Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA...
Transcript of Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA...
-
Nakala ya Mtandao (Online Document)
1
BUNGE LA TANZANIA
________________
MAJADILIANO YA BUNGE
_____________________
MKUTANO WA KUMI NA TANO
Kikao cha Ishirini na Moja – Tarehe 29 Mei, 2014
(Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi)
D U A
Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua
HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI
Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na :-
NAIBU WAZIRI WA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO:
Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015.
AIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI:
Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na
Madini kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015.
MHE. CAPT. JOHN D. KOMBA K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA
MAENDELEO YA JAMII:
Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Jamii Kuhusu
Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014 na Maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio ya
Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015.
MHE. JEROME D. BWANAUSI K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA NISHATI NA
MADINI:
Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini Kuhusu Utekelezaji
wa Majukumu ya Wizara ya Nishati na Madini kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014
-
Nakala ya Mtandao (Online Document)
2
na Maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo
kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015.
MHE. MOSES J. MACHALI (K.n.y. MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI
KWA WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO):
Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani, kwa Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya
Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015.
MHE. RAJAB MBAROUK MOHAMED (K.n.y. MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA
UPINZANI KWA WIZARA YA NISHATI NA MADINI):
Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani, kwa Wizara ya Nishati na
Madini Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka
wa Fedha 2014/2015.
MASWALI KWA WAZIRI MKUU
SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, leo ni maswali kwa Waziri Mkuu bahati
ninamwona Kiongozi wa Kambi ya Upinzani, kama ilivyo kwa mujibu wa Kanuni
zetu yeye ndiye atakayeanza kumwuliza Maswali Waziri Mkuu.
Mheshimiwa Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni.
MHE. FREEMAN A. MBOWE: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kunipa
nafasi ya kumwuliza Mheshimiwa Waziri Mkuu Maswali. Mheshimiwa Waziri
Mkuu, wakati unahitimisha hoja ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, ulitanabaHisha
kwamba, uchaguzi wa Serikali za Mitaa utafanyika kama ilivyo kawaida mwisho
wa mwaka huu 2014.
Vilevile, ulilifahamisha Taifa kwamba, wakati huo huo zoezi la uandikishaji
wapiga kura katika utaratibu mpya wa biometric utakuwa unatumika.
Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa uzoefu wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
Mwaka 2004 na zaidi Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2009 ambao
ulisimamiwa na Sheria ya Serikali za Mitaa, Sura ya 287 na Sheria ya Serikali za
Miji, Sura ya 288, Uchaguzi huu uligubikwa na vurugu nyingi sana.
Pia uliishawahi kutoa kauli huko nyuma kwamba, Serikali itaangalia upya
sheria ile ili pengine kuifanyia marekebisho ya msingi kabla ya uchaguzi wa
mwaka huu 2014 ili matatizo yale yasijirudie tena.
-
Nakala ya Mtandao (Online Document)
3
Mheshimiwa Waziri Mkuu, ni miezi michache imebakia kabla ya Uchaguzi
huo. Unaliambia nini Taifa kuhusu maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
na Vijiji mwisho wa mwaka huu? (Makofi)
WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba tu kueleza kwa ufupi kwamba,
mambo ambayo tumeishaanza kuyafanyia kazi; kwanza ni maandalizi tu ya
kibajeti ambayo tulizungumza wakati wa kuhitimisha Bajeti ya Waziri Mkuu.
Pili, huwa tunakuwa na utaratibu wa kushirikisha wadau wote wakati wa
kuandaa Kanuni ambazo tunafikiria zinaweza zikasaidia katika kusimamia vizuri
zoezi hili. Kwa hiyo, nalo tumeishaanza kuliangalia kwa maana ya kutafuta
Kanuni za mara ya mwisho turekebishe mahali gani ili tuweze kwenda vizuri.
Mheshimiwa Spika, tatu ni hili ambalo amelieleza. Ni kweli kwamba tulitoa
hiyo kauli na tumeishaomba watu wa TAMISEMI waangalie kama kuna maeneo
hasa ambayo tunafikiria pengine yangeweza kufanyiwa marekebisho kabla ya
Uchaguzi Mkuu. Sasa kama yatabainika basi tutaleta hiyo rai mbele yetu.
Wakati huo huo labda niseme tu kwamba, kwa sababu na ninyi ni wadau
wakubwa kwa maana ya vyama vya Upinzani, ni rai yangu tu kwamba na ninyi
mngeanza kulitazama vilevile kama kuna maeneo ambayo mnafikiria
yangeweza kupendekezwa ili na yenyewe tuweze kuyachukua wakati
tunajaribu kutazama na sisi upande wetu, tutashukuru vilevile. (Makofi)
MHE. FREEMAN A. MBOWE: Mheshimiwa Waziri Mkuu, nakushukuru kwa
majibu yako ya awali.
Ni kweli sisi kama wadau muhimu yako maeneo mengi sana ambayo
yanalalamikiwa katika Kanuni hizi ambazo mara ya mwisho zilitungwa mwaka
2009 na ni dhahiri tutatoa mapendekezo mengi tu ya mabadiliko katika Kanuni
hizi ili kuufanya uchaguzi huu uwe huru na amani zaidi.
Mheshimiwa Waziri Mkuu, hata hivyo, tatizo hapa siyo mapendekezo yetu,
ila ni utayari wenu wa kukubali mapendekezo ambayo wadau watayatoa, kwa
sababu tukikumbuka katika uchaguzi wa mwaka 2009 yako mapendekezo
kadha wa kadha ambayo yalitolewa kwa Serikali lakini ikayapuuza na matokeo
yake uchaguzi ule ukaghubikwa na vurugu nyingi.
Sasa badala ya kusubiri wadau wapendekeze bila utaratibu
unaoeleweka unaonaje kama leo utalipa Taifa taarifa kwamba, unakusudia
kuita kikao cha wadau mapema sana ili mambo haya yajadiliwe mapema
kabla hujafika hatua ya kumaliza Kanuni wewe na TAMISEMI ambao ni
washindani katika zoezi hili? (Makofi)
-
Nakala ya Mtandao (Online Document)
4
WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, mnaweza vilevile mkawa na Kanuni
nzuri sana, lakini kama watu wenyewe ambao tunahusika na zoezi dhamira zetu
nazo si nzuri, bado hiyo haiwezi kuwa ni tiba. (Makofi)
Kwa hiyo, nadhani rai ya msingi hapa ni kwamba, sisi wote ambao ni
washirika wakubwa katika zoezi hili pande zote mbili; upande wa Chama cha
Mapinduzi, upande wa vyama vya Upinzani tufike mahali tuone kwamba,
jambo hili ni letu wote na pale ambapo hapastahili kuwa na vurugu hakuna
sababu ya kuwa na vurugu, vinginevyo nadhani rai yako kwangu haina tatizo
hata kidogo.
Tutajitahidi kuona wakati mwafaka, na hata ikibidi pengine kuanza na
mawasiliano formal hivi, brain storming ya Kanuni zenyewe kwa ujumla wake
halafu baadaye twende katika hatua sasa ya kuona ni maeneo gani ambayo
tunafikiri tunaweza tukayafanya.
Tutajitahidi kupitia TAMISEMI tuone wakati ambao tungeweza tukafanya
hilo zoezi. (Makofi)
SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa kumjibu Kiongozi wa
Kambi ya Upinzani. Ninatamani wote walioamka asubuhi wamalizike na
inawezekana tu kama maswali yetu yatakuwa mafupi na hoja zetu fupi na
zingine siyo lazima ku- repeat. Kwa hiyo, ninaanza na Mheshimiwa Murtaza
Mangungu.
MHE. MURTAZA A. MANGUNGU: Mheshimiwa Spika, ahsante sana.
Mheshimiwa Waziri Mkuu, mwaka 1997 Serikali ilichukua uamuzi wa
kuvunja Jiji la Dar es Salaam na liliendeshwa na Tume baadaye yakaja
mapendekezo ya uanzishwaji wa Manispaa za Kinondoni, Ilala na Temeke. Hivi
sasa kuna mkanganyiko mkubwa sana kwenye utekelezaji wa maamuzi kati ya
Halmashauri hizo na Jiji.
Je, ni lini Serikali itachukua uamuzi wa kuondoa mkanganyiko huu na
kuweka mfumo ambao utasaidia kutekeleza majukumu ya Manispaa hizi kama
inavyotakiwa? (Makofi)
WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, ni kweli suala la mfumo au muundo wa
Jiji na uhusiano wake na manispaa zile tatu kwa muda mrefu limekuwa ni tatizo
-
Nakala ya Mtandao (Online Document)
5
ambalo linajitokeza mara kwa mara na ndiyo maana Serikali kwa nyakati
imejaribu kuona ni muundo gani pengine ungeweza ukafaa.
Mtakumbuka mara ya mwisho tulijaribu lakini yale mapendekezo bado
hayakuweza kutatua lile tatizo na tukalazimika kurejea tena kwenye utaratibu
huu wa sasa.
Mheshimiwa Spika, sasa nafikiri ushauri wangu ingekuwa, tuombe
Manispaa zile tatu ambazo ndiyo wadau wakubwa, pamoja na Jiji lenyewe
pengine mngekuwa ndiyo chanzo cha kuibua fikra ambazo mnadhani
zinaweza zikafaa kwa ajili ya muundo wa Jiji la Dar es Salaam.
Mnaweza mkafanya hivyo, kwa kujaribu kutengeneza timu kwanza ya
Wataalam, baadaye mkajaribu kutengeneza timu ya Madiwani lakini wa
maeneo yote, lakini mtumie na uzoefu pengine wa maeneo mengine duniani
kuona mifumo ya miji au majiji yalivyo na kuweza kuona ni namna gani nzuri
tunaweza tukajaribu kuitumia hapa Dar es Salaam.
Nadhani tukifanya hilo pengine litakuwa mwanzo mzuri kwa sababu ninyi
ndiyo wadau wakubwa, badala ya kuanzia juu na kushuka chini. Tuanzie chini ili
tuyalete juu tuone baadaye kama litakubalika. (Makofi)
SPIKA: Mheshimiwa Mangungu swali la pili, fupi kabisa.
MHE. MURTAZA A. MANGUNGU: Mheshimiwa Waziri Mkuu, nakushukuru
sana kwa majibu mazuri yenye matumaini. Ningependa tu kujua kwamba, uko
tayari kusimamia mwongozo na usimamizi wa jambo hili kwa maana hizo
zitakuwa ni mamlaka ambazo mpaka sasa zinasuguana kama tunavyoona Jiji
la Dar es Salaam linazidi kuwa chafu, mifereji ya maji machafu imefurika, kila
mamlaka inasema hili ni jukumu la mwingine.
Sasa kwa kipindi hiki cha mpito. Je, unatoa agizo gani na utayari wako
wa kiasi gani kuweze kuzikutanisha mamlaka hizi na kulisimamia hili jambo chini
ya ofisi yako?
WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, ofisi yangu ndiyo kiongozi wa shughuli
zote za Serikali za Mitaa, ndiyo maana ninalisema hili kwa sababu Manispaa hizi
ziko chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Jiji lenyewe liko chini ya Ofisi Waziri Mkuu.
Rai yangu ya msingi ni hiyo tu kwamba, tulianzishe kule chini ili muweze
kubainisha maeneo ambayo mnayatazama kwamba, kwanza ni tatizo katika
-
Nakala ya Mtandao (Online Document)
6
utekelezaji, tatizo kimfumo na kimuundo, yapande juu baada ya mjadala
mpana kwenye mabaraza yote pamoja na Jiji lenyewe kama tunavyofanya
tunapoanzisha maeneo mapya popote pale.
Mheshimiwa Spika, mimi natamani hili lifanyike zaidi na pengine hata
wadau nje kabisa ya mabaraza haya ili kuweze kuwa na ushiriki mpana zaidi
tuweze kuona namna gani tutaweza kulifanya hili jambo.
Sisi ofisi yetu na TAMISEMI kwa ujumla bado tutakuwa ndiyo wasimamizi
pale mtakapokuwa mmeonesha nia hiyo na namna ambavyo mngependa
zoezi hili liendelee.
MHE. ENG. MOHAMED HABIB JUMA MNYAA: Mheshimiwa Spika, nashukuru
kunipa nafasi ya kumwuliza swali Mheshimiwa Waziri Mkuu ambaye sijamwuliza
swali muda mrefu sana.
Mheshimiwa Waziri Mkuu, tunaelewa kwamba, nchi nyingi duniani
zinakopa na sisi Tanzania hatuna budi kukopa kwa Maendeleo yetu. Hata hivyo,
kumekuwepo na trend katika kipindi kirefu sasa kukopa na inaonekana miradi
yote mikubwa tunakopa kutoka Exim Bank ya China. Sababu hizo zinajulikana
kwa sababu ya unafuu wa riba, masharti na urafiki tulionao na China.
Nini hatima ya nchi yetu ukizingatia kwamba, huko nyuma kuna mikopo
mingi tumeshindwa kulipa ikabidi tusamehewe na ukitazama pia na siasa au
msimamo wetu wa kutofungana na upande wowote?
Mheshimiwa Spika, ahsante sana.
WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, namshukuru sana Ndugu yangu
Mheshimiwa Mnyaa, ingawa swali lake kidogo nadhani hakulitafiti tafiti sana.
Ungelifanyia utafiti ungembana Waziri Mkuu vizuri sana.
Iko sheria ambayo inasimamia suala zima la ukopaji pamoja na madeni.
Sheria ile ndiyo inaisaidia Serikali muda wote kuzingatia yale ambayo
yanastahili.
-
Nakala ya Mtandao (Online Document)
7
Ni kweli nyuma tulikopa, pia ni kweli kwamba mikopo ile ni mikubwa lakini
zoezi lile lililoendeshwa na vyombo vya Kimataifa lilikuwa ni zoezi la jumla katika
kujaribu kusaidia hizi nchi maskini kuziondolea mzigo wa kuja kulipa madeni
hayo baadaye ali mradi ukidhi vigezo fulani. Tanzania tulikidhi na ndiyo maana
tukapata ule msamaha, ulikuwa ni wa jumla na siyo sisi tu, nchi nyingi zilipata
hiyo nafuu.
Kwa hiyo, basi nataka nikuhakikishie tu kwamba, mimi kama Kiongozi wa
Shughuli za Serikali, faraja niliyo nayo ni moja tu kwamba, kwa vigezo vyote sisi
kama nchi bado tuna sifa nzuri sana ya kuendelea kukopa kwa sababu uwezo
huo wa kuweza kulipa haujakiuka yale masharti ya msingi kwa mujibu wa sheria
hiyo.
MHE. ENG. MOHAMED HABIB JUMA MNYAA: Mheshimiwa Spika, nashukuru
kwa jibu hilo zuri la Mheshimiwa Waziri Mkuu.
Nitakuwa na swali moja tu dogo kwamba, uzoefu tulionao Tanzania
katika miradi ambayo imetekelezwa kwa msaada wa Ndugu zetu wa China
huko nyuma, iwe ya viwanda, hospitali na miradi mingine ya kijamii. Mifano iko
ya TAZARA, URAFIKI, hospitali kule Zanzibar, Kiwanda cha Sukari Zanzibar na
kadhalika.
Baada ya muda kumalizika na wao kuondoka, miradi hii tukaachiwa
wenyewe utakuta miradi hii mingi imetupatia na kuleta taabu, na mingine
imetushinda. Pamoja na sababu zetu za kiutawala katika kuendesha hiyo miradi
lakini kuna sababu za standardization ya zile mashine au materials, iwe umeme
au mashine nyingine.
Tumejiandaa vipi sasa na hii miradi yote ambayo tunakopeshwa na
inajengwa kwa msaada wa China (fedha au materials zinazotoka China) ili ziwe
sustainable baadaye baada ya kutuachia wenyewe? Tanzania tunajiandaa
vipi?
SPIKA: Bahati yako, karibu niseme ni swali jipya. Mheshimiwa Waziri Mkuu!
(Makofi/Kicheko)
WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, ni dhahiri swali ni pana sana, lakini
labda tutumie mifano michache tu, maana hapa nadhani anazungumza
mikopo ya China.
-
Nakala ya Mtandao (Online Document)
8
Nichukue kwa mfano ujenzi wa bomba la Gesi kutoka Mtwara kwa
sababu ule mkopo ni mkubwa. Tulichofanya katika zoezi hili wakati huu
tunaendelea kujenga hilo bomba, of course tutakuwa na vijana ambao
tumewaajiri mle. Watabakia na sehemu ya uwezo wa kuweza kusaidia
kuelewa mambo yale madogo madogo ambayo yanaweza kujitokeza katika
usimamizi wa bomba hilo.
Lakini kupitia Nishati na Madini, tumeagiza vilevile kwamba mradi huu ni
mkubwa sana na bomba hili litahitaji kusimamiwa vizuri. Ni vizuri katika wale
vijana ambao tumepata fursa ya kuwapeleka nje kwenda kujifunza mambo
mbalimbali kuhusu gesi moja ya eneo ambalo tulipe umuhimu mkubwa ni
namna tunavyoweza kusimamia suala zima la mkopo huu unaotuwezesha
kuwa na gesi kutumia bomba la Mtwara.
Hivyo itatusaidia vile vile kwenye mabomba mengine ambayo
yatajitokeza kwa sababu bomba hili haliishii Dar es Salaam tuna ndoto za
kwenda Kaskazini, kwenda hata mpaka Kanda ya Ziwa. Kwa hiyo ni lazima
tuwe na wataalamu watakaotuwezesha kusimamia jambo hili vizuri. Hili tunalo
na tumeshaliingiza katika utaratibu wa kuanza kutoa mafunzo kwa vijana.
(Makofi)
SPIKA: Naomba tuendelee na Mheshimiwa Assumpter Mshama.
MHE. ASSUMPTER N. MSHAMA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa
kunipatia nafasi ili nimwulize Mheshimiwa Waziri Mkuu swali moja.
Mheshimiwa Waziri Mkuu, kumekuweko mgogoro mkubwa sana katika
maeneo ya ardhi hasa maeneo ambayo yamegawiwa kwa wawekezaji.
Katika Tanzania nzima ikiwemo na Misenyi wananchi walikuwa wanamiliki
maeneo yao lakini NARCO ikaamua kuuza hayo maeneo kwa wawekezaji.
Lakini wawekezaji wengine wamechukua maeneo makubwa kuliko
mahitaji yao na matokeo yake wameacha Watanzania wengi wakihangaika
hawana mahali pa kulishia wanyama wao na ardhi yao imechukuliwa bila
utaratibu wowote na wakauziana watu ndani ya vitalu vile.
Mheshimiwa Waziri Mkuu, kwa kuwa wewe ndio msimamizi wa mambo
yote ya Serikali hili suala kwa Wizara ya Ardhi limeshindikana unaonaje ukiingilia
kati zikafutwa zile hati wananchi wakarudishiwa maeneo yao na matokeo yake
tukapata amani katika Taifa letu.
Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba maelezo yako.
-
Nakala ya Mtandao (Online Document)
9
WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, ni kweli analolisema Mheshimiwa
Assumpter Mshama kwamba pale Kagera tunayo maeneo ambayo ni
mashamba ambayo zamani yalikuwa yanamilikiwa na NARCO na baadaye
tukayatengenezea utaratibu ambao tulifikiri ungejibu haja ya Serikali ya
kuendeleza ufugaji wa kisasa katika maeneo hayo na kwa njia hiyo tuweze
kuboresha mifugo yetu.
Lakini ni kweli vilevile kwamba uamuzi ule na utekelezaji wake havikuenda
kama tulivyokuwa tumetarajia. Kwa hiyo tulichofanya Serikalini nimeagiza
Wizara kadhaa ambazo sekta hizo zinahusiana kwa karibu sana.
Tupitie kwenye maeneo yote ya mashamba ya NARCO kuweza kubaini
matatizo kwa kila shamba na tuone ni maeneo yapi kwa kweli yanaweza
yakaondolewa katika utaratibu ule. Pengine tukawapa wakulima au wafugaji
kama watakuwepo wafugaji wadogo maana lengo ilikuwa ni kuyatumia kwa
ajili ya kuboresha mifugo.
Sasa ndani yake ofcourse ipo Wizara ya Kilimo, Ardhi, watu wetu wa
TAMISEMI, tumeweka Maliasili na Utalii vilevile kwa sababu hawa wanahusiana
kuna maeneo mengine ambapo tutahitaji utaalamu wao kidogo.
Kwa hiyo, hiyo timu tunafikiri itakapomaliza hilo zoezi nadhani inaweza
ikanisaidia kuweza kushauri au kumshauri Mheshimiwa Rais vizuri zaidi juu ya
jambo hili.
SPIKA: Mheshimiwa Mshama kwa kifupi sana.
MHE. ASSUMPTER N. MSHAMA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana.
Inawezekana labda Mheshimiwa Waziri Mkuu hawakuambii ukweli, kwa sababu
mpaka sasa hivi kwetu zimekuwepo Kamati zaidi ya saba na moja nilikuwemo
mle na uamuzi Waziri wa Mifugo mwaka jana alituambia kwamba wameamua
sasa kurudisha vitalu.
Je, lini utawaambia wananchi hasa wa Misenyi kwamba sasa ni mwisho
na sasa tunakwenda kwenye utaratibu huu?
WAZIRI MKUU: Ziko efforts za Wizara inayohusika. Mimi ninachokisema
hapa nimepanua tu hili wazo, sababu tatizo hili si Kagera tu, mashamba ya
NAFCO yako sehemu mbali mbali, ndiyo maana tukasema tusiiachie Wizara hii
peke yake tuhusishe na Wizara nyingine ili baadaye tuweze kuwa na kauli
pamoja kwa sababu TAMISEMI wanahusika sana.
-
Nakala ya Mtandao (Online Document)
10
Kama hawatakuwa sehemu ya uamuzi kesho na kesho kutwa TAMISEMI
wanaweza wakajikuta tena kupitia Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya
hawaelewi kinachoendelea ni nini.
Kwa hiyo, nataka nikuhakikishie tu kwamba zile jitihada za Wizara kwenye
maeneo ambayo tayari walikuwa wameanza hatukuziingilia sisi lakini tumetaka
tupanue zoezi sasa tuweze kuchukua maeneo yote ya NARCO kwa upana
wake na tuone namna tunavyoweza kuwasaidia. (Makofi)
MHE. RAJAB MBAROUK MOHAMED: Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri
Mkuu, suala langu haliko mbali sana na suala ambalo ameliuliza Mheshimiwa
Assumpter Mshama, ila mimi nitazungumzia zaidi katika madhaifu katika
usimamizi wa rasilimali za Taifa hasa nikizingatia uhifadhi wa mazingira.
Mheshimiwa Waziri Mkuu Tanzania ina eneo la misitu ambalo halipungui
ekari milioni 33 na wastani wa ukataji miti ndani ya nchi yetu kwa mwaka
haupungui ekari 403,000.
Mheshimiwa Waziti Mkuu, na ukataji huu wa miti ndio ambao
unasababisha uchafuzi mkubwa wa mazingira. Wakataji hawa mara nyingi
wanakuwa ni wakataji haramu au huwa hawafanyi kutokana na mipango
ambayo imewekwa na Serikali. Naomba tu kutoka kwako Mheshimiwa Waziri
Mkuu, kauli ya Serikali juu ya ukataji huu mkubwa wa miti nchini.
WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, ukataji wa miti au misitu hapa nchini ni
kweli ni tatizo na lipo. Lakini lazima vilevile tukubali kwamba hiyo ni changamoto
ambayo lazima tuijibu kwa kutumia mbinu mbalimbali.
Nitoe mfano tu wananchi wetu wengi vijijini wengi wanatumia nishati ya
kuni na baadhi ya makabila wanapenda kukata miti hii kabla hata haijakauka
anaikausha baada ya kukata ili aweze kujiandaa vizuri. Ni ukataji haramu kama
unavyosema, lakini ni ukataji ambao haukwepeki katika mazingira ya sasa kwa
sababu nishati ile kwa mwananchi yule ni ya lazima.
Lakini uko ukataji miti ambao unatokana na matumizi ya mbao na hapo
unaweza ukachukua mifano ya shule zote ulizojenga, zahanati zote ulizojenga,
nyumba zote tunazojenga zote tunatumia miti. Ni ukataji ambao kwa upande
mwingine haukwepeki.
-
Nakala ya Mtandao (Online Document)
11
Madawati yote wanayokalia watoto wetu yote ni mbao ambazo
zimetokana na miti. Unaweza ukauita ukataja haramu lakini bado changamoto
yake ni lazima itafutiwe njia mbadala ya namna ya kushughulika na jambo hili.
Kwa hiyo kwa ufupi nataka kusema nini, nakubali kwamba changamoto
ipo lakini nadhani kama Serikali na sisi wote kama wadau wakubwa wa tatizo
hili ni lazima tuweke vichwa pamoja tuone namna gani tutashughulikia jambo
hili.
Moja tamaa niliyonayo ni kwamba pengine gesi hii ambayo Mwenyezi
Mungu ametujalia tuone namna tutakavyoitumia kikamilifu ili sisi wote wakazi
wa mijini kwanza maana ndio watumiaji wakubwa sana wa mkaa tuondokane
na matumizi ya mkaa tuingie katika matumizi ya gesi tutakuwa tumepunguza
sana ile sulubu ya sasa ya mkaa kuja mijini.
Lakini ukifanya hivyo peke yake bado haisaidii ndiyo juhudi za Serikali ni
kujaribu kutumia kila aina ya mbinu. Kuna matumizi ya majiko banifu katika
jitihada za kujaribu kupunguza matumizi ya ukataji wa miti vijijini.
Lakini nadhani tunakokwenda kama nchi zingine zilivyofanya nyingi ni
lazima vilevile gesi hii tuitafutie utaratibu wa kuweza kuifikisha mpaka kwenye
maeneo yale ambayo sasa yanakuwa kimiji ili na yenyewe kutusaidia kuzidi
kupunguza jambo hili.
Lakini mwisho kwa ujumla ni elimu, tunahitaji elimu kubwa kwa
Watanzania kwa sababu wengine wanakata wakati mwingine hana sababu
anaona tu limti linamkera tu. Wakati mwingine watu wanakata kwa sababu
wanataka mifugo ipite sehemu ambako akiona anaona ng‟ombe badala ya
kuona miti anachohitaji huyu mtu ni elimu tu.
Kwa hiyo kwa ujumla nadhani tutahitaji interventions au njia mbalimbali
kuweza kujaribu kutatua hili tatizo ambalo kimsingi ni kubwa sana.
MHE. RAJAB MBAROUK MOHAMED: Mheshimiwa Spika, ahsante pamoja
na majibu ambayo Mheshimiwa Waziri Mkuu amenipa ambayo kwa kweli ni
mazuri.
-
Nakala ya Mtandao (Online Document)
12
Mheshimiwa Waziri Mkuu, hata hivyo ni asilimia nne (4) tu ya ekta hizo
ambazo nimezitaja ndani ya nchi yetu ambazo zimewekewa mipango mizuri ya
matumizi. Asilimia 96 bado Serikali haijaweka msimamo mzuri wa matumizi ya
eneo hili na hii ndiyo inayosababisha hata hivi vita ambavyo sasa hivi tunaviona
vya wafugaji kuingia katika maeneo ambayo yametengwa na mambo
mengine.
Mheshimiwa Waziri Mkuu, lakini kwa upande wa Wizara ya Maliasili
wanasema kwamba asilimia 57 ya mapato ambayo yanatokana na mazao ya
misitu hayakusanywi. Sasa kweli wananchi wana shida wana matatizo yao
mambo ya kuni, madawati lakini je katika eneo hili ambalo la usimamizi wa
upatikanaji wa fedha na matumizi mazuri haya maeneo Serikali inasemaje?
SPIKA:Haya sekta hii halafu unaingia kwenye particular haya Mheshimiwa
Waziri Mkuu.
WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Rajab fundi sana wa kuunganisha mambo.
Mheshimiwa Spika, analosema Mheshimiwa Rajab ni kweli bado kuna
udhaifu katika eneo hili na utaona hata katika Bajeti yetu moja ya eneo ambalo
hatukufanya vizuri sana ni hilo la maduhuli na Wizara ya Maliasili na Utalii wana
eneo kubwa ambalo tunadhani lingeweza kuwa la msaada sana katika
kuongeza Bajeti yetu.
Serikalini tulikaa kujaribu kuona tunafanya nini na hili tatizo la maduhuli
kutokukusanywa kwa mujibu wa Bajeti iliyowekwa. Imefika mahali watu
wanafikiria kwamba pengine tungekuwa na chombo maalum au timu maalum
ambayo kazi yake iwe ni kufuatilia tu maduhuli kwa kila Wizara na kwa kila
taasisi ambayo imepewa jukumu la kukusanya hizo fedha. Kwa hiyo katika
Bajeti ya mwaka huu tutajaribu sana kuona namna ya kuja na utaratibu
wa jambo hili kusimamiwa hatutakuwa ni chombo kwa maana ni chombo cha
kisheria kama TRA ilivyo.
Lakini tumedhani kwamba ndani ya Wizara hizi sisi wenyewe tutatafuta
timu ambayo tutataka tuipe jukumu la ufuatiliaji wa makusanyo wa maduhuli
na hili unalolisema linaweza kuwa ni namna moja pengine ya kuweza kupata
kile ambacho kwa sasa hivi tunakikosa.
MHE. MOSES J. MACHALI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa
fursa nimwulize swali moja dogo la nyongeza.
-
Nakala ya Mtandao (Online Document)
13
Mheshimiwa Waziri Mkuu hivi karibuni kumelipuka ugonjwa wa homa
SPIKA: Hebu vipi la nyongeza kwa nani?
MHE. MOSES J. MACHALI: Hapana swali moja.
SPIKA: Aaa!!! Okay okay.
MHE. MOSES J. MACHALI: Mheshimiwa Waziri Mkuu, hivi karibuni
kumejitokeza ugonjwa ambao unaonekana kutishia watu wengi hapa nchini
ugonjwa wa homa ya dengue.
Taarifa ambazo zinatajwa na watu ambazo nimezisikia ni kwamba
kulikuwa kuna utafiti ambao unafanywa hapa nchini na wataalamu wetu wa
Wizara ya Afya wakitafuta mbu ambao watakuja kuangamiza mbu wa Malaria.
Sasa katika majaribio hayo, wale mbu ndio wamepelekwa matokeo yake
yanaleta janga hili.
Mheshimiwa Waziri Mkuu, nilikuwa naomba kauli ya Serikali kuhusiana na
taarifa hizi ni sahihi kiasi gani ili kuweza kuondoa hofu iliyoko miongoni mwa
Watanzania?
SPIKA: Au umesikia yule Mchungaji. (Makofi/Kicheko)
WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Machali hakunitendea
haki. Swali angemwuliza Waziri wa Afya angefanya vizuri zaidi kuliko mimi. Lakini
ni kweli sasa hivi tuna tatizo la homa ya dengue.
Lakini wakati huo huo ugonjwa wa malaria nao upo. Sasa kama gonjwa
hili limetokana na hizo tafiti au hapana siwezi kulisema kwa sasa maana sijui.
Lakini ninachojua ni kwamba homa hiyo inasababishwa na mbu aina ya aedes
maana tuna aina tatu za mbu. Chanzo chake ni mbu anaitwa aedes.
Sasa huyu mbu yupo muda wote wala sio kwamba ameibuka leo,
hapana. Ni kwamba tu hapa katikati pengine jitihada zilikuwa nzuri tukaweza
kudhibiti akakosa kupanua uwezo wake wa kueneza ugonjwa na utaona
imejitokeza sambamba na mafuriko makubwa yaliyojitokeza.
-
Nakala ya Mtandao (Online Document)
14
Kwa hiyo inawezekana pengine katika kuzaliana walikuja wakapata
upenyo hivi na ndiyo maana tatizo hili likajitokeza. Lakini labda niseme tu
kwamba pengine nitakuwa sikukutendea haki mimi nadhani labda
nitamwomba Waziri wa Afya kwa sababu ni jambo kubwa pengine angekuja
na kauli ya Serikali ili aweze kulieleza vizuri zaidi kwa manufaa ya Watanzania
wote.
SPIKA: Ahsante sana kwa kuokoa muda, sasa nimwite Mheshimiwa
Magdalena Sakaya. Tulikuwa na muda wa kuwasilisha.
MHE. MAGDALENA H. SAKAYA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana.
Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba nikuulize swali moja.
Mheshimiwa Waziri Mkuu, Serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi sana za
walipa kodi kwa ajili ya kutengeneza miundombinu ya barabara hapa nchini.
Hata hivyo Mheshimiwa Waziri Mkuu barabara hizi kwa sehemu kubwa,
kiasi kikubwa zilikuwa zinaharibiwa pamoja na kuwepo na sheria lakini
wanyabiashara wasiokuwa na uzalendo wamekuwa wakizidisha mizigo kwenye
magari yao na hivyo kuonekana barabara zote zimeharibika na tumeshuhudia
migomo mikubwa kwenye barabara zote.
Mheshimiwa Waziri Mkuu, wafanyabiashara wengi wamefanikiwa hata
kuishinikiza Serikali pale sheria inaposimamiwa wamegoma na hivyo Serikali
kuruhusu uharibifu wa barabara kuendelea. Naomba kauli ya Serikali, nini kauli
ya Serikali kuhusiana na barabara kuharibiwa na huku wanaona na huku
Watanzania wanaendelea kuteseka? Ahsante sana. (Makofi)
SPIKA: Mheshimiwa Waziri Mkuu sjui kama umelielewa hili swali?
WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, zaidi ya asilimia 80 ya usafirishaji wa
mizigo na abiria hapa unategemea barabara. Kwa hiyo, ndio uhalisia wake
kwa sasa. Ni hali ambayo inaikumba nchi yetu kwa sababu bado reli
haijaweza kutoa jibu kwa tatizo hili, tutakapokuwa tumeimarisha reli chini ya
Dkt. Harrison Mwakyembe inawezekana kabisa tatizo hili tukaanza kulipunguza.
Lakini pili, barabara zetu hizi za lami zinatengenezwa kwa mfumo wa kitu
kinaitwa surface dressing. Life span yake uwezo wake wa kuishi ni kati ya miaka
10 mpaka 15. Hatutumii concrete asphalt hapana, tumejaribu kwenye
barabara tu ya TANZAM ndio tuliweza kutumia kigezo hicho kwa historia yake.
-
Nakala ya Mtandao (Online Document)
15
Kwa hiyo barabara zote hizi ni za aina hiyo. Sasa unapokuwa na
barabara hizi kwa mfumo huo ambao una mizigo mikubwa hiyo ni tosha kabisa
kuwezesha barabara hizi kutohimili kwa muda mrefu.
Tatu, magari yetu hapa nchini uzito tulioruhusu ni tani 56, nchi nyingi
hawakufika huko ni tani thelathini na thelathini na kitu hivi. Kwa uhalisia wa
kutokuwa na miundombinu ya reli, miundombinu ambayo ingeweza ikasaidia
kupunguza huu mzigo Serikali ilijikuta ikaweka utaratibu huo kwa maana ya
kusaidia tu kuweza kubeba mizigo hiyo kwa urahisi na kwa kutumia magari haya
ambayo tungefikiri yangekuwa ni machache badala ya kuwa na magari mengi
na hivyo kuzidi kuongeza tatizo la msongamano. Lakini kwa kufanya hivyo
bado hatujasaidia sana.
Lakini, nne niseme hili unalolisema kwa bahati mbaya sana jambo hili
halikueleweka vizuri, tatizo hakuna anayesema mtu azidishe mzigo zaidi ya tani
56, hakuna. Si mimi, si Waziri Magufuli si mtu mwingine yoyote na wenye malori
na mabasi wanajua hilo tatizo hapa lipo wapi? Ni kwamba katika kupima uzito
wa magari tunatumia axleload weight ya gari.
Gari inaweza kuwa na excel hizi mbili, tatu, nne, kinachotokea gari hili
katika kubeba huo mzigo unashuka milima unapanda kuna sehemu nyingine
kuna matuta unaruka unashuka.
Kwa hiyo, inawezekana kabisa mzigo ambao umeupima una tani 56
ukasogea kwenye excel ya mbele na kugandamiza ile excel ya mbele. Au
wakati unapanda mlima mzigo uka-slide back, nyuma na kugandamiza ile
excel ya nyuma unapokwenda kupima wanapima hiyo excel weight
kinachotokea inawezekana katika kutereza kwa ule mzigo ukajikuta ule uzito
umeongezeka kwenye excel hiyo kwa kiwango kile ambacho wanasema
hakizidi asilimia 5 au nyuma kwa kiwango hicho.
Sasa sheria nyingi duniani unapokuwa na hiyo allowance wanairuhusu
kwa nini, kwa sababu hujazidisha tani 56 inaruhusiwa na unachofanya pale
unapopima wakakuta kuna hilo tatizo nchi nyingi wanakuambia hebu park gari
jaribu kuona kama unaweza ukapanga hii mizigo tena vizuri halafu uendelee.
Lakini magari mengine ni mzigo ambao ni transit good huwezi
ukaufungua. Ndio maana wanakwambia inapotokea situation hiyo park gari
lakini ukubali kulipa faini kidogo kwa sababu itakubidi tukuruhusu uendelee
ingawa excel ya mbele ina uzito zaidi kuliko inavyotakiwa.
-
Nakala ya Mtandao (Online Document)
16
Mheshimiwa Spika, sasa ubishi ulikuwa katika hiyo allowed percentage
ndiyo ilileta ule ubishi ndiyo maana mimi nikaingilia kati nikasema jambo hili
linachohitaji ni ueleweshwaji na Kanuni hii kuiweka vizuri ili iweze kueleweka kwa
sababu ilionekana kutokueleweka vizuri, tukaomba ushauri wa Mwanasheria
Mkuu wa Serikali, akasema ni kweli Kanuni hiyo inahitaji kuandikwa vizuri.
Vinginevyo mizigo hii isingekuwa inasafiri inaingia Zambia, mizigo hii
ikasafiri ikaingia Burundi kama utakuwa umeweka uzito zaidi ya kiwango
kinachotakiwa. Ndiyo maana nikaingilia kati kwasababu niliona ugomvi ule
haukuwa na tija sana kwa sababu malori yale ndiyo jukumu la kusafirisha mizigo
na hali ilishakuwa mbaya.
Kwa hiyo, hatukupishana na magufuli ingawa watu wanaweza kusema
angalia Waziri Mkuu ameruhusu mizigo ibebe zaidi ya tani 56 hapana tulikuwa
tunazungumza allowable percentage wheather mtu ashushe afanye nini au
vinginevyo ni hilo tu ambalo nimeona nimalizie katika ku-clarify. (Makofi)
SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, Kanuni hazinilamishi kumwambia mtu
aulize swali la nyongeza. Kwa hiyo, tunakushukuru kwa majibu mengine
yalikuwa ni ya kitaalam hasa hili la mwisho na ninawashukuru. Kanuni
hazinilazimishi, muda umepita. Kwa hiyo, tunaendelea Katibu!
MASWALI NA MAJIBU
Na.148
Mkakati wa Kupunguza Maambukizo ya Ukimwi
MHE. MBAROUK SALIM ALI aliuliza:-
Ukimwi bado ni tishio na taarifa zinaonyesha kuwa maambukizi bado ni
makubwa hasa kwa baadhi ya maeneo hapa nchini.
Je, Serikali ina mkakati gani mahsusi wa kupunguza maammbukizi katika
maeneo yaliyoathirika zaidi?
-
Nakala ya Mtandao (Online Document)
17
WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, URATIBU NA BUNGE
alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba kujibu swali la Mhe. Mbarouk Salim
Ali, Mbunge wa Wete, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba Ukimwi bado ni tishio hasa Katika
makundi maalumu kama vile wanaofanya biashara ya ngono, wanaojidunga
sindano wanafanya ngono nzembe na wanaofanya ngono kinyume cha
maumbile.
Mheshimiwa Spika, Serikali ina mikakati kadhaa mahususi ya kupunguza
maambukizi hasa katika maeneo yaliyoathirika zaidi. Baadhi ya mikakati hiyo ni
kama ifuatavyo:-
(i) Kupitia mkakati wa kudhibiti Ukimwi kwa kipindi cha mwaka 2008-2012 na
kuandika mkakati mpya kwa kipindi cha mwaka 2013-2018.
(ii) Kupitia Sera ya Taifa ya Ukimwi ya mwaka 2001 na kuboresha ili kutoa
miongozo bora zaidi ya kupunguza maambukizi.
(iii) Serikali imeandaa mwongozo wa kuelekeza Mikoa namna ya kuandaa
mpango kazi wa Mkoa na kipaumbele ni kuzuia maambukizi kwa kubainisha
viashiria au vichocheo kwa kila Mkoa, Wilaya, Kata, Kijiji na mtu mmoja mmoja.
(iv) Serikali ina andaa mpango wa kuwa mwitikio wa Ukimwi kwa mfumo wa
Kikanda ambapo Wakuu wa Mikoa wa Kanda watakaa pamoja na kuwa na
mikakati ya pamoja.
(v) Kuimarisha huduma za kinga katika Mikoa yenye maambukizi makubwa.
(vi) Kupitia mkakati wa kinga 2009-2012 ili kuhakikisha mkakati wa Taifa
kuhusu Kinga inawekwa kwenye mkakati huu na baadae kutumika katika
maeneo yote hususan maeneo yenye maambukizi makubwa.
(vii) Kuendelea kutoa elimu ya Ukimwi na kubadili tabia kupitia kwa wadau
mbalimbali na vyombo vya habari hususani radio.
(viii) Mifumo ya uratibu usimamizi wa huduma za ukimwi imeimarishwa katika
ngazi za Halmashauri.
-
Nakala ya Mtandao (Online Document)
18
Mheshimiwa Spika, ninapenda kuipongeza Pemba kwa kuzingatia
mikakati ya kupunguza maambukizi ambapo viwango vya maambukizi kwa
Pemba ni vya chini Kitaifa ni kati ya 0.1% hadi 0.4%.
MHE. MBAROUK SALIM ALI: Mheshimiwa Spika, ninashukuru na pia
nimshukuru Waziri kwa majibu yake ingawa amaenda zaidi ki mikakati ya Kisera
kuliko ile mikakati mahususi ambayo nilitegemea niipate lakini pamoja na hayo
ninapenda kumuuliza mawili madogo.
Kwa sasa Serikali imejikita zaidi kupunguza maambukizi ya Mama kwa
Mtoto na pamoja na kwamba Mheshimiwa Waziri ametaja makundi mengi
hapa ambayo ni tishio kwa magonjwa haya sasa nimuulize. Mheshimiwa Waziri
kwamba ana kauli gani. Serikali inasemaje kuhusiana na mkakati wa sifuri tatu
ifikapo 2015 ambapo bado kama miezi sita. malengo hayo yatafikiwaje ikiwa
bado Serikali imejikita zaidi katika kipengele cha kuzuia maambukizi ya Mama
na Mtoto.
Lakini lingine nimwulize Mheshimiwa Waziri kwamba inaonyesha
kwamba katika baadhi ya maeneo kuna baadhi ya makabila hasa katika
maeneo ambayo yana maambukizi makubwa, kuna tatizo sugu la tohara kwa
wanaume, kwamba hawataki kufanyiwa tohara na watu wengi
hawajafanyiwa tohara.
Hili ni tatizo kubwa lakini pia kuna sumu kali inayoenezwa na makabila
hayo hayo kuwa iwapo watu watakubali kufanyiwa tohara ni kuingizwa katika
Uislamu.
Je, Waziri ana kauli gani kuhusiana na suala hilo? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru kupata
nafasi hii kwa niaba ya Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii ningepeda
kuongezea jibu la nyongeza kama ifuatavyo:-
Kuhusu suala la sifuri tatu, kwa maana ya kwamba kuna suala zima la
unyanyapaa, kuna suala zima la maambukizi mapya na suala zima la vifo
kutokana na ukimwi. Mkakati uliopo kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu,
Wizara ya Afya imeandaa maelezo maalumu ambayo tumeshasambaza nchi
nzima kupitia vituo vyote ambavyo tunatoa huduma ya Afya.
-
Nakala ya Mtandao (Online Document)
19
Nitumie fursa hii kuwaeleza Watanzania kazi kubwa ambayo imefanyika
kutokana na tafiti za viashiria katika ngazi ya jamii yaani indicator survey 2008
hali ya ukimwi nchini ilikuwa ni 5.7% lakini katika matokeo ya 2012 ambayo
Mheshimiwa Rais alizindua tarehe 27 Machi, 2013 tafiti hizi zimeonyesha hali ya
ukimwi kushuka na kufikia 5.1% katika nchi.
Kwa hiyo, tunawaomba Waheshimiwa Wabunge nyaraka hizi na
miongozo na mafundisho ambayo tumetoa nchi nzima kupitia vikao vya
maamuzi vya Mikoa ikiwamo Kamati ya Sheria yaani RCC na ngazi ya
Hamashauri katika Baraza yaani Full Council tufuatilie kuhusu utekelezaji
unakwendaje ili tuweze kuangalia hali ya jamii itakuwaje mwaka 2015/2016.
SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa nchi swali la pili.
WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, URATIBU NA BUNGE: Ni
kweli lile alilolisema Mheshimiwa Mbarouk kwamba utafiti umeonyesha hata
kwa Tanzania kwamba wale ambao hawajapata tohara na wale waliopata
tohara wanaoweza kupata maambukizi kwa haraka ni wale ambao
hawajapata tohara.
Utafiti umeonyesha, ndiyo maana hivi sasa kuna jitihada maalum za
Serikali na kampeni hii imeanza kufanikiwa vizuri sana katika Mikoa ambayo
imeoekana ina maambukizi makubwa sana ya Ukimwi.
Labda niseme tu kwamba Mikoa ambayo inaongoza sasa hivi kwa
kiwango cha juu ni Njombe ambayo ni 14.8%, Iringa 9.1%, Mbeya 9%, Shinyanga
7.4%, Ruvuma 7%, Dar es salaam 6.9% Katavi 5.9% na Pwani ni 5.9% tumeanza
kampeni ya makusudi ya kuhakikisha kwamba watu kwa hiari yao
wanakwenda kufanya tohara bila ya gharama na zoezi hili limefanikiwa sana.
(Makofi)
Kwa hiyo, ninataka kutoa wito tu kwa wananchi hasa wanaume
wajitokeze kwa umri wowote ili kuweza kufanya jambo hili kwa sababu
limeonekana kwamba ina faida na inaweza kuwasaidia katika kupunguza
maambukizi.
MHE. DKT. FAUSTINE E. NDUGULILE: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru kwa
kunipatia fursa ya kuuliza swali moja la nyongeza.
Kwa kuwa, sasa hivi takwimu zinaonyesha kwamba maambukizi ya
Ukimwi yanaongezeka sana katika makundi maalumu ikiwamo watumiaji wa
madawa ya kulevya.
-
Nakala ya Mtandao (Online Document)
20
Je, ni lini Seerikali italeta Muswada wa Sheria wa kudhibiri Madawa ya
Kulevya?
SPIKA: Mheshimiwa Waziri ninaomba uende kwenye meza ndiyo
utaratibu.
WAZIRI WA NCHI,OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, URATIBU NA BUNGE:
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, ninapenda kujibu
swali la Mheshimiwa Dkt. Ndugulile, Mbunge wa Kigamboni, swali la
nyongeza kama ifuatavyo:-
Ni kweli Serikali pamoja na marekebisho makubwa ya Sera na Sheria hayo
anayoyasema Mheshimiwa Dkt. Ndugulile, Serikali tunafanya maandalizi
pamoja na Sera ili kuhakikisha kwamba tuna dhibiti na kuimarisha mapambano
dhidi ya madawa ya kulevya.
SPIKA: Tunaendelea swali mnalipenda hilo badilisheni tabia. Mheshimiwa
Suleiman Nchambi.
Na. 149
Ujenzi wa Vituo Afya na Zahanati Kishapu
MHE. SULEIMAN N. SULEIMAN aliuliza:-
Vituo vingi vya Afya pamoja na Zahanati katika Jimbo la Kishapu
vimefikia lenta katika Ujenzi.
Je, Serikali ina mpango gani wa kumaliza vituo hivyo ili wananchi wapate
huduma?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA
MITAA (TAMISEMI) alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, ninaomba
kujibu swali la Mheshimiwa Suleiman Nchambi Suleiman, Mbunge wa Jimbo la
Kishapu, kama ifuatavyo:-
-
Nakala ya Mtandao (Online Document)
21
Miradi ya ujenzi wa zahanati na vituo vya Afya huibuliwa na wananchi
wenyewe kupitia mpango wa Fursa na Vikwazo katika Maendeleo (O&OD) na
unatekelezwa kwa ubia kati ya wananchi na Halmashauri. Halmashauri
huchangia gharama ndogo za utekelezaji wa miradi hiyo kwa kuwezesha
upatikanaji wa vifaa pamoja na usimamizi.
Mheshimiwa Spika, ni kweli katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu vipo
vituo vya Afya 6 na Zahanati 26 ambazo ujenzi wake umeanza na
haujakalimika. Ujenzi wa vituo na zahanati ulianza mwaka 2012/2013 kwa
gharama ya shilingi milioni 77.7 hadi sasa jumla ya Zahanati 6 zipo katika hatua
ya lenta ambazo ni Mangu, Mwaweja, Mwamashimba, Isagala, Busongo na
Msagala na kituo kimoja cha Afya cha Bubiki na vituo vya afya vya Dulisi na
Ng‟wanghalanga vimepanuliwa.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/2014 Halmashauri iliidhinishiwa
shilingi milioni 215.8 kutoka katika Mfuko wa Maendeleo wa Afya ya Msingi
(MMAM) kati ya fedha hizo kiasi kilichopokelewa ni shilingi milioni 187.5 sawa na
87% ya Bajeti Halmashauri imetumia fedha hizi katika ujenzi wa majengo ya
wagonjwa wa nje (OPD) katika vituo vya Afya vya Dulisi na Ng‟wanghalanga.
Mheshimiwa Spika, katika Bajeti ya mwaka 2014/2015 Halmashauri ya
Wilaya ya Kishapu ilitengewa milioni 149.8 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya
MMAM. Kipaumbele cha Halmashauri katika matumizi ya Fedha ni katika
kukamilisha ujenzi wa OPD na kujenga nyumba moja (two in one) katika kituo
cha afya cha Dulisi.
Serikali itaendelea kutenga Bajeti kila mwaka ili kuhakikisha majengo
hayo yanakamilishwa kwa kushirikisha nguvu za wananchi ili Sera ya afya ya
kuwa na kituo cha afya kila Kata na Zahanati kila kijiji iweze kutekelezwa
kikamilifu.
Aidha, ninachukua fursa hii kuzikumbusha Halmashauri zote kuhakikisha
kuwa kipaumbele kinawekwa katika kumalizia miradi ya zamani kabla ya
kuanza miradi mipya. (Makofi)
MHE. SULEIMAN N. SULEIMAN: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru sana
kwanza ninaomba nimpongeze sana Mheshimiwa Waziri Mkuu kupitia Wizara
yake ya TAMISEMI kupitia Wizara yake kwa ushirikiano anaotupa wananchi wa
Kishapu na Halmashauri yetu, ninayo maswali mawili ya nyongeza.
-
Nakala ya Mtandao (Online Document)
22
Kwa kufuata utaratibu wa Bajeti ya milioni mia mbili na mia moja na
hamsini na kwa kuwa Halmashauri ya Kishapu inayo miradi takribani 26 ya
Zahanati za 2013/2014 na Vituo vya Afya zaidi ya kumi kwa 2013/2014.
Sasa swali langu ni hili. Kwa kuwa Vituo vya Afya vitakuwa na thamani ya
zaidi ya shilingi bilioni tatu na Zahanati zitakuwa na thamani ya takribani bilioni
tatu. Kama tutafuata utaratibu wa Bajeti ni wazi kuwa tutakamilisha baada ya
miaka isiyopungua ishirini.
Je, Mheshimiwa Waziri uko tayari kupokea maombi maalum kama
ulivyofanya katika Hospitali yetu ya Wilaya ukatusaidia?
Kwa kuwa Kishapu miradi ya Zahanati na Vituo vya Afya na hospitali ya Wilaya
inakwenda kwa kasi kama nilivyoeleza kuwa watu wa Kishapu ni sharp Mbunge
wao sharp, na wananchi wote ni sharp.
Je, Wizara iko tayari kutuandalia Wafanyakazi ili tunapokamilisha mara
moja wafanyakazi wawepo ili wananchi wa Kishapu wanufaike na Serikali yao
ya Chama cha Mapinduzi (CCM) makini?
SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri ninaomba ujibu kwa kifupi sana.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA
MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Spika, kwanza nikushukuru kwa niaba ya
Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa pongezi zake ambazo amezitoa kwa Ofisi ya
Waziri Mkuu.
Lakini la pili la ushuhuda huyu Kiongozi anayezungumza hapa amefanya
mambo makubwa katika Wilaya yake amehakikisha wamepata Ambulance
tano pale, amehakikisha kwamba amesaidia hospitali ya Wilaya ikafikia hatua
hiyo anayozungumzia hapa.
Amehakikisha kwamba amechangia mifuko 4,000 katika hiyo Halmashauri
yake kwa ajili ya kujenga hiyo Hospitali ya Wilaya. It is my judgment kama
Member wa Parliament kusema kwamba huyu Mbunge ni Mbunge serious
anajua anachofanya katika Halmashauri yake.
-
Nakala ya Mtandao (Online Document)
23
Sasa kuhusu hizi hela anazozizungumza hapa huyu Bwana anazungumza
habari ya shilingi nbilioni sita ndizo zinazungumzwa hapa hela za mwaka huu
tunaokwenda nao ni shilingi bilioni moja na themanini na saba ndizo
walizotengewa kwa ajili ya Bajeti yote kwa mambo ya afya.
Mwaka huu tunaokwenda nao tumewatengea shilingi milioni mia tisa na
hamsini na tatu Development ni shilingi milioni mia mbili na hamsini na
Development kwa mwaka huu tunaokwenda nao ambayo imepitishwa hapa ni
mia moja na arobaini na saba.
Tutakachofanya hapa tutakwenda kuangalia hiyo special request
anayozungumza. Special request ikiombwa na ili watu wengine wajue,
Halmshauri inaambiwa kuwa wewe special request yako uliyoomba
umekubaliwa kiasi hiki. Tutakwenda kuangalia kwenye special request na kwa
kipaumbele chao kwa maana ya (O&OD), tutapeleka huko kama anavyotaka
kushauri Mheshimiwa Mbunge. (Makofi)
Na. 150
Ucheleweshaji wa Kupandishwa Daraja Wakufunzi
wa Vyuo vya Elimu.
MHE. MARTHA M. MLATA (K.n.y. DIANA M. CHILOLO) aliuliza:-
Kumekuwa na malalamiko ya wakufunzi wa vyuo vya Ualimu nchini
kuhusu kucheleweshwa kupandishwa madaraja.
(a) Je, hadi sasa ni wakufunzi wangapi wa vyuo vya Ualimu nchini
hawajapandishwa madaraja?
(b) Je, Serikali gani ina mkakati gani wa kuhakikisha malalamiko hayo
yanamalizwa?
WAZIRI WA NCHI,OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA
alijibu:-
Mheshimiwa Spika, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Diana Mkumbo
Chilolo, Mbunge, lenye sehemu(a) na (b), kama ifuatavyo:-
-
Nakala ya Mtandao (Online Document)
24
(a) Mheshimiwa Spika, Watumishi hupandishwa vyeo kwa kuzingatia sifa
zilizoainishwa katika miundo ya maendeleo ya Utumishi, Ikama
iliyodhihirishwa, Fedha za kulipa mishahara ya Vyeo vipya na utendaji
mzuri wa kazi hakuna sababu ya Watumishi kukaa kwenye Cheo
Kimoja kwa muda mrefu endapo ametimiza vigezo hivi.
(b)
Katika mwaka wa fedha 2013/2014 Serikali ilipanga kuwapandisha vyeo
wakufunzi 696 na hadi kufikia mwezi Machi, 2014 wakufunzi 282 walikuwa
wamepandishwa vyeo wakufunzi 414 hawakupandishwa cheo na kati yao
wakufunzi 247 hawakutimiza masharti ya muundo wao wa maendeleo ya
Utumishi na wakufunzi 167 hawakuleta taarifa zao kiutendaji kazi.
Mheshimiwa Spika, idara ya Utumishi wa walimu (TSD) imewahimiza waajiri
wa wakufunzi hao kuwasilisha taarifa zao ili nao waweze kupandishwa vyeo.
(c) Mheshimiwa Spika, ili kuondokana na malalamiko ya wakufunzi wa vyuo
vya Elimu nchini Serikali imepanga mikakati ifuatayo:-
(i) Kusafisha taarifa za kiutumishi na mishahara ya wakufunzi wa vyuo vya
elimu sambamba na Watumishi wengine wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi ili kuhakikisha kwamba kila mwanafunzi analipwa mshahara sahihi
kulingana na cheo chake cha sasa.
(ii) Kurekebisha mishahara ya wakufunzi hawa kwa wakati kupitia Mfumo wa
Taarifa za kiutumishi na mishahara (HCMIS) pale wanapopandishwa cheo ili
kuepuka madai ya malimbikizo ya mshahara.
(iii) Kuwataka Wakuu wa Vyuo kujaza mkikataba ya utendaji kazi
(Performance Contract) kila mwanzo wa mwaka wa fedha (Mwezi Julai)
kufanya tathimini ya nusu mwaka (Mid-year Performance Review) mwezi
Desemba kwa kufanya tathimini ya ya mwisho wa mwaka (Annual Perfomance
Review) mwezi Juni kwa wakati ili kuepuka uwezekano wa baadhi ya wakufunzi
kukosa taarifa za utendaji kazi wakati wa zoezi la kuwapandisha vyeo.
Mheshimiwa Spika, ninapenda kuwahimiza wakufunzi wa Vyuo vya
Ualimu kuhakikisha kuwa wanasoma na kuelewa sifa zinazotakiwa kwa mujibu
wa Muundo wao wa Utumishi.
MHE. MARTHA M. MLATA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Namshukuru
Mheshimiwa Waziri kwa majibu mazuri, lakini naomba nimuulize tu maswali
mawili ya nyongeza. Kwanza, matatizo ya Walimu pamoja na Wakufunzi wote
yanatokana na kutokuwa na chombo maalum cha kushughulikia matatizo yao
na kwa sababu Mheshimiwa Waziri aliahidi kuitisha kikao maalum cha wadau
-
Nakala ya Mtandao (Online Document)
25
kwa ajili ya kushughulikia na kuhakikisha chombo hicho kinapatikana, naomba
alieleze Bunge hili na Watanzania wote, je, hatua hiyo imefikia wapi?
Mshahara anaopata Mkuu wa Chuo yeyote anaoufahamu yeye
Mheshimiwa Waziri pamoja na Wakuu wa Vyuo hao. Je, unastahili kulingana na
wadhifa huo walionao?
Mheshimiwa Spika, ahsante. (Makofi)
SPIKA: Haya Mheshimiwa Waziri wa Nchi, hicho chombo kina hoja inakuja.
WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA:
Mheshimiwa Spika, ni kweli niliahidi hapa Bungeni kwamba tutawaita wadau
kuhusu kuanzishwa kwa chombo maalum cha kushughulikia masuala ya
Walimu, lakini nilikaa pamoja na Mwenyekiti wa Kamati yako ya Huduma za
Jamii, Mheshimiwa Mama Sitta, tumekaa pamoja, tulishauriana, akaomba
kwanza kabla ya kuwaita wadau, mimi na ofisi yangu twende kwanza
tukajifunze kwa wenzetu Kenya kama walivyofanya wao na baada ya hapo
ndio tuite kikao cha wadau. Kwa hiyo, tumeshaelewana kuhusu suala hili.
Mheshimiwa Spika, suala kuhusu mshahara wa Wakuu wa Vyuo hivi vya
Wlimu. Mshahara wa Mkuu wa Chuo cha Walimu unaendana na muundo wa
utumishi wa wakufunzi wa vyuo hivyo. Kwa hiyo, mshahara ule anastahili na ni
kulingana na muundo wao wa utumishi na pia kuna nyongeza ambayo
anapata kama Mwalimu au kama Mkuu wa Chuo cha Ualimu.
SPIKA: Ngoja tuendelee na swali lingine muda umekwenda. Tunakwenda
Wizara ya Nishati na Madini, Mheshimiwa Profesa Kahigi atauliza swali hilo.
Na. 151
Ukosefu wa Umeme Shule za Bukombe
MHE. PROF. KULIKOYELA K. KAHIGI aliuliza:-
Ukosefu wa umeme katika shule za Msingi na Sekondari katika Wilaya ya
Bukombe ni kikwazo kikubwa katika ufundishaji na kujifunza mashuleni:-
Je, ni lini mradi wa Umeme Vijijini utapeleka umeme katika shule hizo ili
kuboresha huduma ya utoaji na upokeaji elimu ikiwa ni pamoja na elimu ya
TEHAMA?
-
Nakala ya Mtandao (Online Document)
26
NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI, (MHE. CHARLES M. KITWANGA)
alijibu:-
Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Profesa
Kulikoyela Kanalwanda Kahigi, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Serikali ina mpango wa kupeleka umeme Makao
Makuu ya Wilaya ya Bukombe (Ushirombo) pamoja na Vijiji/ maeneo ya jirani
kupitia mradi wa Electricty “v”, ambao ni miongoni mwa miradi iliyopata ufadhili
wa Benki ya Manedeleo ya Afrika (AFDB), Mradi huo unahusu kupeleka umeme
kwenye Vijiji/maeneo zaidi ya 25 Wilayani Bukombe.
Mheshimiwa Spika, umeme katika Mradi huu utaunganishwa kutokea
kituo cha kupozea umeme katika Kijiji cha Ilogi kutoka kwenye kituo kikubwa
cha kupozea umeme cha Bulyankulu. Kazi za Mradi zitahusisha; Ujenzi wa laini
yenye urefu wa kilometa 190 yenye msongo wa kilovoti 33 kutoka Kijiji cha Ilogi
hadi Ushirombo; ufungaji wa vipoza umeme 41; ujenzi wa laini za umeme wa
msongo wa volti 400/230 zenye urefu wa kilometa 88; na kuunganisha wateja
wa awali wapatao 5000.
Mradi huu utagharimu kiasi cha Dola za Marekani 10,328,228. Hatua
iliyofikiwa kwa sasa ni pamoja na vifaa vya ujenzi wa mradi kufika Ushirombo na
Mkandarasi (Eltel Networks) anaendelea na ujenzi wa laini ya msongo wa
kilovoti 33. Mradi huu unatarajiwa kukamilika mwezi Septemba, 2014.
Mheshimiwa Spika, Serikali pia itatekeleza mradi wa umemenuru katika
maeneo mbalimbali nchini, ikiwemo Wilaya ya Bukombe kupitia Mradi wa SSMP
II (Sustainable Solar Market Programme II) utakaoanza kutekelezwa mwezi Julai,
2014. Katika Wilaya ya Bukombe, Mradi utanufaisha wakazi wa vijiji 52, vituo vya
afya viwili (2), dispensary kumi (10), shule 13 na vituo vya Polisi vitatu (3).
Gharama ya utekelezaji wa Mradi kwa loti ya Bukombe ni jumla ya Dola za
Marekani 1,277,023.68 na Mradi unategemewa kukamilika mwezi Juni, 2016.
SPIKA: Ahsante. Mheshimiwa Profesa Kahigi, swali la nyongeza.
MHE. PROF. KULIKOYELA K. KAHIGI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Ninayo
maswali mawili ya nyongeza. Kwanza, namshukuru Naibu Waziri kwa majibu
ambayo yanatia matumaini, lakini tatizo kubwa la miradi hii ya umeme ni
kwamba, ama inachelewa kuanza au inachelewa kukamilika. Mradi huu
alioutaja wa electricity five kwamba ulikuwa ukamilike Juni mwaka huu, lakini
taarifa nilizonazo asubuhi hii ni kwamba, bado upo katika hatua za mwanzo.
-
Nakala ya Mtandao (Online Document)
27
Swali langu la kwanza, Mradi huu utakamilika lini? Maana ulitakiwa ukamilike
Juni mwaka huu.
La pili, umesema kwamba umemenuru utapelekwa Bukombe kuanzia
Julai mwaka huu, naomba tu majina ya Shule kumi na tatu ambazo umesema
kwamba zitapelekewa umeme.
Mheshimiwa Spika, ahsante sana.
SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri majibu!
NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI(MHE. CHARLES M. KITWANGA):
Mheshimiwa Spika, kama nilivyojibu katika swali la msingi kwamba mradi huu
utakamilika Septemba mwaka huu na mkataba ndivyo ulivyo.
Swali lake la pili, naomba mpatie majina ya shule ambazo anazihitaji kwa
sababu siwezi kuyataja yote hapa.
SPIKA: Ahsante naomba muangalie muda na nina swali langu moja
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Mheshimiwa Josephine Chagula atauliza
swali hilo!
Na. 152
Mlipuko wa Malaria Mkoa wa Geita
MHE. JOSEPHINE T. CHAGULA aliuliza:-
Mkoa wa Geita una tatizo kubwa sana la maambukizi ya malaria
yanayosababishwa na mashimo makubwa yalioachwa wazi baada ya
uchimbaji wa madini:-
Je, Serikali ina mpango gani wa kudhibiti uharibifu huo wa mazingira
katika Mkoa huo na kuondoa tatizo la mlipuko wa malaria?
NAIBU WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,
naomba kujibu swali la Mheshimiwa Josephine Thabita Chagula, Mbunge wa
Viti Maalum kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Geita ilipewa hadhi ya kuwa Mkoa Julai, 2011.
Takwimu za matokeo ya utafiti wa Taifa katika ngazi ya kaya (Tanzania HIV,
Malaria Indicator Survey- THMIS), za mwaka 2011/2012, zilionesha kiwango cha
-
Nakala ya Mtandao (Online Document)
28
maambukizi ya malaria Mkoa wa Geita kuwa ni asilimia 33. Kwa takwimu hizi, ni
dhahiri Mkoa wa Geita una kiwango kikubwa cha maambukizi ya malaria kuliko
Mikoa yote nchini, utafiti unaofuata utafanyika 2015/2016 kwani tafiti hizi
hufanyika kila baada ya miaka minne.
Mheshimiwa Spika, mashimo yaliyoachwa wazi baada ya kuchimba
madini husababisha maji kutuama na kuwa chanzo cha mazalio ya mbu.
Vyanzo vingine vya mbu kuzaliana ni vidimbwi, matairi chakavu ya magari,
mashimo ya vyoo na kadhalika. Sheria ya Uchimbaji wa Madini namba 14 ya
2010, pamoja na Sheria ya Usimamizi wa Mazingira Na. 20 ya 2004 na Kanuni
zake za Athari kwa Mazingira za 2005, zinawataka wachimbaji kuonesha
“Mining Closure Plan,” lengo likiwa kuwabana kisheria wenye migodi kufukia
mashimo baada ya uchimbaji wa madini kumalizika. Upande wa mazingira,
mwekezaji anahitajika kufanya tathmini ya athari za mazingira (environmental
impact assessment) na kuacha mazingira yakiwa salama.
Mheshimiwa Spika, kwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais
(Mazingira) na Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, Wizara inazitaka Mamlaka ya
Usimamizi katika mikoa yote kuhakikisha zinasimamia kikamilifu utekelezaji wa
Sheria hizi na kanuni zake.
Mheshimiwa Spika, kutokana na ukubwa wa tatizo la malaria katika
Mikoa yote ya Kanda ya Ziwa, ikiwemo Geita, hatua zinazochukuliwa
kupunguza maambukizi ya malaria ni:- upulizaji wa dawa ya ukoko katika
majumba ili kudhibiti mbu wapevu wa malaria; kuongeza matumizi ya
vyandarua kwa kupitia kampeni ya ugawaji kwa watu wa kaya (Replacement
Universal Mass Campaign kama utakavyofanyika mwakani 2014/2015, Geita
watapata vyandarua vipatavyo 900,000.
Mheshimiwa Spika, aidha, mpango wa kuangamiza mazalio ya mbu kwa
kutumia viuatilifu vya kibaiolojia (bioarvicides) katika Mitaa ya Mji wa Geita
utaanza mara baada ya Kiwanda cha Kuzalisha Viuatililafu iliyojengwa Kibaha
kwa kushirikiana na Serikali ya Cuba kuanza uzalishaji.
SPIKA: Ahsante Mheshimiwa Josephine Chagula, swali la nyongeza.
MHE. JOSEPHINE T. CHAGULA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa
nafasi hii ya kuuliza swali la nyongeza. Nashukuru sana kwa majibu ya Naibu
Waziri lakini nina swali moja tu. Kwa kuwa Naibu Waziri amekiri kwamba, Mkoa
wa Geita unaongoza kwa kuwa na wagonjwa wengi sana wa malaria na hii ni
kutokana na mashimo mengi yayoachwa wazi kwa muda mrefu na wachimbaji
wa madini.
-
Nakala ya Mtandao (Online Document)
29
Je, Serikali sasa haioni kuna haja ya kuleta Sheria ambayo itawataka
wachimbaji hawa wa madini kufukia mashimo yao ya awali kabla ya kuanza
tena kuchimba mashimo mengine, ili tuweze kunusuru afya na maisha ya
wananchi wa Mkoa wa Geita? (Makofi)
SPIKA: Ahsante. Mheshimiwa Naibu Waziri majibu!
NAIBU WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII: Mheshimiwa Spika, suala hili
la mazingira kulingana na Mining Closure Plan ambayo kisheria inabidi wenye
migodi watimize masharti haya. Ndio sababu inalazimu kuainisha bayana
kabisa suala zima la tafiti ya mazingira (Enviromental Impact Assessment)
ambayo inakuwa katika mpango mzima. Lakini kwa kushirikiana na Wizara ya
Madini na Nishati, suala hili tutashirikiana kufuatilia ili kuona taratibu zote za
kisheria zimefuatwa.
SPIKA: Ahsante. Waheshimiwa Wabunge najua mnapenda kuuliza
maswali, lakini muda wenyewe umekwisha. Kwa hiyo, niwatambue wageni
waliopo humu ndani.
Tuna wageni wa Mheshimiwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo ambao ni Wakurugenzi, Wakurugenzi Wasaidizi, Wenyeviti wa Bodi,
Maafisa kutoka Wizarani na Watumishi kutoka Asasi mbalimbali zilizo chini ya
Wizara hiyo. Yupo anayeongoza timu hiyo ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara,
Ndugu Sihaba Nkinga, asimame alipo! Halafu pia yupo na Naibu Katibu Mkuu
Profesa Elisante Ole Gabriel. (Makofi)
Tuna Wageni wa Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
(Mheshimiwa Juma Nkamia), ambao ni Mkurugenzi wa Steps Entertainments
and Steps Solar huyo Ndugu Dileshi Solanky. Kama nime-mess up the names I
am sorry.
Halafu kuna Ndugu Juma Mtetwa-TBC-Ulimwengu wa filamu, asimame
alipo. Okay ahsante, yupo upande huu hapa. (Makofi)
Yupo ndugu Francis Robert ambaye ni Mkurugenzi wa Radio Five.
(Makofi)
Tuna wageni wengine wa Mheshimiwa Naibu Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo ni wanafunzi nane kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma.
Wasimame walipo. (Makofi)
-
Nakala ya Mtandao (Online Document)
30
Wageni wa Mheshimiwa Mwigulu Lameck Nchemba ambao ni wanafunzi
20 kutoka Shule ya Sekondari Tumaini, Singida wakiongozwa na Walimu wao
Ndugu Atupele Mbila Joel na Ndugu Khard Mtoi. Wasimame wanafunzi hawa
kama wapo ndani! Ahsante sana karibuni naomba msome kwa bidii. (Makofi)
Kuna Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communication, Bwana Tido
Mhando alipo asimame! Yeye amekosa nafasi? Okay alikosa nafasi labda,
halafu tuna wageni 27 wa Mheshimiwa Freeman Aikaeli Mbowe, Kiongozi wa
Kambi Rasmi ya Upinzani, Bungeni pamoja nao yupo Diwani wa CHADEMA,
Ndugu Sinock Olenairuko, nimesema vibaya? Wameniandikia CHADEMA.
(Makofi)
Halafu wameniandikia pia na Ndugu Tehera Kipara, Mwenyekiti wa CCM
Kata, hawakusema! Naomba hawa wageni wawili wasimame walipo kama
nimembatiza Chama basi Kiongozi wao, ahsanteni sana. Kwa hiyo, inaonesha
Kiongozi wa Kambi ya Upinzani hana ubaguzi. (Makofi)
Nina wageni wa Mheshimiwa Rajab Mbarouk Mohammed, ambaye ni
Waziri Kivuli, Sera, Uratibu na Bunge ambao ni Wanakwaya wa kwaya ya
Mtakatifu Joseph Mfanyakazi Chuo Kikuu. Haya msimame wanakwaya nyie,
ahsante sana. Ahsante sana sijui Kwaya ya kitu gani hiyo. (Makofi)
Kuna wageni watatu wa Mheshimiwa Dkt. Anthony Mbassa kutoka
Bihalamuro Magharibi wakiongozwa na Ndugu Severine Stephano. Huyu yupo
wapi? Wageni wako wapi? Haya Zephrine yupo pale na wageni wengine
wasimame. (Makofi)
Kuna wageni wa Mheshimiwa Paul Lwanji, Mbunge wa Manyoni
Magharibi ambao ni Mwenyekiti wa Riadha Mkoa wa Singida ambaye ni Ndugu
Elia Nollo na Mwenyekiti wa CCM mstaafu Kata ya Sanjaranda, Ndugu Hassan
Kashinje naomba wasimame walipo, kuna wengine watakosa nafasi. (Makofi)
Kuna Mheshimiwa Profesa Msolla wa Kilolo ambao wanaongozwa na
ndugu Sifuni Makongwa, Mwenyekiti wa UVCCM, Kilolo. Wasimame hao
wageni. Ahsanteni sana. (Makofi)
Kuna wageni wa Mheshimiwa Ester Bulaya ambao ni wanafunzi wa Chuo
Kikuu cha Dodoma na wenyewe wasimame walipo. Ahsanteni sana msome
kwa bidii. (Makofi)
Tuna wageni wanne wa Mheshimiwa Joseph Mbilinyi, Waziri Kivuli Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo wakiongozwa na Ndugu John Mwambigija,
-
Nakala ya Mtandao (Online Document)
31
Mwenyekiti wa CHADEMA, Mbeya Mjini. Wasimame hao wote walipo.
Ahsanteni sana. (Makofi)
Nina wageni waliokuja Bungeni kwa ajili ya mafunzo hawa ni wanafunzi
42 na Walimu watatu kutoka Chuo cha Red Cross, Makole. Naomba
wasimame wote walipo, okay ahsante sana na tunawatakia kazi njema.
(Makofi)
Tuna wanafunzi 31 kutoka Chuo cha Mipango, Dodoma, naomba
msimame mlipo kama mpo. Ahsante sana msome kwa bidii. (Makofi)
Tuna wageni watatu kutoka Aseki Business School wakiongozwa na
Ndugu Omari Kiputiputi, Mkuu wa Chuo cha Aseki hiyo, wasimame walipo.
Ahsanteni karibuni sana na wageni wengine ambao hamkukaribishwa
mnakaribishwa. (Makofi)
Matangazo ya kazi; Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma za
Jamii, Mheshimiwa Margaret Sitta, anaomba niwatangazie Wajumbe wa
Kamati yake kwamba leo saa saba mchana kutakuwa na Kikao katika ukumbi
wa Pius Msekwa C.
Pia mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, Mheshimiwa
Victor Mwambalaswa anaomba niwatangazie Wajumbe wa Kamati yake
kwamba, leo mchana watakuwa na Kikao chao ambacho kitafanyika ukumbi
wa Hazina ndogo Na.125.
Waheshimiwa Wabunge, tumekula sana muda, naomba tuendelee!
MHE. JOHN J. MNYIKA: Mwongozo wa Spika.
SPIKA: Mwongozo baadaye.
HOJA ZA SERIKALI
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa
Mwaka 2014/2015 – Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo
-
Nakala ya Mtandao (Online Document)
32
SPIKA: Sasa namwita Mtoa hoja!
Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara
ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa Mwaka 2014/2015 Kama
Ilivyosomwa Bungeni
WAZIRI WA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO: Mheshimiwa
Spika, naomba nianze kutumia fursa hii kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa
kunilinda na kunipa nguvu ya kutekeleza majukumu yangu na kuniwezesha
kusimama mbele ya Bunge lako Tukufu kuwasilisha bajeti hii.
Mheshimiwa Spika, napenda kutoa pongezi kwa Wabunge wapya
waliochaguliwa hivi karibuni kwa ushindi wa kishindo ambao ni Mheshimiwa
Yusuf Salim Hussein, Mbunge wa Chambani; Mheshimiwa Godfrey William
Mgimwa, Mbunge wa Jimbo la Kalenga; na Mheshimiwa Ridhiwani Jakaya
Kikwete, Mbunge wa Jimbo la Chalinze. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, napenda pia kuchukua fursa hii kuwapa pole familia
za wanahabari, wasanii na wanamichezo pamoja na tasnia nzima za Habari,
Utamaduni na Michezo kwa kuondokewa na wapendwa wetu. Mungu azilaze
roho za marehemu mahali pema peponi. Amina.
Mheshimiwa Spika, kufuatia taarifa iliyowasilishwa leo kwenye Bunge lako
Tukufu na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii,
sasa naomba kutoa hoja kwamba, Bunge lako Tukufu lipokee, lijadili na
kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo na Asasi zake kwa mwaka wa fedha wa 2014/2015.
Mheshimiwa Spika, hotuba yangu imegawanyika katika maeneo makuu
matano kama ifuatavyo:-
Eneo la kwanza, ni Utangulizi; eneo la pili ni Majukumu ya Wizara; eneo la
tatu ni Mapitio ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa mwaka 2013/2014;
eneo la nne ni Mpango na Bajeti kwa mwaka 2014/2015; na eneo la tano ni
Hitimisho.
Mheshimiwa Spika, majukumu ya Wizara; Wizara yangu inatekeleza
majukumu yafuatayo:-
(i) Kuandaa na kusimamia utekelezaji wa Sera za Sekta za Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo;
-
Nakala ya Mtandao (Online Document)
33
(ii) Kuratibu na kusimamia masuala ya maendeleo ya vijana ili kuwawezesha
kujitambua, kujiajiri, kuajirika, kuwajibika na kujitegemea;
(iii) Kuwa Msemaji Mkuu wa Serikali na kusimamia vyombo vya Habari nchini;
Kuratibu na kusimamia maendeleo ya utamaduni nchini;
(iv) Kuratibu na kusimamia maendeleo ya michezo nchini;
(v) Kusimamia utendaji kazi wa Asasi, Miradi na programu zilizo chini ya
Wizara; na
(vi) Kuendeleza, kuwezesha na kuratibu masuala ya kuwajengea uwezo
watumishi wa Wizara.
Mheshimiwa Spika, Mapitio ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa
mwaka wa fedha 2013/2014. Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2013/2014,
Wizara ilipanga kukusanya mapato ya jumla ya shilingi milioni mia nane
themanini na mbili, mia mbili na tatu elfu (882,203,000) kutoka vyanzo
mbalimbali. Hadi kufikia mwezi Aprili, 2014, jumla ya shilingi milioni mia sita sitini
na tatu, ishirini na tisa elfu, mia tano sitini na tisa (663,029,569)zilikusanywa
ambazo ni sawa na asilimia sabini na tano (75%) ya lengo la makusanyo kwa
mwaka. Kwa upande wa fedha za Matumizi ya kawaida, Wizara ilitengewa
jumla ya shilingi bilioni kumi na saba, milioni mia sita ishirini na nane, arobaini na
tano elfu (17,628,045,000).
Mheshimiwa Spika, fedha hizo zilijumuisha Mishahara ya Wizara; shilingi
bilioni mbili, milioni mia sita kumi na saba, mia tano tisini na nane elfu
(2,617,598,000) na Asasi ni Shilingi bilioni sita, milioni mia sita thelathini na tisa, mia
tano ishirini na saba elfu (6,639,527,000). Matumizi Mengineyo ya Wizara ni Shilingi
bilioni nne, milioni mia tisa arobaini na moja, mia tisa ishirini elfu
(4,941,920,000)na Asasi ni shilingi bilioni tatu, milioni mia nne ishirini na tisa
(3,429,000,000).
Mheshimiwa Spika, hadi mwezi Aprili, 2014, jumla ya shilingi bilioni kumi na
tatu, milioni mia mbili tisini na mbili, mia tano thelathini na tisa elfu, mia nne tisini
na nane (13,292,539,498) za Matumizi ya Kawaida zilipokelewa na kutumika.
Kati ya fedha hizo Matumizi Mengineyo ni shilingi bilioni nne, milioni mia saba
arobaini, mia tisa hamsini na saba elfu (4,740,957,000)na Mishahara ni shilingi
bilioni nane, milioni mia tano hamsini na moja, mia tano themanini na mbili elfu,
mia nne tisini na nane (8,551,582,498).
Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Miradi ya Maendeleo, Wizara
ilitengewa jumla ya shilingi bilioni kumi na mbili, milioni mia saba
-
Nakala ya Mtandao (Online Document)
34
(12,700,000,000). Hadi kufikia mwezi Aprili, 2014 jumla ya shilingi bilioni nne, milioni
mia tatu ishirini na saba, mia tano elfu (4,327,500,000) zilipokelewa ambazo ni
sawa na asilimia 34 na shilingi bilioni mbili, milioni mia tatu na kumi na ishirini na
moja elfu (2,310,021,000) zilitumika.
Miradi iliyotekelezwa ni pamoja na Upanuzi wa Usikivu wa Shirika la
Utangazaji Tanzania (TBC), Ujenzi wa Ofisi - BAKITA, Programu ya Urithi wa
Ukombozi wa Bara la Afrika na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana.
Mheshimiwa Spika, Sekta ya Habari; katika mwaka 2013/2014, Wizara
ilikabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo ni pamoja na baadhi ya
Vyombo vya Habari kukiuka sheria kwa kuandika na kurusha habari ambazo
hazizingatii kanuni na maadili ya taaluma ya habari. Pia ongezeko la mifumo
na njia za mawasiliano kama mitandao ya kijamii ambayo mingine imetumiwa
kuathiri maudhui ya habari zinazotolewa.
Mheshimiwa Spika, Wizara imechukua hatua mbalimbali za kukabiliana
na changamoto hizo kwa kutoa onyo na kufungia baadhi ya vyombo vya
habari vilivyokiuka maadili. Wizara pia imeelekeza Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania (TCRA) kutekeleza kikamilifu mpango wa kusajili wamiliki wote wa
mitandao hiyo. Aidha, Wizara inaendelea kutoa elimu na kuwaelekeza wamiliki
na Wahariri wa vyombo vya habari kufuata sheria, kanuni na miongozo
iliyowekwa. Wizara inaendelea kutoa elimu kwa wananchi kukataa kutumia
fursa hizi za mitandao ya kijamii kueneza chuki, uchochezi na vijiwe vya udaku.
Mheshimiwa Spika, kwa kushirikiana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa
Serikali, Wizara imekamilisha maandalizi ya Muswada wa Sheria ya Kusimamia
Vyombo vya Habari na sasa uko katika hatua nzuri za mwisho. Kwa kuzingatia
utaratibu uliopo, Muswada huu utafikishwa katika Bunge lako Tukufu lijalo la
kutunga Sheria.
Mheshimiwa Spika, ili kuweza kuimarisha njia za mawasiliano kati ya
Serikali na wananchi wake, Wizara yangu inafanya maboresho ya Tovuti ya
Wananchi ili kuweza kuimarisha mifumo na muonekano wa Tovuti hiyo.
Maboresho hayo yakikamilika, yatawawezesha wananchi popote walipo
kuwasiliana na Serikali kwa kutumia njia za kisasa. Aidha, itawapunguzia
wananchi gharama za kuwasilisha kero, hoja na maoni mbalimbali katika taasisi
za Serikali. Kazi ya kuijenga upya na kuimarisha Tovuti hiyo ili kuwa na
muonekano mpya unaokidhi mabadiliko ya sasa ya sayansi na teknolojia
inatarajiwa kukamilishwa mwisho wa mwaka wa fedha 2013/2014.
Mheshimiwa Spika, Wizara, imeendelea kukusanya habari, kupiga picha
za matukio mbalimbali ya Serikali na kuzihifadhi katika maktaba; pamoja na
-
Nakala ya Mtandao (Online Document)
35
kuzisambaza kwenye vyombo mbalimbali vya habari kwa lengo la kutoa habari
na kuelimisha jamii. Wizara kama Msemaji Mkuu wa Serikali ilifafanua masuala
na hoja mbalimbali zinazohusu Serikali.
Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuratibu na kusimamia Vitengo
vya Mawasiliano Serikalini kwa lengo la kutoa habari na kuelimisha umma juu ya
utekelezaji wa majukumu ya Serikali. Wizara imetoa mwongozo ulioainisha
taratibu za kuendesha vitengo hivyo na kuhimiza Wizara na Asasi zote za umma
kuajiri Maafisa Mawasiliano Serikalini.
Mheshimiwa Spika, jumla ya mikutano 255 ya wasemaji wa Asasi za
Serikali na Vyombo vya Habari ilifanyika kuwaelimisha wananchi kuhusu shughuli
mbalimbali za Serikali zinazofanyika.
Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2013/2014, Wizara imeendelea kuratibu
ushiriki wa Vyombo vya Habari katika vikao vya Bunge vilivyofanyika Dodoma
na pia kuhakikisha inawapatia vitambulisho waandishi wa habari wa ndani na
nje wenye sifa za taaluma ya Uandishi wa Habari.
Mheshimiwa Spika, Wizara yangu kwa kushirikiana na Wizara ya
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kupitia TCRA ilikamilisha awamu ya kwanza
ya uhamaji wa kutoka katika mfumo wa utangazaji wa analojia kwenda dijiti.
Baada ya zoezi hili tathmini imefanyika ambayo ilionesha mwitikio mzuri wenye
mafanikio. Hivi sasa zoezi hili limeingia katika awamu ya pili iliyoanza tarehe 31
Machi, 2014 na inatarajiwa kukamilika kabla ya tarehe 30 Juni, 2015.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha wa 2013/2014, Wizara kwa
kushirikiana na TCRA imesajili vituo nane (8) vya redio na vituo viwili (2) vya
televisheni na hivyo kuwezesha Tanzania kuwa na jumla ya vituo tisini na tatu
(93) vya redio na ishirini na nane (28) vya televisheni. Pia uhamaji kutoka mfumo
wautangazaji wa analoji kwenda mfumo wa dijiti umesaidia kupanua wigo wa
masafa na kuongeza ubora wa matangazo.
Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka 2013/2014, Kamati ya
Maudhui ilipokea na kushughulikia malalamiko saba ya vituo vya televisheni na
redio kutokana na kurusha vipindi ambavyo vilikiuka maadili ya utangazaji. Kituo
binafsi cha televisheni kilicholalamikiwa kwa kurusha kipindi kilichokiuka kanuni
na maadili ya utangazaji kilipewa onyo. Pia vituo sita vya redio vilivyolalamikiwa
kwa kurusha vipindi vilivyokiuka kanuni za utangazaji na maadili ya uandishi wa
habari vilipewa onyo na vingine kutozwa faini kati ya shilingi laki mbili (200,000)
na shilingi milioni tano (5,000,000).
-
Nakala ya Mtandao (Online Document)
36
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/2014, Shirika la Utangazaji
Tanzania (TBC) imeendelea kuimarisha upanuzi wa usikivu wa Redio na
Televisheni ya Taifa. TBC ilirusha pia matangazo ya vikao vya Bunge moja kwa
moja, pamoja na matangazo ya Bunge Maalum la Katiba kwa lugha za alama,
kwa ajili ya watu wenye mahitaji maalum.
Mheshimiwa Spika, pamoja na kazi hizo, TBC inakabiliwa na tatizo la
uchakavu wa vifaa vya kurushia matangazo. Uchakavu huo wakati mwingine
umesababisha tatizo la kukatika kwa matangazo yakiwemo matangazo ya
Bunge.
Mheshimiwa Spika, naomba Waheshimiwa Wabunge wawe wavumilivu
kwani Wizara imejipanga katika kuendelea kutatua changamoto hizo ili
kuboresha huduma zitolewazo na TBC. Kupitia Bunge lako Tukufu niwaombe
Waheshimiwa Wabunge watuunge mkono kufanikisha malengo tuliyojiwekea
ya kuimarisha TBC.
Mheshimiwa Spika, katika kuendelea kutatua changamoto za TBC,
mwezi Aprili, 2014, imepokea gari jipya la kisasa la matangazo kutoka Serikali ya
Watu wa China. Gari hili litasaidia sana kuongeza nguvu katika kutatua tatizo la
uchakavu wa vifaa. Sambamba na hatua hizo, wataalam watano (5) wa TBC
walipelekwa nchini China kupata mafunzo maalum ya namna ya kutumia gari
hilo pamoja na vifaa husika.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha wa 2013/2014, Kampuni ya
Magazeti ya Serikali (TSN) imeendelea na mkakati wa upanuzi wa Kiwanda cha
Uchapaji. Katika Mkakati huo, Makubaliano na Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB)
yamekamilika ambapo TIB itaipatia TSN mkopo wa shilingi bilioni 2.7 kwa ajili ya
kujenga jengo la kitega uchumi. Hatua hii itasaidia Kampuni kuongeza uzalishaji
na kuweza kufikisha huduma kwa wananchi wengi zaidi.
Mheshimiwa Spika, katika kupanua wigo wa mapato, TSN na Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA) wameingia mkataba wa ubia wa kuendeleza
kiwanja kilichopo Kitalu Na. 27, Central Business Park, Dodoma, kwa ajili ya
kujenga jengo la kupangisha. Maandalizi ya ujenzi yameanza. Ukamilishaji wa
Mradi huu utasaidia Kampuni kujiongezea mapato zaidi.
Mheshimiwa Spika, katika kuboresha usambazaji wa magazeti, Kampuni
imepata pikipiki 20 toka Serikali ya Watu wa China kwa ajili ya usambazaji wa
mijini. TSN pia imeingia makubaliano na kampuni za usafirishaji ili kusafirisha
magazeti ndani na nje ya nchi ili kuwezesha upatikanaji wa habari za ukweli
kwa wakati.
-
Nakala ya Mtandao (Online Document)
37
Mheshimiwa Spika, Sekta ya Maendeleo ya Vijana; katika kushughulikia
masuala ya vijana mwaka 2013/2014, changamoto mbalimbali zimejitokeza
ambazo ni pamoja na baadhi ya Sekretarieti za Mikoa na Halmashauri za
Wilaya kutokuajiri Maafisa Vijana.
Uelewa mdogo wa vijana katika kubuni na kutayarisha maandiko ya
miradi, kuanzisha na kutekeleza miradi endelevu, vijana wengi kukosa ujuzi na
maarifa ya ujasiriamali na biashara ikiwa ni pamoja na kukosa ujuzi wa matumizi
sahihi ya fedha za mikopo wanazopata kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana
na vijana kushindwa kujitambua na kufanya maamuzi sahihi kuhusu maisha yao.
Mheshimiwa Spika, Sekta ya Maendeleo ya Vijana chini ya Wizara yangu
ina vitengo mahsusi vya kushughulikia hizi changamoto za Vijana. Vitengo hivi
ni Uratibu na Uwezeshaji wa Vijana Kiuchumi; Ushauri Nasaha, Makuzi na
Maongozi, pamoja na Mafunzo na Maendeleo ya Ujuzi. Hii ni kwa mujibu wa
instrument ya Wizara.
Mheshimiwa Spika, kwa kupitia vitengo hivi na kushirikiana na Wadau
mbalimbali kama muundo na majukumu ya Wizara yangu yanavyoelekeza,
Wizara yangu imeendelea kuwajengea vijana uwezo wa kiuchumi kwa kuwapa
mafunzo na ujuzi katika maeneo ya ujasiriamali, uanzishaji wa miradi endelevu
ya uzalishaji mali, uongozi, stadi za maisha na matumizi sahihi ya mikopo kwa
kushirikiana na Benki ya NMB. Katika mwaka wa fedha 2013/2014, jumla ya
Viongozi wa vikundi vya vijana 457 na Watendaji 211 kutoka Wilaya na Mikoa
yote nchini wamenufaika na mafunzo hayo.
Mheshimiwa Spika, ili kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana
hasa wanaomaliza Vyuo Vikuu na Vyuo vya Kati, Wizara kwa kushirikiana na
wadau wa maendeleo ya vijana na Wizara mbalimbali kama vile Kilimo na
Ushirika; Ufugaji; Madini na Nishati na Viwanda imeendelea kuhamasisha vijana
kuunda makampuni binafsi ya biashara na vikundi vya kuzalisha mali ili waweze
kujiajiri na kuajiri wengine na kujiletea maendeleo.
Mheshimiwa Spika, pia Wizara inaendeleza mpango wa kutafutia kazi za
kujitolea vijana hawa ili kuwawezesha kupata uzoefu kabla ya ajira. Mpango
umeanzia Dar es Salaam, mfano ambapo vijana 27 wanafanya kazi sehemu
mbalimbali kwa kujitolea. Wizara pia imehamasisha vijana wa Vyuo Vikuu
kujitolea mashuleni kufundisha kwa kusaidiana na Walimu husika.
Mheshimiwa Spika, Wizara vile vile kwa kushirikiana na Shirika la IYF
imeendelea kuandaa kambi za mafunzo yenye lengo la kubadilisha fikra za
vijana nchini kwa malengo chanya ya kujituma, kupenda kazi, kushirikiana,
kupendana, kupenda nchi na kutii sheria. Kwa mfano, mwaka 2013 vijana 800
-
Nakala ya Mtandao (Online Document)
38
kutoka Mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani walihudhuria kambi ya
Kimataifa iliyofanyika mjini Dar es Salaam.
Mheshimiwa Spika, naendelea kutoa wito na kuhimiza wadau wote wa
maendeleo ya vijana nchini, tuendelee kushirikiana katika kuhakikisha kuwa
vijana wetu wanapata uwezo wa kuwajibika na kuchangia katika maendeleo
ya maisha yao na ya Taifa kwa ujumla. Wizara inaendelea kuhimiza Wakuu wa
Mikoa kutenga maeneo kwa kazi za vijana na muitikio unaendelea kuwa mzuri.
Mheshimiwa Spika, kuhusu Mfuko wa Maendelo ya Vijana; napenda
kulitaarifu Bunge lako Tukufu kwamba, mwongozo wa kusimamia Mfuko huu
umeandaliwa na kusambazwa kwa Makatibu Tawala wa Mikoa yote tangu
mwezi Agosti, 2013. Kulingana na Mwongozo huu, kila Halmashauri inahitajika
kuanzisha SACCOS ya Vijana ambayo itashughulikia utoaji wa mikopo hii. Hadi
kufikia Aprili, 2014, Halmashauri 22 kati ya 151 zimeanzisha SACCOS za Vijana.
Nawapongeza sana wale wote walioweza kufanikisha uanzishaji wa SACCOS
hizi kwa wakati.
Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2013/2014, jumla ya Shilingi bilioni 6.1
zilitengwa kwa ajili ya Mfuko huu. Hadi Aprili, 2014, Wizara imepokea kiasi cha
shilingi bilioni mbili (2,000,000,000). Kati ya fedha hizo zilizokopeshwa ni shilingi
milioni mia moja sabini na mbili, mia sita na tisa elfu (172,609,000) kwa Miradi ya
vikundi vya vijana 25. Hata hivyo, Wizara inaendelea na uchambuzi wa maombi
ya vikundi 1,178 yenye thamani ya shilingi bilioni nane, milioni mia nne ishirini na
moja, mia tisa na sita elfu, mia saba hamsini (8,421,906,750) ili kuweza
kuvikopesha vikundi vitakavyotimiza vigezo vilivyobainishwa kwenye mwongozo.
Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2013, Mbio za Mwenge wa Uhuru
zilizinduliwa na Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi tarehe 5 Mei, 2013 katika Kijiji cha
Chokocho, Mkoani Kusini Pemba na kufikia kilele Mkoani Iringa tarehe 14
Oktoba, 2013 na Mgeni Rasmi alikuwa Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mheshimiwa Spika,kupitia mbio hizo, jumla ya miradi ya maendeleo 1,229
yenye thamani ya shilingi bilioni mia moja hamsini na nane, milioni mia tano
themanini na saba, mia sita sitini na saba elfu, mia sita kumi na tatu na senti
arobaini (158,587,667,613.40) ilizinduliwa au kuwekewa mawe ya msingi.
Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2014 umefanyika tarehe 2 Mei,
2014 Mkoani Kagera; na Mgeni Rasmi alikuwa Mheshimiwa Dkt. Mohamed
Gharib Bilal, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mheshimiwa Spika, dhamana ya kuhakikisha hili linafanyika vizuri
wamepewa vijana. Mbio hizi zinalenga kuhamasisha maendeleo ya wananchi,
-
Nakala ya Mtandao (Online Document)
39
kudumisha umoja, amani, upendo na mshikamano wa Kitaifa. Hivyo basi,
hatuna budi sisi sote kuthamini na kuenzi Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa
mustakabali wa Taifa letu.
Mheshimiwa Spika, sambamba na maadhimisho ya kilele cha Mbio za
Mwenge wa Uhuru, Wizara iliratibu maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kitaifa
ambayo yalianza tarehe 8 hadi 14 Aprili, 2013, Mkoani Iringa. Maonyesho katika
Wiki ya Vijana yalishirikisha wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na Ofisi za Mikoa
10, Idara za Serikali 16, Halmashauri za Wilaya 21, Asasi za Kiraia 14, Vikundi vya
Vijana Wajasiriamali 53, Vyuo Vikuu vya Elimu vitatu na Taasisi za Kibenki tatu.
Mheshimiwa Spika, aidha, katika Wiki hiyo, Vijana 300 kutoka makundi
mbalimbali ya Vijana walishiriki katika midahalo ambapo pia walipatiwa
mafunzo ya aina tofauti yenye lengo la kuwajengea uelewa wa masuala
mbalimbali ya maendeleo ya vijana. Kwa mfano, umuhimu wa kuwa na Wiki ya
Vijana kila mwaka, ujasiriamali, dhana ya uwajibikaji, umuhimu wa Mifuko ya
Hifadhi ya Jamii na Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana.
Mheshimiwa Spika, Sekta ya Maendeleo ya Utamaduni; katika mwaka wa
fedha wa 2013/2014, Wizara ilikabiliana na changamoto zilizotokana na athari
za utandawazi na maendeleo yenye kasi kubwa ya sayansi na teknolojia,
mmomonyoko wa maadili kwa watu wa rika mbalimbali, wizi wa kazi za wasanii
kutokana na upatikanaji kirahisi wa kurudufu kazi husika. Malalamiko makubwa
yamekuwa kwamba, hali hii imekuwa ikiwaneemesha mapromota na
wasambazaji wa bidhaa za filamu na muziki ambao sio wasanii.
Mheshimiwa Spika, pamoja na changamoto hizi, Wizara kupitia Sekta ya
Maendeleo ya Utamaduni:- imeimarisha ukusanyaji na uhifadhi wa takwimu za
tasnia ya utamaduni; imetoa mafunzo ya namna ya kuainisha namba za
misimbo (code numbers) za sekta ya utamaduni ambazo zitatumika Kitaifa na
Kimataifa; imefanya tafiti za maktabani za lugha za jamii 10 na utafiti wa
uwandani katika Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani ili kuhifadhi sarufi, misamiati
na istilahi za lugha ya Taifa – Kiswahili; imefanya utafiti wa kina kuhusu mila za
jando na unyago miongoni mwa jamii za Wamakonde, Wamakua na Wayao.
Mheshimiwa Spika, utafiti huo umewezesha kukamilisha maandalizi ya
pendekezo la elementi ya urithi usioshikika ambao hatimaye Serikali itaomba
urithi huo uingizwe kwenye orodha ya urithi wa utamaduni wa dunia
unaotambuliwa na UNESCO. Elementi hiyo ni ya ngoma ya “Nankachanga”
kutoka Kijiji cha Namahonga, Wilaya ya Tandahimba, Mkoa wa Mtwara.
Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana na Wizara ya Habari,
Utamaduni, Utalii na Michezo ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, iliratibu zoezi la
-
Nakala ya Mtandao (Online Document)
40
kuwapata Watanzania wenye sifa stahiki ili kunufaika na fursa zinazotokana na
Tanzania kuwa Makao Makuu ya Kamisheni ya Kiswahili ya Jumuiya ya Afrika
Mashariki. Fursa za ajira katika Kamisheni zitashindaniwa na nchi zote
wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, hivyo ni muhimu kwa Tanzania
kuwa na wagombea sadifu ili kuhimili vishindo vya kinyang‟anyiro hicho. Wizara
hizi mbili zitaendelea kusimamia zoezi hili kuhakikisha fursa ziliz