MKAKATI WA KUJENGA MSINGI WA HUDUMA YA YKM
-
Upload
youthkingdomministries -
Category
Spiritual
-
view
84 -
download
8
Transcript of MKAKATI WA KUJENGA MSINGI WA HUDUMA YA YKM
1
MKAKATI WA KUJENGA
MSINGI
WA HUDUMA YA YKM
2
YALIYOMO UTANGULIZI ....................................................................................................................................... 3
UWEZO WA NDANI (internal ability) ....................................................................................... 4
Uwezo wa ndani ....................................................................................................................................... 4
Vipao mbele vya huduma ........................................................................................................................ 5
Katiba, sera na ofisi zilizopo ndani ya YKM. ............................................................................................ 5
Usimamizi wa rasirimali na usuluhishi .................................................................................................... 6
Uanachama rasmi ..................................................................................................................................... 6
Matukio (events) ...................................................................................................................................... 6
Vyanzo vya fedha ..................................................................................................................................... 8
Matumizi ya teknolojia ............................................................................................................................ 8
Miundo Mbinu. ....................................................................................................................................... 10
Mpango wa muda mrefu ....................................................................................................................... 11
Utekelezaji wa mkakati .......................................................................................................................... 11
Hitimisho ................................................................................................................................................ 12
3
UTANGULIZI Huu ni mpango mkakati wa kujenga na kuimarisha msingi wa huduma ya YKM ndani ya mwaka
2015. Mpango mkakati huu umegusa kwa sehemu kubwa namna ya kujenga uwezo wa ndani wa
huduma katika kufanya kazi zake za kila siku, na hivyo basi kiini cha mkakati huu ni kujenga uwezo
wa ndani wa YKM. Ili kufanikisha kujengwa kwa uwezo wa ndani na kisha kuimarisha msingi wa
huduma, vipengele muhimu vimegusiwa,vipengele hivyo ni; Vipao mbele vya huduma, Katiba,
sera na ofisi zilizopo ndani ya YKM, usimamizi wa rasirimali na usuluhishi , uanachama rasmi,
matukio, vyanzo vya fedha, matumizi ya teknolojia, miundo Mbinu, mpango wa muda mrefu.
Mkakati huu unachambua namna ya utekelezaji wa shughuli za kimkakati kwa kila hatua. Ni imani
ya kwamba mkakati huu utatumika kama dira ya kufanikisha huduma kutimiza wajibu wake katika
maisha ya vijana na taifa la Tanzania.
4
UWEZO WA NDANI (internal ability) Uwezo wa ndani
Msingi mkuu wa taasisi yoyote kufanikiwa ni uwezo wake wa ndani wa kupanga na kutekeleza
shughuli zenye tija. Kwa kuwa taasisi ina wafanyakazi ambao ni watu, basi msingi mkuu wa
maendeleo ya taasisi ni watu wenye uweledi wa kupanga na kutekeleza shughuli zenye tija kwa
ajili ya maendeleo ya watu. Kwa kuwa wafanya kazi wa YKM ni vijana na wanafanya kazi na vijana
kwa ajili ya faida ya vijana katika kutimiza kusudi la uwepo wa huduma, YKM ita andaa mtaala
rasmi wa kuwajengea uwezo watenda kazi ambao ni viongozi.
Maeneo ambayo viongozi wata jengewa uwezo kwa mwaka 2015 ni:
ENEO SABABU
Uongozi wa
kimkakati(Strategic
leadership)
Viongozi wakiwa na mbinu za kuongoza kimkakati, itarahisisha
kufikia vitu tarajiwa ndani ya muda uliopangwa na kwa ufanisi.
Ushauri(Counseling) Utoaji wa ushauri ni jambo la msingi kwa kipindi tulichonacho haswa
ukizingata huduma ina kutana na vijana walio na historia tofauti za
kimaisha (background). Kwa kuwa utoaji wa ushauri siyo sawa na
mazungumzo ya kawaida ni vyema viongozi waka jengewa uwezo wa
kushauri vijana katika masuala tatanishi yanayo wasibu vijana katika
maisha.
Stadi msingi za
teknohama(Basics
skills of IT)
Kwa kuwa teknolojia inakuwa ni vyema viongozi wakapatiwa stadi
msingi za teknohama, ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi na ndani
ya muda uliopangwa.
Kwa kuwa viongozi wa kitaifa wapo katika mikoa tofauti, ni vyema viongozi hawa wakawa
wanakutana mara moja kwa mwezi kwa ajili ya;
Kupata mafunzo ya kujengewa uwezo katika maeno tajwa hapo juu.
Kutathmini hali ya utendaji kazi wa masuala muhimu yaliyojadiliwa katika vikao
vilivyopita.
Kujadili, kufanya maamuzi na kutekeleza makubaliano. Makubaliano yote yatapaswa
kuandikwa katika karatasi (Tazama kiambatanisho cha kwanza).
5
Kwa kuwa katibu mkuu ndiyo mtendaji wa kazi za kila siku za huduma, ofisi hiyo itateua ofisi tatu
ndani ya YKM kuandaa mtaala wa mafunzo wa maeneo matatu yaliyotajwa katika jedwali hapo
juu.Uteuzi huo unapaswa kufanywa tarehe 12 Aprili 2015. Ofisi ya katibu itatoa muda usiozidi
wiki tatu kwa ajili ya kazi hiyo.
Mara baada ya kazi hiyo kukamilika, nakala itawasilishwa ofisi ya katibu mkuu na ofisi hiyo
itaitisha kikao cha kamati kuu tendaji ya huduma kwa lengo la kujadili na kuboresha maeneo ya
uwezeshaji kabla ya kuanzwa kwa utekelezaji.
Vikao vyote vya viongozi vitaratibiwa na ofisi ya katibu mkuu.
Kwa kuzingatia changamoto ya umbali kati ya kiongozi mmoja na mwingine, tarehe 20 Aprili 2015
ofisi ya katibu itatangaza rasmi ya kwamba mikutano mikubwa miwili ambayo ni;
Mkutano mkuu wa mwaka wa huduma.(Mwezi Julai, kila mwaka)
Mkutano wa mwezi februari. (Mwezi februari, Kila mwaka)
Itakuwa ni mikutano rasmi ya kuwajengea uwezo viongozi wa kitaifa. Hivyo basi mkakati
unapendekeza ya kwamba kuwepo na vipindi ambavyo washiriki wake watakuwa viongozi wa
kitaifa tu. Ofisi ya mipango, ofisi ya ukusanyaji rasirimali, ofisi ya mhazini mkuu zitakuwa ni ofisi
kuu katika kutengeneza mpango wa uendeshwaji wa mikutano hiyo. Mpango huo unapaswa uwe
umekamilika miezi mitatu kabla ya tarehe ya mkutano husika.
Vipao mbele vya huduma
Mkakati unapendekeza ofisi ya mkurugenzi mkuu iainishe vipao mbele vya huduma kwa miaka
miwili mfululizo (2015-2016). Ili kufanikisha suala hilo, ni vyema ofisi ya katibu mkuu ikaitisha
kikao cha kujadili vipao mbele vya huduma, iwapo kikao hakitafanikiwa kufanyika ofisi ya katibu
itapaswa kukasimu madaraka ya kuainisha vipao mbele kwa moja ya ofisi au ofisi zaidi ya moja.
Vipao mbele vinapaswa kuwa tayari kabla ya tarehe 20 Aprili 2015.
Katiba, sera na ofisi zilizopo ndani ya YKM.
Mkakati unapendekeza kabla ya tarehe 12 Aprili 2015, ofisi ya katibu mkuu itume katiba ya YKM
kwa kila ofisi ndani ya YKM. Ofisi zote zitapaswa kuandaa sera na taratibu za ufanyaji wa kazi kwa
kufuata msingi wa katiba ya YKM, kazi hiyo inapaswa kufanywa kabla ya tarehe 30 juni 2015.
6
Usimamizi wa rasirimali na usuluhishi
Kwa kuwa ofisi ya ukusanyaji rasilimali ndiyo chombo husika katika usimamizi wa rasirimali za
YKM.mkakati unapendekeza ofisi hiyo itengeneze sera rasmi ya kuratibu usimamizi wa mali zote
zilizomo mikononi wa viongozi wa YKM. Sera hiyo inapaswa kuwa tayari kabla ya tarehe 12 Aprili
2015, na iwasilishwe ofisi ya katibu mkuu, siku saba baada ya ofisi ya katibu kupokea, ofisi hiyo
itapaswa kutuma sera hiyo kwa walezi wa mikoa ya YKM, walezi wa mikoa watapaswa kusoma
sera na kuielewa na kisha kuwatumia wakurugenzi wa mikoa ya YKM.
Kuhusu usuluhishi; Iwapo kutatokea kutoelewana katika utendaji wa kazi, ufanyaji wa maamuzi
na ugawanywaji wa rasirimali (Resources allocation). Mkakati utashauri viongozi kuwa makini
katika utendaji wa kazi.
Wafilipi 2:3-4
“3 Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na
amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake.
4 Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine.”
Uanachama rasmi
Kwa kuwa huduma ina uanachama, basi mkakati unapendekeza wanachama wote wa andikishwe
upya kwa kujaza fomu ya maombi ya uanachama (Tazama kiambatanisho cha pili), pia mkakati
unapendekeza ofisi ya katibu na ofisi ya mipango zipitie katiba ya YKM na kuangalia kipengele
kinachohusiana na uanachama.
Matukio (events)
Ili kuongeza ufanisi wa uandwaaji na ufanyikaji wa matukio, YKM itakuwa na matukio kwa mkoa
wa Dodoma tu kwa kipindi cha mwaka 2015.
Matukio yatakayo fanyika Dodoma ni;
“Kingdom Transformer Leadership Gathering”-Tukio litakuwa likifanyika kila juma pili ya
mwisho wa mwezi.
Matukio ya huduma za YKM mfano “Kingdom inspiration”, “Kingdom ladies”
7
Kwa kuwa mkoa wa Dodoma utahusika katika matukio hayo, mkakati unapendekeza mlezi wa
mkoa aandae utaratibu maalumu wa kuwajengea uwezo viongozi wa mkoa husika ili waweze
kuandaa matukio katika ubora wa hali ya juu.
Mfumo utakao tumika kuwajengea uwezo viongozi wa Dodoma, utakuwa ni mfumo mfano
(Model system) katika kuwajengea uwezo viongozi wa mikao mingine ya YKM, hivyo basi mkakati
unashauri mlezi wa mkoa wa Dodoma afanye mawasiliano na ofisi ya mipango katika kufanikisha
suala hili. Ofisi ya mipango inapendekeza “event guidelines” zitumike. Kwa maelezo zaidi, tazama
kiambatanisho namba tatu(Event guidelines)
Mkakati unapendekeza ofisi ya ukusanyaji wa rasirimali, ofisi ya miradi na ofisi ya habari ifanye
tathmini ya mapungufu yaliyojitokeza katika matukio ya mwaka 2012 mpaka mwaka 2014, ofisi
ya ukusanyaji rasirimali,ofisi ya miradi na ofisi ya habari zinapaswa kuanza kazi hiyo tarehe 12
aprili 2015 mpaka tarehe 2 Mei 2015.Tathimini itapaswa kuzingatia maeneo yafuatayo;
Uandwa aji wa matukio
Uendeshwaji wa matukio
Changamoto ya uuzaji wa bidhaa katika matukio.
Yatokanayo na matukio(out comes)
Changamoto kuu za matukio
Mapendekezo juu ya suluhu (solutions) stahiki zinazopaswa kutekelezwa katika uanda aji
wa matukio.
Mapendekezo ya kupunguza au kuongeza matukio,kwa ajili ya kufanikisha kusudi la
huduma
Ripoti itapaswa kupigwa chapa (printing) na kufungwa (binding).
Tarehe 7 Mei 2015, tathmini itakabidhiwa kwa ofisi ya katibu mkuu na katibu mkuu ataiwasilisha
ofisi ya mkurugenzi mkuu wa taifa. Ofisi ya mkurugenzi mkuu itachukuwa hatua zinazopaswa
kuchukuliwa baada ya kuisoma ripoti, kwa lengo la kuboresha matukio yatakayo fuata.
8
Vyanzo vya fedha
Kwa muda mrefu huduma imekuwa ikitegemea kupata fedha kwa njia ya michango ya hiari
kutoka kwa wadau mbali mbali, hali hii imepelekea kuwepo changamoto katika utendaji. Mkakati
unashauri kuwepo upembuzi yakinifu (analysis) ni kwa jinsi gani huduma inaweza ikapata fedha
za kuendesha shughuli zake.
Mkakati unapendekeza ofisi ya ukusanyanyi rasilimali, ofisi ya miradi, ofisi ya hazina kuu ya
huduma na ofisi ya habari, zifanye kazi hiyo ya upembuzi yakinifu na kuja na mapendekezo
yatakayoweza kutekelezwa kwa ajili ya kuongeza upatikanaji wa fedha katika huduma. Kazi hiyo
inapaswa kufanyika kuanzia tarehe 12 April 2015 mpaka 10 July 2015. (Tazama kiambatanisho
cha nne, mkakati unashauri hatua zilizo ainishwa katika kiambatanisho hicho zifuatwe)
Kwa kuwa kuna ofisi za hazina katika mikoa ya YKM, mkakati unashauri ofisi ya hazina kuu na ofisi
ya miradi, ziandae utaratibu maalumu wa kusimamia fedha zilizopo katika mikoa husikana
uuzwaji wa bidhaa za YKM, utaratibu huo unapaswa uwe tayari kabla ya tarehe 4 Mei 2015 na
usambazwe kwa walezi wa mikoa ili walezi wausambaze utaratibu huo kwa viongozi wao wa
mikoa.
Matumizi ya teknolojia
Mkakati una pendekeza makundi yote ya “WhatsApp” yatumike kama nyenzo muhimu katika
kusuma mbele maendeleo ya YKM. Ni vyema maudhui (content) ya kila kundi yakafanyika msaada
kwa kila mtu aliyepo ndani ya kundi. Kwa kuwa wamiliki wa “WhatsApp” hawatengenezi content
bali “content” hutengenezwa na watu waliopo ndani ya kundi husika, hivyo basi ni busara kila
mwana kundi akatuma jumbe zilizo na maadili, kuelemisha na zenye kutoa msaada.
Msaada wa namna gani?
Kwa kuwa asilimia kubwa ya washiriki katika makundi ya “WhatsApp” ni vijana waliopo chuoni
na baadhi yao ni vijana waliopo nje ya chuo, mkakati unapendekeza “content” iwe katika maeneo
ambayo yana wagusa vijana kwa sehemu kubwa, maeneo hayo ni;
9
Ajira- Baada ya kumaliza chuo kijana atajiajiri au ata ajiriwa. Ni vyema waliopo kwenye
kundi waka wana pashana habari zinahohusu namna gani kijana anaweza akajiajiri au
vitu gani kijana anapaswa kuvifuata ili aweze kuajiriwa na kupata ajira yenye tija kwa
maisha yake binafsi. Matangazo ya kazi hayataruhusiwa kuwekwa, kwani matangazo
yaliyo mengi ni marefu, mkakati ushauri badala ya kuweka tangazo mtoa post aweke
“link” ya tangazo ili mtu atakaye penda kusoma zaidi kuhusu tangazo la ajira afuate “link”
husika.
Suala la kuwa na kipato ni suala la msingi sana katika kipindi hiki, mkakati unapendekeza
siku ya juma tatu iwe ni siku rasmi kwa majadiliano yanayohusu ni namna gani mtu binafsi
unaweza ukajiongezea kipato na masuala ya maendeleo ya mtu. Mjadala utafungwa saa
tano usiku na Mbeba maono wa huduma ya YKM, Raphael J. Lyela.
Mahusiano- Mahusiano ni moja kati ya mambo ambayo yanajadiliwa sana na vijana kila
mahali, kwani wengi wao huwa katika kipindi cha kutafuta wenzi wao wa maisha. Licha
ya mjadala kuwa mkubwa, bado vijana wanafanya makosa mengi ya kimahusiano na
hivyo kuathiri hatma ya maisha yao. Mkakati unapendekeza siku ya juma nne iwe siku
rasmi ya kujadili mahusiao, wanaojadili wanapaswa wawe wa angalifu sana na wenye
hekima, na hivyo basi mchangiaji atapaswa kuchangia ki uadilifu, kwa uangalifu, umakini
ili mchango wake uwe mchango wenye mantiki na si kwa ajili ya mzaha, katika
majadiliano hayo hairuhusiwi kutuma picha zisizo na maadili. Mkakati unashauri kila
kijana aliyepo kwenye kundi husika ajishibishe maarifa juu ya mahusiano pasipo kwenda
kinyume na Mungu.
“Spiritual growth”- Vijana katika kila kundi husika watapaswa kupata mafundisho juu ya
“personal spiritual growth” Kwa kuzingatia neno la Mungu. Aidha wachangiaji
wanashauriwa wawe na uelewa juu ya wanacho changia ili kuondoa upotoshaji,
wachangajia wasichangie kwa lengo la kushinda bali kwa lengo la kuelimishina. Mkakati
unapendekeza siku ya juma tano iwe siku ya mafundisho na majadilino.
10
Kwa kuwa siku ya jumatatu mpaka jumatano zitakuwa na shughuli zilizo ainishwa hapo
juu. Mkakati unapendekeza siku ya alhamisi, iwe siku maalumu ya kufundishwa somo
maalumu kutoka kwa Mbeba maono wa huduma. Raphael J. Lyela watu watapata muda
wa kuuliza maswali juu somo husika na kisha kujibiwa maswali. Siku ya ijumaa itakuwa
siku ya maombi, ofisi ya kuu ya maombi katika huduma itasimamia utaratibu rasmi wa
kuratibu maombi kwa kushikirikiana na ofisi nyingine ndani ya YKM. Siku ya juma mosi ni
siku ya mawasiliano baina ya mtu mmoja na mwingine ndani ya YKM. Siku ya juma pili ni
siku ya kushirikishana namna ya kukabiliana na kuzishinda changamoto za maisha.
Mkakati unapendekeza makundi ya “WhatsApp” yasiwe mahali pa kukutana, bali pawe
ni mahali pa kukuzana katika Nyanja muhimu za maisha, hivyo basi ni muhimu kwa mtu
kabla ya kutuma ujumbe wake afikiria kwa umakini na kufanya maamuzi sahihi, kwa
manufaa ya wengine
Ufanyaji kazi kupitia “WhatsApp”. Mkakati unapendekeza makundi ya viongozi yawe ni
mahali pa kupashana habari zinazohusu kazi na si mazungumzo binafsi.
Kwa kuwa kuna makundi kadhaa ya YKM, mkakati unapendekeza kila kundi liwe na
msimamizi maalumu wa kundi husika, na kila msimamizi atawajibika kwa ofisi kuu ya
habari. Ofisi kuu ya habari itafanya mabadiliko wakati wowote kuhusiana na uendeshwaji
wa makundi kwa lengo la kuongeza ufanisi katika uwajibikaji.
Miundo Mbinu. Ili kuweza kufanikisha kuwaleta vijana pamoja, YKM ita kuwa na mpango rasmi wa kujenga kituo
cha mafunzo ya uongozi kwa vijana, kituo kitaiwa “Leadership Garden”. Kituo kitatumika kama
nyenzo muhimu katika kutimiza kusudi la uwepo wa YKM. Mkakati unapendekeza ofisi ya
mkurugenzi mkuu ipitie pendekezo la kuanzishwa kwa kituo hicho na kulifanyia maamuzi kabla
ya tarehe 20 July 2015. Ili kupata taarifa zaidi juu ya “Leadership Garden” tazama kiambatanisho
namba tano.
11
Mpango wa muda mrefu
Kutakuwa na ujenzi wa chuo kitakacho itwa “Kingdom Transformer leadership Institute”.
Mkakati unashauri hatua za awali zifanyike kabla ya 30 disemba 2015. Hatua hizo ni pamoja na.
Uandikwaji wa andiko la uanzishwaji wa taasisi (Proposal)
Uandwa aji wa mtaala wa mafunzo yatayotolewa (Curriculum).Mkakati unapendekeza
chuo kianze na mitaala miwili, ambayo ni;-
i. Mtaala wa mafunzo ya teknolojia ya habari na mawasiliano (information and
communication technology), ngazi ya cheti
ii. Mtaala wa mafunzo ya usimamizi wa biashara(Business management),ngazi ya
cheti
Kufuata taratibu za kuanzishwa chuo chini ya VETA(Tazama kiambatanisho cha sita)
Kujua taratibu za kupata usajili wa NACTE(Tazama kiambatanisho cha saba)
Mkakati unashauri upembuzi yakinifu ufanyike katika eneo la kujua gharama halisi ya
kuendesha chuo kwa faida ya kipato na utoaji wa elimu bora. ofisi ya mkurugenzi mkuu wa taifa
inapaswa kukasimu kazi hii kwa ofisi zaidi ya mbili ndani ya YKM kabla ya tarehe 20 Aprili 2015,
kwa mantiki hiyo ofisi ya mkurugenzi wa taifa itakuwa msimamizi mkuu wa mradi huu.
Utekelezaji wa mkakati Kwa kuwa utekelezaji wa mikakati huathiriwa na sababu mbalimbali na changamoto
zinazowakumba watekelezaji wa mkakati, ili kuhakikisha utekelezwaji wa mkakati huu ofisi ya
mkurugenzi mkuu na ofisi ya katibu mkuu zita kuwa ofisi zinazosimamia na kufuatilia utekelezaji
wa mkakati mpaka 30 Disemba 2015.
Utekelezaji uta anza rasmi tarehe 12 Aprili 2015 na utakuwa una tathminiwa kila tarehe 12 ya kila
mwezi katika mwaka 2015, baada ya tamko kutoka ofisi ya mkurugenzi mkuu.
Hatua za kufuata kabla ya kutoa tamka la utekelezwaji wa mkakati huu.
Ofisi ya mkurugenzi itapaswa kuitisha kikao kupitia ofisi ya katibu mkuu.
Kazi ya kikao itakuwa ni kujadili mkakati huu, ku ufanyia marekebisho na kukubaliana
namna bora zaidi ya kuutekeleza.
12
Baada ya makubaliano, ofisi ya mkurugenzi mkuu itatoa rasmi tamko.
Mkakati utatekelezwa mpaka tarehe 30 Disemba 2015.
Hitimisho Tathmini kuu ya mkakati itafanyika tarehe 5 Januari 2016.