MWONGOZO WA KUTUMIA - Point Comfort RMA User Guide... · 2020. 6. 18. · • Chumba na chakula cha...

12
Msaada wa Matibabu kwa Wakimbizi MWONGOZO WA KUTUMIA Inaanza kutumika tar. 1 Machi 2018 ® Kampuni ya Unified Administrators, LLC KANSAS

Transcript of MWONGOZO WA KUTUMIA - Point Comfort RMA User Guide... · 2020. 6. 18. · • Chumba na chakula cha...

Page 1: MWONGOZO WA KUTUMIA - Point Comfort RMA User Guide... · 2020. 6. 18. · • Chumba na chakula cha kila siku pamoja na huduma za uuguzi katika chumba binafsi kwa namna fulani au

Msaada wa Matibabu kwa Wakimbizi

MWONGOZO WA KUTUMIA Inaanza kutumika tar. 1 Machi 2018

®

Kampuni ya Unified Administrators, LLC

KANSAS

Page 2: MWONGOZO WA KUTUMIA - Point Comfort RMA User Guide... · 2020. 6. 18. · • Chumba na chakula cha kila siku pamoja na huduma za uuguzi katika chumba binafsi kwa namna fulani au

Utangulizi

Kwa zaidi ya miaka 100 Kamati ya Kuwashughulikia Wakimbizi na Wahamiaji

Marekani (USCRI) imetetea haki na maisha ya watu walio hamishwa makwao

kwa lazima au kwa hiari. USCRI inawapa wakimbizi na watu wengine fursa ya

kutimiza uwezo wao wote wakiwa Marekani. Ustawi wa kimwili na kiakili, na

vilevile upatikanaji wa huduma za matibabu, ni muhimu kwa mafanikio katika

maisha nchini Marekani. USCRI ina mpango wa Msaada wa Matibabu kwa

Wakimbizi (RMA) kwa wageni ambao kwa sababu ya hali yao ya uhamiaji

hawastahiki katika mipango mingine ya Medicaid. RMA inajumuisha manufaa

ya matibabu, tiba ya meno na dawa sawa na Medicaid. Mwongozi huu

unakupa maelezo ya jinsi ya kupata manufaa ya mpango wa RMA.

Manufaa ya RMA yanasimamiwa na Point Comfort Underwriters, Inc. (PCU)

Page 3: MWONGOZO WA KUTUMIA - Point Comfort RMA User Guide... · 2020. 6. 18. · • Chumba na chakula cha kila siku pamoja na huduma za uuguzi katika chumba binafsi kwa namna fulani au

Msaada wa Matibabu kwa Wakimbizi

Je, ninastahiki kupata Msaada wa Matibabu kwa Wakimbizi (RMA)?

Ili ufahamu kama unastahiki kupata RMA, ni sharti ujaze

ombi la kujiunga na RMA. Msimamizi wa shauri katika

shirika linalowapa wakimbizi makazi mapya mahali ulipo

anaweza akakusaidia kutuma ombi. Kwa ujumla, ikiwa

umetimiza vigezo vifuatavyo, basi unastahiki:

1. Hali yako ya uhamiaji ni mkimbizi au hali nyingine

inayoruhusiwa.

2. Unatimiza masharti ya kupata utambulisho kwa

wahamiaji.

3. Unatimiza kima kilichowekwa cha mapato.

4. Huna hadhi ya kujiunga na mpango wa Medicaid,

Mpango wa Bima ya Watoto au bima nyingine yoyote

ya umma au ya binafsi.

Je, naweza kusimamiwa kwa muda

upi na RMA?

Manufaa yako ya RMA huisha moja kwa moja baada ya

miezi 8 tangu unapowasili Marekani, isipokuwa kama

wewe ni mkimbizi ambaye hajatimiza utu uzima na huna

watu wazima walio nawe (URM). Ikiwa wewe ni mkimbizi

ambaye hajatimiza utu uzima na huna watu wazima

(URM), unaweza kupata manufaa ya RMA mpaka

unapofika miaka 23. Zungumza na msimamizi wa shauri

lako katika shirika linalowapa wakimbizi makazi mapya

mahali ulipo ili akupe maelezo zaidi kuhusu hali yako.

Kumbuka kwamba ukihama jimbo la Kansas, manufaa

yako ya RMA huisha moja kwa moja. Utatakiwa kuomba

manufaa ya matibabu katika jimbo jipya unalohamia.

3

Page 4: MWONGOZO WA KUTUMIA - Point Comfort RMA User Guide... · 2020. 6. 18. · • Chumba na chakula cha kila siku pamoja na huduma za uuguzi katika chumba binafsi kwa namna fulani au

KADI YA KITAMBULISHO CHA RMA

Kadi ya Kitambulisho cha RMA ni nini?

Watu wote wanaosajiliwa kwenye mpango wa RMA hupokea

vitambulisho vyao binafsi vya RMA. Unaweza kupata

kitambulisho chako kutoka kwa wakala wa kuwapa wakimbizi

makazi mapya mahali ulipo. Pia unaweza kuomba kadi yako

ya kitambulisho cha RMA kutoka kwa PCU. Piga simu kwa PCU

au uwatumie barua pepe [email protected].

Kitambulisho chako cha RMA kina jina lako, namba yako ya

utambulisho na taarifa nyingine muhimu kuhusu manufaa ya

RMA. Ni muhimu kuwasilisha Kitambulisho chako cha RMA kila

wakati unapotaka kupokea huduma. Ikiwa kuna zaidi ya mtu

mmoja katika familia yako amesajliwa kwenye RMA, basi kila

mmoja atapata kitambulisho chake tofauti. Mtu aliyeandikwa

kwenye Kadi ya kitambulisho pekee ndiye anayeweza kutumia

kadi. Usiazime wala kumpa mtu mwingine kitambulisho chako.

Je, ninafaa kutumiaje kitambulisho

changu cha RMA?

Unafaa kuwa na kitambulisho chako cha RMA kila wakati.

Wasilisha kadi yako kwa daktari wako, hospitali, daktari wa

meno au duka la dawa wakati unatafuta huduma.

Wanaokupa huduma watatumia kitambulisho chako

kuthibitisha ustahiki wako kupata manufaa ya RMA

na kupata taarifa muhimu kuhusu atakayetozwa kulipia huduma unazopokea. Kukosa kuwasilisha kitambulisho chako kunaweza kuchelewesha madai ya malipo na unaweza pia kukosa manufaa yako.

Itakuwaje nikipoteza kitambulisho

changu cha RMA?

Unaweza ukapata kitambulisho kingine kutoka kwa PCU

Wasiliana na PCU ukitumia anwani

[email protected]. Huenda ukaombwa kutoa

taarifa za binafsi ili PCU ithibitishe kwamba ni wewe kabla

kukupa kadi mpaya ya kitambulisho.

Ikiwa kuna mabadiliko katika taarifa zako za binafsi kama

vile anwani yako ya nyumbani, namba ya simu au anwani

ya barua pepe, hakikisha umeifahamisha PCU kupitia

[email protected]. Hakikisha kwamba PCU ina

anwani yako ya barua pepe unayotumia kila wakati.

4

Page 5: MWONGOZO WA KUTUMIA - Point Comfort RMA User Guide... · 2020. 6. 18. · • Chumba na chakula cha kila siku pamoja na huduma za uuguzi katika chumba binafsi kwa namna fulani au

5

HUDUMA ZA AFYA

Je, ni watoa huduma gani ninaweza

kuwatumia?

Unaweza kutumia mtoa huduma yeyote ambaye

anakubali malipo kulingana na viwango vya malipo

vilivyoidhinishwa kwa ajili ya mpango wa RMA. Unaweza

kupata orodha ya watoa huduma ambao wanakubali

viwango hivi hapa rma.pointcomfort.com, au upige simu

kwa PCU ili upate usaidizi. Ikiwa unataka kutumia mtoa

huduma ambaye hayupo kwenye orodha hii, fanya hivi:

1. Pata jina kamili, anwani na namba ya simu ya mtoa

huduma unayotaka kutumia.

2. Wasilisha taarifa hizo kwa PCU.

PCU itawasiliana na mtoa huduma na kujaribu kufikia

makubaliano ya kutoa huduma kwa viwango vya malipo

vilivyoidhinishwa. PCU itakufahamisha kuhusu matokeo ya

mazungumzo hayo.

Kumbuka, unafaa kwenda katika Kituo cha Dharura kilicho

karibu kabisa na wewe wakati wa dharura.

Je, ni huduma zipi za matibabu

zinagharimiwa?

RMA hugharimia huduma nyingi za matibabu ikiwa

huduma hizo ni muhimu kwa afya na hazipiti vigezo fulani.

Baadhi ya huduma zinazolipiwa ni pamoja na:

HUDUMA ZA HOSPITALI

• Chumba na chakula cha kila siku pamoja na

huduma za uuguzi katika chumba binafsi kwa

namna fulani au wadi

• Chumba na chakula cha kila siku pamoja na

huduma za uuguzi katika Chumba cha Wagonjwa

Wanaohitaji Uangalizi Maalumu

• Utumiaji wa vyumba vya upasuaji, matibabu na kupata

nafuu

• Vifaa vya kufunga au kudhibiti majeraha, pamoja

na vitu vingine ambavyo hupewa wagonjwa

ambao wamelazwa

• Matibabu ya Dharura (lazima iwe dharura)

• Dawa unazoandikiwa ukiwa umelazwa

• Huduma za rediolojia, maabara na tiba kwa kutegemea

mawimbi ya sauti

• Matibabu ya Viungo, Tiba kwa Vitendo na

matibabu ya Kunena wakati wa kulazwa

• Huduma za kitaalamu zikiwemo za madaktari

HUDUMA ZA KUTIBIWA NA KUONDOKA

HOSPITALINI/UPASUAJI NA KUONDOKA

• Huduma za kitaalamu zikiwemo za madaktari

• Vifaa vya kufunga au kudhibiti majeraha, pamoja na

vitu vingine ambavyo hupewa wagonjwa ambao

hawajalazwa

KUWAONA MADAKTARI NA KWENDA KLINIKI

• Madaktari na wataalamu

• Matibabu ya viungo, Tiba kwa Vitendo na

matibabu ya Kunena

• Wataalamu wa Tabia/Afya ya Akili walio na kibali

• Huduma za rediolojia, maabara na tiba kwa kutegemea

mawimbi ya sauti

• Huduma za urekebishaji wa maungo

HUDUMA NYINGINE ZINAZOGHARIMIWA

• Usafirishaji wa dharura kwa ambulensi mahali ulipo

• Vifaa vya kudumu vya kimatibabu

• Huduma za matibabu nyumbani

• Huduma za faraja

• Matibabu au tiba ya mionzi

• Tibakemikali

• Usafishaji damu kwa mashine ya figo

• Huduma za oksijeni na gesi nyinginezo

• Huduma za nusu kaputi

• Ukaguzi 1 wa Macho na kupewa miwani 1

• Huduma za masikio zikiwemo kupendekeza,

kuweka au kubadilisha vifaa vya kusikilizia

• Huduma za ukalimani ikiwa daktari

anayekuhudumia anazo

Page 6: MWONGOZO WA KUTUMIA - Point Comfort RMA User Guide... · 2020. 6. 18. · • Chumba na chakula cha kila siku pamoja na huduma za uuguzi katika chumba binafsi kwa namna fulani au

Ni huduma zipi za afya

hazigharimiwi?

• Gharama za ujauzito na matumizi ya mtoto aliyezaliwa

• Bidhaa kwa ajili ya matumizi ya binafsi

• Kupata ushauri kwa njia ya simu au kukosa

kumwona mtaalamu ulivyopangiwa

• Mabadiliko yoyote yanayofanywa kwenye mwili ili

kuboresha mwonekano, au kuliwaza akili au

mawazo

• Mipango ya mazoezi, iwe imependekezwa na

daktari au la

• Upasuaji wa urembo au usio wa kimatibabu

• Matibabu ya utasa, ugumba au nguvu za

kufanya mapenzi

• Huduma au dawa ambazo ni za uchunguzi,

majaribio au za utafiti

• Upasuaji wa macho ili kurekebisha tatizo la

kutoona karibu au mbali au makengeza

• Matibabu ya mrejesho wa kiasili, tiba burudani, tiba

usingizi au tiba muziki

• Huduma au bidhaa unazopewa na mtu wa ukoo

wako au mtu yeyote anayeishi na wewe

• Huduma au bidhaa unazopewa bila malipo

• Ada za kusafiri au malazi

• Matibabu ya kukuza nywele, iwe umeandikiwa na

daktari au la

• Matibabu ya kuzuia kupoteza nywele

• Matibabu ya matatizo ya usingizi

• Huduma au bidhaa yoyote

ambayo Si ya Lazima Kimatibabu

• Huduma au bidhaa nyingine ambazo manufaa au

malipo yake unaweza kuyapata chini ya mkataba au

bima nyingine

(Baadhi ya matibabu yasiyogharimiwa hayawahusi watu

walio chini ya umri wa miaka 21. Wasilaina na PCU kwa

maelezo zaidi.)

6

Page 7: MWONGOZO WA KUTUMIA - Point Comfort RMA User Guide... · 2020. 6. 18. · • Chumba na chakula cha kila siku pamoja na huduma za uuguzi katika chumba binafsi kwa namna fulani au

DAWA ZA KUANDIKIWA

Ninaweza kutumia maduka gani ya dawa? Unaweza kupata dawa unazoandikiwa na daktari kupitia

mtandao wa maduka ya dawa ya MagellanRx

Management. Mtandao huu unajumuisha maduka yote kuu,

kama vile Walmart na CVS, na maduka mengi yaliyo karibu

nawe. Ni sharti uwasilishe kitambulisho chako kwa mfamasia

kila wakati unapotaka dawa uliyoandikiwa. Mfamasia

atathibitisha kwamba wapo kwenye mtandao huo na

kwamba unastahiki kupata dawa ulizoandikiwa na daktari.

MATIBABU YA

MENO

Ninaweza kuhudumiwa na daktari yupi wa meno? Unaweza ukatibiwa na daktari yeyote wa meno aliye

katika mtandao wa DenteMax. Unaweza kupata orodha

ya watoa huduma wa DenteMax katika

www.dentemax.com/findadentist, au piga simu kwa PCU ili

upate usaidizi. Ni watoa huduma wa DenteMax pekee ndio

wanaruhusiwa kufanya matibabu ya meno chini ya RMA.

Ni sharti uwasilsihe kitambulsiho chako cha RMA kwa daktari

wa meno kila wakati unapotaka matibabu ya meno.

Ni dawa zipi za kuandikiwa

hazigharimiwi?

• Dawa asili ikiwa dawa mbadala zinapatikana

• Dawa yoyote unayoandikiwa lakini ni ya matibabu

yasiyogharimiwa

• Dawa unazoweza kununua bila kuandikiwa na daktari

• Unaweza kupata dawa za kuandikiwa zisizozidi dozi ya siku 30

Ni matibabu gani ya meno

yanagharimiwi?

• Matibabu ya dharura ya meno

yanayolenga kumaliza maumivu au kuzuia

maambukizi

• Matibabu ya dharura ya meno kutokana na ajali

• Usafishaji na uchunguzi wa meno

Idhini ya kabla haihitajiki kwa matibabu ya dharura.

Ni matibabu gani ya meno

hazigharimiwi? Huduma zilizoorodheshwa hapo juu pekee ndizo

zinazogharimiwa.

7

Page 8: MWONGOZO WA KUTUMIA - Point Comfort RMA User Guide... · 2020. 6. 18. · • Chumba na chakula cha kila siku pamoja na huduma za uuguzi katika chumba binafsi kwa namna fulani au

8

IDHINI YA KABLA

Ni huduma zipi zinahitaji

kibali cha kabla?

Huduma nyingi zinazogharimiwa sharti zipate kibali cha

kabla. Hii ina maana kwamba sharti upate idhini ya PCU

kabla ya kutibiwa. Matibabu yafuatayo lazima yapate

kibali cha awali:

• Utunzaji wa wagonjwa waliolazwa

• Upasuaji wowote

• Huduma katika kituo cha huduma za muda mrefu

• Huduma za faraja

• Huduma za afya nyumbani

• Tiba ya kurekebisha maungo

• Tiba ya viungo

• Matibabu kwa vitendo

• Matibabu ya kunena

• Kupima mzio

• Vifaa vya kudumu vya kimatibabu

• Tiba ya Akili/Tabia

• Miguu/mikono bandia

• Huduma za viungo saidizi

• Upimaji kwa kutumia kompyuta (CAT Scan)

• Upigaji picha kwa nguvu ya sumaku (MRI)

• Kupandikizwa Kiungo/Tishu ya binadamu

Nifanyeje ili kupata

kibali cha kabla?

Mara tu unapogundua kuwa utahitaji huduma ambayo

inahitaji idhini ya kabla, wewe au mtoa huduma wako

mnapaswa kuwasiliana na PCU kupitia

[email protected] au kwa simu. Utatakiwa

utaje jina lako, namba ya kitambulisho chako, jina la

mhudumu ambaye unapanga kumtembelea, anwani yake

na maelezo ya matibabu unayopanga kupokea. Mara

nyingi PCU inaweza kutoa idhini ya kabla ya mara moja;

hata hivyo wakati mwingine idhini ya kabla inaweza

kuchukua hadi saa 48 ili kukamilisha. Ndiyo maana ni

muhimu kuwasiliana na PCU mara tu unapogundua

kwamba unahitaji matibabu.

Si lazima upate kibali cha kabla kwa matibabu ya dharura;

hata hivyo ni sharti upate idhini haraka iwezekanavyo.

Mara nyingi, mtoa huduma wako atatangulia kuitisha idhini

ya kabla kwa ajili yako. Atahijati maelezo yaliyo kwenye

kitambulisho chako cha RMA.

Watoa huduma wanaweza kuwasilisha maombi ya idhini

ya kabla kwa PCU kwenye pcf.pointcomfort.com.

Unafaa kuwasilisha kitambulisho chako cha RMA kila wakati

unapotafuta huduma.

Itakuwaje nikitibiwa bila Kibali cha

Awali?

Ukitibiwa matibabu ambayo yanahitaji idhini ya kabla na

ukose kupata idhini ya kabla, basi utagharimia matibabu

hayo.

Page 9: MWONGOZO WA KUTUMIA - Point Comfort RMA User Guide... · 2020. 6. 18. · • Chumba na chakula cha kila siku pamoja na huduma za uuguzi katika chumba binafsi kwa namna fulani au

9

KUKATA RUFAA

Itakuwaje ikiwa sitakubaliana na

uamuzi wa Kibali cha Kabla au

madai?

Unapaswa kuanza mara moja mchakato wa Kukata Rufaa

kwa kufuata hatua hizi:

1. Piga simu au uwaandikie PCU ukiwapa maelezo

kamili kuhusu rufaa yako ndani ya siku 30 tangu siku

ulipoomba Kibali cha Kabla au siku ambapo

uliambiwa kwamba utagharimia matibabu yako. Ni

sharti ujumuishe majina na maelezo ya mawasiliano

ya wahudumu wote waliohusika.

2. Ndani ya siku 10 za kazi, PCU itakutumia jibu la

kupokea yako na kuweka muda wa kukamilisha

uchunguzi wowote unaotakikana.

3. Ndani ya siku 30, PCU itakupa majibu kwa

maandishi kuhusu maamuzi juu ya rufaa

uliyokata.

FARAGHA

Kila wakati unapotibiwa, daktari wako huandika

kilichofanyika na kuiweka kwenye faili yako. Faili hii

huwekwa faraghani. Daktari wako anaweza tu kuwapa

watu wengine faili hiyo ikiwa utakubali.

PCU inatakiwa iweke faragha taarifa zinazohusu huduma

za matibabu unazopokea. PCU inaweza tu kuwapa watu

wengine taarifa zako ikiwa utakubali.

Una haki ya kupata nakala za rekodi zako za matibabu

kutoka kwa watoa huduma wako na kutoka kwa PCU.

Unaweza kuomba marekebisho yafanywe kwenye rekodi

zako ikiwa kuna jambo lisilo sahihi. Unaweza ukatakiwa

kumlipa mtoa huduma au PCU ada za kunakili rekodi

unazotaka.

Page 10: MWONGOZO WA KUTUMIA - Point Comfort RMA User Guide... · 2020. 6. 18. · • Chumba na chakula cha kila siku pamoja na huduma za uuguzi katika chumba binafsi kwa namna fulani au

10

Page 11: MWONGOZO WA KUTUMIA - Point Comfort RMA User Guide... · 2020. 6. 18. · • Chumba na chakula cha kila siku pamoja na huduma za uuguzi katika chumba binafsi kwa namna fulani au

ANWANI ZA HUDUMA ZAKO ZA RMA

Maswali kuhusu

ustahiki au manufaa:

[email protected]

1-844-210-2010

Maswali kuhusu

mitandao ya watoa

huduma:

Matibabu ya Kawaida na Meno

[email protected]

1-844-210-2010

rrp.pointcomfort.com

Dawa za Kuandikiwa na Daktari:

[email protected]

1-800-424-0472

Kubali cha Kabla:

[email protected]

1-844-210-2010

rrp.pointcomfort.com

Hali ya Madai:

[email protected]

1-844-210-2010

claims.pointcomfort.com

Rufaa:

[email protected]

1-844-210-2010

MASHIRIKA YA MAKAZI MAPYA KARIBU NAWE

Mashirika ya kuwapa wakimbizi makazi mapya:

Catholic Charities of Northeast Kansas

2220 Central Avenue

Kansas City, KS 66102

(913) 906-8937

International Rescue Committee –

Wichita

1530 S. Oliver Street, Suite #270

Wichita, KS 67218

(316) 351-5495

Episcopal Migration Ministries

401 N. Emporia Avenue

Wichita, KS 67202

(316) 977-9276

International Rescue Committee –

Garden City

1503 East Fulton Terrace

Garden City, KS 67846 (316)

805-6310

11

Page 12: MWONGOZO WA KUTUMIA - Point Comfort RMA User Guide... · 2020. 6. 18. · • Chumba na chakula cha kila siku pamoja na huduma za uuguzi katika chumba binafsi kwa namna fulani au

®

Kampuni ya Unified Administrators, LLC