Web viewAfya ni kule kuwa na hali ya uzima , kimwili,kiakili,na kijamii na sio tu kutokuwa na...

download Web viewAfya ni kule kuwa na hali ya uzima , kimwili,kiakili,na kijamii na sio tu kutokuwa na magonjwa au kudhoofika mwili au akili MANTEP(1995). Huduma

If you can't read please download the document

Transcript of Web viewAfya ni kule kuwa na hali ya uzima , kimwili,kiakili,na kijamii na sio tu kutokuwa na...

Afya ni kule kuwa na hali ya uzima , kimwili,kiakili,na kijamii na sio tu kutokuwa na magonjwa au kudhoofika mwili au akili MANTEP(1995).

Huduma za afya ni huduma zinazotolewa ili kukuwafanya watoto wawe huru kabisa kutokana na kutokuwepo kwa magonjwa au ulemavu Fulani kutokana na kutokuwepo kwa madhaifu na kuwa wazima kimwili ,kiakili na kijamii kutawasaidia kuzingatia masomo kikamilifu, baadhi ya huduma za afya ni hizi zifuatazo kumtibu mwanafunzi,kujua hali za kiafya za mwanafunzi ,kujilinda na magonjwa mbalimbali pamoja na kupata ushirikiano wa wazazi katika kulinda afya za wanafunzi.

Vipo vikwazo au changamoto mbalimbali zinazoweza kuzuia upatikanaji wa huduma ya afya shuleni kamavile , kukosekana kwa rasilimali fedha ,uhaba wa miundo mbinu,uhaba wa watataalamu, hali duni ya jamii(umaskini), Imani potofu ndani ya jamii,na uelew mdogo juu ya umuhimu wa huduma ya afya . Ipo mikakati ya stahiki ya itakayoeza kusaidia kuanzishwa kwa huduma ya afya shuleni kama imeelezewa kama ifuatavyo:-

Uhaba wa rasilimali fedha, ni ile hali ya kukosekana kwa fedha za kuendeshea shughuli mbalimbali pale shuleni. Ili kutatua tatizo hilo Uongozi wa shule kwa kushirikiana na kamati ya shule ,unaweza kuwashirikisha wadau mbalimbali wa elimu kamavile wazazi/walezi,waanasiasa,taasisi za kiserikali na binafsi ili kuweza kuchangisha pesa za kuendeshea huduma ya afya shuleni ikiwa ni pamoja na kununulia madawa na vifaa mbalimbali vya kutolea huduma ya afya shuleni. Uongozi wa shule kwa kushirikiana na kamati ya shule wanaweza kubuni na kuanzisha vyanzo mbadala vya mapato shuleni kama vile kilimo na ufugaji, mfano kilimo cha mboga mboga na ufugaji wa kuku WEU(2006).

Uhaba wa miundo mbinu,Hii ni jumla ya vitu vyote vilivyoundwa vinavyohusiana na huduma hiyo katika eneo Fulani kamavile majengo ,viwanja,barabara na chumba maalum cha kuwekea vifaa na kutolea huduma ,ili kuweza kuondokana na tatizo hili, Uongozi wa shule kwaa kushirikisha wahisani mbalimbali zikiwepo taasisi za fedha kama vile bank za CRDB,NBC,taasisi za mawasiliano kama vile Vodacom, Tigo, taasisi za kidini na makampuni mengine ya kibinafsi yaliyokaribu na eneo hilo ili kwa misaada yao au michango itakayopatikanaa kijengwe chumba maalumu cha kutolea huduma hiyo ikiwa ni pamoja na kununulia vifaa vinavyohusika na kutolea huduma shuleni hapo.

Uelewa duni wa jamii , hii ni hali ya mtu au jamii kutokujua jambo fulani au umuhimu wa jambo hilo katika maisha ,ili kuondokana na hali hii ndani ya jamii , uongozi wa shule,kamati ya shule,viongozi wa kisiasa na serikali walio katika eneo hilo kwa kushirikiana na watu mashuhuri, wenye ushawishi mkubwa katika jamii ili wawahamasishe na kuwapa elimu,ihusianayo na usafi wa mwili mazingira pamoja na umuhimu wa vyoo,ili kuweza kuondokana na magonjwa kama vile kuhara na kipindupindu,elimu hii iitatolewa kwenye vikao vya shule, mikutano ya kisiasa na kupitia taasisi za kidini WEU(2006).

Uhaba wa wataalamu . Hii ni ile hali ya kutokuwepo kwa watu wenye utaalamu juu ya utoaji wa huduma ya afya shuleni . Wizara ya afya na ustawi wa jamii (2007) katika mazingira ya shuleni wataalamu wanaotegemewa kutoa huduma ya afya ni manes na madaktari, kutoka katika zahanati, vituo vya afya na hospitali zilizokaribu na mazingira ya shule lakini katika vituo hivyo, wataalam ni wachache hawatoshelezi kutoa huduma hiyo shuleni na hospitalini. Mkakati wa kutatua ni serikalikupitia watalaamu walioo waliopo kutoa mafunzo na semina elekezi kwa walimu na wanafunzi ili waweze kupata uelewa juu ya huduma ya pamoja na kuitoa pale shuleni ,kuliko kuwa tegemea wataalamu watoke vituoni ili kuja kuhudumia shuleni.

Umaskini , ni ile hali ya ya kukosekana kwa uwezo wa mahitaji ya msingi katika jamii ,ili kuwea kupambana na hali kama hii kwa jamii ,ni kuelimishwa kwa jamii husika kutoka kwa wataalamu mbalimbali ili wajitambue na kuanzisha shughuli mbalimbali za maendeleo zitakazowasaidia kujikwamua kutokana na hali duni/umaskini walionao ndani ya jamii hiyo kuwapatia semina na warsha zenye mafunzo ya ujasiriamali kama vile biashara, ufugaji na kilimo kwanza .MANTEP (1995)

Imani potofu, ni ile hali ya kuwa na mtazamo hasi kuhusiana na jambo Fulani. Mkakati wa kuondokana na hali hii ni kuwashirikisha wadau kama asasi za kiraia ,mashirika ya kidini na serikali, kutoa elimu kwa jamii ili waweze kuondokanaa na imani hizi ambazo ni uchawi wa kuamini mizimu . WEU (2004) wanasema jamii nyingi za kitanzania zimeathiriwa na imani hizi ambazo zinarithishwa toka kizazi kimoja hadi kingine, hisia zinapokuwa na nguvu maelezo ya kisayansi hayapokelewi . Mfano mtoto anapougua magojwa kama degedege badala ya kupelekwa kwa daktari kwa watalaam wa afya wanawapeleka kwa waganga wa kienyeji.

Hivyo ii kuweza kuinua taaluma ya wanafunzi shuleni huduma za afya ni muhimu kwa sababu hupunguza uwezekano wa kupata maradhi ambayo yanaweza kuathiri maendeleo ya wanafunzi kwa ujumla . Ni dhahiri kwamba mwili wenye afya hujenga akili nzuri,hivyo ni vema kuweka hali ambayo itawasaidia wanafunzi kujenga taabia za usafi ili kujenga afya, hii inaweza kufanywa kwa kuweka mazingira safi,kupima afya mara kwa mara, kutoa lishe bora,kuuchukua hatua za kuzuia magonjwa na kutoa vifaa vya burudani.

REJEA

Mantep Institute (1995) Usimamizi wa Elimu, Kiongozi cha Mwalimu Mkuu, Mantep Institute Bagamoyo Tanzania.

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii (2007) Sera ya afya . Wizara ya afya na Ustawi wa Jamii Dar es Salaam.

Wizara ya Elimu na utamaduni (2004) Moduli ya somo la UKIMWI Mpango wa mafunzo ya walimu kazini ,Daraja la Tatu C/B-A. Wizara ya Elimu na Utamaduni, Dar es Salaam Tanzania.