Mungu,
Yohana 1
29 Siku ya pili yake amwona Yesu
anakuja kwake, akasema, Tazama,
Mwana-kondoo wa Mungu,
aichukuaye dhambi ya ulimwengu
Yohana alimwona kuwa Yesu
alikuwa ni mwanakondoo ambaye
amekuja kuchukua dhambi za
ulimwengu. Japokuwa uweza wa
kifalme ulikuwa katika mabega
yake lakini Yesu alikuwa bado
hajawa mfalme na alipokuja
alikuja sio kama mfalme bali kama
ni mtumwa. Kristo mwenyewe
anasema kuwa hakuja hapa
18
duniani kuwa mfalme wa
ulimwengu huu bali katika ufalme
ujao ambao hakutakuwa na
dhambi ndani yake. Yesu alisema,
Yohana 14
2 Nyumbani mwa Baba yangu mna
makao mengi; kama sivyo,
ningaliwaambia; maana naenda
kuwaandalia mahali. 3 Basi mimi
nikienda na kuwaandalia mahali,
nitakuja tena niwakaribishe
kwangu; ili nilipo mimi, nanyi
mwepo.
Hii inaonesha kuwa wakati yupo
hapa duniani bado makao ya watu
wake mbinguni yalikuwa bado
hayajaandaliwa. Na lengo kubwa
la Kristo kurudi kwa Baba ni ili
aandae ufalme ambao watu wake
watakuwa na makao ndani yake.
Hivyo tunaelewa kuwa wakati
Yesu amekuja hapa duniani
alikuwa na uweza wa kifalme
lakini bado hakuwa mfalme kwa
maana bado alikuwa hajaandaa
makao kwaajili ya watu wake.
“Naye ataitwa jina lake, Mshauri
wa ajabu, Mungu mwenye nguvu,
Baba wa milele, Mfalme wa
amani”
Yesu kuwa mshauri wa ajabu
ilitimia wakati yupo hapa duniani
na hata baada ya kurudi mbinguni.
Kwa maana hata sasa Yesu ndiye
mshauri wetu kwa maana
anatupenda na kila siku anataka
tuwe katika hali nzuri kimwili na
kiroho.
“Mungu mwenye nguvu” Kama
jinsi tulivyoona katika somo
lililopita kuwa Yesu alikuwepo
wakati Mungu anaumba dunia.
Yeye naye aliumba dunia na vitu
vyote kwa maana yeye ndiye
alikuwa stadi wa kazi wa Mungu.
Hebu tazama viumbe wa Mungu,
miti, milima, bahari, mawingu ya
angani hivi vyote utaona ubunifu
wake Yesu Kristo. Ni kweli kuwa
yeye ni “Mungu mwenye nguvu”
kwa maana sio tu aliumba vyote,
bali pia alizaliwa na Mungu
mwenye nguvu. Na kwa kutumia
kanuni hii ya Biblia,
Yohana 3
6 Kilichozaliwa kwa mwili ni
mwili; na kilichozaliwa kwa Roho
ni roho.
Na kwa vile Kristo mwenyewe
alisema alizaliwa kabla ya
uumbaji,
Mithali 8
25 Kabla milima haijawekwa
imara, Kabla ya vilima nalizaliwa.
kwa kutumia kanuni hii ambayo
Kristo mwenyewe alisema, ni wazi
kuwa Aliyezaliwa na Mungu ni
Mungu. Na kwa vile Mungu ni
Mungu mwenye nguvu basi ni
19
wazi kuwa aliyezaliwa na Mungu
mwenye nguvu ni Mungu mwenye
nguvu pia. Hivyo Kristo ni Mungu
kwasababu amezaliwa na Mungu.
Na amerithi uungu wa Baba yake
na hata jina lake,
Waebrania 1
4 amefanyika bora kupita malaika,
kwa kadiri jina alilolirithi lilivyo
tukufu kuliko lao.
Kama jina alilorithi ni kuu kuliko
lile la malaika ni wazi kuwa
hakuna jina lingine ila jina la
Mungu. Kama jinsi mtoto
anavyorithi jina la Baba yake,
Kristo amerithi jina la Baba yake
lililokuu kuliko jina la Malaika.
“Baba wa milele” Sasa tuje katika
kiini cha swali na nafikiri ulikuwa
unasubiria kwa hamu kufika katika
sehemu hii, nisingeweza kuanza
mara moja katika sehemu hii bila
kuelezea sehemu zingine kwa
maana ni vyema tukapata uelewa
wa jumla.
Yesu Kristo katika isaya anaitwa
“Baba wa milele” wengi
waliposoma mstari huu walikuja
na hitimisho kuwa Baba ambaye
Yesu alikuwa anamzungumzia
alikuwa ni yeye mwenyewe.
Tukisema kuwa Yesu ndiye Baba
ambaye mara nyingi Yesu alikuwa
anamsemea, hii italeta maana
kuwa Yesu alikuwa anaomba
kwenda kwake mwenyewe, hata
ile sauti iliyosema “Huyu ni
mwanangu mpendwa” ilikuwa ni
sauti ya kwake mwenyewe. Lakini
ukweli ni kwamba Yesu ana Baba
na Baba yake ndiye tunasema
ndiye Mungu wetu.
Yohana 8
19 Basi wakamwambia, Yuko wapi
Baba yako? Yesu akajibu, Mimi
hamnijui, wala Baba yangu
hammjui; kama mngalinijua mimi,
mngalimjua na Baba yangu.
Katika mstari huu tunaelewa kuwa
Yesu na Baba yake ni watu wawili
tofauti. Na hakuna ambaye
atashindwa kuelewa kuwa Baba na
Yesu ni wawili tofauti, kwa maana
kila mmoja ambaye anaamini kuna
Baba, mwana na Roho mtakatifu
lazima aamini kuwa Baba na
mwana ni wawili tofauti.
Sasa kwanini Kristo anaitwa
“Baba wa milele”? tukumbuke
kuwa Yesu alisema,
Yohana 17
24 Baba, hao ulionipa nataka
wawe pamoja nami po pote nilipo,
wapate na kuutazama utukufu
wangu ulionipa; kwa maana
ulinipenda kabla ya kuwekwa
msingi ulimwengu.
Pia Yohana akasema,
20
Yohana 1
12 Bali wote waliompokea
aliwapa uwezo wa kufanyika
watoto wa Mungu, ndio wale
waliaminio jina lake;
Paulo akasema,
Warumi 8
16 Roho mwenyewe hushuhudia
pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi
tu watoto wa Mungu;
Yohana pia akasema,
1 Yohana 5
2 Katika hili twajua kwamba
twawapenda watoto wa Mungu,
tumpendapo Mungu, na kuzishika
amri zake
Sasa tukumbuke kuwa Mungu
aliona vyema kumfanya mwanae
awe sawa na yeye,
Wafilipi 2
6 ambaye yeye mwanzo alikuwa
yuna namna ya Mungu, naye
hakuona kule kuwa sawa na
Mungu kuwa ni kitu cha
kushikamana nacho.
Sasa kwa vile Kristo aliomba
“Baba, hao ulionipa nataka wawe
pamoja nami po pote nilipo,
wapate na kuutazama utukufu
wangu ulionipa; kwa maana
ulinipenda kabla ya kuwekwa
msingi ulimwengu.”
Ni wazi kuwa Wale wote
waliokombolewa na Kristo, Yesu
anahaki ya kuwadai kama ni
watoto wake pia. Na kama kuna
mtoto basi ni lazima kuna Baba.
Kama waliokombolewa na Kristo
ni watoto wa Kristo, basi ni wazi
kuwa Yesu Kristo pia Baba yao.
Ndio maana anamuomba Baba
yake kuwa Watu aliowakomboa
wakae Pamoja nae. Lakini Ni
mpaka watoto wa Kristo
wajulikane ni nani na watoto wa
Shetani wajulikane ni nani ndipo
hapo ambapo Yesu atakaa pamoja
na watoto wake. Wakati tuliopo
bado Ngano na magugu
hayajatengwa. Ni ngumu kujua
nani ni mtoto wa Kristo na nani
siye. Kwa vile Ombi la Kristo ni
kukaa pamoja na watu wake, kama
vile Baba anavyokaa na watoto
wake, ni wazi kuwa ni kweli kuwa
watoto wa Mungu wapo hata sasa
na Yesu atakaa nao katika ufalme
wake,
Tukumbuke kuwa Yesu pia
alisema,
Yohana 17
6 Jina lako nimewadhihirishia
watu wale ulionipa katika
ulimwengu; walikuwa wako,
ukanipa mimi, na neno lako
wamelishika.
Akasema pia,
21
Yohana 16
15 Na yote aliyo nayo Baba ni
yangu; kwa hiyo nalisema ya
kwamba atatwaa katika yaliyo
yangu, na kuwapasheni habari
Kwa vile Yesu anasema kuwa
“walikuwa wako, ukanipa mimi,”
Ni wazi kuwa watoto wa Mungu ni
watoto wa Kristo. Kama jinsi
Mungu ni Baba wa Yesu Kristo,
Yesu Kristo ni Baba wa wote
aliowakomboa. Hivyo ni kweli
kuwa Kristo ni Baba wa milele wa
wote aliowakomboa kwa damu
yake.
“Lakini Kristo akiisha kuja, aliye kuhani
mkuu wa mambo mema yatakayokuwapo,
kwa hema iliyo kubwa na kamilifu zaidi,
isiyofanyika kwa mikono, maana yake,
isiyo ya ulimwengu huu, wala si kwa damu
ya mbuzi na ndama, bali kwa damu yake
mwenyewe aliingia mara moja tu katika
Patakatifu, akiisha kupata ukombozi wa
milele. (Waebrania 9:11-12)
Naye Neno ni Mungu
Kama jinsi tulivyoona hapo juu ya
kuwa Kristo alizaliwa na Mungu
hata kabla ulimwengu
haujaumbwa. Na kwa vile Kristo
amesema kuwa alizaliwa
inamaana kuwa kuna kipindi
ambacho hakuwepo ila Baba yake
alikuwepo. Mwana wa Mungu
alianza kuwa mwana pale
alipozaliwa na Mungu. Na Mungu
alianza kuwa Baba pale alipomzaa
mwana. Hatujui ni wakati gani
mwana alizaliwa na Baba lakini
tunachojua ni kwamba Alikuwa
mwana wa Mungu hata kabla ya
kuumbwa kwa chochote kile. Kwa
hiyo kwa vile alizaliwa na Mungu
ni lazima arithi uungu wa Baba
kwa maana ndio asili ya Baba
yake. Hivyo Yesu ni Mungu kwa
asili na mamlaka yale aliyorithi
kwa Baba yake.
Lakini unaweza kuuliza sasa
Mungu hasa ni nani? Katika
mantiki hii inabidi tutegemee
maneno ya Kristo na pia maneno
ya mitume kuwa Mungu mmoja
ambaye anafaa kutambuliwa kuwa
ni Mungu ni Baba yake Yesu
Kristo pekee. Lakini hii haizuii
mwana kuabudiwa kwa maana
kama tukimwabudu Mwana basi
tunamwabudu Baba. Kwa maana
Baba aliona vyema Mwana awe
kama yeye yani afanane naye.
22
Lakini japokuwa Mwana na yeye
anauungu na ni Mungu, lakini
hakuwahi kusema kuwa yeye ni
nafsi ya Pili ya Mungu mmoja, au
kuna zaidi ya Mungu mmoja wala
hajawahi kusema kuwa yeye ni
Mungu wa Pili. Mwana wa Mungu
anamnyanyua Baba yake kuwa ni
Mungu ambaye sisi tunatakiwa
kumwabudu, Mungu aliyempa
yote mwana. Na hicho ndicho
alichofundisha kuwa,
Yohana 20
17 Yesu akamwambia. Usinishike;
kwa maana sijapaa kwenda kwa
Baba. Lakini enenda kwa ndugu
zangu ukawaambie, Ninapaa
kwenda kwa Baba yangu naye ni
Baba yenu, kwa Mungu wangu
naye ni Mungu wenu
Hatuwezi kukosa kuelewa kuwa
Kristo anamnyoshea kidole Baba
yake kama ndiye Mungu ambaye
tunatakiwa kumwabudu. Kwahiyo
tunaweza kusema kuwa Kuna
Mungu mmoja ambaye ni Baba wa
Yesu Kristo.
“Mlisikia ya kwamba mimi naliwaambia,
Naenda zangu, tena naja kwenu. Kama
mngalinipenda, mngalifurahi kwa
sababu naenda kwa Baba, kwa maana
Baba ni mkuu kuliko mimi” (Yohana
14:28)
23
SOMO LA NNE
ROHO MTAKATIFU NI
NANI?
Sio lengo langu nikuchoshe kwa
kusoma sana mambo mengi. Na
nimeona niishie sehemu hii kama
ndio sehemu ya mwisho ya hiki
kijarida kidogo. Kama unataka
kusoma kwa kina zaidi kuhusu
Fundisho la utatu unaweza
kudownload kitabu kidogo
kinachoitwa “UKWELI KUHUSU
FUNDISHO LA UTATU” katika
website
Ukweliwasasa.wordpress.com.
Utabarikiwa zaidi wakati unasoma
hicho kitabu. Sasa tuangalie
kuhusu Roho mtakatifu. Ili kujibu
swali letu je Roho mtakatifu ni
nani? Inabidi tuanze na mstari huu
kwa maana ndio mstari pekee
katika Biblia ambao unaoeleza
wazi zaidi.
2Wakorintho 3
17 Basi Bwana ndiye Roho;
walakini alipo Roho wa Bwana,
hapo ndipo penye uhuru
Katika kujua Roho mtakatifu ni
nani kila mtu ni lazima aanzie
katika mstari huu. Mstari unaeleza
wazi kuwa Bwana Yesu Kristo
ndiye Roho mtakatifu. Na kama
ndiye Roho inamaana yeye si mtu
mwingine tofauti. Tukumbuke
Yesu aliwahi kuwaambia
wanafunzi wake kuwa.
Mathayo 28
20 na kuwafundisha kuyashika
yote niliyowaamuru ninyi; na
tazama, mimi nipo pamoja nanyi
siku zote, hata ukamilifu wa dahari
Alisema wazi kuwa yupo pamoja
nasi siku zote mpaka ukamilifu wa
dahari. Tukumbuke kuwa maneno
haya Yesu aliyasema kuwa ni yeye
mwenyewe ndiye atakaye kuwa na
watu wake mpaka ukamilifu wa
dahari. Tukisema kuwa Roho
mtakatifu ni tofauti na Yesu
inamaana tunasema kuwa kwasasa
Yesu hayupo na sisi. Lakini Biblia
inasema kitu tofauti kuwa ni Yesu
mwenyewe ndiye atakayekuwa
pamoja na watu wake mpaka
mwisho.
Najua unaweza kuwa na wakati
mgumu kuelewa kile ninachotaka
kumaanisha. Na wenda
unamaswali mengi uniulize,
mojawapo ni Kama Bwana Yesu
ndiye Roho Mtakatifu, kwanini
aseme kuwa atakuja msaidizi
mwingine?
Hili ni swali wengi wameuliza
lakini ni swali ambalo linajibika.
Ili tuweze kujibu hili swali ambalo
wenda unaweza ukawanalo
kichwani, inabidi tuangalie,
24
Yohana 14
16 Nami nitamwomba Baba, naye
atawapa Msaidizi mwingine, ili
akae nanyi hata milele; 17 ndiye
Roho wa kweli; ambaye
ulimwengu hauwezi kumpokea,
kwa kuwa haumwoni wala
haumtambui; bali ninyi
mnamtambua, maana anakaa
kwenu, naye atakuwa ndani yenu.
Tukumbuke ule mstari ambao
tulikwisha soma, wa Mathayo
28:20,
“na kuwafundisha kuyashika yote
niliyowaamuru ninyi; na tazama,
mimi nipo pamoja nanyi siku zote,
hata ukamilifu wa dahari”
Yesu anasema kuwa Huyo
msaidizi atakaa pamoja nao milele.
Kwa vile Yesu alisema kuwa ni
yeye mwenyewe ndiye atakaye
kaa na watu wake siku zote na
hakuna wakati ambao hatokaa na
watu wake inamaana kuwa huyo
msaidizi sio mwingine ile yeye
mwenyewe kwa maana ni yeye
ndiye aliyeahidi kuwa atakaa na
watu wake.
Pia Yesu aliwaambia wanafunzi
wake kuwa Huyo msaidizi
“watamtambua” lakini ulimwengu
hauwezi mtambua. Katika hali ya
kawaida hatuwezi mtambua mtu
tusiyemjua. Kwa kawaida kabisa
tunamtambua mtu tunayemjua au
tulishamuona tayari. Kitendo cha
kwamba Yesu anawaambia kuwa
Watamtambua Huyo msaidizi ni
wazi kuwa wanafunzi wake
walikuwa wanamjua huyo
msaidizi. Hata Daudi alikuwa
anamjua msaidizi. Alisema,
Zaburi 118
7 Bwana yuko upande wangu,
msaidizi wangu, Kwa hiyo
nitawaona wanaonichukia
wameshindwa.
Daudi alitambua kuwa Bwana
ndiye msaidizi wake siku zote.
Bwana sio msaidizi tu kwa Daudi
bali ni msaidizi wa wote ambao
wanaitwa kwa jina lake. Yesu
anaongezea na kusema kuwa huyo
msaidizi anakaa nao. Katika kauli
hii utagundua kuwa huyo msaidizi
sio mtu ambaye atakuja kukaa nao
kwa mara ya kwanza hapana bali
tayari huyo msaidizi anakaa nao.
Sidhani katika maelezo haya
utapata ugumu kuweza kuelewa
vyema. Yesu anasema kuwa huyo
msaidizi “anakaa kwenu” tunaona
kuwa sentensi iliyotumika hapa ni
ile ya wakati wa sasa “Anakaa
kwenu” wakati ile aliyosema kuwa
“atakuwa ndani yenu” ni ya wakati
ujao. Ni wazi kuwa Yesu Kristo
alikuwa anawaonesha kuwa yeye
ndiye msaidizi ambaye anakaa nao
lakini inabidi arudi kwa Baba ili
25
aweze kukaa ndani yao. Yesu
alisema,
Yohana 14
18 Sitawaacha ninyi yatima; naja
kwenu. 19 Bado kitambo kidogo
na ulimwengu haunioni tena; bali
ninyi mnaniona. Na kwa sababu
mimi ni hai, ninyi nanyi mtakuwa
hai.
Katika mstari huu aliyosema Yesu
kuna jambo ambalo hautapata
ugumu kulielewa. Yesu alisema
kuwa hatowaacha yatima.
Kwamba hatowaacha katika hali
ambayo hawana msaidizi. Hakuna
wakati ambao Bwana Yesu
hakuwa msaidizi wa wanadamu,
alikuwa msaidizi kwa Daudi
hawezi shindwa kuwa msaidizi wa
wanafunzi wake. Atakuwa nao
siku zote, na kwa kuongezea hapo
Yesu anasema kuwa Bado kitambo
kidogo na ulimwengu haumuoni
tena bali wao wanamuona. Hebu
tutumie sekunde kadhaa
kutafakari.
Anasema kuwa Hatowaacha
yatima bali anakuja kwao, Wakati
anakuja kwao ulimwengu
haumuoni bali wanafunzi wake
pekee ndiyo wanaomuona. Je
maneno haya Yesu alikuwa
anazungumzia ujio wake wa Pili
Mawinguni? Ukweli ni wazi kuwa
ni hapana, kwanini ni hapana? Ni
kwasababu Imeandikwa,
Ufunuo 1
7 Tazama, yuaja na mawingu; na
kila jicho litamwona, na hao
waliomchoma; na kabila zote za
dunia wataomboleza kwa ajili
yake. Naam. Amina.
Kila jicho litamuona wakati Yesu
Kristo anapokuja kwa mara ya pili.
Lakini kwanini atakapokuja
atajifunua kwa wanafunzi wake na
hatojifunua kwa ulimwengu?
Tukumbuke kuwa hili ndilo jambo
ambalo wanafunzi wake walielewa
na wakamuuliza kwanini anataka
kufanya hilo
Yohana 14
22 Yuda (siye Iskariote),
akamwambia, Bwana, imekuwaje
ya kwamba wataka kujidhihirisha
kwetu, wala si kwa ulimwengu?
Walielewa vyema kuwa Yesu
alikuwa na mpango
wakujidhihirisha kwao na wala sio
kwa ulimwengu. Hii inamaana
kuwa alipowaambia wanafunzi
wake kuwa,
Yohana 16
16 Bado kitambo kidogo nanyi
hamnioni; na tena bado kitambo
kidogo nanyi mtaniona.
26
Japokuwa mstari huu unaweza
kutupa maana kuonyesha ujio
wake kwa mara ya pili, lakini pia
unatuonesha baada ya kufufuka
kwake. Kwa maana ni kweli kuwa
baada ya kufufuka kwake
wanafunzi wake walimuona. Na
hata leo hii tunamuona Yesu katika
maisha yetu. Si kwa sura, bali kwa
mambo anayotufanyia. Hivyo
kwavile Yesu aliahidi kuwa
hatotuacha yatima yeye
mwenyewe atakuja kukaa na sisi
na sio tu katika kipindi
atakapokuja kwa mara ya pili, bali
hata sasa yupo nasisi inamaan
kuwa, Yesu Kristo anakaa na sisi
sio kwa kuonekana kwa mwili bali
anakaa na sisi katika Roho yeye
ndiye msaidizi wetu.
Lakini kwanini Yesu
alimzungumzia msaidizi kama ni
mtu mwingine tofauti na yeye?
Kwa mfano,
Yohana 16
14 Yeye atanitukuza mimi, kwa
kuwa atatwaa katika yaliyo yangu
na kuwapasha habari
Yesu alipokuwa anamzungumzia
msaidizi mwingine kama ni mtu
tofauti na yeye, ni kwasababu ya
utenda kazi. Tukumbuke kuwa
wakati Yesu alipokuwa katika
ubinadamu alikuwa katika mipaka
ya ubinadamu. Katika mwili wa
kibinadamu ilikuwa haiwezekani
yeye kuwa ndani ya watu wake. Na
kuwa kila sehemu kwa wakati
mmoja. Lakini katika Roho
anaweza kuwa ndani yetu na
kuishi ndani yetu na kuwa kila
sehemu kwa wakati mmoja. Katika
roho alikuwa na uwezo wa
kuwakumbusha yale aliyoyasema
na hata pale ambapo walikuwa
hawajaelewa alikuwa
anawaelewesha kikamilifu.
Tukisema kuwa Roho mtakatifu ni
mtu tofauti kabisa na Yesu Kristo
itakuwa ni tofauti kabisa na ile
ahadi ambayo Yesu mwenyewe
alisema kuwa atakuwa pamoja nao
hata ukamilifu wa dahari.
Tukumbuke alisema kuwa ni yeye
mwenyewe ndiye atakaye kuwa
pamoja nao sio mtu mwingine.
Kutokana na hili ndio maana Paulo
anasema wazi kuwa Bwana Yesu
ndiye Roho mtakatifu.
Tukumbuke Pia Yesu alisema
kuwa huyo Msaidizi mwingine ni
roho wa Kweli. Lakini hatupati
ugumu kuelewa kuwa Yesu Kristo
mwenyewe ndiye kweli, kwa
maana alisema,
Yohana 15
6 Yesu akamwambia, Mimi ndimi
njia, na kweli, na uzima; mtu haji
kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
27
Kwa vile huyo msaidizi ni roho wa
kweli, na kweli ni Yesu Kristo
mwenyewe, tunaelewa kuwa Yesu
Kristo ndiye Huyo msaidizi Roho
mtakatifu.
Mara nyingi tunaposikia neno
“Roho mtakatifu” huwa akili yetu
inaenda mbali sana. Kwa vile neno
hili limetolewa katika lugha ya
kiingereza yani “Holyspirit”
tunaelewa kuwa katika utafsiri,
neno halisi lingetakiwa liwe
“Roho takatifu” tutakapoweka
katika akili zetu uelewa kuwa
Kuna “Roho takatifu” ya Mungu
na ya Kristo, inatosha
kutuelewesha kuwa Roho takatifu
ya Yesu Kristo ni yeye mwenyewe
wala sio mtu mwingine. Kwa
maana hata wanadamu wanaitwa
“Roho”
Ezekieli 18
20 Roho itendayo dhambi, ndiyo
itakayokufa; mwana hatauchukua
uovu wa baba yake, wala baba
hatauchukua uovu wa mwanawe,
haki yake mwenye haki itakuwa
juu yake, na uovu wake mwenye
uovu utakuwa juu yake.
Kwa kusema “Roho itendayo
dhambi ndiyo itakayokufa”
Hakuna mtu ambaye atapata
ugumu kuelewa inamaanisha kuwa
“Mtu atendaye dhambi ndiye
atakayekufa” Kwa maana mtu ni
roho hata wewe unayesoma Roho
yako sio mtu mwingine tofauti na
wewe mwenyewe.
Hivyo pale ambapo Yesu
alimsemea Msaidizi mwingine
kama ni mtu tofauti, hakuwa na
maana kuwa yeye hatokaa pamoja
nao na kuwasaidia bali kwamba
utendaji kazi wake utakuwa tofauti
na utendaji kazi wake alipokuwa
katika mwili. Katika Roho
atafanya makubwa zaidi kuliko
alivyokuwa katika mwili. Hata
ukisoma kitabu cha Matendo
utaona kuwa baada ya msalaba
ukristo ulienea zaidi kuliko kabla
ya msalaba.
Ninachotaka uelewe ni kwamba
Biblia inaposema “Roho
mtakatifu” basi unatakiwa uelewe
kuwa ni uwepo wa Baba na mwana
wao wenyewe sio mwingine. Kwa
maana kama Mungu ni Roho na
Bwana Yesu ni Roho,
Yohana 4
24 Mungu ni Roho, nao
wamwabuduo yeye imewapasa
kumwabudu katika roho na kweli
Ina maana ni wazi kuwa kwa
ujumla tunapozungumzia Roho
mtakatifu sio mwingine ila uwepo
wa Baba na Mwana. Kama
tutasema kuwa Roho wa Mungu ni
tofauti na Mungu mwenyewe na
roho wa Kristo ni tofauti na Kristo
28
mwenyewe, Inamaana hata
ukisema kuwa Mungu ni nafsi tatu
bado hautakuwa sahihi kwa maana
itakuwa kuna
1. Mungu Baba
2. Mungu Roho Wa Baba
3. Mungu Mwana
4. Mungu Roho Wa Mwana
5. Mungu Roho Mtakatifu
6. Mungu Roho Wa Roho
Mtakatifu.
Nafikiri hata wewe unaona hakuna
utatu tena bali kuna usita na bila
shaka hautakubali. Paulo alisema
wazi kuwa kuna Roho wa Mungu
na kuna roho wa Kristo,
Warumi 8
9 Lakini ikiwa Roho wa Mungu
anakaa ndani yenu, ninyi
hamwufuati mwili; bali mwaifuata
roho. Lakini mtu awaye yote
asipokuwa na Roho wa Kristo,
huyo si wake.
Kama unaamini kuwa Roho wa
Mungu sio tofauti na Mungu
mwenyewe na Roho wa Kristo sio
tofauti na Kristo mwenyewe
kwanini inakuwa ngumu kuamini
ninaposema kuwa Roho mtakatifu
ndiye Yesu Kristo na ni Baba
mwenyewe? Kwa maana majina
“Roho wa Mungu” na “Roho wa
Kristo” na “Roho mtakatifu” ni
kitu kimoja na ni jambo hilo hilo.
Ni uwepo wa Baba na Mwana.
Kristo aliwahi kusema kuwa,
Ufunuo 3
20 Tazama, nasimama mlangoni,
nabisha; mtu akiisikia sauti yangu,
na kuufungua mlango, nitaingia
kwake, nami nitakula pamoja
naye, na yeye pamoja nami.
Naomba nikuulize swali, ni lini
ambapo Yesu Kristo alikuja kula
na wewe? Kwa vile Kristo hawezi
kusema uongo, ni wazi kuwa Pale
unaposali kwaajili ya chakula na
wakati unakula Kristo anakuwa
anakula na wewe japokuwa
haumuoni. Hata sasa Kristo
amekuwa anakula pamoja na
wewe muda wote na anatembea na
wewe kila siku na kile saa, najua
hili nililosema hauwezi kukataa,
hivyo ni kweli kuwa Yesu yupo
pamoja na wewe lakini sio katika
mwili kwamba utamuona bali
katika Roho. Kama ukisema kuwa
Roho na Kristo ni wawili tofauti
inamaana Yesu alisema uongo
kwa maana hakuna siku
uliyomuona amekuja kula na
wewe. Kwa maana aliposema
atakuja kukaa na kula pamoja na
wewe alisema ni yeye mwenyewe
sio mwingine.
29
“Na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku
zote, hata ukamilifu wa dahari”.
(Mathayo 28:20)
Ubatizo wa Yesu.
Nimeona pia nizungumzie Kuhusu
ubatizo wa Yesu Kristo kwa
maana kuwa wengi wanaotumia
tukio hilo la ubatizo wa Yesu kama
ni hoja ya kutofautisha Baba
Kristo na Roho mtakatifu.
Tusome,
Luka 3
22 Roho Mtakatifu akashuka juu
yake kwa mfano wa kiwiliwili,
kama hua; sauti ikatoka mbinguni,
Wewe ndiwe Mwanangu,
mpendwa wangu; nimependezwa
nawe.
Tuanze kuzungumzia ile sauti
iliyonena. “Wewe ndiwe
Mwanangu, mpendwa wangu;
nimependezwa nawe.” Ilikuwa ni
sauti ya Baba aliyembinguni. Na
alisema hadharani ili kila mmoja
aweze kumwamini Mwana kuwa
yeye ndiye aliyemtuma. Lakini
japokuwa Baba alinena wazi
wengi hawakumwamini.
Sasa Roho mtakatifu alishuka
kama Huwa, na watu walimwona
huyo Huwa akishuka, wengi leo
hii wamekuwa na uelewa kuwa
Roho mtakatifu ni njiwa. Na wengi
wamejaribu kumchora njiwa kama
ndiye Roho mtakatifu. Pia wengi
wanaposoma kisa cha kubatizwa
kwake Yesu wameishia kuwa na
mtazamo kuwa katika tukio hilo
Baba, mwana, na Roho wote
walikuwepo pale Mtoni. Lakini
tunasahau kuwa Yesu alisema,
Yohana 4
24 Mungu ni Roho, nao
wamwabuduo yeye imewapasa
kumwabudu katika roho na kweli.
Ukweli ni kwamba Ni Mungu
ndiye aliyeshuka kwa mfano wa
kiwiliwili kama hua na sio mtu
mwingine yoyote. Mungu ni roho,
na Roho ndiye aliyeshuka kama
njiwa, inamaana ni wazi kuwa ni
Mungu mwenyewe ndiye
aliyeshuka kama njiwa pale mtoni.
30
Mungu asingeweza kushuka na
utukufu wake pale mto Yordani
kwa maana hakuna ambaye
angeishi. Na aliposhuka
akamtangaza mwanae wazi wazi
akisema kuwa huyu ni Mwanangu
Mpendwa.
Hivyo ni Baba na Mwana pekee
ndio waliokuwepo katika tukio la
ubatizo.
Kuzaliwa kwake Yesu.
Hili nalo ni jambo Muhimu
ambalo ni lazima tulielewe. Watu
wote ambao wanaamini kuwa na
imani ya Kikristo wanaamini kuwa
Mariam alipata Mimba kwa uweza
wa Roho mtakatifu.
Luka 1
35 Malaika akajibu akamwambia,
Roho Mtakatifu atakujilia juu
yako, na nguvu zake Aliye juu
zitakufunika kama kivuli; kwa
sababu hiyo hicho
kitakachozaliwa kitaitwa
kitakatifu, Mwana wa Mungu.
Malaika Gabrieli alimwambia
Mariam kuwa atapata Mimba kwa
uweza wa Roho mtakatifu. Na yule
atakayezaliwa atakuwa ni mwana
wa Mungu. Kila mmoja anaamini
katika huu ukweli ya kwamba
Yesu Kristo hapa duniani alizaliwa
sio kama wengine wanavyozaliwa
yeye alizaliwa bila mwingiliano
wa Baba na Mama. Kipengele hiki
huwa mara nyingi
hatukizungumzii na mara nyingi
huwa tunakiruka lakini kina
umuhimu wake kwa maana
tukielewa hapa itakuwa ni rahisi
kuelewa yote niliyokuwa najaribu
kusema katika somo hili.
Sasa swali linakuja na ninapenda
kukuuliza wewe unayesoma, Nani
ndiye chanzo cha Mariam kuwa na
Mimba, je ni Mungu Baba au ni
Roho mtakatifu?
Kama ni Roho mtakatifu inamaana
kuwa Mungu hausiki kabisa na ile
Mimba ya Mariam, sasa kwa vile
Mariam alipata mimba kwa uweza
wa Roho mtakatifu, Baba wa Yesu
hapa duniani alikuwa ni nani?
Mungu Baba au ni Roho
mtakatifu?
Najua kuwa nimeuliza maswali
magumu, lakini lengo ni kukuleta
katika uhalisia wa mambo na
kuanza kutafakari vyema. Kama
unaamini kuwa Mungu Baba ni
tofauti na Roho mtakatifu, basi ni
Roho mtakatifu ndiye Baba wa
Yesu Kristo hapa duniani na sio
Mungu Baba.
Lakini najua mtu yoyote
akikuuliza Baba wa Yesu
alipozaliwa hapa duniani alikuwa
ni nani, hutosita kusema alikuwa
ni Mungu Baba sio Roho
31
mtakatifu. Kwa nini hatusemi
alikuwa ni Roho mtakatifu? Ni
kwasababu Mungu Baba ndiye
huyo Roho mtakatifu. Ndio maana
tunaona mara nyingi Yesu Kristo
anamtaja Mungu Baba kuwa ndiye
Baba yake wala sio Roho
mtakatifu.
Hivyo hivyo kokote unapoona
Roho mtakatifu ametajwa basi jua
ni uwepo wa Mungu mwenyewe
na wa Yesu Kristo mwenyewe.
Kanisa la Thiatira
Tunaendelea katika kuchunguza
Maandiko, sasa tungalie Kanisa la
thiatira katika kitabu cha ufunuo.
Na ninaomba usome maneo
ambayo nitayakoleza .
Ufunuo 2
18 Na kwa malaika wa kanisa
lililoko Thiatira andika; Haya
ndiyo anenayo Mwana wa
Mungu, yeye aliye na macho yake
kama mwali wa moto, na miguu
yake mfano wa shaba
iliyosuguliwa sana. 19 Nayajua
matendo yako na upendo na imani
na huduma na subira yako; tena
kwamba matendo yako ya mwisho
yamezidi yale ya kwanza. 20
Lakini nina neno juu yako, ya
kwamba wamridhia yule
mwanamke Yezebeli, yeye ajiitaye
nabii na kuwafundisha watumishi
wangu na kuwapoteza, ili wazini
na kula vitu vilivyotolewa sadaka
kwa sanamu. 21 Nami nimempa
muda ili atubu, wala hataki
kuutubia uzinzi wake. 22 Tazama,
nitamtupa juu ya kitanda, na hao
wazinio pamoja naye, wapate
dhiki kubwa wasipotubia matendo
yake; 23 nami nitawaua watoto
wake kwa mauti. Na makanisa yote
watajua ya kuwa mimi ndiye
achunguzaye viuno na mioyo.
Nami nitampa kila mmoja wenu
kwa kadiri ya matendo yake.24
Lakini nawaambia ninyi wengine
mlioko Thiatira, wo wote wasio na
mafundisho hayo, wasiozijua
fumbo za Shetani, kama vile
wasemavyo, Sitaweka juu yenu
mzigo mwingine. 25 Ila mlicho
nacho kishikeni sana, hata
nitakapokuja. 26 Na yeye
ashindaye, na kuyatunza matendo
yangu hata mwisho, nitampa
mamlaka juu ya mataifa, 27 naye
atawachunga kwa fimbo ya
chuma, kama vyombo vya
mfinyanzi vipondwavyo, kama
mimi nami nilivyopokea kwa Baba
yangu. 28 Nami nitampa ile nyota
ya asubuhi. 29 Yeye aliye na sikio,
na alisikie neno hili ambalo Roho
ayaambia makanisa.
Hatutaangalia maana ya huu
unabii, lakini tunaangalia yule
aliyenena huu unabii. Mstari wa
mwanzo kabisa inanesha
anayenena hayo maneno ni mwana
32
wa Mungu Yesu Kristo. Lakini
mstari wa Mwisho inaonesha
kuwa aliyekuwa anaongea hayo
maneno alikuwa ni Roho
mtakatifu. Ni wazi kabisa Mwana
wa Mungu ndiye roho mtakatifu na
tunarudi tena kwenye hitimisho
yetu kuwa Roho mtakatifu ni roho
ya Baba na Mwana na ni Baba
mwenyewe na Mwana
mwenyewe.
“Malaika akajibu akamwambia, Roho
Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu
zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli;
kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa
kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu”.
(Luka 1:35)
Nani aliyemtuma Yesu duniani?
Kristo alipoanza kazi yake ya
kuhubiri alianza kwa kusema,
Luka 4
18 Roho wa Bwana yu juu yangu,
Kwa maana amenitia mafuta
kuwahubiri maskini habari njema.
Amenituma kuwatangazia
wafungwa kufunguliwa kwao, Na
vipofu kupata kuona tena,
Kuwaacha huru waliosetwa,
Yesu alisema kuwa ni Roho wa
Bwana ndiye aliyemtuma Duniani.
Kama jinsi nilivyokwisha kusema
hapo mwanzo, kama unaamini
kuwa Roho wa Bwana ni tofauti
kabisa na Mungu mwenyewe ni
wazi kuwa Yesu hajatumwa na
Mungu Baba bali na Roho wa
Bwana.
Lakini kama unaamini kuwa Yesu
alitumwa na Mungu Baba kuja
hapa duniani basi ni lazima uamini
kuwa Mungu Baba ndiye Roho wa
Bwana. Yesu alisema,
Yohana 5
36 Lakini ushuhuda nilio nao mimi
ni mkubwa kuliko ule wa Yohana;
kwa kuwa zile kazi alizonipa Baba
ili nizimalize, kazi hizo zenyewe
ninazozitenda, zanishuhudia ya
kwamba Baba amenituma.
33
Inamaana kuwa Roho wa Bwana
ambaye Yesu alisema amemtuma
kuwatangazia wafungwa
kufunguliwa kwao sio mwingine
ila Mungu Baba. Kama jinsi
nilivyosema hapo mwanzo kuwa
tunapozungumzia Roho mtakatifu
ni uwepo wa Baba na Mwana.
HITIMISHO.
Pole sana kwa kusoma maelezo
marefu sana ambayo nimeandika.
Lakini ilikuwa ni muhimu niweze
kueleza hili jambo kwa urefu
kidogo ili uweze kuelewa kile
ambacho Biblia inasema. Ni
mpango wa Mungu siku zote tujue
ukweli na ukweli huo utuweke
huru. Kama jinsi tulivyoona Biblia
haijasema kuwa Mungu ni nafsi
tatu, na ushahidi wa kimaandiko
unaonesha wazi kuwa hakuna
nafsi tatu. Kama unaona
yaliyonenwa katika kijarida hiki
kidogo ni maneno ya kweli, basi
unaweza kuamini. Lakini kama
unaona yaliyonenwa humu sio
sahihi basi usiamini. Mungu na
akubariki.