Kumtangaza Kristo Kwa Mataifa: Jumbe 100 Kuhusu Utume · 2018. 8. 28. · Warumi Rum 1 Wakorintho...
Transcript of Kumtangaza Kristo Kwa Mataifa: Jumbe 100 Kuhusu Utume · 2018. 8. 28. · Warumi Rum 1 Wakorintho...
-
1
-
2
Kumtangaza Kristo Kwa Mataifa: Jumbe 100 Kuhusu Utume
Unaowezeshwa Na Roho Mtakatifu. © 2018 (Swahili), Machapisho Ya AIA.
Haki Zote Zimehifadhiwa. Hakuna sehemu yoyote ya hiki kitabu inayoweza
kunakiliwa, kuhifadhiwa katika mfumo wa aina yoyote wa kusoma, au hata
kutumwa kwa namna yoyote – kielektroniki, kwa mitambo, kwa kudurufu,
kurekodiwa, au vinginevyo vyote – bila ya kupata ruhusa ya maandishi kabla
ya kufanya hivyo kutoka kwa mwenye haki miliki. Lakini nukuu fupi
zitakazotumiwa kwa ajili ya marejeo ya majarida au magazeti zinaruhusiwa.
Maandiko yote yanayotumiwa katika kitabu hiki, yanatoka katika Biblia ya
Kiswahili: UNION VERSION, © Chama Cha Biblia Tanzania Na Kenya,
2004. Haki Zote Zimehifadhiwa.
Kuna Maandiko yatakayofafanuliwa ili kueleweka vizuri. Mtafsiri atafanya
hivyo itakapobidi, na Maandiko hayo yatajulikana kwa alama hii: TLR, yaani
TAFSIRI YA LUGHA RAHISI.
Maelezo ya Chapisho katika Library of Congress Cataloging-in-Publication
Data
Miller, Denzil R., 1946–
Kumtangaza Kristo Kwa Mataifa: Jumbe 100 Kuhusu Utume Unaowezeshwa
Na Roho / Denzil R. Miller
1. Bibilia. 2. Theolojia Ya Vitendo: Stadi Za Kutunga Hotuba. 4. Umisheni 5.
KiPentekoste. 6. Roho Mtakatifu.
Kimefasiriwa Tanzania na Mchgj Simon Joel Vomo
© 2018 AIA Publications, Springfield, MO, USA
Printed in
Chapisho La Miaka Kumi Ya Pentekoste
Wavuti: www.DecadeofPentecost.org
www.ActsinAfrica.org
http://www.decadeofpentecost.org/http://www.actsinafrica.org/
-
3
Vitabu vya Biblia ~ Ufupisho Utumiwao Kitabuni Humu ~
Agano La Kale
Mwanzo Mwa
Kutoka Kut
Walawi Law
Hesabu Hes
KumbuKumbu Kumb
Yoshua Yosh
Waamuzi Amu
Ruthu Rut
1 Samweli 1Sam
2 Samweli 2Sam
1 Wafalme 1Fal
2 Wafalme 2Fal
1 Nyakati 1Nya
2 Nyakati 2Nya
Ezra Ezr
Nehemia Neh
Esta Est
Ayubu Ayu
Zaburi Zab
Mithali Mit
Mhubiri Mhu
Wimbo Ulio Bora Wim
Isaya Isa
Yeremia Yer
Maombolezo Ombo
Ezekieli Eze
Danieli Dan
Hosea Hos
Yoeli Yoe
Amosi Amo
Obadia Oba
Yona Yon
Mika Mik
Nahumu Nah
Habakuki Hab
Sefania Sef
Hagai Hag
Zekaria Zek
Malaki Mal
Agano Jipya
Mathayo Mt
Marko Mk
Luka Lk
Yohana Yn
Matendo Mdo
Warumi Rum
1 Wakorintho 1Kor
2 Wakorintho 2Kor
Wagalatia Gal
Waefeso Efe
Wafilipi Flp
Wakolosai Kol
1Wathesalonike 1The
2Wathesalonike 2The
1 Timotheo 1Tim
2 Timotheo 2Tim
Tito Tit
Filemoni Flm
Waebrania Ebr
Yakobo Yak
1 Petro 1Pet
2 Petro 2Pet
1 Yohana 1Yoh
2 Yohana 2Yoh
3 Yohana 3Yoh
Yuda Yda
Ufunuo Ufu
-
4
-
5
Yaliyomo
Vitabu vya Biblia ...................................................................................... 3
Yaliyomo................................................................................................... 5
Orodha Ya Walioandika Mahubiri ............................................................ 9 Utangulizi ................................................................................................ 15
SEHEMU YA 1: KUITANGAZA INJILI.
1 Kumtangaza Kristo Kwa Mataifa ...................................................... 22 2 Machozi Ya Mavuno ......................................................................... 24
3 Mtangaze Kristo Kwa Viumbe Vyote ............................................... 26
4 Tangaza Kwa Mataifa ....................................................................... 28
5 Ihubiri Injili ....................................................................................... 30
6 Yesu: Wa Kuigwa Katika Kuvuna Roho .......................................... 32
7 Mambo Manne Ya Lazima Kwa Ajili Ya Mavuno ........................... 34
8 Injili Hii Itahubiriwa ......................................................................... 36
9 Sisi Hatutaacha Kutangaza ................................................................ 38
10 Kuitangaza Kikamilifu Injili Ya Kristo ........................................... 40
11 Tumaini Moja Kwa Ajili Ya Dunia ................................................ 42
SEHEMU YA 2: AGIZO KUU
12 Amri Ya Kwanza Ya Agizo Kuu: “Ombeni!” .................................... 46
13 Amri Ya Pili Ya Agizo Kuu: “Nendeni!” ....................................... 48
14 Amri Ya Tatu Ya Agizo Kuu: “Hubirini!”...................................... 50
15 Amri Ya Nne Ya Agizo Kuu: “Shuhudieni!” ..................................... 52
16 Agizo Kuu Haliishi ........................................................................ 54
17 Kupata Mahali Pako Katika Agizo Kuu ............................................. 56
18 Kuli Ishi Agizo Kuu ........................................................................ 58
19 Nendeni Na Kufanya Wanafunzi .................................................... 60
20 Kulitimiza Agizo Kuu ..................................................................... 62
21 Usiondoke Nyumbani Bila Huyo! ................................................... 64
22 Kulielewa Agizo Kuu ...................................................................... 66
23 Kulitii Agizo Kuu............................................................................ 68
24 Maneno Makuu Manne Kwa Ajili Ya Mavuno .............................. 70 25 “Watu Wa Agizo Kuu” ................................................................... 72
26 Mitazamo Kuhusu Agizo Kuu ........................................................ 74
-
6
SEHEMU YA 3: ARI KWA AJILI YA WALIOPOTEA
27 Kusimamiwa Na Msalaba ...............................................................78
28 Utume Wa Mungu—Utume Wetu ..................................................80
29 Hivi Sasa Ni Saa Ngapi? .................................................................82 30 Kununua Mashamba Wakati Ambapo Inaonekana Haileti Maana .84
31 Kuhamasishwa Kwa Ajili Ya Utume ..............................................86
32 Mawe Matatu Ya Msingi Kwa Ajili Ya Umisheni ..........................88 33 Ni Wakati Wa Mavuno: Hebu Tujihusishe .....................................90
34 Mavuno Yameiva, Tayari Kuvunwa ...............................................92
35 Shauku Ya Mungu Kwa Ajili Ya Mataifa .......................................94
36 Kuchochea Shauku Yetu Kwa Ajili Ya Waliopotea .......................96
37 Kushirikiana Na Mungu Katika Utume Wake ....................................98
38 Yule Mwanamke “Asiye Wa Maana” ........................................... 100
39 Mungu Mwenye Kutafuta ............................................................. 102
40 Mapigo Ya Moyo Wa Mungu Kwa Ajili Ya Watu Waliopotea .... 104
41 Umisheni, Moyo Wa Mungu ......................................................... 106
42 Kweli Kuu Nne Kuhusu Mavuno .................................................. 108
43 Kujitoa Kwa Ajili Ya Dunia .......................................................... 110
44 Hazina Za Ufalme ......................................................................... 112
45 Kipaumbele Cha Mavuno.............................................................. 114
SEHEMU YA 4: ROHO MTAKATIFU NA UMISHENI
46 Swali La Pentekoste ...................................................................... 118
47 Umisheni Unao-ongozwa Na Roho Mtakatifu .................................. 120
48 Mapenzi Ya Mungu Kwa Ajili Yako ............................................ 122 49 Kuwezeshwa Kuzungumza ........................................................... 124
50 Ishara Za Kimisheni Za Pentekoste ............................................... 126
51 Kumtegemea Roho Katika Umisheni ............................................ 128
52 Mtakuwa Mashahidi Wangu ......................................................... 130
53 Roho Asema, “Nendeni!” .............................................................. 132
54 Moto Uendelee Kuwaka ................................................................ 134
55 Kusukumwa Na Roho Kuitangaza Injili ....................................... 136 56 Nguvu Yako Ili Kushuhudia ......................................................... 138
SEHEMU YA 5: WITO WA MUNGU
57 Miguu Inayopendeza ..................................................................... 142 58 Yesu Anaita ................................................................................... 144
59 Wito Mkuu Wa Kristo ................................................................... 146
-
7
60 Mwokozi Anayetuma .................................................................... 148 61 Tumebarikiwa Ili Kutii .................................................................. 150
62 Waliotumwa Na Kristo ................................................................. 152
63 Mungu Anayeita ............................................................................ 154 64 Kuchaguliwa Kwa Ajili Ya Utume Wake ..................................... 156
65 Imani Zenye Kina Sana Kuhusu Umisheni ................................... 158
66 Mungu Anaita! Je, Unasikiliza? .................................................... 160
67 Wito Wa Mungu............................................................................ 162 68 Kuitwa Kufanya Kazi Kwa Ajili Ya Ufalme .................................. 164
SEHEMU YA 6: KUINGIA KUTENDA KWA AJILI YA UMISHENI
69 Kufuata Mfano Wake Yesu ........................................................... 168
70 Vitu Vitano Muhimu Kwa Umisheni ............................................ 170
71 Shughuli Tatu Za Umisheni Za KiMkakati ................................... 172
72 “Dunia Ya Tusipo” ........................................................................ 174
73 Nguvu Ya Mmoja.......................................................................... 176
74 Changamoto Mbili Kubwa Za Kimishenari .................................. 178
75 Mpango Wa Mungu Wa Umishenari ............................................ 180
76 Zaburi Ya Kimsihenari Kwa Kila Mtu .......................................... 182
77 Injili Kuenea Bila Kuzuiwa ........................................................... 184
78 Karima Kuu Ya Mungu Kwa Afrika ............................................. 186
79 Kipimo Cha Kanisa La Kimisheni ................................................ 188
80 Kauli Mbiu Ya Umisheni .............................................................. 190
81 Hatua Tisa Kuelekea Eneo La Umisheni ...................................... 192
82 Kuvuna Mataifa: Nini Kinachohitajika ......................................... 194
83 Wakati Wa Kupanda Na Kuvuna .................................................. 196 84 Utume Wa Kutuma Wa Kanisa ..................................................... 198
85 Watawezaje Kusikia? .................................................................... 200
86 Kwa Njia Yoyote Iwezekanayo .................................................... 202 87 Kanuni Nne Za Mavuno ................................................................ 204
88 Sabini Na Mbili Pamoja Na Wewe ............................................... 206
89 Kuwa Mkristo Wa Dunia Nzima ................................................... 208 90 Hadithi Kuu Iliyowahi Kusimuliwa .............................................. 210
91 Roho Mtakatifu: Mwongozaji Katika Umisheni ........................... 212
92 Kila Mahali! .................................................................................. 214
93 Gharama Ya Umisheni .................................................................. 216 94 Masomo Ya Umisheni Toka Kwa Eliya ....................................... 218
-
8
SEHEMU YA 7: MAOMBI NA VITA YA KIROHO
95 Kuhamasishwa Kwa Ajili Ya Umisheni ....................................... 222
96 Maombi Na Utume Wa Mungu ..................................................... 224
97 Kumshinda Adui ........................................................................... 226 98 Tuwasaidie Kwa Maombi Yetu ..................................................... 228
99 Maombi Yenye Kufungua ............................................................. 230
100 Maombi Na Kazi Ya Umisheni ................................................... 232
Orodha Ya Maandiko Yaliyotumiwa .................................................... 235
Vitabu Vingine Vya Miaka Kumi Ya Pentekoste ................................. 239
-
9
Orodha Ya Walioandika Mahubiri
AC Al Crane Mchungaji wa Assemblies of
God, Crowley, Texas. USA
(Mahubiri Namba 71)
BD Brett Deal Mishenari wa Assemblies of God
huko Senegal (Mahubiri Namba
58, 72)
BVW Barbara VanWyke Mishenari wa Assemblies of God
huko Botswana (Mahubiri Namba
90)
CGS Christopher Gornold-Smith Mishenari wa Assemblies of God
katika taasisi ya International
Media Ministries (Mahubiri
Namba 20)
CK Claver Kabandana Rais wa Pentecostal Assem-blies
of God huko Rwanda (Mahubiri
Namba 6)
DB Darlene Banda Mkuu wa Chuo, Assemblies of
God Bible College huko Lusaka,
Zambia (Mahubiri Namba 70)
DC Don Corbin Mkurugenzi Wa Wamishenari
Afrika Nzima (1985-2002)
(Mahubiri Namba 30, 31, 95)
DG Dean Galyen Mishenari wa Assemblies of God,
Afrika (Mahubiri Namba 34)
DM Daniel Mbiwan Mwangalizi Mkuu wa Full Gospel
Mission huko Cameroon
(Mahubiri Namba 77)
DMc Daniel McGaffee Mchungaji wa Chi Alpha Chuoni,
Chuo Kikuu Cha Jimbo Chico,
Chico, California, Marekani
(Mahubiri Namba 96)
DRM Denzil R. Miller Mkurugenzi Wa Acts in Africa
Initiative, Springfield, Missouri, Marekani (Mahubiri Namba 1, 7,
8, 9, 10, 21, 24, 25, 26, 35, 36, 50,
52, 53, 65, 66, 78, 79, 80, 81, 82,
83, 84, 94, 97)
-
10
EC Edward Chitsonga Rais wa Malawi Assemblies of
God (Mahubiri Namba 3)
EG Edwin Gbelly Rais wa Liberia Assemblies of
God (Mahubiri Namba 37, 64)
EKA Emmanuel Kwasi Amoafo Kasisi Mwambata wa Kanisa
Anglikana Kenya Mtaa wa Christ
Church, Nairobi, Kenya
(Mahubiri Namba 16)
EML Enson Mbilikile Lwesya Mwanatimu wa AIA; Mwenyekiti
wa Tume Ya Umisheni wa Dunia
Ya AAGA Na Mchungaji
Kiongozi wa Kanisa la
International Christian Assembly,
Lilongwe, Malawi (Mahubiri
Namba 49)
EYA Emil Yaovi Adote Rais wa Benin Assemblies of God
(Mahubiri Namba 69)
GB Greg Beggs Mkurugenzi wa Wamishenari
Afrika Nzima (Mahubiri Namba
2, 27, 57)
GC Gaylan Claunch Makamu Askofu Na Mkurugenzi
Wa Umisheni, Jimbo la North
Texas la Assemblies of God
Marekani (Mahubiri Namba 40,
42)
GM Greg Mundis Mkurugenzi Mkuu Wa Umisheni
Wa Assemblies of God Duniani,
Springfield, Jimbo la Missouri,
Marekani (Mahubiri Namba 51)
JB Jason Branson Mchungaji wa Kanisa la First
Assembly of God, LaGrange,
Jimbo la Georgia, Marekani
(Mahubiri Namba 29)
JDE Jimmy D. Easter Mtumishi Wa Assemblies of God
(Mahubiri Namba 59, 73)
JF Jerry Falley Mkurugenzi wa taasisi ya Link-
Up Africa, Springfield, Missouri,
Marekani (Mahubiri Namba 5, 61,
62)
-
11
JL Jimmy Lemons Mratibu wa Nchi
Zinazozungumza Kifaransa katika
Chuo cha Pan Africa Theological
Seminary huko Togo (Mahubiri
Namba 76)
JLE John L. Easter Mkurugenzi wa taasisi ya Africa’s
Hope, Springfield, Missouri,
Marekani (Mahubiri Namba 32,
74)
JM Jim Mazurek Mishenari wa Assemblies of God
huko Chile (Mahubiri Namba 63)
JN Jeff Nelson Mishenari Mkazi katika Evangel
University, Springfield, Missouri,
Marekani (Mahubiri Namba 54)
JO Jerry Orf Mchungaji wa Kanisa la First
Assembly of God, Mansfield,
Missouri, Marekani (85, 98)
JS Jerry Spain Mkurugenzi wa Wamishenari
Eneo la Afrika Mashariki (1992-
2000) (Mahubiri Namba 44, 45)
JTG Joegbéan Tokpah Rais wa Guinea Assemblies
Gbanamou God (Mahubiri Namba 48)
LB Lipenga Banda Katibu Mkuu wa Zambia
Assemblies of God (Mahubiri
Namba 46)
LC Lazarus Chakwera Rais wa Malawi Congress Party;
Rais wa Malawi Assemblies of
God (1989-2013) (Mahubiri
Namba 47)
LE Lavonna Ennis Mishenari wa Assemblies of God,
The Gambia (Mahubiri Namba
93)
LT Loren Triplett Mkurugenzi wa Umisheni,
Assemblies of God Duniani
(1989-1997) (Mahubiri Namba
43, 67)
-
12
MO Michel Ouedraogo Rais wa Burkina Faso Assemblies
of God (Mahubiri Namba 86)
MRT Mark R. Turney Mkurugenzi Mwenza, Acts in
Africa Initiative; Katibu Mkuu
Wa Muungano wa Assemblies of
God Afrika (Mahubiri Namba 11,
26, 55, 68, 88)
NB Nate Beggs Mishenari wa Assemblies of God
Afrika (Mahubiri Namba 17)
PFM Paul Frimpong-Manso Askofu Mkuu wa Ghana
Assemblies of God (Mahubiri
Namba 19, 33, 91)
PW Peter Watt Askofu Mkuu wa Assemblies of
God Afrika Kusini (Mahubiri
Namba 99, 100)
PY Paul York Mkufunzi Wa Umisheni Katika
Tamaduni Tofauti, Chi Alpha,
Marekani (Mahubiri Namba 56)
RSK Reuben S. Kachala Kiongozi wa Kituo cha
Uhamasishaji, huduma ya Frontier
Missions International, Lilongwe,
Malawi (Mahubiri Namba 23, 89)
SC Sarah Cariens Mishenari wa Assemblies of God,
Afrika Kusini (Mahubiri Namba
18)
SE Scott Ennis Mishenari wa Assemblies of God
nchini The Gambia (Mahubiri
Namba 4, 60, 92)
SH Scott Hanson Kiongozi Mkakati wa Assemblies
of God Afrika Kwa Ajili Ya
Kuwafikia Watu Ambao
Hawajafikiwa, (Mahubiri Namba
22, 75)
SP Steve Pennington Mkurugenzi wa Wamishenari wa
Assemblies of God katika Afrika
Mashariki (Mahubiri Namba 38,
39, 87)
-
13
UA Uche Ama Mwana Timu wa AIA na
Mkurugenzi wa Umisheni wa
Nchi za Nje wa Assemblies of
God Nigeria (Mahubiri Namba
12, 13, 14, 15)
WS Waly Sarr Rais wa Senegal Assemblies of
God (Mahubiri Namba 41)
-
14
-
15
Utangulizi
Kanisa la Assemblies of God katika Afrika linajizatiti na kuhamasisha
kuhusu umisheni. Katika kipindi chao cha Miaka Kumi ya Mavuno, kuanzia
mwaka wa 2010 hadi 2020, makanisa hamsini ya kitaifa ambayo yanaunda
Muungano wa Assemblies of God Afrika (AAGA) yamejizatiti kutuma
wamishenari wengi katika maeneo mengi ambayo hayajafikiwa, na yenye
watu wengi ambao hawajafikiwa katika nchi zao wenyewe na katika nchi
jirani. Katika juhudi hizo, makanisa ya kitaifa na ya mahali pamoja hujikuta
katika ngazi au hatua mbalimbali za maendeleo. Mengine yamekwisha
simika na kujenga idara zenye nguvu za umisheni na wanatuma hata
wamishenari kwenda shambani. Mengine ndiyo kwanza yameanzisha
utaratibu huo. Kwa hali yoyote ile, wote wamejizatiti kufanya sehemu yao
katika kutuma ujumbe wa Kristo kwa watu wasiofikiwa na maeneo ambayo
hayajafikiwa, katika Afrika na hata kwingineko.
Mungu ameibariki sana Assemblies of God ya Afrika. Kanisa hili kwa
sasa linatoa taarifa kwamba kuna washirika milioni 22 yenye kukutania
katika makanisa 8,100 katika bara zima. 1 Lakini, Yesu alifundisha kwamba
Baraka za namna hiyo huambatana na wajibu au majukumu mengi. Alisema
hivi: “Yeye aliyepewa vingi, vingi vitahitajika kutoka kwake” (Luka 12:38,
TLR). Hakika, hayo yanalihusu kanisa la Assemblies of God Afrika. Moja
ya majukumu makubwa (na changamoto) ni kuhamasisha na kuwatuma
jeshi kubwa la wamishenari kwenda shambani – halafu, kuwategemeza kwa
maombi na fedha. Hebu fikiri kitu gani kingetokea kama ari au shauku ya
kuyafikia mataifa kwa ajili ya Kristo ingepandwa katika mioyo ya hao
washirika wote milioni 22 wa Assemblies of God Afrika.
Ili jambo hili litokee, kuna mambo mawili ambayo lazima yatokee.
Kwanza, Assemblies of God ya Afrika lazima iendelee kukutana na kupokea
umwagiko wa Roho Mtakatifu. Tunamshukuru Mungu kwamba anaendelea
kumwaga Roho Wake juu ya kanisa la Afrika. Lakini, huu uamsho wa
KiPentekoste lazima upanuke na kushika kasi. Wakati Yesu alipokuwa
analihamasisha kanisa Lake pale Yerusalemu, aliwaagiza waende duniani
kote na kuhubiri habari njema kwa kila mtu. Ila, aliwaagiza wakae
Yerusalemu kwanza mpaka wawe wamevikwa nguvu au uweza wa Roho
(Luka 24:49). Mwisho, muda mfupi kabla hajapaa mbinguni, aliwaacha kwa
kutoa ahadi ya mwisho, hivi:
1 Kwa mujibu wa takwimu za 2015.
-
16
“Lakini mtapokea nguvu, Roho Mtakatifu akiisha kuwajia, nanyi mtakuwa
mashahidi wangu…mpaka miisho ya dunia” (Matendo 1:8, TLR). Ili
kutimiza hatima yao ya umishenari, Assemblies of God Afrika lazima
iongeze maombi yake kwa Bwana wa Mavuno. Ni lazima waombe hivi: “Ee
Bwana! Kwa neema yako, mimina juu yetu Roho wako, na ututie nguvu
kutimiza Utume Wako hapa duniani.”
Kingine ambacho lazima kitokee katika Assemblies of God ya Afrika
ni kwamba wachungaji lazima waanze kuhubiri mara kwa mara na kwa
ufanisi sana juu ya umisheni. Hapo ndipo shauku kwa ajili ya mataifa
ambayo hayajafikiwa itakapopandwa ndani ya mioyo ya watu wa Mungu.
Lakini, kwa bahati mbaya sana kanisa la Assemblies of God Afrika
halina kawaida ya karne nyingi ya kuhubiri juu ya umisheni, tofauti na
Kanisa la Magharibi. Utamaduni huu wa Kanisa la Magharibi ulianza
zamani – siku za William Carey, mwishoni mwa karne ya kumi na nane.
Wakati kanisa la Afrika limekuwa likifukuzia kwa mafanikio sana swala la
uinjilisti na kupanda makanisa, katika mipaka yao kitaifa, kihistoria ni
kwamba hawajawahi kutafuta kujihamasisha kwa ajili ya umisheni wa
kuifikia dunia. Matokeo yake ni kwamba hawajaendeleza desturi ya muda
mrefu ya kuhubiri juu ya umisheni.
Hiki kitabu kimetayarishwa kushughulikia swala hilo. Kimeandaliwa
kama kitabu rejea kwa ajili ya wachungaji wa Kiafrika wanaotaka
kuhamasisha makanisa yao kwa ajili ya umisheni. Wachungaji na viongozi
wa kanisa wanaweza kutumia mahubiri haya kuwaamsha na kuwafundisha
watu wao kanuni za umisheni, na hata utendaji wake. Kitabu hiki kinafuata
kitabu cha kwanza cha mihutasari ya jumbe kilichochapishwa na Acts in
Africa Initiative (AIA) mwaka wa 2011. Kitabu cha kwanza kiliitwa,
Kuitangaza Pentekoste: Jumbe 100 Kuhusu Nguvu ya Roho Mtakatifu.2
Mafanikio makubwa ya kitabu kile cha kwanza yamekuwa mazuri sana.
Kufikia sasa, kimetafsiriwa kutoka lugha ya Kiingereza hadi lugha zingine
sita za Kiafrika, ikiwa ni pamoja na Kifaransa, Kireno, Kiswahili, KiMoor
na KiAmharik. Kimegawanywa kwa zaidi ya wachungaji elfu 35,000 katika
nchi 31 za Afrika. Kinatumiwa katika nchi za Marekani Kati na Kusini, na
hata Ufilipino. Ofisi za AIA zimepokea shuhuda nyingi jinsi kitabu hivyo
kinavyotumiwa, na jinsi maelfu ya Wakristo Waafrika wanabatizwa kwa
Roho Mtakatifu kama matokeo ya kitabu hicho. Mchungaji mmoja
2 Hivi vitabu viwili na vingine vingi vinaweza kupakuliwa bure katika mfumo
wa barua pepe kwenye tovuti hii: www.DecadeofPentecost.org. Vinaweza
kununuliwa kama vitabu kupitia blogu yangu binafsi, hii ifuatayo:
www.DenzilRMiller.com.
http://www.decadeofpentecost.org/http://www.denzilrmiller.com/
-
17
Mwafrika alisema, kwa furaha sanad, “Kitabu hiki cha Kuitangaza Pentekoste kimeleta uamsho kwa kanisa letu la nchi.” Tunaomba kitabu hiki
nacho kiwe na mguso na mafanikio kama hayo.
Wachangiaji
Mihutasari hii 100 katika hiki kitabu imechangiwa na kutolewa na
wahubiri arobaini na tano wa KiPentekoste. Wahubiri hao ni pamoja na
wamishenari wa Kiafrika na viongozi wa umisheni, wamishenari wa
KiMarekani, na wachungaji wanaohusika na mambo ya umisheni. Mimi
binafsi nimechangia moja ya nne ya mihutasari hiyo. Utaweza kumtambua
kila mchangiaji kwa herufi mbili za jina lake zitakazokuwa mwisho wa kila
muhtasari. Halafu ulinganishe hizo herufi mbili kwa orodha inayotolewa
katika ukurasa wa 9 hadi 12 inayoitwa “Orodha ya Wachangiaji”. Vile vile,
baada ya jina la kila mchangiaji na maelezo yake, utakuta katika mabano
orodha ya mahubiri aliyochangia.
Ninataka kutoa shukrani zangu za dhati kwa kila mmoja katika hao
waliochangia kwa kuturuhusu kutumia mihutasari yao bila gharama yoyote.
Jinsi Ya Kutumia Hiki Kitabu
Niruhusu nikushauri jinsi unavyoweza kutumia hiki kitabu. Mchakato
huanza kwa kuchagua ujumbe. Kwa mfano: Kama unataka kuhubiri kutoka
andiko Fulani, unaanza msako wako kwa kuangalia “Orodha Ya Maandiko
Yaliyotumika” iliyoko mwishoni mwa kitabu hiki. Msako huo utakuongoza
ufikie mahubiri yoyote ambayo yamekwisha andaliwa kutegemeana na
ujumbe ulioandaliwa kutokana na andiko lako ulilochagua.
Pengine unataka kuhubiri ujumbe wa umisheni, lakini huna uhakika wa
kile unachotaka kuhubiri. Kama ni hivyo, unaweza kuchambua katika kitabu
uone ujumbe unaofaa. Pengien uanzie kwenye “Orodha Ya Yaliyomo”
mwanzoni mwa kitabu. Kwa kufanya hivyo, utaona kwamba kitabu
kimegawanywa katika sehemu kuu saba, ambazo ni pamoja na hizi
zifuatazo:
Kuitangaza Injili
Agizo Kuu
Ari Na Shauku Kwa Waliopotea
Roho Mtakatifu Na Umisheni
Wito Wa Mungu
Kuhamasisha Kwa Ajili Ya Umisheni
Maombi Na Vita Ya Kiroho
-
18
Kipengele kimoja katika hivi kinaweza kukuvutia. Hapo utaanza kutafuta
ujumbe katika sehemu hiyo husika katika kitabu, na kwa njia hiyo
kurahisisha msako au utafutaji wako.
“Mahubiri Katika Sentensi Moja” ni sehemu inayoweza kukusaidia pia.
Kwa kusoma hiyo sentensi moja ambayo ni kama majumuisho ya ujumbe,
inakuwa rahisi kwako kupata wazo upesi kama ungependa kutafiti zaidi au
hapana. Kama mada inakuvutia, basi unaweza kutazama muhtasari husika
kwa ukaribu zaidi.
Pengine ungetaka kufikia lengo Fulani katika mahubiri yako. Kwa
mfano: Unataka kuwahamasisha wasikilizaji wako kuombea umisheni, au
unataka wao wamfungulie Mungu mioyo yao ili wasikie sauti Yake
anapowaita kwa umisheni. Kama ndivyo, itakubidi upitie ile sehemu
inayoitwa “Kusudi La Mahubiri” ambayo ndiyo huanza kila muhtasari. Kwa
namna hiyo, unaweza kuchagua ujumbe ambao utakusaidia kufikia lengo
lako.
Zidi kuona kwamba kila muhtasari kwenye kitabu hiki umeandaliwa
kutosha kwenye kurasa mbili Kwa kufanya hivyo nimejaribu kuweka
maudhui ya kutosha kwenye kila muhtasari ili kumpa mtumiaji mwelekeo
ulio dhahiri juu ya kilichomo na jinsi ujumbe unavyotiririka. Hapo hapo,
nimejaribu kufanya mambo kwa kifupi kiasi cha kuwapa wahubiri na
waalimu nafasi ya kutosha kukuza na kutengeneza jumbe hizo kulingana na
mahitaji pekee ya wasikilizaji wao. Unapojiandaa na kuombea ujumbe
husika, na kuhubiri muhtasari wowote katika hizi, ninaamini kwamba Roho
Mtakatifu atakuvuvia kwa mawazo mapya ya jinsi ya kuandaa na kupanua
jumbe zako mwenyewe za umisheni.
Zipo njia nyingi mbalimbali za wewe kutumia ule muhtasari
utakaokuwa umechagua. Njia ya kwanza na iliyo dhahiri ni kuhubiri ujumbe
huo kama ulivyoandikwa. Lakini ni kitu halisi kwamba kutataka
kutengeneza ujumbe wako uendane na mazingira yako binafsi ambayo yana
upekee wake, na kulenga mahitaji mahsusi ya wasikilizaji wako. Pia,
utapenda kuongeza vitu vyako vya zaidi ulivyopata vya kuongezea kwenye
ujumbe husika. Pamoja na hayo, unapo-omba na kutafakari mahubiri hayo,
Roho Mtakatifu atazungumza na wewe. Kwa hakika utahitaji kuingiza hayo
mambo uliyopata na kuyaongeza kwenye ujumbe wako. Na ni hakika
kwamba utataka kuongezea mifano yako na hata vichekesho kidogo kwenye
huo ujumbe. Kwa maneno mengine ni kwamba, ninakutia moyo ufanye
mahubiri hayo kuwa ya kwako.
-
19
Jinsi Ya Kuhubiri Ujumbe Mkuu Wa Umisheni
Namalizia kwa mawaidha machache juu ya jinsi unavyoweza kuchukua
hii mihutasari ya mahubiri ili uweze kuhubiri jumbe kuu za kimisheni.
Jazwa na Roho Mtakatifu. Kwanza: Ili uweze kuhubiri ujumbe wa
umisheni wenye ufanisi – au ujumbe wowote ule – ni lazima uwe umejaa
Roho Mtakatifu. Mara nyingi sana katika Kitabu cha Matendo ya Mitume,
mitume walianza mahubiri yao kwa kujazwaa na Roho Mtakatifu (Matendo
2:4 na 14; 4:8; 4:31). Hakuna mbadala wa mahubiri yanayotolewa kwa
nguvu za kujazwa na Roho. Hakuna kiwango chochote cha haiba binafsi ya
mtu au mbinu za maonyesho kinachoweza kuchukua mahali pa kukosekana
kwa Roho juu ya mhubiri. Acha Yesu awe mfano wako. Yeye alipoanza
huduma, alitamka hivi: “Roho wa Bwana yuko juu yangu, kwa sababu
amenitia mafuta ili kuhubiri habari njema…” (Luka 4:18).
Mahubiri yawe ya kwako. Kama ilivyopendekezwa hapo nyuma, ufanye ujumbe husika uwe wa kwako. Yaani kwa maneno mengine, ukisha chagua
muhtasari wa ujumbe utakaohubiri, anza “kuuingiza” ndani yako. Ingiza
ujumbe huo ndani ya moyo wako na akili zako kwa kutafakari na hali ya
maombi, ukiusoma mara kadhaa. Katika akili zako, jihubirie ujumbe huo
mara kadhaa. Unapofanya hivyo, itikia ujumbe wenyewe. Jali unasema nini.
Kama unahitaji kusimama kidogo na kuomba, basi fanya hivyo. Kama
unahitaji kutubu, fanya hivyo pia.
Vile vile, ni muhimu sana kukariri andiko la ujumbe husika pamoja na
maandiko mengine muhimu yatakayotumika katika ujumbe. Hiyo itasaidia
pia kuweka ujumbe huo katika moyo wako. Hiyo pia itakusaidia wakati wa
mahubiri. Kwa kuwa mistari ya Maandiko iko moyoni mwako na katika
akili yako, mahubiri yako yatatiririka kwa ubora na kwa urahisi sana.
Wasikilizaji wako watasikia jinsi unavyoguswa na kile unachokisema, na
jinsi unavyojua na kutawala mada yako, na wataitikia vizuri zaidi yale
unayosema. Itakuwa msaada sana kwako kukariri yale mambo makuu ya
mahubiri yako. Kwa kufanya hivyo, utawekwa huru kutoka kuangalia kitini
ulichoandika, na utaweza kusema na watu wako moja kwa moja na kwa
ushawishi mkubwa.
Toa ujumbe wako. Unapohubiri ujumbe wako wa umisheni, zingatia
mambo mawili. Kwanza, usiwe na maneno mengi. Maana yake ni kwamba
usijaze ujumbe wako kwa maneno mengi yasiyo ya lazima, au hata mawazo
yasiyofaa. Bakia kwenye mada yako. Kumbuka lengo lako, na usiseme
chochote ambacho hakitakusaidia kufikia lengo hilo. Pili, unapohubiri, lenga madhabahu. Yaani, kila utakachosema lazima kiwe kimeandaliwa
kuwafanya watu kujitoa, au kufanya maamuzi. Kisha, unapohitimisha
ujumbe wako, “tupa nyavu”. Kama mvuvi anavyotupa wavu wake ndani ya
maji na kuvuta samaki walionaswa kuingia kwenye mtumbwi wake, wewe
-
20
pia unapaswa “kutupa nyavu” kwa kuwaalika watu wafike madhabahuni.
Waie wajiweke tayari kwa ajili ya utume wa Mungu na wawezeshwe na
Roho ili kufanikisha jambo hilo.
Kwa mawazo hayo, ninakupa kitabu hiki. Ni maombi yangu ya dhati
kabisa kwamba utakitumia mara kwa mara kama kifaa kwa ajili ya
kuhamasisha kanisa la Kristo kuwafikia mataifa kwa ngvu za Roho
Mtakatifu.
Ningependa kusikia kutoka kwako jinsi mihutasari hii ilivyokuwaidia.
Tafadhali tuma shuhuda na mahitaji ya kuombewa kwa anwani hii ya barua
pepe: [email protected].
Ni mimi,
Dkt. Denzil R. Miller
Mhariri
-
21
-
22
1 Kumtangaza Kristo Kwa Mataifa
Ujumbe Wenyewe Katika Sentensi Moja: Ni lazima tuyatangazie
mataifa habari za Kristo katika nguvu za Roho Mtakatifu.
Kusudi La Ujumbe: Watu wajazwe na Roho na kujitolea na kujikabidhi
kumtangaza Kristo kwa mataifa.
Maandiko Ya Ujumbe: Marko 16:15-18
Utangulizi 1. Kama watu ambao ni wamishenari wa Mungu, wote tumeitwa
kumtangaza Kristo kwa mataifa.
2. Agizo Kuu la Marko linaweka jambo hilo wazi zaidi: “Enendeni
duniani kote mkahubiri habari njema kwa uumbaji wote.”
3. Ujumbe huu utazungumzia mambo manne muhimu kuhusu wajibu
wetu wa kumtangaza Kristo kwa mataifa: Utume wetu, Mbinu
yetu, Namna tunayofanya hivyo, na Itikio linalotakiwa kutoka
kwetu.
I. UTUME WETU—DUNIA NZIMA A. Yesu alisema, “Nendeni duniani kote…” (Mk 16:15).
1. Wakati mwingine alisema, “Hii injili ya ufalme itahubiriwa
duniani kote [oikoumeme, dunia yenye watu], kuwa kama ushuhuda kwa mataifa yote [ethne, kundi la watu]; ndipo mwisho
utakuja” (Mt 24:14).
B. “Duniani kote” ni pamoja na…
1. Kila mahali: “Mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu,
na Uyahudi wote…mpaka mwisho wa dunia” (Mdo 1:8).
2. Kila mtu: “mkahubiri…kwa kila kiumbe” (ms.15).
3. Kila watu: “Enendeni basi, na kufanya wanafunzi katika
mataifa yote (Kiyunani: ethne au makundi ya watu, makabila)” (Mt 28:19).
B. Kitakachohitajika: Wengine watakwenda; wengine watatuma.
(Soma Rum 10:13-15a).
1. Kristo anawaita wengine waende.
a. Waondoke nyumbani na kuacha familia na kwenda nchi
za mbali na katika tamaduni ambazo hawajazizoea, na
kutangaza habari njema.
2. Yeye anatuita sisi wengine wote tuhusike kutuma.
a. Kutoa fedha ili kuwategemeza wale wanaokwenda.
b. Kuwaombea wamishenari, na waliopotea. 3. Hakuna asiyehusika.
II. UJUMBE WETU—HABARI NJEMA
A. Yesu alisema, “Nendeni duniani kote mkaihubiri injili…”
-
23
1. Habari njema (Injili) ni ujumbe wa kufa kwa Yesu msalabani, na
kufufuka Kwake toka kwa wafu kwa utukufu mwingi.
2. Inahusisha wito kwa watu kutubu dhambi zao na kumwamini
Kristo peke Yake ili waokoke (Mk 1:15; Mdo 20:21).
B. Kutenda kwetu (au kutokutenda) kuna matokeo ya milele.
1. Yesu alisema, “Kila atakayeamini na kubatizwa ataokoka, lakini
kila asiyeamini atahukumiwa” (ms. 16).
2. Vile vile kuna matokeo ya kutokwenda na kutotangaza au
kuhubiri:
a. Soma na kujadili: Ezekieli 3:17-19
C. Tusiruhusu jumbe za hali ya chini kutuelekeza pembeni.
1. Onyo la Paulo kwa Timotheo (2Ti 4:3-5).
2. Ujumbe wa Kristo tu ndiyo utakaoleta uzima wa milele
(Yn 17:3).
III. MBINU YETU—NGUVU YA ROHO MTAKATIFU A. Yesu aliahidi hivi: “Na hizi ishara zitawafuata…” (ms.17-18)
1. Haya yote ni kazi ya Roho Mtakatifu (Mdo 4:30-33).
2. Katika Matendo: “Kisha wanafunzi walitoka na kwenda
kuhubiri kila mahali, na Bwana alifanya kazi pamoja nao na
kulithibitisha neno lake kwa ishara zilizofuatana nalo” (Mdo
16:20).
3. Huduma yenye kuwezeshwa na Roho na kutiwa nguvu,
inaonekana katika kitabu cha Matendo.
B. Yesu ameahidi nguvu hiyo hiyo kupatikana kwetu sisi siku za leo.
1. Ahadi Yake ya mwisho: (Mdo 1:8) “Mtapokea nguvu…”
2. Amri Yake ya mwisho: (Mdo 1:4-5) “Msiondoke
Yerusalemu, bali ingojeeni ile zawadi ambayo Baba yangu
aliahidi…”
IV. ITIKIO LETU LINALOTAKIWA—UTII A. Andiko letu linasema, “Ndipo wanafunzi walitoka na kuhubiri kila
mahali…”
1. Yaani, walitii amri ya Bwana Yesu.
B. Mungu anataka itikio hilo hilo kutoka kwetu siku ya leo.
1. Yesu alisema: “Mkinipenda, mtatii ninayoagiza” (Yn 14:15).
2. Ni lazima tutii kwa kwenda, kutoa, na kuomba.
Kumalizia, Na Wito Kwa Watu Kuja Mbele
1. Njoo sasa ujitolee kwa ajili ya utume wa Kristo.
2. Njoo utiwe nguvu na Roho Mtakatifu.
[ DRM ]
-
24
2 Machozi Ya Mavuno
Ujumbe Wenyewe Katika Sentensi Moja: Hata katika nyakati ngumu, ni
lazima tupande mbegu ya Injili, tukimwamini Mungu kwa mavuno.
Kusudi La Ujumbe: Kuwatia watu moyo wahubiri Injili hata katikati ya
majaribu makubwa, na ugumu.
Maandiko Ya Ujumbe: Zaburi 126:4-6
Utangulizi 1. Katika hii “Zaburi Ya Kupanda,” wale waliokuwa utumwani
walirudi Sayuni—wanachokuta ni magofu tu.
a. Wakati wanapofurahia uhuru wao, hapo hapo wanalia
wanapokumbuka utukufu wa kwanza wa mji huo.
b. Wanapojenga upya mji wao ulioharibika, na kupanda mbegu
zao za thamani katika mashamba yao makavu, wanalia.
c. Lakini kwa imani wanamtazama Mungu kwa ajili ya mavuno
yaliyoahidiwa.
2. Leo tunalia kwa ajili ya Afrika.
a. Katika Afrika, Shetani anao mateka wegi sana.
b. Afrika kwa namna nyingi, ni magofu, kama Sayuni ilivyokuwa.
1) Inasumbuliwa na vita, njaa na ukame, magonjwa, na ufisadi.
c. Lakini, wakati tunapoililia Afrika, ni lazima tupande mbegu pia.
3. Katika andiko letu, tunajifunza masomo muhimu sana kuhusu
kupanda na kuvuna, kama ifuatavyo:
I. SHAUKU YA KITUME: KUTAMANI KUPANDA
Soma ms. wa 6 “Yeye aendaye kupanda akilia machozi…” A. Wakati wa ukame, mara nyingi tunajaribiwa tusifanye chochote.
1. Kwa sababu ya maumivu, tunajaribiwa kuweka mbegu. B.
Hata hivyo, shauku ya kitume inatuhamasisha kwenda
shambani kupanda, kwa gharama yoyote.
1. Ukame na njaa havipaswi kumzuia mkulima kupanda mbegu.
2. Wakulima wa KiAfrika wanaelewa maana uya kupanda kwa
machozi. Katika nyakati za ukame, wanajaribiwa kula hata
mbegu iliyohifadhiwa kwa majira yajayo. Wanalia, lakini
bado wanapanda mbegu shambani, wakiamini kwamba
Mungu atawapa mavuno.
C. Shauku ya kitume hutusukuma sisi kupanda hata katika nyakati ngumu.
1. Tunasukumwa na Imani katika Bwana wa Mavuno (Mt 9:38),
na mavuno ya roho za watu yaliyoahidiwa (Gal. 6:9), na kwa nguvu za Roho Mtakatifu (Mdo 11:12).
2. Mara nyingi, machozi ndiyo bei itolewayo na Ufalme kwa
ajili ya maendeleo.
-
25
II. RASILMALI ZA KITUME: MPANDAJI NA MBEGU ms. 6: “…akiwa amebeba mbegu za kupanda…”
A. Injili ni kama mbegu nzuri (Lk 11:8; 1Pet 1:23).
1. Kamwe usiwe na mashaka juu ya nguvu yake ya -
kuwakomboa watu (Rum 1:16).
2. Ni habari njema kwa ajili ya watu wote, haidhuru ni wagumu
kiasi gani, wamepotea kiasi gani, au wanaonekana kuwa
mbali kiasi gani kutoka kwenye neema ya Mungu.
B Injili inaendelea kubadilisha maisha ya watu mamilioni kwa
mamilioni.
1. Imebadilisha jamii ambazo hapo kwanza zilikuwa zinajificha
kwa hofu ya mizimu yao ya kiasili na kuzifanya kuishi maisha
ya ushindi.
2. Imebadilisha makundi ya watu ambao mwanzo walikuwa
wanawanyanyasa, kuwauza na kuwaumiza wanawake wao,
mpaka kuwa watu ambao sasa wanawasimika wanawake
kuwa watumishi wa Injili.
3. Imewabadilisha watu waliokuwa wamejaa choyo na ubinafsi
kuwa watu wanaoweza kutoa kwa sehemu kubwa sana ili
kutegemeza shughuli ya Kristo.
C. Maisha yaliyobadilishwa ni mbegu nyingine nzuri (Mt 12:23; Lk
8:15).
1. Mungu huwasambaza watu Wake duniani kama mbegu.
III. UHAKIKA WA KITUME: IMANI KATIKA MUNGU WA
MAVUNO (ms.6 “…atarudi kwa nyimbo za furaha, akiwa amebeba
miganda yake.”) A. Uhakika wetu uko katika Mungu wa mavuno.
1. Tunajua atakuwa mwaminifu kwa ahadi katika Neno Lake.
2. Anayo mamlaka na nguvu za kusababisha mavuno yatokee.
3. Atatengeneza mazingira ya kawaida na ya kiroho kwa ajili ya
mavuno.
B. Tuna uhakika kwamba mfumo wa mavuno wa Mungu unafanya kazi.
1. Tunaamini kwamba kupanda mbegu kuta leta mavuno.
2. Mbegu zinapopandwa na mvua zinyeshe, hakuna
kinachoweza kuzuia mbegu isichipuke na kuzaa.
Kumalizia, Na Wito Kwa Watu Kuja Mbele: 1. Basi, tutafanya nini wakati tutakapoikuta Sayuni (yaaniAfrika) ikiwa
magofu? Je, tutakimbia kwa sababu ya hofu? Hapana! Kwa machozi
tutapanda mbegu na kumwamini Mungu kwa ajili ya mavuno.
2. Njoo sasa, na ujitoe kwa ajili ya kupanda mbegu ya Injili.
[ GB ]
-
26
3 Mtangaze Kristo Kwa Viumbe Vyote
Ujumbe Wenyewe Katika Sentensi Moja: Ni lazima tumtangaze Kristo
kwa viumbe vyote.
Kusudi La Ujumbe: Watu wajitoena kuwa tayari kutii amri ya Kristo
kuhubiri habari njema kwa viumbe vyote.
Maandiko Ya Ujumbe: Marko 16:15-20
Utangulizi 1. Katika maandiko yetu, Yesu anatoa Agizo Lake Kuu.
2. Anatuamuru sisi kwenda “duniani kote na kuhubiri habari njema
kwa viumbe vyote.”
3. Katika andiko hili, tunajifunza kanuni tatu zenye nguvu sana juu
ya wajibu wetu wa kumtangaza Kristo kwa viumbe vyote:
I. KUMTANGAZA KRISTO KWA VIUMBE VYOTE NI AMRI
YA BWANA A. Yesu ametuamuru sisi kwenda “duniani kote na kuihubiri habari
njema kwa kila kiumbe” (Mk 16:15).
B. Amri hii ilitoka chumba cha utawala wa mbinguni, yaani, kutoka
mamlaka iliyo juu zaidi ya zote (Mt 28:18).
C. Yesu ameamuru, hivyo sisi ni lazima tutii.
1. Utii ni lazima (Yn 14:15, 31).
2. Utii ni fursa kwa ajili ya wana na binti wote wa Mungu.
II. KUMTANGAZA KRISTO KWA VIUMBE VYOTE NDIYO
MSINGI KWA AJILI YA WATU KUAMINI NA KUOKOKA A. Yesu aliendelea na kusema hivi: “Yeyote atakayeamini na
kubatizwa ataokoka, na yeyote asiyeamini atahukumiwa” (ms.16).
1. Kazi yetu si kuhukumu, bali kuwaita watu wamwamini Kristo
(Yn 3:16-17).
B. Ni lazima tuambie viumbe vyote kwamba Yesu anaokoa.
1. Yesu alitangaza Injili (Mk 1:15).
2. Paulo alitangaza Injili (Mdo 16:31).
3. Sisi pia ni lazima tuitangaze Injili.
C. Kama wakiamini, wataokoka.
1. “Yeyote aaminiye na kubatizwa, ataokoka” (ms.16).
2. Je, umemwamini Kristo ili upate wokovu?
a. Ikiwa bado, fanya hivyo sasa hivi!
b. Yeye “ana nguvu za kuokoa” wote waliitao jina Lake (Is 63:1; Rum 10:13).
III. KUMTANGAZA KRISTO KWA VIUMBE VYOTE NDILO
KUSUDI LA ISHARA NA MAAJABU
-
27
A. Yesu alizidi kuahidi kwamba, “Na ishara hizi zitawafuata wale
waaminio: Katika jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha
mpya; watashika nyoka kwa mikono yao; na watakapokunywa
sumu kali, haitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya
wagonjwa, nao watapona” (Mk 16:17-18).
B. Ni lazima twende katika nguvu za Roho Mtakatifu, tukimtazamia
Mungu kuithibitisha Injili kwa ishara na maajabu.
1. Yesu alihudumu katika nguvu ya Roho (Lk 4:18; Mdo 10:38).
2. Kama tutakuwa waaminifu kuitangaza Injili, Mungu
atathibitisha maneno yetu kwa ishara za kimuujiza, na
maajabu.
a. Alithibitisha mahubiri ya wanafunzi (Mk 16:20).
b. Alithibitisha mahubiri ya Paulo (Rum 15:18-19).
c. Atathibitisha mahubiri yetu.
C. Lakini, tusisahau kamwe kwamba kusudi la ishara ni kuithibitisha
Injili na kuwaelekeza watu kwa Kristo.
1. Filipo huko Samaria (Mdo 8:5).
2. Wakati Mungu anapotoa miujiza, hatupaswi kamwe kusahau
kusudi la hiyo miujiza—kuwaelekeza watu kwa Kristo.
Kumalizia, Na Wito Kwa Watu Kuja Mbele
1. Njoo sasa, na ujitoe kwa ajili ya kumtangaza Kristo kwa viumbe
vyote.
2. Njoo utiwe nguvu na Roho Mtakatifu.
[ EC ]
-
28
4 Tangaza Kwa Mataifa
Ujumbe Wenyewe Katika Sentensi Moja: Ni lazima tuwatangazie
mataifa kwamba Yesu Kristo ni Mwokozi na Mfalme.
Kusudi La Ujumbe: Kuwaita watu wajitoe ili kutangaza ujumbe wa
wokovu wa Mungu kwa mataifa.
Maandiko Ya Ujumbe: Zaburi ya 96:1-13
Utangulizi 1. Daudi aliandika hii Zaburi ya 96 wakati aliporudisha Sanduku La
Agano katika mji wa Yerusalemu (Linganisha 1Ny 16:7, 23-33 na
Zab 96:1-13).
2. Ni wimbo wa kimishenari wenye kusherehekea jinsi Yahwe
alivyo mfalme juu ya dunia yote.
3. Katika hii Zaburi, Mungu anatuita sisi kutoa matangazo ya aina
tatu kwa mataifa, kama ifuatavyo:
I. TUNATAKIWA KUYATANGAZIA MATAIFA KWAMBA
MUNGU NI MWOKOZI A. Daudi anaita dunia nzima imwabudu Yahwe (ms.1-2).
1. Hii ni sawa kwa sababu mataifa yote kwa kweli ni mali ya
Mungu.
2. Kama itikio la ukuu Wake, mataifa yote na watu wote
wanapaswa kumwimbia Mungu “wimbo mpya” (ms.1).
3. Siku moja, hilo litafanyika na kutimia (Uf 5:9-10).
B. Kama watu wa Mungu ambao ni wamishenari, kuabudu kwetu
lazima kugeuke kuwa ushuhuda, kama ifuatavyo:
1. Hatutakiwi tu kuabudu utukufu wa Mungu, bali tunatakiwa
“kuutangaza utukufu wake katikati ya mataifa…” (Zab 96:3).
2. Tunapaswa “kuzitangaza habari njema za wokovu Wake siku
hata siku” (ms.2).
C. Yesu ndiye ujumbe tunaotangaza kwa mataifa.
1. Tunapaswa kutangaza kwamba Yesu ndiye Mwokozi wa
binadamu wote.
2. Yeye ndiye aliyetupa sisi wokovu na kuawshinda maadui wa
roho zetu (Ef 1:19-23; Kol 2:13-15).
3. Sawa na mitume, kamwe tusiache kutangaza kwamba Yesu
ndiye Mwokozi (“Hatuwezi kuacha kusema!”—Mdo 4:20).
II. TUNATAKIWA KUYATANGAZIA MATAIFA KWAMBA
MUNGU NI MKUU
A. Tunamtumikia Mungu aliye mkuu.
1. Katika Zaburi ya 95 Daudi alizungumza juu ya ukuu wa
Mungu (ms.4-6).
-
29
2. Yeye “asifiwe sana” (ms 4). (Tazama pia Kut 15:11.)
3. Tunamtumikia Mwokozi aliye Mkuu:
a. Yesu ni “Mfalme wa wafalme, na Bwana wa mabwana”
(1Tim 6:15).
b. Yeye ni Mwokozi wa dunia yote! (Yn 4:44; 1Yn 4:14).
B. Ni lazima tutangaze ukuu Wake kwa mataifa.
1. Daudi anatuambia nini tufanye: tumtangaze Yeye! (ms.3).
2. Vile vile anatuambia kwa nini tufanye hivyo: Yeye ni mkuu!
(ms.4).
3. Yesu si “asifiwe sana” tu, bali pia anatakiwa atangazwwe
sana – kwa njia kubwa (Mk.15:15-16).
III. TUNATAKIWA KUYATANGAZIA MATAIFA KWAMBA
MUNGU NI MTAKATIFU A. Daudi anayaita mataifa “kumwabudu Bwana katika uzuri wa
utakatifu” (ms.9).
1. Hii ni mara ya pili anatuita tuabudu.
2. Hapa panafunua mapigo ya moyo wa kimishenari wa hii
Zaburi―makundi yote ya watu siku moja yatamwabudu
Mfalme (ms.10).
B. Je, Bwana anataka “sadaka” gani kutoka kwetu?
1. Anataka tumpe Yeye vyetu vyote (Mk 8:34-38).
2. Ni lazima tuishi mbele Yake katika “uzuri wa utakatifu” (ms. 9).
3. Yeye anakuja kwa ajili ya “kanisa tukufu, lisilo na doa wala
kunyanzi wala chochote cha namna hiyo,” kanisa ambalo ni
“takatifu, lisilo na mawaa” (Ef 5:27).
C. Ni lazima tutangaze utakatifu Wake katikati ya mataifa.
1. Ni lazima “tuseme katikati ya mataifa kwamba Bwana
anatawala.”
2. Kwa mara nyingine tena, kuabudu kunabadilika a kuwa
ushuhudiaji (ms.10).
a. “Jamaa za watu” sasa wanaitwa kumtangaza katikati ya
mataifa (ms.7).
b. Ukiri huu unatoa changamoto kwa miungu ile yote, na
watawala wengine wote pamoja na mamlaka zote – kuna
Mfalme mmoja tu.
Kumalizia, Na Wito Kwa Watu Kuja Mbele 1. Kristo ametuagiza tujiunge Naye kutangaza utawala wa Mungu
kwa mataifa (Mt 23:14; 28:19-20).
2. Njoo! Jitoe mwenyewe kwenda, kutoa na kuomba ili mataifa
yaweze kusikia juu ya wokovu wa Mungu ulio katika Yesu Kristo.
[ SE ]
-
30
5 Ihubiri Injili
Ujumbe Wenyewe Katika Sentensi Moja: Ni lazima tuihubiri Injili kwa
uaminifu, katika nguvu za Roho Mtakatifu.
Kusudi La Ujumbe: Ili waamini wajitoe wenyewe kuihubiri Injili na
ishara zikifuatana nao.
Maandiko Ya Ujumbe: Marko 16:15–20
Utangulizi 1. tumesoma Agizo Kuu la Yesu katika Marko 16.
2. Hapo, Yesu anatuambia sisi “kuhubiri habari njema,” yaani, ni lazima
tutangaze ujumbe wa Kristo kwa mkazo na kwa ushawishi mkubwa.
3. Kutokana na maandiko haya, tunaweza kujifunza masomo
muhimu matatu, kama ifuatavyo:
I. YESU AMETUAMURU TUHUBIRI A. Yesu ametuamuru sisi, “Nendeni…na kuhubiri.”
1. Soma tena Marko 16:15
2. Tunatakiwa kwenda kila mahali—na kwa kila mtu. 3. Tunatakiwa tupeleke na kutoa ujumbe wa Injili…
a. …kwamba Yesu alilipa gharama ya dhambi zetu na sasa
anatoa uzima wa milele kwa wote watakaomwamini Yeye.
b. Ni lazima hao watubu na kuziamini hizo habari njema (Mk
1:15).
B. Ni lazima tuhubiri Injili kwa sababu hatima ya milele ya watu
inahusika.
1. Yesu alisema hivi: “Kila aaminiye na kubatizwa, ataokoka, lakini
kila asiyeamini atahukumiwa” (ms.16).
2. Hatupaswi kupuuza hii kazi ambayo ni ya maana sana.
C. Basi, kila mwamini lazima aihubiri Injili.
1. Je, utatii amri ya Kristo kuihubiri Injili?
2. Lakini, Yesu hajatuamuru kuhubiri tu…
II. YESU AMETUTUMA NA KUTUPA NGUVU
A. Pamoja na amri ya Yesu kwamba tukahubiri, ipo ahadi ya nguvu.
1. Hebu soma ms. 17-18: “Na ishara hizi zitafuata…”
2. Ahadi hii ni kwa “yeyote aaminiye.”
3. Yaani, ni pamoja na wachungaji, wamishenari, waalimu wa
Shule ya Jumapili ya watoto na waalimu wa Uanafunzi na
Maandiko, washirika wote na kila kijana anayeamini. B. Ikiwa tutakwenda na kuamini, Kristo atalithibitisha Neno kwa
ishara zisizokuwa za kawaida.
1. Lakini kumbuka, ni lazima twende “katika Jina Lake,”yaani,
chini ya mamlaka Yake na kwa ajili ya utukufu Wake.
-
31
2. Hizo ishara za kimuujiza zitahusisha…
a. Ukombozi wa kiungu (“watatoa pepo”)
b. Usemaji wa kiungu (“watanena kwa lugha mpya”)
c. Uponyaji wa kiungu (“watu wagonjwa…. watapona”)
d. Ulinzi wa kiungu (“sumu ya nyoka…haitawadhuru”).
C. Hii nguvu isiyo ya kawaida, ya kuhubiri Injili, huja wakati
tumebatizwa na Roho Mtakatifu.
1. Amri ya mwisho ya Yesu, na ahadi (Soma Mdo 1:4-5, 8)
2. Wanafunzi waliipokea hiyo ahadi siku ile ya Pentekoste (2:4).
3. Walianza kuhubiri Injili huku ishara zikifuatana nao.
III. YESU ANATUTAZAMIA SISI KULIKUBALI NENO LA
MUNGU
A. Baada ya kupokea hiyo amri wanafunzi walikubali neno la Kristo
na kutii amri Yake.
1. Baada ya kutoa amri hiyo, Yesu alichukuliwa kwenda
mbinguni.
2. Mara ile ile wanafunzi wakatii. “Walitoka na kwenda kila
mahali, wakihubiri kote kote” (ms.20).
B. Mara wakagundua kwamba hawakuwa peke yao.
1. “Bwana alifanya kazi pamoja nao, akithibitisha Neno Lake
kwa ishara zilizoambatana nalo” (ms.20).
2. Yesu kwa Roho Wake alikuwa hapo pembeni yao.
3. Kwa sababu hiyo waliona matokeo ya kushangaza sana.
C. Leo hii, Yesu anataka kufanya hivyo hivyo kupitia kwa kila
mmoja wetu.
1. Yesu aliweka hilo wazi katika Yohana 14:12, kwamba:
“Yeyote anayeniamini mimi atafanya hayo ambayo nimekuwa
nikifanya. Tena atafanya hata makubwa zaidi ya haya, kwa
sababu mimi nakwenda kwa Baba.”
2. Si makubwa kwa ubora, bali makubwa ki-idadi.
D. Tunahitaji nini leo ili kufanya huduma kwa njia hii?
1. Ni lazima tu-uamini ujumbe.
2. Ni lazima tutiwe nguvu na Roho.
3. Ni lazima twende katika Jina la Yesu. 4. Ni lazima tuhubiri habari njema kwa ujasiri.
5. Ni lazima tumtazamie Mungu kulithibitisha Neno kwa ishara za kimuujiza zitakazofuata.
Kumalizia, Na Wito Kwa Watu Kuja Mbele 1. Njoo sasa, ujitoe kwa ajili ya kuhubiri Injili.
2. Njoo sasa, utiwe nguvu na Roho Mtakatifu.
[ JF ]
-
32
6 Yesu: Wa Kuigwa Katika Kuvuna Roho
Ujumbe Wenyewe Katika Sentensi Moja: Yesu ametupa sisi mfano wa
uvunaji roho tunaoweza kuufuata.
Kusudi La Ujumbe: Kuwatia moyo watu na kuwahamasisha wawe
wanaovuna roho kama Yesu.
Maandiko Ya Ujumbe: Yohana 4:4-42
Utangulizi 1. Yesu alikuwa mvuna roho wa kwanza, na aliye mkuu sana.
2. Katiki habari hii ya Mwanamke Kisimani, Yesu ametupa mfano
tunaoweza kufuata.
3. Ona mambo matatu jinsi Yesu alivyomvuta huyo mwanamke
kwake Yeye Mwenyewe:
I. ONA JINSI YESU ALIVYOMPA INJILI YULE MWANAMKE
A. Yesu alianza kwa ombi rahisi kwa yule mwanamke.
1. Alimwambia hivi: “Naomba unipe maji ninywe” (ms.7).
2. Hii ilikuwa ndoano, kitu cha kuanzishia mazungumzo.
3. Yule mwanamke alishangaa, kwa sababu Yesu alikuwa
mwanamume Myahudi, huku yeye akiwa mwanamke
Msamaria (ms.9).
4. Ni lazima tuanzishe kwa makusudi mazungumzo na watu
waliopotea.
B. Yesu alimshirikisha yule mwanamke habari njema.
1. Alimfunulia kwamba Yeye ndiye Masiya (ms.25-26).
2. Alimpa maji yaliyo hai (ms.13-14).
3. Kama Yesu, sisi nasi ni lazima tuwashirikishe Injili watu
waliopotea.
II. ONA JINSI MWANAMKE YULE ALIVYOMWITIKIA YESU A. Yule mwanamke Msamaria alikuwa na kiu, lakini si cha maji ya
kawaida tu.
1. Yesu alimwambia juu ya maji ya kiroho (ms.13-14).
2. Mwanamke alimwomba Yesu ampe hayo maji yaliyo hai
(ms.15).
B. Mwanamke alikuwa tayari kukubali kwamba alikuwa anaishi maisha
ya dhambi.
1. Yesu alifunua mtindo wake wa maisha ya dhambi (ms.16-18).
2. Mwanamke alikiri dhambi yake na kutubu (ms.17, 19). C. Yule mwanamke alitubu na kumwamini Yesu (ms.25-29).
1. Alikiri dhambi yake.
2. Aliweka Imani yake katika Kristo.
-
33
D. Yule mwanamke alipeleka ujumbe wa Yesu kwa wengine (ms.28-
30).
1. Wasamaria kutoka ule mji walimwamini Yesu kwa sababu ya
ushuhuda wa yule mwanamke (ms.30).
2. Sisi ni lazima tufanye kama yule mwanamke Msamaria.
III. ONA JINSI YESU ALIVYOWAFUNDISHA WANAFUNZI
WAKE
A. Yesu aliwafundisha juu ya umuhimu wa kuzivuna roho.
1. Kufanya mapenzi ya Baba na kuzivuna roho vilikuwa
“chakula” Chake―yaani, kitu kilichompa Yeye kuishi
(ms.31-34).
2. Ndivyo inavyotakiwa kuwa hata kwetu siku za leo.
3. Yesu ameagiza kwamba sisi twende na kufanya mataifa yote
kuwa wanafunzi (Mt 28:18-20).
4. Waliopotea hawawezi kuokoka kama hakuna atakayekwenda
na kuwaambia kuhusu Yesu (Rum 10:13-15).
B. Yesu aliwafundisha kuhusu uharaka katika kuzivuna roho.
1. Mavuno ni sasa—sio miezi minne kutoka sasa (ms.35).
2. Ni lazima tuvune roho sasa, kabla hatujachelewa milele (Yn
9:4).
C. Yesu aliwafundisha juu ya thawabu ya kuvuna roho.
1. Anayevuna roho hupata “malipo ya milele” (ms.36).
2. Apandaye na avunaye hufurahi kwa pamoja (ms.36-37).
3. Na mbingu hufurahi pamoja nao (Lk 15:10).
Kumalizia, Na Wito Kwa Watu Kuja Mbele: 1. Yesu ndiye mvuna roho tunayepaswa kumwiga. Ni lazima tufuate
hatua Zake.
2. Njoo sasa ujitoe kuwa mtu anayevuna roho.
[ CK ]
-
34
7 Mambo Manne Ya Lazima Kwa
Ajili Ya Mavuno
Ujumbe Wenyewe Katika Sentensi Moja: Ikiwa tunataka kukamilisha
uvunaji, ni lazima kwa ujasiri mkubwa tukubaliane na “Mambo
Manne Ya Lazima Kwa Ajili Ya Mavuno”, ya Kristo.
Kusudi La Ujumbe: Watu wapate kujitoa wenyewe kumtangaza Kristo
kwa mataifa katika nguvu za Roho Mtakatifu.
Maandiko Ya Ujumbe: Luka 24:33-49
Utangulizi 1. Kuna vitu ambavyo ni lazima... na vingine ambavyo ni lazima
kidogo ... na vitu vingine ni vya lazima kabisa!
2. Yesu anazungumzia mambo manne ya lazima yanayohusiana na
mavuno.
3. Ona maneno katika mstari wa 46 "basi, ikawa lazima" 4. Neno la Kiyunani linalotafsiriwa “lazima” (edei) linamaanisha
“ulazima ulio dhahiri” au “ulazima unaofunga” (kwa mujibu wa
Kamusi ya Kiyunani ya Vine).
5. Basi, Yesu anadhihirisha lazima nne, zenye kufunga wahusika,
kuhusiana na mavuno—yaani vitu vine ambavyo ni lazima kwa
ajili ya wokovu wa mwanadamu:
I. ILIKUWA NI LAZIMA KABISA KWA YESU KUFA MSALABANI “Ilimpasa Kristo kuteswa…”
(ms.46).
A. Kanuni ya milele: “Pasipo damu kumwagika…hakuna ondoleo [la
dhambi]” (Ebr 9:22).
B. Pale msalabani, Kristo alilipa gharama kwa ajili ya watu wote.
1. “Bwana ameweka juu yake maovu yetu wote” (Isa 53:6).
C. Bila msalaba = Hakuna ukombozi = Hakuna mavuno.
II. ILIKUWA NI LAZIMA KABISA KWA YESU KUFUFUKA
KUTOKA KWA WAFU “Ilimpasa Kristo…afufuke toka kwa
wafu…” (ms.46)
A. Kristo alijenga huduma Yake yote kwenye tukio la ufufuo.
1. Mfano: Wakati waliokuwa wanamshutumu walipomwuliza,
“Tuonyeshe ishara”, Yeye aliwaambia juu ya kufufuka
Kwake (Mt 9:38-40). 2. Alijenga yote aliyosema na kudai kwenye kufufuka Kwake.
B. Angalia Paulo anavyosema kuhusu ufufuo wa Kristo:
1. “Ikiwa Kristo hajafufuliwa…. Kuhubiri kwetu hakuna faida;
Imani yetu ni bure; sisi ni mashahidi wa uongo; na bado tumo
katika dhambi zetu” (1Kor 15:14-17).
-
35
2. Mtu ni lazima aamini kuhusu ufufuo ili aweze kuokoka
(Rum 10:9-10).
C. Pasipo ufufuo: Hakuna ukombozi, hakuna mavuno.
III. NI LAZIMA KABISA INJILI IHUBIRIWE KWA MATAIFA
YOTE. “Ilikuwa lazima…toba na ondoleo la dhambi vihubiriwe kwa Jina Lake kwa mataifa yote…” (ms.46-47).
A. Matokeo ya zile lazima mbili za kwanza husimama au kuanguka
kwenye lazima ya tatu.
1. Ondoa yoyote moja, na mpango wa Mungu wa ukombozi
unaharibika.
2. Ilikuwa ni lazima kabisa kwa Yesu kuteseka, lakini hiyo
haikutosha…Alipaswa afufuke toka kwa wafu. Lakini cha
kushangaza, hata hiyo haitoshi…
3. Ni lazima vile vile kwamba watu wasikie juu ya hayo na
kuamini juu ya kifo Chake na kufufuka Kwake (Rum 10:9-
10).
4. Hebu soma na kueleza kidogo Warumi 10:13-14.
B. Tumepata fursa ya kuwa na sehemu katika mpango wa Mungu wa
ukombozi:
1. Yeye tu ndiye angeweza kuteseka msalabani, na ni Mungu tu
ndiye angeweza kumfufua toka kwa wafu; lakini, kazi ya
kumtangaza kwa mataifa tumepewa sisi kanisa Lake.
2. Kwa hiyo, Kristo ametupa sisi Agizo: Mk16:15-16.
IV. NI LAZIMA KABISA KWA KANISA KUTIWA NGUVU NA
KUWEZESHWA KWA ROHO MTAKATIFU KUIFANIKISHA ILE KAZI “…nanyi ni mashahidi…lakini kaeni humu mjini, hata
mvikwe uwezo utokao juu” (ms.48-49). A. Ili kanisa liweze kufanikisha hii kazi ya kuhubiri Injili kwa
mataifa, ni lazima kutiwa nguvu na Roho Mtakatifu.
1. Hii ndiyo lazima ya nne kwa ajili ya mavuno.
B. Kabla ya Yesu kupaa mbinguni, aliliachia kanisa kazi, amri na
hadi (Mdo 1:4-8).
1. Kazi: “Mtakuwa mashahidi wangu…” (ms.8b)
2. Amri: “Mngojeni…Roho Mtakatifu” (ms.4-5)
3. Ahadi: “Mtapokea nguvu…” (ms.8a)
C. Ni lazima tutiwe nguvu na Roho.
Kumalizia, Na Wito Kwa Watu Kuja Mbele 1. Ni lazima tukubali na kushika yale mambo manne ambayo ni
“lazima kwa ajili ya mavuno.”
2. Njoo sasa ili utiwe nguvu na Roho na ujitolee kwa
upya kwa ajili ya mavuno. [ DRM ]
-
36
8 Injili Hii Itahubiriwa
Ujumbe Wenyewe Katika Sentensi Moja: Kazi ya msingi ya kanisa ni
kuhubiri Injili kwa mataifa yote kabla Yesu hajarudi mara ya pili.
Kusudi La Ujumbe: Watu waweze kujitoa kwa ajili ya kupeleka Injili
kwa mataifa yote.
Maandiko Ya Ujumbe: Mathayo 24:3-14 (mkazo ni kwenye ms.14)
Utangulizi
1. Angalia kwa makini swali la wanafunzi kwa Yesu:
a. “Nini itakuwa ishara [katika umoja] ya kuja kwako, na ya mwisho wa dunia?” (Mt 24:3).
b. Yesu anaanza jibu Lake kwa kueleza sifa za mwenendo wa
kipindi cha wakati huu.
1) Vitu ambavyo kimsingi si ishara za wakati wa mwisho. 2) Stanley Horton, akitoa mchango wake kuhusu jibu la
Yesu katika mstari wa 3, aliandika hivi, “Basi Yesu
alichukua muda kuwaonya wanafunzi Wake kuhusu vikwazo
ambavyo vingeweza kuwaondoa kwenye shughuli yao
kubwa ya kueneza Injili.” (Katika kitabu chake kiitwacho
The Promise of His Coming, uk.33) 2. Mwisho, katika mstari wa 14, Yesu anajibu swali lao kama
ifuatavyo: “Injili hii ya ufalme itahubiriwa duniani kote…”
a. George Eldon Ladd anasema juu ya mstari huu, kama
ifuatavyo: “pengine ndiyo mstari mmoja wa muhimu sana
katika Neno la Mungu.”
b. Ndiyo kiini cha kuelewa historia.
c. Katika Mt 24:14 Yesu anazungumzia dhana tatu muhimu sana
kuhusu ufalme wa Mungu:
I. UJUMBE WA UFALME
A. Yesu anaanza ahadi hii hivi: “Hii Injili ya ufalme…”
1. Ona maneno haya: “Hii Injili…” 2. Yaani, ni Injili ile ile ambayo ilihubiriwa na Yeye na mitume.
3. Hakuna Injili nyingine. (Soma Gal. 1:6-9.)
B. Hii Injili aliyosema Yesu ni ipi? 1. Hii Injili ya ufalme ni ujumbe kwamba Yesu alikuja kujenga
ufalme wa Mungu duniani.
2. Ni ujumbe wa kifo cha Yesu na kufufuka Kwake.
a. Soma 1Kor 15:1-4; 1Kor 2:1-2: “Yesu Kristo…amesulubiwa” 3. Injili ya ufalme inahusisha onyesho la mamlaka ya ufalme na nguvu.
a. Mt 12:28: "Kama mimi kwa Roho wa Mungu ninatoa ..."
b. Lk 9:1-2 “Aliwapa nguvu…aliwatuma…”
c. 1Kor 2:4: Kwa maneno na katika maonyesho.
-
37
4. Hii Injili ya ufalme inawaita watu “kutubu na kuamini habari njema” (Mk 1:5).
C. Tunapaswa kuanzisha mfumo huu katika shughuli zetu zote za umisheni.
II. UTUME WA UFALME
A. Katika Mt 24:14 Yesu anaendelea kusema hivi: “…itahubiriwa
duniani kote kuwa ushuhuda kwa mataifa yote…”
1. Utume wa kanisa ni kushuhudia ulimwengu.
2. Linganisha Mt 24:14 na Mt 28:18-20.
B. Katika Mt 24:14, Yesu anadhihirisha upana wa utume: 1. Sisi tunatakiwa kwenda “duniani kote.” a. Neno “Dunia” kwa Kiyunani oikoumeme, maana yake ni
dunia inayokaliwa na watu.
b. Matendo 1:8 inataja “mwisho wa nchi.”
2. Sisi tunatakiwa kuwa “mashahidi kwa mataifa yote.” a. “Mataifa” kwa Kiyunani ethne, yaani makabila, au
makundi ya watu.
C. Yesu anatuhakikishia mafanikio ya hakika. 1. "Hii Injili...ita hubiriwa. Itatokea! 2. Swali, basi, siyo “Je, itatimia?” bali ni “Je, sisi tutakuwa na
sehemu katika hili?”
3. Biblia inatupa picha kuhusu wakati ujao, yaani mpaka
mbinguni, kama ifuatavyo:
a. Hapo tunawaona watu kutoka “kila kabila na lugha na
jamaa na taifa” (Ufu 5:9, pia ona Ufu 7:9).
4. Sisi tunaweza kuwa na sehemu katika huu ukusanyaji mkuu wa
mavuno makubwa sana ya roho za watu.
III. KUKAMILIKA KWA UFALME
A. Yesu anamalizia Mt 24:14 kwa kusema, “…ndipo mwisho
utakapokuja.”
1. Je, mwisho ni lini?
2. Baada ya hii Injili ya ufalme kuhubiriwa duniani kote kuwa
kama ushahidi kwa kila taifa.
3. MANENO YA Stanley Horton, “Mungu atakuwa na watu
waliokombolewa kwa damu ya Yesu ‘kutoka kila…taifa…’
Mpaka atakapowapata, mwisho hautakuja. Basi, tunachohitaji,
si kujali zaidi juu ya kitakachotokea, bali kujali juu ya
kuenezwa kwa Injili.” (Katika kitabu kiitwacho Promise, uk.33) B. Tunaweza kusaidia kuharakisha “kasi” ya kurudi kwa Bwana kwa
kuihubiri Injili katika dunia yote. (Soma 2Pet 3:12.)
Kumalizia, Na Wito Kwa Watu Kuja Mbele
Njoo sasa ujitoe mwenyewe kwa Kristo na utume Wake. [ DRM ]
-
38
9 Sisi Hatutaacha Kutangaza
Ujumbe Wenyewe Katika Sentensi Moja: Ni lazima tuamue kutangaza
kwa uaminifu ujumbe wa Kristo katika nguvu ya Roho Mtakatifu.
Kusudi La Ujumbe: Kwamba, watu wajikabidhi na kujitoa wenyewe kwa
Kristo na kutangaza Injili Yake.
Maandiko Ya Ujumbe: Matendo 4:1-20 (angalia mstari wa 8 na 20)
Utangulizi 1. Wakati mwingine wachungaji hujaribiwa kuhubiri jumbe
zinazopendwa, lakini za hali ya chini, zisizo na uzito.
a. Matokeo yake ni kwamba wanaacha ujumbe wa kweli wa Injili.
b. Leo tunajifunza somo muhimu sana kutoka kwa Petro na
Yohana.
2. Simulia hadithi ya kukamatwa na ukiri wa akina Petro na Yohana
katika Matendo sura ya 4. (Wakati walipoagizwa kuacha kuhubiri
katika jina la Yesu, walijawa na Roho Mtakatifu na kujibu hivi:
“Hatuwezi kuacha kusema juu ya Kristo!”)
3. Tutafanya vizuri sana kujitoa kwa namna nne:
I. Kujitoa Namba 1: “HATUTAACHA KUMTANGAZA KRISTO
KWA WALIOPOTEA” A. Cha kusikitisha ni kwamba, makanisa mengi yanayojiita “ya
KiPentekoste” yameachwa ujumbe wa Kristo kwa kuhubiri “Injili
zingine” (angalia Gal 1:6-9).
B. Lakini, wakati walipoamriwa kuacha kumhubiri Kristo, mitume
walijibu hivi: “Hatuwezi kuacha kusema juu ya Kristo!”
C. Kristo alikuwa ndiyo ujumbe mmoja wa kanisa katika kitabu cha
Matendo.
1. Filipo alikwenda Samaria na kumhubiri Kristo (Mdo 8:5).
2. Paulo alimhubiri Kristo kwa askari jela wa Filipi (Mdo 16:30+).
3. Petro: “Wala hakuna wokovu katika mwingine yeyote…”
(Mdo 4:12).
D. Kamwe tusiache kuhubiri ujumbe wa Kristo.
II. Kujitoa Namba 2: “HATUTAACHA KUHUBIRI KATIKA
NGUVU YA ROHO MTAKATIFU” A. Mitume na wahubiri katika kitabu cha Matendo walimtangaza
Kristo katika nguvu ya Roho.
1. Petro Siku ya Pentekoste (Mdo 2:4, 14, 22-24). 2. Petro tena (Mdo 4:8-12).
B. Sisi pia ni lazima tumtangaze Kristo katika nguvu za Roho Mtakatifu.
1. Amri ya Yesu ya mwisho ni hii: Mdo 1:4-5: “Msiondoke Yerusa-
lemu, bali ingojeeni ile zawadi iliyoahidiwa na Baba yangu…”
-
39
2. Ahadi ya mwisho ya Yesu ni hii: Mdo 1:8: “Ninyi mtapokea
nguvu…”
3. Mwombe Roho aje juu yako na akujaze sasa hivi.
III. Kujitoa Namba 3: “HATUTAACHA KUPANDA MAKANISA YA
KIMISHENARI, YALIYOTIWA NGUVU NA ROHO
MTAKATIFU” A. Katika kitabu cha Matendo, mitume walipanda makanisa ya
kimishenari yaliyotiwa nguvu na Roho.
1. Yaani, makanisa ambayo kwa haraka yangepanda makanisa
mengine ya kimishenari, yaliyotiwa nguvu na Roho
Mtakatifu.
2. Kama kanisa la Antiokia (Mdo 11:19-21).
3. Matokeo ya hilo ni kwamba makanisa yaliongezeka sana
katika Dola ya Rumi.
B. Sisi pia ni lazima tupande makanisa ya kimishenari yaliyotiwa
nguvu na Roho Mtakatifu.
1. Yaani, makanisa yaiyotiwa nguvu na Roho Mtakatifu…
a. …na karibuni yatapanda makanisa mengine ya aina hiyo hiyo.
b. …na yatajihusisha katika kutuma wamishenari.
2 Makanisa aina hii hayatawezekana pasipo mpango wa
makusudi, uliochambuliwa vizuri sana wa kuyapanda.
IV. Kujitoa Namba 4: “SISI HATUTAACHA KUHAMASISHA
MAKANISA YETU KWA AJILI YA UMISHENI”
A. Mitume walipowahamasisha makanisa ya kimisheni
yaliyowezeshwa na Roho Mtakatifu, walifanya hivyo kwa kusudi
la kuieneza Injili “katika Yerusalemu, na Uyahudi yote, mpaka
miisho ya dunia” (Mdo 1:8).
1. Kila kanisa la mahali pamoja lazima lihamasishwe kushiriki
katika kazi ya umisheni.
2. Kila aaminiye ni lazima afundishwe juu ya wajibu wake
binafsi wa kushiriki katika umisheni.
B. Wote ni lazima tushiriki katika umisheni kwa njia tatu:
1. Ni lazima wote twende kwa waliopotea na kuwashirikisha Injili. 2. Ni lazima wote tuombe kwa ajili ya mavuno nyumbani na
nchi za ng’ambo.
3. Ni lazima wote tutoe kwa ajili ya kazi ya umisheni.
Kumalizia, Na Wito Kwa Watu Kuja Mbele 1. Njoo ujitoe mwenyewe kwa Kristo na kwenye kutangaza Injili
Yake kwa waliopotea.
2. Njoo utuwe nguvu na Roho ili uweze kuitangaza Injili.
[ DRM ]
-
40
10 Kuitangaza Kikamilifu Injili Ya Kristo
Ujumbe Wenyewe Katika Sentensi Moja: Tunawajibika “kuitangaza
kikamilifu Injili ya Kristo” kwa wote.
Kusudi La Ujumbe: Kwamba Wakristo waweze kujitoa wenywe kikami-
lifu kabisa kuitangaza kikamilifu Injili nyumbani na duniani kote.
Maandiko Ya Ujumbe: Warumi 15:15-21
Utangulizi 1. Katika mstari wa 19 Paulo anatamka hivi: “Mimi nimeitangaza
kikamilifu kabisa Injili ya Kristo.”
2. Basi, nini maana ya “kutangaza kwa ukamilifu” Injili?
3. Kutokana na mstari wetu, tunajifunza kwamba sisi tunakuwa
tumeitangaza Injili kikamilifu wakati tu tunapokuwa tumefanya mambo matatu:
Kwanza, tunakuwa tumeitangaza Injili kikamilifu…
I. WAKATI TUMEKWISHA KUTANGAZA KWA UWAZI NA
USAHIHI KABISA UJUMBE WA YESU KRISTO
A. Sisi kama watu wa Mungu ambao ni wamishenari, wajibu wetu
wa msingi ni kuutangaza ujumbe wa kufa kwa Kristo msalabani,
na ufufuo Wake wa ushindi kutoka kaburini.
1. Paulo alielewa huu wajibu mkubwa wa kipekee.
a. Aliwaambia Warumi (ms.19): “Mimi nimehubiri
kikamilifu kabisa…”
b. Akaendelea hivi (ktk ms.20): “Siku zote imekuwa shauku
yangu kuihubiri Injili…”
2. Alifafanua Injili kuwa ni ujumbe wa Kristo kufa, kuzikwa, na
kufufuka. (Soma 1Kor 15:1-4.)
3. Ni “nguvu ya Mungu iletayo wokovu.” (Soma War 1:16-17.)
B. Kutangaza kikamilifu Injili pia ni pamoja na kuwaita watu
wapokee Imani na toba (Mk 1:15; Mdo 20:21).
C. Kwa ujasiri kabisa, ni lazima tuitangaze “injili kamili”…
1. Yesu anaokoa! Yesu anaponya! Yesu anabatiza watu kwa
Roho Mtakatifu! Yesu anakuja tena!
Halafu, tunakuwa tumeitangaza Injili kikamilifu…
II. WAKATI TUNAPOKUWA TUMEONYESHA NGUVU YA
INJILI KWA “ISHARA NA MIUJIZA KWA NJIA YA NGUVU
ZA ROHO MTAKATIFU” A. Kuitangaza Injili kikamilifu ni zaidi ya kuzungumza tu: ni pamoja na
kuonyesha nguvu za ufalme. (Soma 1Kor 4:20.)
1. Paulo aliwaambia Warumi kwamba aliweza kuwavuta watu
wa Mataifa “kwa nguvu za ishara na miujiza, kupitia nguvu za
Roho” (ms.18-19).
-
41
2. Mahali pengine, aliwakumbusha Wathesalonike jinsi
ambavyo Injili iliwafikia. (Soma 1The 1:5.)
3. Aliendelea kuwakumbusha Wakorintho…(Soma 1Kor 2:4.)
4. Sisi pia tutazamie Mungu kuthibitisha kutangazwa kwa Injili
na “ishara zinazofuatana” (Mk 16:15-20).
B. Mfano wa Agano Jipya unahusisha kutangazwa kwa Injili na
maonyesho:
1. Yesu alionyesha mfano (Mt 4:23).
2. Filipo alifuata mfano wa Yesu (Mdo 8:5-7).
3. Paulo alitumia mbinu hiyo hiyo huko Listra (Mdo 14:7-10).
C. Kama na sisi tutafuata mfano huo wa Agano Jipya, inabidi tufanye
mambo mawili:
1. Ni lazima tutiwe nguvu kwa Roho Mtakatifu (Lk 24:49; Mdo 1:8).
2. Ni lazima tufanye mambo kwa Imani jasiri, kama Paulo huko
Listra (Mdo 14:9-10).
Mwisho, tunakuwa tumeitangaza Injili kikamilifu tu…
III. WAKATI TUMEPELEKA INJILI HADI MAHALI AMBAPO
KRISTO HAJULIKANI
A. Ona jinsi ambavyo Paulo anaunganisha “kutangaza Injili
kikamilifu” na kuhubiriwa kwa Injili “mahali ambapo Kristo
hajawahi kujulikana”:
1. “Kwa hiyo, kutoka Yerusalemu mpaka maeneo yote
kuzunguka Iliriko, nimeitangaza Injili ya Kristo kikamilifu.
Imekuwa shauku yangu kila mara kuihubiri Injili mahali
ambapo Kristo hakuwa anajulikana…” (ms.19-20).
2. Halafu ananukuu maneno ya nabii Isaya : “Wale ambao
hawakuambiwa juu yake wataona, na wale ambao
hawajasikia, wataelewa” (ms.21; rejea Isa 52:15).
B. Yesu anatutazamia kwenda “duniani kote na kuhubiri habari
njema kwa viumbe vyote” (Mk 16:15).
1. Sisi wote tunashiriki katika wajibu wa kumtangaza Kristo
kwa mataifa.
2. Wengine lazima waende, wengine lazima watume, lakini wote
lazima washiriki (Rum 10:13-15).
3. Sisi hatuja“tangaza kikamilifu Injili ya Kristo” mpaka
tutakapokuwa tumeshirikisha habari za Kristo kwa wale
ambao hawajawahi kusikia hizo habari.
Kumalizia, Na Wito Kwa Watu Kuja Mbele
Njoo, jitoe kikamilifu wewe mwenyewe ili kuhubiri Injili kwa
ukamilifu kabisa. Njoo utiwe nguvu na kuwezeshwa na
Roho Mtakatifu [ DRM ]
-
42
11 Tumaini Moja Kwa Ajili Ya Dunia
Ujumbe Wenyewe Katika Sentensi Moja: Ni lazima tutangaze ujumbe
wa matumaini yaliyomo katika Kristo kwa dunia, kwa nguvu za Roho
Mtakatifu.
Kusudi La Ujumbe: Ni ili wasikilizaji wajazwe na Roho Mtakatifu, na
kujitoa kutangaza ujumbe wa msalaba kwa watu wote.
Maandiko Ya Ujumbe: 1 Wakorintho 1:17-25
Utangulizi 1. Njia pekee ya dunia kumjua Mungu ni kwa kanisa lililojaa nguvu
za Roho linapotangaza Injili ya Kristo.
2. Katika 1Kor 1-2, Paulo anatoa hoja yenye nguvu na kufafanua
zaidi kweli hii.
I. PAULO ANATOA HOJA KWAMBA UJUMBE WA MSALABA
NDIYO TUMAINI MOJA KWA AJILI YA DUNIA (1Kor 1:17-
25)
A. Kuhubiri ujumbe wa msalaba huonekana upumbavu kwa dunia.
1. Ni “upumbavu,” tena ni “kikwazo” (1Kor 1:23).
B. Watu wa kimwili hujitazama wenyewe na uwezo wao ili kupata
majibu kwa matatizo yao mazito na ya ndani sana.
1. Tangu mwanzo wa wakati, watu wamejaribu kutafuta viongozi
sahihi, na mipango mizuri ya kiuchumi, kijamii na kielimu.
2. Hiyo mipango yote (hata ile iliyo bora kabisa) hatimaye
hushindwa.
a. Watu wasiokuwa wa kiroho hujaribu kutibu dalili huku
wakipuuzia mzizi unaosababisha matatizo yao.
b. Ugonjwa halisi ni dhambi, na dawa pekee ya dhambi ni
Kristo.
c. Mwanadamu hataweza kamwe kupata majibu yeye peke
yake (1Kor 1:20).
C. Kinacho-onekana kwa dunia kuwa upumbavu na udhaifu kwa
kweli ndiyo hekima ya Mungu na nguvu Yake kuokoa (ms. 24-25).
1. Sisi hupatanishwa na Mungu kupitia toba na kumwamini Kristo.
2. Kristo kweli ndiyo Tumaini Moja Tu kwa dunia.
II. PAULO ANAENDELEA KUTOA HOJA KWAMBA NI LAZIMA
TUTANGAZE UJUMBE WA MATUMAINI KATIKA KRISTO
KWA UAMINIFU A. Huko Korintho, Paulo kwa makusudi kabisa analenga kwenye
kutangazwa kwa ujumbe wa Yesu Kristo aliyesulubiwa.
1. Soma 1Kor 2:1-2.)
2. Alichagua kutotangaza ujumbe mwingine wowote.
-
43
3. Aliandika 1Wakorintho kwa sababu kanisa lilikuwa
linapoteza mwelekeo wa ujumbe wa Injili.
4. Kanisa hilo Lilikuwa linapoteza uwezo wake wa kuwa shahidi
wenye nguvu sana kwa ajili ya Kristo.
B. Kanisa la Korintho – kama kanisa linguine lolote – lilikuwa
limeitwa kuendeleza utume wa Mungu kupitia ushuhuda uliotiwa
nguvu na kuwezeshwa na Roho Mtakatifu.
1. Kila kanisa la mahali pamoja limeitwa kuwa jeshi la
kimisheni.
5. Paulo akuwa anajali juu ya kanisa pamoja na uwezo wake wa
kutekeleza utume wa Mungu.
C. Kwa hiyo Paulo aliwasihi waweke kando tofauti ndogo ndogo na
kuungana kwenye ujumbe wa Injili (1Kor 1:10).
III. MWISHO, PAULO ANATOA HOJA KWAMBA, ILI KUWEZA
KUTANGAZA KWA UFANISI UJUMBE WA MATUMAINI, NI
LAZIMA TUTEGEMEE NGUVU YA ROHO MTAKATIFU
(1Kor 2:3-5, 10-14)
A. Nguvu za Roho Mtakatifu zilimwezesha Paulo kufikisha kwa ngu-
vu sana ujumbe wa Kristo kwa Wakorintho. (Soma 1Kor 2:3-5.)
B. Kama Paulo, sisi pia tunahitaji nguvu za Roho ili kuweza
kutangaza ujumbe wa Kristo katika mazingira yetu.
1. Tunamhitaji Roho ili kuelewa ujumbe husika (1Kor 2:10, 12).
2. Tunamhitaji Roho ili kufundisha ujumbe husika (ms.13).
3. Tunamhitaji Roho kuonyesha uhalisi wa ujumbe husika (ms.4-5).
4. Tunamhitaji Roho kuaminisha na kufungua mioyo ili kupokea
ujumbe husika.
C. Korintho ilianzishwa kwa uamsho mkubwa, wenye madhihirisho
ya nguvu za Roho Mtakatifu.
1. Lakini wakaanza kujikwaa na kuangalia mambo yao ya
binafsi.
2. Paulo anashughulikia baadhi ya vitu vilivyowaondoa kwenye
kujali mambo muhimu baadaye katika 1Kor.
D. Katika Matendo 1:8, Yesu alieleza nguvu inayohitajika kumtangaza
Kristo.
Kumalizia, Na Wito Kwa Watu Kuja Mbele Njoo uwezeshwe na Roho Wake ili usaidie katika kutimiza huo utume.
[ MRT ]
-
44
-
45
-
46
12 Amri Ya Kwanza Ya Agizo Kuu: “Ombeni!” ~ Amri Za Agizo Kuu ~
Ujumbe Wenyewe Katika Sentensi Moja: Ili kushiriki kwa ufanisi
mkubwa katika Agizo Kuu, ni lazima tutimize amri ya maombi.
Kusudi La Ujumbe: Watu wajitoe kuomba kwa ajili ya mavuno.
Maandiko Ya Ujumbe: Mathayo 9:35-38
Utangulizi
1. Katika andiko letu la ujumbe, Yesu alisema kuhusu shamba
laenye mavuno. (Soma ms. 35-37.)
a. Watu walikuwa “wananyanyasika, na wasio na msaada.”
b. Kwa sababu hiyo, Yesu anawaagiza wanafunzi Wake hivi:
“Ombeni!” (v.38).
2. Ujumbe huu ni kuhusu Njia Tano za sisi kuombea mavuno:
I. OMBENI KWA AJILI YA NGUVU ZA MAVUNO (Mt 9:35-38)
A. Yesu aliwapa wanafunzi Wake maagizo dhahiri kuhusu maombi,
hivi:
1. Walitakiwa waombe kwa “Bwana wa Mavuno.” 2. Walitakiwa kuomba kwa ajili ya “watenda kazi wengine waingie
katika shamba Lake la mavuno.”
3. Kwa maneno mengine, walitakiwa waombe kwa ajili ya
Nguvu Ya Mavuno.
B. Kuvuna mavuno kunahitaji rasilmali.
1. Inahitajika rasilmali watu—Kwa hiyo, ni lazima tuombe.
2. Inahitajika rasilmali fedha —Kwa hiyo, ni lazima tuombe.
C. Nguvu ya Mavuno pia inahitaji upangaji kimkakati.
1. Ni lazima tushirikiane na Roho Mtakatifu ili kuwapanga
watenda kazi wa mavuno mahali anapotaka waende.
2. Basi, ni lazima tuombe hekima na maongozi.
II. OMBENI KWA AJILI YA MASHAMBA YA MAVUNO (Soma Yn 4:35-36.)
A. Yesu aliwaambia wanafunzi Wake, “Yatazameni mashamba.”
1. Aliwaambia kwamba mavuno “ni mengi” (Mt 9:37) na
“yameiva” (Yn 4:35)
2. Maneno Ni mengi ni maelezo kuhusu ukubwa wake—na neno
yameiva ni maelezo juu ya “utayari” wake. B. Kwa sababu mavuno yameiva, muda ni kitu muhimu cha
kuzingatia, yaani, kuna uharaka.
1. Ni lazima tuvune mavuno kabla hatujachelewa sana.
C. Kwa hiyo, ni lazima kuomba kwa ajili ya shamba la mavuno.
-
47
III. OMBENI KWA AJILI YA KITAKACHOPATIKANA ( Ufu 5:9.)
A. Yohana aliona wakati ujao na kuona kitakachokuwa kimepatikana
katika mavuno makuu ya Mungu siku za mwisho.
1. Aliona kundi kubwa la watu “kutoka kila kabila na lugha na
jamaa na taifa” (Ufu 5:9).
B. Watafiti wanakadiria kwamba kuna makundi ya watu kiasi cha
16,000 na zaidi duniani.
1. Kila kikundi kimoja katika hivi ni lazima kiwakilishwe
miongoni mwa hao waliokombolewa.
2. Mpaka sasa, kiasi cha makundi ya watu 6,600 na zaidi
hayajafikiwa.
3. Ni lazima tupige hatua ya kuwafikia wale wote ambao bado
hawajafikiwa.
C. Ni lazima tuombe kwamba kanisa lijizatiti kufikia makundi ya
watu ambao hawajafikiwa.
IV. OMBENI DHIDI YA ADUI WA MAVUNO (Soma Mt 13:19; 28; 2Kor 4:4)
A. Adui wa mavuno ni Shetani. (Soma Mt 13:19, 28.)
1. Sisi tuko katika vita ya kiroho (Efe 6:12).
B. Adui hupinga mavuno kwa njia tatu:
1. Yeye “huondolea mbali” nguvu za ile mbegu ya Injili (ms.19).
2. Hupanda magugu (watenda maovu) kati ya ngano (Mt 13:25).
3. Hupofusha akili za wasioamini (2Kor 4:4).
C. Ni lazima tupigane vita za kiroho kwa silaha za kiroho (2Kor 10:4).
1. Silaha mojawapo ni maombi (Efe 6:18).
V. OMBENI UWEZO WA KUVUNA MAVUNO (Soma Mdo 1:8.)
A. Ni lazima tuwe na nguvu ya Mungu ili kuweza kufanya na
kufanikisha kazi ya Mungu.
1. Yesu aliahidi nguvu kwa ajili ya kushuhudia (Mdo 1:8).
2. Tunapokea nguvu ya Roho wakati tunapobatizwa katika Roho
Mtakatifu (Mdo 2:4).
3. Mavuno ya Agano Jipya yalianza siku ile ya Pentekoste (Mdo
2:41).
B. Ili shughuli ya kimisheni ya kanisa ifanikiwe, ni lazima itiwe
nguvu na kuwezeshwa na Roho Mtakatifu.
C. Nguvu ya Roho inapatikana kwa maombi.
1. Yesu alisema, “Ombeni nanyi mtapewa” (Lk 11:9). 2. Nguvu ya Roho pia hudumishwa kwa maombi.
Kumalizia, Na Wito Kwa Watu Kuja Mbele
1. Kuombea umisheni si jambo la hiari. Ni amri! [ UA ]
-
48
13 Amri Ya Pili Ya Agizo Kuu: “Nendeni!” ~ Amri Za Agizo Kuu ~
Ujumbe Wenyewe Katika Sentensi Moja: Ni lazima twende na
kumtangaza Kristo kwa mataifa katika nguvu za Roho Mtakatifu.
Kusudi La Ujumbe: Watu waweze kujitoa wenyewe kutii amri ya Kristo
ya kwenda kwa mataifa.
Maandiko Ya Ujumbe: Mathayo 28:18-19; na Mathayo 21:28-31
Utangulizi 1. Mistari yetu inazungumzia wajibu wetu kama wanafunzi wa
Kristo kwenda kwa mataifa.
2. Andiko la kwanza linajulikana kama “Agizo Kuu.”
3. Andiko la pili ni ule mfano (hekaya) wa watoto wawili. (Simulia
hadithi yenyewe)
a. Mtoto wa kwanza alisema hatakwenda, halafu akatubu, na
akaenda.
b. Mtoto wa pili alisema atakwenda—lakini hakwenda.
c. Mtoto wa kwanza ndiye aliyetenda mapenzi ya baba yake.
d. Somo hapa: Utii ni zaidi ya ukiri – ni kutenda.
4. Kiwango cha utii wetu ndicho kiwango tunachofanya mapenzi ya
Mungu.
5. Ujumbe huu unahusu sisi kutii Agizo Kuu.
a. Matamko matano kuhusu ni kwa nini twende, na jinsi
tunavyopaswa kwenda:
I. KWA NINI NI LAZIMA TWENDE (Mt 28:19)
A. Ni lazima twende kwa sababu Yesu ametuagiza sisi twende.
1. Yeye ndiye Bwana wa Mavuno mwenye “mamlaka yote
mbinguni na duniani” (ms.18).
2. …kwa sababu kwenda ni alama ya uaminifu na upendo wetu
Kwake.
a. Maneno ya Yesu: “Mkinipenda mimi, mtatii…
(Yn 14:15).
3. …kwa sababu ni lazima tuwe na huruma kwa ajili ya
waliopotea (2Kor 5:14).
B. Itikio letu lisiwe kusema , “Tutakwenda,” halafu tusiende.
Badala yake, liwe hivi: “Ndiyo, tutakwenda,”na kweli twende.
II. MAHALI AMBAPO NI LAZIMA TWENDE (Mdo 1:8)
A. Yesu kwanza aliwatuma wanafunzi Wake kwa “kondoo waliopotea wa Israeli” (Mt. 10:5; 15:24).
1. Lakini, wakati “walio Wake” walipomkataa, Injili ilikwenda kwa
kila mmoja ambaye ange “liamini jina Lake (Yn 1:11-12).
-
49
B. Hatimaye Yesu akaagiza kwamba Injili ipelekwe kwa kila kundi
la watu, kila mtu binafsi, na kila mahali duniani (Mt 28:19; Mk
16:15; Mdo 1:8).
1. Kwa “dunia yote…kwa kila taifa” (Mt 24:14).
2. Kwa “wenye hekima na wapumbavu” (Rum 1:14).
3. Mpaka “mwisho wa nchi” (Mdo 1:8).
4. Kila mahali ambapo “Kristo hatajwi” (Rum 15:20).
C. Kwa hiyo basi, hebu twende kila mahali na kuzitangaza habari
njema!
III. WAKATI TUNAOTAKIWA KWENDA (Yn 4:35)
A. Ni lazima twende sasa! 1. Maneno ya Yesu: “Yatazameni mashamba. Yamekwisha kuwa
tayari kuvunwa” (ms. 35)
2. Alikuwa anazungumzia uharaka wa uvunaji. 3. Maneno ya Yesu: “Maadamu bado ni mchana, ni lazima kuifanya
kazi Yake Yeye aliyenituma. Usiku unakuja, ambapo hakuna
anayeweza kufanya kazi” (Yn 9:4).
B. Je, kwa sasa uko tayari, kwenda, kuomba na kutuma?
IV. JINSI TUNAVYOTAKIWA KWENDA (Mdo 26:16)
A. Ni lazima twende kama “watumishi na mashahidi” (Mdo 26:16)
B Ni lazima tuwe na mtazamo wa mtumishi (siyo bwana).
1. Sisi tunapaswa kuhudumu kama “kondoo katikati ya mbwa
mwivu” (Mt 10:16).
2. Ni lazima twende kama watumishi, wenye kutegemea moja kwa
moja uwepo wa Kristo na nguvu za Roho (Mt 28:20; Mdo 1:8).
C. Kusudi la kwenda ni kuwa shahidi kwa ajili ya Kristo (Lk 24:46-48).
V. NINI CHA LAZIMA KWENDA NACHO (Mk 3:14; Mdo 1:8)
A. Kwanza: Ni lazima twende na ujumbe.
1. Yesu alisema, “…mtakuwa mashahidi wangu…” (Mdo 1:8). 2. Tunashuhudia kwa ajili ya Kristo na kuhusu Kristo.
B. Pili: Ni lazima twende na nguvu ya Roho Mtakatifu.
1. Maneno ya Yesu: “Mtapokea nguvu, wakati Roho Mtakatifu
atakapokuja juu yenu…” (Mdo 1:8).
2. Pasipo nguvu ya Roho, sisi tutashindwa hakika.
3. Lakini katika nguvu za Roho, hakika tutafanikiwa.
Kumalizia, Na Wito Kwa Watu Kuja Mbele 1. Njoo sasa, ujitoe kwa ajili ya utume wa Kristo.
2. Njoo utiwe nguvu na Roho Mtakatifu. [ UA ]
-
50
14 Amri Ya Tatu Ya Agizo Kuu: “Hubirini!” ~ Amri Za Agizo Kuu ~
Ujumbe Wenyewe Katika Sentensi Moja: Ni lazima tuhubiri Injili kwa
uaminifu kila mahali na kwa kila mmoja.
Kusudi La Ujumbe: Kwamba watu wa Mungu wajitoe wenyewe kuhubiri
Injili kwa waliopotea.
Maandiko Ya Ujumbe: 1 Wakorintho 1:21; Mathayo 24:14
Utangulizi 1. Nini kinachotofautisha mahubiri na hotuba za wanasiasa na
wasanii?
a. Maudhui ya ujumbe na nia au kusudi la msemaji.
b. Ujumbe wa wanasiasa na wasanii ni ahadi zisizo na kitu – na
nia yao ni kujipigia debe.
c. Ujumbe wa mhubiri ni Kristo – na nia au kusudi lake ni
wokovu kwa waliopotea.
2. Ujumbe huu utakazia wajibu wetu wa kuhubiri Injili kwa watu
wote kila mahali kabla Yesu hajarudi.
a. Paulo alisema, “Mungu, kupitia upumbavu wa kile kilichokuwa
kinahubiriwa, alipendezwa kuwaokoa wale wote walioamini”
(1Kor 1:21).
b. Yesu alitamka hivi: “Injili hii ya ufalme ita