Mume Kunyonya Matiti Ya Mke Wake - Imaam Ibn ´Uthaymiyn
-
Upload
wanachuoni -
Category
Documents
-
view
421 -
download
3
description
Transcript of Mume Kunyonya Matiti Ya Mke Wake - Imaam Ibn ´Uthaymiyn
Mume Kunyonya Matiti Ya
Mke Wake
Fataawa Za Wanachuoni
Swali:
Je, mke huwa haramu kwa mume wake
akinyonya matiti yake mara nne?
Imaam Muhammad bin Swaalih bin
'Uthaymiyn:
Allaah Kamhalalishia mume kufurahi kwa
mkewe atakavyo. Anaweza hata kufanya
naye mapenzi kwa njia mbalimbali. Allaah
(Ta´ala) Kasema:
���ؤم �رث �م ���وا �رم أ�� ���م
"Wake zenu ni konde kwenu. Basi
ziendeeni konde zenu vyovyote
mpendavyo." (al-Baqarah 02 :223)
Zingatia kauli "basi ziendeeni konde zenu
vyovyote mpendavyo." Konde ni mahali pa
rutuba ambapo ni tupu ya mwanamke.
Hivyo ni halali kwa mume kufanya kitendo
cha ndoa kwenye tupu ya mke sawa
ikifanywa kwa mbele, kwa nyuma, kwa
kusimama, kwa kulala au kupitia nafasi
nyingine yoyote kwa sharti iwe ni kwenye
tupu yake ya mbele. Hali kadhalika,
anaweza kufurahi naye kwa kumkumbatia,
kumkisi na kumbusu vile apendavyo.
Kilichoharamishwa tu ni yeye [mume]
kufanya naye kitendo cha ndoa wakati wa
hedhi na liwati [nyuma].
Kulingana na kanuni hii ya jumla, anaweza
kunyonya maziwa ya mkewe. Hawi [mke]
haramu kwake [mume] hata kama lau
atakunywa maziwa yake. Haya ndio maoni
ya jamhuri. Ili kunyonyesha kuathiri ni
lazima mtu awe chini ya miaka miwili.
Baada ya hapo hakuathiri kitu chochote.
Hali kadhalika ni lazima kunyonyesha
kufanyike angalau mara tano ili
kuharamike. Vinginevyo hakuathiri
chochote.
Chanzo: Nuur 'alaad-Darb (16A)