Tolea la pili - Tawi la Bagamoyo Aprili...

download Tolea la pili - Tawi la Bagamoyo Aprili 2013digitalbrush.co.ke/sites/crdb/newsletters/finish/4-newsletters/24... · kwa mtaji wetu wa fedha na kuonyesha tumedhamiria kuendelea kutoa

If you can't read please download the document

Transcript of Tolea la pili - Tawi la Bagamoyo Aprili...

TemboNEWs (KISWAHILI) Web

Angaza picha hii kwakutumia smartphoneilikuipata tovuti yetu

Tolea la pili - Tawi la Bagamoyo Aprili 2013

3. Kutoka kwa Mhariri

4.

7.

8.

Wasifu wa Mfanyakazi:

Ntike Nsekela

12.

18.

Taarifa ya Ndani:

Mji wa Kale Unaovutia Biashara ya Utalii

16.

Msaada kwa Jamii - Njombe

20.

Mwongozo wa Wateja:Furahia wepesi wa kununua bidhaa kwa njia ya mtandao

21.

Nguzo za Historia:Bagamoyo maeneo ya kihistoria

22.

Picha:Historia ya Bagamoyo

Mhariri:

Ms. Tull y Esther Mwambapa

Waandishi:Dk Charles Kimei

Saugata BandyopadhyayGodwin Semunyu

Ujumbe kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji

Wasifu wa Mteja:Shule ya Sekondari ya Premier - Bagamoyo

Jukumu la benki katika maendeleo ya kijamiiMaoni kutoka kwa Naibu Mkurugenzi Mtendaji

Katika Toleo hili...

3

i nafasi nyingine kwetu sisi kuweza kupata fursa ya kuwashirikisha katika mafanikio madogo na makubwa ya kibiashara kwa mwaka 2012. Mwaka 2013 unatupa nafasi ya kipekee kusherekea nafasi nyingine

tena ya mafanikio yetu kwa pamoja. Mafanikio haya ni kwa sababu yenu wateja wetu na daima tunashukuru kwa kuwa nasi.

Nina furaha kuleta kwenu toleo hili la TemboNews litakaloainisha mikakati mbalimbali ambayo tumeichukua kama Benki na pia tutaliangazia kwa ukaribu zaidi tawi letu la Bagamoyo.

Kwa ujumla, leo naendelea kuwajulisha kuwa ndoto ya Benki ya CRDB ni kutoa huduma bora kwa wateja na kuwasaidia kukua kiuchumi. Mwaka 2012, tuliendelea kujidhatiti kutoa huduma za kibenki nchini kote. Tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuendeleza biashara pamoja na kuongeza uwezo wa wateja, iwe ni mteja binafsi, wateja wa makampuni makubwa, wafanyabiashara wadogo wadogo na wafanyabiashara wa kati. Tunaendelea na dhamira ya kwenda sambamba na mabadiliko ya mahitaji ya wateja wetu ili kutoa huduma stahiki.

Katika toleo lililopita tulielezea ufunguzi rasmi wa tawi la Inyenyeri nchini Burundi. Utakubaliana nasi kuwa kuingia kwetu nchini Burundi ni alama tosha ya kukua kwa mtaji wetu wa fedha na kuonyesha tumedhamiria kuendelea kutoa huduma bora za kibenki kwenye ukanda huu wa Afrika Mashariki.

Mwaka huu tunaendelea kuwa na ushirikiano wa karibu zaidi na wateja, kwa kuwakaribisha kutupa uzoefu wao na jinsi ambavyo tunaweza kuwahudumia vizuri zaidi.

Katika toleo hili tunawaletea Bi. Aysha Shamte Mzee mmiliki wa Shule ya Sekondari ya Premier iliyopo Bagamoyo. Bi Aysha anatuelezea jinsi Benki ya CRDB ilivyosaidia kufanya ndoto yake ya kumiliki shule kuwa kweli.

Pia tuna habari, makala na picha mbalimbali za mji mkongwe wa Bagamoyo zitakazokupa mwanga mpya wa mji huo.

Karibu;

Tully Esther MwambapaMhariri

Kutoka kwaMhaririN

5

Ujumbe toka kwaMkurugenzi Mtendaji

Ndugu Mteja

Ninayo furaha kuweka bayana kuwa Benki ya CRDB imeendelea kupiga hatua nzuri katika ukuaji wa biashara na chapa yake kama taasisi kubwa ya fedha na yenye kuheshimika. Kwa miaka mingi mfululizo tumekuwa tukitekeleza

mikakati yetu ili kufikia ndoto zetu za kuwa benki bora katika ubunifu, benki inayomjali mteja katika kila inachofanya na benki yenye kutegemewa katika Afrika. Ninafuraha kutamka kwamba ndoto hii imeendelea kudhihirika katika utekelezaji na kwa msaada wenu tumeendelea kukaa katika mstari sahihi.

Mwaka huu, tumeweka kwa pamoja mpango mkakati wetu wa miaka mitano (2013 2017) ambao umelenga kuifanya benki kuwa chaguo la kwanza la wote. Tumeanza kutekeleza mikakati hii kwa kufanya marekebisho madogo lakini ya muhimu kwenye dira na adhma yetu ili kufikia matarajio ya wateja wetu.

Dira yetu sasa inasomeka kuwa benki bora ambayo inatimiza matakwa ya wateja na kutoa gawio bora kwa wanahisa wake. Kipekee hii inakuweka wewe mteja wetu

kwenye kitovu cha mipango yetu ya kibiashara na kutupa fursa ya kukuhudumia vizuri zaidi.

Adhma yetu sasa itakuwa kutoa huduma na bidhaa zenye ushindani na ubunifu; kwa kutumia teknolojia ili kufikisha huduma za kipekee kwa wateja wetu na kutengeneza thamani kwa wadau wote. Tunaamini kwa kufanikisha hili tutawahakikishia wateja wetu kupata huduma bora za benki na hatimaye kuwawezesha kufikia mafanikio bora.

Kiutawala, tumesonga hatua moja mbele kuhimiza misingi yetu ya kampuni itakayo kuhakikishia wewe kama mteja kufurahia mara zote unapohudumiwa nasi.

Wafanyakazi wetu wamebobea katika misingi yetu ya kampuni, Weledi, Kujituma, Ari, Ushirikiano, Ukarimu na Uhodari. Misingi hii itatawala utoaji wa huduma kwako na kukuwezesha ufurahie huduma bora katika njia bora zaidi.

Hivyo hivyo, tuko makini kuimarisha mtaji wetu kwa kuongeza rasilimali zetu maradufu kwa miaka mitano ijayo. Hii inawezekana kwa kuendelea kutuunga mkono na tunatumaini kwamba mipango yetu ya kuunganisha njia mbalimbali za ufikishaji huduma na kukufanya kufurahia huduma wakati tukiendelea kusogeza huduma jirani nawe. Uimarishaji wa njia za utoaji huduma unamaanisha kuwa utapatiwa huduma zetu kupitia njia tofauti za kielektroniki ikiwemo mashine za ATM, mashine za malipo (POS), Huduma za Benki kwa njia ya mtandao (Internet Banking), Huduma za benki kwa kutumia simu za mkononi (SimBanking), MPESA na huduma zingine za benki kupitia simu ya mkononi, huduma kupitia matawi ya kawaida, huduma za matawi yanayotembea, kituo cha huduma kwa wateja na huduma za uwakala.

Naamini kuwa kwa ushirikiano wenu na muhimu zaidi maoni yenu, kwa pamoja tutajenga taasisi itakayoendelea kuleta mabadiliko kwa vizazi vijavyo na kutengeneza fursa zaidi mbeleni. Nina imani kwamba tumechagua njia ambayo si tu inatutofautisha na washindani wetu na inafikia matarajio tofauti kwa makundi yote ya wateja wa ndani na wale wa kimataifa.

Vilevile, ningependa kutangaza tumezindua dawati maalum litakaloshughulika na mahitaji maalum ya biashara na nchi za Mashariki ya Mbali kama vile India na China. Tafadhali tumia muda wako kwa kujumuika nasi katika haya mafanikio na tutafurahi kupata maoni juu ya changamoto yoyote unayoweza kuwa nayo.

Asante.

Dr. Charles KimeiMkurugenzi Mtendaji

7

Maoni toka kwa Naibu Mkurugenzi mtendaji

kwa nini benkini muhimu kwamaendeleoya jamiiNa Saugata Bandyopadhyay

Jamii inapambana kwenye shughuli za uzalishaji katika maisha ya kila siku. Shughuli hizi zinazoiletea kipato jamii zinatengeneza sehemu muhimu ya mfumo wa kijamii na kifedha.

Asilimia ndogo sana ya wanajamii katika jumuiya hizi wanapenda kujihusisha na shughuli za benki na kujiwekea akiba kidogo katika benki hususan mahali ambapo huduma ya benki inapopatikana.

Shughuli za kiuchumi katika jamii nyingi ni chache na muda mwingine fursa za shughuli nyingi za kujipatia kipato zinaletwa na wawekezaji toka nje ya nchi ambao wanapenda kuajiri wafanyakazi toka nje kuliko wazawa wa ndani. Hii ni kwa sababu wazawa wengi wanaweza kuwa hawana elimu au mafunzo yanayohitajika kwa nafasi hizo. Jambo hili huwavunja moyo wana jamii kwa sababu mapato yote yatokanayo na uwekezaji huo, kama vile mahoteli ya ufukweni, makampuni ya kimataifa, n.k hayairudii jamii husika bali huwanufaisha wawekezaji na nchi zao.

Katika jamii benki inaweza kuonekana kama taasisi kwa ajili ya kuwahudumia wasomi, matajiri na watu wenye kipato katika jamii tu. Huu ni mtazamo potofu kabisa utokanao na ukosefu wa taarifa sahihi. Katika zama hizi za uchumi wa kisasa, mabenki yamekuwa yakibadilisha maisha ya jamii kupitia bidhaa na huduma zake zinazoboresha uchumi wa wananchi.

Chukulia mfano uchumi wa jamii ya watu wa mji wa Bagamoyo kisha weka pamoja na huduma za benki zilizopo, utakubaliana na mimi kuwa uwepo wa benki

umeanza kubadili maisha ya watu wa mji huu, kama inavyoshuhudiwa ukuaji wa uwezo wa biashara na ongezeko la shughuli za uzalishaji. Benki ni suluhisho tosha katika jamii ya aina hii kwa sababu ya rasilimali na uwezo wa kuwaelimisha juu ya faida na matokeo ya huduma zinavyoweza badilisha maisha yao.

Naamini benki ni kitega uchumi tosha katika jamii kama tukiweza shinda mioyo ya wateja wagumu kupitia mafunzo, kampeni na mazungumzo na mteja mmoja mmoja ili kuelimisha jamii majibu ya changamoto na fursa za kila siku za taasisi hizi za fedha.

Mabenki na taasisi zingine za fedha ni njia bora ya zakutoa elimu sahihi kwa jamii ikiwemo; kuanzisha biashara mpya na kuboresha biashara kupitia mikopo. Shule mpya zitajengwa na kuongeza idadi ya wenye elimu katika jamii, hii itaongeza kujiamini katika uwekezaji na shughuli mbalimbali zinazoiongezea kipato jamii. Jamii itakuwa na shughuli nyingi za uzalishaji za kila siku zinazoongeza kipato na uwezo wa kujiwekea akiba.

Inachukua muda na inahitaji kudhamiria ili kupata wateja makini na wanaohitaji kukopa ili kuwekeza katika biashara zao au kuanzisha biashara mpya. Hii ina maana kuwa, ni muhimu kwa taasisi za fedha kuwekeza katika jamii.

[Mwandishi ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB]

Nitike NsekelaJinsi benki ya CRDB ilivyotimiza ndoto ya

ya kuwa Afisa wa Benki

Ni mtu mwenye bashasha, mchangamfu na mpenda watu.Huonekana mkali kidogo, lakini ni mtu aliejipanga kupatamatokeo mazuri katika kazi yake.

Tembo News: Je ni lini ulianza kazi Benki?Nitike: Nilipata kazi yangu ya kwanza mwezi Machi tarehe 5, 1989. Baada ya kumaliza masomo, nilikaa nyumbani mwaka mmoja nikitafuta kazi kwa sababu nilipangiwa kazi ambayo sikuipenda ya ufugaji wa ngombe wa maziwa, ambayo ni tofauti na kazi niliyonayo sasa. Kwa wakati wetu kupata kazi ilikuwa rahisi sana. Kwa ujumla kipindi umalizapo shule tu unakuwa na kazi inakusubiri.

Tembo News: Ufugaji wa ngombe wa maziwa ni nini? Ulisoma kitu gani kwa wakati huo?Nitike: Nilisoma katika chuo cha kilimo na kupata diploma ya ufugaji wa ngombe wa maziwa. Nilifanikiwa kumaliza masomo ila sikuipenda sana ile kazi na niliamua kutafuta kazi nyingine na ndio nikafanikiwa kupata kazi ya benki. Nilipenda sana kazi za benki kwa sababu ndugu yangu alikuwa anafanya kazi benki na alifanikiwa kunishawishi kupenda na kutamani kufanya kazi za benki.

Tembo News: Kwa kifupi tueleze kuhusu maisha yako binafsi?Nitike: Nimekuwa na maisha ya utulivu na nadhani nastahili kumshukuru Mungu sana kwa hilo. Mafanikio haya yote yametokana na familia yangu japokuwa baba alifariki wakati nipo mdogo. Baba alifariki mwaka 1977 na nilikuwa bado mdogo sana.Tembo News: Uliwezaje kustahimili pigo hilo?Nitike: Ilikuwa ngumu katika kila kitu. Baba alikuwa mwalimu katika shule niliyosoma na kifo chake kilinipa wakati mgumu hasa baada ya kumzika. Nilishindwa kuzuia hisia zangu shuleni. Ulikuwa wakati mgumu sana mpaka ilibidi nihamie

shule nyingine. Baadae nilipona na nilijipa moyo kuwa maisha lazima yaendelee.

Tembo News: Tunapenda kufahamu nafasi ya kazi ya kwanza ulipoajiriwa?Nitike: Nilianza kama msimamizi wa mikopo pale Makao Makuu wakati huo Lumumba. Wakati huo ilikuwa inaitwa Benki ya Ushirika na Maendeleo Vijijini na kiasi kikubwa ilikuwa Benki ya uwekezaji. Majukumu hayo mapya yalinipa hamasa ya kazi ukizingatia historia ya masomo niliyosoma kwa vile muda mwingi nilikuwa nashughulika na wakulima ambao wangependa kupata mikopo ya benki. Niliweza kufahamu mahitaji yao haraka na kutathmini athari za mkopo kwa benki kwa kutumia ujuzi wangu wa kilimo kabla ya kutoa mkopo.

Tembo News: Je ni lini ulianza kazi Benki?Nitike: Nilipata kazi yangu ya kwanza mwezi Machi tarehe 5, 1989. Baada ya kumaliza masomo, nilikaa nyumbani mwaka mmoja nikitafuta kazi kwa sababu nilipangiwa kazi ambayo sikuipenda ya ufugaji wa ngombe wa maziwa, ambayo ni tofauti na kazi niliyonayo sasa. Kwa wakati wetu kupata kazi ilikuwa rahisi sana. Kwa ujumla kipindi umalizapo shule tu unakuwa na kazi inakusubiri.

Tembo News: Ufugaji wa ngombe wa maziwa ni nini?Ulisoma kitu gani kwa wakati huo?Nitike: Nilisoma katika chuo cha kilimo na kupata diploma ya ufugaji wa ngombe wa maziwa. Nilifanikiwa kumaliza masomo ila sikuipenda sana ile kazi na niliamua kutafuta kazi nyingine na ndio nikafanikiwa kupata kazi ya benki. Nilipenda sana kazi za

9

Bi. Ntike Nsekela na wafanyi kazi wa benki ya CRDB tawi la Bagamoyo. Kutoka kushoto - Martina Amos-BC,Denis Njau-B/0, Filbert Maro- MAD na Brighton Mwengama- Driver.

9

Nitike Nsekela, (48) ni Mtumishi wa Benki aliebobea. Akiwa na uzoefu wa zaidi ya miaka 20 katika masuala ya benki, Nitike anasema alitimiza ndoto yake ya kazi pale alipoanza kazi kwa iliyokuwa Benki ya Ushirika na Maendeleo ya vijijini na baadae ilipobadilishwa na kuwa Benki ya CRDB.Mwanzo alipata mafunzo kama Afisa kilimo katika Nyanja ya Ufugaji wa ngombe wa maziwa, ni wazi hiyo kada inatofautiana na kazi yake ya sasa. Lakini ingeweza kukisiwa kuwa mtu hufuata ndoto zake. Nitike kwa sasa ni Meneja wa Benki ya CRDB, tawi la Bagamoyo. Anasimulia hadithi yake ya mafanikio na changamoto alizopitia kupitia mahojiano na jarida la Tembo News na mtayarishaji wa makala hii Bw. Godwin Semunyu.

10

benki kwa sababu ndugu yangu alikuwa anafanya kazi benki na alifanikiwa kunishawishi kupenda na kutamani kufanya kazi za benki.

Tembo News: Kwa kifupi tueleze kuhusu maisha yako binafsi?Nitike: Nimekuwa na maisha ya utulivu na nadhani nastahili kumshukuru Mungu sana kwa hilo. Mafanikio haya yote yametokana na familia yangu japokuwa baba alifariki wakati nipo mdogo. Baba alifariki mwaka 1977 na nilikuwa bado mdogo sana.

Tembo News: Uliwezaje kustahimili pigo hilo?Nitike: Ilikuwa ngumu katika kila kitu. Baba alikuwa mwalimu katika shule niliyosoma na kifo chake kilinipa wakati mgumu hasa baada ya kumzika. Nilishindwa kuzuia hisia zangu shuleni. Ulikuwa wakati mgumu sana mpaka ilibidi nihamie shule nyingine. Baadae nilipona na nilijipa moyo kuwa maisha lazima yaendelee.

Tembo News: Tunapenda kufahamu nafasi ya kazi ya kwanza ulipoajiriwa?Nitike: Nilianza kama msimamizi wa mikopo pale Makao Makuu wakati huo Lumumba. Wakati huo ilikuwa inaitwa Benki ya Ushirika na Maendeleo Vijijini na kiasi kikubwa ilikuwa Benki ya uwekezaji. Majukumu hayo mapya yalinipa hamasa ya kazi ukizingatia historia ya masomo niliyosoma kwa vile muda mwingi nilikuwa nashughulika na wakulima ambao wangependa kupata mikopo ya benki. Niliweza kufahamu mahitaji yao haraka na kutathmini athari za mkopo kwa benki kwa kutumia ujuzi wangu wa kilimo kabla ya kutoa mkopo. Mwaka 1996 benki ilibinafsishwa na kuwa Benki ya CRDB, nililazimika kubadilisha nafasi na kuwa karani wa fedha. Nilifanya kazi kwenye matawi tofauti kama Lumumba, Arusha, Tower na baadae Geita nilipoenda kuanzisha tawi jipya na hapo ndipo nilipoanza rasmi kusimamia majukumu ya uongozi wa tawi mnamo mwaka 2008.

Tembo News: Tueleze uzoefu wa uongozi mpaka sasa?Nitike: Tofauti na watu wengine wanavyofikiria, kwangu uongozi nimeuona rahisi sana. Nadhani ni kwasababu ya kufanya kazi muda mrefu kama msimamizi na kubadilika kwa hiyo nafasi kwenda utawala ilikuwa ni kama kubadilisha majukumu tu. Kufanya kama msimamizi nilikuwa na wastani wa watu saba mpaka kumi wa kuwasimamia na hicho ndicho kilichonisaidia

katika uongozi. Nafasi ya usimamizi iliniandaa vizuri kuchukua nafasi ya uongozi.

Lakini sio kwamba kwangu ilikuwa rahisi sana. Kuna changamoto mbalimbali kama kupata matokeo mazuri ndani ya timu , ni kazi ngumu na inahitaji ujuzi na uvumilivu.

Tembo News: Ni changamoto gani unazopitia ukiwa kazini?Nitike: Sijakutana na changamoto nyingi labda kwasababu ninafanya kazi kulingana na mazingira. Hii inakupa uwezo wa kukua katika ujuzi na maarifa. Lakini, changamoto kubwa niliyopitia ni kuweza kuendana na mabadiliko ya benki wakati inabadilika kutoka benki ya uwekezaji na kuwa benki ya biashara. Nilitakiwa kuanza kuzoea nidhamu ya benki mpya ambayo ilihitaji mafunzo sana na ilinichukua mwaka kuanza kuelewa benki ya biashara. Baadae niliweza na ndo maana mpaka leo nipo hapa.

Tembo News: Tunaomba utueleze jinsi unavyotumia muda wako wa kazini/kwa siku nzima? Nitike: Naweza sema naanza siku kwa shauku na ari. Naanza siku kwa kufanya kikao na timu, tunajadili na kupitia maagizo toka makao makuu kwa ufupi na kuendelea kutoa huduma kwa wateja. Kama unavyojua benki ina kazi nyingi lakini kusikiliza na kutatua matatizo ya wateja ndiyo kazi yangu kubwa kwa siku nzima.

Tumetengeneza utamaduni hapa Benki ya CRDB wa wafanyakazi wote kujifunza desturi za benki na kuwamilikisha. Kila siku mfanyakazi mmoja ana jukumu la kutuelezea na kujipima jinsi tulivyoweza fikia au kutofikia malengo. Hii imetusaidia kukuza mahusiano na wateja na kutoa huduma bora zaidi.

Tembo News: Je umeshawahi kumfukuza mtu kazi?Nitike: Kwa kweli hapana hiyo sio utamaduni wa Benki ya CRDB, tunaajiri watu wanaofaa na tunakuza na kuendeleza vipaji vyao. Naamini hizo taratibu ndizo zinafanikisha kustawi kwa benki. Utaratibu wa kuajiri unasaidia kuchagua watu wanaofaa katika benki. Mfumo bora wa kuajiri ndio unaosaidia kuwa na watu wanaofaa. Tunaamini kuchagua watu wanoafaa, mafunzo na ushirikiano ndio chachu ya kupata matokeo mazuri.

Tembo News: Jinsi ulivyo na mafanikio katika kazi yako, ni ujumbe upi unawapa vijana wanaotaka kuwa maofisa wa benki?Nitike: Kufanya kazi benki kunahitaji kuwa mkweli kitabia. Kuwa mtu unayependa kujifunza na kila wakati kuwa mvumilivu ili uweze kukua. Pia kama kijana unatakiwa kujua hakuna kitu kinakuja kirahisi na kila unalofanya au utakachofanya siku moja utaona matunda yake. Usiwe mchaguzi na kila siku penda kufanya kazi zaidi ya kile ulichopangiwa.

[Mwandishi ni Meneja uhusiano katika Benki ya CRDB]

12

Benki ya CRDB ilvyoboresha ndoto yaBi Aysha Mzee kujenga shule ya sekondari ya Premier.

Ndoto kuwa kweli

DNa Tully Esther Mwambapa

k. Eleanor Roosevelt aliwahi kuzungumza kuwa mambo mema hutokea kwa wale wanaoamini katika ndoto zao .Aysha Mzee ni mwanamke mfanyabiashara mwenye uelewa, fasaha na shauku juu ya elimu. Kwa zaidi ya miaka kumi amefanya kazi kwa

bidii kuweza kutimiza ndoto ya maisha yake ya kumiliki na kuendesha shule binafsi ya sekondari inayo kidhi mahitaji ya elimu kwa watoto wa sekondari wa Bagamoyo na Tanzania nzima kwa ujumla.

Aysha aliweka akiba kutoka katika shughuli mbalimbali za biashara na alipofikisha shilingi milioni 50, alianza kuwekeza na kufanyia kazi ndoto yake. Haikuwa rahisi hata kidogo. Mradi ulihitaji mtaji mkubwa wa kuwekeza kwa kujenga madarasa , kuajiri walimu na kusaili wanafunzi. Niliweza kujibana na kila senti ya fedha niliyokuwa nayo niliwekeza katika hii shule na haikuwa kazi rahisi alisema

Kwa zaidi ya miaka mitano ya kuweka akiba, niliweza nunua heka thelathini za kiwanja na kuanza mradi wa ndoto yangu. Mwaka 2010, shule ya sekondari Premier ilifunguliwa ikiwa na madarasa machache na kusaili wanafunzi wa kike 28 wa kidato cha nne. Wanafunzi hawa walitolewa shule mbalimbali na walikuwa wanarudia mara nyingi sana.Naamini kila mtoto ana haki ya kupata elimu, wote wanaojiweza, wa kawaida na wasiojiweza kabisaAysha alielezea.

Akiwa na walimu tisa tu na aliendesha shule kwa falsafa yenye moto elimu kwa maendeleo zaidi- Aysha na timu yake walifanya kazi kwa bidii na kuweza kusaili wanafunzi na mnamo Januari 2011, shule ilipata wanafunzi wa kidato cha kwanza kutoka shule mbalimbali .

Akiwa na azma ya kuiwezesha shule kukua kwa hatua , Aysha na timu yake walianzisha darasa la kidato cha pili likiwa na idadi ya wanafunzi 22. Wanafunzi walipitia mitihani mbalimbali ya kujipima na wanafunzi 13 tu kati ya hao ndo waliweza kufaulu kwa kuwa na uwezo wa kufanya mitihani ya kidato cha pili . Kwa maana hiyo, pamoja na uchanga wa shule, ilifanikiwa kuwa na madarasa yaliyokamilika ya kidato cha kwanza, kidato cha pili na kidato cha nne.

Kidato cha pili kilifanikiwa kufanya vizuri sana kwenye mtihani wa taifa wa daraja hilo na kuitanga-za vyema shule na kuipandisha nafasi na kuwa moja kati ya shule zenye kufanya vizuri nchini Tanzania na kushika namba 23 kati ya shule 365.

kulipa mishahara mfululizo. Nina mkopo unaoniwezesha kushughulikia gharama za uendeshaji na hili limeniwezesha kuwa na uhakika wa kulipa mishahara ya walimu na imesaidia kuhamasisha walimu kufanya kazi kwa juhudi zaidi

Anasema msaada na mwongozo anaoupata toka benki ya CRDB vimemjengea uwezo wa kufikiri na kuboresha dira ya kuwa nguli wa elimuna kituo bora cha elimu Bagamoyo.

Aysha anasema, Benki ya CRDB inamwezesha kuendesha miradi yake kwa wakati na urahisi na imeboresha ndoto yake.

Anaongeza kusema kuwa ushirikiano anaoupata toka Benki ya CRDB katika miradi yake umeanza kubadilisha jamii inayozunguka shule yake. Kazi mpya zimeweza kutengenezwa kwa wanakijiji ambao walikuwa wanaishi kwenye umasikini na hali ngumu na sasa wanajishughulisha na biashara mbalimbali kuweza kujikimu maisha.

Aysha Mzee anatarajia kuifanya shule ya sekondari Premier kuchukua chaguo la watu na anatarajia shule kuwa na wanafunzi 880 na walimu 60. Mpaka sasa shule inauwezo wa kuwa na wanafunzi zaidi ya 350. Bado tuna kazi kubwa ya kufanya lakini kwa ushiriakiano wa Benki ya CRDB, naamini tutafanikiwa. Alisema

(Mwandishi ni Mkurugenzi katika Idara ya Masoko, Utafitina Huduma kwa wateja)

Haya yalikuwa matokeo mazuri sana kwetu na yalichochea na kutupa sifa, hasa kwa walimu na yalitupa moyo sana aliongeza Aysha.

Shule ilifanya vizuri katika masomo mbalimballi, Historia ilishika nafasi ya 2, Fizikia nafasi ya 3, Giografia ilishika nafsi ya 3, biashara nafasi ya 7, utunzaji mahesabu nafasi ya 20 na kingereza nafasi ya 23.

Lakini shule haikufanya vizuri katika somo la Kiswahili na tulishika nafasi ya 80 kati ya shule 365.Tunalifanyia kazi kubadilisha matokeo haya na tumeweka ratiba nzuri kuhakikisha tunapata matokeo mazuri.

Mpaka sasa shule ya Sekondari Premier tuna walimu 18 na jumla ya wanafunzi 168. Haya ni mafanikio makubwa sana ukizingatia tumeanza kutoa huduma kwa mwaka mmoja tu. Shule imepanga kusaili wanafunzi wa kidato cha tano mwezi wa 3 mwaka huu tumejipanga vizuri kufanikisha malengo haya. Nina uhakika tutapata matokeo mazuri mwaka huu Aysha aliongea kwa furaha.

Kwa ujumla Aysha anasema mafanikio hayo yamechangiwa sana baada ya kuanza kutumia fursa zinazotolewa na Benki ya CRDB. Benki ya CRDB tawi la Bagamoyo ni mshirika wao katika uwezeshaji wa mikopo uliowawezesha kumalizia miradi mbalimbali pamoja na

14

kulipa mishahara mfululizo. Nina mkopo unaoniwezesha kushughulikia gharama za uendeshaji na hili limeniwezesha kuwa na uhakika wa kulipa mishahara ya walimu na imesaidia kuhamasisha walimu kufanya kazi kwa juhudi zaidi

Anasema msaada na mwongozo anaoupata toka benki ya CRDB vimemjengea uwezo wa kufikiri na kuboresha dira ya kuwa nguli wa elimuna kituo bora cha elimu Bagamoyo.

Aysha anasema, Benki ya CRDB inamwezesha kuendesha miradi yake kwa wakati na urahisi na imeboresha ndoto yake.

Anaongeza kusema kuwa ushirikiano anaoupata toka Benki ya CRDB katika miradi yake umeanza kubadilisha jamii inayozunguka shule yake. Kazi mpya zimeweza kutengenezwa kwa wanakijiji ambao walikuwa wanaishi kwenye umasikini na hali ngumu na sasa wanajishughulisha na biashara mbalimbali kuweza kujikimu maisha.

Aysha Mzee anatarajia kuifanya shule ya sekondari Premier kuchukua chaguo la watu na anatarajia shule kuwa na wanafunzi 880 na walimu 60. Mpaka sasa shule inauwezo wa kuwa na wanafunzi zaidi ya 350. Bado tuna kazi kubwa ya kufanya lakini kwa ushiriakiano wa Benki ya CRDB, naamini tutafanikiwa. Alisema

(Mwandishi ni Mkurugenzi katika Idara ya Masoko, Utafitina Huduma kwa wateja)

Haya yalikuwa matokeo mazuri sana kwetu na yalichochea na kutupa sifa, hasa kwa walimu na yalitupa moyo sana aliongeza Aysha.

Shule ilifanya vizuri katika masomo mbalimballi, Historia ilishika nafasi ya 2, Fizikia nafasi ya 3, Giografia ilishika nafsi ya 3, biashara nafasi ya 7, utunzaji mahesabu nafasi ya 20 na kingereza nafasi ya 23.

Lakini shule haikufanya vizuri katika somo la Kiswahili na tulishika nafasi ya 80 kati ya shule 365.Tunalifanyia kazi kubadilisha matokeo haya na tumeweka ratiba nzuri kuhakikisha tunapata matokeo mazuri.

Mpaka sasa shule ya Sekondari Premier tuna walimu 18 na jumla ya wanafunzi 168. Haya ni mafanikio makubwa sana ukizingatia tumeanza kutoa huduma kwa mwaka mmoja tu. Shule imepanga kusaili wanafunzi wa kidato cha tano mwezi wa 3 mwaka huu tumejipanga vizuri kufanikisha malengo haya. Nina uhakika tutapata matokeo mazuri mwaka huu Aysha aliongea kwa furaha.

Kwa ujumla Aysha anasema mafanikio hayo yamechangiwa sana baada ya kuanza kutumia fursa zinazotolewa na Benki ya CRDB. Benki ya CRDB tawi la Bagamoyo ni mshirika wao katika uwezeshaji wa mikopo uliowawezesha kumalizia miradi mbalimbali pamoja na

16

Msaada Kwa Jamii - Njombe

2. Mkuu wa Wilaya ya Njombe Mh. SarahDumba akikabidhi zawadi zilizotolewa naBenki ya CRDB tawi la Njombe kwaMkuu wa kituo cha Tumaini IlundaSister Coletha

3. Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakiwakwenye picha ya pamoja na Mkuu waWilaya ya Njombe Mh. Sarah Ndumba,Mkuu wa Kituo cha Tumani Ilunda SisterColetha na baadhi ya watoto wa kituo

1.Wafanyakazi wa Benki ya CRDB-Njombewakishusha bidhaa na vyakula vilivyotolewa kwa kituo cha Tumaini Ilunda

Benki ya CRDB kupitia tawi lake la Njombe ilitoa msaada wa vifaa na chakula kwenye kituo cha

watoto yatima cha Tumaini Ilunda kilichopo Njombe. Vitu mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya

milioni moja vilitolewa ikiwamo unga, mchele, maharagwe, sukari, mafuta na sabuni. Mgeni rasmi

katika tukio hilo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Njombe Mh. Sarah Dumba.

17

Msaada Kwa Jamii - Njombe

4. Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Njombe Mh. SaraDumba na Mkuu wa Kituo cha Tumaini Ilunda Sister Coletha

6. Afisa Masoko wa Benki ya CRDBBw. Emmanuel Kiondo akiagana nawatoto wa kituo cha Tumaini Ilunda

5. Watoto wa kituo cha Tumaini Ilundawakionyesha michezo mbalimbalikwa wageni waalikwa

18

Mji wa Kale Unaovutia Biashara ya Utalii

Mvuto wa Dini

Bwaga Moyo

Na Godwin Semunyu

Mji wa Bagamoyo kwa asili ni mji wa pwani na wenye kuvutia sana. Bagamoyo ina uoto bora wa asili na inavutia sana kwabiashara, hususani utalii. Bagamoyo ni mji wenye historia ya kidini na makao makuu ya zamani ya wajerumani hapa Afrika mashariki. Huu ni mji ulioanzishwa mwishoni mwa karne ya 18, una historia ya kipekee na kuathiriwa sana na tamaduni za wafanyabiashara wa kihindi na waarabu, serikali ya Ujerumani na wamisionari wa kikristo. Bagamoyo imepambwa na maeneo ya kuvutia, hivyo kuleta kumbukumbu ya kipekee ya uingiaji wa dini hapa Afrika Mashariki.

Majengo ya kale ni viashiria dhahiri vya miaka ya mwanzo ya wakati wa ukoloni. Hapa hakuna kipingamizi na neno Bwaga Moyo kama wenyeji wanavyoita na ni tafsiri ya waswahili wa pwani. Neno hili Bwagamoyo liliashiria kukata tamaa kwa watumwa walipokuwa wakifika mahala hapa maana ndio ilikuwa mwisho wa safari ya walipotoka na mwanzo wa safari ya kuelekea bara la Ulaya na Amerika. Watumwa wali bwaga mioyo kwa kukata tamaa.

Mji wa Bagamoyo uko takribani kilometa 75 Kaskazini mwa Jiji la Dar es Salaam katika pwani ya bahari ya Hindi.

Upo karibu na na kisiwa cha historia cha Zanzibar na ukaribu huu unaongeza kuvuma kwa pepo nzuri za bahari.

Wingi wa Watu Mji wa Bagamoyo umeshamiri biashara na idadi ya watu ni wastani. Watu wake wamejikita katika shughuli mbalimbali kama kilimo, uvuvi na biashara ndogondogo. Kwa mujibu wa wenyeji biashara inazidi kushamiri kutokana na kuendelea kuja kwa wageni wengi hivyo kuongeza muamko wa mji huu.

Mitaani watu wanajishughulisha sana na shughuli zao za kila siku, wenyeji wa Bagamoyo ni wakarimu na wenye upendo. Mitaani sauti za pikipiki maarufu kama Boda Boda husikika na kupiga kelele lakini zinarudisha matumaini ya kuwaingizia vipato wakazi wa mji huu, hususani vijana. Tunaweza kukubaliana kwamba uwepo wa biashara nyingi umetoa ishara kwamba mji umechangamka na kukua na hii inatosha kuonyesha kuwa kuna haja ya kuwa na huduma maalumu za kibenki, ambazo Benki ya CRDB inatoa kwa kiwango bora ili kuchochea kasi hii ya maendeleo.

Nilifanya ziara fupi na kutembelea sehemu mbalimbali za kihistoria za mji huu. Wakazi wengi wa Bagamoyo ni waumini wa dini ya kiislamu, na pia Kanisa la kale kabisa Afrika Mashariki linapatikana katikati mji huu.

Nilianza safari yangu kwa kutembelea makumbusho ya kanisa la Holy Ghost linalopatikana katika jengo kongwe. Jengo hili ni la karne ya 18 na lilijengwa na msanifu majengo kutoka bara la Ulaya mwaka 1876 na walitumia mawe ya matumbwe yaliyotoka kwenye bahari Hindi. Jengo hili ni muhimu sana katika historia ya waumini wa kikatoliki na wakazi wa Bagamoyo kwa ujumla. Jengo hili ni makumbusho yenye vivutio mbalimbali toka enzi za biashara ya utumwa na kuhifadhi viumbe vya baharini. Matembezi katika makumbusho haya yanakupa ufahamu jinsi maisha yalivyokuwa katika karne ya 18 na kukupa hamasa ya kupenda kujua Historia.

19

Miaka 145 ya Mbuyu

Mnara wa historia

Kwa mbali kidogo umesimama mti wa mbuyu. Ni mti mkubwa uliokaa katika eneo hilo kwa karibu karne moja na nusu na una historia inayofurahisha.

Mbuyu huu ulipandwa mwaka 1868 na Padri Anthony Horner (CSSP) ambae inaaminika alichukua mbegu ya mbuyu kutoka katika kisiwa cha Reunion (kisiwa cha Ufaransa katika bahari ya Hindi). Padre Horner ni mwanzilishi wa Parokia ya Roho Mtakatifu ya Bagamoyo.

Mti huu wa mbuyu una simulizi nyingine tofauti, inamuhusu muuguzi wa kifaransa Madamme de Chevalier aliyekuwa akifanya kazi katika kituo cha afya huko Zanzibar mwaka 1895. Inaaminika kwamba madamme de Chevalier alifunga mnyororo katika mti huu ili aweze kumfunga punda wake hapo kipindi yeye anahudumia wagonjwa katika hospitali ya misheni (Kanisa).

Kadri mti ulivyokuwa unakuwa mkubwa ,mnyororo nao unamezwa taratibu.Kipande cha mnyororo kimebaki kama kivutio cha watalii, wanahisroria na waumini wa kikristo. Mwaka jana ,jumba la makumbusho limeongeza kipande cha mnyororo chenye pingiri 34 kutunza urithi huu wa mnyororo ulioanza kupotea.

Unaonyesha muonekano wa kuvuta hisia za wengi japo ni mnara mweupe wa kanisa la kwanza lilojengwa mnamo mwaka 1872.

Mnara huu unabeba umuhimu mkubwa kidini kwani ndipo mahali mwili wa hayati mmishionari David Livingstone uliwekwa baada ya kufariki mnamo Februari 1874, Japo ilikuwa kwa usiku mmoja kabla ya kusafirisha kwa ajili ya mazishi Westminister Abbey mjini London. Kanisa lilibomolewa ingawa mnara ulibaki kama kumbukumbu muhimu ya kihistoria.

Majengo ya kale na historia ya kidini ni hazina kubwa ya mji wa Bagamoyo na ni kivutio kikubwa kinachoonyesha mabadiliko toka enzi za kale mpaka wakati huu wa enzi hizi za teknolojia.Mchanga wa bahari na upepo mwanana toka katika fukwe mbalimbali vinaweza kuwa vivutio vilivyowashawishi wamisionari kujenga kanisa la kwanza upande wa bara katika ukanda wa Afrika Mashariki.

[Mwandishi ni Meneja uhusiano katika Benki ya CRDB]

20

Makumbusho ya Kanisa la Roho Mtakatifula Katoliki Misheni

Majengo ya kale ya Kaole

(Source -untamed horizons.com)

Kwa KifupiBwaga Moyo nguzo za kihistoria

Linapatikana karibu kilomita mbili kaskazini mwa mji, kupitia barabara yenye miti mirefu ya miembe. Kanisa la Roho Mtakatifu la katoliki Misheni, ambalo ni jumba la makumbusho, ni moja kati ya sehemu maarufu za Bagamoyo na kivutio kikubwa cha watalii.

Majengo ya kale ya Kaole yanapatikana kusini mwa Bagamoyo. Katikati ya majengo haya ndipo kuna mabaki ya msikiti wa kale uliojengwa karne ya 13 ambao ni kati ya misikiti yenye muda mrefu zaidi Tanzania na Afrika ya Mashariki. Ulijengwa katika kipindi ambapo Sultan wa Kilwa alipokua na mamlaka juu ya biashara ya pwani, zamani kabla Bagamoyo haijachukuliwa kuwa na umuhimu wowote.

Karibu yake kuna msikiti wa pili ambao ulikuwepo tangu karne ya 15, pamoja na makaburi karibu 22 ambayo mengi yake ni ya tangu kipindi hicho. Miongoni wa makaburi hayo kuna makaburi yaliyojengewa ya washirazi yanayofanana na yale ya Tongoni. Mashariki ya majengo hayo ya kale, baada ya kupita lundo la miti ya mikoko utaikuta bandari ya kale ambayo ilikua ikitumika kipindi Kaole ni mashuhuri.

21

Bwaga Moyo historia

Kwa Picha

Furahia wepesi wa kununua bidhaa kwa njiaya mtandao na Benki ya CRDB

Mwongozo wa Mteja

Manunuzi kwa njia ya mtandao yanaendelea kushika kasi nchini Tanzania kadri ya miaka inavyozidi kwenda. Mfumo huu wa manunuzi unawapa watanzania wengi njia mbadala ya kufanya manunuzi kwa utulivu kutoka majumbani au ofisini kwao. Leo hii, wafanya biashara wa reja reja na wa jumla wanatoa wigo wa kufanya manunuzi kwa njia ya mtandao katika bidhaa na huduma mbalimbali. Vivyo hivyo, watu wengi wanazidi kujenga mazoea ya kutumia njia za kisasa za kibenki pamoja na kutumia kadi za kielectroniki kufanya manunuzi.

Wepesi unaotokana na kufanya manunuzi kwa njia ya mtandao hauwezi kusisitiziwa kwa namna ambavyo mtu hujionea mwenyewe. Kwa kuongezeka kwa biashara na nchi za nje, baadhi ya watu tayari wanafanya manunuzi kwa njia ya mtandao na kisha kusafirisha bidhaa katika nchi zao. Unaweza kufikiria ni kwa jinsi gani unapata utulivu wa kiakili kama utaweza kuepuka usumbufu wa misongamano ya barabarani na mitaa yenye misongamano ya watu ili kufanya manunuzi.

Kama Benki bunifu na yenye kupiga hatua, Benki ya CRDB, imetambua mwelekeo huu mpya wa kulipia huduma na kutoa suluhisho ili kukidhi mahitaji ya wateja wetu kupitia huduma yetu ya benki kwa njia ya mtandao. Leo hii kama unatamani kufanya malipo ya huduma kwa njia ya mtandao ukiwa hapa Tanzania, suluhisho lako bora ni huduma ya malipo ya huduma wa njia ya mtandao kutoka benki ya CRDB inayokupa wepesi na yenye kuaminika. Malipo ya huduma kwa njia ya mtandao kutoka benki ya CRDB yanakupa ulinzi na usalama zaidi wa kufanya manunuzi kwa njia ya mtandao kupitia mtandao wetu popote duniani kwa kutumia kadi ya Tembocard VISA na Tembocard Master Card.

Ili kuanza kutumia huduma hii, utahitaji kufungua akauti uipendayo kutoka benki ya CRDB.Ni rahisi kufungua akaunti ya benki ya CRDB

Hatua ya 1: Fika katika tawi la benki ya CRDB lililopo jirani nawe. Omba fomu ya kufungulia akaunti unayohitaji mfano, Akaunti binafsi ya akiba, Akaunti ya wanafunzi, au Akaunti ya Malkia.

Hatua ya 2: Fata maelekezo wakati wa ujazaji wa fomu. Unaweza kuomba msaada unaohitaji kwa afisa yoyote wa benki ya CRDB. Wakati unajaza fomu tafadhali onyesha ni kadi gani unahitaji kati ya VISA au MasterCard kwa kuwa zote zinakuwezesha kufanya manunuzi kwa njia ya mtandao. Kadi ni bure na inachukua si zaidi ya wiki 2 ili kadi yako kuwa tayari. Utajulishwa kupitia ujumbe wa simu ya mkononi kadi yako itakapokuwa tayari.

Vitu vinvyohitajika kwa ajili ya kufungua akaunti ya Benki ya CRDB Picha 2 za paspoti (Hasa zenye weupe nyuma) Nakala ya kitambulisho kama ni hati ya kusafiria au leseni

ya udereva(Leseni mpya) Wadhamini wawili unaowafahamu na ambao wanaweza

kuwasiliana na benki pindi itakapohitajika. (Tunakushauri kuchagua watu unaowaamini)

Kiasi cha kuanzia kinatokana na aina ya akaunti utakayofungua

Fomu ya kufungua akaunti iliyojazwa kwa usahihi

Hatua ya 3: Fanya maombi ya kufanya manunuzi kwa njia ya mtandao- Pale utakapo pokea kadi yako tayari, wasiliana na tawi lako na kuwaomba wakuwezeshe akaunti yako kufanya manunuzi kwa njia ya mtandao na pia huduma za kibenki kwa njia ya mtandao. Utahitajika kujaza fomu na ndani ya masaa (48) ya kazi akaunti yako itawezeshwa kupata huduma hiyo.

Kufikia hatua hii, utakuwa na uwezo wa kufurahia wepesi wa kufanya manunuzi kwa njia ya mtandao kwa kuwa na uwezo wa kufanya hivyo kupitia viganjani mwako.

22