Taafifa kwa vyombo vya habari (kisahili) Ipsos Tanzania september 2015
-
Upload
ipsos -
Category
Data & Analytics
-
view
231 -
download
15
Transcript of Taafifa kwa vyombo vya habari (kisahili) Ipsos Tanzania september 2015
Dar es Salaam, Tanzania
September 24, 2015
Utafiti juu ya Maswala ya Uchumi, Siasa, tamaduni na mambo ya kijamii Utafiti wa
robo ya tatu 2015
Utangulizi
Huu ni utafiti unaofanywa na kampuni ya Ipsos Tanzania kila baada ya miezi mitatu. Utafiti
huu unadhaminiwa na lpsos. Utafiti huu unatumila kutoa taarifa kwa umma kuhusu masuala
tofauti ya nchi. Utafiti huu ulifanyika kupitia njia ya mahojiano ya ana kwa ana na ulianza
tarehe 5 – 22 Septemba 2015 katika kiwango cha kaya katika mikoa yote ya Tanzania Bara.
Sampuli imewakilishwa katika kiwango cha kitaifa (margin of error 2.3% at 95% confidence
interval)
Alama za muhtasari za utafiti nchini Tanzania:
1) Changamoto nyingi za kimaendeleo ambazo hazijafikiwa zinasubiria awamu ya
serikali ifuatayo ya Tanzania, kwa yeyote atakaye shinda katika uchaguzi huu.
2) Kwa kigezo cha kwamba hakuna hata eneo moja kati ya maeneo ya sera lililokuwa
na watu waliyozidi nusu waliyoonyesha imani katika chama tawala, hii inaashiria
kwamba uchaguzi huu utakuwa na ushindani mkubwa kuliko chaguzi zote tangu
nchi ilipoanzisha mfumo wa vyama vingi.
3) Kwa ujumla, zaidi ya mara mbili ya watanzania wanaunga mkono CCM ukilinganisha
na CHADEMA; Hata hivyo kuna baadhi ambao wanaonekana kutojihusisha na
chama chochote cha siasa .
4) Katika kipindi cha utafiti, J. Magufuli wa CCM anaongoza kwa 2-1 (62% vs 31%)
dhidi ya mpinzani wake mkuu E. Lowassa wa (Chadema/Ukawa).Ingawa tofauti kati
yao ilikuwa ni ndogo kwa wahojiwa ambao hawakuwa na maamuzi au ambao
hawakuweka wazi chaguo lao. Hii inamaanisha kuwa shughuli za kampeni
zinazoendelea katika kipindi kilichobaki zinaweza kuleta mabadiliko makubwa katika
matokeo ya uchaguzi
5) Akiwa anaongoza kwa kiasi kikubwa dhidi ya mpinzani wake katika makundi tofauti
ya idadi ya watu, mgombea wa CCM ana mvuto mkubwa miongoni mwa wanawake
na watu wanaoishi vijijini kuliko miongoni mwa wanaume na watu wanaoishi mijini.
Vivyo hivyo kwa upande wa umri ,ambapo wazee wameridhika zaidi na CCM.
Matokeo ya kina
A. Ajenda ya maendeleo
1. Watanzania wanakubaliana vikubwa kuhusiana na matatizo yanayoikabili nchi,
yakiwemo yale yanayothibitisha umaskini ambayo yametajwa mara kwa mara:
gharama za maisha, njaa, usambazaji wa maji, uzalishaji katika kilimo, n.k.
2. Hii inathibitishwa na uwepo wa hali ya umaskini katika maeneo ya wahojiwa (89%),
ikiwemo kiwango kidogo cha uboreshaji wa maeneo ya mjini tofauti na maeneo ya
kijijini. (89% vs. 95%).
3. Vivyo hivyo, vitu hivyo vya msingi katika maendeleo kama vile miundombinu na
huduma za afya ni kipaumbele kikubwa kwa watanzania cha kukabili umaskini.
B. Maswala kabla ya uchaguzi : Vyama vya siasa na Wagombea.
1. Katika kipindi cha utafiti, karibia robo tatu ya watanzania walikuwa wana muelekeo
wa chama fulani cha siasa (78%), na karibia wote hao, walikuwa wameshafanya
maamuzi juu ya nani watakaomchagua (70%). Hali kadhalika kiasi fulani cha
wahojiwa walisema kwamba kuna uwezekano mkubwa (11%) au kuna uwezekano
wa kiasi fulani (7%) kwamba watampigia kura mgombea tofauti wa urais tarehe 25
Oktoba.
2. Katika suala la maeneo makuu 7 ya sera za maendeleo (mf. Miundombinu, elimu,
afya, nk) karibia mara mbili ya idadi hiyo ya watanzania wameonyesha kuwa na
imani na CCM katika kuwasimamia tofauti na Chadema, pasipokuwa na takwimu za
kitofauti katika uwiano wa majibu yao.
3. Mgawanyiko huu unaashiria jinsi mashabiki wa vyama vikuu vya siasa walivyojigawa,
ambapo mashabiki wa CCM ni mara mbili ya wale wa chama pinzani, Chadema
(60% vs. 29%)
4. Vile vile katika kipindi cha utafiti, mgombea wa CCM J. Magufuli ana washabiki
karibia mara mbili Zaidi ya mpinzani wake E. Lowassa miongoni mwa wale
waliokwishafanya maamuzi (62% vs 31%)
5. Mgombea wa CCM anaushabiki mkuwa kwenye vigezo viwili (jinsia na Makazi); Kwa
kuangalia jinsia ushabiki kwa mgombea wa CCM na Chadema, kuna tofauti ya 17%,
wakati kwa upande wa wanawake tofauti inaongezeka kwa 30% Hali kadhalika
miongoni mwa wakazi wa vijjijini tofauti inaongezeka kwa 20%. Lakini inapungua kwa
5% kwa kuangalia wakazi wa mjini.
6. Vile vile watu wazima wanaonekana kushabikia CCM, kukiwa na tofauti ndogo ya
ushabiki inayopokea toka kwa kundi la vijana na wazee
7. Ikiwa umebakia mwezi mmoja kamili kufikia tarehe ya uchaguzi; ni theluthi mbili tu ya
wale walionyesha msimamo wa nani watamchagua ambao hawatobabadilisha
maamuzi yao (70%) ikiacha theuthi moja ya wale ambao wanaweza kubadilisha
mawazo yao kuanzia sasa na October 25.
Survey Methodology /Njia ya kufanya utafiti
Walengwa katika utafiti huu walikuwa ni watanzania wenye umri wa miaka 18 na
zaidi, kati ya hao 1,836 wanaoishi maeneo ya mjini na kijijini Tanzania bara
walihojiwa. The margin-of-error attributed to sampling and other random effects is +/-
2.3 with a 95% confidence level. Kwa maelezo ya kidemografia angalia nakala ya Power
Point iliyoambatanishwa.
Utafiti ulifanyika kati ya tarehe 5-22 Septemba 2015. Taarifa zilikusanywa kwa njia
ya mahojiano ya ana kwa ana kwa kutumia simu za kisasa za mkononi.
ALAMA MUHIMU KWA AJILI YA VYOMBO VYA HABARI/ WASOMAJI.
1. UTAFITI HUU HAUKUWEZA KUWEKA DHAHIRI NI WAHOJIWA WAPI KATI YA
HAWA WOTE WATAENDA KUPIGA KURA TAREHE 25 OKTOBA KATIKA VITUO
VYAO VYA KUPIGA KURA. KUTOKANA NA HISTORIA YA KIPINDI CHA NYUMA
AMBAPO KIASI CHA UHUDHURIAJI WA WAPIGA KURA KINATOFAUTIANA
SEHEMU ZOTE NCHINI. MATOKEO YA SAMPULI HII HAYAWEZI KUTUMIKA
KUTABIRI MATOKEO HALISI HATA KAMA UCHAGUZI UNGEFANYIKA KESHO.
2. UKIZINGATIA MUDA ULIOBAKI KUAZIA SASA MPAKA TAREHE 25 OKTOBA
PAMOJA NA KAMPENI ZINAZOENDELEA, HAKUNA UHAKIKA KUWA MATOKEO
YA UTAFITI HUU HAYATABADILIKA KATI YA SASA MPAKA SIKU YA UCHAGUZI.
For further clarification or comments, please contact:/ Kwa maelezo zaidi
au maoni wasiliana na ;
Charles Makau Dr. Tom Wolf
Country Head: Ipsos Tanzania Research Analyst
[email protected] [email protected]
+ 255 22 277 5851 / 277 5628
David Luhinda
Project Manager
+ 255 22 277 5851 / 277 5628
twitter.com/ipsostanzania
facebook.com/ipsostanzania
http://www.ipsos.co.tz/
http://www.ipsos.com