RIPOTI YA KAMATI YA FEDHA, BIASHARA NA KILIMO YA BARAZA … · 2019-02-15 · Ripoti ya Kamati ya...
Transcript of RIPOTI YA KAMATI YA FEDHA, BIASHARA NA KILIMO YA BARAZA … · 2019-02-15 · Ripoti ya Kamati ya...
Ripoti ya Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo inayotokana na ufuatiliaji utekelezaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Biashara na Viwanda pamoja na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2018/2019. 1
RIPOTI YA KAMATI YA FEDHA, BIASHARA NA KILIMO YA BARAZA LA WAWAKILISHI
ZANZIBAR KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019
1. UTANGULIZI
Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo ni miongoni mwa Kamati nane za Kudumu za
Baraza la Wawakilishi iliyoundwa kwa mujibu Kanuni ya 106, Jadweli la Kwanza la
Kanuni za Kudumu za Baraza la Wawakilishi, Toleo la mwaka 2016. Kamati hiyo
imepangiwa kutekeleza majukumu yafuatayo:
i. Kufuatilia utekelezaji wa maagizo ya Kamati yaliyotolewa kwenye ripoti
ya Kamati ya mwaka uliotangulia.
ii. Kufuatilia utekelezaji wa Sera na Mipango ya Wizara husika kwa kadiri Spika
atakavyoelekeza kwa mujibu wa malengo yaliyowasilishwa Barazani wakati wa
usomaji Bajeti na Hotuba nyengine za Waziri alizotoa katika Baraza.
iii. Kufuatilia utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo ya Kitaifa na ya Wananchi ya
Wizara husika.
iv. Kuchunguza na kufuatilia mapato na matumizi ya kila mwaka ya Serikali na
kuona kwamba matumizi yaliyofanywa yalizingatia thamani halisi ya fedha.
v. Kuchambuwa mapendekezo ya Serikali kuhusu makadirio ya Wizara husika ya
mapato na matumizi ya kila mwaka.
vi. Kushughulikia Miswada ya Sheria itakayokabidhiwa kwake na Spika.
vii. Kuchambuwa ahadi zote za Wizara zilizo chini ya Kamati kama zitakavyokuwa
zikitolewa katika Baraza na kufatilia utekelezaji wa ahadi hizo.
viii. Kuzingatia na kutekeleza jambo jengine lolote litakalopelekwa kwake na Spika.
Katika kutekeleza majukumu yaliyopo hapo juu, Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo
inasimamia utekelezaji wa majukumu ya Wizara zifuatazo:
Wizara ya Fedha na Mipango;
Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi; na
Wizara ya Biashara na Viwanda.
1.1 MUUNDO WA KAMATI
Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo imeundwa na Wajumbe saba na Makatibu wawili
wafuatao:
1. Mhe. Dkt. Mwinyihaji Makame - Mwenyekiti;
2. Mhe. Hamida Abdalla Issa - Makamu Mwenyekiti;
3. Mhe. Ali Salum Haji - Mjumbe;
4. Mhe. Wanu Hafidh Ameir - Mjumbe;
5. Mhe. Masoud Abrahman Masoud - Mjumbe;
6. Mhe. Moh’d Mgaza Jecha - Mjumbe;
7. Mhe. Nadir Abdul-latif Yussuf - Mjumbe;
Ripoti ya Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo inayotokana na ufuatiliaji utekelezaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Biashara na Viwanda pamoja na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2018/2019. 2
8. Ndg. Asma Ali Kassim - Katibu; na
9. Ndg. Said Khamis Ramadhan - Katibu.
1.2 UTARATIBU WA KAZI ZA KAMATI
Katika utekelezaji wa kazi zake chini ya Kanuni ya 108 ya Baraza la Wawakilishi, Kamati
ilifanya kazi kwa utaratibu wa kupokea taarifa tofauti za kila robo mwaka (quarterly
reports) za utekelezaji wa malengo ya Bajeti ya Wizara, kupokea taarifa za utekelezaji wa
Maagizo ya Kamati, kukutana na wadau mbali mbali wa sekta zinazosimamiwa na
Kamati pamoja na kukagua baadhi ya maeneo na miradi mbali mbali inayosimamiwa na
Wizara zinazohusika ili kuona hatua za utekelezaji zilizofikiwa.
Kwa mwaka wa fedha 2018/2019, hadi Kamati inawasilisha ripoti yake mbele ya Baraza
hili tukufu ilifanya kazi zake kwa mizunguko mitatu kwa muda wa wiki sita, Unguja,
Pemba na Tanzania Bara.
1. Mzunguko wa kwanza ulianzia tarehe 27 Agosti, 2018 hadi tarehe 31 Septemba,
2018 Unguja na tarehe 03 Septemba, 2018 hadi tarehe 07 Septemba, 2018 Pemba.
2. Mzunguko wa pili ulianzia tarehe 05 Novemba, 2018 hadi tarehe 09 Novemba,
2018 Unguja na tarehe 12 Novemba, 2018 hadi tarehe 16 Novemba, 2018
Tanzania Bara.
3. Mzunguko wa tatu ulianzia tarehe 14 Januari, 2019 hadi tarehe 18 Januari, 2019
Pemba na tarehe 21 Januari, 2019 hadi tarehe 25 Januari, 2019.
Ripoti hii imeandaliwa kwa kufuata maelekezo ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984,
Sheria ya Baraza la Wawakilishi na Kanuni zake (Toleo la 2016), Taarifa za utekelezaji wa
malengo ya Wizara, ziara mbali mbali za ndani na nje ya Zanzibar, Taarifa za utekelezaji
wa maagizo ya Kamati na ripoti mbalimbali zilizotokana na tafiti zilizofanywa na Wizara
zinazosimamiwa na Kamati hii.
Ripoti ya Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo inayotokana na ufuatiliaji utekelezaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Biashara na Viwanda pamoja na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2018/2019. 3
2. WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO
Wizara ya Fedha na Mipango ndio roho ya nchi yetu kiuchumi ambayo inasimamia
makusanyo yote ya Serikali na kufanya malipo kwa Taasisi za Serikali ili ziweze
kutekeleza majukumu yao ipasavyo. Aidha, Wizara hii pia ndio inayohusika na upangaji
wa Bajeti kuu ya Serikali na mpango mzima wa matumizi yaliyokusudiwa. Kwa mwaka
2018/2019, Wizara ya Fedha na Mipango ilipanga kutekeleza Programu Kuu zifuatazo:
a) Programu kuu ya Uendeshaji na Uratibu wa Wizara ya Fedha na Mipango;
b) Programu kuu ya Usimamizi na Uwekezaji wa Mali za Umma;
c) Programu kuu ya Usimamizi wa Bajeti na Fedha za Umma;
d) Programu kuu ya Usimamizi wa Mfuko Mkuu wa Serikali;
e) Programu kuu ya Kuratibu Mipango ya Kitaifa na Maendeleo ya Watendakazi;
f) Programu kuu ya Usimamizi wa Uchumi Mkuu; na
g) Programu kuu ya Utawala na Uendeshaji wa Tume ya Mipango.
Programu hizo zinatekelezwa na Wizara ya Fedha na Mipango kupitia Idara zifuatazo:
i. Idara ya Mipango, Sera na Utafiti;
ii. Idara ya Uendeshaji na Utumishi;
iii. Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali;
iv. Idara ya Bajeti;
v. Idara ya Fedha za Nje;
vi. Idara ya Mitaji ya Umma;
vii. Idara ya Hesabu za Ndani;
viii. Idara ya Fedha za Kodi;
ix. Mamlaka ya Ununuzi na Uondoshaji wa Mali za Umma; na
x. Ofisi Kuu Pemba.
Mbali na Idara hizo na kutokana na umuhimu wake, Wizara ya Fedha na Mipango
inakamilisha muundo wake kwa Taasisi zifuatazo zinazojitegemea:
i. Tume ya Mipango
ii. Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB);
iii. Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ);
iv. Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA);
v. Mfuko wa Barabara (ZFR);
vi. Shirika la Bima la Zanzibar (ZIC);
vii. Bodi ya Rufaa za Kodi Zanzibar (Tax Appeal Board);
viii. Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF);
ix. Mahkama ya Rufaa za Kodi; na
x. Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali.
Ripoti ya Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo inayotokana na ufuatiliaji utekelezaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Biashara na Viwanda pamoja na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2018/2019. 4
Kadhalika, Wizara ya Fedha na Mipango inazo Taasisi kadhaa ambazo ni za Muungano
lakini zinafanya kazi zake hapa Zanzibar. Taasisi hizo ni:
i. Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA);
ii. Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA);
iii. Benki Kuu ya Tanzania (BOT); na
iv. Tume ya Pamoja ya Fedha (JFC) - Tawi la Zanzibar.
Katika kuhakikisha fedha za Serikali zilizotolewa kwa Wizara ya Fedha na Mipango na
zinatumika kama ilivyokusudiwa, Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo ilifanya vikao
tofauti kuhoji utekelezaji wa Programu ambazo Wizara imeingiziwa fedha na kufanya
ziara kadhaa zilizolenga kujionea na kutathmini thamani ya halisi ya fedha “Value for
Money”. Aidha, Kamati ilikusudia pia kuangalia mafanikio yaliyopatikana na
changamoto zilizopo katika utekelezaji wa Programu za Wizara ya Fedha na Mipango
pamoja na miradi ya Maendeleo.
2.1 UTEKELEZAJI WA PROGRAMU ZA WIZARA
Kwa mwaka wa fedha 2018/2019, utekelezaji wa Programu zote za Wizara ya Fedha na
Mipango ulipangiwa kuingiziwa jumla ya shilingi 154,764,013 bilioni. Hadi kufikia
Disemba 2018, jumla ya shilingi 134.68 bilioni ziliingizwa kutekeleza mambo tofauti sawa
na asilimia 89 ya makadirio. Aidha, kwa kipindi hicho, jumla ya shilingi 21.02 bilioni
zilipangwa kukusanywa ambapo hadi kufikia Disemba 2018, jumla ya shilingi 18.99
bilioni sawa na asilimia 90 ya makadirio zimekusanywa. Tathmini ya utekeleza
unaotokana na matumizi ya fedha hizo unaonekana katika utekelezaji wa Programu Kuu
zifuatazo.
2.2 PROGRAMU KUU YA URATIBU NA UENDESHAJI WA WIZARA
Programu hii imekusudia kuweka mazingira bora kwa wafanyakazi, kuwa na mipango na
sera ya sekta za fedha iliyoimara nchini itakayosaidia kukuza uchumi pamoja na
kuhakikisha shughuli zilizopangwa kwa sekta ya fedha zinatekelezwa. Utekelezaji wa
Programu hii unafanywa na Idara ya Mipango, Sera na Utafiti, Idara ya Uendeshaji na
Utumishi na Afisi Kuu Pemba. Miongoni mwa mambo ambayo yametekelezwa na
Programu hiyo ni:
2.3 UJENZI WA AFISI YA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO PEMBA
Kamati inaipongeza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kufikiria na kutekeleza Mradi
mkubwa wa Ujenzi wa Afisi mpya ya Wizara ya Fedha na Mipango Pemba kwa pesa
zake wenyewe. Hakika ujenzi wa Afisi hizo ambazo zitatumiwa na Wizara tatu za Serikali
(Wizara ya Fedha na Mipango Pemba na Taasisi zake, Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria,
Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Taasisi zake pamoja na Wizara ya Kazi,
Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto utaondoa changamoto kwa watendaji ya
kufanya kazi katika mazingira yasiyoridhisha. Kamati imeridhihwa na ubora wa ujenzi
huo inaonekana wazi kwamba jengo litakapomalizika litakuwa limezingatia thamani
halisi ya fedha “value for money”. Kadhalika, jengo hilo pia ni la kisasa na limezingatia
Ripoti ya Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo inayotokana na ufuatiliaji utekelezaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Biashara na Viwanda pamoja na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2018/2019. 5
uwepo wa miundombinu ya watu wasiojiweza kwa kuwatengenezea mazingira mazuri
yatakayowawezesha kufika hadi katika ukumbi mkubwa wa mikutano uliopo juu ya
jengo na kutumia huduma mbali mbali ikiwemo vyoo maalum vilivyojengwa kwa ajili
yao.
Jengo hilo limejengwa na Kampuni ya Mzalendo “Quality Building Contractor” (QBC)
na kusimamiwa na Mshauri Elekezi “Zanzibar Consultant Limited” lilianza mwezi wa
Septemba, 2016 kukiwa na dhana ya kujengwa ghorofa mbili na kutarajiwa kumalizika
mwezi Machi, 2018. Baada ya kufanya tathmini ya ujenzi huo, Wizara iliona kwamba
ujenzi huo uwe wa ghorofa tatu na kupelekea muda wa kukamilika kwake kuwa
Disemba, 2018. Kutokana na ukosefu wa baadhi ya vifaa vikiwemo aluminium,
umefanya ujenzi huo ukadiriwe kumalizika mwishoni mwa mwezi wa Februari, 2019.
Ujenzi huo wenye ukubwa wa eneo la mita za mraba 9,988 umepangwa kutumia shilingi
13.6 Bilioni hadi kumalizika kwake ambapo hadi Kamati inatembelea jengo hilo, jumla
ya shilingi 11.4 Bilioni zilikuwa tayari zimeshalipwa. Majengo yatakuwa na baadhi vifaa
muhimu vikiwemo “transformer” tatu na “switch gear” yake, sehemu kubwa ya kuegesha
gari, vipoza hewa 202 na “lift” nne ambapo moja ni kwa matumizi ya ukumbi pekee.
Aidha, jengo litakuwa na vifaa vya uhakika vya kiusalama vinavyotumia teknolojia ya
kisasa ikijumuisha “CCTV Camera, fire horse” na “portable fire extinguisher, fire detector,
call point” vitakavyoshughulikia ajali za moto kabla moto haujawaka.
CHANGAMOTO
1. Upungufu wa baadhi ya vifaa vikiwemo ‘aluminium’ za Madirisha na Milango.
Hili limetokana na kuzorota kwa taratibu za utoaji wa vifaa hivyo bandarini
baada ya Watendaji wa TBS kuhitaji kufanya ukaguzi zaidi ili kujiridhisha
kutokana na kunatetesi kuwa mzigo ulioingizwa umezidi na hauendani na
maelezo yaliyoainishwa katika nyaraka husika.
2. Ucheleweshwaji wa vifaa vya ujenzi uliopelekea kubadilika badilika kwa muda wa
ujenzi.
3. Kutokuwepo kwa vifaa vya ukaguzi wa watu watakaoingia katika jengo hilo.
Vifaa hivi havijazingatiwa kuwemo katika mkataba.
MAONI, USHAURI NA MAAGIZO YA KAMATI
1. Wizara ihakikishe inamsimamia ipasavyo Mkandarasi wa ujenzi huo ili afuatilie
kwa karibu upatikanaji wa vifaa vianavyohitajika kwa wakati.
2. Kamati inaitaka Wizara iwe makini katika kusimamia ujenzi huo na kuepuka
sababu za mara kwa mara zisizokuwa na mashiko zinazopelekea kuongezeka kwa
muda wa ujenzi.
3. Wizara ichukuwe hatua muafaka ya kuweka vifaa vya ukaguzi katika mlango
mkubwa wa kuingia katika jengo.
Ripoti ya Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo inayotokana na ufuatiliaji utekelezaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Biashara na Viwanda pamoja na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2018/2019. 6
4. Wizara ihakikishe inaingia mikataba na kampuni za usafishaji zenye uwezo wa
kusafisha pamoja na kuisimamia kwa ukaribu sana kampuni hiyo ili iweze
kutekeleza kazi zake ipasavyo.
2.4 UJENZI WA JENGO LA BENKI YA WATU WA ZANZIBAR (PBZ) WETE
Jengo la Tawi la Benki ya Watu wa Zanzibar Wete hapo awali lilikuwa likitambuliwa
kama Hoteli ya Serikali lilianza rasmi kufanyiwa matengenezo makubwa tarehe 25
Oktoba, 2018 chini ya Mjenzi “Grasshopper Building Construction Ltd.” na Mshauri
Elekezi Benki ya Watu wa Zanzibar. Ujenzi huo utakaokuwa na ghorofa tatu,
unatarajiwa kukamilika tarehe 25 Februari, 2019 na kutumia jumla ya shilingi bilioni
1,210,917,239,000 (ikijumuisha kodi) kutoka katika Mfuko Mkuu wa Serikali. Hadi
Kamati inatembelea jengo hilo katika mwezi wa Januari 2019, jumla ya shilingi milioni
145,200,000 tayari zilikuwa zimelipwa na Serikali ambapo ujenzi ulifikia asilimia hamsini
ya utekelezaji.
Kamati inaipongeza Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango kwa kutekeleza
kivitendo azma ya kuwapelekea karibu wananchi wake huduma za kibenki pamoja na
kutumia fedha nyingi kujenga na kuimarisha majengo mbali mbali ya kutolea huduma
hizo. Kufanya hivyo kutapelekea wafanyakazi na wateja wa benki hiyo wawe katika
mazingira mazuri (better conducive working environment). Jengo hilo litakuwa na
huduma zote zinazopatikana katika tawi lolote la Benki ya Watu wa Zanzibar zikiwemo
maeneo ya wapokeaji na watoaji fedha (tellers), chumba cha kuhifadhia fedha, mashine
mbili za kielektroniki (ATM), Ofisi za Bodi ya Mapato Zanzibar, vyumba vya kulala
wafanyakazi (floor ya juu), ukumbi mkubwa, vifaa vya usalama (CCTV Camera) na
sehemu za kuegesha gari. Licha ya mipango hiyo mizuri, bado jengo linakabiliwa na
changamoto zifuatazo:
CHANGAMOTO
1. Udogo wa eneo la kuegeshea gari kwa vile eneo liliopo linategemewa kuchukua
gari zisizozidi kumi na moja.
2. Kukosekana mazingira rafiki yatakayowawezesha ndugu zetu walemavu kufika
katika ghorofa ya pili na tatu za jengo hilo.
3. Kutozibwa vizuizi vya pembeni mwa ngazi kunakoweza kusababisha usumbufu
kwa watoto au kupenya na kuanguka.
4. Fedha alizolipwa Mjenzi ni kidogo sana ukilinganisha na kazi iliyofanyika, hili
linaweza kuisababishia Serikali kuongeza muda wa ujenzi kwa kushindwa
kutekeleza wajibu wao.
Ripoti ya Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo inayotokana na ufuatiliaji utekelezaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Biashara na Viwanda pamoja na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2018/2019. 7
MAONI, USHAURI NA MAAGIZO YA KAMATI
1. Wizara kupitia PBZ iwatafute wanaomiliki wa eneo lililowazi liliopo karibu na
jengo hilo ili waweze kulinunua na kulifanya kuwa ni eneo la maegesho ya gari.
2. Wizara ya Fedha na Mipango wafanye utaratibu wa kutengeneza miundombinu
itayowezesha watu wenye ulemavu kupata fursa ya kuingia na kufurahia huduma
zitakazotolewa na Benki hiyo.
3. Wizara ihakikishe Mjenzi anakamilishiwa malipo yake haraka iwezekanavyo.
4. Wizara ihakikishe inaziba vyuma vinavyosaidia mtu anapopanda au kushuka ngazi
ili watoto wasiweze kupenyeza miguu yao na kuwahatarishia maisha yao.
5. PBZ iwe makini kumsimamia mjenzi ili aezeke bati kwa umakini wa hali ya juu
kwa vile kuna nyumba nyingi zilizoezekwa kwa mabati kama hayo (Danida)
zinavuja.
2.5 BODI YA RUFAA ZA KODI ZANZIBAR
Bodi ya Rufaa za Kodi Zanzibar ni chombo cha Serikali kilichoundwa na Sheria Nam. 1 ya
mwaka 2006 ikiwa na lengo la kusikiliza kesi za madai ya walipaji kodi ambao
hawakuridhishwa na maamuzi yaliyofanywa na Taasisi za kodi (TRA na ZRB). Bodi hii
ina jumla ya wajumbe wanne ambao wanateuliwa na Waziri wa Fedha na Mipango
pamoja na Mrajis anaeteuliwa na Jaji Mkuu.
Chanzo kikuu cha malalamiko hayo ni Taasisi za kodi kutozingatia ipasavyo taratibu za
ulipaji kodi kwa mujibu wa Sheria au pande mbili kushindwa kukubaliana na makadirio
ya kodi (Tax assessment) yaliyofanywa na Taasisi ya Kodi. Bodi hio ina hadhi ya
Mahakama ya Mkoa (Quasi judicial) ambapo Mrajis wake ni Hakimu wa Mahakama ya
Mkoa.
Kiutendaji, Bodi imeanza rasmi kutekeleza majukumu yake mwaka 2013 (2010 - 2012
hapakuwa na shauri lililowasilishwa mbele ya Bodi). Hadi Kamati ilipoitembelea Bodi
hiyo ilikuwa na jumla ya mashauri 10 ambapo mashauri 6 yaliwasilishwa na ‘Zanzibar
Telecom Limited’ (Zantel) dhidi ya TRA. Bodi tayari imeshatoa uamuzi wa shauri moja
linalowahusu Zan Tours Limited dhidi ya ZRB kwa kukubaliana kuliondoa shauri hilo
katika Bodi.
Kamati imeshangazwa na hali iliyopo kwamba Bodi hiyo bado haijitegemei moja kwa
moja badala yake inapata bajeti yake kupitia Wizara ya Fedha na Mipango, suala hili
linazorotesha utendaji wa Bodi hiyo kwa vile hushindwa kutoa maamuzi yanayofaa kwa
wakati kwani baadhi ya muda hulazimika kutembelea maeneo ambayo wao wanaona
yatawasaidia katika kuharakisha kutoa maamuzi lakini wanashindwa kutokana na
upungufu wa fedha.
Ripoti ya Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo inayotokana na ufuatiliaji utekelezaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Biashara na Viwanda pamoja na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2018/2019. 8
CHANGAMOTO
1. Kutojitegemea kikamilifu kwa Bodi ya Rufaa za Kodi ni changamoto sugu
inayokwamisha utendaji wa Bodi hiyo kwani inategemea kupata fedha za
uendeshaji kutoka Wizara ya Fedha na Mipango.
2. Ukosefu wa Afisi ya uhakika ya kuendeshea shughuli zao.
3. Kushindwa kukaa pamoja kwa Mlalamikaji na Mlalamikiwa kupitia vielelezo vya
makadirio ya kodi katika kipindi ambacho Mlalamikaji anapinga makadirio hayo
katika Taasisi husika. Kinachofanyika Taasisi (hususan ZRB) huwa wanachukua
vielelezo Ofisini kwa hatua ya maamuzi bila ya kumshirikisha Mlalamikaji.
4. Kutokuwepo kwa Maofisa husika wakati kesi inapoletwa mbele ya Bodi
isipokuwa huwa wanakuwepo wanasheria tu. Hili hutokezea katika kesi
zinazoihusu ZRB.
5. Bodi kutokuwa na uwezo wa kufuatilia katika maeneo husika ili kujiridhisha kati
ya maelezo yanayotolewa na vielelezo husika. Mfano kwenda Ofisi za Uhamiaji
Uwanja wa ndege au katika Ofisi za Watembeza Watalii kuhakiki wageni
waliopita kuelekea Hoteli inayolalamikiwa ili kupata picha kwa kiasi gani Hoteli
hiyo imeingiza kipato na kushindwa kulipa makadirio yaliyopangwa.
6. Mianya iliopo kwenye sekta za ukusanyaji wa kodi hupelekea mrundikano wa kesi
kwenye Bodi hiyo.
7. Kuwepo kwa kesi nyingi zisizokua na msingi ambazo hutokana na
wafanyabiashara wasio waaminifu kukwepa kodi na wanapobainika hukwazana
na taasisi za kodi na hatimaye kufungua kesi ya rufaa za kodi.
8. Baadhi ya wakusanya kodi hukosa uadilifu kwenye kazi zao jambo ambalo
linaikosesha mapato nchi yetu.
MAONI, USHAURI NA MAAGIZO YA KAMATI
1. Wizara ichukue hatua zifaazo kuhakikisha Bodi hiyo inakuwa ni chombo
kinachojitegemea kikamilifu ikiwemo kupatiwa Ofisi na kutengewa fedha za
kutosha kama zilivyo Bodi nyengine.
2. Taasisi za Kodi zikae pamoja na Walalamikaji wao wanaoweka pingamizi ya
makadirio ya Kodi waliyopatiwa ili kutatua tofauti iliyopo baina yao na
kupunguza idadi ya kesi zitakazopelekwa katika Bodi.
3. Wizara iitake ZRB ipeleke Maofisa wanaohusika na lalamiko na sio kuwaachia
wanasheria pekee wakati lalamiko linapofikishwa katika Bodi ili iwe rahisi kufikia
maamuzi.
4. Wizara ihakikishe kwamba inaiwezesha ipasavyo Bodi ili iweze kuyatembelea
maeneo ambayo yatawasaidia katika kuharakisha kutoa maamuzi.
5. Taasisi za kukusanya Kodi zihakikishe zinafuata utaratibu kikamilifu ili kupunguza
pingamizi na malalamiko ya Kodi yanayowasilishwa katika Bodi.
Ripoti ya Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo inayotokana na ufuatiliaji utekelezaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Biashara na Viwanda pamoja na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2018/2019. 9
6. Watendaji wa taasisi za ukusanyaji wa kodi wawe waadilifu na wasikubali
kurubuniwa na wajanja wachache wenye nia ya kukwepa kodi.
7. Kamati inaitaka ZRB kuimarisha mfumo wake wa makadirio ya walipa kodi
(assessment) ili kupunguza wimbi la malalamiko na kesi za rufaa za kodi
zinazowakabili.
2.6 BODI YA RUFAANI ZA KODI YA TANZANIA BARA
Kamati ilifanya ziara ya kubadilishana uzoefu katika Bodi ya Rufaani za Kodi pamoja na
Baraza la kodi Tanzania Bara mara baada ya kupata maelezo kutoka Bodi ya Rufaa za
Kodi Zanzibar. Vyombo hivyo vimeundwa kwa ajili ya kuweka usawa kati ya
wafanyabiashara na Taasisi za kodi nchini. Miongoni mwa kazi zinazofanywa na
vyombo hivyo ni kusikiliza na kutoa hukumu ya rufaa za kodi ambapo upande
usioridhika na uamuzi uliotolewa na Bodi utakata rufaa kwenye Baraza la kodi. Upande
usioridhika na maamuzi yaliyotolewa na Baraza utakata rufaa Mahakama ya Rufaa ya
Tanzania kwani hukumu inayotolewa na Baraza hilo ni sawa na hukumu ya Mahakama
Kuu. Aidha, vyombo hivyo hutoa ushauri kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania pamoja na
uelewa kwa wananchi kuhusu masuala ya kodi.
Bodi ina wajumbe kumi na mbili ambao wanaongozwa na Mwenyekiti akisaidiana na
Makamo Wenyeviti watatu ambapo mmoja kati ya hao lazima atoke Zanzibar.
Lakushangaza, muda mrefu umepita Bodi haijawahi kupata Makamo Mwenyekiti kutoka
Zanzibar kwa vile chombo kinachosikiliza na kutoa maamuzi ya kesi zinazotoka taasisi za
kodi (Bodi ya Mapato Zanzibar na Mamlaka ya Mapato Tanzania) kipo Zanzibar. Kwa
upande wa Baraza, linatakiwa kuwa na wajumbe wasiopungua kumi na mbili.
Mwenyekiti wake ni lazima awe na sifa za kuwa Jaji pamoja na Makamo Wenyeviti
watatu ambao watateuliwa na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania mmoja wapo
akitokea upande wa Zanzibar ambaye atateuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania akishirikiana na Rais wa Zanzibar.
Vyombo hivyo vinaongozwa na sheria inayoitwa: Tax Revenue Appeal Act, Cap 408.
Mwaka 2015, Baraza la Kodi lina Mwenyekiti lakini nafasi za Makamo Wenyeviti bado
hazijajazwa. Kimsingi, hali hiyo inatokana na mgongano wa kisheria kati ya sheria ya
Tanzania Bara na ile ya Zanzibar Namba Nam. 1 ya mwaka 2006. Aidha, kuna baadhi ya
kesi walizowahi kuzitolea uamuzi ikiwemo kesi ya Zantel ikaelezwa kwamba Bodi haina
uwezo wa kutoa maamuzi. Mbali na hayo, kuna utofauti wa uwezo wa mamlaka
kuamua kesi kwa vile Baraza (Tribunal) inahadhi ya kuwa sawa na Mahakama kuu ya
Zanzibar.
Ripoti ya Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo inayotokana na ufuatiliaji utekelezaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Biashara na Viwanda pamoja na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2018/2019. 10
CHANGAMOTO
1. Kuna mgongano wa kisheria unasababisha Bodi kushindwa kufikia malengo yake.
2. Bado Makamo Mwenyekiti kutoka Zanzibar hajateuliwa kushiriki katika shughuli
za Baraza.
3. Inaonekana hakuna mashirikiano ya dhati kati ya vyombo hivyo viliopo Tanzania
Bara na Zanzibar.
MAONI, USHAURI NA MAAGIZO YA KAMATI
1. Kuna haja Bodi zote mbili za rufaa ya kodi kukaa pamoja kujadili utofauti uliopo
hususan wa kisheria na kiutendaji.
2. Kamati inashauri kuanzishwa mashirikiano ya kiutendaji baina ya bodi hizo kwa
lengo la kuiletea tija nchi zetu.
2.7 PROGRAMU KUU YA USIMAMIZI NA UWEKEZAJI WA MALI ZA UMMA
Programu hiyo imekusudia kusimamia mitaji ya umma ili kuhakikisha inakwenda
sambamba na mabadiliko ya kiuchumi pamoja na kuwepo kwa uwazi na usawa wa
tathmini ya bidhaa zinazonunuliwa katika taratibu za manunuzi. Utekelezaji wa
Programu hiyo unafanywa na Mamlaka ya kukuza uwekazaji Zanzibar, Idara ya Mitaji ya
Umma, Mamlaka ya Manunuzi na Uondoshaji wa Mali za Umma na Idara ya Uhakiki
Mali. Miongoni mwa mambo ambayo yamefuatiliwa na Kamati ni:
2.8 MAMLAKA YA KUKUZA UWEKEZAJI ZANZIBAR (ZIPA)
Katika miaka ya 1980, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ilifanya maamuzi ya kubadilisha
mfumo wa uchumi kwa kuzishirikisha kikamilifu Sekta binafsi katika kuuendeleza uchumi
wa nchi (engine of growth). Katika kulisimamia hilo, Serikali iliunda vyombo tofauti
ikiwemo Kituo cha Uwekezaji Zanzibar (ZIC), Mamlaka ya Maeneo huru, Bandari huru,
Mamlaka ya Uwekezaji Vitega Uchumi na hatimae hivi karibuni kumeundwa Mamlaka
ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA). Hii ni Mamlaka inayojitegemea iliyopo chini ya
usimamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango.
Hiki ndicho chombo kikuu Zanzibar chenye uwezo wa kutoa ruhusa na ithibati ya
uwekezaji kwa Mtanzania au Mgeni kuwekeza katika maeneo ya Zanzibar. Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar kwa makusudi iliamua kuunda chombo hiki kwa kutambua
umuhimu wa sekta binafsi kutoka ndani na nje ya nchi kujitokeza kuwekeza na kuchangia
katika maendeleo ya kiuchumi ya nchi yetu hususan katika masuala ya hoteli, ujenzi wa
maeneo ya kufurahishia watoto na ujenzi wa nyumba za kisasa za makaazi. Kwasasa,
ZIPA imefanikiwa kuunda Kituo cha Uwekezaji (one stop centre) ndani ya Ofisi yake
iliyopo Maruhubi ambapo Maofisa wengi wa taasisi za Serikali wanafanya kazi zao katika
Ofisi hiyo ili kuwarahisishia wawekezaji kuanza Miradi waliyoikusudia kuitekeleza ndani
ya siku tatu iwapo amekamilisha taratibu zote zinazohitajika. Ni ukweli usiofichika kuwa
kukamilika kwa kituo cha huduma kwa wawekezaji kutasaidia sana kuondoa urasimu
ambao wawekezaji walikuwa wanakumbana nao.
Ripoti ya Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo inayotokana na ufuatiliaji utekelezaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Biashara na Viwanda pamoja na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2018/2019. 11
Kamati ya Fedha, Bisahara na Kilimo kwa pamoja imesikitishwa sana na hali ya
uwekezaji katika Kisiwa cha Pemba ambayo haitowi hata matumaini kwa wawekezaji
kuvutika na kuamua kuweka mitaji yao kwa lengo la kutoa huduma lakini pia kupata
faida ya kile walichowekeza. Hili limegunduliwa na Kamati baada ya kuarifiwa kwamba
baadhi ya wawekezaji wanaondoka nchini hususan wakati wa kiangazi kutokana na
ukosefu wa maji Mahotelini.
Sambamba na hayo, maeneo huru ya Micheweni ambayo yametengwa maalum kwa
uwekezaji Pemba yana mipango mingi iliyomo vitabuni lakini hakuna mwendelezo
(improvement) wowote uliofanywa katika maeneo hayo kutokana na ukosefu wa
miundombinu ya barabara, maji safi na salama, umeme na bandari itakayowawezesha
wawekezali kuingiza malighafi kwa urahisi nchini.
Afisi Kuu ya ZIPA Pemba imekagua miradi 13 ya hoteli ambapo miradi sita inaendelea
kutoa huduma (imekamilika), miradi sita iko kwenye hatua ya ujenzi na mradi mmoja
mpya umefanyiwa ukaguzi wa awali. Kwa upande wa uendelezaji wa maeneo huru ya
Micheweni, Mamlaka imelipima eneo lenye urefu wa 3.7 km ambalo linatarajiwa
kujengwa barabara kwa kiwango cha fusi na inajiandaa na zoezi la ulipaji wa fidia kwa
wananchi watakaoathirika na ujenzi wa barabara hiyo.
CHANGAMOTO
1. Mapato yanayokusanywa yameonekana kuwa ni kidogo sana ukilinganisha na
idadi ya miradi ya uwekezaji iliyopo.
2. Kutoshirikishwa ipasavyo kwa ZIPA wakati wa uanzishwaji wa baadhi ya miradi
ya uwekezaji, jambo ambalo huiweka ZIPA kwenye wakati mgumu pale
wanapohusishwa kwenye utatuzi wa migogoro ya miradi hiyo.
3. Kukosekana kwa Miradi ya Uwekezaji katika Viwanda vya kusarifu, kusindika
mazao ya kilimo yakiwemo mwani, Machungwa, embe na tungule ambayo ndio
yanayoendana na mazingira tuliyonayo Zanzibar.
4. Wizara ya Ardhi haijayatambua maeneo ya Wawekezaji na kuikabidhi ZIPA kama
walivyoelekezwa na Serikali na kudai kwamba wanasubiri ‘Master plan’ ya
maeneo yote ya nchi nzima ikamilike wakati maeneo ya uwekezaji yanajulikana.
5. Kukataliwa kupatiwa eneo na Idara ya Misitu kwa ajili ya Muwekezaji kujenga
Hoteli (Vault) huko katika Msitu wa Kiuyu Mbuyuni, Pemba.
6. Baadhi ya wenyeji wasiopenda maendeleo ya nchi yetu hufanya udangavyifu wa
kuomba eneo la kuwekeza kutoka ZIPA na kulipa gharama ndogo anazotakiwa
Mzawa lakini baadae huwauzia Wageni.
7. Baadhi ya watendaji katika Taasisi za Serikali wanakuwa wazito kutekeleza wajibu
wao kwenye masuala ya uwekezaji nchini na kupelekea kuchelewa au
Ripoti ya Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo inayotokana na ufuatiliaji utekelezaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Biashara na Viwanda pamoja na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2018/2019. 12
kutotekelezwa kabisa kwa baadhi ya miradi au mwekezaji kuamua kuondoka
nchini na kuwekeza kwengine.
8. Kutopewa na Serikali asilimia 100 ya ruzuku ya mishahara na matumizi mengine
kwa ZIPA ambapo kwa sasa wanapatiwa asilimia 80.
9. Kutokuwepo kwa kiwanja cha Ofisi ya Baraza la Wawakilishi, ZIPA inasema hilo
sio eneo la uwekezaji isipokuwa ni eneo la wananchi wa Fumba kama ilivyokuwa
kabla ya “Master Plan” ya mwanzo. Kwa hivyo, jukumu la kutoa maeneo kama
hayo lipo Wizara ya Ardhi, ingawa “Master Plan” yote ya Fumba wahusika wakuu
ni ZIPA.
10. Maslahi duni kwa watendaji wa ZIPA ambao wanafanya kazi na wawekezaji
ambao ni watu wenye fedha za kutosha.
11. Mshahara mdogo anaolipwa Mkurugenzi Mtendaji wa ZIPA kwani analipwa
mshahara uliosawa na Mkurugenzi wa kawaida tofauti na wadhifa na cheo chake.
12. Kukwama kwa Miradi ya Uvuvi kunakosababishwa na Idara ya Uvuvi yenyewe
kukosa kutoa mashirikiano kwa ZIPA.
13. Ucheleweshwaji wa vibali vya ukodishwaji ardhi (Land Lease) kwa wawekezaji
wenye nia ya kuwekeza nchini unapelekea baadhi yao kuvunjika moyo na kukosa
hamu ya kuendeleza miradi yao.
14. Upungufu wa watendaji wa Mamlaka kwa upande wa Pemba. Mamlaka ina jumla
ya watendaji 8 ambapo kati yao wawili wako masomoni na watatu ni walinzi
katika Afisi na maeneo huru ya Micheweni.
15. Uhaba wa fedha za kuitangaza ipasavyo Zanzibar kuwa ni eneo zuri la kuwekeza.
16. Ukosefu wa Afisi kuu ya kudumu kwa upande wa Pemba ambapo watendaji
hufanya shughuli zao kwenye mazingira yasiyoridhisha.
17. Ukosefu wa elimu juu ya faida za uwekezaji kwa vijana waliopo Pemba hususan
maeneo ya vijijini unawafanya vijana hao kuchukia uwekezaji nchini na hivyo
kushindwa kutumia fursa za ajira zinazotokana na uwekezaji katika maeneo yao.
MAONI, USHAURI NA MAAGIZO YA KAMATI
1. Kamati inaishauri ZIPA kuchukua juhudi za makusudi kuhakikisha mapato
wanayokusanya yanaongezeka.
2. Wizara ya Fedha na Mipango ishirikiane na Wizara husika kuhakikisha kwamba
kabla Mradi haujaanza kutekelezwa ni lazima upitie ZIPA kama inavyoelekezwa
na sheria ya Uwekezaji nchini.
3. ZIPA iongeze juhudi katika kuhamasisha wawekezaji wa viwanda vya kusindika
matunda.
4. Wizara ya Fedha na Mipango ikae na Wizara inayoshughulikia Ardhi kumaliza
changamoto ya kutotambuliwa kwa maeneo ya uwekezaji nchini.
Ripoti ya Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo inayotokana na ufuatiliaji utekelezaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Biashara na Viwanda pamoja na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2018/2019. 13
5. Kamati inaitaka Wizara kukaa na Wizara inayoshughulikia Kilimo ili kutatua
changamoto ya kutokubaliwa kwa Mwekezaji wa Mradi wa kujenga Hoteli
(Vault) kwa kuzingatia kwamba Mradi huo usiharibu maliasili na mazingira ya
msitu ulipo.
6. Kamati inaitaka Wizara kukaa na Wizara ya Utumishi wa Umma kushughulikia
suala la “Scheme of Service” ya ZIPA ambayo wameiandaa kwa muda mrefu bila
ya kushughulikiwa.
7. ZIPA ifanye ufuatiliaji na tathmini ya Miradi iliyoruhusiwa ili kuchunguza kama
hakuna udanganyifu uliofanyika na kupatiwa kibali cha uwekezaji mwenyeji kwa
bei ya chini na baadae kumuuzia Mgeni.
8. Kamati inaitaka Wizara kuwachukulia hatua zinazostahiki wale wote
watakaogundulika kufanya udanganyifu na kuwauzia maeneo wawekezaji wageni
kinyume na taratibu.
9. Wizara ya Fedha na Mipango ikae na Wizara inayoshughulikia Ardhi ili
kuhakikisha Mpango wa Matumizi ya Ardhi katika eneo la Makaazi ya watu
Fumba unakwamuka ili kuweka mazingira mazuri kwenye upande wa uwekezaji.
10. Wizara iwapatiye ZIPA asilimia 100 ya ruzuku ya mishahara na matumizi mengine
badala ya asilimia 80 inayotolewa hivi sasa ili waweze kuijipanga na kutekeleza
majukumu yao ipasavyo.
11. Kamati inashauri Wizara ya Fedha na Mipango ihakikishe inakutana na Wizara
inayoshughulikia Utumishi wa Umma kuyapitia upya maslahi ya Mkurugenzi
Mtendaji wa ZIPA ili aweze kuwa tofauti na mshahara wa Wakurugenzi wengine.
12. Wizara ya Fedha na Mipango ihakikishe inakutana na Wizara inayoshughulikia
Kilimo kutatua changamoto ya kukwama kwa Miradi ya Uvuvi.
13. Wizara ihakikishe inaanzisha kituo cha huduma kwa wawekezaji “One Stop
Center” kwa upande wa Pemba ili iwaondolee usumbufu wawekezaji wanaohitaji
kuwekeza kisiwani humo.
14. Kamati inapendekeza kuongezwa watendaji wa ZIPA kisiwani Pemba ili waweze
kukidhi mahitaji ya utendaji wenye ufanisi mkubwa.
15. Kamati inashauri Serikali kuitengea ZIPA fungu maalum kwa ajili ya kuitangaza
Zanzibar ndani na nje ya nchi.
16. Kamati inaitaka Wizara ya Fedha na Mipango ikutane na Wizara inayoshughulikia
Ardhi kushauriana na hatimae kuipatia Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar
Mpango Mkuu “Master Plan” ya Uwekezaji kwa ajili ya kuifanyia kazi.
Ripoti ya Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo inayotokana na ufuatiliaji utekelezaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Biashara na Viwanda pamoja na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2018/2019. 14
2.9 MRADI WA “MPAPINDI HOLIDAY AND DIVING COMPANY LIMITED”
Mradi huu uliopo kwenye kijiji cha Makangale, Wilaya ya Micheweni, Mkoa wa
Kaskazini Pemba, ulithibitishwa na Mamlaka ya Ukuzaji Vitega Uchumi Zanzibar (ZIPA),
ulisajiliwa na kupewa hati ya ukodishwaji wa Ardhi (land lease) mwaka 2004 ukiwa chini
ya umiliki wa raia wawili wa kigeni wa Afrika Kusini Bwana Marek Kloryga na Mkewe
wenye hisa sawa za umiliki.
Mwekezaji alipewa cheti cha ruhusa ya ujenzi wa vibanda vya kulaza wageni mwaka
2005 na shughuli za ujenzi wa mradi huo zilianza rasmi katika mwezi wa Septemba,
2006. Mwaka 2007, shughuli za ujenzi wa mradi huo zilisita kutokana na kuishiwa mtaji
na kuamua kuingia ubia na Bwana Ray Champion. Haikuchukua muda, wabia hao
walipelekana Mahakamani kutokana na mbia mmoja (Ray Champion) kulitangaza eneo
hilo kuwa lake na anataka kulikabidhisha kwa mtu mwengine.
Mwekezaji aliomba kubadilishiwa hati ya ukodishwaji ardhi kutoka jina la “Mpapindi
Holiday and Diving Company Ltd.” na kuwa “Pemba Sports Fishing Club” ili aepukane
na changamoto zilizomkabili hapo awali na kuingia kwenye kesi iliyodumu kwa zaidi ya
miaka saba.
Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo imesikitishwa na taarifa ya upotevu wa ramani ya
eneo la mradi huo jambo ambalo limeitia aibu kubwa kwa nchi yetu. Kitendo hicho
kimewaweka njia panda wawekezaji hao kwa kushindwa kuingia kwenye mkataba wa
matumizi ya ardhi kwa muda wa miaka 30 na kupelekea kuikosesha nchi yetu fedha za
kigeni.
CHANGAMOTO
1. Mradi kukabiliwa na kesi Mahakamani katika kipindi cha awali cha uanzishwaji
wake jambo lililositisha uendelezaji wa mradi huo na kuchukua muda mrefu hadi
kumalizika kwa kesi hiyo mwaka 2016.
2. Uchelewaji wa upatikanaji wa hati ya ubadilishaji wa jina la mradi ambayo
Mwekezaji ameiomba kwa Bodi ya Uhaulishaji Ardhi Zanzibar kwa muda wa
mwaka mzima ni suala jengine linalokwamisha mradi huu.
3. Kuwepo kwa migogoro ya mara kwa mara ya kujitokeza watu wanaodai umiliki
wa sehemu ya eneo hilo.
4. Ukatwaji wa miti hususan muda wa usiku hupelekea kuathiri msitu wa maumbile
uliopo katika eneo hilo.
5. Sura ya udanganyifu na ubabaishaji wa mwekezaji.
Ripoti ya Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo inayotokana na ufuatiliaji utekelezaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Biashara na Viwanda pamoja na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2018/2019. 15
MAONI, USHAURI NA MAAGIZO YA KAMATI
1. Kamati inaitaka Wizara ya Fedha na Mipango kufanya kikao cha dharura baina
yake na Wizara inayohusika na Ardhi na Taasisi zote zinazohusika ili kutatua
changamoto zilizopo.
2. Serikali ifuate ipasavyo vigezo ilivyojiwekea kisheria kwa ajili ya uwekezaji
unaofaa nchini.
3. Kamati inaitaka Mamlaka inayohusika kutayarisha ramani nyengine ya eneo hilo
haraka iwezekanavyo ili hatua za mradi huo ziendelee na wananchi wapate
manufaa yaliyokusudiwa.
4. ZIPA iwe makini inaposhughulikia maombi ya uwekezaji na kujiridhisha na
mwekezaji husika kabla ya kuuthibitisha mradi huo.
2.10 UTEKELEZAJI KWA TAASISI ZINAZOJITEGEMEA
2.10.1 BODI YA MAPATO ZANZIBAR (ZRB)
Bodi ya Mapato Zanzibar ilianzishwa mwaka 1996 na kuanza kazi rasmi mwaka 1998.
Hiki ndio chombo kikuu Zanzibar na ni roho ya Serikali katika ukusanyaji mapato kupitia
ongezeko la thamani yaani ‘VAT’, kodi ya zuio la biashara (excise duty), kodi ya Hoteli
na kodi nyengine za ndani. Kwa kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2018/2019,
taasisi hiyo ilipangiwa kukusanya jumla ya shilingi 103.26 bilioni ambapo hadi kufikia
Disemba 2019, jumla ya shilingi 90.80 bilioni zilikusanywa sawa na asilimia 88 ya
makadirio. Kwasasa Bodi hiyo ina mpango wa kuanzisha mfumo wa ulipaji kodi kwa
kutumia mashine za ‘EFD’ pamoja na kwenda kwenye mfumo wa ‘E-Service’ ambayo
itampa fursa mlipa kodi kulipia kodi yake na kupata huduma papo hapo.
CHANGAMOTO
1. Makusanyo yanayotokana na TRA (excise duty) huwa yanachelewa kuingizwa
katika hesabu ya ZRB.
2. Bado kuna wafanyabiashara ambao hawatowi risiti wakati wa mauziano
yanapofanyika.
3. Kutotumika kwa mashine za EFD kunasababisha mapato mengi kupotea.
4. Kukosekana utaratibu wa kuwapatia wananchi wanye mahitaji ya leseni mbili au
tatu kwa wamiliki wa magari mengi.
5. Ushuru mdogo kwa gari nyingi mbovu ambazo zinaingia Zanzibar hasa za abiria,
taxi na daladala.
6. Bado kuna myanya mingi katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali.
7. Kutokuwepo kwa wataalamu wa kutosha wa ukusanyaji mapato katika ngazi ya
Serikali za Mitaa hususan ukizingatia mfumo wa ugatuzi.
Ripoti ya Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo inayotokana na ufuatiliaji utekelezaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Biashara na Viwanda pamoja na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2018/2019. 16
MAONI, USHAURI NA MAAGIZO YA KAMATI
1. ZRB ichukue juhudi za makusudi kuhakikisha mapato yanatoyotoka na makusanyo
kutoka TRA yanaingia nchini na kuchangia kwenye mfuko mkuu wa Serikali.
2. Serikali iharakishe uwekaji wa mfumo mpya wa utoaji risiti kwa njia za
kielektroniki.
3. ZRB ianzishe utaratibu wa mtu mmoja kuwa na leseni mbili au zaidi. Kufanya
hivyo kutawaepusha wananchi wenye magari zaidi ya moja na kupata usumbufu
wa askari barabarani.
4. ZRB ihakikishe inaongeza Ushuru kwa gari mbovu zinazoingizwa Zanzibar, ili nchi
yetu isiwe jaa la bidhaa mbaovu zikiwemo za magari.
5. Wizara ya Fedha na Mipango ihakikishe inawapatia mafunzo ya kutosha
watendaji wa Serikali za Mitaa juu ya ukusanyaji wa mapato.
6. Wizara ihakikishe inanzisha mfumo wa ulipaji kodi kwa njia ya Mtandao (E-
services).
7. Kamati inasisitiza ZRB kuwapatia mafunzo watendaji wa Bodi ya Mapato
Zanzibar (ZRB) ambao wanahusika moja kwa moja na matumizi ya mashine za
EFD kabla ya kuwasili mashine hizo nchini ili kurahisisha matumizi yake.
8. Wizara kupitia ZRB iandae programu za mafunzo kwa watumiaji wa mashine hizo
(wafanyabiashara) ili kuhakikisha mashine zinatumika ipasavyo na kuongeza pato
la Taifa kama inavyotegemewa.
2.10.2 MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA (TRA)
Mamlaka ya Mapato Tanzania ilianzishwa mwaka 1995 lakini ilianza kazi rasmi mwaka
1996. Mamlaka hiyo inaongozwa na Bodi ya Wakurugenzi ikiwa na majukumu ya msingi
ya kukusanya kodi pamoja na kuishauri Serikali kuhusu masuala ya kodi. Katika
ukusanyaji wa kodi, awali walikuwa wakitumia mfumo wa utoaji mizigo Bandarini wa
‘Ascudo Plus Plus’ lakini mfumo huo ulikuwa na changamoto nyingi kwa vile uliundwa
mahsusi kutumika kwa nchi zisizokuwa na Bahari au Bandari (land locked countries).
Kwa vile Tanzania inazo Bandari kadhaa ambazo zinatumika kupokea mizigo kutoka
sehemu tofauti, mfumo wa Ascudo haukuweza kutoa huduma ipasavyo kwani
iliwalazimu Maofisa wa teknolojia ya habari kufuatilia wao wenyewe mizigo iliyoingia
na kwa vile mizigo huwa mingi husababisha foleni, muda mwingi kupotea na kulikuwa
na mdororo wa utoaji mizigo.
Ili kuondosha changamoto hizo, Mamlaka iliamua kutumia mfumo unaoitwa ‘Tanzania
Customs Intergrated System (Tancis)’ ambao umetengenezwa na Wakorea wakishirikiana
na wataalamu wazalendo katika mifumo yake mingi ya utoaji mizigo Bandarini na katika
baadhi ya maeneo waliedelea kutumia ‘Ascudo Plus Plus’. Aidha, kuna mifumo mingine
imeunganishwa na mfumo wa Tancis ikiwemo mfumo wa usalama ambao unasaidia
mifumo mingine kufanya kazi. Kuwepo kwa mfumo huo, unazisaidia hata mifumo
mingine ya Serikali kupata taarifa kamili za kodi wanapoingia katika mfumo wa Tancis.
Faida kubwa za mfumo huo ni: unaongeza mapato, kupunguza muda na gharam za
usafirishaji biashara; inaongeza uwazi; utaratibu wa malipo ya ukaguzi unakuwa rahisi,
unapunguza wafanyakazi wasiokuwa na ulazimu mkubwa mfano unatoa ripoti
Ripoti ya Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo inayotokana na ufuatiliaji utekelezaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Biashara na Viwanda pamoja na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2018/2019. 17
wenyewe, hivyo hakuna haja ya kuwepo muandikaji ripoti; kawaida mfumo wa Ascudo
hauruhusu kufanya mabadiliko mpaka uombe ridhaa kutoka Ulaya kwa aliyeutengeneza
wakati Tancis baada ya kufanyiwa marekebisho, mfumo hivi sasa unaruhusu marekebisho
kufanywa na Maofisa wa TRA wenyewe.
Tarehe 11 Januaari, 2019 mfumo wa Tancis umeanzishwa rasmi na kutumika Zanzibar.
Mfumo huo umeonesha mafanikio makubwa ikiwemo urahisi na ufanisi katika utekelezaji
wake. Matumizi ya mfumo huo, unawafanya Maofisa wa TRA kuweza kujua ufanisi wa
kazi wa Bandari zote ziliopo Zanzibar na Tanzania kwa ujumla wake wakiwa wapo
Ofisini.
CHANGAMOTO
1. Upungufu wa Wafanyakazi katika Ofisi za TRA hususan wataalamu wa ‘ICT’
wanaotumika kuendesha mfumo wa Tancis.
2. Kukosekana eneo la kutosha la kukagulia na kuhifadhia mizigo inayoteremshwa
kutoka katika meli kupitia kwenye makontena.
3. Kuwepo kwa eneo dogo wanalotumia Maofisa wa TRA Bandarini Zanzibar
kufanyia kazi zao ambalo baadhi ya wakati huwafanya wafanyabiashara
kukusanyika wakisubiri huduma.
4. Matumizi mabaya ya misamaha ya kodi kwa baadhi ya taasisi za dini ambao
huitumia fursa hiyo kwa maslahi binafsi.
5. Kuwepo kwa ujanja wa baadhi ya wafanyabiashara kupunguza makadirio ya
gharama za mizigo kwa nia ya kukwepa kulipa kodi stahiki.
6. Kuwepo kwa wadaiwa sugu wa kodi.
MAONI, USHAURI NA MAAGIZO YA KAMATI
1. Ni busara Wizara ya Fedha na Mipango ikashauriana na Mamlaka ya Mapato
Tanzania kuajiri wafanyakazi wapya ili kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa kodi
Bandarini.
2. Wizara ya Fedha na Mipango ikutane na Shirika la Bandari Zanzibar kuzungumzia
suala la uwezekano wa kutumia Taasisi za Serikali au binafsi kuandaa eneo nje ya
Bandari hiyo kwa lengo la kuweka makontena.
3. TRA inalazimika kufuatilia kwa umakini mkubwa misamaha yote ya kodi
inayotolewa ili kujiridhisha inatumika kama masharti yake yanavyoelekeza.
4. TRA iendelee kutafuta njia mbadala za kuwashughulikia wanaokwepa kulipa
ushuru pamoja na wadaiwa sugu.
2.10.3 BENKI YA WATU WA ZANZIBAR (PBZ) - MTAA WA LUMUMBA, DSM
Tawi la PBZ Lumumba ni moja katika ya matawi matatu yaliopo Jijini Dar es Salaam.
Matawi mengine yapo TAZARA na Kariakoo. Matawi yote hayo yana jumla ya
wafanyakazi 51 wa kudumu lakini pia wanao wafanyakazi wa Mkataba. Matawi hayo
yanafanya kazi katika majengo ya kukodi ambapo zaidi ya shillingi milioni 900 hutumika
kwa mwaka kwa ajili ya kulipia gharama za kodi ya majengo hayo. Mpango uliopo ni
kufungua tawi jengine katika mji wa Dodoma ifikapo Juni, 2019.
Ripoti ya Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo inayotokana na ufuatiliaji utekelezaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Biashara na Viwanda pamoja na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2018/2019. 18
Kamati inaipongeza Benki ya Watu wa Zanzibar kwa juhudi wanazozichukua katika
utekelezaji wa majukumu yao hususan kwa kufanikiwa kuweka mfumo mpya na
wakisasa unaoweza kwenda sambamba na ushindani wa soko la ndani na nje ya
Zanzibar. Kuwepo kwa mfumo huo, kutaiwezesha PBZ kumudu kutoa huduma za “Visa”
na “Master card” kwa wateja wake, kuruhusu matumizi ya kibenki mtandaooni
“Internet Banking System” na kuongeza wigo wa kuwa na wateja wengi na mawakala
wa benki. licha ya mafanikio hayo, Kamati bado haijaridhishwa na ufanisi wa huduma
zinazopatikana kupitia “ATM mechine” kwani wateja wanaendelea kulalamika kwa
kukosekana fedha katika mashine hizo, kuwepo kwa fedha ndogo ndogo tupu na
huharibika mara kwa mara.
CHANGAMOTO
1. Matawi ya PBZ Dar es salaam ni machache sana.
2. Bado PBZ haijafanikiwa kuwavutia wafanyakazi wengine kufungua ‘account’
katika benki hiyo hususan katika kambi za jeshi.
3. PBZ haijafungua Matawi mengine katika maeneo ya Arusha na Mwanza.
4. PBZ bado haijajitangaza ipasavyo ndani na nje ya nchi.
MAONI, USHAURI NA MAAGIZO YA KAMATI
1. PBZ ichukue juhudi za makusudi kufungua matawi mengine Dar - es Salaam.
2. PBZ ihakikishe inaweka vivutio vya kutosha ili wafanyakazi wa Wizara tofauti za
Muungano ziweze kufungua ‘account’ katika benki hiyo.
3. PBZ ifungue Matawi mengine katika maeneo ya Arusha na Mwanza.
4. Ili kuimarisha utendaji na kuongeza wateja zaidi, PBZ ijitangaze ndani na nje ya hi.
2.10.4 MFUKO WA HIFADHI YA JAMII (ZSSF)
Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (ZSSF) ni Taasisi ya SMZ iliyoundwa kwa sheria Nam. 2 ya
mwaka 1998 kwa lengo kuu la kuwahifadhi wanachama waliostaafu kwa mujibu wa
sheria na wanapopatwa na majanga ambayo husitisha au kupunguza kipato chao
kutokana na sababu mbali mbali kama vile , ulemavu, maradhi au kifo. Mfuko pia
huongeza wigo kwa kukusanya michango mbali mbali kutoka kwa wanachama wake
(Taasisi za Serikali na Binafsi) ili michango hiyo iweze kuwasaidia wanachama hao baada
ya kumaliza utumishi wao. Katika kuhakikisha Mfuko huo unakuwa endelevu, ZSSF
hutumia michango hiyo kuiwekeza kwenye miradi tofauti ili iweze kuzalisha faida.
ZSSF ina miradi mbalimbali ambayo imewekeza kwa ajili ya uendelezaji wa mfuko.
Miongoni mwa Miradi hiyo ni ujenzi wa nyumba za kisasa za Makaazi ziliopo Mbweni
wenye ukubwa wa eneo la mita za Mraba 55,000 kwa ajili ya wananchi wa kipato cha
kati. Mradi huo umeanza mwaka 2015 na kutarajiwa kumaliza mwaka 2018 ambao
unasimamiwa na Kampuni ya Habconsult Ltd. ya Dar es Salaam na mjenzi wake ni
Kampuni ya Dezo Civil Contractor ya Dar es Salaam. Mradi huo umepanga kujenga
Ripoti ya Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo inayotokana na ufuatiliaji utekelezaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Biashara na Viwanda pamoja na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2018/2019. 19
jumla ya majengo 18 yenye ghorofa saba kila moja ambazo zinatarajiwa kuwa na
vyumba 253 kwa nyumba za kati ya vyumba viwili, vitatu na vinne kwa gharama ya
shilingi 43.7 bilioni. Nyumba hizo ni za biashara ambazo zitanunuliwa kwa fedha taslim
au malipo ya kodi kwa nia ya kumiliki au kupitia mkopo wa Benki. Ujenzi wa majengo
matano ya awamu ya kwanza unakamilishwa ikiwa ni pamoja na kukabidhiwa wateja
nyumba zao.
Hadi Kamati ilipotembelea mfuko huo mwezi wa Agosti 2018, jumla ya Tsh. 16.41 bilioni
zimeshatumika kutekeleza ujenzi huo na Tsh. 839 milioni
zimeshalipwa na wananchi tofauti kwa ununuzi wa nyumba 20. Aidha, Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar imeonesha nia ya kununua majengo matano; moja la vyumba vinne,
moja la vyumba vitatu na matatu ya vyumba vitatu wakati Benki Kuu ya Tanzania (BOT)
ilitarajiwa kusaini mkataba wa jengo moja la vyumba vitatu. Gharama za nyumba hizo ni
Tsh. 168.82 milioni kwa nyumba yenye vyumba viwili, Tsh. 190.84 milioni kwa nyumba
yenye vyumba vitatu na Tsh. 249.56 milioni kwa nyumba ya vyumba vinne.
Kimsingi, Kamati haikuridhishwa na kiwango cha ujenzi wa nyumba hizo kwani vifaa
vilivyotumika ni vya kiwango cha chini haviendani na gharama halisi za mradi huo.
Kadhalika, ujenzi huo haukulenga kumsaidia mwananchi wa kipato cha chini na cha kati
kumudu gharama za ununuzi wa nyumba hizo kwani Kamati imegundua kuwa
mwananchi wa kipato cha kati atalazimika kutumia muda mwingi hadi atafikia katika
kiinua mgongo ili kulipia gharama za nyumba ya vyumba viwili. Kwa mantiki hiyo,
mradi haukukidhi azma ya Marehemu Mzee Abeid Aman Karume, Rais wa Kwanza wa
Zanzibar ya kuwapatia makaazi bora wakwezi na wakulima, ikizingatiwa kwamba mradi
huo unaendeshwa kwa michango yao lakini huwanufaisha wananchi wa kipato cha juu.
Kupitia Programu Kuu ya kutoa hifadhi ya jamii, ZSSF imeanza kuendeleza ujenzi wa
jengo la kibiashara la Michenzani Makontenani. Aidha, mradi wa ujenzi wa nyumba za
kisasa za Kwahani umeanza na Serikali tayari imeshakubaliana na Kampuni za CCECC na
LINGHANG GROUP kutekeleza mradi huo.
CHANGAMOTO
1. Kuna uwezekano mkubwa wa Mkandarasi kushindwa kukamilisha nyumba hizo
ndani ya wakati.
2. Kushindwa kukabidhi hati ya umiliki wa nyumba hizo kwa watu
waliokwishakamilisha malipo kutokana na Bodi ya ‘Condominium’ kushindwa
kukutana.
3. Kutokuwepo eneo la kutosha la kuegesha gari katika mradi huo lenye kukidhi
haja ya watu watakaotarajiwa kukaa katika nyumba hizo.
Ripoti ya Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo inayotokana na ufuatiliaji utekelezaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Biashara na Viwanda pamoja na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2018/2019. 20
4. Kukosekana kwa vifaa vya kuashiria uwepo wa moto (fire detectors) katika
majengo hayo.
5. Kutopatikana Mkurugenzi Mwendeshaji mara tatu katika ziara za kamati ingawa
ratiba imethibitishwa na afisi yake.
MAONI, USHAURI NA MAAGIZO YA KAMATI
1. ZSSF ihakikishe inajenga majengo bora, ya kisasa na ya bei nafuu ambayo
wananchi wa kawaida wataweza kuzimudu.
2. Kamati inaitaka ZSSF ihakikishe Mkandarasi anakamilisha mradi huo kwa wakati.
3. Wizara kwa kushirikiana na ZSSF ihakikishe wanunuzi wa nyumba za mradi huo
wanapatiwa hati za umiliki wa nyumba hizo mara tu baada ya kukamilisha
malipo.
4. ZSSF ihakikishe inatumia mbinu mbadala itakayowezesha kupatikana kwa eneo la
kutosha la kuegesha magari ili kukidhi haja ya watu wanaotarajiwa kukaa katika
nyumba hizo.
5. ZSSF ihakikishe kunakuwepo kwa vifaa vya kuashiria uwepo wa moto (fire
detectors) katika majengo hayo.
2.10.5 SHIRIKA LA BIMA ZANZIBAR
Shirika la Bima Zanzibar limeanzishwa mwaka Juni, 1969 Chini ya Sheria ya Mitaji ya
Umma Nam. 4 ya 2002 ikiwa na dhima kuu ya kuwarudishia hali waliyokuwa nayo
wateja wao kabla majanga hayajawakumba. Utendaji wa Taasisi hii unasimamiwa na
Mamlaka ya Usimamizi wa Bima ya Tanzania (TIRA).
Kamati inalipongeza Shirika la Bima Zanzibar kwa hatua ya maendeleo iliyofikia ya
kuonesha mfano kwa Mashirika au Taasisi nyengine za Serikali kwa kutawanya matawi
yake hadi kufika Dar - es Salaam, Mwanza, Mbeya, Dodoma na maeneo mengine ya
Tanzania Bara. Shirika limefikia mafanikio hayo kutokana na mashirikiano makubwa kati
yake na Bodi ya Wakurugenzi inayosimamia kazi zake. Kadhalika, Shirika limejenga jengo
lake la kisasa liliopo Mpirani na kulikodisha kwa taasisi mbalimbali zikiwemo Benki ya
Watu wa Zanzibar na Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa (NHIF).
Changamoto kubwa inayolikabili shirika hili ni matumizi makubwa ya fedha za kulipia
gharama za fidia kwa wanachama. Hali hii inazorotesha uimarikaji wa mapato ya Shirika
hilo kwani kuna baadhi ya wanachama huwa wananunua gari zilizokuwa zimeshatumika
na kufanya makisio ya gari mpya au wakiona vyombo vyao vimeshachakaa huvichoma
moto kwa makusudi na kudai malipo. Lakushangaza na kubwa zaidi kuna baadhi ya
vyombo mara tu baada ya kusajiliwa havichukui muda huharibika na kuendelea
kuharibika huku vikidai mrejesho kutoka Shirika.
Ripoti ya Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo inayotokana na ufuatiliaji utekelezaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Biashara na Viwanda pamoja na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2018/2019. 21
CHANGAMOTO
1. Bado Taasisi inatumia majengo ya kukodi tena kwa gharana kubwa huko
Tanzania Bara.
2. Ajali nyingi zinatokea na kusababisha kuongezeka kwa madai kutoka kwa
wanachama.
3. Taasisi imetumia gharama kubwa katika utengenezaji wa Meli ya M.V Mapinduzi
II kwa vile imekatiwa Bima lakini haikukaa muda mrefu ikaharibika bila ya
kufahamika kwa uwazi sababu za msingi za maharibiko hayo. Shirika la Bima la
Zanzibar kwa kushirikiana na taasisi nyengine za bima (co insurer) zimeingia
mkataba na Shirika la Meli kwa ajili ya Bima kwa M.V Mapinduzi II ambapo mara
tu baada ya maharibiko hulazimika kufidia gharama za matengenezo ambazo ni
kubwa mno.
4. Baadhi ya Kampuni za Bima hazilipi fedha za vitabu vilivyojaa na kupatiwa vitabu
vyengine.
5. Baadhi ya Wafanyakazi wa Shirika hilo huwa si waaminifu kwani hutoa siri na
nyaraka za shirika kwa watu wasiostahiki.
6. Kukosekana Bima ya wakulima kwa vipando vyao.
MAONI, USHAURI NA MAAGIZO YA KAMATI
1. Kamati inalishauri Shirika kuwa na mpango wa kununua kiwanja au jengo kwa
ajili ya kulitumia kama Ofisi ya Shirika huko Tanzania Bara na kulikodisha kwa
taasisi nyengine ili kujiongezea mapato.
2. Shirika lishirikiane ipasavyo na Jeshi la Polisi pamoja na Taasisi nyengine ili liweze
kutoa elimu kuhusu umuhimu wa Bima na mbinu bora zitakazotumiwa kukinga
ajali.
3. Kamati inalitaka Shirika kuwa makini na wadanganyifu wanaoweka makadirio ya
gari mpya wakati wa ukataji bima ingawa gari aliloingiza nchini limeshatumika.
4. Kamati inalitaka Shirika kuwafuatilia mawakala wote wasiolipa malimbikizo ya
madeni yao na kukataza kabisa utoaji wa vitabu vya Bima pasi na kulipia kitabu
cha awali alichopewa wakala.
5. Kamati inalishauri Shirika kuwa makini sana wakati wa kuingia mikataba ya Bima
kwani baadhi ya vyombo huwa havichukui muda mrefu vinaharibika na
kulisababishia Shirika kulipa gharama.
6. Shirika liweke adhabu kali na kuzitekeleza kivitendo kwa wale wote
watakaobainika wanatoa siri za Afisi.
7. Kamati inalishauri Shirika kuanzisha Bima maalum kwa ajili wakulima, wafugaji na
wavuvi nchini.
Ripoti ya Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo inayotokana na ufuatiliaji utekelezaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Biashara na Viwanda pamoja na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2018/2019. 22
2.11 PROGRAMU KUU YA USIMAMIZI WA MFUKO MKUU WA SERIKALI
Programu hiyo imekusudia kufanya malipo maalum ya Serikali pamoja na kufanya
malipo ya madeni ya Serikali. Utekelezaji wa Programu hiyo unafanywa na Idara ya
Muhasibu Mkuu wa Serikali.
Kwa kipindi kirefu, Baraza hili lilikuwa likinyanyua sauti ya pamoja kutaka Wizara ya
Fedha na Mipango itekeleze kivitendo utaratibu wa kuwabadilisha Wahasibu (job
rotation) ili kuondosha kuzoeleka katika taasisi zao. Hatua hii ni muhimu kwa kuwalinda
wahasibu na Makampuni, taasisi na watu wenye kipato kikubwa kuwarubuni na kuathiri
utendaji wao. Lakushangaza, zoezi hilo jema limewekewa vikwazo na baadhi ya
Viongozi wa Umma kwa kutumia nafasi zao vibaya na kuwafanya watendaji
wanaohusika kuwa na wasiwasi wa maisha yao.
Kamati inakemia vikali kitendo hicho na kuwataka Viongozi wa umma kuacha tabia hiyo
kwani utekelezaji wa uhamisho huo unafanywa kwa mujibu taratibu za kifedha kwa
lengo la kuimarisha demokrasia katika utendaji. Iwapo desturi kama hizo zitakuwa
zinaendelezwa, ufanisi hautopatikana na kuathiri watendaji wanaochapa kazi kwa
maslahi ya Zanzibar.
Kamati inaupongeza mfuko kwa kutumia jumla ya shilingi 6.87 bilioni kuwalipa pencheni
wastaafu 13,000 kila mwezi. Licha ya mafanikio hayo, Mfuko pia umetumia jumla ya
4.00 bilioni kuwalipa mafao (kiinua mgongo) wananchi ambao wamemaliza utumishi
wao kwa mujibu wa sheria.
CHANGAMOTO
1. Baadhi ya Viongozi kuingilia utendaji wa Mfuko na kuathiri utekelezaji wa
majukumu ya msingi ya mfuko huo.
2. Baadhi ya wakati hutokea wastaafu wetu kuchelewa kupata viinua mgongo vyao.
MAONI, USHAURI NA MAAGIZO YA KAMATI
1. Kamati inawashauri Viongozi wa Umma na watendaji wengine kuacha kuingilia
masuala ya uhamisho wa Wahasibu kwani masuala hayo yanafanywa kwa mujibu
wa taratibu zinavyoelekeza.
2. Kamati inaishauri Wizara kulishughulikia ipasavyo na kwa wakati suala la malipo
ya kiinua mgongo na pencheni kwa watumishi wetu mara tu baada ya kustaafu.
Ripoti ya Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo inayotokana na ufuatiliaji utekelezaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Biashara na Viwanda pamoja na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2018/2019. 23
2.12 PROGRAMU KUU YA UTAWALA NA UENDESHAJI WA TUME YA MIPANGO
Kamati inatoa pongezi kwa mradi huu kwa ujenzi wa mitaro ya kupitishia maji machafu
inayojengwa katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo kwa binti Amran, Kwerekwe na
Sebleni. Mwelekeo wa matokeo wa miradi hiyo inaonekana kuleta mafanikio makubwa
kwani wananchi wa Jang’ombe na maeneo ya jirani yamebakia kuwa makavu tofauti na
siku zilizopita ambapo katika kipindi cha mvua za masika au vuli, wananchi wetu
huamua kuhama kutokana na kuingiliwa na maji ya mvua.
Kwa vile Tume ndio chombo kikuu cha kuratibu utekelezaji wa ZUSP, Kamati inatoa
pongezi kwa mradi wa ujenzi wa mitaro ya kupitishia maji machafu inayojengwa katika
maeneo mbalimbali nchini ikiwemo kwa binti Amran, Mwanakwerekwe na Sebleni.
Mradi huo umeleta mafanikio makubwa kwa kuwaondolea usumbufu wa kutuama maji
ya mvua kwa wananchi wa maeneo mbali mbali. Kamati inaiomba ZUSP kuchukua
juhudi za makusudi kuhakikisha miundombinu iliyoharibiwa ikiwemo barabara na maji
inarudishwa katika hali yake ya awali ili iendelee kuwahudumia wananchi wetu.
ZUSP imepanga kutekeleza Mradi wa kuweka taa za Barabarani (street light II) katika
maeneo ya barabara za Unguja yenye kilomita 15.4 na kilomita 17 kwa Pemba. Barabara
zitakazopatiwa huduma hizo kwa Unguja ni barabara ya Uwanja wa ndege - Mnazi
Mmoja, Mwanakwerekwe - Kiembesamaki na Kinazini Kariakoo mpaka Kilimani. Kwa
upande wa Pemba ni barabara za miji yote mitatu ya Pemba (Mkoani, Chake chake na
Wete) ikijumuisha barabara za Limbani - Wete Miji, Mtemani - Bopwe, Mtemani -
Kinyasini na Abdalla Mzee - Bandarini. Mradi huo utakapomaizika, utaiweka miji yetu
iking’ara muda wote wa usiku.
CHANGAMOTO
1. Kuchukua muda mrefu kumalizika kwa baadhi ya miradi.
2. Kuharibiwa kwa miundombinu kunakosababishwa na ujenzi wa Miradi hiyo
ikiwemo mabomba ya maji na barabara.
MAONI, USHAURI NA MAAGIZO YA KAMATI
1. Kamati inashauri Wizara kuelekeza nguvu zake kwenye maeneo ya ng’ambo
ambayo yana idadi kubwa ya wakaazi na ni jirani sana na mji wetu.
2. Kamati inaitaka Tume kubuni miradi mingine itakayokuwa na maslahi na nchi
yetu.
3. Kamati inaitaka Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar kwa kushirikiana na
Wizara ya Fedha ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa makini sana wakati
Ripoti ya Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo inayotokana na ufuatiliaji utekelezaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Biashara na Viwanda pamoja na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2018/2019. 24
nchi yetu inapohitaji mikopo kwani imebainika kuwa, baadhi ya washirika wa
maendeleo hutoa masharti magumu na yasiyokuwa na maslahi kwa nchi zetu.
4. Kamati inaitaka Wizara kufanya usimamizi madhubuti wa miradi ya maendeleo
nchini, kwani kumejitokeza wimbi la miradi ambayo haikamiliki kwa wakati
kutokana na sababu mbalimbali na kuitia hasara Serikali.
Ripoti ya Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo inayotokana na ufuatiliaji utekelezaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Biashara na Viwanda pamoja na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2018/2019. 25
3. WIZARA YA KILIMO, MALIASILI, MIFUGO NA UVUVI
Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi ni moja kati ya Wizara muhimu ambayo
imebeba sekta zinazoigusa jamii moja kwa moja kwani takriban zaidi ya asilimia arubaini
ya wananchi wetu wanategemea kipato chao kupitia sekta hizo. Kwa upande wa
mchango wa sekta hizo kiuchumi, kiasi cha asilimia 29.7 ya pato la nchi yetu
limechangiwa na sekta hii muhimu ya kilimo. Kutokana na umuhimu wake, Serikali
imewekeza katika sekta hiyo ili kusaidia kupunguza umasikini katika nchi yetu.
a) Programu kuu ya Uendeshaji na Uratibu wa Wizara ya Kilimo;
b) Programu kuu ya Maendeleo ya Kilimo;
c) Programu kuu ya Maendeleo ya Rasilimali za Misitu na Maliasili zisizorejesheka;
d) Programu kuu ya Maendeleo ya Mifugo;
e) Programu kuu ya Maendeleo ya Uvuvi;
Programu hizo zinatekelezwa na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kupitia
Taasisi na Idara zifuatazo:
i. Idara ya Mipango, Sera na Utafiti;
ii. Idara ya Uendeshaji na Utumishi;
iii. Idara ya Kilimo;
iv. Idara ya Misitu na Maliasili zisizorejesheka;
v. Idara ya Umwagiliaji maji;
vi. Idara ya Uhakika wa Chakula na Lishe;
vii. Idara ya Maendeleo ya Mifugo;
viii. Idara ya Maendeleo ya Uvuvi;
ix. Taasisi ya Utafiti wa Kilimo;
x. Chuo cha Kilimo Kizimbani;
xi. Wakala wa Serikali wa Huduma za Matrekta na zana za kilimo.
xii. Wakala wa Utafiti wa Mifugo;
xiii. Kampuni ya Uvuvi Zanzibar (ZAFICO); na
xiv. Afisi Kuu Pemba.
3.1 UTEKELEZAJI WA PROGRAMU KUU ZA WIZARA
Katika kipindi cha Julai hadi Disemba 2018, Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi
ilipanga kuingiziwa jumla ya shilingi 38.13 bilioni ambapo hadi Disemba, Wizara
iliingiziwa shilingi 58,087,125,299 sawa na asilimia 152 ya makadirio kwa ajili ya
kutekeleza Programu zake. Kamati imetembelea na kupitia ripoti mbali mbali za Wizara
hiyo na kugundua mambo yafuatayo:
Ripoti ya Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo inayotokana na ufuatiliaji utekelezaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Biashara na Viwanda pamoja na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2018/2019. 26
3.2 PROGRAMU KUU YA UENDESHAJI NA URATIBU WA WIZARA YA KILIMO
Programu hiyo imekusudia kuweka mazingira bora kwa wafanyakazi, kuwa na mipango
na sera ya sekta za fedha iliyoimara nchini itakayosaidia kukuza uchumi pamoja na
kuhakikisha shughuli zilizopangwa kwa sekta ya fedha Pemba zinatekelezwa. Utekelezaji
wa Programu hiyo unafanywa na Idara ya Mipango, Sera na Utafiti, Idara ya Uendeshaji
na Utumishi na Afisi Kuu Pemba.
3.3 OFISI YA AFISA MDHAMINI PEMBA
Afisi ya Afisa Mdhamini - Pemba ni Afisi muhimu ambayo inasimamia na kuratibu Idara
zote zinazofanya kazi chini ya Wizara ya kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Pemba.
Pamoja na juhudi kubwa zinazochukuliwa na Afisi ya Wizara ya Kilimo Pemba, Kamati
imebaini kuwa bado zao la mwani halijawanufaisha wananchi wetu kama
ilivyokusudiwa. Licha ya ugumu wa ukulima wa mwani, asilimia kubwa ya wananchi wa
ukanda wa pwani hujihusisha na kilimo hicho lakini bado bei ya zao hilo ni ndogo
isiyolingana kabisa na hali ya maisha.
Kamati inaipongeza Serikali kwa mipango yake ya kuanzisha kiwanda cha kusarifu
mwani na inashauri utekelezaji wa mpango huo ufanyike haraka iwezekanavyo ili
kuwaondolea wananchi ugumu wa maisha kwa kuongeza thamani ya zao hilo.
CHANGAMOTO
1. Vyanzo vingi vya mapato havijasimamiwa ipasavyo na kuweza kuiongezea
mapato Serikali.
2. Bado wakulima wetu wanaendelea kulima kilimo cha zamani cha mpunga na
kupelekea kipato chao kuwa kidogo.
3. Maofisa ugani hawaonekani kuwafikia wakulima kwenye maeneo yao na
kuwapatia msaada wa kitaalamu pale wanapohitaji.
4. Halmashauri zetu hazina uwezo wa kutosha kuhakikisha wakulima wetu
wanapata elimu ya ukulima wenye tija.
5. Baadhi ya misingi ya umwagiliaji maji imejengwa kwa udongo kwenye mabonde
ya mpunga na kupelekea kuharibika mara kwa mara hususan katika kipindi cha
mvua.
6. Uchelewaji mkubwa wa upatikanaji wa pembejeo za kilimo cha mpunga
zikiwemo mbegu na mbolea.
7. Baadhi ya makampuni ya mwani husafirisha kwa mwani mbichi na kupelekea
kuharibu bei ya mwani na taswira nzima ya nchi yetu katika soko la Kimataifa.
Ripoti ya Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo inayotokana na ufuatiliaji utekelezaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Biashara na Viwanda pamoja na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2018/2019. 27
MAONI, USHAURI NA MAAGIZO WA KAMATI
1. Afisi ihakikishe inavitambua vyanzo vya mapato vilivyopo ambavyo bado
havijaanza kukusanywa pamoja na kuibua vyanzo vyengine vipya.
2. Afisi itoe elimu ya kutosha kwa wakulima ili waweze kulima kilimo cha kisasa cha
kibiashara ambacho kinatumia eneo dogo lakini kipato chake huwa kikubwa.
3. Pamoja na Serikali kuamua kugatua baadhi ya maeneo yake na kuyapeleka
Halmashauri, bado utendaji wa Halmashari hizo upo chini, hivyo Afisi ihakikishe
inatoa ushirikiano wa hali na mali katika kuendeleza kilimo na hata kuwashirikisha
katika vikao vyao.
4. Afisi ihakikishe pembejeo za kilimo zinapatikana kwa wakati ili wakulima waweze
kulima kwa wakati na kufaidika na kilimo chao.
5. Afisi ijikite zaidi na ujenzi wa mitaro ya maji kwa kutumia saruji ili kuiwezesha
kudumu kwa kipindi kirefu.
6. Afisi ihakikishe inawaelimisha wananchi kuhusu athari za uuzaji mwani mbichi
katika Soko la Kimataifa na kuwachukulia hatua wale wote wanaohusika na
kadhia ya kusafirisha mwani mbichi nje ya nchi.
3.4 PROGRAMU KUU YA MAENDELEO YA KILIMO
Programu hiyo imekusudia kuboresha uzalishaji wa kilimo kwa kuongeza eneo la
umwagiliaji maji kwa kutumia teknolojia na usimamizi endelevu, kuimarisha na
kuendeleza tafiti za kilimo na maliasili pamoja na kuongeza wataalamu wa fani ya kilimo
na mifugo, kuimarisha upatikanaji wa huduma bora za kilimo kwa wakulima na
kuhakikisha upatikanaji wa chakula na lishe. Utekelezaji wa Programu hiyo unafanywa
na Idara ya Umwagiliaji maji, Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Kizimbani, Idara ya Kilimo na
Idara ya Uhakika wa Chakula na Lishe. Miongoni mwa mambo ambayo Kamati iliyaona
kwenye Programu hiyo ni:
3.5 SHAMBA LA RAZABA - MAKURUNGE BAGAMOYO
Shamba la RAZABA ni lenye historia ndefu inayodhihirisha udugu na umoja wa
Watanzania. Shamba hilo lililopo Bagamoyo lina ukubwa wa hekta 26,812 ambalo
lilitolewa na Rais wa awamu ya Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Marehemu Mwalimu Julius K. Nyerere kwa Rais wa Awamu ya Pili wa Zanzibar
Mheshimiwa Aboud Jumbe Mwinyi mwaka 1977, kwa lengo la kuiwezesha Zanzibar
kuwa na eneo la ardhi kwa uendelezaji wa sekta ya mifugo ili iweze kumudu ongezeko
la idadi ya wakaazi wake ambayo inaongezeka siku hadi siku.
Baada ya muda mrefu kupita bila ya shamba hilo kuendelezwa, Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ilikabidhiwa hekta 20,595 kwa ajili ya kuzitumia kwenye
shughuli za maendeleo ambapo hekta 10,000 tayari amepewa mwekezaji kwa ajili ya
uanzishaji wa kiwanda cha sukari. Eneo la Zanzibar lililobakia ni jumla ya hekta 6,217
Ripoti ya Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo inayotokana na ufuatiliaji utekelezaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Biashara na Viwanda pamoja na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2018/2019. 28
ambazo hadi Kamati inafika katika eneo hilo hakuna shughuli zozote za uzalishaji
zinazoendelea.
CHANGAMOTO
1. Uvamizi wa shamba hilo unaofanywa na wananchi kwa ajili ya makaazi na
uanzishaji wa mabwawa ya samaki. Jumla ya kaya 80 zilivamia katika shamba hilo
kwa ajili ya makaazi.
2. Kuna wafugaji binafsi ambao wamehodhi sehemu ya shamba hilo na kulitumia
kwa shughuli zao za ufugaji.
3. Kuwepo kwa Bandari bubu zipatazo 19 katika ukanda wa pwani wa shamba hilo
ni suala linalohatarisha usalama wa wananchi wa Bagamoyo na Taifa kwa ujumla.
4. Igawa eneo lililopo shamba hilo ni ndani ya ukanda wa Uwekezaji Kiuchumi
(EPZ), shamba haliwezi kutumika kwa ajili ya uwekezaji kutokana na kukosekana
hati miliki.
5. Kutoendelezwa kwa shamba hilo kunasababisha watu tofauti kuvutiwa na
kudanganywa kwa kuuziwa viwanja.
6. Uhaba wa walinzi wa shamba hilo.
7. Walinzi wa shamba hilo kutishiwa maisha na wananchi waliovamia shamba.
MAONI, USHAURI NA MAAGIZO YA KAMATI
1. Kwa vile shamba hivi sasa limekabidhiwa kwa Chuo cha Kilimo Kizimbani, Kamati
inaishauri Serikali kufikiria maudhui ya awali ya shamba hilo kwa kuwashirikisha
wafanyabiashara binafsi wanaoleta ng’ombe wa kuchinja ili walitumie shamba
hilo na Serikali kutoza kodi.
2. Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi izifanyie matengenezo makubwa
nyumba za makaazi ya wafanyakazi wake waliopo Bagamoyo.
3. Wizara ihakikishe inaongeza idadi ya walinzi kwenye shamba hilo.
4. Kamati inaitaka Wizara kuimarisha maslahi ya Wafanyakazi wake walioppo
Bagamoyo.
5. Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na Serikali ya Wilaya ya Bgamoyo ifanye
juhudi za makusudi kuwaondoa wavamizi wa shamba la Makurunge. Kamati
imeshtushwa na taarifa kwamba baadhi ya wavamizi hao wanaishi shambani hapo
kwa muda mrefu na tayari wameshazaa na kujukuu.
3.6 KILIMO CHA MBOGA KISAKASAKA
Kilimo ni sekta inayoajiri asilimia kubwa ya wananchi katika nchi nyingi zinazoendelea.
Wakulima huamua kujikita kwenye kilimo cha mazao mbalimbali kutokana na mazingira
yao. Kamati ilitembelea jumla ya wakulima 89 wa mazao ya mbogamboga katika eneo
la Kisakasaka ili kujua maendeleo waliyofikia na changamoto wanazokabiliana nazo
katika shughuli zao za kila siku.
Ripoti ya Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo inayotokana na ufuatiliaji utekelezaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Biashara na Viwanda pamoja na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2018/2019. 29
Kamati iliarifiwa kuwa Mabwana na Mabibi shamba hawawajibiki ipasavyo
kuwatembelea wakulima katika maeneo ya kilimo na kuwashauri njia za ukulima bora na
kukabiliana na changamoto zinazojitokeza. Kamati imesikitishwa na kitendo hicho
kinachosababisha usumbufu kwa wakulima na kupelekea kutumia njia za kienyeji kuhami
mazao yao jambo ambalo hupunguza mavuno.
CHANGAMOTO
1. Kuwepo kwa wadudu waharibifu wa mazao katika maeneo wanayolima.
2. Ukosefu wa maji ya uhakika kwa ajili ya umwagiliaji shambani. Hadi wakati
Kamati ilipowatembelea, wakulima hao walikuwa wakiendesha shughuli za
umwagiliaji kwa njia za kizamani ambazo hutumia nguvu na muda mwingi.
3. Ukosefu wa miundombinu mizuri ya barabara inayopelekea wakulima kusafirisha
mazao kwa njia zisizo rasmi kutokana na ukweli kwamba barabara wanayopaswa
kuitumia haipo katika hali ya kuridhisha.
4. Ushindani mkubwa wa soko unaochangiwa zaidi na uingizwaji wa tungule kutoka
Tanzania Bara hususan katika msimu wa mavuno ya tungule kwa wakulima wetu.
5. Migogoro ya ardhi inayowakabili wakulima kwenye maeneo yao kutokana na
watu wachache kuhodhi ardhi bila ya kuitumia na hivyo kuwakosesha wengine
fursa za kujiajiri.
MAONI, USHAURI NA MAAGIZO YA KAMATI
1. Kamati inaitaka Wizara kushughulikia suala la upatikanaji wa maji kwa ajili ya
kukidhi mahitaji ya umwagiliaji wa kisasa kwa njia ya matone (drip irrigation).
2. Wizara iwapatie wakulima wetu utaalamu wa kulima kilimo cha vitunguu kwani
inasemekana ardhi ya eneo la kisakasaka inakubali zao hilo.
3. Wizara ihakikishe inawapatia wakulima pembejeo za kilimo ili wazalishe kwa
wingi zao hilo.
4. Kamati inaisisitiza Wizara ya Kilimo kufanya tafiti mbalimbali kuhusu ardhi na
matumizi yake ili kuwaelekeza wananchi walime kilimo bora kwa maslahi yao na
Taifa hili.
5. Wizara kwa kushirikiana na Wizara ya Biashara ihakikishe inadhibiti soko kwa
kuzuwia bidhaa zinazotoka nje ya nchi ambazo zinazalishwa nchini kutoingia
Zanzibar ili wakulima wetu waweze kupata soko la bidhaa wanazozalisha.
6. Kamati inaitaka Wizara ishirikiane na Halmashauri husika kuwasimamia vyema
Mabwana na Mabibi shamba na kuhakikisha wanawapatia wakulima wetu
msaada unaostahiki.
Ripoti ya Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo inayotokana na ufuatiliaji utekelezaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Biashara na Viwanda pamoja na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2018/2019. 30
3.7 KILIMO CHA MPUNGA BONDE LA CHAANI KIKOBWENI
Bonde la Mpunga la Chaani Kikobweni lina ukubwa wa ekari 165 zinazolimwa na
wakulima 187 kati yao 133 ni wanawake na 54 wanaume. Bonde hilo lina wakulima wa
kilimo cha juu (kinachotegemea mvua) na wengine wanalima kilimo cha umwagiliaji maji
kinachosimamiwa na Kamati za wakulima waliogawika kwa mujibu wa maeneo
waliyotoka. Kituo kina matrekta manne, mawili ni mazima lakini mawili mabovu
yanasubiri matengenezo.
Kwa mwaka wa fedha 2018/2019, Wizara ilipangiwa kutumia jumla ya shilingi 1.5 bilioni
kwa ajili ya ununuzi wa pembejeo za kilimo. Kiwango hicho ni kidogo ikilinganishwa na
jumla ya shilingi 4.5 bilioni zilizotengwa kwa mwaka uliopita. Kwasasa jumla ya Ekari 53
tayari zimeshaendelezwa kwa ajili ya Kilimo cha Umwangiliaji maji na wakulima wake
wameshapatiwa pembejeo kwa asilimia mia moja kupitia Mradi wa ERPP. Mradi huo
unaosimaniwa na Idara ya Umwagiliaji maji umelenga kuzalisha mbegu bora za msingi
kilo 400, kuandaa ziara ya mafunzo kwa Jumuiya za umwagiliaji kutoka skimu 16 Unguja
na Pemba, kujenga na kutengeneza miundombinu katika skimu tisa za umwagiliaji maji.
Mradi huo umejenga msingi wa saruji mita 1,200 Mtwango (canal lining) na mita 600
Kwalembona.
Kamati imebaini mapungufu makubwa ya upatikanaji wa pembejeo kwa wakulima wa
juu (wanaotegemea mvua) ambao wanahudumiwa na Serikali. Tofauti kubwa iliyopo
katika ununuzi wa pembejeo baina ya wakulima wa juu na wa umwagiliaji ni suala
linalohitaji kufikiriwa kwa kina kwani wakulima wa juu wanachangia shilingi 26,000
wakati wakulima wa umwagiliaji wanachangia shilingi 13,000 kwa lita. Aidha, huduma
za ulimaji na uburugaji pia haziridhishi kwa wakulima wa juu kwani Kamati iliarifiwa
kuwa wakulima wachache tu ndio waliolimiwa ingawa msimu wa kilimo ulikuwa
ukingoni.
CHANGAMOTO
1. Uhaba wa Matrekta ya kufanyia kazi.
2. Upungufu wa Pembejeo za kilimo hususan kwa wale wanaolima kilimo cha
mpunga wa kutegemea mvua.
3. Mwamko mdogo wa baadhi ya wakulima kuchangia fedha za kupatiwa huduma
za matrekta kwa wakati mwafaka.
4. Ukosefu wa banda la kuhifadhia vitendea kazi.
5. Ukosefu wa banda la wakulima kwa ajili ya kufanyia shughuli zao.
6. Upungufu wa mafundi wa matrekta katika kituo hicho kwani kituo kina fundi
mmoja tu ambae hana uzoefu wa kutosha.
7. Upungufu wa ziara za viongozi kuwatembelea wakulima husuan katika kipindi
cha maandalizi ya kulima.
Ripoti ya Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo inayotokana na ufuatiliaji utekelezaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Biashara na Viwanda pamoja na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2018/2019. 31
MAONI, USHAURI NA MAAGIZO YA KAMATI
1. Wizara ya kilimo ihakikishe inaongeza idadi ya Matrekta katika kituo cha kilimo
cha Chaani Kikobweni kwa ajili ya kulimia na kuburugia kwani wakulima
wamehamasika na wameonesha uwezo mkubwa wa kujitolea na kuchangia fedha
za kupatiwa huduma hiyo.
2. Wizara ihakikishe inatoa pembejeo za kilimo kwa wakulima wote tena bila ya
kuwepo tafauti ya bei na aina ya kilimo mtu anacholima kama cha umwagiliaji au
cha kutegemea mvua.
3. Idara ya kilimo pamoja na kamati ya wakulima wa Chaani Kikobweni
wawahamasishe wakulima wao kufanya malipo ya huduma za matrekta mapema
iwezekanavyo ili waweze kulimiwa mapema.
4. Kamati inaishauri Wizara ya kilimo kujenga banda la kuhifadhia matrekta na
kuyanunusuru kuathiriwa na jua kali au mvua ili kuyazidishia uhai wa maisha yao.
5. Viongozi wa Serikali na kisiasa wawe wafanye ziara kwa wakulima mara kwa
mara ili waweze kugundua changamoto wanazokabiliana nazo na mafanikio halisi
waliyofikia.
3.8 PROGRAMU KUU YA MAENDELEO YA RASILIMALI ZA MISITU NA MALIASILI
ZISIZOREJESHEKA
Programu hiyo imekusudia kukuimarisha na kuendeleza uhifadhi wa misitu na kuimarisha
mazingira ya misitu. Utekelezaji wa Programu hiyo unafanywa na Idara ya Misitu na
Maliasili zisizorejesheka. Miongoni mwa mambo ambayo Kamati iliyagundua kwenye
Programu hiyo ni:
Kamati iliarifiwa kwamba kwa kipindi hiki, nchi yetu inajitosheleza kwa rasilimali ya
mchanga ambapo maeneo matatu yaliyopendekezwa kwa ajili ya uchimbaji
yamekaguliwa na kufanyiwa tathmini ya kina cha mchanga kilichopo. Kwa kipindi cha
Julai - Disemba 2018, makusanyo halisi ya uzalishaji wa mawe, mchanga na kokoto ni
jumla ya shilingi 240,355,000.
Licha ya hali hiyo, Kamati inaitaka Wizara iwe makini na uvunaji wa rasilimali hizo
ikizingatiwa jiografia ya nchi yetu ni visiwa. Ni dhahiri kuwa umakini mkubwa
unahitajika katika matumizi ya rasilimali hizo ili ziweze kutumika kwa muda mrefu na
kuepukana na uagizaji wa mchanga kutoka nje ya nchi.
3.9 MSITU WA HIFADHI YA VUMAWIMBI NGEZI
Msitu wa Hifadhi ya Vumawimbi Ngezi ni msitu mkubwa kuliko misitu yote iliyopo
Pemba na ndio msitu wa pili kwa ukubwa Zanzibar baada ya Msitu wa Hifadhi ya
Jozani. Msitu huo ulianza kuhifadhiwa tokea mwaka 1959 na mwaka 2004 ukatambulika
rasmi kuwa ni Msitu wa Hifadhi ya Vumawimbi. Msitu huo wenye hekta 2,900
umezungukwa na vijiji 10 vyenye wakaazi 21,000. Kutokana na utafiti uliofanywa na
wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kuna aina 355 ya miti inayopatikana
ndani ya msitu huo ambayo 11 inaweza kutumika kwa matumizi ya utengenezaji wa
dawa tofauti. Aidha, msitu huo una miti mingi ambayo haipatikani popote duniani.
Ripoti ya Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo inayotokana na ufuatiliaji utekelezaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Biashara na Viwanda pamoja na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2018/2019. 32
Kamati inaipongeza Wizara kwa juhudi inazozichukua za kuhamasisha wananchi
kuendelea kufanya utalii wa ndani kwa kutembelea maeneo yaliyomo Zanzibar na sio
kuamua kwenda nje wakati hayo wanayoyafuata huko mengine yanapatikana hapa hapa
Zanzibar. Licha ya changamoto zilizopo, Msitu umeweza kuendeleza hadhi yake ya kuwa
msitu wa Hifadhi, kwa ujenzi wa Mkahawa na eneo la Mapokezi na kubakiza asilimia
thelathini ya makusanyo yanayotokana na msitu huo ili yatumike kwa maendeleo ya
Hifadhi.
CHANGAMOTO
1. Kuwepo kwa mbwa wanaoingia katika msitu na kuua wanyama waliomo ndani
ya msitu.
2. Baadhi ya wanavijiji wanaouzunguka msitu huo wanapika pombe za kienyeji
(gongo) ndani ya msitu huo.
3. Kuvamiwa kwa msitu na baadhi ya watu kwa kukata miti. Historia inaonesha
Msitu uliwahi kuvamiwa na watu kutoka Kenya waliokuwa na Misumeno ya
moto na kukata magogo.
4. Uhaba mkubwa wa walinzi wa msitu huo kwani msitu una jumla ya walinzi 8
wanafanya shughuli za doria.
5. Ubovu wa barabara ya kufika katika eneo la msitu.
6. Msitu umepitiwa na njia katikati na kusababisha watu kupita kila wakati, jambo
hilo huleta usumbufu hususan katika masuala mazima ya kiulinzi.
7. Madai ya wananchi kuhodhi eneo la msitu huo. Kumejitokeza ukoo wa Mjaja na
kusema sehemu ya msitu imemilikiwa na wazee wao tangu zamani. Hivyo mara
kwa mara hujaribu kujenga na Idara hulazimika kubomoa.
8. Kujitokeza baadhi ya watu kutaka kuweka uwekezaji ndani ya msitu hususan kwa
kujenga hoteli.
9. Ukosefu wa mkahawa kwa ajili ya wageni wanaotembelea eneo hilo.
10. Ukosefu wa njia za ndani zinazotumika kuingia katika ziwa Taufik lililomo katika
msitu huo ili kuwawezesha watalii kufika hadi katikati ya ziwa hilo na kujionea
viumbe vilivyomo ndani yake.
11. Kutokuwepo kwa kipaa kilichojengwa juu ya mashine za zamani zilizokuwa
zikitumika kupasulia mbao pamoja na maelezo yanayoelezea historia ya mashine
hizo.
12. Kukosekana kwa vyoo ndani ya msitu ambavyo vingeweza kutumiwa na watu
wanaoutembelea msitu huo.
Ripoti ya Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo inayotokana na ufuatiliaji utekelezaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Biashara na Viwanda pamoja na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2018/2019. 33
MAONI, USHAURI NA MAAGIZO WA KAMATI
1. Kamati inaitaka Wizara kulitumia eneo lililowekwa kwa ajili ya uwekezaji na eneo
la msitu libakie kuwa ni eneo la Hifadhi ya Taifa wala lisijengwe hoteli au nyumba
za makaazi.
2. Wizara ihakikishe inalifuatilia suala la ujenzi wa barabara itakayouzunguka msitu
kupitia eneo la Machopeni na kuungana na kijiji cha Makangale.
3. Wizara ihakikishe miti yote hatarishi kwa maisha ya miti mingine ambayo imo
ndani ya Msitu inadhibitiwa ipasavyo.
4. Wizara ihakikishe mbwa wanaoingia katika msitu na kuua wanyama waliomo
ndani ya msitu wanadhibitiwa.
5. Idara ya Misitu na Maliasili zisizorejesheka ihakikishe inadhibiti wapika ulevi
(gongo) ndani ya msitu.
6. Wizara ihakikishe inadhibiti uvamizi wa watu wote wanaoingia katika msitu na
kukata miti.
7. Wizara ihakikishe inatatua changamoto ya uhaba mkubwa wa walinzi wanaolinda
msitu huo.
8. Wizara ihakikishe inatatua mgongano uliopo kati ya watendaji wa msitu na ukoo
wa Bwana Mjaja unaodai sehemu ya msitu inamilikiwa na wazee wao tangu
zamani.
9. Wizara ihakikishe hakuna mtu atakaeruhusiwa kuwekeza katika eneo la msitu
pamoja na kutafuta hatimiliki ya maeneo ya msitu na yale ya uwekezaji.
10. Idara ya Misitu na Maliasili zisizorejesheka ihakikishe inakamilisha ujenzi wa
sehemu ya mapokezi na mkahawa kwa ajili ya wanaotembelea eneo hilo la msitu
huo.
11. Wizara ihakikishe inajenga vijia vidogo vidogo vitakavyomuwezesha Mtalii
kuingia na kufika katika maeneo ya vivutio yaliyomo katika msitu huo bila
usumbufu.
12. Wizara ihakikishe inazihifadhi kwa kuzijengea kipaa pamoja na kuziwekea
maelezo mashine za zamani zilizokuwa zikitumika kupasulia mbao.
13. Ni wajibu wa Wizara kujenga vyoo ndani ya msitu ambavyo vitaweza kutoa
huduma kwa watu wanaoutembelea msitu huo.
14. Idara ya misitu itafute mbinu za kuyaondoa maji yanayotuwama kipindi cha mvua
kwenye njia kuu iliyopita katika msitu huo.
Ripoti ya Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo inayotokana na ufuatiliaji utekelezaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Biashara na Viwanda pamoja na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2018/2019. 34
3.10 MSITU WA KIUYU MBUYUNI
Msitu wa Kiuyu Mbuyuni ni msitu wa zamani sana uliotangazwa kuwa msitu wa hifadhi
tangu mwaka 1987 ukiwa na hekta 770 lakini kwa sasa msitu huo una hekta 270. Hivi
karibuni kuna Mwekezaji amejitokeza kutaka kujenga hoteli ndani ya msitu huo kupitia
Mradi unaoitwa ‘Vault’ utakaochukua hekta 150 za msitu huo. Kamati inaitaka Wizara
kupiga marufuku uwekezaji wa kujenga hoteli ndani ya msitu huo isiyokuwa rafiki na
mazingira kwa ajili ya kuulinda msitu.
CHANGAMOTO
1. Kutofahamika ipasavyo maeneo ya msitu huo kwani eneo lililotangazwa katika
Gazeti Rasmi la Serikali ni kubwa ukilinganisha na uhasilia ulivyo hivi sasa.
2. Kutokezea kwa Muwekezaji kutaka kuwekeza ndani ya msitu husika kwa kujenga
hoteli inayoaminika haitokuwa rafiki na mazingira ya uendelezwaji wa Msitu.
3. Kukosekana kwa njia ya kufika katika eneo la Msitu.
MAONI, USHAURI NA MAAGIZO YA KAMATI
1. Wizara ichukue juhudi za makusudi kutoa uelewa kwa jamii kuhusu uwepo wa
msitu wa Kiuyu Mbuyuni na maeneo yake ili eneo lililotangazwa katika Gazeti
Rasmi la Serikali liweze kueleweka na kuhifadhika.
2. Wizara ihakikishe eneo la msitu huo linafikika ipasavyo.
3.11 PROGRAMU KUU YA MAENDELEO YA MIFUGO
Programu hiyo imekusudia kuongeza uzalishaji na ubora wa mifugo na mazao yake
pamoja na kuimarisha huduma za utibabu wa mifugo kwa wanajamii. Utekelezaji wa
Programu hiyo unafanywa na Idara ya Maendeleo ya Mifugo. Miongoni mwa mambo
ambayo yametekelezwa na Programu hiyo na Kamati kuyatolea ushauri ni:
3.12 JUMUIYA YA WAFUGAJI KUKU
Jumuiya ya Wafugaji kuku iliopo Mwanakwerekwe imeanzishwa mwaka 2016 ikiwa na
lengo la kuwawezesha wafugaji wa kuku Zanzibar kufuga katika kiwango kinachotakiwa,
kuwapatia elimu ya ufugaji bora pamoja na kuhakikisha wafugaji hao wanapata
vifaranga vilivyo bora.
Kamati imegundua kuwepo kwa mahitaji makubwa ya kuku hususan kwenye sekta ya
utalii ambayo wafugaji wetu wa ndani hawajaweza kuyakidhi. Kwa mantiki hiyo, Kamati
inaiomba Wizara ya Kilimo kuwasaidia wafugaji wetu kwa kuwapatia utaalamu wa
ufugaji wa kisasa utakaowawezesha kuzalisha kuku wengi katika ubora unaokubalika.
Kadhalika, Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na Wizara ya Biashara zihakikishe kuku
wanaoingizwa ndani ya Zanzibar kutoka nje wanawekewa kodi kubwa ili waweze
kuwanyanyua wafugaji wa ndani.
Ripoti ya Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo inayotokana na ufuatiliaji utekelezaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Biashara na Viwanda pamoja na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2018/2019. 35
CHANGAMOTO
1. Ukosefu wa fedha za kununulia dawa na vyakula vya kuku.
2. Ukosefu wa machinjio ya kisasa.
3. Utaratibu unaotumika kuwapatia mikopo wafugaji hao ni mgumu
MAONI, USHAURI NA MAAGIZO YA KAMATI
1. Kamati inashauri wafugaji wa kuku wapatiwe ruzuku ya kununulia dawa, mayai,
vifaranga na vyakula vya kuku kama wanavyopatiwa wakulima wa mpunga.
2. Wizara kwa kushirikiana na Serikali za mitaa kujenga machinjio ya kisasa
yatakayotoa huduma bora na kulinda afya za walaji.
3. Wizara iwahamasishe wakulima kulima mahindi ili yaweze kukobolewa na
kutumika kama chakula cha kuku.
4. Wafugaji wa kuku wapatiwe mikopo nafuu itakayowawezesha kumudu gharama
za uendelezaji wa shughuli zao.
5. Kamati inaitaka Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na Wizara ya Biashara
kukifufua kiwanda cha chakula cha kuku kilichokuwepo hapo awali na
kukabidhiwa wafugaji wa kuku kukiendesha.
6. Wizara ya Kilimo na Wizara ya Biashara ipange fungu maalum kwa ajili ya
kuwasaidia wafugaji kuku kwa kuwapatia mikopo nafuu.
7. Wizara ihakikishe kodi zinazotozwa kwa wafugaji kuku zinapunguzwa kwani
inawasababishia gharama kubwa za uzalishaji.
3.13 PROGRAMU KUU YA MAENDELEO YA UVUVI
Programu hiyo imekusudia kuongeza uzalishaji wa samaki na mazao mengine ya baharini
pamoja na kuendeleza uvuvi wa kienyeji na kusimamia rasilimali za baharini kwa
matumizi endelevu. Utekelezaji wa Programu hiyo unafanywa na Idara ya Maendeleo ya
Uvuvi. Miongoni mwa mambo ambayo yametekelezwa na Programu hiyo ni:
3.14 MRADI WA KUSIMAMIA UVUVI KUSINI MAGHARIBI MWA BAHARI YA HINDI
(SWIOFISH)
Mradi wa kusimamia Uvuvi Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi (SWIOFISH), huu ni
mradi unaosimamiwa na Idara ya Maendeleo ya Uvuvi ambao umelenga kutoa huduma
za kutengeneza mpango wa utekelezaji wa uvuvi wa kipaumbele wa pweza, samaki wa
miambani na samaki wa jamii ya dagaa, kujenga Ofisi mbili za uhifadhi wa mazingira ya
maeneo ya Hifadhi ya ghuba ya “Changuu Bawe Marine Conservation Areas”
(CHABAMCA) na “Tumbatu Marine Conservation Areas” (TUMCA). Mradi pia
umelenga kukarabati Ofisi za maeneo ya Hifadhi ya MIMCA, MENAI na PECCA pamoja
na kusimamia ujenzi wa Bandari ya Uvuvi (Jetty) katika eneo la Kampuni ya Uvuvi
ZAFICO.
Mradi umeshampata mjenzi wa Ofisi mbili za CHUMBAMCA na TUMCA na Mkataba
wake tayari umesharudi kutoka kwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar ambapo ushauri
na maelekezo yaliyotolewa yameshafanyiwa kazi. Aidha, ukarabati wa Ofisi za MENAI
Ripoti ya Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo inayotokana na ufuatiliaji utekelezaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Biashara na Viwanda pamoja na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2018/2019. 36
na MIMCA unaendelea wakati PECCA umeshakamilika. Kwa upande wa ujenzi wa
Bandari ya Uvuvi, tangazo la kumpata Mshauri Elekezi wa kuandaa mchoro
limeshatolewa.
3.15 KAMATI ZA WAVUVI MENAI, PECCA NA MIMCA.
Kwa vipindi tofauti, Kamati ilipata fursa ya kukutana na Kamati za uvuvi Unguja na
Pemba ambazo zinawaunganisha wavuvi kutoka maeneo mbalimbali nchini. Kamati hizo
zimeundwa kisheria kwa lengo la kusaidia uhifadhi wa mazingira ya ukanda wa bahari na
kupelekea upatikanaji wa mazao mengi ya baharini. Kamati za uvuvi zimegawika katika
sehemu kuu tatu, kamati ya MIMCA inayofanya kazi zake za uhifadhi katika ukanda wa
Kaskazini Unguja wakati kamati ya MENAI ukanda wa Kusini Unguja na kamati ya
PECCA inashughulika na uhifadhi wa ukanda wa bahari wa Pemba.
Kamati hizo zinasaidia katika uhifadhi wa matumbawe ambayo ndiyo mazalio ya samaki,
kuimarisha ulinzi wa maeneo ya hifadhi ya bahari, kupiga vita uvuvi haramu, kutatua
migogoro ya wavuvi na ndio chombo kikuu kinachounganisha baina ya wavuvi na
Serikali.
Kupitia ziara hizo, Kamati iligundua mambo kadhaa ambayo yanazorotesha maendeleo
ya uvuvi nchini yakiwemo ukosefu wa mtaji kwa ajili ya kuvua uvuvi wa kisasa jambo
ambalo hupelekea kupata mavuno kidogo. Visiwa vyetu vina idadi kubwa ya wavuvi
ambao wanaendesha shughuli zao kwa njia za asili. Wavuvi hao hujikuta wanafanya kazi
kila uchao bila ya kujua hatma yao na familia zao kutokana na kipato duni
wanachojipatia (chungu jiko). Ili kupambana na hali hiyo, Kamati ya Fedha, Biashara na
Kilimo inaishauri Serikali kuharakisha mpango wake wa kuwapatia vyombo vya kisasa
wavuvi wetu. Sambamba na hilo, Kamati ya PECCA inaiomba Serikali kutoingizwa
samaki kutoka nchi za nje (perdue) kisiwani Pemba kama wanavyoingizwa kwa kasi
kisiwani Unguja. Kufanya hivyo kutawakosesha soko la ndani la samaki wao na kurejesha
nyuma juhudi zao za kupambana na umasikini.
Tunaipongeza Serikali kwa uamuzi uliochukuwa wa kuwapatia vyombo wavuvi wa
Zanzibar kupitia mradi wa MACEMP ili kuongeza kipato chao kulingana na kazi
wanayoifanya. Hata hivyo, Kamati haikufurahishwa na utaratibu uliotumika wa
kuvigawa vyombo hivyo kupitia Waheshimiwa ambao walivigawa bila ya kuzingatia
mahitaji halisi ya wavuvi, hatimae vyombo vingi viliishia kuuzwa na kutofikia lengo
lililokusudiwa. Tunaiomba Serikali inapochukua hatua ya ugawaji wa vyombo iwapatie
wahusika watakaonufaika na vyombo hivyo.
Licha ya visiwa vyetu kuwa na utajiri mkubwa wa mazao ya baharini, bado wavuvi wetu
hawajafanikiwa kuyavuna ipasavyo kutokana na kutokuwa na utaalamu na nyenzo za
kuyafikia. Hivyo, Kamati inaiomba Serikali kuwapatia utaalamu wa uvuvi wa kisasa,
kuwatengenezea viwanda vya samaki na kuwapatia meli kubwa za uvuvi ili waweze
kupata samaki walio bora kwani uvuvi unaoendeshwa hivi sasa ni wa kiwango cha chini
ambao hauna tija kubwa kwao.
Ripoti ya Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo inayotokana na ufuatiliaji utekelezaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Biashara na Viwanda pamoja na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2018/2019. 37
Kwa masikitiko makubwa, Kamati imerudishwa nyuma na utendaji wa baadhi ya
Viongozi wa Serikali yetu kwa kitendo cha kutaka kuwanyang’anya wanakamati ya
PECCA baadhi ya maeneo yaliyomo ndani ya hifadhi (kisiwa cha Misali, Uvunje na Njau)
kwa ajili ya kuyaendeleza kiutalii bila ya kushauriana na Kamati. Kitedo hicho
kimeikasirisha PECCA na kutaka eneo lao la hifadhi lisitumike kinyume na madhumuni ya
awali kwa maslahi ya wachache.
CHANGAMOTO
1. Upungufu mkubwa wa vitendea kazi ikiwemo boti za uokozi na ukaguzi, vespa na
gari za kuwapitia wavuvi wengine wadogo na kuwaokoa hususan katika nyakati
za upepo unaosababisha maafa makubwa kwa wavuvi.
2. Uvamizi wa maeneo ya hifadhi kwa matumizi mbadala.
3. Upungufu mkubwa wa mapato ya kuendeshea shughuli za uvuvi. Kamati za uvuvi
hazina mapato ya kutosha jambo ambalo husababisha mzunguko wa fedha kuwa
mdogo kiasi cha kushindwa kukidhi mahitaji yao ya msingi.
4. Utaratibu wa ukataji leseni za uvuvi kwenye Halmashauri unawakwaza wavuvi
wetu kwani huendesha shughuli zao katika sehemu tofauti.
5. Usumbufu wanaoupata wavuvi wakiwa katika shughuli zao pale wanapolazimika
kuchukua mafuta ya akiba kwa njia ya mageloni.
6. Kutonufaika na fedha za mnada katika masoko yao.
7. Kukosekana kwa mashirikiano ya kutosha kati ya Wavuvi na wawekezaji nchini.
8. Changamoto zilizojitokeza kwenye mfumo wa doria kwani wavuvi
wanapopeleka taarifa za kuwepo muhalifu, askari wa KMKM wanachelewa kufika
katika eneo husika.
9. Kutofuatwa kwa Kanuni ya Uhifadhi wa Bahari ambayo imeeleza wazi kwamba
asilimia 30 ya mapato yanayotokana na maeneo ya hifadhi yatumiwe kwa
maendeleo kamati hizo.
10. Mgongano wa maslahi baina ya Kamati za Uvuvi na Halmashauri kwa baadhi ya
masoko ambayo yamegatuliwa ilhali ujenzi wake umefanywa kwa nguvu za
wavuvi wenyewe.
MAONI, USHAURI NA MAAGIZO YA KAMATI
1. Kutokana na ukweli kwamba maeneo ya hifadhi yanalindwa na wananchi
wenyewe kupitia Kamati za Uvuvi kwa njia ya kujitolea, Kamati inaitaka Wizara
ya Kilimo na Serikali kwa ujumla kuwaunga mkono wananchi hao na kuilinda
hifadhi hiyo kwa kuwapatia vyombo vya ulinzi vikiwemo boti ya doria.
2. Kamati inaishauri Wizara kuanzisha Viwanda vya Kisasa vya Kusarifu Samaki na
pweza nchini ili kuinua hali za wavuvi wetu.
3. Wizara izisaidie utaalamu Kamati za uvuvi ili waweze kujiongezea kipato na
kuendesha maisha yao.
4. Serikali iwapatie ruhusa maalum wavuvi wanaovua sehemu za mbali kuchukua
mafuta ya ziada kwenye vyombo vyao. Jambo la msingi ni kuhakikisha mafuta
hayo yanahifadhiwa katika vyombo salama na kutumika kwa mujibu wa ruhusa
iliyotolewa.
Ripoti ya Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo inayotokana na ufuatiliaji utekelezaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Biashara na Viwanda pamoja na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2018/2019. 38
5. Serikali ilifuatilie kwa haraka mgogoro uliopo kati ya wavuvi wa Uvinje na
mwekezaji kabla haujaleta athari.
6. Wizara ya Kilimo ishirikiane na Wizara ya Serikali za Mitaa kuwaondoshea wavuvi
mzigo wa kulipa fedha zisizostahiki kwa sheha.
7. Kamati inaitaka Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na Wizara ya Serikali za Mitaa
kuwaondolea usumbufu wavuvi kwa kuendelea na mfumo wa ukatishaji wa leseni
kupitia Idara ya Uvuvi ikizingatiwa kwamba wavuvi ni watu wa kuhamahama
kutoka sehemu moja hadi nyengine kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli zao.
Utaratibu wa kukatisha leseni kwenye Halmashauri unawakwaza wavuvi hao.
8. Wizara ihakikishe Kanuni ya Uhifadhi wa Uvuvi Baharini inafuatwa kwa
kuwapatia Kamati za Wavuvi asilimia 30 ya mapato yanayotokana na hifadhi zao.
9. Idara ya Uvuvi ipatiwe fedha nyengine za kuanzisha maeneo tengefu ya uhifadhi
wa matumbawe.
10. Idara ya Uvuvi iandike miradi ya kukabiliana na changamoto za tabia nchi na
kuziwasilisha kwa washirika wa maendeleo.
11. Wizara ihakikishe inawapa taaluma wavuvi ya jinsi gani wataweza kutengeneza
matumbawe bandia na kuyatumia katika kuhifadhi bahari inayowazunguka.
3.16 UFUGAJI WA PWEZA
Katika hatua za kusimamia uvuvi na wavuvi wetu, kamati ilifika kijiji cha Mtende
kuonana na Wananchi waliokubaliana kufunga pweza ili kuongeza faida katika zao hilo.
Utaratibu huo umeanza mwaka 2017 na hadi kamati inatembelea eneo hilo tayari
walikuwa wameshafunga na kufungua uvunaji wa pweza kwa vipindi viwili ambapo
kipindi kimoja kinachukua miezi mitatu.
Wafugaji wa pweza huzalisha takriban tani nne kwa siku ya mwanzo ya bamvua na
hupungua kidogo kwa siku zinazofuatia. Kiwango hicho ni kikubwa lakini hakiwapatii
manufaa makubwa wazalishaji kutokana na kutokuwa na viwanda vya kusarifu pweza
nchini. Matokeo yake ni kuongezeka kwa wafanyabiashara wa pweza ambao hununua
bidhaa hiyo na kupeleka nchi jirani zenye viwanda.
Kamati imesikitishwa na baadhi ya wananchi wa maeneo hayo waliodai kuwa ufungaji
wa pweza unaongeza ukali wa maisha kwa vile hukosha shughuli ya kufanya katika
kipindi wanachofunga pweza kutokana na kutokuwa na shughuli mbadala ya
kuendeshea maisha yao kwa kipindi hicho. Hivyo, Kamati inawasihi wananchi wa
maeneo hayo kutafuta shughuli nyengine za kiuchumi kama ukulima wa mazao ya
chakula na biashara ili kunyanyua kipato chao.
Ripoti ya Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo inayotokana na ufuatiliaji utekelezaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Biashara na Viwanda pamoja na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2018/2019. 39
CHANGAMOTO
1. Kuvamiwa kwa eneo lililofungwa na wavuvi wa vijiji vya karibu hususan siku
wanayofungua uvunaji.
2. Kukosekana ulinzi madhubuti katika eneo lililofungwa (bwachi).
3. Kukosekana kwa boti za doria katika eneo hilo ambapo wavamizi hushindwa
kukamatwa.
4. Baadhi ya wavuvi wanaovamia eneo hilo huvua kwa kutumia njia zisizokubalika
na kuharibu bahari na rasilimali zilizomo.
MAONI, USHAURI NA MAAGIZO YA KAMATI
1. Wizara ihakikishe inaanzisha maeneo mengine ya kufungwa kwa ajili ya kufuga
pweza.
2. Idara ya Uvuvi iwahamasishe wavuvi na wananchi wanaoishi katika maeneo hayo
kuweka ulinzi ikiwa ni pamoja na kuwapatia vitendea kazi.
3. Wizara ihakikishe inawapatia boti ya doria wavuvi wa eneo hilo.
4. Wizara kupitia Idara ya Uvuvi ihakikishe inawahamasisha na kuwaelimisha wavuvi
kuhusu athari za uvuvi haramu kwa maliasili za bahari kwa maslahi yetu na vizazi
vijavyo.
3.17 UKULIMA WA MWANI
Mwani ni zao la biashara lililoanza kuzalishwa nchini mwetu mwanzoni mwa miaka ya
tisini. Kilimo cha mwani kimeajiri asilimia kubwa ya akina mama wa vijiji vya ukanda wa
Kusini Unguja na sehemu mbalimbali nchini. Awali, wakulima hao walijishughulisha na
harakati za kilimo cha choroko, uvumbikaji wa makumbi kwa ajili ya kutengeneza
kamba, uanikaji wa dagaa na kujipatia riziki zao. Kamati ilipata fursa ya kukutana na
wakulima wa mwani wa ukanda wa kusini na kufahamishwa namna wanavyoendesha
shughuli zao. Changamoto kubwa iliyopo Zanzibar na Duniani kiujumla ni mabadiliko ya
tabia nchi ambayo huwafanya wakulima wa mwani kusogea mbele zaidi baharini
(kwenye maji mengi) kuendesha shughuli zao. Hatua hiyo imewaweka katika wakati
mgumu kutokana na kuongezeka kwa gharama za uzalishaji.
Kuna aina mbili kuu za mwani ambazo wakulima wetu wamezoea kuzilima hapa
Zanzibar za Cottonee na Spinosum. Mwani wa aina hiyo huwa hauna soko kubwa
ulimwenguni lakini kuna mwani wa Agar glacelaria ambao unalimwa sana Indonesia
ndio wenye soko duniani. Mwani wa aina hiyo haupo sana hapa kwetu visiwani lakini
Wizara ya Kilimo imo katika utafiti wa kuangalia wapi unaweza ukalimwa pamoja na
kutafuta wawekezaji kuwekeza katika eneo hilo. Pamoja na Wizara kuendelea na utafiti,
kuna taarifa kwamba mwani wa aina hiyo umeonekana maeneo ya bahari ya Fumba na
baadhi ya sehemu za Pemba.
Ripoti ya Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo inayotokana na ufuatiliaji utekelezaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Biashara na Viwanda pamoja na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2018/2019. 40
Kisiwa cha Fundo kina wakulima wengi wa mwani mnene wanaolima kwa kiwango
kikubwa. Lakushangaza ni kwamba, hadi leo wakulima hao hawajaendelezwa na
kupelekea kushindwa kuzalisha ipasavyo mwani katika msimu uliopita mara baada ya
kukumbwa na upepo mkali uliosababisha mwani kukatika na kupotea baharini.
Kufuatia ziara ya Mheshimiwa Rais nchini Indonesia, matunda yake yameanza kuonekana
kwani Wizara ya Biashara na Viwanda imo kwenye hatua za mwisho za maandalizi ya
ujenzi wa kiwanda cha kusarifu mwani Zanzibar na hivi karibuni Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar inategemewa kutia saini makubaliano ya ujenzi huo kati yake na Kampuni
kutoka Indonesia. Kamati inaamini kwamba kuwepo kwa kiwanda hicho kutainua soko
la zao hilo, kuimarisha maisha ya wakulima wetu pamoja na kuiongezea mapato Serikali
yetu.
CHANGAMOTO
1. Bei ndogo ya mwani ambayo hailingani kabisa na uzito wa kazi yenyewe na ukali
wa maisha unaowakabili wakulima.
2. Upungufu mkubwa wa vifaa unaopelekea baadhi ya wakulima kukopa vifaa hivyo
vikiwemo kamba za kufungia mwani bahari na mitaimbo ya kutobolea miamba.
3. Ukosefu wa vyombo vya kupakilia mwani (vihori) kwa ajili kubebea mwani
kutoka baharini kuja nao nchi kavu.
4. Kilimo cha mwani kimekumbwa na wadudu waharibifu ambao huathiri mwani na
kupelekea upungufu wa mapato kwa wakulima.
5. Uhaba wa maeneo ya kuendeshea shughuli za mwani kutokana na kujengwa kwa
mahoteli katika fukwe ambazo wakulima wa mwani walizitumia kwa ajili ya
kuanikia mwani. Hii inatokana na ukweli kwamba ujenzi wa Mahoteli
haujazingatia mpango wa ujenzi wa kuacha mita thelathini kutoka ufukwe wa
bahari.
6. Ushiriki mdogo wa vijana kwenye kilimo cha mwani unaotokana na mapato
yasiyoridhisha kwa wakulima na kushawishika zaidi kuingia kwenye sekta ya
utalii.
7. Bado boti za kubebea mwani hazijananunuliwa wala hazijapangiwa fungu lake
kama ilivyoelekezwa katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwamba kutanunuliwa
boti 500.
8. Kufanyiwa hadaa na baadhi ya masheha kwa kuwalazimisha kutoa kodi
iliyokuwa haina utaratibu unaoeleweka wanapomaliza mavuno ya mwani na
kuusafirisha kwa gari.
Ripoti ya Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo inayotokana na ufuatiliaji utekelezaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Biashara na Viwanda pamoja na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2018/2019. 41
MAONI, USHAURI NA MAAGIZO YA KAMATI
1. Kutokana na kilio kikubwa cha wakulima wa mwani nchini, Kamati inaiomba
Serikali kuu kupitia Wizara ya Kilimo na Wizara ya Biashara kuandaa utaratibu
maalum wa kusimamia uzalishaji, ununuzi na uuzaji wa zao la mwani kwa njia
zitakazowanufaisha wakulima kama lilivyo zao la karafuu.
2. Wizara iendelee kufanya tafiti ili kujua aina za mwani zinazostawi nchini mwetu
na zinazoweza kuzalishwa kwa kiwango kikubwa na wakulima wetu.
3. Kamati inaishauri Wizara ya kilimo na Wizara ya Biashara kujenga viwanda vya
mwani ili kuongeza thamani ya zao hilo na kuwapatia tija wananchi.
4. Kamati inaiomba Wizara kuwashirikisha wakulima wa mwani na wananchi wa
maeneo ya uwekezaji kwenye vikao vya maamuzi vinavyofanywa baina yake na
wawekezaji ili kuwa na makubaliano ya pamoja kwa maslahi ya pande zote.
5. Kamati inaishauri Wizara kuwahamasisha wakulima wa mwani kuanzisha biashara
nyengine kupitia vikundi vyao ili kujikwamua na hali ngumu ya maisha,
6. Kamati inaiomba Serikali kuongeza fungu la bajeti kwa Idara ya Maendeleo ya
Uvuvi na Mazao ya Baharini ili iweze kujinunulia vifaa na madawa ya kuwapatia
wakulima kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa mwani wa kiwango na ubora
unaokubalika.
7. Kamati inapendekeza kwamba kiwanda cha mwani kijengwe kusini Unguja kwani
ndio sehemu yenye wakulima wengi na uzalishaji mkubwa wa mwani.
8. Wizara iwaandae wakulima wa mwani kwa kuwatengenezea mazingira bora ya
kulima mwani wa kisasa ili waweze kukidhi mahitaji ya kiwanda
kitakachojengwa.
3.18 SOKO LA SAMAKI NA MBOGA MBOGA - TUMBE
Soko la Samaki na mboga mboga - Tumbe lilianza kujengwa mwaka 2011 chini ya
ufadhili wa MACEMP (kupitia Kampuni ya ujenzi ya Ngogo iliyopo Iringa Tanzania Bara)
kwa gharama ya Shilingi 1,074,881,077 na kufunguliwa rasmi na Mheshimiwa Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein mwaka 2015.
Kwa bahati mbaya, baada ya kutumika kwa miezi miwili soko hilo likakumbwa na
migogoro kadhaa kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Micheweni na Wavuvi wa maeneo
hayo iliyochangiwa zaidi na itikadi za kisiasa. Hadi kufikia 2017, Soko likaanza tena
kutumika likiwa chini ya usimamizi wa Kamati ya Maendeleo ya Uvuvi, Halmashauri ya
Wilaya ya Micheweni na Kamati ya Soko.
Kamati ilitembelea Soko hilo mwezi wa Agosti, 2018 na kukuta changamoto nyingi
zinazolikabili ikiwa ni pamoja na kutoingizwa ndani ya soko mashine ya kuzalishia baridi
ya kuhifadhia Samaki kwa takriban miaka minane. Hali hiyo ilisababishwa na mlango wa
kupitishia kuwa mdogo ukilinganisha na mashine husika. Vile vile kulikuwa na tatizo la
kutoingia vizuri hewa safi ndani ya soko kutokana na kuwepo madirisha na bati
lisilopitisha mwangaza, ukosefu wa sehemu kubwa ya kuuzia samaki (Mnada) kwani
eneo lipo la kutosha lakini bado halijatengenezwa na kuwekwa sawa. Pia soko lilikuwa
Ripoti ya Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo inayotokana na ufuatiliaji utekelezaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Biashara na Viwanda pamoja na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2018/2019. 42
na ukosefu wa maji kutokana na kuondolewa huduma hiyo na ZAWA kwa madai ya
kushindwa kufanya malipo.
Kamati inampongeza Afisa Mdhamini wa Wizara ya Kilimo kwa kuisimamia Idara ya
Maendeleo ya Uvuvi na kutekeleza ushauri wa Kamati kivitendo kwa kukamilisha zoezi
zima la kuweka ndani mashine ya barafu na kuuza barafu hiyo kwa wavuvi.
CHANGAMOTO
1. Ukosefu wa mikopo kwa wavuvi itakayowasaidia kununua mashine za boti na
kuongeza kipato katika uvuvi wao.
2. Kukosekana kwa mshauri wa matumizi bora ya soko hilo, vyanzo vya mapato na
ugawaji wake.
3. Uwezekano wa kumudu kuihudumia mashine kubwa ya kuzalisha barafu. Pamoja
na kuwepo mafundi kutoka Tanzania Bara wanaoiendesha mashine hiyo kwasasa,
mahitaji ya kuwepo wataalamu wazalendo ni lazima. Kwa vile mashine ni kubwa
sana na ya pekee kwa Zanzibar ambayo inahitaji fedha na uangalifu wa hali ya
juu.
4. Mahitaji makubwa ya fedha kulipia umeme kwani mashine inatumia “unit” 15
kwa saa moja.
MAONI, USHAURI NA MAAGIZO WA KAMATI
1. Wizara ya Kilimo ihakikishe inawapatia utaalamu wafanyakazi watakaoendesha
mashine ya kuzalishia barafu na ubaridi wa kuhifadhia Samaki.
2. Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Micheweni
ihakikishe inaweka utaratibu mzuri wa kulipa gharama za matengenezo pamoja na
umeme wa mashine ya barafu.
3. Kamati inaiagiza Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya
Micheweni itafute chombo maalum cha uokozi kwa wavuvi watakaopata ajali
baharini.
4. Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na Afisi ya Halmashauri ya Wilaya ya
Micheweni iandae utaratibu wa kuwapatia mikopo wavuvi itakayowasaidia
kununua mashine za boti na kuongeza kipato katika uvuvi wao.
5. Kamati inaishauri Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya
Micheweni kutafuta mtaalamu wa kuwashauri juu ya matumizi bora ya soko hilo,
vyanzo vyake vya mapato na ugawaji wake.
6. Kamati inazitaka Kamati za uvuvi nchini kuunganisha nguvu zao na kutatua
changamoto zinazowakabili wavuvi wote kwa ujumla.
Ripoti ya Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo inayotokana na ufuatiliaji utekelezaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Biashara na Viwanda pamoja na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2018/2019. 43
7. Ili kuendeleza masoko nchini, Kamati inawataka madalali kuwa waadilifu na
kuhakikisha fedha zinaingia kwenye mfuko wa soko kama zilivyopangwa na
kutumika kwa ajili ya utoaji huduma za soko.
8. Kamati inashauri Serikali za Wilaya kusimamia vyema taratibu za uendeshaji wa
masoko nchini.
3.19 WAKALA WA SERIKALI WA HUDUMA ZA MATREKTA NA ZANA ZA KILIMO
Serikali ya awamu ya kwanza chini ya Uongozi wa Marehemu Mzee Abeid Aman
Karume, iliweka azma ya kukiendeleza kilimo kwa kutumia Matrekta kwa lengo la
kuwaondoshea njaa wananchi wake kwa kuwaandalia mazingira mazuri ya uhakika wa
chakula na lishe bora, kuwapunguzia umasikini na kuongeza pato la mtu mmoja mmoja
na Taifa kwa ujumla na kufikia nchi yenye uchumi wa kati. Kulipa nguvu suala hilo,
ilinunua matrekta hamsini ya awali. Mwaka 1966, Karakana ya Matrekta iliundwa
Mbweni na mwaka 2017, Wakala wa Serikali wa Huduma za Matrekta na Zana za
Kilimo kupitia Hati iliyosainiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein iliundwa ikiwa pamoja na mengine
inatekeleza azma ile ile ya Rais wa Kwanza ya kukiendeleza kilimo cha Matrekta
Zanzibar.
Wakala una wafanyakazi 127 (Unguja 96 na Pemba 31) wengi wao wapo katika hatua ya
kukaribia kustaafu. Wakala una matrekta 74 (Unguja 47 na Pemba 27) ya aina ya ”New
Holland, Mahindra & Mahindra na Massey Ferguson ambapo matrekta 34 ni mazima na
yanaendelea kufanya kazi vizuri (Unguja 24 na Pemba 10), matrekta 27 mabovu lakini
yanaweza kutengenezeka (Unguja 18 na Pemba 9) wakati matrekta 13 mabovu wala
hayawezi kutengenezeka (Unguja 5 na Pemba 8).
Lengo kuu la Wakala ni kutoa huduma bora za matrekta kwa Wakulima wetu kwa
kununua vipuri kwa ajili ya kuyafanyia matengenezo matrekta mabovu ambayo
yanaweza kutengenezeka. Tokea Wakala uanzishwe ulikuwa unaongozwa na Tangazo la
Kisheria ”Legal Notice” ambapo ulipelekea kukabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo
upungufu wa fedha, vifaa na vitendea kazi pamoja na upungufu mkubwa wa
wafanyakazi, Ili kupunguza na ikibidi kuondosha baadhi ya changamoto, kwa
kushirikiana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, Wizara ya Kilimo tayari imekamilisha
Mswada wa kuanzisha Wakala wa Serikali wa Huduma za Matrekta na Zana za Kilimo
(Government Agency for Tractors and Farm Machineries Services) 2018 na katika
mkutano huu utasomwa kwa mara ya pili.
Ripoti ya Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo inayotokana na ufuatiliaji utekelezaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Biashara na Viwanda pamoja na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2018/2019. 44
CHANGAMOTO
1. Ufinyu wa bajeti unaoukabili wakala husababisha ucheleweshaji wa utoaji wa
huduma kwa wakati, kwa ufanisi na kwa utaratibu unaokubalika.
2. Wafanyakazi wengi wa Wakala wanakaribia umri wa kustaafu na utalaamu wao
hauendani na mahitaji ya sasa.
3. Uchakavu wa vifaa, mashine, vitendea kazi na miundombinu ya majengo na
maeneo ya kutendea kazi ya Wakala unapelekea kuwa na gharama kubwa za
uendeshaji.
4. Kuchelewa kulimiwa na kuburugiwa kwa wakulima wa mpunga
kunakosababishwa zaidi na kuchelewa kufanyiwa matengenezo matrekta kabla ya
msimu kuanza.
5. Kutotumika ipasavyo kwa baadhi ya mashine (Mashine ya kuchongea) kwa vile
siku hizi watu huwa hawachongi vifaa vya gari zao isipokuwa huwa wananunua
vilivyotumika (Used items).
6. Ukosefu wa zana za kisasa za kilimo kwa wakulima wetu jambo ambalo
limepelekea kushuka kwa kiwango cha uzalishaji wa mazao ya kilimo.
7. Baadhi ya vifaa vya kuonea na kuchomea “welding” vimeharibika na kuathiri
utendaji na afya za wafanyakazi.
8. Karakana haina usafi wa kutosha kwani baadhi ya sehemu zimezongwa na
mabuibui.
9. Mwamko mdogo wa wananchi kuhusu kuchangia huduma za trekta za shilingi
30,000 kwa kulima na shilingi 30,000 kwa kuburuga.
MAONI, USHAURI NA MAAGIZO YA KAMATI
1. Kutokana na umuhimu wa Wakala huu, Kamati inaishauri Serikali kuipatia fungu
lake la fedha.
2. Kwa kushirikiana na Bodi ya Wakurugenzi, Wizara iwasilishe maombi ya ajira za
wafanyakazi wapya Serikalini ili kufanya kazi za wakala kwa ufanisi.
3. Kamati inautaka Wakala uhakikishe unavifanyia matengenezo vifaa chakavu,
mashine pamoja na miundombinu ya majengo.
4. Wizara ihakikishe inatangaza zabuni ya ununuzi wa vipuri vya matrekta mapema
iwezekanavyo ili matrekta yawahi kutengenezwa na wananchi wawahi kulimiwa
na kuburugiwa maeneo yao kwa wakati unaotakiwa.
5. Wakala wa Matrekta Pemba ihakikishe inachukua juhudi ya kusafisha na kuondoa
taka zote zilizopo katika Karakana ya wawi.
6. Wizara ihakikishe Matrekta mabovu yanatengenezwa haraka ili yawahi
kuwatumikia wananchi bila ya kuchelewa muda wa kuchimbua na kuburuga
maeneo ya wananchi.
7. Wizara ihakikishe inaipatia Wakala zana za kisasa za kufanyia kazi.
Ripoti ya Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo inayotokana na ufuatiliaji utekelezaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Biashara na Viwanda pamoja na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2018/2019. 45
8. Wizara kupitia Wakala wa Matrekta iwahamasishe wananchi kuhusu kuchangia
huduma za malipo ya trekta.
9. Kamati inautaka Wakala kuihimiza Kampuni ya “Luma international Ltd.”
iliyoshinda zabuni ya kununua vifaa vya mategenezo vya Wakala kuviwasilisha
kabla ya wakati wa kulima kumalizika.
Ripoti ya Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo inayotokana na ufuatiliaji utekelezaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Biashara na Viwanda pamoja na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2018/2019. 46
4. WIZARA YA BIASHARA NA VIWANDA
Katika awamu hii ya ushajiishaji maendeleo kupitia uchumi wa viwanda Tanzania na
Zanzibar kwa ujumla, Wizara ya Biashara na Viwanda imebeba mzigo huo kuhakikisha
inapanga mipango madhubuti itakayowesha upatikanaji wa Viwanda hususan
vinavyoendana na maumbile na mazingira ya kisiwa chetu. Ili kufanikisha hilo, Wizara
imeandaa Programu Kuu nne zifuatazo kwa lengo la kututoa hapa tulipo na kuelekea
katika uchumi wa kati unaotegemea zaidi viwanda.
a) Programu kuu ya Uendeshaji na Uratibu wa Wizara ya Biashara na Viwanda;
b) Programu kuu ya Maendeleo ya Viwanda na Ujasiriamali;
c) Programu kuu ya Ukuzaji na Uendelezaji wa Biashara;
d) Programu kuu ya Viwango na Tathmini ya Ubora;
Programu hizo zinatekelezwa na Wizara ya Biashara na Viwanda kupitia Taasisi au Idara
zifuatazo:
i. Idara ya Mipango, Sera na Utafiti;
ii. Idara ya Uendeshaji na Utumishi;
iii. Idara ya Biashara na Ukuzaji Masoko;
iv. Idara ya Maendeleo ya Viwanda na Ukuzaji Ujasiriamali;
v. Shirika la Biashara la Taifa (ZSTC);
vi. Baraza la Kusimamia Mfumo wa Utoaji Leseni (BLRC);
vii. Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS);
viii. Baraza la Taifa la Biashara Zanzibar;
ix. Tume ya Ushindani Halali wa Biashara na Kumlinda Mtumiaji (FCC);
x. Wakala wa Maendeleo ya Viwanda Vidogo Vidogo, Vidogo na vya Kati
(SMIDA);
xi. Wakala wa Usajili wa Biashara na Mali Zanzibar (PBRA); na
xii. Afisi Kuu - Pemba.
4.1 UTEKELEZAJI WA PROGRAMU KUU ZA WIZARA
Kwa mwaka wa fedha 2018/2019, Wizara ya Biashara na Viwanda iliidhinishiwa
matumizi ya jumla ya shilingi 11,363.8 milioni ambapo kwa kipindi cha Julai hadi
Disemba jumla ya shilingi 3544.22 milioni ziliingizwa na kutumika. Kwa upande wa
mapato, jumla ya shilingi 1,513.061 milioni zilikadiriwa kukusanywa na Wizara kwa
mwaka wa fedha 2018/2019.
4.2 PROGRAMU KUU YA MAENDELEO YA VIWANDA NA UJASIRIAMALI
Programu hiyo imekusudia kuongeza pato la sekta ya uzalishaji viwandani pamoja na
kuimarisha mazingira mazuri ya maendeleo ya Wajasiriamali wadogo na wakati.
Utekelezaji wa Programu hiyo unafanywa na Idara ya Viwanda na Wakala wa
Maendeleo ya Viwanda Vidogo Vidogo, Vidogo na vya Kati (SMIDA). Miongoni mwa
mambo ambayo yametekelezwa na Programu hiyo na Kamati kuyatolea ushauri ni:
Ripoti ya Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo inayotokana na ufuatiliaji utekelezaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Biashara na Viwanda pamoja na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2018/2019. 47
4.3 KIWANDA CHA KUSARIFU TUNGULE
Hichi ni kiwanda cha wajasiriamali kinachomilikiwa na kikundi cha “Gando
Enterpreneurship Program (GEP)” chenye wanachama 948 waliopo katika maeneo
tofauti kisiwani Pemba. Kikundi hichi kilianza mwaka 2012 kwa uendelezaji wa shughuli
za kilimo zilizolenga kuwatoa wajasiriamali kwenye kilimo cha matumizi ya nyumbani na
kuanzisha kilimo cha biashara. Hadi Kamati ilipowatembelea, jumla ya vikundi 55
vimeendelezwa chini ya mwamvuliwa wa GEP. Bidhaa wanazozalisha ni pamoja na
tomato, chili “sauce”, jamu, sabuni za maji, “lotion” na mafuta ya mgando. Kikundi
kimefanikiwa kupata mashine za kusarifu tungule kupitia mradi wa MIVARF ambapo
walichangia asilimia 25 na Mradi kutoa asilimia 75 zilizobakia. Kikundi hicho kina
mpango wa kujenga chumba cha kuhifadhia tungule ili ziweze kukaa kwa muda mrefu
bila ya kuharibika.
Kuwepo kwa GEP kumepelekea kupatikana umoja wa wajasiriamali wadogo, kuinua
pato la mwananchi mmoja mmoja, kuzalisha fikra za pamoja kati ya wajasiriamali na
kuwaweka pamoja wajasiriamali na taasisi mbalimbali za Serikali kama ZBS na Wizara ya
Biashara na Viwanda. Kutokana na jitihada zilizooneshwa na wajasiriamali hao, kuna
umuhimu mkubwa kwa Wizara ya Biashara na Viwanda kuwasaidia hata kwa kuwapatia
mikopo kwani uwezo wa kulipa wanao. Ni busara kwa Serikali kurahisisha upatikanaji
wa vifungashio nchini ili kupunguza gharama za usafiri na ushuru. Hatua hio ni muhimu
katika kuwajengea uwezo Wajasiriamali wadogo kuzalisha kwa gharama nafuu na hivyo
kuwawezesha kumudu ushindani wa biashara uliopo sokoni.
CHANGAMOTO
1. Upungufu wa mtaji hususan wa uendeshaji wa kiwanda cha kusarifu tungule.
Mara kadhaa kikundi hicho hukosa fedha hata za kununulia malighafi (tungule).
2. Ukosefu wa jengo la kisasa litakalowawezesha kufikia kiwango cha kiwanda
kinachostahiki kuzalisha bidhaa mbalimbali zikiwemo za chakula.
3. Kutokamilika matengenezo chumba cha baridi (coldroom) kunapelekea uzalishaji
wa bidhaa zao kusita mara tu msimu wa tungule unapomalizika.
4. Kiwanda kinakabiliwa na ushindani wa kibiashara na wazalishaji wakubwa.
5. Kukabiliwa na gharama kubwa za ununuzi vifungashio kutoka Tanzania Bara au
Nairobi.
MAONI, USHAURI NA MAAGIZO YA KAMATI
1. Kamati inaiomba Serikali iandae mkakati maalum wa kuwapatia vifungashio hivyo
nchini ili angalau wapunguze gharama za usafirishaji.
2. Kamati inaitaka Wizara ya Biashara na Viwanda kwa kushirikiana na taasisi
nyengine za Serikali na wadau binafsi wawe wabunifu wa kutafuta mwendelezo
wa mradi (project sustainability) ili kuyaendeleza yale mazuri yanayoanzishwa na
mradi husika.
Ripoti ya Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo inayotokana na ufuatiliaji utekelezaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Biashara na Viwanda pamoja na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2018/2019. 48
3. Kikundi kichukue juhudi za kujitangaza ili kiweze kutambulika na kupata soko la
bidhaa kinazozalisha.
4.4 KIWANDA CHA SUKARI CHA MAHONDA
Kiwanda cha sukari cha Mahonda kilianzishwa miaka ya 1960 chini ya usimamizi wa
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China. Kwa kipindi
cha takriban miaka 15 kiwanda kilikuwa hakifanyi kazi. Mwaka 2015, kiwanda hicho
kilitengenezwa kwa kuwekwa mashine mpya na za kisasa zilizopelekea uzalishaji
kuongezeka hadi kufikia tani 400 kwa mwezi ambazo zilizokuwa zikiongezeka maradufu
siku hadi siku na kufikia tani 800. Kiwanda kina uwezo wa kuzalisha hadi tani 1,250
kutegemeana na upatikanaji wa malighafi. Katika kutekeleza azma ya Serikali ya
kukifufua kiwanda hicho, Serikali iliahidi kukipatia kiwanda ardhi ya kutosha ya hekta
6,644 kwa ajili ya kuzalisha malighafi ya miwa pamoja na kuhakikisha soko la sukari
itakayozalishwa linapatikana.
Baada ya kumaliza matengenezo na kuanza kazi, kiwanda kilikabiliwa na changamoto
kubwa ya kuwepo tani nyingi za sukari kiwandani pasi na kupata soko. Serikali ilikuja na
maamuzi ya busara ya kuzuia uvamizi usiokuwa na tija katika biashara ya Sukari kwa
kuchagua wafanyabiashara sita wakubwa Zanzibar waliopewa kibali cha kuleta Sukari
Zanzibar. Matokeo yake takriban tani 6,000 zilizokuwepo, tani 5,600 zimeshanunuliwa
na kubakia tani 400 kwa sasa. Miongoni mwa mafanikio yaliyopatikana kwamba Serikali
imepata kodi ya zaidi ya shilingi 1.3 milioni na kuajiri Wazanzibari zaidi ya 800 kwa ajira
ya moja kwa moja na ajira isiyokuwa ya moja kwa moja kiwandani.
CHANGAMOTO
1. Kiwanda kutopatiwa ardhi ya kutosha kama ilivyoahidiwa na Serikali.
2. Kuyumba kwa soko la sukari kwani kuna tani 400 kwasasa zimebakia ghalani.
3. Bado kuna wafanya biashara wanakwepa kununua sukari katika kiwanda hicho.
4. Nyumba ambazo Kiwanda imepewa na Serikali zilikuwa mbovu na haziko katika
hali nzuri. Baadhi ya nyumba hizo milango ilikuwa ishatolewa.
5. Kiwanda hakijakabidhiwa nyumba zake ambazo Serikali iliamua wakabidhiwe
lakini baadhi ya nyumba hizo bado zinakaliwa na watu wengine.
6. Uelewa mdogo wa Wakulima wanaoshughulikia ukataji miwa katika mashamba
ya Kiwanda.
Ripoti ya Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo inayotokana na ufuatiliaji utekelezaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Biashara na Viwanda pamoja na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2018/2019. 49
MAONI, USHAURI NA MAAGIZO YA KAMATI
1. Wizara ihakikishe inakipatia Kiwanda ardhi ya kutosha kama ilivyoahidiwa na
Serikali.
2. Wizara ihakikishe inaipatia soko sukari inayozalishwa Mahonda kwani mpaka
Kamati inatembelea kiwanda hicho kuna tani 400 zilikuwa zimebakia ghalani.
3. Wizara iwapatie Wakulima wa miwa elimu ya msingi itakayowawezesha
kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kupelekea kupata mavuno bora kwa
maslahi yao, kiwanda na Taifa kwa ujumla.
4.5 ZIARA YA KAMATI KATIKA VIWANDA VYA KUSAGA UNGA, KUCHAKATA NA
KUTENGENEZA JUISI YA EMBE - MKURANGA NA MWANDEGE.
Kamati ya fedha, Biashara na Kilimo ilipata fursa ya kutembelea viwanda tofauti
vinavyosimamiwa na “Bakhresa Group of Companies”, vikiwemo Kiwanda cha unga
kilichopo Mtoni Unguja kilichoanzishwa mwaka 1990 na kufufuliwa upya mwaka 2010,
Kiwanda cha kuzalisha unga kilichopo Buguruni (TAZARA) kilianzishwa mwaka 1983 na
viwanda vya kuchakata na kutengeneza juisi ya embe viliopo Mkuranga Mwandege na
Vingunguti. Lengo la ziara hiyo ni kuongeza uelewa juu ya uzalishaji wa viwanda vyetu
vya ndani kuelekea kwenye uchumi wa viwanda. Kamati inaamini kwamba kujifunza
kwa kuona itajenga uwezo wa kuchukua mazuri yaliyojitokeza, changamoto
wanazokabiliana nazo na njia wanazitumia kukabiliana na changamoto hizo ili waweze
kuishauri Wizara husika njia bora za kuendeleza viwanda nchini kwa maslahi ya Taifa
letu.
Kamati imeelezwa kuwa viwanda vyote vya Kampuni ya Bakhresa viliopo Kipawa,
Mzizima, Buguruni na Zanzibar vinauwezo wa kuzalisha zaidi ya tani 3,000 za unga kwa
siku ambavyo vimetoa ajira kwa Watanzania wengi na kupunguza mzigo wa upungufu
wa ajira nchini.
Kwa upande wa viwanda vya kuchakata na kutengeneza juisi ya embe hutumia embe
aina ya Dodo, Boribo na Viringe kutengenezea juisi. Embe hizi hupatikana kwa wingi
Bagamoyo, Mtwara, Lindi, Rufiji, Dodoma, Tabora, Tanga na Moshi. Kiwanda
kinashindwa kuchukua embe kutoka Zanzibar kwa sababu huwa zina wadudu wengi
jambo ambalo linaweza kuhatarisha usalama wa bidhaa wanayoitengeneza pamoja na
watumiaji bidhaa hiyo. Baadhi ya wakati watendaji wa kampuni huwatembelea
wakulima na kuwapatia mbegu na utaalamu utakaowasaidia kulima kwa ufanisi na
kupata mavuno bora.
Kiwanda cha Bakhresa kilichopo Maruhubi ni miongoni mwa viwanda vya mwanzo vya
Bakhresa kilichokuwa kikizalisha mtindi na samli. Mwaka 1990, kiwanda hicho kilifungwa
kwa ajili ya kufanyiwa matengenezo na mwaka 2010 kilifunguliwa upya na kujikita na
uzalishaji wa unga wa ngano pekee. Kiwanda hicho kimeajiri wafanyakazi 125 hadi 130
na kinauwezo wa kuzalisha tani 1,020 kwa siku.
Ripoti ya Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo inayotokana na ufuatiliaji utekelezaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Biashara na Viwanda pamoja na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2018/2019. 50
CHANGAMOTO
1. Kutokana na udogo wa Bandari yetu, meli kubwa za mizigo hushindwa kufika
nchini na kusababisha Serikali kukosa mapato tuliyojipangia.
2. Kuwepo kwa utitiri wa kodi wanazolipa wafanyabiashara na wawekezaji nchini.
Kuna takriban kodi tisa wanazolipa wafanyabiashara hao zikiwemo ZRB, TRA,
ZFDA, ZBS, Mkemia Mkuu, Ofisi ya ‘Atomic Energy’, ZIPA, Kamisheni ya Kazi
pamoja na Manispaa. Ni jambo la kushangaza kwamba baadhi ya kodi hizo
zinaingiliana na kuwapa wakati mgumu wawekezaji nchini.
3. Matumizi mabaya ya msamaha wa kodi unaotolewa na Serikali kwa bidhaa
muhimu za chakula kwa kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Wafanyabiashara wengi huitumia fursa hii kuingiza bidhaa hizo kwa wingi na
kuuza kwa bei ya kawaida mara tu baada ya kumalizika mwezi huo. Kitendo
hicho huwapatia faida kubwa wafanyabiashara hao na kuwapa changamoto
kubwa wazalishaji wa ndani.
4. Ukosefu wa wafanyakazi kutoka Zanzibar katika baadhi ya fani ikiwemo fani ya
ufundi wa mfumo wa umeme katika mashine na kupelekea kiwanda kuchukua
wataalamu kutoka nje ya Zanzibar, hali hiyo huwaongezea gharama za uzalishaji.
5. Kukatika umeme mara kwa mara bila ya taarifa kunawasababishia usumbufu wa
kuzianzisha upya mashine.
6. Kutokupewa virutubisho vya unga kutoka Serikalini.
7. Kuvamiwa kwa malori ya kiwanda na wakaazi wa maeneo ya karibu wakati wa
kuingiza ngano.
MAONI, USHAURI NA MAAGIZO YA KAMATI
1. Ni vyema Wizara ya Biashara na Viwanda ikakaa na Wizara ya Elimu na Mafunzo
ya Amali kuangalia uwezekano wa kuwasomesha vijana wetu fani ya ufundi wa
mfumo wa umeme katika mashine ili waweze kumudu ushindani uliopo Afrika
Mashariki na kwengineko.
2. Wizara ya Biashara na Viwanda ianzishe utaratibu wa kuwapatia ruzuku ya
virutubisho wamiliki wa Viwanda vya unga.
3. Wizara ishirikiane na Taasisi za kodi ili waweze kuandaa utaratibu wa malipo ya
kodi katika Taasisi moja (one stop center). Hili litawapunguzia muda
wafanyabiashara na kukuza faida zao.
4. Wizara kwa kushirikiana na Taasisi za kodi iandae vipeperushi vitakavyotoa taarifa
za mabadiliko ya vielelezo anavyotakiwa mfanyabiashara aende navyo katika
Taasisi za Kodi wakati wa kuongeza muda leseni yake.
4.6 PROGRAMU KUU YA VIWANGO NA TATHMINI
Programu hiyo imekusudia kuandaa na kuimarisha viwango ili kumlinda mtumiaji.
Utekelezaji wa Programu hiyo unafanywa na Taasisi ya viwango Zanzbar. Miongoni
mwa mambo ambayo yametekelezwa na Programu hiyo na Kamati kuyatolea ushauri ni:
Ripoti ya Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo inayotokana na ufuatiliaji utekelezaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Biashara na Viwanda pamoja na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2018/2019. 51
4.7 TAASISI YA VIWANGO ZBS PEMBA
Taasisi ya Viwango ni miongoni mwa vyombo muhimu Zanzibar vilivyoanzishwa kwa
lengo la kukagua na kudhibiti ubora wa vifaa na vyakula viliopo au vinavyoingizwa
Zanzibar kutoka nje. Chombo hicho kimeundwa na sheria Nambari 1 ya mwaka 2011.
Kwa upande wa Pemba, Taasisi hiyo ina Ofisi tatu (Mkoani, Chake chake na Wete)
pamoja na wafanyakazi watano ambapo wawili ndio wataalamu wa ukaguzi
wanaofanya kazi katika Bandari ya Wete na Mkoani.
Kamati imesikitishwa na uchache wa watendaji wa Taasisi hio kwa upande wa Pemba
ikizingatiwa kwamba wafanyakazi hao wanatakiwa kufanya kazi kwenye bandari zote za
Pemba bila ya kuwa na usafiri wa uhakika wa kuwafikisha kwenye maeneo yao ya kazi.
Hali hiyo hupelekea uwezekano wa kuingia bidhaa zisizokua na ubora kisiwani humo
hususan wakati wa usiku.
Kwa upande wa ZBS Wete, Taasisi imepewa sehemu ndani ya jengo la Shirika la Bandari
wakati ZBS Mkoani imepewa Ofisi katika jengo la ZTC ambalo linafanya kazi zake kwa
mujibu wa sheria. Kwa upande wa Chake chake wanayo Ofisi wanayoendelea kuifanyia
matengenezo itakayotumika kama Ofii kuu ya ZBS Pemba. Sambamba na ufinyu wa Afisi
za kufanyia kazi, ZBS inakabiliwa na uchache wa vifaa vya kufanyia ukaguzi ikiwemo
mtandao wa intaneti unaowawezesha kuwasiliana na Taasisi nyengine na viwango
duniani.
CHANGAMOTO
1. Ufahamu mbaya wa wananchi kuhusu majukumu ya ZBS yanagongana na ZFDA.
2. Ukosefu wa baadhi ya vifaa muhimu na vya msingi katika upimaji wa bidhaa
tofauti zikiwemo mafuta ya ‘service’ za gari, vifaa vya kupimia ubora wa mipira
ya gari, vifaa vya ujenzi pamoja na bidhaa za vyakula.
3. Kuwepo kwa baadhi ya bidhaa hadi leo zinatumia alama ya ubora ya sehemu
nyengine ikiwemo TBS ya Tanzania Bara wakati bidhaa hizo zinazalishwa na
kutumika Zanzibar.
4. Uhaba wa wafanyakazi na udogo wa Ofisi.
5. Ukosefu wa fedha za utekelezaji wa malengo yao kwani fedha wanayoiomba
huwa haipatikani kwa asilimia mia moja.
6. Gharama kubwa za upatikanaji wa nembo ya ubora ya ZBS kwa wajasiriamali.
MAONI, USHAURI NA MAAGIZO YA KAMATI
1. ZBS ihakikishe inatoa mafunzo kwa wananchi kuwaelewesha tofauti iliyopo na
mipaka yake kiutendaji na ZFDA kwani kidhahania wananchi wanaona Taasisi
hizo zinafanya kazi zinazofanana.
Ripoti ya Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo inayotokana na ufuatiliaji utekelezaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Biashara na Viwanda pamoja na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2018/2019. 52
2. Wizara ya Biashara na Viwanda kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango
ihakikishe inaipatia ZBS fedha za kutosha ili waweze kununua vifaa vya msingi
katika shughuli zao za ukaguzi na upimaji.
3. ZBS itoe taalum ya viwango vinavyoinishwa katika bidhaa tofauti ikiwemo saruji
ili iwaeleweshe wananchi pamoja na Waheshimiwa Wawakilishi matumizi sahihi
ya bidhaa hizo.
4. ZBS ipige marufuku bidhaa zinazozalishwa Zanzibar na kutumika Zanzibar
kutumia alama ya ubora isiyokuwa ZBS.
5. ZBS iwashauri wafanyabiashara kuwachukua maofisa wa wake kuwasaidia upimaji
au ukaguzi wa bidhaa hususan wanapoenda kununa ili kuepuka kununua bidhaa
isiyokidhi viwango na hatimae kuangamizwa au kurudishwa ilipotoka.
6. ZBS ifuatilie kwa karibu suala la ajira ya wafanyakazi wake wapya watatu na
kupeleka maombi mengine ya wafanyakazi kwa ajili ya Afisi ya Pemba.
4.8 PROGRAMU KUU YA UENDESHAJI NA URATIBU WA WIZARA
Programu hiyo imekusudia kutoa huduma za uendeshaji na manunuzi kwa ufanisi,
kufanya mapitio na kuoanisha sera za biashara, viwanda na kufanya utafiti pamoja na
kuratibu shughuli za Wizara Pemba. Utekelezaji wa Programu hiyo unafanywa na Idara
ya Mipango, Sera na Utafiti, Idara ya Uendeshaji na Utumishi na Afisi Kuu Pemba.
4.9 UONGOZI NA WATENDAJI WA WIZARA
Katika mwezi wa Agosti 2018, Kamati ilikutana na uongozi na watendaji wa Wizara na
kuarifiwa kwamba Wizara ya Biashara na Viwanda inao uwezo kwa mujibu wa sheria
kudhibiti bei ya baadhi ya bidhaa zikiwemo unga na sukari. Kwa nia njema, Wizara pia
hutoa msamaha wa kodi hususan katika mwezi Mtukufu wa Ramadhan kwa bidhaa ya
tende ili kuwapunguzia makali ya maisha wananchi wetu. Lakushangaza, msamaha huo
hutumika kama njia ya kuwanufaisha wafanyabiashara na familia zao. Kwa mantiki hiyo,
kuna haja kwa Wizara kuchukua maamuzi magumu ya kudhibiti vitendo hivyo kwa
kuzuia misamaha hiyo au kuruhusu baadhi ya wafanyabiashara chini ya usimamizi
maalum.
Hivi karibuni, wananchi wengi wameanza kujishughulisha na biashara ya dagaa na
kulisafirisha nchi jirani ili kijiongezea kipato. Kuwepo kwa shughuli hizo kumepunguza
kiwango cha utegemezi kwa kuajiri wananchi mbalimbali. Kamati imebaini kuwa
biashara ya dagaa ni yenye tija kubwa kwa wananchi wetu, lakini bado inakabiliwa na
tatizo la kukosa usimamizi wa vyombo vinavyohusika na kupelekea wajanja wachache
kufaidika zaidi kupitia nguvu za wananchi wetu. Hivyo, Kamati inaishauri Wizara
kuwapatia utaalamu wa njia bora za uanikaji wa dagaa vijana hao ili kuongeza thamani
na mapato yake.
Ripoti ya Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo inayotokana na ufuatiliaji utekelezaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Biashara na Viwanda pamoja na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2018/2019. 53
Wizara pia imesimamia uchumaji wa Karafuu na utoaji wa mikopo, ununuzi pamoja na
uuzaji wa Karafuu ndani na nje ya nchi yetu. Kwa mwaka 2017/18, jumla ya wachumaji
193 wameanguka katika mikarafuu ambapo 176 walianguka Pemba na waliobakia ni kwa
upande wa Unguja. Kati ya hao, wachumaji 152 tayari wameshalipwa fidia ambapo
jumla ya shilingi 106,530,000 zilitumika.
Kwa mwaka wa fedha 2017/18, jumla ya shilingi 191,000,000 milioni zilitolewa kwa
wachumaji Karafuu na hadi Kamati inatembelea Afisi ya Ofisa Mdhamini jumla ya shilingi
179,760,000 zililipwa sawa na asilimia 94 ya fedha zote na kubakia jumla ya shilingi
11,240,000 mikononi mwa wananchi ambao wengi wao walipata hasara kutokana na
mvua kubwa zilizowakabili hususan katika kipindi cha uvunaji. Pamoja na fedha nyingi
kupatikana kutokana na biashara ya karafuu lakini mzunguko wa fedha hizo ni mdogo
kwani hazionekani kuwekwa katika Benki zetu. Sambamba na hayo Kamati imeshauri
Wizara mambo yafuatayo:
CHANGAMOTO
1. Ukusanyaji mdogo wa mapato kupitia vyanzo vinavyosimamiwa na Wizara hii
ulikuwa chini kwa kipindi ambacho kamati ilipoitembelea.
2. Wakala wa Maendeleo ya Viwanda Vidogo Vidogo, Vidogo na vya Kati (SMIDA)
wamepatiwa fedha kidogo sana ukilinganisha na walichokiomba au mahitaji yao
kwani wameshindwa hata kuweka mazingira mazuri ya kufanyia kazi.
3. Kumekuwa na ongezeko kubwa la ushindani wa kibiashara nchini jambo ambalo
linarudisha nyuma wafanyabiashara wadogo wadogo.
4. Ukosefu wa usimamizi bora wa biashara ya dagaa.
5. Bado kuna baadhi ya wafanya biashara hawajarudisha fedha walizokopeshwa na
ZSTC.
6. Uhaba wa wafanyakazi katika shamba la Mtakata.
7. Ukosefu wa hatimiliki ya shamba la Mtakata.
8. ZSTC bado wanawalipa wafanyabiashara za uvunaji karafuu kwa fedha taslim.
Utaratibu wa aina hiyo husababisha wizi kutokea.
9. Wafanyabiashara hawahifadhi fedha zao Benki na kusababisha mzunguko mdogo
wa fedha pamoja na kuhatarisha usalama wao kwa kuvamiwa na kuibiwa.
10. Kutolipwa fidia kwa baadhi ya wachumaji karafuu walioanguka katika mikarafuu
MAONI NA USHAURI WA KAMATI
1. Wizara iandae mikakati madhubuti kuhakikisha ukusanyaji wa mapato
unaongezeka.
2. Wizara ihakikishe SMIDA inapatiwa fedha kama walivyopanga ili iweze kufikia
lengo la uchumi wa viwanda Zanzibar.
Ripoti ya Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo inayotokana na ufuatiliaji utekelezaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Biashara na Viwanda pamoja na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2018/2019. 54
3. Kamati inaishauri Wizara kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya wafanyabiashara
wote watakaobainika wanauza bidhaa zilizopitwa na wakati wa matumizi yake ili
kuwalinda wananchi wetu na madhara makubwa yanayoweza kuwapata.
4. Kamati inaishauri Wizara kuwaelimisha Wajasiriamali kujitangaza kwa kutumia
fursa za maonyesho yanayofanyika katika Maadhimisho ya Sherehe za Mapinduzi
ya Zanzibar za kila mwaka, siku ya Wakulima Sabasaba - Dar es Salaam na
yanayofanyika nje ya nchi.
5. Wizara iweke utaratibu mzuri wa uendeshaji wa biashara ya dagaa kwa upana
wake kwani inatoa ajira kwa wananchi wengi na ni biashara yenye tija.
6. Wizara ihakikishe inawalipa fidia wachumaji karafuu waliobakia ambao
walioanguka katika mikarafuu.
7. Wizara ichukue juhudi za makusudi kuhakikisha wafanyabiashara wa karafuu
wanafungua hesabu “account” Benki ya Watu wa Zanzibar.
8. Wizara kupitia ZSTC iwafuatilie wafanyabiashara ambao hawajarudisha fedha
walizokopeshwa kwa kuvuna karafuu.
9. Wizara ihakikishe hatimiliki ya shamba la Mtakata inapatikana.
10. Wizara ihakikishe wafanyakazi wa kutosha wanakuwepo katika shamba la
Mtakata.
4.10 JUMUIYA YA WAFANYABIASHARA, WENYE VIWANDA NA WAKULIMA
(CHAMBERS OF COMMERCE)
Jumuiya ya Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Wakulima ni moja ya Jumuiya
isiyokuwa ya Serikali yenye mchango mkubwa katika uimarishaji wa uchumi wa Zanzibar
kwa vile ndio chombo kikuu kinachoweza kuwaunganisha wafanyabiashara na wakulima
na kuwakutanisha na Serikali yao kushauriana kuhusu mambo ya msingi yatakayofanyiwa
kazi na kuleta tija nchini. Pamoja na mambo mengine, Jumuiya hiyo kwa upande wa
Pemba inakabiliwa na changamoto kubwa zifuatazo:
CHANGAMOTO
1. Kuwepo mapungufu katika Jumuiya hiyo kwa kutokuwa na nafasi ya muwakilishi
kutoka upande wa Pemba.
2. Utitiri wa kodi kwa Wajasiriamali wadogo zinazowasababishia kutopata
maendeleo ya biashara.
3. Kukosekana kwa wafadhili wanaochangia fedha kwa ajili ya maendeleo ya
Jumuiya hiyo.
4. Ukosefu wa Viwanda vidogo vya kusarifu mazao yanayozalishwa Zanzibar ili
yaweze kuhifadhiwa na kutumika kwa muda mrefu zaidi.
5. Wakulima wa mboga na mwani kutopatiwa ruzuku kutoka Serikalini kwa ajili ya
kuendeleza shughuli zao.
6. Ukosefu wa Afisi kwa Jumuiya ya Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Wakulima
Pemba.
Ripoti ya Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo inayotokana na ufuatiliaji utekelezaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Biashara na Viwanda pamoja na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2018/2019. 55
MAONI, USHAURI NA MAAGIZO YA KAMATI
1. Jumuiya ya Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Wakulima Pemba ipatiwe fursa
ya kuwa na wawakilishi kutoka Pemba.
2. Katiba ya Jumuiya hiyo irekebishwe na kuwepo kufungu kitakachoeleza Pemba
kuwa ni zoni.
3. Wajasiriamali wapunguziwe kodi ili waweze kumudu gharama za uendeshaji wa
biashara zao.
4. Jumuiya ihakikihe inajipanga vyema katika utekelezaji wa majukumu yao na sio
kutegemea wafadhili.
5. ZBS iweke gharama toshelevu itakayowawezesha Wajasiriamali kupata alama ya
ubora wa ZBS.
6. Wizara ihakikishe inaimarisha sekta ya Viwanda kwa kujenga viwanda vidogo
vidogo ili wananchi wapate ajira na soko la kuuzia bidhaa wanazozizalisha.
7. kama ilivyo katika karafuu, wakulima wa Mwani na mboga nao wapatiwe ruzuku
au mikopo.
8. Kuna haja yakufanya utafiti utakaobainisha wazi sababu zinazopelekea kufa kwa
miche ya Mikarafuu iliokuwa imeatikwa kinyume na mabotea.
9. Jumuiya ipatiwe Ofisi yake kwa upande wa Pemba ili viongozi waweze kukutana
na kuyatafutia maamuzi changamoto zinazojitokeza.
4.11 JUMUIYA ZA WAFUGAJI WA NYUKI
Katika mwezi wa Novemba, 2018 Kamati ilizitembelea Jumuiya za wafugaji wa nyuki na
vikundi vya kufuga nyuki vilivyotokana na Jumuiya hizo Unguja na Pemba. Kwa upande
wa Unguja, Kamati ilitembelea Jumuiya ya Wafugaji nyuki Zanzibar “ZABA” yenye Ofisi
yake kitogani ambayo ina jumla ya wanachama 194 illiyounganisha wafugaji wa nyuki
1,046 wa Unguja. Lengo la Jumuiya hiyo ni kutoa taaluma kwa wafugaji nyuki kuhusu
ufugaji wakisasa, kuhamasisha uzalishaji wa asali bora inayomfikia mlaji kwa kusarifiwa
kwa mashine na bila ya kuguswa kwa mkono. Chini ya ufadhili wa Jumuiya
inayojitegemea ya MLFM & CARIPLO ya Italy, jumuiya hiyo imejenga Ofisi yake ya
kisasa na kupatiwa baadhi ya vifaa vikiwemo mashine ya kukamulia, kuchujia na
kihifadhia asali.
Kuwepo kwa Jumuiya hiyo kumesaidia kuzaliwa kwa vikundi tofauti vya ufugaji nyuki
ikiwemo kikundi cha ukulima wa nyuki kiliopo Paje kiitwacho “Paje Woman Bee
Farmer” (PAWOBEFA) kilichoanzishwa mwaka 2016.
Kamati pia ilifika katika Jumuiya ya Wafugaji wa nyuki Pemba (PEBA) iliyopo
Machomane Pemba ambayo ilianzishwa mwaka 2013 na kupata usajili wake rasmi
mwaka 2014 ikiwa na wajumbe waanzilishi 20 (wanaume 15 na wanawake 5). Kwasasa
Ripoti ya Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo inayotokana na ufuatiliaji utekelezaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Biashara na Viwanda pamoja na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2018/2019. 56
Jumuiya ina wanachama 62 inayowaunganisha wafugaji nyuki wote waliopo Pemba
pamoja na kuwapatia mafunzo ya uendeshaji wa shughuli zao ikiwemo matumizi ya
miundombinu ya ufugaji wa nyuki wa kisasa ili waweze kupunguza umasikini na
kujiongezea kipato. Mwaka 2017, Jumuiya hiyo imekamilisha ujenzi wa Ofisi yak echini
ya ufadhili wa IFAD, kununua kompyuta moja, vifaa vya kisasa vya kutengenezea na
kupimia asali, nta pamoja na ununuzi wa nguo za kuvunia asali. Kwasasa Jumuiya inalo
soko la kutosha kwani wamepata mnunuzi anataka lita 5,000 za asali halisi. Licha ya
mafanikio hayo, Jumuiya inakabiliwa na changamoto zifuatazo:
CHANGAMOTO
1. Jumuiya hizo zina uhaba wa vitendea kazi ikiwemo pikipiki na gari za kufuatilia
wafugaji waliopo katika maeneo tofauti ya Unguja na Pemba, ‘rain boot’, na
masanduku ya kufugia nyunki.
2. kuwepo kwa wadudu waharibifu wanaoathiri asali kama vile sisimizi, siafu,
koyokoyo, uvi na mijusi, nondo kichwa, mbawa kavu na chawa wa nyuki.
3. Ukosefu wa elimu ya kutosha hususan kwa wanachama wao.
4. Uhaba wa rasilimali fedha.
5. Kuzuiliwa kwa masanduku na pikipiki za jumuiya na watendaji wa Wizara ya
Kilimo.
MAONI, USHAURI NA MAAGIZO YA KAMATI
1. Wizara kupitia SMIDA izisaidie Jumuiya hizo kwa kuwapatia mikopo
itakayowawezesha kukuza mtaji na kununulia baadhi ya vitendea kazi.
2. Wizara ya Biashara na Viwanda ikutane na Wizara ya Kilimo kulitafutia suluhisho
tatizo la kuzuiliwa kwa masanduku na pikipiki za Jumuiya hizo.
3. Wizara kupitia Idara ya Misitu ihakikishe inafuatilia kwa karibu na kutafuta dawa
ya kuulia wadudu wote wanaozorotesha ukulima wa Asali Pemba na Unguja.
4. Wizara iweke utaratibu wa kuwapatia wanajumuiya elimu ya ufugaji nyuki wa
kisasa japo kwa kuchukua wanachama wawili na kuwaelimisha na wao kuwa
mabalozi kwa kuwafundisha wakulima wenzao.
5. Wizara kwa kushirikiana na ZBS itengeneze mazingira ya kuwaelekeza na
kuwasaidia Jumuiya kufikia viwango vya kupata alama ya ubora na kuwapatia
alama hiyo kwa gharama nafuu.
Ripoti ya Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo inayotokana na ufuatiliaji utekelezaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Biashara na Viwanda pamoja na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2018/2019. 57
5. HITIMISHO
Kwa ujumla, Kamati imefanikisha majukumu yake ya kufuatilia utekelezaji wa kazi zake
ilizojipangia katika Wizara na taasisi zilizo chini ya Wizara hizo zilizoainishwa katika
ripoti hii. Kamati inazipongeza Wizara na Taasisi hizo kwa mashirikiano yao ya dhati
kwa Kamati katika kufanikisha kazi zake pamoja na juhudi zinazochukuliwa katika
utekelezaji wa kazi zao. Kamati inaziomba Taasisi hizo ziongeze juhudi ili kuimarisha
uchumi na maendeleo ya nchi yetu.
Wizara zinazosimamiwa na Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo zichukuwe juhudi za
makusudi kutekeleza ipasavyo maagizo yote yaliyotolewa na Kamati hii kwa lengo la
kuwapatia wananchi wetu huduma bora na kuongeza Pato la Taifa.
Kamati pia inapenda kutoa shukurani kwa wale wote waliofanikisha kazi za Kamati kwa
mwaka wa fedha 2018/2019 na kuwezesha taarifa za Kamati kutayarishwa na kuwasilisha
kunakohusika. Kamati inawashukuru kwa dhati viongozi na watendaji wote wa Serikali
na Baraza la Wawakilishi kwa utendaji mzuri wa shughuli zao za kila siku.
XXXXXXXXXXXXX Mwisho XXXXXXXXXXXXX