UZINDUZI WA PEKE: TEMBO WA MWISHO ALIYEBAKI HAI KAMPENI DHIDHI YA UJANGILI

1
FOR IMMEDIATE RELEASE _______________________ TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI UZINDUZI WA PEKE: TEMBO WA MWISHO ALIYEBAKI HAI KAMPENI DHIDHI YA UJANGILI Je, itakuwaje kama tembo wote nchini Tanzania watakwisha na kubaki tembo mmoja tu? Utafanyaje? Utajisikiaje urithi wetu huu wa kustaajabisha ukipotea katika kizazi chetu? Alama Art and Media Production, ikisaidiwa na Nafasi ArtSpace, Ubalozi wa Wamarekani, World Wildlife Fund Tanzania, na kwa kushirikiana na PAMS Foundation na shirika la Africa Inside Out (AIO) lingependa kuwataarifu kuhusu uzinduzi wa sanaa ya ‘Peke; Tembo wa Mwisho Aliyebaki Hai’,yenye ukubwa unaokaribia tembo halisi iliyotengenezwa na msanii Paul Ndunguru kwa kutumia kioo nyuzi (fibgrelass) kwa dhumuni ya kukuza ufahamu na kuendeleza mjadala katika jamii kuhusu ujangili unaofanyika nchini Tanzania. Ingawa kumefanyika jitihada nyingi za kukabiliana na tatizo hili la ujangili, ni chache ambazo zimehusisha jamii. ‘Peke’ atatembezwa katika vitongoji mbalimbali vya Dar es Salaam na kisha kuzinduliwa rasmi katika viwanja vya Mnazi Mmoja. Uzinduzi utasindikizwa na tamasha la muziki na burudani kutoka kwa Wahapaha Band, Jhiko Man, T-Africa, Baba Watoto na burudani mbalimbali ikiwemo ucheshi, sarakasi, sanaa ya jamii, na mengi zaidi. Muhtasari wa Taarifa Jina la kampeni: Peke: Tembo wa Mwisho Aliyebaki Hai. Kampeni ya Dhidi ya Ujangili Imeandaliwa na: Alama Art and Media Production Msaada kutoka: Nafasi ArtSpace, U.S. Embassy, WWF, PAMS Foundation, AIO Wapi: Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam Tarehe: Jumamosi, 21 Machi 2015, kuanzia saa 9 mchana – saa 2 usiku Kuhusu Kampeni ya ‘Peke’ Dhumuni ya ‘Peke’ ni kutumia sanaa ili kupinga ujangili na kutetea uhifadhi wa urithi wa Tanzania. Tanzania ilijaaliwa kuwa na zaidi ya robo ya tembo wote duniani wa asili ya Kiafrika. Lakini, hivi sasa, Tanzania imepoteza karibia nusu ya tembo hao wote kutokana na ujangili. Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali, kati ya mwaka 2009 na 2013, Tanzania ilipoteza tembo wengi zaidi kuliko nchi yoyote nyingine kutokana na ujangili. Takwimu kutoka serikali zinakadiria kuwa tembo 30 huuliwa kila siku nchini Tanzania kwa ajili ya meno yao kuuzwa. Hii ina maana kuwa zaidi ya tembo 10,000 huuliwa kila mwaka kwa ajili ya meno yao. Kwa mwendo huu, kuna uwezekano mkubwa sana kwa kupotea kabisa kwa tembo nchini Tanzania ndani ya kizazi chetu. Jambo la kustaajabisha lakini ni kwamba thamani ya tembo mmoja aliyehai kutokana na pesa za utalii anazoziingiza ni zaidi ya mara 76 ya tembo aliyeuwawa na kuuzwa meno yake! Vilevile, watu wengi hawafahamu kuwa tembo hujua sana kujali. Ni kawaida kwa tembo kupatwa na wasiwasi juu ya familia yake, pia hutunza tembo wenzake waliojeruhiwa na huzunika sana wenzao wanapokufa. Tunawezaje kufikisha ujumbe huu kwa jamii na pia iweze kuelewa jinsi gani hasa tembo nchoni Tanzania walivyo katika hatari kubwa ya kupotea ? Tunawahamasishaje wanajamii kutaka kuchukua hatua za kuleta mabadiliko katika ulindaji wa rasilimali zetu za asili? Kampeni ya ‘Peke’ inalenga kufanya hivyo kwa kumpeleka tembo katika jamii. Kwani, ingawa Watanzania wameshawahi kumsikia tembo, ni wachache sana wamewahi kumuona kwa macho yao. Kwa taarifa zaidi, wasiliana na: Paul Ndunguru (0788 566 662)

description

UZINDUZI WA PEKE: TEMBO WA MWISHO ALIYEBAKI HAIKAMPENI DHIDHI YA UJANGILI

Transcript of UZINDUZI WA PEKE: TEMBO WA MWISHO ALIYEBAKI HAI KAMPENI DHIDHI YA UJANGILI

Page 1: UZINDUZI WA PEKE: TEMBO WA MWISHO ALIYEBAKI HAI KAMPENI DHIDHI YA UJANGILI

FOR IMMEDIATE RELEASE

_______________________ TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

UZINDUZI WA PEKE: TEMBO WA MWISHO ALIYEBAKI HAI KAMPENI DHIDHI YA UJANGILI

Je, itakuwaje kama tembo wote nchini Tanzania watakwisha na kubaki tembo mmoja tu? Utafanyaje? Utajisikiaje urithi wetu huu wa kustaajabisha ukipotea katika kizazi chetu?

Alama Art and Media Production, ikisaidiwa na Nafasi ArtSpace, Ubalozi wa Wamarekani, World Wildlife Fund Tanzania, na kwa kushirikiana na PAMS Foundation na shirika la Africa Inside Out (AIO) lingependa kuwataarifu kuhusu uzinduzi wa sanaa ya ‘Peke; Tembo wa Mwisho Aliyebaki Hai’,yenye ukubwa unaokaribia tembo halisi iliyotengenezwa na msanii Paul Ndunguru kwa kutumia kioo nyuzi (fibgrelass) kwa dhumuni ya kukuza ufahamu na kuendeleza mjadala katika jamii kuhusu ujangili unaofanyika nchini Tanzania.

Ingawa kumefanyika jitihada nyingi za kukabiliana na tatizo hili la ujangili, ni chache ambazo zimehusisha jamii. ‘Peke’ atatembezwa katika vitongoji mbalimbali vya Dar es Salaam na kisha kuzinduliwa rasmi katika viwanja vya Mnazi Mmoja. Uzinduzi utasindikizwa na tamasha la muziki na burudani kutoka kwa Wahapaha Band, Jhiko Man, T-Africa, Baba Watoto na burudani mbalimbali ikiwemo ucheshi, sarakasi, sanaa ya jamii, na mengi zaidi.

Muhtasari wa Taarifa Jina la kampeni: ‘Peke: Tembo wa Mwisho Aliyebaki Hai. Kampeni ya Dhidi ya Ujangili Imeandaliwa na: Alama Art and Media Production Msaada kutoka: Nafasi ArtSpace, U.S. Embassy, WWF, PAMS Foundation, AIO  Wapi: Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam Tarehe: Jumamosi, 21 Machi 2015, kuanzia saa 9 mchana – saa 2 usiku

Kuhusu Kampeni ya ‘Peke’ Dhumuni ya ‘Peke’ ni kutumia sanaa ili kupinga ujangili na kutetea uhifadhi wa urithi wa Tanzania.

Tanzania ilijaaliwa kuwa na zaidi ya robo ya tembo wote duniani wa asili ya Kiafrika. Lakini, hivi sasa, Tanzania imepoteza karibia nusu ya tembo hao wote kutokana na ujangili. Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali, kati ya mwaka 2009 na 2013, Tanzania ilipoteza tembo wengi zaidi kuliko nchi yoyote nyingine kutokana na ujangili. Takwimu kutoka serikali zinakadiria kuwa tembo 30 huuliwa kila siku nchini Tanzania kwa ajili ya meno yao kuuzwa. Hii ina maana kuwa zaidi ya tembo 10,000 huuliwa kila mwaka kwa ajili ya meno yao. Kwa mwendo huu, kuna uwezekano mkubwa sana kwa kupotea kabisa kwa tembo nchini Tanzania ndani ya kizazi chetu.

Jambo la kustaajabisha lakini ni kwamba thamani ya tembo mmoja aliyehai kutokana na pesa za utalii anazoziingiza ni zaidi ya mara 76 ya tembo aliyeuwawa na kuuzwa meno yake! Vilevile, watu wengi hawafahamu kuwa tembo hujua sana kujali. Ni kawaida kwa tembo kupatwa na wasiwasi juu ya familia yake, pia hutunza tembo wenzake waliojeruhiwa na huzunika sana wenzao wanapokufa.

Tunawezaje kufikisha ujumbe huu kwa jamii na pia iweze kuelewa jinsi gani hasa tembo nchoni Tanzania walivyo katika hatari kubwa ya kupotea ? Tunawahamasishaje wanajamii kutaka kuchukua hatua za kuleta mabadiliko katika ulindaji wa rasilimali zetu za asili? Kampeni ya ‘Peke’ inalenga kufanya hivyo kwa kumpeleka tembo katika jamii. Kwani, ingawa Watanzania wameshawahi kumsikia tembo, ni wachache sana wamewahi kumuona kwa macho yao. Kwa taarifa zaidi, wasiliana na: Paul Ndunguru (0788 566 662)