Mwongozo wa Utekelezaji - ra-training … Implementation... · Umeandaliwa kwa kushirikiana na...
-
Upload
phungkhanh -
Category
Documents
-
view
341 -
download
3
Transcript of Mwongozo wa Utekelezaji - ra-training … Implementation... · Umeandaliwa kwa kushirikiana na...
Mwongozo wa Utekelezaji wa wakulima wadogo wa Chai Africa
Umezingatia Mwongozo wa mtandao wa Kilimo Endelevu -Sustainable Agriculture Network (SAN)
Shukrani
© 2011 Rainforest Alliance Haki zote zimehifadhiwa
Mwandishi:Reiko Enomoto, Technical Capacity Manager, Sustainable Agriculture Division, Rainforest Alliance
Mtaalamu MwandamiziWinnie Mwaniki, Regional Projects Manager, Rainforest Alliance
Kuchapa na michango ya kiutaalamu:Marc Monsarrat, Manager (East Africa & South Asia), Rainforest AllianceKathrin Resak, Technical Coordinator (Africa & Asia), Rainforest Alliance Sylvia Rutatina, Rainforest Alliance Tanzania Coordinator Washington Ndwiga, Rainforest Alliance Trainer, Partner AfricaMark Omondi, Rainforest Alliance Trainer, Partner Africa Jane Nyambura, Regional Manager, Partner AfricaPeter Mbadi, Project Manager, KTDAAlfrick Sang, Sustainable Agriculture Coordinator, KTDADr. F. N. Wachira, Director, Tea Research Foundation of Kenya Gabriel Tuei, Unilever KenyaZakaria Mitei, Unilever Kenya Livingstone Sambai, Unilever KenyaJagjeet Kandal, Unilever Mark Birch, UnileverRia Kearney, Tata Global BeveragesSebastian Michaelis, Tata Global BeveragesSarah Roberts, Ethical Tea PartnershipJoseph Wagurah, Ethical Tea Partnership
Upigaji Picha: Reiko Enomoto, Rainforest Alliance Kathrin Resak, Rainforest AllianceWinnie Mwaniki, Rainforest AllianceWashington Ndwiga, Partner AfricaTea Research Foundation of Kenya
:
Huu mwongozo wa utekelezaji umeandaliwa, umechapishwa na kusambazwa kutokana na msaada wa Dutch Sustainable Trade Initiative (IDH), Flemish Authorities (FICA), Tata Global Beverages na Unilever Plc.
Umeandaliwa kwa kushirikiana na Africa Now, Kenya Tea Development Agency (KTDA) na Ethical Tea Partnership
Mwongozo wa Utekelezajiwa Wakulima wadogo wa Chai Africa
Utangulizi
Sura ya 1:Mbinu Shirikishi za Uthibitiwa wadudu na magonjwa
Sura ya 2:Taratibu Salama za kushughulika na madawa
Sura ya 3: Uthibiti wa takataka
Sura ya 4:Hifadhi ya mifumoya ekolojia
Sura ya 5:Hifadhi ya maji
Sura ya 6:Hifadhi ya udongo
Sura ya 7:Maisha bora na mazingira mazuri ya kazi
Sura ya 8:Usimamizi wa shamba
1
Uta
ngulizi Utangulizi
kuhusu kilimo endelevu
Chai ni mojawapo ya mazao muhimu katika Mashariki na Kusini mwa Afrika, na pia ni
chanzo cha kipato kwa wakulima wengi wadogo. Pamoja na hayo, iwapo shughuli zisizo
endelevu zikiachwa ziendelee, zitachafua mazingira, zitachakaza maji au udongo na
kunyonya wafanyakazi. Kwa njia hii, uzalishaji wa chai hauwezi kudumu kwa muda mrefu.
.
Ili kuhakikisha kuwa uzalishaji wa chai unaendelea hadi siku zijazo, inabidi kushirikiana
katika kuhamasisha shughuli endelevu katika ngazi ya mkulima mdogo. Ni muhimu
kuhakikisha kuwa kila mzalishaji anachukua jukumu la kuzalisha chai kwa njia endelevu.
Jinsi gani wakulima wanaweza kuzalisha chai kwa
njia endelevu? Huu “Mwongozo wa Utekelezaji”
unaonyesha njia rahisi na zinazotekelezeka za
kilimo endelevu katika mashamba ya wakulima
wadogo wa chai katika nchi za Afrika.
Yaliyomo katika mwongozo huu yamezingatia
“Mwongozo wa Kilimo Endelevu” uliochapichwa
July 2010 na Mtandao wa Kilimo endelevu.
Mwongozo huu umejumuisha maeneo yote muhimu
endelevu. Hii ni nakala muhimu pale mzalishaji
anapoamua kuwa na ithibati (cheti) ya Rainforest
Alliance.
2
Uta
nguliziMasharti ya kupata ithibati (cheti)
Kupata wastani wa asilimia themanini ( 80%) kwa kanuni zote
(Jumla ya vigezo ni 99)
Kupata asilimia hamsini (50%) kwa kila kanuni (Kuna kanuni 10)
Kufaulu vigezo vyote vya lazima (Kuna vigezo 15 vya lazima)
1.
2.
3.
Kiwango cha chini cha kufaulu ili kupata ithibati ya Rainforest Alliance ni
kama ifuatavyo.
kwa upande wa wakulima wadogo, vigezo vingi haviwahusu. Katika
mwongozo huu, tumelenga vigezo ambavyo vinawahusu na ni
muhimu kwa wakulima wadogo. Tafadhali tia maanani kuwa
mwongozo huu haujahusisha vigezo vyote vya kanuni na pia
hauhusishi mashamba makubwa.
Yaliyomo katika mwongozo
Sura ya 1:Mbinu Shirikishi za Uthibiti wa wadudu na magonjwa
Sura ya 2: Taratibu Salama za kushughulika na madawa
Sura ya 3: Uthibiti wa takataka
Sura ya 4: Hifadhi ya mifumo ya ekolojia
Sura ya 5: Hifadhi ya maji
Sura ya 6: Hifadhi ya udongo
Sura ya 7: Maisha bora na mazingira mazuri ya kazi
Sura ya 8: Usimamizi wa shamba
Mwongozo huu una sura 8, kila mojawapo inaendana na kanuni za mwongozo
Inaendana na: Kanuni ya 8
Inaendana na: Kanuni ya 6
Inaendana na:Kanuni ya 10
Inaendana na:Kanuni ya 2
Inaendana na:Kanuni ya 4
Inaendana na:Kanuni ya 9
Inaendana na:Kanuni ya 5
Inaendana na:Kanuni ya 1
3
Ukurasa wa 4
Ukurasa 10
Ukurasa 14
Ukurasa 15 Ukurasa 25
Ukurasa 23
Ukurasa 22
Ukurasa 18
Mbin
u shir
ikishi
za ut
hibiti
wa
wadu
du na
mag
onjw
aSura ya 1
4
Upandaji Unapopanda mche wa chai, chagua aina inayostahimili
wadudu na magonjwa kama vile utitiri na Mbu wa chai. Ni
vizuri kupanda aina tofauti za chai, badala ya aina moja.
Unapopanda aina tofauti, kila moja ipandwe kwenye boma
tofauti kurahisisha usimamizi.
Kupanda aina zilizochaguliwa kwa umakini
Kama shamba lilikuwa
limeathirika na ugonjwa wa
mizizi, kama vile Amilaria,
ugojwa huo unaweza bado
kushikiliwa na mizizi ya mashina
yaliyobaki. Kwa hiyo, inatakiwa
kuondoa gamba kuzunguka mti
ili kuzuia chakula kutoka kwenye
majani kwenda kwenye mizizi
kupitia magamba ya mti. Njia hii
itasababisha kuua wadudu
kwenye mizizi. PaliziMagugu yanatakiwa yathibitiwe kwa njia zifuatazo, bila
kunyunyiza madawa.
Kutumia matandazo kwenye chai changa au mashina
yaliyokatwa
Kutumia matandazo kwenye chai changa au mashina
yaliyokatwa
Kung'oa magugu kwa mkono
Mbinu shirikishi za uthibiti wa wadudu na magonjwa
Matumizi ya madawa sio njia pekee ya kuthibiti wadudu na magonjwa. Mashina
ya chai yakitunzwa vizuri yakawa na afya nzuri hasa nchi za Africa, yatastahimili
mashambulizi ya wadudu wa muda mfupi, bila kutumia madawa. Unyunyiziaji wa
madawa unaua wadudu rafiki asilia na kunaweza kusababisha kutokea kwa
mlipuko wa magonjwa yasiyoweza kuthibitiwa. Katika kipengele hiki, tunajifunza
jinsi ya kuthibiti wadudu na magonjwa kwa njia endelevu
Matandazo na chai iliyofunga vizuri
inazuia mwanga kupenya hadi ardhini,
hivyo uthibiti wa magugu yasiote. Palizi
ya jembe inaweza kuharibu mizizi ya
mashina ya chai. Ni vyema kung'oa
magugu kwa mkono.
Matandazo kwenye chai changa
Palizi ya mkono
Kuondoa gamba kuzunguka mti
5
Kukata chaiKukata chai ni muhimu kwa kufanya mashina yawe na afya na yenye kuzalisha. Ina faida
zifuatazo.
Matawi yaliyokatwa yanatoa virutubisho kwenye udongo yanapooza,
yanazuia magugu yasiote,huhifadhi unyevu wa udongo na kuzuia
mmomonyoko.
4.
Unapokata mashina ya chai ya umri mkubwa, zingatia kimo cha sentimita 60. Kama ukikatia chini sana, maji ya mvua yanayoruka kutoka ardhini yanaweza kuwa na vimelea vya magonjwa na kuingia kwenye kidonda
Baada ya kukata, tumia matawi hayo kufunika chai iliyokatwa ili kuzuia chai isiunguzwe na jua au barafu. Baada ya hapo, unaweza kutandaza juu ya udongo kama matandazo. Usiondoe matawi yaliyokatwa kwa ajili ya kuni.
Kuthibiti panyaFuko na panya waharibuo mizizi ya chai wanaweza kuthibitiwa
kwa kuchimba mifereji, na kwa kupanda mimea inayowafukuza
kama vile utupa (Tephrosia vogelli), bangi pori (Tagetes minuta),
vitunguu maji na vitunguu saumu. Epuka kuwaua.
Utupa uliopandwa kwenye shamba
Bangi pori
Wasiliana na wataalamu
wa kilimo kama unataka
kutumia majani ya utupa
kama dawa ya kuthibiti
wadudu.
2. Kukata chai kunahamasisha ukuaji wa matawi na majani mapya.
1. Kukata mashina na matawi yenye magonjwa kuzuia kusambaa
kwa magonjwa katika sehemu nyingine ya mmea
3. Kukata chai kunathibiti urefu wa meza hivyo kurahisisha uchumaji.
Mbin
u s
hir
ikis
hi za
uth
ibiti w
a w
adudu n
a m
ago
njw
a
6
Amilaria Shina lililokufa au lenye ufa wenye utando mweupe, ni dalili ya kushambuliwa na Amilaria.
Amilaria ni ugonjwa wa fangasi inayoenezwa kupitia mfumo wa mizizi. Tahadhari
isipochukuliwa ugonjwa utasambaa na kushambulia shamba lote.
Shina lenye ufa karibu na ardhiShina lililokufa
Shina lililokauka au lenye majani ya njano
Shina lenye ufa juu kidogo ya ardhi lenye utando mweupe kama nyuzinyuzi
Kama kuna shina
lililoshambuliwa na Amilaria,
unatakiwa kung'oa shina lote
ikiwemo mizizi na kuacha
wazi juu ya ardhi
Baada ya kung'oa shina lililoadhirika, unaweza kupanda chai
kwa msimu unaofuata. Kama ni sehemu kubwa iliyong'olewa,
eneo linaweza kupandwa kwa mimea inayorutubisha udongo
kama vile nyasi aina ya Guatamala.
Nyasi aina ya Guatamala
Ung'oaji wa shina lote ikiwemo mizizi
Mbin
u s
hir
ikis
hi za
uth
ibiti w
a w
adudu n
a m
ago
njw
a
7
Uthibiti wa mpasuko wa gamba kwenye shina au matawi (phomopsis – stem canker) Kama ukiona mpasuko wa gamba kwenye shina au
matawi, hiyo ni dalili ya shambulio la Phomopsis.
Phomopsis ni ugonjwa wa fangasi unaopenya kupitia
vidonda vilivyo wazi kwenye shina au matawi. Vidonda
hivyo vinaweza kusababishwa na palizi ya jembe au
shambulio la panya.
Tawi lenye vidonda vilivyodidimia
Majani yaliyogeuka kuwa njano
Ili kuthibiti mpasuko wa gamba kwenye shina au matawi, ondoa
matawi yaliyoadhirika na kuyachoma. Uchomaji unaruhusiwa
kwa ugonjwa huu tu kwani ndiyo njia pekee ya kuudhibiti.
Unapochoma, hakikisha unakuwepo ili kuthibiti moto
usisambae.
Kuzuia mpasuko wa gamba kwenye shina au matawi,
unatakiwa kuchagua aina za chai zenye kustahimili phomopsis
wakati unapopanda eneo jipya. Epuka kutumia palizi ya jembe,
kwani jembe linaweza kuumiza mashina bila kutarajia.
Kuchoma matawi yaliyoshambuliwa na Phomopsis
Uthibiti wa kuoza kwa shina (Hypoxylon wood rot). Kuoza kwa shina ni ugonjwa wa fangasi unaoshambulia matawi mama. Matawi
yaliyoadhiriwa huanza kuoza na kuwa na mabaka meusi kwa nje. Kuthibiti kuoza kwa
matawi, ondoa matawi yaliyoshambuliwa na nyunyiza dawa ya ukungu ya kopa kwa ajili ya
fangasi kwenye vidonda. Wakati wa kukata chai yenye umri mkubwa, hakikisha kuwa
unakata kwenye urefu unaotakiwa (sentimita 60) ili kuzuia mdudu kufikia vidonda.
Shina zima lililoadhirika na Hypoxylon
Mabaka meusi kwenye shina
Mbin
u s
hir
ikis
hi za
uth
ibiti w
a w
adudu n
a m
ago
njw
a
8
Mbu wa chai (Helopeltis -Tea mosquito bug)Mbu wa chai wanavyonza majani machanga na kuacha mabaka meusi kutokana na mate
yake. Majani yaliyoshambuliwa yanaadhiri ukuaji.
Majani yaliyoathirika kutokana na Mbu wa chai
Mbu wa chai
Majani yaliyofyonzwa na Mbu wa chai
Kuondoa majani yote machanga
Kuthibiti shabulio la Mbu wa chai, inashauriwa
kuchuma majani yote machanga na kuacha
majani yaliyokomaa shambani. Hii njia inaitwa
“uchumaji wa kugandamiza”. Kwa kuondoa
majani yote machanga ambayo yangeliwa na
Mbu wa chai, idadi yao inaweza kuthibitiwa. Ili
kuzuia kushambuliwa na Mbu wa chai, ni
muhimu kuchagua aina ya chai zinazostahimili
shambulio la Mbu wa chai unapopanda chai
changa.
Vidukari (Aphids)Vidukari ni wadudu wanaoshabulia majani machanga.
Uchumaji wa kugandamiza na kupunguza siku za
kuchuma ni njia madhubuti ya kudhibiti wingi wao.
Majani yaliyoshambuliwa na vidukari
Vikobe (Ladybirds) ni maadui
asilia wa vidukari. Vikobe
wanawala vidukari na kuthibiti
idadi yao. Kunyunyiza dawa
hakutauwa tu vidukari bali pia
vikobe. Kwa kutokunyunyiza
dawa, unalinda vikobe na
kudumisha njia asilia ya uthibiti
wa vidukariVikobe wanawala vidukari
Mbin
u s
hir
ikis
hi za
uth
ibiti w
a w
adudu n
a m
ago
njw
a
9
Utitiri (mites)
Kuna aina nyingi za utitiri kama vile utitiri wa
zambarau, utitiri wekundu n.k. Majani
yaliyoadhirika kwa utitiri yanabadilika rangi
na kuwa ya kahawia
Shamba lililoharibiwa na utitiri wekundu
Majani yaliyoadhirika na utitiri wekundu
Uwekaji wa mbolea ya kutosha
Mashina yenye afya yanaweza kustahimili adhari za utitiri.
Uwekaji wa mbolea ya kutosha unaimarisha mashina ya
chai. Upandaji wa aina za chai zenye kustahimili ni njia ya
kuzuia shambulizi la utitiri
Tuthibiti wadudu na magonjwa kwa njia
endelevu katika mashamba yetu na kudumisha
mashina yenye afya na yanayotoa mazao
mengi
Mbin
u s
hir
ikis
hi za
uth
ibiti w
a w
adudu n
a m
ago
njw
a
Tara
tibu s
alam
a za
ku
shughulika
na
mad
awa
Taratibu salama za kushughulika na madawa
Sura ya 2
Wakulima wenye ithibati (cheti) wasifanye shughuli zenye kuathiri afya zao au afya za watu
wengine. Kama unatumia madawa kwenye mboga au wanyama, yanatakiwa yawekwe na
yashikwe kwa usalama na pia yatumike katika njia salama, kwa ajili ya usalama wako, wa
familia yako na majirani.
Hairuhusiwi kunyunyiza madawa bila kutumia vifaa vya kujikinga.
Hiki ni kigezo cha lazima.Usipokidhi kigezo hiki utaadhiri vikubwa upatikanaji wa ithibati wa kikundi husika
Kumbuka:
Kichuja sumu (Sio kizuia vumbi. Kizuia vumbi hakina chujio la sumu)
Koti la mvua au kizibau cha kukinga mgongo
Glovu za plastikimgongo
Aproni iliyotengenezwa kwa mfuko wa plastiki (inashauriwa kama kizuia dawa cha ziada kama koti halifuniki miguu vizuri)
Kumbuka: Tumia mfuko wa plastiki ambao haukutumika kwa bidhaa za madawa (nafaka n.k.) Usitumie mfuko wa mbolea
Buti za plastiki
Kizuia vumbi
Miwani kwa ajili ya kukinga macho
Kumbuka kwamba sehemu zote za mwili zinatakiwa kufunikwa
Vifaa vya Kujikinga (PPE)
10
Unaweza kuvuta madawa kupitia mdomo au pua.
Mchanganyiko wa dawa unapovuja, utalowanisha nguo zako na hivyo kuguza ngozi yako
Mchanganyiko utalowanisha mikono yako na kuingia mwilini kupitia ngozi
Kama hutavaa buti, dawa pia itaguza ngozi yako
Koti lisilopitisha maji
Tara
tibu s
alam
a za
ku
shughulika
na
mad
awa
Kuvaaa vifaa vya kinga ni muhimu sio tu wakati wa kunyunyizia mboga, bali pia wakati wa kunyunyiza dawa kwa ng'ombe na uwekaji wa mbolea.
Utunzaji salama wa madawa
Madawa
Madawa
Inakuwaje kama ukihifadhi madawa ndani ya vyumba mnamoishi? Hewa ya sumu inayotoka kwenye madawa yaliyohifadhiwa inaweza kuathiri afya ya familia yako
Kama ukitunza madawa jikoni mwako, mwanafamilia anaweza kuchukua na kuweka kwenye chakula bila kufahamu kama ilikuwa ni dawa
Kama ukitunza madawa chumba cha kulala, watoto wanaweza kuziona na kuzinywa kwa kufikiri ni kinywaji.
Madawa
Kama ukiweka madawa sehemu iliyo wazi bila kofuli, watoto wanaweza kuyafikia na kuyachukua wakati wanacheza, au yanaweza kuibiwa.
Madhara ya kutotunza madawa kwa uangalifu yanaweza kusababisha kifo kwa mwanafamilia
Madawa
11
Kwa uwekaji wa mbolea, unatakiwa kuvaa angalao glovu, buti na aproni
Tara
tibu s
alam
a za
ku
shughulika
na
mad
awa
Ni vyema kununua kiwango kile cha madawa kinachohitajika kutumiwa wakati huo, ili isikulazimu kutunza madawa nyumbani. Pale unapotakiwa kutunza madawa yaliyobaki, zingatia yafuatayo hapa chini jinsi ya kuhifadhi madawa kiusalama kwa ngazi ya shamba la mkulima mdogo
Sehemu ya hifadhi iliyotengenezwa kwa pipa la chuma
Stoo iliyotengenezwa kwa kibanda cha zamani cha kuku
1. Kama unahitaji kutunza chupa za madawa, sio lazima kujenga ghala la kuhifadhia au jengo. Kibanda kidogo kinaweza kutosha kwa mkulima mdogo. Kwa mfano, unaweza kulitengeneza pipa la chuma, sanduku la chuma, mbao au kibanda cha kuku kisichotumika kwa kuyatunzia. Ni muhimu kuwa kifaa hicho hakiwekwi ndani ya nyumba.
Ukubwa na muundo
2. Vifaa visivyopitisha majiUnaweza kutengeneza stoo kwa kutumia vifaa vinavyopatikana katika sehemu husika ambavyo havipitishi maji. Paa lake lisiwe linapitisha maji. Kama unatumia mbao, unatakiwa kutandaza karatasi ya plastiki ili kama dawa ikimwagika bahati mbaya isivyonzwe na mbao hizo.
Ndani ya kibanda cha mbao kumetandazwa karatasi ya plastiki.
3. KufungiaStoo inatakiwa kufungwa, na ufunguo unatakiwa kutunzwa kwa umakini. Ni muhimu kuifunga ili watoto au watu wengine wasifungue na kuyachukua madawa yaliyo ndani.
4. Alama ya tahadhariWeka alama ya tahadhari kwenye stoo ili ijulikane wazi kwa yeyote kuwa kuna vitu vya hatari ndani.
Shelfu ya mbao iliyotandazwa karatasi ya plastiki
12
Tara
tibu s
alam
a za
ku
shughulika
na
mad
awa
Kupanda wigo hai
Unaponyunyiza madawa, unatakiwa kuhakikisha kuwa watu wapitao jirani na shamba lako
hawaadhiriwi na dawa zisambaazo kutoka shambani. Kuzuia kuzambaa kwa madawa,
inashauriwa kupanda wigo hai kuzunguka shamba lako. Wigo hai pia unahifadhi viumbe hai
na kuunganisha mifumo ya ikolojia shambani.
Wigo hai
Shamba la chai
Shamba la chai
Shamba la
Wigo hai
Wigo hai
Umbali kati ya nyumba na maeneo ya uzalishajiKama familia yako au wafanyakazi wanaishi shambani, ni muhimu kuacha umbali kidogo
kutoka kwenye nyumba na shamba. Kama mashamba ya chai au bustani ya mboga iko
jirani na nyumba, watu waishio ndani ya nyumba au watoto wanapocheza hapo nyumbani
wataadhiriwa na madawa yatakayokuwa yanasambaa wakati wa kunyunyiza. Unaweza
kuzuia kusambaa huko kwa kuacha umbali kidogo na kupanda wigo hai.
Umbali kutoka shambani na nyumba
Shamba lililo karibu kabisa na nyumba
13
Uthibiti wa takatakaSura ya 3
Uth
ibiti w
a ta
kata
ka
Takataka zinaweza kuwa na manufaa tena, kama
zitatumika kwa shughuli nyingine au kutengeneza
kitu kingine.Kutokuthibiti taka kunachafua hewa,
maji na udongo shambani mwako. Kama ukichoma
taka za plastiki au makasha matupu ya dawa, hewa
ya sumu hutoka na kuathiri afya ya familia yako.
Tuthibiti takataka inavyotakiwa ili kuwa na mazingira
safi shambani mwako.
Kuchoma takataka hairuhusiwi
Uthibiti wa taka hai (taka zinazooza)
Taka za jikoni na samadi za mifugo zinaweza
kuozeshwa kutengeneza mboji. Unapoziozesha,
hakikisha unazigeuza kila wiki 2-3 ili kupitisha
hewa na kuhifadhi joto la kutosha ili kuziozesha
Uthibiti wa takataka za plastiki na makasha ya madawaTaka za plastiki na makasha ya madawa zikusanywe tofauti. Safisha makopo ya
madawa mara tatu na yatoboe kabla ya kuyahifadhi. Baada ya kuzitenga, kampuni au
uongozi wa mradi (Group Administrator) izichukue na kuziteketeza kwa njia ambayo
haitachafua mazingira.
Zisiachwe shambani.
Mfuko kwa ajili ya makasha ya madawa
Mfuko kwa ajili ya taka za plastiki
Chombo cha kukusanyia taka za plastiki
14
Hifad
hi ya
mfu
mo
wa
iko
lojia
Kama una maeneo yafuatayo shambani mwako, ni ekolojia muhimu ya kuhifadhiwa
Eneo lenye miti ya asili
Eneo lenye wanyama adimu au mimea
Kijito au mto
Chanzo cha maji
Eneo chepechepe au oevu
Mbuga za hifadhi au maeneo
yaliyotengwa na serikali
Maeneo haya yanatakiwa kuhifadhiwa kwa
sababu yanatunza aina ya viumbe mbalimbali
ambavyo ni muhimu, na kuyapoteza maeneo
haya kutaharibu vibaya mazingira kama vile
upotevu wa viumbe adimu, mmomonyoko wa
udongo na uchafuzi wa maji.
Kwa hiyo, yasibadilishwe kuwa shamba la
chai.
Usikate miti, usiwinde, usilimeIli kuyalinda maeneo hayo, inatakiwa kutokukata miti kwa ajili ya kuni kutoka katika maeneo
hayo, kuwinda wanyama, kulima mazao au kunyunyiza madawa. Hii inahitaji mawasiliano
ya kiufasaha kwa wafanyakazi wote na wanafamilia
Hifadhi ya mfumo wa ikolojiaSura ya 4
Kutokuharibu maeneo hayo ya asili ni kigezo cha lazima..
NB:
15
Hifad
hi ya
mfu
mo
wa
iko
lojia
Upandaji wa miti ya asiliIli kuhifadhi bionuwai ya eneo, unaweza kupanda miti ya asili mpakani mwa shamba, kando
ya vyanzo vya maji na maeneo ya mitelemko mikali. Ni muhimu kupanda miti ya asili, na
siyo miti ya kigeni kwa sababu miti ya asili inaboresha hali ya hewa ya eneo husika na hali
ya udongo, na inaweza kutunza bionuwai maalum.
Mtelemko mkali uliopandwa miti ya asili
Upandaji wa miti ya asili
Mfano wa miti ya asili katika Africa Mashariki
Kuacha ukanda wa bafa Inashauriwa kuacha ukanda wa bafa au uoto wa asili kati ya shamba na maeneo
yaliyohifadhiwa ili kuhakikisha kwamba dawa hazitapenya na pia shughuli za kilimo
hazitayaharibu maeneo hayo
Msitu
Ukanda wa bafa
Shamba
Eneo chepechepe au oevu
Ukanda wa bafa
Shamba
16
Kifabakazi MpodoMueri, MkomahoyaMruka MfurufuruMianziMwangati Mvengi au Mzambarau mwitu Mfuu
Unaweza kuwa na bustani ya miti ya asili ili kuzalisha miche mwenyewe
Hifad
hi ya
mfu
mo
wa
iko
lojia
Kuunganisha mifumo ya ikolojia
Ili wanyama na ndege waweze kutoka sehemu moja hadi nyingine, wanahitaji misitu
iliyounganika. Kama msitu ukitenganishwa kwa mashamba, wanyama hawawezi kupita kwa
uhuru. Kama vyanzo vya maji havijaunganishwa na msitu, wanyama hawawezi kuyafikia
hayo maji.
Misitu iliyounganishwa ambayo wanyama na ndege wanaweza kupita
Viraka vya misitu vilivyounganika
Kuunganisha mifumo ya ikolojia unaweza
kupanda miti pembeni mwa shamba ili
kuunganisha viraka vya msitu, au kuhifadhi
maeneo ya ushoroba (corridor) ya misitu
17
Uhuru wa ndege na wanyama kupita
Kuzuia mwingiliano
Misitu iliyoharibiwa na kutenganishwa kwa mashamba ambapo wanyama na ndege hawawezi kupita
Kuzuia mwingiliano
Hifadhi ya majiSura ya 5
Hifad
hi ya
maj
i
Kuosha vifaa
Maji ni raslimali muhimu kwa maisha yetu na kwa kilimo. Katika sura hii, tutajifunza jinsi ya kuyafanya yawe safi na jinsi ya kulinda vyanzo vya maji
Baada ya kunyunyiza dawa, unatakiwa kuosha bomba lililotumika na vifaaa vyako vya kujikinga. Maji yaliyotumika kuoshea vifaa hivyo yana sumu, kwa hiyo usipoyathibiti vizuri, yanaweza kuchafua mazingira.
Vifaa visisafishwe kwenye mito, mferej au bwawa.
Unaponyunyizia bustani za mboga,
safisha vifaa na mwaga maji hayo
shambani.
Unaponyunyizia au kuosha mifugo, safisha vifaa na mwaga maji hayo kwenye shimo. Shimo hilo liwe limejazwa mkaa, ambao husaidia kuchuja hayo maji. Usikate miti ya asili kutengeneza mkaa.
Shimo lililojazwa mkaa
Kumbuka pia kuosha vifaa vya kinga. Yathibiti maji yaliyooshea kama ilivyoelezwa hapo juu.
18
Ndoo itumikayo tu kwa kuoshea vifaa
Uthibiti wa maji taka nyumbani
Kuoshea nguo kwenye mito kunayachafua maji. Kumwaga maji taka ya jikoni nje ya nyumba kunachafua mazingira na kusababisha mazalia ya mbu. Maji taka ya nyumbani yanatakiwa kuthibitiwa vizuri.
Maji machafu ya majumbani yanapokuwa machache, yanaweza kuthibitiwa kwa kuyamwaga kwenye mtaro uliochimbwa kwenye bustani. Mtaro unatakiwa upandwe migomba au magimbi, vyote viwili vinavyonza maji vizuri.
Bomba(kama mita 1)
Kumwaga maji machafu kwenye mtaro uliochimbwa kwenye eneo la bustani
Mtaro Migomba Magimbi
Maji Machafu
Kama ukiona maji yametuwama kwenye bustani, kiwango cha maji machafu ni kingi ukilinganisha na uwezo wa udongo kuyafyonza, au aina ya udongo hauna uwezo mkubwa wa kufyonza maji. Kwa hali hii, unaweza kuchimbia bomba ili maji yapenye ndani ya ardhi badala ya kuelea juu ya udongo bustanini.
19
Hifadhi ya m
aji
Ung’oaji wa mikaratusi (eucalyptus) jirani na chanzo cha majiMiti ya mikaratusi ni chanzo cha kuni, lakini
ikipandwa jirani na ardhi chepechepe (oevu), mto,
kijito au kisima, inafyonza maji mengi kiwango cha
kukausha chanzo cha maji. Kama kijito au kisima
kikikauka, kitaadhiri maisha ya familia yako na
wanajamii wengine. Tunatakiwa kulinda vyanzo vya
maji.
Kukata miti ya mikaratusi iliyopandwa jirani na mto
Baada ya kuondoa miti ya mikaratusi kijito hiki kilianza kurudi katika hali yake
Kijito kinakauka kwa sababu ya mikaratusi
Miti ya mikaratusi
Hakuna kulima jirani na vyanzo vya majiInashauriwa kutokulima jirani na vyanzo vya maji. Unaponyunyiza madawa, yanapenya
hadi kwenye maji na kuyachafua. Kulima jirani na vyanzo vya maji kunasababisha udongo
kumomonyoka kwenda kwenye maji.Tuhifadhi maeneo kandokando ya vyanzo vya maji
kwa kuacha uoto wa asili au kupanda tu mazao ambayo hayahitaji kutifuatifua udongo na
yasiyonyunyiziwa madawa.
Udongo uliomomonyoka
Upenyaji wa madawa
20
Hifadhi ya m
aji
Uvunaji wa maji
Maji ni muhimu kwa maisha, na tunahitaji kuwa na maji ya kutosha kwa maisha yetu. Uvunaji wa maji ya mvua ni njia ya unafuu na madhubuti ya kupata maji. Unaweza kukinga maji yanayodondoka kwenye paa la nyumba na kuyahifadhi kwenye pipa. Yanaweza kutumika kwa matumizi mbalimbali ya nyumbani ikiwemo kunywa baada ya kuyatibu au kuyachemsha. Mvua ni chanzo muhimu cha maji hivyo inabidi tujue jinsi ya kukitumia vyema.
Hakuna kutupa taka kwenye vyanzo vya maji
Kutupa taka kwenye vyanzo vya maji hairuhusiwi. Tunatakiwa kutunza vyanzo vya maji ili kuyafanya masafi kwa maisha ya wanyama na jamii
Kutokutupa taka kwenye vyanzo vya maji ni kigezo cha lazima
NB:
21
Hifad
hi ya
maj
i
Hifadhi ya udongo
Sura ya 6
Uthibiti wa mmomonyoko wa udongo
Hifad
hi ya
udo
ngo
Pale penye mtelemko mkali, udongo huwa na tabia ya kumomonyoka siku hadi siku. Kama hutathibiti mmomonyoko huo, utazidi kuwa mbaya zaidi.
Ili kuthibiti mmomonyoko, unaweza kupanda mawewe (Napier grass) na miti ya asili kwenye maeneo yaliyo katika adhari ya mmomonyoko. Mawewe yanashikilia udongo vizuri na yanasaidia kama malisho ya mifugo.
Mawewe
Kutokuchoma motoUchomaji moto unaribu mboji na viumbe hai
kwenye udongo, na kufanya udongo wako
kupoteza rutuba. Kuandaa mashamba kwa
kutumia moto hairuhusiwi.
Kutokuchoma moto ili kuandaa mashamba ni kigezo cha lazima
NB:
22
Mgema uliofunikwa kwa mimea
Udongo ni kiini cha kilimo. Tunatakiwa tuhakikishe kwamba udongo shambani haupotei kwa
njia ya mmomonyoko.
Maisha bora na mazingira mazuri ya kazi
Sura ya 7
Nyumba za wafanyakazi
Kama unaajiri wafanyakazi shambani mwako, wawe wanatendewa haki. Wafanyakazi wako
wanahitaji mazingira safi na salama
Mai
sha
bora
na
maz
ingi
ra
maz
uri y
a ka
zi
Kama una wafanyakazi wapatiwao nyumba, tuhakikishe kwamba zina usalama na ni bora.
1. Vyumba
Vyumba ambavyo wafanyakazi na familia zao wanamoishi au kulala visihifadhi madawa,
mbolea au makasha yake au mifuko. Kusiwe na maji yanayovuja kutoka darini au ukutani
Dari iliyoharibika inayovuja majiMadawa na mbolea chumbani Mifuko ya mbolea kwenye ukuta
2. Jiko
Jiko linapokuwa halina
sehemu ya kupitisha moshi,
moshi unaosambaa kwenye
chumba husababisha madhara
kiafya, kuharibu mapafu na
macho ya wafanyakazi na
familia zao. Jiko lenye bomba
la kutolea moshi linalinda afya
zao na kuboresha maisha yao.
Wafanyakazi wanaumizwa na moshi uliojaa chumbani
Boresha jiko ili moshi utoke kupitia kwenye bomba. Jiko hili lililoboreshwa pia linatumia kuni chache
Moshi
3. Choo
Nyumba za wafanyakazi ziwe na vyoo visafi
23
4. Sehemu ya kufulia
Nyumba za wafanyakazi ziwe
na sehemu ya kuoshea nguo.
Hawatakiwi kwenda mtoni
kufua nguo zao
Karo la kufulia Kufulia nguo mtoni
Huduma ya maji salama Wafanyakazi waishio au wafanyao kazi
shambani wanatakiwa kupata maji safi
na salama ya kunywa. Mara zote
yawepo maji yaliyochemshwa au yaliyo
salama kwa ajili yao.
Watoto Shambani
Usiajiri watoto chini ya miaka 15 kama mfanyakazi shambani
Kusaidia kufanya kazi shambani tu masaa ya nje na muda wa masomo
Watoto chini ya miaka 15
wanaweza kusaidia kwenye
shamba la familia, ili mradi
wanahudhuria shule na
hawafanyi shughuli za hatari
Kutokuajiri watoto chini ya miaka 15 ni kigezo cha lazima
NB:
24
• Chini ya miaka 15
• Kuajiriwa kama mfanyakazi shambani
• Kutokuhudhuria shule kwa sababu ya kazi
Mai
sha
bo
ra n
a m
azin
gir
a m
azuri
ya
kazi
Usimamizi wa shambaSura ya 8
Usi
mam
izi w
a sh
amba
Utunzaji wa kumbukumbuInashauriwa kuweka kumbukumbu ya shughuli muhimu. Kwa kuweka kumbukumbu,
unaweza kurejea shughuli zilizopita, kuzichunguza na kupata njia ya kuziboresha. Kwa
kuangalia rekodi, wakaguzi wa ndani na wa nje wataona kuwa unasimamia shamba lako
vizuri.
Hizi ni kumbukumbu zinazotakiwa kuwekwa
katika ngazi ya shamba.
Madawa yaliyotumika
Mbolea zilizotumika
Vibarua/Wafanyakazi
Mafunzo kwa wafanyakazi
Upandaji wa miti
Tarehe za kuchuma na chai iliyochumwa.
•••
••
•
•
Shamba
Tarehe
Aina ya dawa au mbolea
Kiasi
Dozi
Jina la mhusika aliyefanya
kazi hiyo
Aina ya kifaa
kilichotumika
Kumbukumbu za kuweka za
matumizi ya madawa na mbolea
Tarehe
Mada
Mkufunzi
Majina ya waliohudhuria
Sahihi au dole gumba ya
waliohudhuria
Kumbukumbu gani
ziwekwe kwa mafunzo
ya wafanyakazi
••••••
Tarehe
Jina
Aina ya kazi
Masaa ya kazi
Mshahara
Kumbukumbu za
kutunza za wafanyakazi
walioajiriwa
••
••
•
UhakikiWakulima na vikudi daima wasichanganye chai isiyo na ithibati (cheti) na yenye ithibati
katika hatua yoyote. Chai yenye ithibati inatakiwa itengwe katika ahatua zote za uzalishaji:
kwenye banda, wakati wa kusafirisha, katika mapokezi kiwandani, wakati wote wa
uzalishaji kiwandani hadi usafirishaji wa chai iliyotengenezwa.
Usichanganye chai iliyo na ithibati na isiyo na ithibati ni kigezo cha lazima
NB:
Usafiri tofauti wa chai iliyotoka kwenye mashamba yenye ithibati Njia (line) tofauti ya
kutengeneza chai iliyo na ithibati
Chai zenye ithibati zilizofungwa na kutengwa ili kutambuliwa 25