Web viewKwa kufanya hivyo kutanuongezea mkulima kipato chake na pato la taifa kwa ujumla. ......
Transcript of Web viewKwa kufanya hivyo kutanuongezea mkulima kipato chake na pato la taifa kwa ujumla. ......
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI
CHUO CHA UALIMU MARANGU
DIPLOMA YA KAWAIDA YA ELIMU YA MSINGI
SOMO.STADI ZA RAMANI NA JIOMOFIKIMSIMBO:05202
KAZI YA KIKUNDIWASHIRIKI.
1. PAUL MEELA---------------------------------183072. SALEHE SEIPH-------------------------------183163. MARIJANI SHABANI-----------------------182824. YONA MABALA------------------------------183315. STEVEN MVUONI---------------------------183236. SIKUJUA SARIZA--------------------------7. YOHANA MARIUS--------------------------18330
Swali:Chunguza shughuli ya kilimo cha Kahawa katika eneo la Marangu ,kisha onesha :-
i. Chimbuko la shughuli husika.ii. Namna inavyofanyika.
iii. Umuhimu /mchango wake kwa wahusika.iv. Hali ya shughuli hiyo kwa sasav. Changamoto zake.
vi. Mapendekezo kwa ajili ya maboresho.vii. Mustakabathi wa shughuli husika.
Yaliyomo
1. Dibaji…………………………………………………………………………i
2. Shukrani……………………………………………………………………..ii
3. Chimbuko la shughuli ya kilimo cha kahawa……………………………...
4. Namna shughuli ya kahawa inavyofanyika……………………………….
5. Umuhimu wa shughuli wa kahawa kwa wahusika……………………….
6. Hali ya shughuli ya kahawa kwa sasa……………………………………..
7. Changamoto zake…………………………………………………………...
8. Mapendekezo kwa ajili ya maboresho……………………………………
9. Mustakabadhi wa shuhuli ya kahawa……………………………………
10. Rejea……………………………………………………………………….
Dibaji
Kahawa ni zao ambalo linawaingizia wananchi kipato kikubwa sana na taifa kwa ujumla zao la
pili ni tumbaku ambayi inalimwa zaidi kanda za kati kwa kuona umuhimu wa zao hili tumeona
tulifwatilie kwa kufanya utafiti na kuona maendeleo ya zao hili ambalo ni sehemu kubwa na
mchango mkubwa wa mwananchi yeyote na taifa kwa umjumla.
Zao hili hulimwa zaidi katika mikoa ya Arusha,Kilimanjaro,kagera ,Rukwa na Kigoma.
Kwa kuzingatia umuhimu wa zao hili tumeweza kutembelea maeneo zao hili linapolimwa
ambapo ni maeneo ya Marangu na maeneo ya Maua ipo katika eneo hili.
Zao hili linaonyesha kukumbwa na changamoto nyingi sana,licha ya kuwa an faida kubwa kwa
taifa na jamii ambayo wanalima zao hilo.
i
Shukrani
Napenda kuwashukuru wafuatao kwa mawaidha na misaada mbalimbali waliotupa katika
kuafanya swali hili.
Uongozi wa chuo cha Ualimu Marangu kwa kuturuhusu kutoka nje ya chuo na kwendakupata
taarifa toka kwa wakulima wanaojihusisha na zao hili.
Wakufufunzi wa somo la stadi za ramania na Jiomofiki kwa kutupa maelekezo mazuri ya swali
na ufafanuzi nini swali linahitaji.
Mtaalamu wa kilimo cha kahawa mama ………………kwa kutupa maelekezo mazuri kuhusu
shughuli hii.
Ofisi ya chama cha ushirika Ashira kwa kutupokea na kutupa maelekezo mazuri.
Tunawashukuru wanachuo wote kwa ushauri maelekezo na hoja katika kufanya kazi hii.
ii
1. Chimbuko la zao la kahawa
Baadhi ya vyama maarufu vya wakulima vilivyoanziswa enzi hizo ni Kilimanjaro Native
Planters Assosiation mwaka 1925 chama hiki kilikuwa na malengo yafuatayo:-
i. Kuboresha hali ya wakulima na kupanga bei nzuri ya zao la kahawa.
ii. Kupinga wakoloni kuweka bei ya zao kahawa.
iii. Kuunganisha wakulima wote wa kahawa ili wawe na sauti moja ili kutetea maslai yao.
Baadae wananchi wa kilimanjaro walibadili jina la chama cha Kilimanjaro Native Planters
Assosiation na kukiita Kilimanjaro Native Cooperative Union (KNCU) . Kipango R.(2011)
Kuna aina mbili za kahawa Robusta na Arabika. TET(1995)
Kahawa iliingia tanzania na kizinduliwa mwaka 1830 ililetwa na wamisionari wakatolilki huko
morogoro kwenye milima ya Uluguru.mwaka 1893 ililetwa kilema maeneo ya maua katika
maeneo ya Marangu wanalima kahawa aina ya Arabiaka.
Vilevile kahawa ilimwayo nchini Kenya ilitoka Kilema-Moshi.(TET 1981)
Arabika hulimwa pia mikoa ya Kilimanjaro,Meru,Oldendai,Pare.
2. Namna inavyofanyika
1. Kwanza kabisa ni kuandaa kitalu na kuweka mbolea ya samadi kuweka udongo na kuuchanganya na unapiga mstari wakusia . Katiaka mashimo hayo mkulima huweka mshimo mbolea ya samadi mshimo hayo huachwa wazi kwa muda wa mwezi au miezi miwili ili mbolea ioze na kupoa.Otmar(1964)
Umbali wa mstari mmoja na mwingine ni sentimeta 15 na mbegu na mbegu sentimeta 15. Mstari
unalala chini mgongo unaangalia juu na kufunika na udongo nusu nchi.
Unaweka matandazo ya majani makafu ya majani yasiyo na mbegu kisha unamwagilia kwa
kutumia kopo lenye matundu maana ukitumia ndoo itachimaba.
Umwagiliaji ni asubuhi na jioni maana mchano joto linaunguza, kuota kwa mbegu ni siku 60
hadi siku 90 ili iote upesi unailoweka kabla ya kusia kwa masaa 12 hadi 24 ili iote haraka.
Inatakiwa iote urefu wa sentimeta 15 hadi 30 kabla yakupelekwa shambani.
SHAMBANI
Unaandaa shamba unachimba mashimo miezi mitatu kabla ya kupanda mche urefu uwe
sentimeta 60 na upana sentimeta 60 shimo hadi shimo ni meta 3 kwa meta 3 .Unapochimba
mashimo baada ya miezi miwili unaweka mbolea na kufukia na kusimamisha miti katikati ya
shimo kama alama mwezi wa tatu unachukuwa sepeto unachimba katikati na unachukuwa mche
na mizizi yake unaupanda katikati na kisha unatandaza majani makafu na kuanza kumwagilia
na muda mzuri wakupanda miche hii inakuwa ni jioni ili mmea ukae katika hali ya kuto kupata
jua ili uweze kuanza kushika vizuri ardhini.
Mmea hukaamiaka mitatu
MAGONJWA
Kahawa ni zao kubwa la biashara linaloliingizia taifa fedha nyingi za kigeni. Ni la pili baada ya
Tumbaku. Lakini zao hili linakabiliwa na changamoto nyingi ambazo ni magonjwa na wadudu
achilia mbali Pembejeo, haya yote yanamuhusisha moja kwa moja mkulima..
1. CHULEBUNI (CBD).
Chulebuni ama kama ujulikanavyo kama Coffee Berry Disease (CBD), ni ugonjwa mbaya sana
na huenea kwa kasi. Mbuni ulioshambuliwa haufi ila mkulima anaweza kupoteza mpaka asilimia
90 ya mavuno kama hatazingatia namna bora ya kuuzuia. CBD huathiri matunda ya kahawa hasa
kanda za juu na kati. Ushambuliaji ni mkubwa zaidi wakati wa masika kwani CBD hupenda hali
ya unyevu na hali ya baridi.
Dalili na madhara ya CBD:
* CBD hushambulia mibuni katika hatua tatu muhimu ambazo ni:
. Maua yanapochanua.
. Punje zikiwa changa na laini.
. Punje zinazoiva.
* Madhara makubwa hutokea walati punje zikiwa changa na laini amnapo:
. Maua yaliyoshambuliwa hunyauka na kuanguka.
. Vidonda vyeusi na vilivyobonyea huonekana kwenye matunda yaliyoshambuliwa. Mengi huoza
na kudondoka. Yaliyobakia hukaukia kwenye mti na kuwa chanzo cha uambukizaji kwenye
mavuno ya msimu unaofuata.
* Matunda yaliyoiva hukaukia kwenye matawi na huvunwa kama buni.
* Hupunguza zao kwa asilimia kati ya 30 na asilimia 60 wakati mwingine hufikia hadi asilimia
90.
* Kudhibiti CBD hufikia hadi asilimia 35 ya gharama za uzalishaji.
* Hupunguza ubora wa kahawa kwa kiasi kikubwa.
Jinsi ya kuzuia chulebuni (CBD):
- Panda aina mpya ya kahawa inayohimili mahambulizi ya Chulebuni ambayo ni mkombozi
dhidi ya ugonjwa huu hatari.
- Punguza kivuli shambani.
-Kata matawi kwa wakati na sahihi. Ondoa maotea mara kwa mara.
- Ondoa masalia ya buni zilizoathirika na teketeza kwa moto.
- Kwangua magamba kwenye mashina machafu ya kahawa.
- Anza kunyunyizia vizuia kuvu kukinga matunda machanga ndani ya wiki tatu kabla ya mvua za
msimu kuanza.
- Hamasisha majirani kuzuia chulebuni kwa wakati mmoja.
3. KUTU YA MAJANI (LEAF RUST).
Mtenga, D.J. (2008) Tofauti katika uwezo wa kutoa ukinzani kwa chulebuni (Colletotrichum kahawae)na kutu ya majani (Hemileia vastatrix) katika aina za mkusanyiko wa kahawa zilizopo TaCRI Lyamungu.Utafi ti kwa ajili ya Shahada ya Uzamili, Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine, Morogoro,
Tanzania.
Kutu ya majani ni ugonjwa unaoathiri majani ya kahawa hasa kanda za chini na kati. Ugonjwa
huu unaathiri kahawa aina zote; Robusta na Arabika. Kutu ya mjani isipodhibitiwa inaweza
kupunguza mavuno kwa asilimia 60.
Dalili za ugonjwa:
Majani yaliyoshambuliwa hutokeza madoa madoa ya manjano chini ya jani
Madhara yake:
. Kutu ya majani hupunguza eneo la jani la kutengeneza chakula. Pia hudababisha kupukutika
kwa majani yanayolisha matunda na kukuza mmea.
. Kwa hali hiyo husababisha madhara ya mmea kutoa punje ndogo zenye ubora hafifu.
. Ugonjwa ukishamiri hukausha matawi, shina zima na hatimaye mti mzima kufa.
Hali zinazochangia kuenea kwa kutu ya majani:
- Unyevu wa hewani unapokuwa zaidi ya aslimia 80 na unapoambatana na kivuli cha kupita kiasi
kwenye shamba.
- Msongamano wa machipukizi na matawi katika mti wa kahawa.
Jinsi ya kudhibiti ugonjwa wa kutu ya majani:
- Punguza kivuli kuzunguka mti wa kahawa.
- Pogolea machipukizi na matawi katika mti wa kahawa.
Kuzuia kutu ya majani:
i) Panda aina mpya zinazovumilia magonjwa ya kutu ya majani na chulebuni.
ii) Boresha huduma muhimu ikiwa ni pamoja na lishe ili kuongeza uvumilivu wa magonjwa
hususani ugonjwa wa kutu ya majani.
iii) Tumia viua kuvu kwa wakati na vipimo sahihi. Unyunyiziaji wa kwanza ufanywe ndani ya
wiki tatu kabla ya mvua kunyesha, na kuendelea hadi mara tatu mpaka nne kwa msimu.
iv) Shirikisha na majirani kudhibiti kutu ya majani.
MAGONJWA MENGINE YA KAHAWA.
Yapo magonjwa mengine kadhaa ya kahawa ambayo umuhimu wake umemezwa na magonjwa
mawili niliyozungumzia hapo juu. Ningependa kuyataja tu baadhi yake pamoja na mbinu za
kuyazuia au kuyatibu.
3. BAKAJANI (Brown eye spot).
Ugonjwa huu huenezwa na kimelea aitwaye "Cercospora cofficola". Hudhibitiwa kwa utunzaji
bora wa shamba na kutumia morututu.
4. UGONJWA WA PUNJE ( Bean disease).
Huu huambukizwa na kuvu aitwaye "Nematospora coryli" akienezwa na kimatira. Ili kuepukana
na ugonjwa huu, ni lazima kuchukua hatua za kumdhibiti kimatira.
5. UGONJWA WA MASHINA (Scarly bark disease).
Ugonjwa huu hujulikana kama "Ukungu" kwa wakulima walio wengi, upo wa aina mbili ambao
wakulima huwa wanashindwa kutofautisha na huuita kwa ujumla wake Ukungu. Aina hii ya
kwanza ya ukungu huambukizwa na kuvu aitwaye "Fusarium lateritium". Hakuna udhibiti wa
kitaalam mpaka sasa ila kung'oa mti mzima na kupanda upya. Ukishang'oa choma mti hapohapo
na acha kwa muda angalau hata misimu miwili au mitatu kisha panda upya.
6. UGONJWA WA KUOZA MIZIZI (Root rot disease).
Huu ugonjwa unafanana kabisa na ugonjwa wa mashina, ni ukungu wa aina ya pili kama
unavyojulikana na wakulima wengi. Huambukizwa na kuvu aitwaye "Armillaria mellea".
Hakuna udhibiti ila kung'oa na kupanda upya baada ya muda wa misimu miwili au mitatu hivi.
Ndugu zangu wakulima, wataalam na wadau wote wa kilimo, hakikisheni mnajitahidi kwa kadri
inavyowezekana kudhibiti magonjwa hayo. Kwa kufanya hivyo kutanuongezea mkulima kipato
chake na pato la taifa kwa ujumla.
Ugonjwa wa majani
Ni ugonjwa wa fangasi mbaya sana ambao hushambuli majani,shina na matawi
Ili kilimo hiki kiwe na mafanikio kuna makundi ya watu au hatua za mkulima anazotakiwa kuwa
muangalifu ziko saba ili kuuza zao lake lenye ubora husika nazo ni:-
i. Wakulima-
Wassifanye kitu chochote bila kushauriwa na wataalamu kuanzia dawa ,kupanda miche na hatua
zote za kilimo cha zao la kahawa.
ii. Wasindikaji
Kusafisha sehemu ya kuhifadhia kahawa ,kuhakikisha kahawa kavu isichanganye na kahawa
mbichi pamoja na kukagua ubora wa maji.
iii. Wakoboaji
Hii ni kudumisha usafi katika maeneo ya kukobolea,vifaa vyote visafishwe kabla ya kuanza
kutumua na baada ya kumaliza kutumia magunia yanayopendekezwa ni ya katani na isichangane
gunia la kahawa kavu na kahawa mbichi.
iv. Watunzaji
Kuhifadhi kahawa katika eneo kavu na liwe limepuliziwa dawa ya kuulia vijidudu(fumigation)
pia usitumie dawa yoyote kuhifadhia bila kukubaliana na mnunuzi na usichanganye stoo ya dawa
na sehemu ya kuhifadhia kahawa.
v. Wasafirishaji
Kusafirisha kahawa safi,iwekwe kwenye magunia ambayo hayajatumika mapya kabisa
usisafirishe kahawa na dawa.
vi. Watafiti
Tuwe tunakagua mabaki ya dawa marakwamara na kuangalia kiwango cha uchanganyaji wa
dawa hizo wakati wakuzitumia pia kuwaelwesha wadau wote hapo juu ili soko la kahawa
liendelee kudumu nakuendelea vizuri.
vii. Seriakali na TCB.
Kuweka na kufwatilia kanuni zilizowekwa hapo juu na kutoa usahuri kwa serikali jinsi ya
kuzitekeleza..
Kahawa hustawi vizuri katika sehemu zenye mwinuko ulio kati meta 1400 na 2000 na kwenye
sehemu za udongo wenye rutuba unaopitisha maji kwa urahisi. Pia wastania wa mvua
inayohitajika kwa mwaka ni kati ya milimeta 900 hadi 1800.
Amri nane: taratibu bora za utunzaji wa kahawa:
• Kupalilia;
• Udhibiti wa magonjwa na wadudu wasumbufu;
• Kuweka matandazo;
• Urutubishaji wa udongo – kuweka mbolea;
• Kumwagilia pale maji yanapopatikana;
• Kupogolea machipukizi;
• Kupanda miti ya kivuli kwa mpangilio; na,
• Kupangilia matawi.
4. UMUHUMU WA HUGHULI HII
Katika shughuli hii kuna umuhimu mkubwa sana kama ifuatavyo:-
a. Kupeleka watoto shule kwa ajili ya ada na michango mingine ya shule.
b. Uhusaidia katika kupata fedha za kujenga nyumba .
c. Nidhamana ya kupewa mkopo kwa ajili ya kilimo hiki kama utatimiza vigezo ambapo
kikezo kikubwa cha kupata mkopo uwe unalima au unajihusisha na kilimo hiki na
umesajiliwa na chama cha ushirika (KNCU).
d. Shughuli hii hutoa ajira kwa watanzania kwa kuajiri Makarani,wenyeviti wna wahasibu
na bodinzima kwa ajili ya kufwatilia na kusimamia shughuli hii kupitia vyama vya
ushirika.
e. Kupata elimu sahihi juu ya kilimo cha zao hili wataalamu wa kilimo hutembelea
wakulima na kuwashauru namna ya kulima vizuri na kupata mazao bora.
5. Hali ya shughuli hii kwa sasa
Shughuli hii ya kilimo cha kahawa hali yake si nzuri maana wananchi wengi wameng’oa na
kupanda mahindi na migomba ya ndizi kwa sababu bei ya zao hili imeshuka sana licha ya
pembejeo zake kupanda bei sana na wananchi wengi wakaona hamna haja ya juendelea na
kilimo cha zao hili.
Na wengi wao walibaki kuwa wakulima wadogo wadogo.
6. Changamoto ya zake
Chimilila, C. I., H.M. Temu and F.B. Swai (2008). Mifumo ya ukulima na riziki, na
vikwazo
vya tija, ubora na faida ya kilimo cha kahawa kwa wakulima wadogo. Ripoti ya
kitaalamu
ya utafi ti uliofanyika kwa wakulima wa kahawa wa Kilimanjaro, Arusha na Mbinga.
Taasisi ya
utafi ti wa kahawa Tanzania, Moshi, Tanzania. Kurasa 79.
Kilimo cha zao hili kinakabiliwa na changanoto zifuatazo:-
i. Bei ya madawa ya kulia wadudu kuwa na bai kubwa kiasi cha wakulima wengi
kushindwa kununua.
ii. Ufanyajiwa kazi kubwa malipo nikidogo wakati wa kuuza .
iii. Miche hupatikana kwa shida na bei ya mche mmoja ni shilingi miatano 500.
iv. Wakulima wakitembelewa na wataalamu kukataa kuelimishwa na wataalamu na kufuata
jinsi wanavyofahamu na hawataki kubadilika na kilimo chakisasa maana kinatuma
gharama kubwa sana.mfano kupulizia dawa kila baada ya siku 21.
v. Siasa iliingilia kati na wakulima kugundua halina faida kwao linafaida kwa viongozi
wengi wakaamua kuachana na zao hili.
vi. Vijana wengi kutokupenda kulima zao hili na kukimbilia mjini kwa ajili ya biashara na
shughuli nyingine.
vii. Kutokuwa na uaminifu kwa viongozi swanaoongoza vyama vya kisimamia kililmo hiki
cha kahawa.
viii. Mabadiliko ya hali yahewa mvua hazinnyeshi tena kwa wingi kama miaka ya nyuma .
ix. Ukosefu wa dawa ya kutibu baadhi na magonjwa na kusababisha kung’oa mmea wote
licha ya kuchukua muda mrefu hadi kutoa mazao.
x. Kilimo cha zao la kahawa huchukuwa muda mrefu tangu kupanda hadi kupata mavuno ukilinganisha na mazao mengine kwa mfano kilimo cha migomba na kilimo cha mahindi.
7. Mapendekezo kwa ajili yamaboresho
Yafuatayo ni mapendekezo juu ya kilimo hiki cha kahawa kama ifuatavyo:-
i. Sherikali ipandishe bei ya zao hili ukilinganisha na soko la dunia.
ii. Pembejeo zipatikane kama mbolea na madawa ya kuulia wadudu.
iii. Miche ya kisasa ipatikane yakutosha na iuzwe kwa bei nzuri ambayo wakulima wengi
wataimudu.
iv. Serikali ifufue ofisi za ushirika ambao zimekufa kwa ngazi ya kijiji na kata kwa sasa
zi,mebaki kwa ngazi ya wilayani tu.
v. Elimu itolewe ilpasavyo kwa wakulima.
vi. Wataalamu waajiriwe wakutosha kwa maendeo zao hili linapolimwa ili kuwashauri
wakulima na kuwasaidia.
vii. Somo la kilimo cha kahawa liwekwe kwenye mtaala wa elimu kwa ngazi zote ili
kuwasaidia swanafunzi na vijana kujifunza kulima zao hili.
viii. Wanasiasa waachae kabisa kutumia zao hili kama njia ya kumba kura ili wachaguliwe
kushika nafasi mbalimbali bila matumaini yoyote wanapopata nafasi hiyo.
ix. Serikali iweke ruzuku kwenye bembejeo za zao hili kama motisha kwa wakuli,na na
kutambua mchango wao.
8. Mustakabali wa shughuli ya kilimo cha kahawa
Kilimo cha zao hili kimeendelea kudorora siku hadi siku na sasa kinaelekea kutoweka kabisa
kwa baadhi ya maeneo. .
Ukiangalia maofisi mengi yaliyokuwa yanashughulikia zao hili yamechakaa na kufungwa kabisa
na mengine yamekuwa magofu kabisa.
Kimsingi, Tanzania huzalisha aina mbili za kahawa: Arabika laini iliyooshwa (kiasi cha
55% ya jumla ya kahawa inayozalishwa), Robusta inayokaushwa kwa jua (kiasi cha
40% ya kahawa inayozalishwa), pamoja na kiasi kidogo cha Robusta ya asili
inayokaushwa kwa jua (chini ya 5% ya kahawa yote inayozalishwa). Zaidi ya 90% ya
kahawa inayozalishwa husafirishwa na kuuzwa kwenye soko la kimataifa. Kiasi cha
Kahawa inayosafirishwa nje imekuwa ni kati ya magunia 600,000 na 950,000 kwa
miongo miwili iliyopita. Wanunuzi wakubwa katika soko la dunia ni Japan (kiasi cha
30% ya thamani ya mauzo ya nje), ikifuatiliwa na Marekani (kiasi cha 15% ya thamani
ya mauzo ya nje), halafu Ujerumani, Italia na Ubelgiji (takriban 10% ya thamani ya
mauzo ya nje kwa kila nchi). Asilimia 25 iliyosalia inagawanywa miongoni mwa nchi
nyingi tofautitofauti kutoka Finland hadi Swaziland. Jumla ya thamani ya mauzo ya
nje ilifikia kiasi cha Dola za Marekani milioni 145 mwaka 2011 (ITC COMTRADE).
Wakati takwimu za uzalishaji zikionekana kutobadilika sana, mabadiliko makubwa
yametokea kwenye mkusanyiko na chanzo cha uzalishaji wa kahawa ya Tanzania.
‐ Kiasi cha uzalishaji wa kahawa ya Robusta kimeongezeka mara mbili katika kipindi
cha miaka thelathini iliyopita.
‐ Kwa upande waArabika laini, uzalishaji katika eneo la Kaskazini (Kilimanjaro, Arusha,
Manyara na Tanga), umeshuka sana, ambapo maeneo ya Kusini (Mbeya na Mbinga)
kumekuwepo na ongezeko kubwa. Kumekuwepo na mabadiliko machache ya
uzalishaji wa Arabika ngumu ya asili (maeneo ya Tarime).
Kuna mikakati mbalimbali iliyowekwa kama ifuatavyo:-
“Dhumuni kuu la mkakati huu ni:
“Kuongeza uzalishaji na ubora wa kahawa kitaifa ili kuboresha mapato katika mnyororowote wa thamani, hususan wakulima wa kahawa”. (TaCRI 2011)
Malengo ya kimsingi ni kama ifuatavyo:
• Ongezeko la uzalishaji wa kahawa safi kwa mwaka kutoka wastani wa sasa wa tani
50,000 hadi angalau tani 80,000 kufikia mwaka 2016 na tani 100,000 kufikia mwaka
2021.
• Kuongeza ubora wa kahawa utakaodhihirishwa na ongezeko la bei ya ziada kwenye
masoko ya nje kutoka 35% ya jumla ya uzalishaji ya sasa hadi angalau 70% kufikia
mwaka 2021.
• Hisa ya bei halisi (FOB) ya mkulima kwenye kahawa inayosafirishwa nje inaboreshwa
kufikia angalau 75% ifikapo mwaka 2021.
Rejea
-Programu ya uendeshaji Tija na Ubora (2011) Tasisi ya utafiti wa kahawa Tanzania
(TaCRI).
-Tasnia ya Kahawa Tanzania (2012)Mkakati wa maendeleo mwaka 2011 hadi 2021.
-Coffee Authority of Tanzania (1983)commision of the European communities.
-Tasisi ya ustawishaji wa Kahawa Tanzania(2008) Moshi-Lyamungu.
-Taasisi ya Elimu,(1981)Jiografia kwa wanafunzi wa shule za msingi,kitabu cha nne –Dar
es salam.
-Kipango R.(2011) historia kitabu cha mwanafunzi darasa la sita,Ben and Coimpany
Limited –dar es salamu .
-Otarm P.O.S.B(1964)Mkulima Stadi,ndaad mission press,peramiho,Tanzania.