MEM 100 Online

11
Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali kwa ajili ya News Bullettin hii ya Wizara ya Nishati na Madini Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected] HABARI ZA NISHATI &MADINI Toleo No. 100 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Desemba 31, 2015 - Januari 6, 2016 Bulletin News http://www.mem.go.tz Soma habari Uk. 2 Kampuni itakayohusika na rushwa kunyimwa kazi Katibu Mkuu MEM ni Prof. Justus Ntalikwa n Manaibu ni Prof. James Mdoe na Dkt. Paulina Pallangyo Prof. James Mdoe Prof. Justus Ntalikwa

description

JARIDA LA WIZARA YA NISHATI NA MADINI TOLEO LA 100

Transcript of MEM 100 Online

Page 1: MEM 100 Online

Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali kwa ajili ya News Bullettin hii ya Wizara ya Nishati na Madini

Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]

Habari za nisHati &madini

Toleo No. 100 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Desemba 31, 2015 - Januari 6, 2016

BulletinNews

Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizara ya Nishati na Madini

Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]

http://www.mem.go.tz

HABARI ZA NISHATI &MADINI

Toleo No. 51 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Tarehe - 23-29 Januari , 2015

JWTZ wapongezwa kunusuru mtambo wa Msimbati-Uk4

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, anayeshughulikia Madini Stephen Masele

Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Charles Kitwanga

Mkurugenzi Mtend-aji wa TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba

Mkurugenzi Mkuu wa REA, Dk. Lutengano Mwakahesya

Wabunge Soma habari Uk. 2

Waimwagia sifa MEM, TANESCO, REA

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AZINDUA RASMI BODI YA TANESCO -Uk2

Soma habari

Uk. 2Kampuni itakayohusika na rushwa kunyimwa kazi

Katibu Mkuu MEM ni Prof. Justus Ntalikwan Manaibu ni Prof. James Mdoe

na Dkt. Paulina Pallangyo

Prof. James Mdoe Prof. Justus Ntalikwa

Page 2: MEM 100 Online

2 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

Na Mohamed Saif

Serikali imesema Kampuni za kusambaza umeme vijijini zitakazobainika kujihusisha na vitendo vya rushwa na unyanyasaji kwa wananchi

zitachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kunyimwa zabuni kwa miradi itakayofuata.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alisema hayo hivi karibuni katika kikao chake na kampuni ya Urban and Rural Engineering Services (UR) inayotekeleza mradi wa usambazaji umeme katika mkoa wa Kagera.

“Tulipitisha azimio kuwa kampuni yoyote itakayobainika kuhusika na

rushwa ama vitendo vya unyanyasaji haitopewa tena kazi katika miradi ijayo,” alisema.

Agizo hilo linafuatia malalamiko kutoka kwa Mbunge wa Karagwe, Innocent Bashungwa pamoja na baadhi ya madiwani wa wilaya hiyo ambao walimueleza Waziri Muhongo kuwa miradi ya umeme vijijini wilayani humo imegubikwa na vitendo vya rushwa ambavyo vimesababisha maeneo yaliyokusudiwa kukosa huduma.

Bashungwa alisema kukithiri kwa vitendo vya rushwa miongoni mwa wafanyakazi wa kampuni hiyo, kumesababisha mradi huo kutekelezwa nje ya maeneo yaliyokusudiwa.

Mbunge huyo alisema kuwa baadhi ya wananchi katika wilaya ya Karagwe wanafungiwa umeme wa

REA kwa bei ya juu na huku wengine wakicheleweshwa kuunganishiwa hadi watoe rushwa.

Vilevile, ilielezwa kuwa baadhi ya maeneo ya vijiji vya Nyakayanja na Nyaishozi vya Karagwe kuna baadhi ya wananchi ambao walifungiwa mita na baadaye kuondolewa bila maelezo yoyote.

Kwa upande wake Mratibu wa mradi huo kutoka kampuni ya UR, Mhandisi Julius Kateti alikiri kuwepo kwa tuhuma za rushwa kwa wafanyakazi wake na kwamba alikwishaanza kuchukua hatua.

Alisema hadi sasa kampuni hiyo imewafukuza wafanyakazi 32 baada ya kuletewa malalamiko na wananchi na viongozi wa maeneo husika.

Aliongeza kwamba Kampuni inapata chamgamoto kubwa ya kusimamia mradi huo kwani wafanyakazi wengi wanatoka maeneo ya vijiji ambavyo miradi inafanyika na kwamba wamekuwa wakipita mitaani kwa kushirikiana na baadhi ya viongozi wa vijiji kuchangisha fedha kwa wananchi ili wapatiwe huduma.

Baada ya kusikiliza pande zote

mbili, Waziri Muhongo aliagiza kifanyike kikao mjini Bukoba tarehe 30 mwezi huu chini ya uenyekiti wa Mkuu wa Mkoa wa Kagera na kushirikisha Mbunge na madiwani hao, REA na TANESCO ili kujadili suala hilo.

Vilevile Profesa Muhongo aliagiza REA ifanye tathmini ya maeneo yote yaliyo katika wigo wa kupewa umeme ili kuona kama mkandarasi amefanya kazi kama ilivyo katika mkataba wake.

Mbali na hilo, Profesa Muhongo aliagiza vyombo vya dola ikiwemo Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kufuatilia tuhuma hizo ili hatua stahiki zichukuliwe.

Waziri Muhongo aliiagiza TANESCO kutoa Elimu kwa wananchi wa

Mkoa wa Kagera kuanzia tarehe 30 mwezi Disemba kwa kushirikiana na madiwani kuhusu masuala ya taratibu za kupata umeme na gharama za kuunganishiwa huduma hiyo.

Profesa Muhongo alitoa wito kwa wananchi ambao hawapo kwenye wigo kuwa wavumilivu wakisubiri awamu nyingine itakayofuata.

Kampuni itakayohusika na rushwa kunyimwa kazi

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akisikiliza malalamiko ya Madiwani wa wilaya ya Karagwe kuhusu tuhuma za rushwa zinazohusisha wafanyakazi wa kampuni ya Urban and Rural Engineering Services (UR). Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, John Mongella.

Mbunge wa Karagwe, Innocent Bashungwa (kushoto) akizungumzia malalamiko ya wananchi wa wilaya ya Karagwe kuhusiana na tuhuma za rushwa zinazowakabili wafanyakazi wa kampuni ya Urban and Rural Engineering Services (UR).

Na Asteria Muhozya

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu

katika Wizara mbalimbali tarehe 30 Disemba, 2015. Katika uteuzi huo, Rais Magufuli amemteua Prof. Justus W. Ntalikwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini ambaye anachukua nafasi ya Mhandisi Omar Chambo aliyekuwa Katibu Mkuu.

Kabla ya uteuzi huo, Profesa Ntalikwa alikuwa Mkuu wa Chuo cha Sayansi ya Dunia- (Jiolojia, Mafuta pamoja na Gesi Asilia) (Earth Sciences) katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM). Vilevile Prof. Ntalikwa ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST).

Akizungumza na MEM Bulletin katika mahojiano mafupi kuhusu uteuzi huo, Prof. Ntalikwa, ameeleza kuwa, ameupokea vizuri na kwamba anatarajia kutumia uzoefu na taaluma yake kusimamia utekelezaji wa majukumu

ya Sekta za Nishati na Madini kwa ufanisi.

Aidha, wengine walioteuliwa ni Prof. James Epifania Mdoe, na Dkt. Paulina Pallangyo ambao wanachukua nafasi ya Naibu Katibu Mkuu ambayo awali ilikuwa ikishikiliwa na Mhandisi Paul Masanja.

Kabla ya uteuzi huo, Prof. Msofe alikuwa Mkuu wa Idara ya Kemia, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (USDM). Makatibu hao wanatarajiwa kuapishwa rasmi kushika nyadhifa hizo Januari 1, 2016.

Katibu Mkuu MEM ni Prof. Justus Ntalikwa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli

Page 3: MEM 100 Online

3BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

TOLEO MAALUM ZIARA YA PROF. MUHONGO KANDA YA ZIWA

TahaririMEM

Na Badra Masoud

Five Pillars oF reForms

KWa HaBari PiGa simU KitenGo cHa maWasiliano

Bodi ya uhariri

MharIrI Mkuu: Badra MasoudMsaNIfu: Lucas Gordon

WaaNDIshI: Veronica simba, asteria Muhozya, Greyson Mwase Teresia Mhagama, Mohamed saif, rhoda James ,

Nuru Mwasampeta na Zuena Msuya

increase eFFiciencyQUality delivery

oF Goods/service

satisFaction oF tHe client

satisFaction oF BUsiness Partners

satisFaction oF sHareHolders

tel-2110490FaX-2110389

moB-0732999263

Tusherehekee Mwaka Mpya umeme ukiwaka!!

tel-2110490FaX-2110389

moB-0732999263

Profesa Muhongo aibana TANESCO

Ijumaa Januari 1, 2016 ni siku ambayo Watanzania na watu wote ulimwenguni wanaungana kwa pamoja kusherehekea Sikukuu ya kuuaga mwaka 2015 na kuukaribisha mwaka 2016.

Kwa hakika Sikukuu hii ni kubwa hivyo, Watanzania na watu wengine duniani wana kila sababu ya kusherehekea kwa amani na furaha sikukuu hiyo. Hivyo, ili kutimia kwa sherehe hizo, hakuna asiyelewa moja ya huduma muhimu kukamilisha Sikukuu hiyo ni upatikanaji wa huduma ya umeme.

Umeme huleta furaha, na inapotokea umeme kukatika ghafla nyakati za usiku wakati ambapo familia au kundi la watu wanaangalia TV, utasikia wakitoa sauti za masikitiko na unapowaka wanashangilia huku wakipiga kelele.

Kwa dalili hizo ni wazi kwamba katika Sikukuu hii ya kuukaribisha mwaka 2016 kwa namna moja ama nyingine huduma ya umeme ni kichocheo kikubwa katika kufanikisha shamra shamra na pia kuhakikisha usalama.

Mwaka Mpya ambao husherehekewa nyakati za usiku katika maeneo mbalimbali nchini ambapo maeneo hayo yote huhitaji mwanga wa taa ili watu wote wapate kusherehekea kwa amani mwanzo hadi mwisho wa sherehe hizo.

Hayo ni maeneo machache tu niliyoyataja ambayo yanaonyesha umuhimu wa umeme bila kusahau majumbani ambapo huko ndiyo familia hukutana kwa ajili ya kusherehea.

Sababu hizo ndizo zinazopelekea kuonyesha kwamba Wizara ya Nishati na Madini na TANESCO wana dhamana kubwa waliyoibeba katika kuhakikisha kwamba Watanzania wanapata huduma hiyo ya umeme; Hii ni kusema kwamba wahusika hawana budi kuhakikisha umeme unapatikana katika kipindi chote cha Sikukuu.

Hivyo hivyo, tunatambua na kuheshimu agizo la Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kuwazuia Watendaji wa Wizara na TANESCO kwenda likizo katika kipindi hiki cha Sikukuu.

Tunaamini kwamba Prof. Muhongo ana nia njema na kuwajali sana Watanzania ndiyo maana ameamua kupigana kufa na kupona kuhakikisha tatizo la umeme na tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara linakoma na hasa katika kipindi hiki cha Sikukuu.

Bila kusahau kwamba Prof. Muhongo ameamua yeye kutokusherehekea Mwaka Mpya kwa kuendelea na ziara za kukagua vituo vya kuzalisha umeme na ofisi za kutoa huduma za TANESCO ambapo kwa sasa yupo Kanda ya Ziwa ambapo pia anakutana na Wachimbaji wadogo wa madini wa Kanda hiyo.

Tunasema Prof. Muhongo songambele, Watanzania wanaelewa vema dhamira yako ya kizalendo katika kuhakikisha kuwa umeme wa kutosha, uhakika na wa bei nafuu unapatikana ili nchi yetu iweze kuwa katika kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.

Na Mohamed Saif

Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) limeagizwa kuhakikisha hadi kufikia tarehe 3 Januari 2016 liwe limekamilisha kufunga umeme kwenye Jengo la

Ofisi za Serikali la Mpakani mwa Tanzania na Rwanda (One Stop Border post) lililopo eneo la Rusumo wilayani Ngara.

Agizo hilo limetolewa jana na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alipofanya ziara kwenye Mpaka wa Tanzania na Rwanda kwa ajili ya kukagua maendeleo ya mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia maji wa Rusumo.

Akizungumza katika ziara hiyo, Afisa Mfawidhi wa Kituo cha Forodha cha Rusumo, Laurent Gabriel alisema umeme kwenye jengo hilo umekuwa ukikatika mara kwa mara na hivyo kusababisha usumbufu kwa wananchi wanaohitaji huduma kwenye Ofisi zilizopo katika jengo hilo.

Gabriel aliendelea kueleza kuwa kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliwa na matatizo ya kukatika mara kwa mara kwa umeme na pia kukosekana kwa huduma ya mtandao wa kununua umeme kutoka nchini Rwanda.

Aidha, Profesa Muhongo alizungumza

na wananchi wanaoishi maeneo ya mpakani hapo na walimueleza kusikitishwa kwao kuona jengo hilo linatumia umeme kutoka nchi jirani ambao hata hivyo walisema umekuwa ukikatika mara kwa mara na hivyo kusababisha shughuli nyingi za Serikali kukwama.

Baada ya kuelezwa taarifa hiyo, Profesa Muhongo alisema jambo hilo halikubaliki kwani tayari umeme wa Tanesco umefika kwenye eneo hilo hivyo aliiagiza TANESCO kuharakisha uunganishaji wa huduma ya umeme kwenye jengo hilo.

“Haileti maana kutumia umeme kutoka nchini Rwanda wakati Tanesco wanao umeme ambao tayari umefika mpakani hapa. TANESCO hakikisheni kufikia Jumapili ijayo (tarehe 3 Januari, 2016) jengo hili liwe limeunganishwa na umeme,” aliagiza.

Waziri Muhongo alimuelekeza Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Honorata Chitanda kufuatilia suala hilo kwa ukaribu ili ifikapo tarehe hiyo umeme uwe umefungwa kwenye jengo hilo.

Ziara hiyo ya Profesa Muhongo ni muendelezo wa ziara za kukagua mitambo na miundombinu ya umeme nchini ambapo kwa sasa yupo Mkoani Kagera na tayari amekamilisha kutembelea miradi ya umeme iliyopo maeneo ya Mikoa ya Kusini, Kaskazini, Kati na Kanda ya Ziwa.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alipotembelea eneo la Maporomoko ya Maji ya Mto Rusumo

Page 4: MEM 100 Online

4 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

TOLEO MAALUM ZIARA YA PROF. MUHONGO KANDA YA ZIWA

Kagera kuunganishwa Gridi ya TaifaNa Mohamed Seif, Bukoba

Serikali imesema ifikapo mwaka 2018 Mfumo wa umeme katika Mkoa wa Kagera utakua umeingizwa kwenye Gridi ya Taifa.

Hayo yalisemwa hivi karibuni na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alipofanya ziara mjini Bukoba, Mkoani Kagera ili kukagua miundombinu ya umeme.

Ilielezwa kwamba Mkoa huo kwa sasa unapata umeme kutoka nchini Uganda ambao umekuwa ukikatika mara kwa mara na hivyo kulilazimu Shirika la Umeme (TANESCO) kutumia mitambo yake inayotumia mafuta ambayo hata hivyo haikidhi mahitaji ya umeme ya Mkoa.

Profesa Muhongo aliliagiza shirika hilo kuhakikisha linaharakisha taratibu za kuunganisha mkoa wa Kagera kwenye umeme wa Gridi ya Taifa.

“TANESCO ni lazima muharakishe mipango ya kuunganisha mkoa huu kwenye gridi ya taifa ili kuwapatia wananchi huduma ya umeme wa uhakika,” aliagiza.

Aidha, Profesa Muhongo aliiagiza TANESCO kuhakikisha mafuta ya kuendeshea mitambo hiyo yanakuwepo yakutosha kwa muda wote.

Alisema ifikapo mwaka 2025, Tanzania itaingia kwenye uchumi wa kati ambao utatokana na uwekezaji mkubwa kwenye viwanda ambavyo vitahitaji umeme wa kutosha na uhakika.

Mbali na hilo, Profesa Muhongo aliliagiza Shirika la Tanesco mara baada ya mkataba uliopo wa kuuziana umeme kati ya Tanzania na Uganda kuisha, wahakikishe wanaingia mkataba wa muda mfupi lengo likiwa ni kuepusha kuwa ndani ya mkataba wakati tayari mkoa huo utakua kwenye gridi ya taifa.

Akielezea hali ya umeme mkoani humo, Meneja wa Tanesco Kanda ya Ziwa, Mhandisi Amos Maganga alisema kwa sasa Tanzania inanunua umeme kwa gharama ya senti za Marekani 8.4 kwa kila yuniti.

Alisema Tanzania inao mkataba wa kununua umeme kutoka Uganda kiasi cha megawati 10 ambao unahudumia wilaya za Bukoba Mjini na Vijijini, Karagwe, Muleba na Misenyi.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akimsikiliza Mhandisi wa kituo cha kufua umeme wa dharura cha Kibeta- Bukoba mjini, Mhandisi Filbert Mlaki wakati wa ziara yake kituoni hapo . Kituo hicho chenye mitambo minne, kina uwezo wa kuzalisha megawati 2.1 ambao hutumiwa pale umeme wa kutoka Uganda unapokatika.

Waziri wa nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akikagua moja ya mtambo wa kuzalisha umeme wa Kituo cha Kibeta

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa pili kushoto) akimsikiliza Mhandisi Filbert Mlaki.

Moja ya mtambo wa kuzalisha umeme katika kituo cha kufua umeme wa dharura cha Kibeta- Bukoba mjini.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Kagera, John Mongella kabla ya kuanza ziara ya kukagua miundombinu ya umeme mkoani humo.

Page 5: MEM 100 Online

5BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

TOLEO MAALUM ZIARA YA PROF. MUHONGO KANDA YA ZIWA

Na Mohamed Saif

Wananchi wa Kijiji cha Nyarukongora, Kata ya Biharamulo mjini w a m e m p o n g e z a Waziri wa Nishati na

Madini, Profesa Sospeter Muhongo kwa namna anavyoshughulikia matatizo ya umeme nchini na kwamba ni mfano wa kuigwa kwa viongozi wengine.

Pongezi hizo zimetolewa juzi katika mkutano wake na wananchi wa kijiji hicho ambapo walimpongeza kwa juhudi zake za kutafuta suluhisho la matatizo ya umeme nchini.

Katika mkutano huo, wananchi hao pia walililalamikia Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) kwa kushindwa kupeleka huduma ya umeme kijijini hapo.

Walieleza kwamba waliwasilisha maombi ya kusambaziwa umeme kwenye Ofisi za Tanesco Biharamulo lakini hadi hivi sasa hakuna kilichofanyika kijijini hapo.

Kufuatia malalamiko hayo, Waziri Muhongo aliliagiza shirika hilo, Ofisi ya Biharamulo kuwa kufikia tarehe 2 Januari wawe na jawabu la lini watapeleka huduma hiyo kijijini hapo.

“Ikifika tarehe 2 mwezi Januari, mpeleke taarifa kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kumueleza ni lini mtaanza ujenzi wa miundombinu ya kusambaza umeme kwenye kijiji hiki,” aliagiza.

Profesa Muhongo alisema Tanesco hawapaswi kukaa kusubiri wateja badala yake wanatakiwa kutafuta wananchi wenye mahitaji ya umeme ili wapelekewe

huduma. “Nyinyi mnatafuta fedha sasa ni kwanini mnachukua muda mrefu kuwaunganisha wanaohitaji huduma; tulikubaliana nyinyi mnapaswa kutafuta wateja sio wateja wawatafute nyinyi,” alisema.

Aliwataka watendaji wa shirika hilo kuacha tabia ya kufanya kazi kwa mazoea kwa kukaa ofisini wakati wapo wananchi ambao wanahitaji huduma ya nishati ya umeme na ambao wapo tayari kulipia gharama zinazohitajika kwa ajili ya kuunganishwa na huduma husika.

Akizungumza kwenye mkutano huo, Diwani wa Kata ya Biharamulo

mjini, David Mnyankunda alimshukuru Profesa Muhongo kwa kutembelea kijiji hicho na kumueleza kuwa wananchi wengi kijijini hapo wapo tayari kuunganishiwa umeme na vilevile wamejiandaa kulipia gharama inayohitajika kwa ajili ya kuunganishwa.

“Tunayo imani kubwa kwamba ujio wako hapa kwetu tatizo la umeme hapa kijijini litakuwa historia. Tumeshuhudia utendaji wako na namna ambavyo umekua ukitatua kero mbalimbali za wananchi kwenye masuala ya umeme,” alisema.

Aidha, Profesa Muhongo alitembelea Kituo cha Kuzalisha umeme kwa mafuta cha Biharamulo chenye uwezo wa kuzalisha megawati 1.4 na pia alikagua ujenzi wa miundombinu ya mradi wa kuzalisha umeme wa megawati 2.5 unaojengwa wilayani humo.

Waziri Muhongo aliwaagiza Tanesco kuhakikisha wanasimamia mradi huo kwa karibu na kwa umakini ili ukamilike ndani ya muda uliokusudiwa na vilevile aliwakumbusha watendaji wa shirika hilo kuwa ifikapo tarehe 15 mwezi ujao maombi yote ya zamani ya kuunganishiwa umeme yawe yamefanyiwa kazi vinginevyo wajiandae kuacha ama kuachishwa kazi.

Naye Meneja wa Tanesco Kanda ya Ziwa, Mhandisi Amos Maganga alimuhakikishia Waziri Muhongo kuwa atasimamia vema na kwa karibu utekelezaji wa maagizo yake na kueleza kwamba hatoruhusu utendaji mbovu wa watendaji walio chini yake.

Na Mohamed Saif

Ofisi ya Afisa Madini Mkazi Bukoba imeagizwa kugawa maeneo ya uchimbaji kwa wachimbaji wadogo wa madini ya Bati

(Tin) katika wilaya ya Kyerwa.Agizo hilo limetolewa hivi karibuni

wilayani Kyerwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alipofanya ziara katika maeneo ya uchimbaji madini ya bati na kuzungumza na wachimbaji wadogo kwenye maeneo hayo.

Awali wachimbaji hao walimueleza Waziri Muhongo kwamba wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa maeneo ya uchimbaji ambapo walisema kwa sasa wanafanya shughuli hiyo ya uchimbaji wa madini katika maeneo yasiyokuwa yao.

Walitaja changamoto nyingine kuwa ni ukosefu wa vifaa vya kisasa kwa ajili ya uchimbaji, gharama kubwa za kuendesha shughuli za uchimbaji hasa upatikanaji wa maji na kutokuwa na soko la uhakika.

Kufuatia maelezo hayo, Profesa Muhongo alimuagiza Afisa Madini Mkazi Ofisi ya Bukoba, Ally Ally kueleza ni vipi Ofisi yake imejipanga kuhakikisha inatatua changamoto zinazowakabili wachimbaji hao

ambapo Afisa Madini huyo alieleza kwamba vipo viwanja 40 na kingine kimoja chenye ukubwa wa kilomita za mraba 71.

Profesa Muhongo aliagiza maeneo hayo yagawiwe kwa wachimbaji wadogo na kumuagiza Afisa huyo kuharakisha kukutana na wachimbaji ili kuwaonesha na kukubaliana kuhusu maeneo hayo.

Mbali na hilo, waziri Muhongo aliagiza Wakala wa Madini Tanzania (GST) kufanya utafiti wa awali katika maeneo hayo ili kubaini kiwango cha madini ya Bati kilichopo kwenye maeneo hayo lengo likiwa ni kuwarahisishia wachimbaji hao kuchimba kwenye maeneo yenye madini na siyo kubahatisha.

Profesa Muhongo alisema hakutakuwa na gharama yoyote ya utafiti na hivyo kuwataka wachimbaji hao kutoa ushirikiano kwa watafiti hao pamoja na kusaidia kulinda vifaa vitakavyotumika katika utafiti.

“Msikae kama watu waliopotea; GST watakuja hapa wiki ijayo na kuanza utafiti kwa kipindi kisichopungua mwezi mmoja; hamtolipia gharama ya utafiti; mnachotakiwa kufanya ni kuwapa ushirikiano katika kipindi chote cha utafiti,” alisema.

Akizungumzia suala la soko na bei ya madini hayo, Profesa Muhongo alisema Serikali kupitia Shirika la Madini la Taifa

(STAMICO) imeanzisha kampuni tanzu ya Kyerwa Tin Company Limited (KTCL) maalum kwa ajili ya kununua madini ya bati.

Alisema kampuni hiyo ya KTCL itanunua madini hayo kwa bei nzuri ya ushindani lengo likiwa ni kuwakomboa wachimbaji hao kuondokana na uhaba wa soko na vilevile kuzuia utoroshwaji

wa madini hayo nchi jirani.Profesa Muhongo aliwasihi

wachimbaji hao kuwa wazalendo na vilevile aliagiza Ofisi za kampuni hiyo ya KTCL kuwa wazi siku zote ili kuwaondolea usumbufu wachimbaji. “Kampuni hii itanunua madini yenu kwa bei ya ushindani; kwahiyo hakuna sababu ya nyinyi kutorosha madini,” alisema.

Vilevile waziri Muhongo aliiagiza STAMICO kufanya haraka kuanzisha Kituo cha Uchenjuaji madini kwenye eneo hilo ambapo ilielezwa kuwa ifikapo tarehe 1 Juni mwakani, kituo husika kitaanza kazi.

Profesa Muhongo aagiza wachimbaji wa madini ya bati wapewe maeneo

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akizungumza na wachimbaji wadogo wa Bati wa wilaya ya Kyerwa. Wa kwanza kushoto ni Afisa Madini Mkazi Ofisi ya Bukoba, Ally Ally.

Biharamulo wamkubali Profesa Muhongo

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akizungumza na baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Nyarukongora, Kata ya Biharamulo mjini.

Page 6: MEM 100 Online

6 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

TOLEO MAALUM ZIARA YA PROF. MUHONGO KANDA YA ZIWA

Na Mohamed Saif

Serikali imeagiza kumalizika haraka kwa majadiliano ya usambazaji umeme katika Kata ya Murongo wilayani Kyerwa.

Agizo hilo limetolewa hivi karibuni na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alipofanya mazungumzo na wananchi waishio maeneo hayo.

Kwa nyakati tofauti wananchi wa kata hiyo walimueleza Profesa Muhongo kwamba ni takriban mwaka mmoja sasa hawajawashiwa umeme tangu nyumba zao zimefungiwa mita za umeme na Kampuni ya binafsi ya Armstone.

Akizungumza katika mkutano huo, Diwani wa Kata ya Murongo, Sevelini Bugaha alisema shughuli nyingi za kiuchumi zinasuasua kutokana na

kukosekana kwa huduma ya nishati ya umeme.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Armstone, Josephat Lujara alisema kuwa kampuni yake ilipaswa kusambaza umeme Murongo lakini kumekuwepo na mvutano wa muda mrefu na Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) kuhusiana na usambazaji wa umeme kwenye eneo hilo.

Kufuatia maelezo hayo, Waziri Muhongo alielekeza suala la usambazaji umeme katika kata hiyo litatuliwe haraka na hivyo aliagiza Wizara, Tanesco, Ewura na Kampuni ya Armstone wakutane kwa ajili ya kumaliza tatizo hilo.

Waziri Muhongo alisema endapo majadiliano hayo yatashindwa kuleta tija, Mkandarasi wa Umeme wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ambaye ana jukumu la kusambaza umeme mkoani

Wananchi wa Kata ya Murongo, wilaya ya Kyerwa wakimsikiliza Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani).

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akimsikiliza Diwani wa Kata ya Kyerwa, Sevelini Bugaha akizungumzia matatizo ya huduma ya umeme kwenye kata hiyo

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya kusambaza umeme ya Armstone, Josephat Lujara (kushoto) akieleza sababu za kuchelewa kwa mradi wa umeme Kata ya Murongo. Wa kwanza kulia ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, John Mongella.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akizungumza na wananchi wa Kata ya Murongo, wilaya ya Kyerwa.

Waziri muhongo atoa maelekezo KyerwaKagera asambaze katika eneo hilo.

“Wananchi wanachohitaji ni umeme, hatuwezi kusubiri mvutano kati ya hizi pande mbili wakati Watanzania wanateseka na shughuli zao nyingi zikikwama,” alisema.

Waziri Muhongo aliagiza mara baada ya majadiliano hayo ya kesho, usambazaji umeme uanzie kwenye taasisi ambazo ni shule, nyumba za ibada na vituo vya afya.

Akizungumzia mradi wa umeme vijijini, Profesa Muhongo alisema ifikapo mwezi Julai mwakani Awamu ya Tatu ya mradi huo itaanza ambapo vijiji ambavyo havikupata umeme Awamu ya Pili vitaunganishiwa huduma hiyo. “Tunatarajia kufikia Awamu ya Tano ya Mradi vijiji vyote nchini vitakua vimeunganishwa na umeme,” alisema.

Akizungumzia utekelezaji wa mradi wa umeme vijijini kwa mkoa wa Kagera, Mkandarasi kutoka kampuni ya Urban and Rural Engineering Services Limited (UR), Mhandisi Julius Kateti alisema kampuni yake ipo tayari kusambaza umeme katika kata hiyo ya Murongo na kwamba shughuli hiyo itachukua siku kumi kukamilika.

Page 7: MEM 100 Online

7BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

TOLEO MAALUM ZIARA YA PROF. MUHONGO KANDA YA ZIWA

Na Mohamed Seif

Mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Nishati

na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ameanza kwa kishindo kutekeleza ahadi zake kwa wananchi wa jimbo hilo na huku akiahidi maendeleo kwa kasi zaidi.

Profesa Muhongo alidhihirisha hayo juzi katika kijiji cha Murangi, mkoani Mara katika kikao chake na baadhi ya wananchi wa jimbo hilo, watendaji wa Halmashauri ya Musoma vijijini na madiwani huku lengo la kikao likiwa ni kujadili mipango na miradi ya uchumi na maendeleo ya jimbo hilo.

Katika kikao hicho, iliazimiwa kuanzishwe Mfuko wa Elimu wa Jimbo ambapo Profesa Muhongo aliahidi kutoa kiasi cha Shilingi Milioni mia moja ambazo atakopeshwa na Bunge kwa ajili ya kununulia gari.

Alisema badala ya kununulia gari, fedha hiyo

ataiingiza kwenye Mfuko huo ili kuleta maendeleo kwenye jimbo hilo. “Dhamira yangu ni kuhakikisha jimbo letu linasonga mbele kiuchumi na kimaendeleo na siyo maneno bila mipango madhubuti,” alisema.

Katika maelezo yake ya mikakati ya maendeleo kwa jimbo hilo, Profesa Muhongo alisema kufikia Mwezi Januari mwanzoni, ataanzisha Ofisi tano za Mbunge jimboni humo ili kufikisha huduma kwa wananchi kiurahisi.

Alisema Ofisi hizo zitakuwa na mtumishi mmoja ambaye ataajiriwa na Mbunge na atapatiwa vitendea kazi vya kuanzia ambavyo ni pikipiki ili kumuwezesha kuwafikia wananchi kirahisi na kompyuta mpakato (laptop) kwa ajili ya kutunza taarifa na mawasiliano.

Profesa Muhongo alitaja maeneo ambayo ofisi hizo zitaanzishwa kuwa ni kijiji cha Murangi ambapo ndio patakua makao makuu, Busekela, Sangana, Mugango na Nyegine na pia alitoa wito kwa vijana wa maeneo hayo kuomba kazi kwa nafasi husika

na kwamba watakaofaulu watatakiwa kuwepo maeneo hayo ili kila watakapohitajika waweze kupatikana kiurahisi.

Alisema usaili wa kuwapata watumishi hao utafanyika tarehe 26 na 27 mwezi huu na watakaofaulu wataanza kazi tarehe 1 Januari, 2016 kwa uangalizi wa kipindi cha miezi mitatu (probation period) na alitaja vigezo vitakavyotumika katika kuwapata kuwa ni elimu kuanzia kidato cha nne na ujuzi wa kompyuta.

Mbali na hilo, katika kuimarisha elimu jimboni humo, Profesa Muhongo ametoa vitabu vya kujifunzia vipatavyo 20,000 (elfu ishirini) katika shule mbalimbali na huku kipaumbele kwa wakati

huu ni kwa shule zilizofanya vibaya kwenye matokeo ya mwaka huu.

Alisema tayari ameagiza vitabu vingine 22,000 kutoka nchini Marekani na vitakapoingia nchini ameagiza Madiwani kuvisambaza kwenye shule ambazo hazina vitabu vya kutosha.

Mbunge huyo alisema kwa kutumia Mfuko huo wa Elimu wa Jimbo, pamoja na fedha za Halmashauri, kila shule itapatiwa huduma ya umeme, maji pamoja na kujenga na kukarabati shule hizo pamoja na nyumba za walimu.

Akizungumzia suala la miundombinu ya barabara, Mbunge huyo aliahidi kusimamia ujenzi wake ambapo

alisema barabara kutoka Musoma mjini hadi makao makuu ya jimbo itajengwa kwa kiwango cha lami na alisema tayari tathmini imeanza na itakamilika mwishoni mwa mwezi huu.

Mbali na hilo, kwa barabara zilizo chini ya Halmashauri, Profesa Muhongo aliagiza madiwani wakae na kupitisha bajeti kwa ajili ya kukarabati barabara hizo na aliagiza kikao hicho kifanyike kabla mwezi huu haujamalizika.

Kuhusu suala la Afya, Profesa Muhongo alisema tayari ameagiza gari la wagonjwa ambalo linatarajiwa kuingia nchini ndani ya wiki mbili zijazo.

Kikao hicho cha maendeleo ya jimbo la Musoma vijijini kilihudhuriwa na wadau mbalimbali wa maendeleo kutoka ndani na nje ya nchi miongoni mwao kukiwa na wazawa wa jimboni humo ambao kwa sasa wanaishi nje ya jimbo hilo na wageni kutoka Ujerumani.

Profesa muhongo: maendeleo ni kwa vitendo sio maneno

Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akizungumza jambo wakati wa kikao chake na wananchi wa jimbo hilo pamoja na wadau wa maendeleo.

Baadhi ya wananchi waliohudhuria Kikao cha Profesa Muhongo (hayupo pichani).

Page 8: MEM 100 Online

8 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

MAKALA

Na Veronica Simba

Moja ya mambo ambayo h u z u n g u m z w a na kujadiliwa kwa kiasi kikubwa hapa nchini ni mchango

unaotolewa na Kampuni za Madini kwa jamii, hususan zilizo jirani na Migodi inayomilikiwa na Kampuni hizo.

Hoja kuu ambayo hutawala mijadala hiyo ni iwapo Kampuni husika zinatoa mchango unaostahili katika kusaidia jamii zinazowazunguka kupitia miradi na huduma mbalimbali ambazo ni tofauti na tozo, ushuru, kodi na malipo mengine yoyote yanayolipwa kisheria kulingana na mikataba iliyoingiwa baina ya Migodi husika na Serikali.

Wapo wanaosema kwamba huduma au mchango unaotolewa na Kampuni za madini nchini siyo wa kiwango stahiki na wapo wanaoamini kwamba Kampuni husika zinasaidia jamii kwa kiwango kinachostahili.

Lengo la Makala hii siyo kuegemea upande wowote, isipokuwa kuangazia hoja ya msingi kuhusu Miradi ya Huduma kwa Jamii maarufu kama Corporate Social Responsibility kwa lugha ya kigeni au kwa kifupi CSR. Makala inaeleza maana halisi ya CSR ikiwa ni pamoja na nini hasa kinapaswa kufanywa na Kampuni za Madini katika kutekeleza utoaji huduma kwa jamii. Vilevile, Makala inamulika namna jamii husika zinavyoipokea miradi hiyo na kushiriki kwa upande wao katika kuhakikisha wanaboresha

hali zao kiuchumi na kijamii.Wakizungumza hivi karibuni

lakini kwa nyakati tofauti kuhusu Miradi ya Huduma kwa Jamii, hususan itolewayo na Kampuni za Madini nchini, Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kati – Magharibi, Humphrey Mmbando na Kamishna Msaidizi kutoka Ofisi ya Madini – Geita, Laurian Lwebembera walisema hakuna sheria inayowabana au kuelekeza Kampuni husika zitoe huduma kwa jamii kwa kiasi au kiwango gani.

Makamishna hawa wanakiri kuwa kuna kipengele katika Sera na Sheria ya Madini kinachoelekeza Migodi kutoa huduma kwa jamii lakini kipengele hicho hakielezi kiwango maalum kinachopaswa kutolewa.

“Ni vema wananchi wakafahamu kwamba huduma za jamii zinazotolewa na Kampuni za Madini ni kwa matakwa na utashi wa kampuni husika kwa ajili ya kujenga mahusiano mema na jamii zinazowazunguka, lakini hakuna sheria inayowabana kufanya hivyo kwa kiwango fulani maalum,” anafafanua Kamishna Lwebembera.

Kwa kuufahamu ukweli huo, sasa tuangazie huduma ambazo zimekuwa zikitolewa kwa jamii na baadhi ya Kampuni zinazomiliki Migodi mikubwa ya Madini hapa nchini ili kwa kuutumia ufahamu huo tuwe na msingi mzuri kuainisha iwapo huduma husika zinatolewa kwa kiwango stahiki ama la.

Hivi karibuni nilitembelea Migodi ya Madini ya Dhahabu ya Geita (Geita Gold Mine – GGM) unaomilikiwa na

Kampuni ya Anglo Gold Ashanti, Buzwagi - unaomikiwa na Kampuni ya Acacia pamoja na Mgodi wa Almasi wa Mwadui unaomikiwa na Kampuni ya Petra Diamonds.

Katika Migodi hiyo mitatu, huduma zinazotolewa kwa jamii kwa kiasi kikubwa zinashabihiana na hata maelezo kuhusu utaratibu unaotumika kuibua miradi husika pamoja na utaratibu unaotumika kutenga fedha za utekelezaji wake yanafanana kwa kiasi kikubwa.

Kwa ujumla, miradi mikubwa ya kijamii inayotekelezwa na Migodi hiyo ni pamoja na kuanzisha na kuwezesha vikundi vya ushonaji, kuchomelea vyuma (welding), kutengeneza matofali ya kisasa ambayo hupachikwa wakati wa ujenzi badala ya kutumia sementi na mchanga, vikundi vya ulimaji wa mbogamboga pamoja na vikundi vinavyojihusisha na kilimo cha mazao mbalimbali kama vile Mpunga na Alizeti.

Miradi mingine ni pamoja na ujenzi wa majengo ya shule mbalimbali sambamba na nyumba za Waalimu, Vituo vya Afya, Ofisi za Serikali hususan kwa ngazi ya Kata na Vijiji, Vituo vya kulelea watoto yatima, Barabara na Miradi ya maji safi.

Manase Ndoroma ni Meneja wa Miradi ya Jamii katika Mgodi wa Geita (GGM), unaomilikiwa na Kampuni ya Anglo Gold Ashanti. Akizungumzia utaratibu unaotumiwa na Kampuni yake katika kuibua na kutekeleza Miradi kwa jamii anasema zipo kanuni kuu sita zinazoongoza utendaji kazi katika Kampuni hiyo na mojawapo ni kuhakikisha majirani wanaozunguka Mgodi wananufaika.

Anasema, Kanuni hiyo inawaongoza katika kuhakikisha jamii inayozunguka Mgodi huo inanufaika kwa namna mbalimbali na kwamba kwa kawaida, Serikali ikiwa ni pamoja na Halmashauri za Vijiji husika hushirikishwa katika kuibua mawazo ya miradi inayofaa.

Maelezo ya Ndoroma kuhusiana na utaratibu unaotumika katika kuibua miradi ya jamii yanashahibiana kwa kiasi kikubwa na ya Ofisa Mahusiano kwa Jamii wa Mgodi wa Mwadui, Joseph Kaasa ambaye anasema wananchi husika wanashirikishwa

Kampuni za Madini na Miradi ya Kijamii

Mojawapo ya Barabara iliyojengwa kwa kiwango cha Lami kwa ufadhili wa Mgodi wa Buzwagi mjini Kahama. Barabara hii ipo Mtaa wa Nyahanga na ina urefu wa Kilomita 5.65

Ofisa Mahusiano kwa Jamii wa Mgodi wa Almasi wa Mwadui, Joseph Kaasa akionyesha moja ya nyumba za Walimu iliyojengwa kwa ufadhili wa Mgodi huo. Hapo ni katika Shule ya Msingi Idukilo iliyopo mkoani Shinyanga.

>>Inaendelea Uk. 9

Page 9: MEM 100 Online

9BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

MAKALA

moja kwa moja kupitia Kamati maalum iliyoundwa ikijumuisha Mwenyekiti, Mtendaji na Mwakilishi mmoja kutoka kila Kijiji katika Vijiji Nane (8) vinavyozunguka Mgodi husika.

Mathalani, Kaasa anasema mahitaji ambayo yameonekana kupewa kipaumbele na wananchi wa Vijiji vyote Nane ni suala la elimu. Anatoa mfano wa Kijiji kimojawapo cha Idukilo ambacho kilikuwa na Shule moja tu ya msingi. “Watoto kutoka pande zote za Kijiji husika walikuwa wakilazimika kutembea umbali wa Kilomita 10 kwenda katika shule hiyo iliyopo Makao Makuu ya Kijiji hicho. Kufuatia hali hiyo, wananchi wenyewe waliomba kujengewa Shule nyingine na tayari utekelezaji wake umeanza ambapo Shule inajengwa katika Kitongoji cha Musangombolwa,” anafafanua Kaasa.

Akifafanua zaidi, Ofisa huyo anayeshughulikia mahusiano ya jamii anasema inatarajiwa kuwa ifikapo mwezi Machi mwaka 2016 ujenzi utakuwa umekamilika kuwezesha madarasa ya kutosha kuingia wanafunzi 250 ambayo ndiyo idadi yao halisi mpaka sasa.

Naye, Antonia Kiondo ambaye ni Ofisa Mahusiano wa Mgodi wa Buzwagi hayuko tofauti sana na Maofisa wenzake kutoka Migodi ya Geita na Mwadui. Yeye pia anasisitiza kuwa wananchi wa Vijiji vinavyozunguka Mgodi huo ndiyo waamuzi wa Miradi ya Maendeleo inayopaswa kutekelezwa.

Antonia anataja miradi ambayo wananchi wamekuwa wakiipendekeza na ambayo Mgodi wa Buzwagi umekuwa ukiitekeleza kuwa ni pamoja na elimu,

miundombinu pamoja na kuwezesha vikundi vya kuwainua wananchi kiuchumi.

Nilipata pia fursa kuzungumza na baadhi ya wananchi hususan viongozi wa vikundi mbalimbali vilivyowezeshwa kuanzisha miradi ya kujiimarisha kiuchumi, Waalimu Wakuu wa Shule zinazopewa misaada na Migodi pamoja na Wasimamizi wa Vituo vya kulea watoto yatima vinavyofadhiliwa na Migodi hiyo.

Akizungumzia maendeleo ya Mradi wa Shamba la Mpunga linalomilikiwa na Kikundi cha Wakulima katika Kijiji cha Saragulwa mkoani Geita, Mwenyekiti wa Kikundi hicho, Bwana Yuda Ng’hindi anasema yeye na wanachama wenzake waliomba kuwezeshwa katika mradi huo kupitia mkutano wa kijiji ambapo Mgodi wa Geita ulikubali na utekelezaji wake ulianza kwa kujengewa mabwawa ya maji ambayo ilikuwa ni moja ya changamoto kubwa katika utekelezaji wa mradi husika.

Bwana Ng’hindi anaeleza kuwa walianza kupandikiza miche ya Mpunga katika Shamba hilo la Mfano ambalo kwa kuanzia linatumika kama Shamba Darasa. Anasema Shamba hilo lina ukubwa wa ekari Sita (6) ambazo kwa kilimo cha kawaida hupata mavuno ya Gunia 60 mpaka 70 za Mpunga “lakini kwa kilimo hiki cha kisasa tunaamini mavuno yatavuka Gunia 100.”

Naye Mwenyekiti wa Mauzo wa Kikundi cha Umoja wa Wafugaji Nyuki kilichopo Kata ya Mwendakulima katika Halmashauri ya Mji wa Kahama, Rehema Juma anaeleza mafanikio na Mradi huo mpaka sasa kuwa kwa msaada wa Mgodi wa Buzwagi, kikundi kimepata mafunzo ya ufugaji Nyuki

ambayo yamewasaidia kuweza kuendesha shughuli za ufugaji wa Nyuki kwa ubora zaidi, pamoja na kupatiwa Mizinga ya kufugia Nyuki 120 ya kawaida na 60 ya kisasa.

Mwingine ni Daktari Sam Phillip wa Kituo cha Afya Maganzo, Shinyanga. Yeye anasema kwa msaada wa Mgodi wa Mwadui, Kituo hicho kimepata huduma ya umeme pamoja na ujenzi wa majengo mbalimbali ikiwemo Wodi ya Watoto.

Hao ni baadhi tu ya wananchi walioeleza manufaa wanayoyapata kupitia Miradi ya Kijamii inayotolewa na Migodi ya Madini niliyoitaja. Hata hivyo kwa ujumla wake, pamoja na kubainisha changamoto kadhaa, wananchi hao wameonesha kufarijika na huduma hizo ambazo zinalenga kuboresha hali yao kiuchumi na hata huduma mbalimbali muhimu zikiwemo za afya na elimu.

Rai yangu kwa wananchi wanaozunguka Migodi na kupata huduma mbalimbali za kijamii ni kuhakikisha wanazitumia fursa hizo ipasavyo ili kuhakikisha wanajikwamua kiuchumi. Hawapaswi kubweteka kwa kudhani kuwa uwezeshwaji huo utakuwepo kwa muda wote, badala yake waweke bidii zaidi ili hata pale misaada itakapofikia mwisho kwa namna yoyote waweze kusimama wenyewe.

Tusiishie tu kulalama kuwa tunanyonywa na Kampuni za Madini na kwamba hazisaidii ipasavyo jamii zilizo jirani yake, bali kwa upande mwingine yatupasa tupime uwiano wa huduma za kijamii zinazotolewa na Kampuni husika na namna wananchi husika kwa upande wao wanavyozichangamkia kwa kutimiza wajibu wao na kuhakikisha wanashiriki kikamilifu kujiletea maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Shamba la kisasa la Mpunga lililopo katika Kijiji cha Saragulwa, Geita mjini. Lina ukubwa wa ekari Sita na linamilikiwa na Kikundi cha Wakulima kutoka Kijiji husika chini ya ufadhili wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita.

Kampuni za Madini na Miradi ya Kijamii

Profesa Muhongo: Umeme ni Injini ya UchumiNa Mohamed Saif

Serikali imesema inakaribisha wawekezaji wenye nia ya kuwekeza kwenye umeme wa gesi asilia nchini.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alitoa wito huo juzi katika muendelezo wa ziara yake ya kukagua miundombinu ya umeme Kanda ya Ziwa.

Waziri Muhongo alisema kampuni zenye nia ya kuwekeza kwenye uzalishaji wa umeme kwa kutumia gesi asilia zinakaribishwa kwani fursa za

uwekezaji kwenye sekta husika nchini ni nyingi.

Alisema wawekezaji wanakaribishwa kujenga mitambo ya kufua umeme kwenye maeneo mbalimbali ambapo kuna matoleo ya gesi asilia.

Aliyataja maeneo hayo yenye matoleo ya gesi asilia kuwa ni Mikoa ya Mtwara, Lindi katika kijiji cha Somangafungu wilayani Kilwa na vilevile Mkoa wa Pwani maeneo ya Bungu na Mkuranga.

“Shirika la Petroli Nchini (TPDC) wanayo gesi asilia ya kutosha kuzalisha umeme mwingi kwa hiyo kama kuna

Mtanzania anayetaka kuwekeza ajitokeze,” alisema.

Waziri Muhongo aliongeza kwamba Shirika la Umeme (TANESCO) watajenga njia ya kusafirisha umeme ya kilovoti 400 kutoka Kilwa hadi Dar es Salaam.

Akizungumzia chanzo kingine cha kuzalisha umeme cha makaa ya mawe, alisema sasa hivi ukaguzi unaanza wa kubaini fursa za uzalishaji wa umeme “Umeme ni injini ya uchumi,” alisema.

Aidha, alipokuwa Wilayani Chato, Profesa Muhongo alisema kwamba TANESCO wataanza kazi ya ujenzi wa kituo cha kupozea umeme (sub station)

katika wilaya hiyo ili kuongeza nguvu ya umeme wilayani humo.

Aliagiza kuwa TANESCO imsimamie Mkandarasi anayetekeleza umeme vijijini katika Wilaya hiyo ya Chato ili kuhakikisha anamaliza kazi yake ifikapo tarehe 31 mwezi Machi mwaka huu 2016.

Vilevile Profesa Muhongo alimuagiza Meneja wa TANESCO Kanda ya Ziwa, Mhandisi Amos Maganga pamoja na Mkandarasi wa umeme vijijini kukagua maeneo yote ambayo mkandarasi huyo alipewa kufanya kazi na kutoa taarifa kwa Mkuu wa Wilaya ya Chato.

>>Inatoka Uk. 8

Page 10: MEM 100 Online

10 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

 

Maonesho ya 5 ya Kimataifa ya Vito ya Arusha yenye aina mbalimbali za vito zikiwemo

Tanzanite , Ruby, Sapphire , Tsavori te , Rhodol i te , Spessart i te , Tourmaline,

Chrysobery l na Almasi yanatarajiwa kuvutia

Zaidi ya kampuni 100 za wafanyabiashara na wachimbaji madini ya Vito kutoka Tanzania na

nchi zingine za Afrika Mashariki, Kati na Kusini; na zaidi ya wanunuzi 500 kutoka zaidi ya nchi 25

ulimwenguni

Jisajili na Ushiriki Sasa!!!

Wasiliana na: Kamati ya Maandalizi AGF Simu: +255 784352299 or +255 767106773

Barua pepe: [email protected]

:ama Ofisi za Madini za Kanda

Yameandaliwa na Wizara ya Nishati na Madini

kwa kushirikiana na Chama cha Wafanyabiashara wa Madini (TAMIDA)

Prof. muhongo awaasa madiwani kuwatumikia wananchiNa Mohamed Saif

Mbunge wa Musoma Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ameapa

kwenda sambamba na Halmashauri ya Musoma Vijijini pamoja na Madiwani.

Alisema hayo juzi katika kijiji cha Murangi, Mkoani Mara kwenye kikao chake na wananchi wa jimbo hilo, wadau wa maendeleo na watendaji wa Halmashauri husika.

Alisema wananchi wanalalamika kuwa hadi asilimia 90 ya mapato ya Halmashauri yanapotea na huku miradi mingi ya maendeleo ikisimama kwa kukosa fedha.

Profesa Muhongo alibainisha kuwa ameviomba vyombo vya Dola ikiwemo Ofisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuchunguza Halmashauri ya Musoma Vijijini, Madiwani wote wa jimboni humo na wafanyakazi wa Halmashauri hiyo.

“Michezo iliyokuwa ikifanyika zamani ya ubadhirifu wa mapato inabidi muache mara moja; siwafichi nimeomba msaada wa vyombo vya dola kuwachunguza,” alisema.

Alisisitiza kwamba endapo kuna fedha inayopaswa kurudi kwa ajili ya kufanya maendeleo irudishwe haraka vinginevyo hatua za kisheria

zitachukuliwa dhidi ya wote wanaokwamisha miradi ya jimbo hilo.

Aliagiza kuwa tenda zote za Halmashauri pamoja na mapato yawekwe wazi ili kunufaisha wananchi. “Tenda zote za Halmashauri ziwekwe wazi, tusijekulaumiana huko tuendako,” alionya.

Aidha, Profesa Muhongo alitumia kikao hicho kuwaasa wananchi wa Musoma Vijijini kuepukana na ukabila. “Sisi wote masikini, halafu mtu anataka kuleta ukabila, hilo halifai, hatuwezi kuliacha liote mizizi,” alisema.

Akizungumzia nafasi yake ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Muhongo alisema ameteuliwa kwa uchapakazi na sio kwa ukabila na kwamba kipaumbele ambacho yeye binafsi siku zote anakitumia ni uchapakazi na uadilifu na sio suala la ukabila wala upendeleo.

Alisema matatizo yaliyo chelewesha maendeleo jimboni humo ni pamoja na ukabila na hivyo aliwaasa wananchi kuepukana na suala hilo. “Ukiona mtu anazungumzia masuala ya ukabila huyo hatufai, yatupasa sote kwa pamoja tumuepuke maana hana nia njema na maendeleo yetu,” alisema.

Alisema wenye fikra finyu za kiutendaji ndio wanaokimbilia ukabila na rushwa na hivyo kuweka wazi kwamba suala hilo hatoliruhusu na atalikemea kila inapobidi kwa manufaa ya wananchi wote.

Page 11: MEM 100 Online

11BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini

 

ADVERTISEMENTAPPOINTMENT OF DIRECTORS TO CONSTITUTE THE BOARD OF DIRECTORS OF STAMICO

The desire to appoint a Competent Board of Directors The Ministry of Energy and Minerals (MEM) of the Government of the United Republic of Tanzania as mandated under the Public Corporations Act and, in that on behalf of the Shareholder of State Mining Corporation (STAMICO), would like to recruit able and competent Tanzanians to constitute and serve in the Board of Directors of STAMICO. It is desired that upon their appointment as such as required under the Law, members of the Board of Directors of STAMICO will lead and govern this strategic Corporation to highest levels of performance in terms of: investing strategically in the mining industry and provide quality services in the management of mines, exploration, drilling, consultancies and other related business particularly to the artisanal and small scale miners for the benefit of the present and future generations. It is expected that under the governance of this Board of Directors, STAMICO shall go forward in recording desirable positive contributions to the wellbeing of the Nation at all respects; thus, satisfying the needs and desires of its shareholder, the Government; investors; customers; development partners; and other stakeholders. In these regards, the Ministry shall closely monitor the performance of the Board of Directors as required under the Law, and in line with pre-agreed Key Performance Indicators (KPIs). The KPIs shall reflect the expectation outlined in major policy documents of the Government, the law governing the sector, STAMICO’s contractual obligations and those of its customers and other stakeholders. Qualification/Qualities of individuals to be appointed as members of the Board of Directors MEM therefore desires that the Board of Directors of STAMICO shall be composed of individuals who have demonstrated significant achievements in their respective professional careers in business management and their service in either public or private sector, or both. The aspirants must possess requisite knowledge; intelligence and experience to enable them make significant contribution in the Board of Directors’ decision making process.

In light of Government policies and priorities on one hand, and the Corporations Mission and Vision on the other hand, the individuals are expected to possess qualifications and qualities and experience that will add value in the Mining sector. Specifically, the following qualities are considered desirable to any candidate aspiring to become member of the Board of Directors of STAMICO:

1. Education: it is desirable that a candidate should hold a graduate degree from a respected college or university majoring in the fields of, natural sciences, economics, finance, engineering, law, or management/administration. Possession of a Masters or doctoral degree will be an added advantage;

2. Experience: a candidate must have extensive experience (not less than 10 years) in his/her professional career and must demonstrate positive track record of performance in management in either public or private service, or both. An ideal candidate should have sufficient experience to fully appreciate and understand the responsibilities of a director in a challenging company like STAMICO;

3. International Experience: experience working in either senior management or as director in international organization/corporations relevant to the Mining industry will be considered as an advantage to a candidate’s profile;

4. Individual Character and Integrity: a candidate must be a person of highest moral and ethical character, impeccable record and integrity. Also a candidate must exhibit independence and demonstrate personal commitment to serve in the Corporation’s and public interests:

5. Personal Qualities: a candidate must have personal qualities that will enable him/her to make substantial active contribution in the Board’s decision-making process. These qualities include intelligence, self-assuredness, independence, highest ethical standing, practical knowledge to corporate governance standards, willingness to ask difficult questions, inter-personal skills, proficiency in communication skills and commitment to serve,

6. Knowledge of the Sector: a candidate must have sufficient knowledge of STAMICO’s work and situation and issues affecting the Mining sector in Tanzania. Also a candidate must have particular knowledge of STAMICO’s or rather, the mining sector’s stakeholder’s desires, needs and challenges, like those of the Government, development partners, investors, regulators, customers etc.

7. Courage: a candidate must be able and willing to make right decisions at all times, even if the same would make the person look difficult or unpopular;

8. Availability: a candidate must be willing to commit, as well as have, sufficient time available to discharge his or her duties as member of the Board of Directors. Therefore, a desirable candidate should not have other corporate board memberships;

9. Compatibility: a candidate should be able to develop good working relationship with other members of the Board of Directors and members of senior management of the Company: and

10. Conflict of Interest: a candidate must not be in a position of conflict of interest with Corporation’s activities. Invitation to apply: the Ministry invites candidates who possess the mentioned qualifications and qualities to apply to be considered for appointment as directors and serve in the Board of Directors of STAMICO. Applications from Public Servants will not be considered. Interested candidates must write and submit their applications by 15th January 2016 demonstrating their respective qualifications and qualities, attaching Photostat copies of their testimonials and detailed CVs to:-

The Permanent Secretary,Ministry of Energy and Minerals,5 Samora Machel Avenue,P.O. Box 2000, 11474 DAR ES SALAAMEmail: [email protected]

Kwa wadau wa sekta za Nishati na Madini, tembelea kurasa mpya za Wizara kwenye Mitandao ya Kijamii ya Twitter na Facebook kwa anuani ya ‘Nishati na Madini’ Karibu tuhabarishane na

tujadili kuhusu sekta za Nishati na Madini kwa maendeleo ya Watanzania wote.Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA MINISTRY OF ENERGY AND MINERALS