Miaka 50 ya Mahkama Zanzibar
-
Upload
annurtanzania -
Category
Documents
-
view
254 -
download
0
Transcript of Miaka 50 ya Mahkama Zanzibar
-
8/14/2019 Miaka 50 ya Mahkama Zanzibar
1/6
MAHKAMA NDANI YA MIAKA 50 ILIYOPITA ZANZIBAR: MAFANIKIO NA
CHANGAMOTO
Na ALI UKI, MHADHIRI WA SHERIA, ZANZIBAR UNIVERSITY.
TAREHE: 16 NOVEMBA, 2014
Utangulizi
Mahkama imetimiza miaka 50 tokea Mapinduzi ya Januari 12, 1964. Mahkama1, moja
katika mihimili mitatu. Katika utekelezaji wa majukumu yake, Mahkama imepita katikavipindi saba tofauti vya uongozi wa nchi ama vimesaidia mafanikio au chachu za
changamoto. Vipindi vya uongozi ni kuanzia 1964 mpaka 1972 chini ya uongozi wa
marehemu Sheikh Abeid Amani Karume, kutoka 1972 mpaka 1984 chini ya uongozi wa
Alhaj Aboud Jumbe, kutoka 1984 mpaka 1985 chini ya uongozi wa Alhaj Ali HassanMwinyi, kutoka 1985 mpaka 1990 chini ya uongozi wa marehemu Sheikh Idris
Abduwakil, kutoka 1990 mpaka 2000 chini ya uongozi wa Dk. Salmin Amour, kutoka
2000 mpaka sasa 2010 chini ya uongozi wa Mheshimiwa Amani Abeid Karume na 2010hada sasa chini ya uongozi wa Dk. Ali Mohamed Shein.
Vipindi tofauti vya uongozi vimetoa misukumo ya mabadiliko, maendeleo na
changamoto za Mahkama. Misukumo iliyotokea ambayo imeleta athari katika utendajikazi wa Mahkama imesababishwa na mapinduzi fikra za kuendesha mambo wenyewe,
misukumo na mageuzi ya siasa, uboreshaji wa sekta ya Mahkama, upanuzi wa siasa za
demokrasia na uhuru wa Mahkama.
Mkusanyiko huu utasaidia kujenga taswira ya utendaji kazi wa Mahkama na kielelezo
kikubwa cha mafanikio ya Mahkama. Michango itakayotolewa itakuwa ni kioo na
itasaidia kuimarisha utendaji kazi wa Mahkama na wala haitokuwa chanzo cha chuki chakutizama sura ya aliyetoa mchango.
Baadhi ya Vigezo vya Mafanikio na Changamoto zinazoikabili Mahkama Zanzibar
Mafanikio na changamoto za Mahkama Zanzibar zinaweza kutathminiwa katika vigezo
tofauti. Baadhi ya vigezo ni hivyi vifuatavyo:
(i) Kisheria;(ii) Watendaji kazi;(iii) Ubora wa maamuzi (seriousness of judgements)yanayotolewa na Mahkama;(iv) Uhusiano wa uongozi wa Mahkama na watendaji kazi wa Mahkama;(v) Msukumo wa kisiasa katika utendaji kazi wa Mahkama;(vi) Uhuru wa Mahkama;(vii) Uelewa wa sheria wa wananchi;(viii) Imani ya wananchi kwa Mahkama za Zanzibar;
1 Kifungu cha 5A (1) cha Katiba ya Zanzibar ya 1984 kinasema kwamba Zanzibar itafuata mfumo wa
mgawanyo wa madaraka kati ya mamlaka tatu, Mamlaka ya Utendaji, Mamlaka ya Kutunga Sheria na
Kusimamia Utekelezaji wa Shughuli za Umma na Mamlaka ya Kutekeleza Utoaji wa Haki.
-
8/14/2019 Miaka 50 ya Mahkama Zanzibar
2/6
-
8/14/2019 Miaka 50 ya Mahkama Zanzibar
3/6
(8)Mahkama za Watoto5: Chini ya Sheria hii, Mahkama ya Watoto imeanzishwa nakesi za Mahkama hii zitasikilizwa na Hakimu wa Wilaya kinyume na awali
Hakimu wa Mahkama ya Mkoa alipewa uwezo wa kusikiliza kesi zotezinazohusiana na mtoto.
(9)Uhuru wa Mahkama6: Katiba ya Zanzibar ya 1984 inatambua uhuru waMahkama Zanzibar.(10) Majaji wa Mahkama Kuu kutoondolewa kiholela7. Majaji wamepewakinga maalum ya kuondoshwa katika nyadhifa zao. Awali Jaji wa Mahkama Kuu
angeliweza kuondoshwa kwa mujibu wa utashi wa rais (at the pleasure of the
president).(11) Kuanzishwa Sheria ya Mahkama Kuu8No. 2 ya 1985(12) Jaji Mkuu kutokuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya
Mahkama: Baada ya malalamiko, Sheria ya Tume ya Utumishi imefanyiwa
marekebisho na Jaji Mkuu sio mwenyekiti wa Tume.(13) Tume ya Utumishi ya Mahkama kutambuliwa katika Katiba9(14) Ongezeko la majaji: Mahkama Kuu ya Zanzibar ina jumla ya majaji sita
wakiwemo majaji wanawake.(15) Kuwepo majaji na mahakimu wanawake: Majaji na mahakimuwanawake wamekuwa sehemu wa watendaji wa Mahkama wanaotoa haki.
(16) Ongezeko la Mahakimu: Idadi ya Mahakimu imefikia 63, 47 wapoUnguja na 16 wapo Pemba.
(17) Idadi ya Makadhi Imeongezeka: Wapo makadhi 15, 10 wapo Unguja(akiwemo Kadhi Mkuu na Naibu Kadhi Mkuu) na watano wapo Pemba.
(18) Maslahi ya majaji na mahakimu kuongezwa: Maslahi ya watendajihawa yameboreshwa sana kulinganisha na taasisi nyengine. Lakini mahakimu wa
Mahkama za Mwanzo wanasikitika.
(19) Kuondoshwa Mahkama za wananchi (The Peoples Courts No. 11 of1969) ambazo zilizokuwa hazifuati mfumo wa sheria ya utoaji haki.
(20) Ongezeko la majengo ya Mahkama Unguja na Pemba.(21) Kurejeshwa huduma za mawakili katika Mahkama Zanzibar.(22) Kurejeshwa huduma za mavakil.(23) Idadi ya mawakili walioruhusiwa na Mahkama Zanzibar kuongezeka.
Zaidi ya mawakili 100 wamesajiliwa na Mahkama Kuu Zanzibar.
(24) Mashirikiano ya Mahkama naasasi za kiserikali na kiraia kuongezeka.(25) Kuanzishwa Siku ya Mahkama (Law Day).
5Sheria Namb. 6 ya 2011.6
Kifungu cha 5A (3) kinasema kuwa hakuna mamlaka itakyoingilia Mamlaka nyengine isipokuwa na kwakadri ilivyoelezwa katika Sheria.7Kifungu cha 95 (5) cha Katiba ya Zanzibar kinasema kwamba Jaji wa Mahkama Kuu ataondolewa kazini
na Rais ikiwa suala la kuondolewa kwake limepelekwa kwa Tume iliyoundwa kwa madhumuni hayo chini
ya kijifungu cha (6) cha kijifungu hiki na Tume hiyo imependekeza kwa Rais kwamba Jaji huyo anafaa
kuondolewa kutokana kazi zake au kutokana na tabia zake mbaya.8Sheria Namb. 2 ya 1985.9Kifungu cha 102 cha Katiba ya Zanzibar kinasema kwamba kutakuwa na Tume ya Utumishi ya Mahkama
ambayo muundo, kazi na uwezo wake utakuwa kama ilivyoelezwa na Sheria iliyotungwa na Baraza la
Wawakilishi.
-
8/14/2019 Miaka 50 ya Mahkama Zanzibar
4/6
Changamoto za Mahkama Zanzibar
(1)Rushwa:Tuhuma za harufu ya rushwa kuwepo kwa baadhi ya watoa maamuziwa Mahkama. Ni vigumu kuithibitisha kwasababu wanaolalamika hawapo tayari
kutoa ushahidi. Vile vile, malalamiko yanasikika baada ya kutolewa maamuzi nasio wakati kesi inaendelea. Aidha, kuwepo watu wa kati wa kuunganisha rushwa(middlemen)baina ya baadhi ya watoa haki na wahusika wa kesi/shauri. Rushwa
ya Mahkama imegawika mafung yafuatayo: (a) rushwa ya muhali (b) rushwa ya
fedha na (c) rushwa ya hisia (perceived corruption).(2)Tuhuma za ushawishi wa wanasiasa kuingilia utendaji kazi wa Mahkama
Zanzibar. Inadaiwa kwamba mwenendo na maamuzi ya kesi yanashika (influence)
na nguvu za wanasiasa wa ngazi tofauti.
(3)Mahkama kuwa masafa marefu na wananchi: Inakuwa vigumu wananchikwenda mahkamani. Kwa mfano, mkaazi wa Tumbatu au Nungwi inambidi
asafiri hadi Mfenesini ikiwa kesi/shauri linalomhusu lipo katika Mahkama ya
Mkoa, Mfenesini. Tatizo la masafa linaumiza zaidi kesi inapoingia hatua ya rufaakatika Mahkama ya Mkoa au Mahkama Kuu ya Zanzibar.
(4)Majengo ya Mahkama ni mabovu na makongwe: Mfano wa jengo la Mahkamala Makunduchi na Mfenesini.
(5)Ukosefu wa nafasi katika majengo ya Mahkama: Kwa mfano, jengo laMahkama Kuu, Zanzibar lilijengwa mwaka 1908 kukidhi idadi ya wananchi ya
wakati huo, lakini halijafanyiwa utanuzi na linafanyiwa mabadiliko ya ndani
(internal modification).Baadhi ya Mahakimu hulazimika kutumia chumba kimojakuendesha kesi tofauti tena kwa wakati mmoja. Jengo la Mahkama ya Wilaya ya
Mwanakwerekwe halitoshi na Afisi ya Waendesha Mashtaka ni ndogo mno.
(6)Uelewa mdogo wa sheria: Idadi kubwa ya wananchi hawafahamu sheria nabaadhi ya wakati wanatarajia Mahkama iamue kwa kufuata matamanio yao.
(7)Ukosefu wa Maktaba:Mahkama haina maktaba ya kisasa, ukosefu wa ripoti zasheria na vitabu vya sheria vitakavyowasaidia majaji na mahakimu kuongeza
uwezo.(8)Ukosefu wa usafiri kwa Mahakimu:Kinyume na majaji, mahakimu hulazimika
kutumia usafiri wa umma na baadhi ya wakati kujikuta wapo pamoja ndani ya
gari na ndugu au jamaa ya wahusika kesi jambo ambalo huwatia hofu ua usalamawao.
(9)Bajeti ya Mahkama ni finyu:Bajeti ya Serikali imekuwa ndogo na kikomo chabajeti (ceiling) kinatolewa na Wizara ya Fedha. Aidha fedha zinazoinishwa na
Baraza la Wawakilishi zinapatikana kwa asilimia chache. Kwa mfano mwaka wafedha 2010/2011, jumla ya shilingi 550,000/- za bajeti ya maendeleo
ziliidhinishwa lakini zilizopatikana ni shilingi 275,000,000/-, mwaka wa fedha
2012/2013 jumla ya fedha za bajeti ya maendeleo zilizoinishwa na Baraza la
Wawakilishi ni shilingi 100,000,000/- lakini zilizopatikana ni asilimia 17 tu yafedha hizo. Mwaka wa fedha 2013/2014 jumla ya fedha za bajeti ya maendeleo ni
shilingi 150,000,000/- lakini hapana uhakika wa kupatikana fedha zote.
(10) Mashahidi kutofika mahkamani: Imekuwa tabia baadhi ya mashahidikutofika mahkamani kutoa ushahidi. Hii inaathiri mno maamuzi ya Mahkama.
-
8/14/2019 Miaka 50 ya Mahkama Zanzibar
5/6
(11) Ucheleweshaji wa kesi: Baadhi ya watendaji wa Mahkamawanatuhumiwa kuchangia kwa kiasi kikubwa kesi kuchelewa kwa visingizio
tofauti.(12) Mzigo mkubwa wa kesi kwa mahakimu: Kwa mfano, hakimu wa
Mahkama ya Mkoa alikuwa na wastani wa kesi 59 kwa mwaka 2012.10
Hakimu
wa Mahkama ya Wilaya alikuwa na wastani wa kesi 178 kwa mwaka 2012.
11
Hakimu wa Mahkama ya Mwanzo alikuwa na wastani wa kesi 104 kwa mwaka2012.
12Wastani wa kesi wa Jaji wa Mahkama Kuu ni 14 kwa mwaka 2012
13
(13) Utafiti hafifu na uwezo mdogo wa watendajiwa Mahkama. Baadhi yamaamuzi ya Mahkama katika ngazi zote yanaonyesha kukosekana utafiti wa kinawa marudio na uchambuzi makini. Baadhi ya mawakili waliohojiwawalisema
kwamba inasikitisha kuona kwamba watendaji wa Mahkama wa ngazi zote
wanashindwa kufahamu utaratibu wa mwenendo wa kesi (procedure)na kuathiri
haki. Aidha. makadhi wanalalamikiwa kutotumia kitabu au vitabu vya aina moja.Kila kadhi anategemea kitabu anachokipendelea binafsi. Hii inasabisha tofauti ya
maamuzi kwa mujibi wa vitabu vya marejeo.
(14)
Majaji na mahakimu kufunga ushahidi:Baadhi ya wakati, majaji aumahakimu kufunga ushahidi. Jukumu la kufunga ushahidi la la upande wa
mashtaka. Athari yake ni kukatwa rufaa, mfano Mahkama ya Rufaa Tanzania
lakini maamuzi ni kesi ianze kusikilizwa tena jambo ambalo linaathiri mno
upatikanaji wa mashahidi kwa mara ya pili.(15) Mahakimu wapya kutopata mafunzo ya Mahkama: Baadhi ya
mahakimu wanaajiriwa moja kwa moja kutoka Chuo Kikuu na bila ya kupata
mafunzo wanapewa kesi. Matokeo yake ni ukiukwaji wa utaratibu katikaupatikanaji wa haki. Inadaiwa kwamba baadhi ya mahakimu wapya hawajiamini
na wanababaika mno anapokuwa wakili mbele yao.
(16) Majaji na Mahakimu:Utafiti umeonyesha kwamba baadhi ya mawakiliwanalalamika kwamba majaji na mahakimu wanaegemea zaidi upande wamashtaka katika kuendesha kesi na baadhi ya wakati majaji/mahakimu
wanajisahau na kuuliza maswali kama wanawasilisha kesi (make submission,)
wanauliza maswali ya kujenga kesi ya upande wa mashtaka dhidi yawalalamikiwa.
(17) Majalada ya kesi kufichwa: Utafiti unaonyesha kwamba baadhi yamakarani ama kwa kupewa maelekezo na majaji au mahakimu auwanawasingizia, huficha majalada ya kesi ili kudhoofisha utendaji wa haki.
(18) Baadhi ya Majaji na mahakimu kuwachagulia wakili wahusika wakesi: Ushahidi unaonyesha kwamba watoa haki huwapigia simu mawakili na
kuwaelekeza kupokea kesi kutoka kwa mlalamikaji au mlalamikiwa. Kitendo hikikinadhoofisha haki kutendeka na kuonekana kutendeka.
(19) Vitisho dhidi ya wahusika wa kesi:Utafiti unaonyesha kwamba baadhiya majaji na mahakimu ni wakali sana na hutoa kauli zinazowatisha au
kuwakatisha tama wahusika wa kesi.
10Tanzania Human Rights Report, Part II on Zanzibar, 2012, pg 321.11Ibid.12Ibid, pg. 322.13Ibid, pg 321.
-
8/14/2019 Miaka 50 ya Mahkama Zanzibar
6/6
(20) Mahudhurio ya majaji na mahakimu kazini: Utafiti unaoyeshakwamba mahudhurio ya waheshimiwa hawa yanalalamikiwa. Wanafika na
kuondoka kazini kwa kufuata ratiba binafsi za mambo yao.(21) Kigezo kinachotumiwa na Jaji Mkuu kupanga kesi:Utafiti unaonyesha
kwamba Mheshimiwa Jaji Mkuu hana kigezo maalum cha kupanga kesi kwa
majaji wa Mahkama Kuu. Baadhi ya wakati, majaji wanalalamikiwa kukataakupokea kesi bila ya sababu ya msingi ya sheria.(22) Wazee wa Mahkama: Inalalamikiwa kwamba Vifungu vya 239, 240,
242, vya Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai Namb. 7 ya 2004 hakifuatwi
katika kuteua wazee wa Mahkama na wengine hawana uwezo wa kusoma.(23) Uteuzi wa Majaji:Inashauriwa kwamba mawakili wakazingatiwa katika
uteuzi wa majaji wa Mahkama Kuu ili kupatikana watendaji wazuri wa kutoa
haki.
(24) Kuondoshwa kazini mahakimu:Utafiti unaonyesha kwamba baadhi yamahakimu waliondoshwa kazini kwa visingizio vya siasa.
(25) Imani ndogo ya wananchi kwa Mahkama:Utafiti umeonyesha kwambawananchi wa Zanzibar wana imani ndogo ya uwezo na uadilifu wa baadhi yawatendaji wa Mahkama na wanasikika wakisema kwamba haki itapatikana
Mahkama ya Rufaa ya Tanzania na Haki haipatikani Mahkama za
Zanzibar
(26) Vifaa vya kisasa vya teknolojia katika shughuli za Mahkama.Hitimisho
Yaliyoelezwa katika mada hii ni machache kati ya mafanikio na changamoto za
Mahkama. Mafanikio na changamoto nyengine zitaelezwa na washiriki. Ni muhimu
Mahkama ikawa makini kusikiliza hususan changamoto ili kuzifanyia kazi kwa
madhumuni ya kufanikisha utendaji wa haki. Maoni yatakayotolewa na washirikiyasitumike kama daraja la kujenga chuki baina ya washika dau wa sekta ya Sheria.
Inawezekana baadhi ya mafanikio na changamoto zimesababishwa na Sheria ziliopo.Uongozi wa Mahkama ujitahidi kuboresha baadhi ya mambo na kushinikiza
kuongezwa zaidi bajeti ya Mahkama ambayo imekuwa kikwazo cha utendaji haki
hapa Zanzibar.