Risala ya kiongozi muadhamu wa mapinduzi ya kiislamu kwa vijana wa ulaya na amerika kaskazini

3
Risala ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa Vijana wa Ulaya na Amerika Kaskazini 21/01/2015 Bismillahir Rahmanir Rahim Kwa vijana wote wa Ulaya na Amerika Kaskazini Matukio ya hivi karibuni ya nchini Ufaransa na mfano wake katika baadhi ya nchi za Magharibi yamenifanya niamue kuzungumza nanyi moja kwa moja kuhusu matukio hayo. Ninakukhutubuni na kukulengeni nyinyi (vijana) si kwa sababu ya kutaka kubeba jukumu la wazazi wenu, hapana bali ni kwa sababu mustakbali ya mataifa na nchi zenu yamo mikononi mwenu; na pia ni kwa sababu ninaona shauku na hamu ya kutafuta ukweli ni kubwa sana katika nyoyo zenu. Hapa siwalengi viongozi na wanasiasa wenu kwani ninaamini kuwa wanafanya makusudi kutenganisha njia ya siasa na njia ya ukweli na uhalisia wa mambo. Ninapenda kuzungumza nanyi kuhusu Uislamu, hususan kuhusiana na sura ya Uislamu ambayo inaoneshwa kwenu. Kuna njama nyingi zimefanyika katika kipindi cha zaidi ya miongo miwili iliyopita, takriban tangu baada ya kusambaratika Umoja wa Kisovieni kwa ajili ya kuifanya dini tukufu ya Kiislamu kuwa adui mkubwa anayetisha. Kueneza chuki dhidi ya Uislamu na kutumia vibaya suala hilo, kwa bahati mbaya ni jambo la zamani sana katika hostoria ya kisiasa ya Magharibi. Hapa sina nia ya kuonyesha ni vitendo gani vya kueneza chuki vilivyoenezwa kwa mataifa ya Ulaya hadi hivi sasa. Nyinyi wenyewe kwa kutupia jicho kitogo tu utafiti wa kiukosoaji uliofanywa hivi karibuni kuhusiana na historia mtaona kuwa katika uandishi mpya wa historia, kuna miamala na vitendo visivyo vya kiuaminifu na vya upotoshaji vilivyofanywa na tawala za Magharibi dhidi ya mataifa mengine duniani na dhidi ya tamaduni za mataifa mbali mbali ya dunia. Historia ya Ulaya na Marekani imejaa mambo ya aibu ya kuwafanya watu watumwa katika enzi za ukoloni. Historia hiyo imejaa maovu ya aibu kama ya ukatili waliofanyiwa watu wasio Wazungu na wasio Wakristo. Watafiti na waandishi wenu wa historia wanachanganyikiwa na wanaemewa na kuingiwa na tahayuri kila wanapoona umwagaji mkubwa wa damu uliofanyika kwa jina la dini ya Kikristo imma kwa jina la Ukatoliki au Uprotestani au kwa jina la utaifa na ukabila na kaumu ya taifa fulani na kuwatwisha walimwengu vita vya kwanza na vya pili vya dunia. Kuwa na hisia hizo za kuona aibu kwa vitendo hivyo ni jambo la kupongezwa na lengo langu katika kukumbushia faharasa hiyo ndefu ya maovu yaliyofanywa na nchi za Magharibi si kuchimbua na kutoa aibu za historia hiyo, bali lengo langu ni kukutakeni muwaulize wasomi wenu, kwa nini mara zote wananchi wa nchi za Magharibi wanaamka na kujua ukweli baada ya kupita makumi kadhaa ya miaka na baadhi ya wakati wanaamka baada ya kupita mamia kadhaa ya miaka? Kwa nini hisia za ndani ya nyoyo za wananchi wa Magharibi mara zote lazima zitegemee mambo yaliyopita muda mrefu nyuma, si masuala ya sasa hivi? Kwa nini kunawekwa vizuizi vya kuwafikia inavyotakiwa watu wa Magharibi utambuzi na mambo kuhusu suala muhimu kama Uislamu na umuhimu wa kuamiliana kwa njia sahihi na utamaduni na tafakuri ya

Transcript of Risala ya kiongozi muadhamu wa mapinduzi ya kiislamu kwa vijana wa ulaya na amerika kaskazini

Page 1: Risala ya kiongozi muadhamu wa mapinduzi ya kiislamu kwa vijana wa ulaya na amerika kaskazini

Risala ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa Vijana wa Ulaya na Amerika

Kaskazini

21/01/2015

Bismillahir Rahmanir Rahim

Kwa vijana wote wa Ulaya na Amerika Kaskazini

Matukio ya hivi karibuni ya nchini Ufaransa na

mfano wake katika baadhi ya nchi za Magharibi

yamenifanya niamue kuzungumza nanyi moja

kwa moja kuhusu matukio hayo.

Ninakukhutubuni na kukulengeni nyinyi (vijana)

si kwa sababu ya kutaka kubeba jukumu la wazazi

wenu, hapana bali ni kwa sababu mustakbali ya

mataifa na nchi zenu yamo mikononi mwenu; na

pia ni kwa sababu ninaona shauku na hamu ya

kutafuta ukweli ni kubwa sana katika nyoyo zenu.

Hapa siwalengi viongozi na wanasiasa wenu

kwani ninaamini kuwa wanafanya makusudi kutenganisha njia ya siasa na njia ya ukweli na

uhalisia wa mambo.

Ninapenda kuzungumza nanyi kuhusu Uislamu, hususan kuhusiana na sura ya Uislamu ambayo

inaoneshwa kwenu. Kuna njama nyingi zimefanyika katika kipindi cha zaidi ya miongo miwili

iliyopita, takriban tangu baada ya kusambaratika Umoja wa Kisovieni kwa ajili ya kuifanya dini

tukufu ya Kiislamu kuwa adui mkubwa anayetisha. Kueneza chuki dhidi ya Uislamu na kutumia

vibaya suala hilo, kwa bahati mbaya ni jambo la zamani sana katika hostoria ya kisiasa ya

Magharibi.

Hapa sina nia ya kuonyesha ni vitendo gani vya kueneza chuki vilivyoenezwa kwa mataifa ya

Ulaya hadi hivi sasa. Nyinyi wenyewe kwa kutupia jicho kitogo tu utafiti wa kiukosoaji

uliofanywa hivi karibuni kuhusiana na historia mtaona kuwa katika uandishi mpya wa historia,

kuna miamala na vitendo visivyo vya kiuaminifu na vya upotoshaji vilivyofanywa na tawala za

Magharibi dhidi ya mataifa mengine duniani na dhidi ya tamaduni za mataifa mbali mbali ya

dunia. Historia ya Ulaya na Marekani imejaa mambo ya aibu ya kuwafanya watu watumwa

katika enzi za ukoloni. Historia hiyo imejaa maovu ya aibu kama ya ukatili waliofanyiwa watu

wasio Wazungu na wasio Wakristo. Watafiti na waandishi wenu wa historia wanachanganyikiwa

na wanaemewa na kuingiwa na tahayuri kila wanapoona umwagaji mkubwa wa damu

uliofanyika kwa jina la dini ya Kikristo imma kwa jina la Ukatoliki au Uprotestani au kwa jina la

utaifa na ukabila na kaumu ya taifa fulani na kuwatwisha walimwengu vita vya kwanza na vya

pili vya dunia.

Kuwa na hisia hizo za kuona aibu kwa vitendo hivyo ni jambo la kupongezwa na lengo langu

katika kukumbushia faharasa hiyo ndefu ya maovu yaliyofanywa na nchi za Magharibi si

kuchimbua na kutoa aibu za historia hiyo, bali lengo langu ni kukutakeni muwaulize wasomi

wenu, kwa nini mara zote wananchi wa nchi za Magharibi wanaamka na kujua ukweli baada ya

kupita makumi kadhaa ya miaka na baadhi ya wakati wanaamka baada ya kupita mamia kadhaa

ya miaka? Kwa nini hisia za ndani ya nyoyo za wananchi wa Magharibi mara zote lazima

zitegemee mambo yaliyopita muda mrefu nyuma, si masuala ya sasa hivi? Kwa nini kunawekwa

vizuizi vya kuwafikia inavyotakiwa watu wa Magharibi utambuzi na mambo kuhusu suala

muhimu kama Uislamu na umuhimu wa kuamiliana kwa njia sahihi na utamaduni na tafakuri ya

Page 2: Risala ya kiongozi muadhamu wa mapinduzi ya kiislamu kwa vijana wa ulaya na amerika kaskazini

Kiislamu?

Nyote mnajua vyema kwamba, kujaribu kuidunisha na kueneza chuki na woga dhidi ya wengine

ndiyo mbinu kuu inayotumiwa na watu madhalimu wanaopenda kujinufaisha binafsi. Natumia

fursa hii kukutakeni mjiulize ndani ya nafsi zenu kwamba kwa nini siasa kongwe za kueneza

woga na chuki, hivi sasa zimeongezewa nguvu mno kwa namna isiyo na mfano dhidi ya Uislamu

na dhidi ya Waislamu? Kwa nini muundo wa nguvu duniani hivi sasa unapenda kuiweka

pembeni fikra ya Kiislamu na kuwa mkali kila fikra hiyo inapojitokeza? Kwani kuna kitu gani

kizuri na cha thamani ndani ya Uislamu ambacho kinasumbua mipango ya madola makubwa na

hivi kuna manufaa gani yanayopata madola hayo pale yanapoeneza sura ghalati na isiyo sahihi

kuhusu Uislamu? Hivyo basi ombi langu la kwanza kabisa kwenu ni kufanya uchunguzi na

udadisi kuhusu misukumo na malengo ya kufanyika kampeni kubwa mno ya kuenezwa sura

isiyo sahihi kuhusiana na Uislamu.

Ombi langu la pili ni kwamba katika konesha kwenu radiamali kuhusu wimbi hili kubwa la

kuhukumu mambo bila ya utafiti wa kina na kabla ya kutokea kwake, fanyeni juhudi za kupata

elimu ya moja kwa moja kutoka katika dini yenyewe ya Kiislamu. Mantiki sahihi inahukumu

kwamba mtu anatakiwa ajue udhati na uhalisia wa kitu anachofanywa akiogope na kukaa mbali

nacho.

Mimi sishikilii kwamba mukubaliane na mtazamo wangu au mtazamo mwingine wowote wa

Kiislamu. Hapana, bali ninachosema mimi ni kuwa, msiruhusu jambo hili muhimu na safi na

lenye taathira kubwa katika dunia ya leo lifikishwe kwenu kwa malengo na shabaha zilizojaa

upotofu. Msiruhusu watu wanaofanya mambo kwa kupenda kujionesha na magaidi

wanaotumiwa na madola ya Magharibi ambao wanajifanya ndio wawakilishi wa Uislamu,

kuziteka akili na fikra zenu. Fanyeni juhudi za kuuelewa Uislamu kupitia vyanzo sahihi na

marejeo yake ya awali na ya moja kwa moja. Utafuteni Uislamu kupitia Qur'ani na sira na

maisha ya Mtume wake Mtukufu (rehema za Allah ziwe juu yake na Aal zake). Hapa ninapenda

kukuulizeni, hivi hadi hivi sasa mumewahi kuisoma Qur'ani Tukufu? Je mafundisho ya Mtume

wa Uislamu (rehema Allah ziwe juu yake na Aal zake) na mafundisho yake yaliyojaa

ubinaadamu na maadili mema mumewahi kuyatalii na kuyasoma? Je hadi hivi sasa

mumeshawahi kupata ujumbe wa Uislamu kupitia vyanzo vingine visivyo vyombo vyenu vya

habari? Je hadi hivi sasa imeshakupitikieni kujiuliza vipi dini hii ya Kiislamu na kwa kutumia

misingi na matukufu gani imeweza kuleta ustaarabu mkubwa wa kielimu na kifikra duniani kwa

karne nyingi na kumzawadia mwanadamu wasomi na wanafikra wakubwa?

Ninachopenda kukuombeni ni kwamba msiruhusu njama za kuoneshwa sura mbaya na ovu

kuhusiana na Uislamu kuwa kizuizi katika hisia zenu na kukuzueni kuhukumu mambo

kiuadilifu. Leo hii zana za kisasa za mawasiliano zimevunja mipaka ya kijiografia, hivyo

msiruhusu wakufungeni ndani ya mipaka ya kupandikizwa na isiyo na ukweli. Ijapokuwa mtu

mmoja mmoja hawezi kuziba mapengo yote yaliyopandikizwa kwa muda mrefu sasa, lakini kila

mmoja wenu anaweza kujenga daraja la fikra na insafu kwenye mapengo hayo kwa lengo la

kujielimisha yeye mwenyewe mambo sahihi na vile vile kuwaelimisha watu wanaomzunguka.

Hii ni changamoto iliyowekwa tangu zamani baina ya Uislamu na nyinyi vijana. Ijapokuwa

changamoto hiyo ni kubwa, lakini inaweza kuzusha maswali mapya katika akili zenu

zinazopenda kuchunguza na kudadisi mambo. Kufanya juhudi za kutafuta majibu ya maswali

hayo ni fursa nzuri ya kukuwezesheni kupata uhakika mpya. Hivyo msiipoteze fursa hii ya kuwa

na welewa sahihi na usio wa kuhukumu mambo kinyume na insafu na uadilifu na kabla ya

kutokea kwake kuhusiana na dini tukufu ya Kiislamu. Msipoteze fursa hili ili kwa kuzingatia

kupenda kwenu kujua ukweli na uhakika, pengine vizazi vinavyokuja vikaandika historia ya

Page 3: Risala ya kiongozi muadhamu wa mapinduzi ya kiislamu kwa vijana wa ulaya na amerika kaskazini

miamala ya kipindi hiki baina ya Uislamu na Magharibi, kwa muono wa wazi na hisia nzuri za

ndani ya moyo.

Sayyid Ali Khamenei

1/11/1393 (Hijria Shamsia)

(Januari 21, 2015).