JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA TAASISI YA …
Transcript of JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA TAASISI YA …
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA
UTAFITI WA RUSHWA YA NGONO KATIKA TAASISI ZA ELIMU YA JUU:
UCHUNGUZI KIFANI WA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM NA DODOMA
JUNI, 2020
i
MUHTASARI RASMI (EXECUTIVE SUMMARY)
Usuli
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) ilifanya utafiti kwa lengo la
kuwezesha upatikanaji wa taarifa za kisayansi zitakazosaidia kukabiliana na vitendo vya rushwa
ya ngono katika Taasisi za elimu ya juu nchini. Aidha utafiti huu uliongozwa na malengo
mahususi yafuatayo; Kuwezesha kupata taarifa za kina kuhusu kuwepo kwa tatizo la rushwa ya
ngono; Kuchunguza sababu za kuwepo vitendo vya rushwa ya ngono; Kutathmini uwepo na
ufanisi wa mifumo ya udhibiti wa ndani ya maadili juu ya vitendo vya rushwa ya ngono; na
Kutoa mapendekezo yatakayowezesha Taasisi na Serikali kwa jumla kupambana na kuzuia
rushwa ya ngono kwenye taasisi za elimu ya juu.
Jukumu hili la TAKUKURU linatokana na matakwa ya kifungu cha 7 (a) na (c) cha Sheria ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11/2007. Kwa mujibu wa kifungu hiki, TAKUKURU
inao wajibu wa kuzuia rushwa katika taasisi za umma na binafsi kwa kufanya chambuzi za
mifumo katika taasisi hizo ili kubaini uwepo wa mianya ya rushwa na kisha kutoa ushauri wa
namna bora ya kudhibiti mianya hiyo.
Vilevile, TAKUKURU imefanya utafiti huu kama njia mojawapo ya kutekeleza moja ya
malengo ya Mkakati wa Taifa Dhidi ya Rushwa na Mpango wa Utekelezaji Awamu ya Tatu
(NACSAP III), “kuimarisha ufanisi, uwazi na uwajibikaji wa utoaji huduma katika sekta ya
umma na binafsi”. Ili kufanikisha utafiti huu, TAKUKURU iliingia ubia na Asasi ya Kiraia ya
WFT (Women Trust Fund) kama sehemu ya utekelezaji wa NACSAP III wa kujenga daraja na
wapiganaji wa vita dhidi ya rushwa. NACSAP III imebainisha majukumu ya wadau mbalimbali
kwenye vita dhidi ya rushwa. Kwa upande wa Asasi za Kiraia, baadhi ya majukumu ni pamoja
na: (i) kufanya utafiti na mafunzo kuhusu rushwa, maadili na utawala bora (ii) kuimarisha
kiwango cha uwazi na uwajibikaji katika shughuli zao, pamoja na (iii) kushiriki katika kampeni
za maadili ya Taifa na Utawala Bora (URT: 2007).
ii
Pamoja na kwamba Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imechukua hatua kadhaa za
kupambana na rushwa, ikiwemo rushwa ya ngono, bado yapo malalamiko ya rushwa ya ngono
hapa nchini. Zipo sababu nyingi za kuendelea kuwepo kwa malalamiko ya rushwa ya ngono,
ambazo ni pamoja na: matumizi mabaya ya madaraka; mikakati dhaifu ya kutekeleza sheria za
rushwa ya ngono; uelewa hafifu; kutokutambua kina na athari za tatizo la rushwa ya ngono; na
jamii kulionea aibu suala hili. Hali hii inasababisha waathiriwa wa rushwa ya ngono kuendelea
kuumia kimya kimya ambapo wakosaji kuendelea na vitendo hivi bila kuchukuliwa hatua stahiki
za kisheria.
Rushwa ya ngono hugeuza haki ya muombwaji kuwa upendeleo na siyo stahiki yake. Inapohusu
kumpokonya mtu haki yake, husababisha madhara kwenye nyanja mbalimbali kama vile kupata
jeraha lisilotibika kwenye maisha yake na mahala pengine anaweza kugeuzwa mtumwa wa
ngono, na hivyo kushindwa kukuza vipaji vyake vya uhalisia. Hali hii huathiri uchumi wa taifa
Kwanini utafiti wa rushwa ya ngono?
Pamoja na kutambua athari za rushwa ya ngono kwa wahanga, jamii na hata uchumi, hili ni eneo
ambalo halijafanyiwa utafiti wa kina hapa nchini. Tofauti na aina nyingine za rushwa
zinazotumia ubadilishaji wa vitu yakinifu au ridhaa ya mtoa rushwa na mpokea rushwa, hii ni
rushwa inayotokana na tabia ya mdai rushwa kutumia mamlaka yake kushawishi, kushinikiza
ngono badala ya vitu yakinifu.
Licha ya kutumia taarifa na maarifa ya kina yatokanayo na utafiti huu kuhusu suala hili la
rushwa ya ngono linavyoumiza taifa, jamii, taasisi, na watu binafsi wakiwemo waathirika, utafiti
huu ni nyenzo muhimu kwa watunga sera na sheria katika kushughulikia tatizo la rushwa ya
ngono. Dhamira ni kuchangia kwenye juhudi mbalimbali za kupambana na kuzuia vyanzo vikuu
vya uendelezaji wa vitendo vya rushwa ya ngono.
Kwanini Vyuo vya Elimu ya Juu?
Dira ya Taifa inadhamiria ifikapo mwaka 2025, Tanzania itakuwa ni nchi ya Taifa la wasomi na
wenye kupenda kujielimisha. Hivyo basi tatizo au changamoto yoyote inayogusa sekta ya elimu
iii
itaathiri ufikiwaji wa dira hii. Elimu ya juu ni kiwanda cha kuzalisha nguvu kazi ya taifa hivyo
husaidia kukuza uchumi na kuwezesha nchi kufikia malengo yake ikiwa ni pamoja na kufikia
uchumi wa viwanda.
Hivi karibuni kumekuweko na malalamiko mengi kuhusu uwepo wa matukio ya rushwa za
ngono kwenye taasisi za elimu ya juu, na hivyo utafiti huu utawezesha kubainisha kina cha
tatizo, kwanini hali hii, nini kifanyike na namna ya kulishughulikia suala hili.
Kwa nini Chuo Cha Dar es Salaam na Dodoma?
Hivi ni miongoni mwa vyuo vinavyomilikiwa na umma hapa nchini. Kinadharia, ni vyuo
vinavyohitajika au vinavyotarajiwa kuwa mfano katika utawala bora. Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam (UDSM) ndiyo chuo cha kwanza cha umma hapa nchini kilichozalisha viongozi wengi
kuliko vyuo vyote. Aidha, ndicho chuo cha kwanza katika Bara la Afrika kuzalisha fikra za
kimapinduzi, zilizoweza kunoa viongozi wengi walioweza kuchanganua jinsi Bara la Afrika
lilivyoporwa rasilimali zake na linavyoendelea kufukarishwa. Kimantiki, ni chuo ambacho
kinapaswa kuongoza fikra mbadala ikiwa ni pamoja na fikra zinazopinga unyanyasaji wa
kijinsia. Vilevile, ni chuo kikubwa nchini na kinachodahili wanafunzi wengi zaidi. Kwa mwaka
2017/2018 pekee, chuo hiki kilifanya udahili wa wanafunzi 13,626 ambao ni sawa na 21% ya
wanafunzi wote waliodahiliwa kwenye taasisi za elimu ya juu nchini kwa mwaka.
Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kipo Makao Makuu ya nchi na kichanga kwa kulinganisha
na UDSM. Kimantiki, chuo hiki hakikuhitaji kuandika sera, au miongozo mipya kwani kilikuwa
na fursa ya kujifunza kutoka chuo cha UDSM kuhusu masuala mengi ikiwa ni pamoja na kanuni
na miongozo inayokataza rushwa ya ngono katika taasisi za elimu ya juu. Vilevile, ni chuo
chenye udahili wa wanafunzi wengi. Kwa mfano, kwa mwaka wa masomo 2017/2018, chuo hiki
kilidahili wanafunzi 9,151 (Tanzania Commission for Universities – TCU, 2018).
Hivyo, vyuo hivi viwili vilihusishwa katika utafiti huu kutokana na historia ya vyuo hivi, umiliki
wake (vyuo vya umma) na wingi wa udahili wa wanafunzi. Hivi ndivyo vyuo vikuu vikubwa
viwili vinavyomilikiwa na Serikali na vinavyoongoza kwa kudahili wanafunzi wengi zaidi
iv
nchini. Aidha, kutokana na ukubwa wake na idadi kubwa ya wanafunzi nchini, utafiti uliona
kuwa ni sehemu sahihi ya kuweza kuchunguza na kujenga msingi wa kisayansi kuhusu rushwa
ya ngono nchini.
Taarifa na mapendekezo yatokanayo na utafiti huu yanaweza kutumiwa na vyuo na taasisi
nyingine za umma, sekta binafsi na asasi za kiraia kujitathmini katika maeneo yaliobainishwa na
hivyo, kuweza kubuni mikakati ya kukabiliana na tatizo la rushwa ya ngono kwa kuzingatia
uhalisia wa taasisi husika.
Mbinu za ukusanyaji wa taarifa
Taarifa za msingi zilikusanywa kwa kutumia madodoso, usaili, majadiliano ya vikundi na ziara
za watafiti katika vyuo tafitiwa. Taarifa za upili (secondary data) zilipatikana kwa uchambuzi wa
nyaraka zikiwemo sera, sheria, kanuni na miongozo mbalimbali inayosimamia vyuo hivyo.
Aidha, kazi za tafiti zinazohusu rushwa ya ngono zilipitiwa. Taarifa zilizokusanywa
zilichambuliwa kwa kutumia programu tumizi ya kuchambua taarifa za sayansi ya jamii (SPSS)
na taarifa nyingine zilichambuliwa kwa kufanya uchambuzi wa maudhui.
Muhtasari wa mambo makuu yaliyojitokeza kwenye utafiti
Kwa ujumla, utafiti umebaini kwamba tatizo la rushwa ya ngono kwenye vyuo vilivyoshiriki lipo
na kwamba tatizo hili ni kubwa na si la kupuuzwa. Shuhuda za waathiriwa wa rushwa ya ngono
pamoja na shuhuda za uwepo wa watuhumiwa ambao hawajachukuliwa hatua zilitolewa.
Vilevile, utafiti ulibaini kuwepo kwa sera, miongozo na sheria ndogondogo zinazoharamisha
rushwa ya ngono kwenye taasisi zote za umma ikiwa ni pamoja na vyuo vikuu. Kwa mfano,
Kanuni za Utumishi wa umma (2014, kanuni ya 36) zimepiga marufuku kwa mwajiri au
mtumishi wa umma kufanya aina yoyote ya udhalilishaji wa kijinsia kwa kumtaka mwajiriwa
kufanya ngono au kufanya aina yoyote itakayosababisha kufanyika ngono kama kigezo cha ahadi
ya kupendelewa kazini, au kulazimisha ngono ili mwajiriwa kuepuka vitisho ambavyo vitaathiri
ajira yake au kutumia kigezo cha ngono ili mwajiriwa aepuke vitisho dhidi ya maslahi ya sasa au
ya baadae katika ajira yake.
v
Vyuo vyote viwili vina kanuni za maadili za watumishi; Kanuni za Maadili kwa Watumishi wa
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (2018) na kanuni za maadili Chuo Kikuu Dodoma (2012).
Kanuni hizi zinabatilisha na kutoa katazo la kutumia rushwa ya ngono kutoa ufaulu, kufanya
vitendo vinavyoashiria ngono, au kufanya mawasiliano yanayoashiria uhitaji wa rushwa ya
ngono. Aidha, zinakataza kumsumbua au kumnyanyasa mtu yeyote yule anayetoa taarifa juu ya
unyanyasaji wa kingono (UDSM, 2018).
Pamoja na kuwepo kwa miongozo na kanuni zinazokataza rushwa ya ngono, utafiti ulibaini
mapungufu kwenye uwajibikaji wa udhibiti wa matumizi mabaya ya mamlaka hivyo kutoa
mianya inayosababisha kuwepo kwa vitendo vya rushwa ya ngono. Jambo hili lilielezwa
kusababishwa na kutokuwepo utashi wa dhati kwa wale waliopewa dhamana ya uongozi na
watoa huduma katika kushughulikia tatizo la rushwa ya ngono kikamilifu. Tabia za kuwalinda
wakosaji, zimesababisha kutokuimarisha ufuatiliaji wa sera na miongozo, kutokusimamia
maadili ya watendaji kwenye suala hili na kushindwa kuchukua hatua stahiki za kinidhamu kwa
wale wanaoendeleza vitendo vya rushwa ya ngono kwenye taasisi husika. Mifano ilitolewa ya
wahadhiri wanaodaiwa kujihusisha na rushwa ya ngono wanavyoendelea kupewa nyadhifa
mbalimbali za uongozi na vyeo vya kitaaluma. Shuhuda zilitolewa kuhusu vitisho kwa watoa
taarifa wakiwa waathiriwa au wahadhiri/watumishi wa vyuo husika. Shuhuda zilitolewa kuhusu
wanafunzi waliopendelewa na kupewa aidha ajira au kupewa udhamini wa masomo
(scholarship) bila kustahili pale ambapo wamekubali kutoa rushwa ya ngono. Shuhuda nyingine
zilitolewa kwa kuwepo watuhumiwa waliopewa adhabu kidogo sana kulingana na kosa, kwa
mfano mhadhiri kupewa likizo ya mwaka iliyomwezesha kuendelea na shughuli zake za ushauri
wa kitaalam na hatimaye kurudi chuoni kuendelea na shughuli kama kawaida baada ya muda huo
kupita. Shuhuda zilitolewa kwa uongozi wa vyuo kutokufanyia kazi mapendekezo ya kamati za
maadili hasa kwa masuala yanayohusu rushwa ya ngono. Ukosefu wa utashi na uwajibikaji
unakatisha tamaa waathiriwa wa rushwa ya ngono au watendaji wenye maadili kutoa taarifa
kuhusu vitendo vya rushwa ya ngono.
Utafiti ulibaini mapungufu kwenye mifumo ya utahini inayotoa mwanya kwa wahadhiri kutumia
vibaya mamlaka yao. Shuhuda zilitolewa kuhusu wanafunzi waliofelishwa kutokana na kukataa
rushwa ya ngono au wanafunzi wa kiume kufelishwa kwa vile marafiki wao wa kike wamekataa
vi
kutoa rushwa ya ngono. Shuhuda zilitolewa kuhusu kubadilishwa kwa alama za mitihani hata
baada ya matokeo kutoka rasmi. Shuhuda zilitolewa kuhusu wanafunzi waliopendelewa kwenye
kupewa alama za juu na hatimaye kuajiriwa chuoni bila kustahili.
Mapungufu yamejitokeza kwenye mifumo ya vyombo vya kusimamia utekelezwaji wa sera na
miongozo hususan kwenye suala la rushwa ya ngono. Kamati za maadili kushindwa kudhibiti
rushwa ya ngono, vitengo vya jinsia kukosa nyezo za kiuchunguzi za kuthibitisha makosa ya
rushwa ya ngono na uwezo wa kuelimisha jamii kuhusu rushwa ya ngono, ofisi za mshauri wa
wanafunzi na vitengo vya jinsia kukosa uwezo wa kutathmini, kufuatilia na kukusanya ushahidi
juu ya malalamiko ya rushwa ya ngono yanayowasilishwa kwao.
Utafiti ulibaini mianya mingine inayosababisha kuendelezwa kwa rushwa ya ngono ikiwa ni
pamoja na ukosefu wa huduma za msingi kwa wanafunzi kama vile nyumba za kulala (hostels),
mikopo, pamoja na mifumo ya ajira za wakufunzi isiyozingatia weledi na maadili ya kazi
kwenye baadhi ya taasisi za elimu (teaching ethics).
Aidha, utafiti umebaini kuwa Sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa Na. 11/2007 inatoa
mwanya kwa wasio na mamlaka kuwashawishi kwa makusudi wenye mamlaka kuwapa ngono.
Jambo hili lilifanikiwa kutokana na wahadhiri au watumishi wasio waadilifu wa kutozingatia
kanuni na taratibu zinazowaongoza kwenye utendaji wao.
Mapendekezo
Kutokana na matokeo tajwa, utafiti umebainisha mapendekezo machache yaliyotokana na
mijadala ya washiriki wa utafiti huu. Umuhimu wa kuboresha na kuimarisha mifumo ya
uwajibikaji kwenye kupambana na rushwa ya ngono ulijitokeza kama eneo la kipaumbele
kwenye kupambana na tatizo la rushwa ya ngono ndani ya vyuo vya elimu ya juu na taasisi
nyingine za umma na za sekta binafsi. Mapendekezo yalibainishwa kwa kila mdau:
Serikali
Iuwajibishe uongozi wa vyuo vikuu kwenye kujenga mazingira wezeshi na salama kwa
wanafunzi na wafanyakazi katika ngazi zote ili kuwezesha wanafunzi wa kike na kiume
kupata na kufaidi haki ya elimu katika ngazi hii pamoja na kuwezesha upatikanaji wa
elimu bora;
vii
Iimarishe mifumo ya ajira ya wafanyakazi wote, hususan wakufunzi na viongozi kwa
kuwapa mafunzo ya ualimu na uongozi wale wote wenye kuajiriwa chuoni ili kuwapa
nyenzo za uwajibikaji wa kuzingatia maadili ya kufundisha na kuongoza katika taasisi za
elimu;
Iongeze fedha za uendeshaji vyuoni na hususan zinazohitajika kwenye kuimarisha
huduma za kuwezesha kuboresha utoaji wa elimu ikiwa ni pamoja na huduma za malazi
kwa wanafunzi ili kupunguza mianya inayotumiwa na wasimamizi na watoa huduma hizi
kwa kuweka sharti la ngono kwa wanafunzi;
Isimamie uwajibikaji wa uongozi wa chuo kuhusu masuala ya jinsia na hususan rushwa
ya ngono kwa kuwawajibisha viongozi waimarishe Kamati za Maadili ndani ya vyuo;
Kuendelea kuijengea uwezo TAKUKURU wa kuweza kuchunguza na kumfikisha
mtuhumiwa mahakamani bila kuhitaji kibali cha Mkurugenzi wa Mashtaka; na
Ifanye mapitio ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11/2007 ili
kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa ya ngono.
Uongozi wa Vyuo
Uboreshe mifumo ya udhibiti na uwajibikaji kwenye kuimarisha mifumo ya kusimamia
maadili, mifumo ya utahini, mifumo ya kutoa taarifa na kulinda watoa taarifa pamoja na
kuwajibisha watuhumiwa wa vitendo hivyo;
Uimarishe taasisi na kamati zinazoshughulikia masuala ya maadili ya watumishi wake
ikiwa ni pamoja na kamati za maadili, vitengo vya jinsia, ofisi ya mshauri wa wanafunzi
kwa kuwapatia nyenzo, vitendea kazi na mafunzo ya kuwawezesha kushughulikia
masuala ya rushwa ya ngono pamoja na unyanyasaji wa kijinsia kwenye vyuo; na
Uimarishe mahusiano na TAKUKURU kwenye kutoa elimu, kupeleleza na kuchukua
hatua stahiki kwa wale wote wenye kutuhumiwa kujihusuisha na vitendo vya rushwa ya
ngono.
viii
Vitengo/Taasisi za Jinsia
Kujijengea uwezo wa uelewa wa Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na.
11/2007 kuhusu rushwa ya ngono ili waweze kusimamia utekelezaji wake vyuoni; na
Kuwajengea wanafunzi na jamii yote ya chuo uelewa wa suala la rushwa ya ngono ili
waweze kujitetea na kupambana nalo.
Asasi za kiraia
Kutumia taarifa hii kuimarisha vita dhidi ya rushwa ya ngono;
Kuendeleza na kuimarisha ubia kati yake na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa (TAKUKURU) kwenye vita dhidi ya rushwa ya ngono, hasa kwenye utafiti na
elimu ya umma; na
Kujijengea uelewa wa pamoja wa sheria ya Kuzuia na Kupambana na rushwa hususani
vipengele vinavyoelezea rushwa ya ngono ili kuweza kuendeleza mapambano dhidi ya
rushwa ya ngono.
Wanafunzi wa Vyuo
Waongeze jitihada katika masomo, wazingatie maadili, wasikubali kurubuniwa, wavunje
ukimya na kupaza sauti kunapotokea viashiria vya kuwanyima haki zao, na wachukue
hatua stahiki pale wanapopokonywa hizo haki.
Wadai kuimarishwa kwa mikakati iliyobainishwa katika miongozo na sheria ndogondogo
za kuzuia na kudhibiti rushwa ya ngono;
Wafikishe malalamiko yao TAKUKURU kwa kupitia kamati zao, taasisi za kiraia na hata
wao wenyewe; na
Waungane na kushiriki zaidi kwenye kampeni za kupambana na rushwa ya ngono.
ix
SHUKRANI
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) inatoa shukrani zake za dhati kwa
wadau wote walioshiriki katika kufanikisha utafiti huu. Kwa kuwa sio rahisi kuwataja wote kwa
majina na vyeo, tunaomba wote wapokee shukrani hizi zinazotambua michango yao kwenye
kufanikisha kazi hii. Hata hivyo, TAKUKURU inawiwa kushukuru uongozi, watumishi na
wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Dodoma (UDOM) na Dar es Salaam (UDSM) kwa ushirikiano
wa karibu kwenye mchakato wote wa kukamilisha zoezi hili. Kipekee tunashukuru Mfuko wa
Udhamini wa Wanawake Tanzania (Women Fund Tanzania Trust - WFT) kwa kuwezesha utafiti
huu, Prof. Ruth Meena na Bi. Anneth Meena kwa kutoa utaalam wao katika utafiti huu, Dkt.
Alfred Wimana Sebahene wa Chuo Kikuu cha St. John na Dkt. Tatu Mkiwa Nyange wa Chuo
Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kwa kushiriki katika kufanikisha utafiti huu.
x
YALIYOMO
MUHTASARI RASMI (EXECUTIVE SUMMARY)................................................................................... i
SHUKRANI ................................................................................................................................................. ix
YALIYOMO ................................................................................................................................................. x
ORODHA YA MAJEDWALI .................................................................................................................... xii
ORODHA YA VIFUPISHO ...................................................................................................................... xiii
SURA YA KWANZA .................................................................................................................................. 1
1.0 UTANGULIZI .............................................................................................................................. 1
1.1 Maelezo ya tatizo .......................................................................................................................... 2
1.2 Lengo kuu ..................................................................................................................................... 2
1.3 Madhumuni mahsusi ..................................................................................................................... 2
1.4 Maswali ya utafiti ......................................................................................................................... 3
1.5 Umuhimu wa utafiti ...................................................................................................................... 3
SURA YA PILI ............................................................................................................................................. 5
2.0 MAPITIO YA MACHAPISHO .................................................................................................... 5
2.1 Nadharia ya utafiti ............................................................................................................................... 5
2.1.1 Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania Na. 11/2007 .......................................... 5
2.1.2 Kanuni za Mienendo na Maadili kwa Watumishi wa Umma ...................................................... 6
2.1.3 Kanuni za Utumishi wa Umma, 2014 .......................................................................................... 7
2.1.4 Kanuni za Maadili kwa Watumishi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Dodoma ................. 8
2.3 Ukubwa wa tatizo ............................................................................................................................... 9
2.4 Kiunzi cha dhana ............................................................................................................................... 11
2.5 Maana tumizi .................................................................................................................................... 11
2.5.1 Rushwa ya ngono ....................................................................................................................... 11
2.5.2 Huduma ...................................................................................................................................... 12
2.5.3 Mamlaka .................................................................................................................................... 12
xi
SURA YA TATU ....................................................................................................................................... 13
3.0 MBINU ZA UTAFITI ................................................................................................................ 13
3.1 Usanifu wa utafiti ........................................................................................................................ 13
3.2 Eneo na muda wa utafiti .............................................................................................................. 13
3.3 Sampuli ............................................................................................................................................ 14
3.4 Ukubwa wa sampuli ........................................................................................................................ 14
3.5 Mbinu za ukusanyaji wa taarifa ....................................................................................................... 14
3.6 Uchambuzi wa taarifa ................................................................................................................. 16
SURA YA NNE .......................................................................................................................................... 17
4.0 MATOKEO YA UTAFITI ................................................................................................................... 17
4.1 Wasifu wa wahojiwa ......................................................................................................................... 17
4.2 Uwepo wa rushwa ya ngono ............................................................................................................. 18
4.3 Sababu za kuwepo vitendo vya rushwa ya ngono ............................................................................. 20
4.4 Mifumo ya udhibiti ya ndani dhidi ya rushwa ya ngono .................................................................. 24
4.5 Mbinu zinazotumika kushawishi rushwa ya ngono .......................................................................... 30
SURA YA TANO ....................................................................................................................................... 35
5.0 HITIMISHO NA MAPENDEKEZO .................................................................................................... 35
5.1 Hitimisho........................................................................................................................................... 35
5.2 Mapendekezo .................................................................................................................................... 37
Marejeo ....................................................................................................................................................... 40
VIAMBATISHO......................................................................................................................................... 42
xii
ORODHA YA MAJEDWALI
Jedwali 1: Mgawanyo wa hojaji.................................................................................................................. 15
Jedwali 2: Idadi ya makundi kwenye majadiliano ya vikundi .................................................................... 15
Jedwali 3: Idadi ya wahojiwa lengwa ......................................................................................................... 16
Jedwali 4: Wasifu wahojiwa kwa njia ya hojaji .......................................................................................... 17
Jedwali 5: Mwitiko wa uelewa wa dhana ya na uwepo wa rushwa ya ngono ............................................ 19
Jedwali 6: Mwitiko wa wahojiwa kuhusu sababu za rushwa ya ngono ...................................................... 21
Jedwali 7: Mwitiko wa wahojiwa kuhusu uwepo wa sera, miongozo na taratibu za udhibiti rushwa ya
ngono .......................................................................................................................................................... 25
Jedwali 8: Mwitiko wa wahojiwa kuhusu mbinu zinazotumika kushawishi rushwa ya ngono .................. 31
xiii
ORODHA YA VIFUPISHO
ARIS - Academic Registration Information System
FGD - Focus Group Discussion
JMT - Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
MUCE - Mkwawa University College of Education
TAKUKURU - Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
TAMWA - Tanzania Media Women Association
TI - Transparent International
TWJA - Tanzania Women Judges Association
SPSS - Statistical Package for the Social Sciences
UDSM - University of Dar es Salaam
UDOM - University of Dodoma
WFT - Women Fund Tanzania – Trust
1
SURA YA KWANZA
1.0 UTANGULIZI
Rushwa ya ngono inafasiliwa na wanazuoni kama matumizi mabaya ya madaraka, ili
kujinufaisha kingono visivyo halali au pasipo kuwa na makubaliano ya pande zote mbili
zinazohusika katika ngono (Tanzania Women Judge Association, 2011; Yusuph, 2016). Aina hii
ya rushwa haitumii fedha au vitu kushawishi ila hutumia nguvu ya kisaikolojia kumshawishi
mhanga kutoa mwili wake kingono ili kupata huduma au haki. Mhusika anayedai aina hii ya
rushwa ni lazima awe na madaraka au mamlaka ambayo anaamua kuyatumia vibaya kwa
kujaribu kushawishi au kukubali kupewa ngono kubadilishana na utekelezaji wa mamlaka yale
aliyonayo. Watu wa namna hii hutumia madaraka au mamlaka waliyonayo kwa lengo la
kujinufaisha wao wenyewe na siyo kutumia mamlaka hayo kutekeleza majukumu yao kama
inavyotarajiwa na kwa kuzingatia weledi, uadilifu, sheria na usawa.
Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007 imeharamisha rushwa ya
ngono kwa kukataza mtu yeyote mwenye mamlaka kutumia mamlaka aliyonayo katika
kutekeleza majukumu yake kudai au kulazimisha upendeleo wa kingono au upendeleo mwingine
wowote kama kigezo cha kutoa ajira, kupandisha cheo, kutoa haki au upendeleo wowote
unaotambulika kisheria. Aidha, hivi karibuni, Serikali kupitia Bunge la Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania imefanya maboresho ya sheria mbalimbali ikiwemo Sheria ya Uhujumu Uchumi1.
Kupitia maboresho hayo, kosa la rushwa ya ngono limetajwa kuwa moja ya makosa ya uhujumu
uchumi2 na adhabu yake kwa mtu anayekutwa na hatia ni kifungo kisichopungua miaka 20 na
kisichozidi miaka 30 au kifungo pamoja na adhabu nyingine yoyote chini ya sheria hiyo na
iwapo sheria nyingine itatoa adhabu kali zaidi ya adhabu iliyotolewa na Sheria ya Uhujumu
Uchumi kupitia mabadiliko tajwa hapo juu basi Mahakama imeruhusiwa kutoa adhabu hiyo
ambayo ni kubwa.3
1 No.3 Written Laws (Miscellaneous Amendments) Act 2016
2 Section 16(b) of the Written Laws (Miscellaneous Amendments) Act 2016
3 Section 13 (3) Written Laws (Miscellaneous Amendments) Act 2016 "(2) Notwithstanding provision of a different
penalty under any other law and subject to subsection (3), a person convicted of corruption or economic offence
shall be liable to imprisonment for a term of not less than twenty years but not exceeding thirty years, or to both that
2
Hata hivyo, pamoja na kuwepo kwa sheria, taratibu na kanuni za maadili na mienendo (Codes of
conduct and ethics) ambazo kimsingi zinaharamisha vitendo vyote vya unyanyasaji wa kijinsia
(sexual harassment), rushwa ya ngono bado ni tatizo linaloisumbua jamii. Tatizo hili linachangia
kuzalisha wataalam wasio na weledi kwa kurudisha nyuma ubora wa elimu inayotolewa katika
vyuo vya elimu ya juu nchini. Taasisi za elimu ya juu ni viwanda vya kuandaa wataalam
wanaotarajiwa kuingia kwenye fani mbalimbali za utoaji huduma, uzalishaji, na kuwa walezi wa
familia. Kwa kuzingatia umuhimu wao, wataalam hao wanapaswa kuhitimu wakiwa wameiva
kimaadili na kiweledi. Hivyo, tatizo hili katika Taasisi za elimu ya juu nchini linahitaji
kuangaliwa kwa ukaribu ili kuepusha madhara yanayoweza kutokea huko baadae kwa
wanafunzi, wahadhiri na jamii kwa ujumla.
1.1 Maelezo ya tatizo
Kumekuwepo na ongezeko la malalamiko kutoka kwa wadau mbalimbali wakiwemo watunga
sera, wanazuoni, wahadhiri, wanafunzi na wananchi kuwa wanafunzi wa kike katika Taasisi za
elimu ya juu (vyuo vikuu) nchini wanalazimishwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na baadhi
ya wahadhiri au watumishi waliopo kwenye nafasi za madaraka ili waweze kupata upendeleo au
haki. Malalamiko hayo yamejitokeza kwenye mitandao ya kijamii yakidai kwamba rushwa ya
ngono imekithiri katika vyuo vikuu (Mwai, 2018). Pamoja na kuwepo kwa malalamiko haya,
hakuna taarifa rasmi kutoka vyuo vikuu zilizofikia TAKUKURU kwa ajili ya kuchunguza na
kuchukua hatua stahiki za kukabiliana na tatizo hilo kwenye vyuo vya elimu ya juu.
1.2 Lengo kuu
Lengo la utafiti huu ni kuwezesha upatikanaji wa taarifa za kisayansi zitakazosaidia kukabiliana
na vitendo vya rushwa ya ngono katika Taasisi za elimu ya juu nchini.
1.3 malengo mahususi
Ili kufikia lengo la utafiti huu, malengo mahususi yafuatayo yaliongoza utafiti huu:-
(i) Kuwezesha kupata taarifa za kina kuhusu kuwepo kwa tatizo la rushwa ya ngono;
imprisonment and any other penal measure provided for under this Act; Provided that, where the law imposes penal
measures greater than those provided by this Act, the Court shall impose such sentence.
3
(ii) Kuchunguza sababu za kuwepo vitendo vya rushwa ya ngono;
(iii) Kutathmini uwepo na ufanisi wa mifumo ya udhibiti wa ndani ya maadili juu ya vitendo
vya rushwa ya ngono; na
(iv) Kutoa mapendekezo yatakayowezesha Taasisi na Serikali kwa jumla kupambana na
kuzuia rushwa ya ngono kwenye taasisi za elimu ya juu.
1.4 Maswali ya utafiti
(i) Je wadau wanauelewa wa dhana hii ya rushwa ya ngono?
(ii) Je hali ya tatizo la rushwa ya ngono katika chuo hiki ikoje?
(iii) Je nini chanzo cha kuwepo vitendo vya rushwa ya ngono?
(iv) Je kuna mifumo ipi ya udhibiti wa vitendo vya rushwa ya ngono katika Taasisi za
elimu ya juu?
(v) Je kuna ufanisi wa mifumo ya udhibiti wa vitendo vya rushwa ya ngono?
(vi) Je ni mbinu gani zinatumiwa kufanya ushawishi wa rushwa ya ngono katika
Taasisi za elimu ya juu?
(vii) Ni nini kifanyike ili kupambana na hatimaye kuzuia rushwa ya ngono
1.5 Umuhimu wa utafiti
Utafiti huu ni muhimu kwa sababu zifuatazo: -
(i) Utaisaidia Serikali kufahamu ukubwa wa tatizo la rushwa ya ngono katika taasisi
za elimu ya juu na namna ya kukabiliana nalo kwani ni dhahiri kuwa kwa sasa
hakuna taarifa sahihi juu ya ukubwa wa tatizo hili;
(ii) Kuweka msingi kwa ajili ya kufanya utafiti wa kina utakaohusisha sampuli kubwa
na wigo mpana kwa siku za usoni. Hii ni kwa sababu taarifa zilizopo kwa sasa ni
finyu na hazitoshelezi kufanyika kwa marekebisho ya kisera na kisheria;
(iii) Utasaidia kuongeza mwamko kwa jamii kuhusu tatizo na madhara ya rushwa ya
ngono nchini;
(iv) Utasaidia kuongeza kasi ya kupambana na tatizo la rushwa katika sekta ya elimu
na hasa wakati huu ambapo Serikali imeonesha dhamira ya kweli ya kutokomeza
rushwa na vitendo vyote vya ufisadi; na
4
(v) Utasaidia kufahamu iwapo kanuni za mienendo/maadili za vyuo vikuu zimesaidia
kudhibiti rushwa ya ngono au la, na hatua sahihi zinazopaswa kuchukuliwa.
5
SURA YA PILI
2.0 MAPITIO YA MACHAPISHO
Sura hii inahusisha mapitio ya machapisho mbalimbali; ikijumuisha uchambuzi wa maandiko
mbalimbali, kanuni, Sheria na taratibu zilizoandikwa kuhusu rushwa na rushwa ya ngono.
2.1 Nadharia ya utafiti
2.1.1 Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania Na. 11/2007
Lengo kuu la Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11/2007 ni kukuza utawala bora
na kutokomeza rushwa. Katika kufanikisha hayo sheria inatoa msingi wa kitaasisi na kisheria
kuwezesha kuzuia na kupambana na rushwa kwa njia tofauti zikiwa ni pamoja na kuelimisha,
kuchambua mifumo ya utendaji wa Taasisi za umma na binafsi, na kuchunguza.4 Sheria hii
imeweka kifungu mahususi cha kuzuia rushwa ya ngono ambacho kinabainisha kuwa ni kosa
kwa mtu mwenye mamlaka kudai au kuomba rushwa ya ngono kwa mtu yeyote kama sharti la
kutoa ajira, upendeleo, kumpandisha cheo, kumpatia haki au huduma maalum.5
Sheria ya Kuzuia na Kupambana namba 11 ya mwaka 2007 imetamka kosa hili chini ya kifungu
cha 25, kama kinavyoeleza:
“Any person being in a position of power or authority, who in the exercise of
his authority, demands or imposes sexual favours or any other favour on any
person as a condition for giving employment, a promotion, a right, a privilege
or any preferential treatment, commits an offence….”
Ambapo kwa tafsiri isiyo rasmi kifungu hiki kinasema:
“Mtu yeyote mwenye mamlaka katika kutekeleza majukumu yake anadai,
anaweka sharti la ngono au upendeleo mwingine wowote kama kigezo cha
kutoa ajira, kupandisha cheo, kutoa haki au upendeleo wowote unaotambulika
kisheria atakuwa ametenda kosa.”
4 Kifungu cha 7 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na rushwa
5 Kifungu cha 25 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11/2007
6
Kifungu kinabainisha mambo muhimu yanayosababisha au uwepo wake yanatengeneza rushwa
ya ngono, ambayo: Kwanza, mtu mwenye mamlaka ambapo kwa mazingira ya Taasisi za Elimu
ya juu ni Wahadhiri na Watawala. Pili, Katika utekelezaji wa majukumu yake kama vile kutoa
alama kwenye mitihani, kupandisha vyeo, uhamisho na malazi. Tatu, Kumwekea sharti la ngono
mtaka huduma kama mwanafunzi au mtumishi wa chuo ili kupata huduma au upendeleo
wowote.
Aidha, hivi karibuni, Serikali kupitia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imefanya
maboresho ya sheria mbalimbali ikiwemo Sheria ya Uhujumu Uchumi6. Kupitia maboresho
hayo, kosa la rushwa ya ngono limetajwa kuwa moja ya makosa ya uhujumu uchumi7 na adhabu
yake kwa mtu anayekutwa na hatia ni kifungo kisichopungua miaka 20 na kisichozidi miaka 30
au kifungo pamoja na adhabu nyingine yoyote chini ya sheria hiyo na iwapo sheria nyingine
itatoa adhabu kali zaidi ya adhabu iliyotolewa na Sheria ya Uhujumu Uchumi kupitia mabadiliko
tajwa hapo juu basi Mahakama imeruhusiwa kutoa adhabu hiyo ambayo ni kubwa.8
Hata hivyo nadharia hii imeonesha udhaifu kama wa kutoharamisha ukuadi, mhitaji huduma
kutoa rushwa ya ngono kwa mtoa huduma na mazingira ambayo upande wa mtoaji na mpewa
huduma wanapokubaliana kupeana rushwa ya ngono. Kanuni za mienendo na maadili kwa
watumishi wa umma, kanuni za utumishi wa umma, kanuni za maadili kwa watumishi na
wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Dodoma zinaweza kusaidia katika udhibiti wa
rushwa ya ngono.
2.1.2 Kanuni za Mienendo na Maadili kwa Watumishi wa Umma
Kanuni hizi zilizotengenezwa chini ya Sheria ya Utumishi wa Umma zinakataza mtumishi
yeyote wa umma kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mtumishi mwenzake au mtu mwingine
katika eneo la kazi na vitendo vyovyote vile vyenye kusababisha usumbufu wa kingono (Sexual
6 No.3 Written Laws (Miscellaneous Amendments) Act 2016
7 Section 16(b) of the Written Laws (Miscellaneous Amendments) Act 2016
8 Section 13 (3) Written Laws (Miscellaneous Amendments) Act 2016 "(2) Notwithstanding provision of a different
penalty under any other law and subject to subsection (3), a person convicted of corruption or economic offence
shall be liable to imprisonment for a term of not less than twenty years but not exceeding thirty years, or to both that
imprisonment and any other penal measure provided for under this Act; Provided that, where the law imposes penal
measures greater than those provided by this Act, the Court shall impose such sentence.
7
harassment) mahala pa kazi. Aidha, kanuni zimekataza mtumishi yeyote kuweka sharti la ngono
kwa mtumishi mwenzake; kubaka, kutomasa, kumshikashika mtumishi kwa makusudi kwa
namna inayoashiria uhitaji wa ngono, kufanya au kuonesha ishara za vitendo, kelele na utani
wenye kuashiria uhitaji wa ngono na kutoa maoni ya kingono dhidi ya mtumishi mwenzake.9 Hii
inamaanisha kuwa, wahadhiri au watumishi wa vyuo vya elimu ya juu wanakatazwa na kanuni
hizi kujihusisha na masuala ya rushwa ya ngono baina yao na watumishi wengine au wanafunzi
wanaowafundisha na au kuweka masharti ya kingono katika kutoa haki au huduma. Hivyo,
wanawajibika kiweledi kukataa vishawishi vyovyote vya kingono vinavyofanywa na watumishi
wenzao au wanafunzi ikiwa ni kwa lengo la kujipatia manufaa kutoka kwa mhadhiri au mtumishi
mwingine wa chuo.
2.1.3 Kanuni za Utumishi wa Umma, 2014
Kanuni za utumishi wa umma zimeweka makatazo mbalimbali ambayo kimsingi yanalenga
kuzuia rushwa ya ngono katika utumishi wa umma. Kanuni ya 35 imeweka wazi kuwa ni
marufuku kwa mtumishi wa umma akiwa katika kituo chake cha kazi au nje, kujihusisha na
vitendo ambavyo vinakiuka maadili ya jamii yakiwemo ujeuri, matusi, lugha chafu au aina
yoyote ya udhalilishaji wa kijinsia ambao utapelekea ukiukwaji wa Haki za Binadamu. Katazo
hili kimsingi limegusa rushwa ya ngono kwani rushwa ya ngono inadhalilisha jinsi, inakiuka
haki za binadamu na iko kinyume na maadili ya watanzania.
Vilevile, kanuni ya 36 imepiga marufuku kwa mwajiri au mtumishi wa umma kufanya aina
yoyote ya udhalilishaji wa kijinsia kwa kumtaka mwajiriwa kufanya ngono au kufanya aina
yoyote itakayopelekea kufanyika ngono kama kigezo cha ahadi ya kupendelewa kazini, au
kulazimisha ngono ili mwajiriwa kuepuka vitisho ambavyo vitaathiri ajira yake au kutumia
kigezo cha ngono ili mwajiriwa aepuke vitisho dhidi ya maslahi ya sasa au ya baadae katika ajira
yake.
Aidha, mwajiri amekatazwa na kanuni kutumia lugha isiyostahiki inayoashiria kutaka ngono, au
kuonesha tabia ya wazi ya kufanya ngono kama vile kujishika sehemu za siri au kufanya kitendo
chochote kinachoashiria ufanyikaji wa ngono.
9 Kanuni II (6) ya Kanuni za Mienendo na Maadili kwa watumishi wa Umma,
8
Kwa msingi huo, kanuni zimeweka wazi kuwa mtu yeyote atakayefanya matendo ya ngono kama
yalivyofafanuliwa atachukuliwa hatua za kinidhamu au jinai. Ikiwa kosa hilo ni la jinai mhusika
atafikishwa katika vyombo vya sheria ikiwemo TAKUKURU.
Pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuweka msingi wa kisheria na
kikanuni wa kukataza rushwa ya ngono, bado taasisi za elimu ya juu nchini, kila moja kwa nafasi
yake, zimeweka kanuni mbalimbali za maadili zinazobatilisha mahusiano ya kingono baina ya
wanafunzi na wahadhiri au watumishi wa Taasisi husika.
2.1.4 Kanuni za Maadili kwa Watumishi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Dodoma
Kanuni za maadili kwa watumishi na wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam za mwaka
2018 zinabatilisha na kutoa katazo la kutumia rushwa ya ngono kutoa ufaulu, kufanya vitendo
vinavyoashiria ngono, au kufanya mawasiliano yanayoashiria uhitaji wa rushwa ya ngono.
Aidha, kanuni hizo zinakataza kumsumbua au kumnyanyasa mtu yeyote yule anayetoa taarifa
juu ya unyanyasaji wa kingono (UDSM, 2018).
Kwa upande wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Kanuni ya 3.8 imeweka katazo kwa mtumishi yeyote
wa chuo kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi na mwanafunzi ambaye wana uhusiano wa
moja kwa moja wa kimasomo. Aidha, watumishi wa ngazi ya juu katika chuo wamekatazwa
kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi wanaowasimamia ili kuepuka kushusha
hadhi ya chuo, maadili pamoja na weledi katika utekelezaji wa majukumu ya chuo. Pia, kanuni
hizo zimekataza mtumishi yeyote kushikanashikana na mwanafunzi akiwa na lengo la kuhitaji
ngono kutoka kwa mwanafunzi huyo na kwa mujibu wa Kanuni hizo, ni marufuku mwanafunzi
au mhadhiri kumdhalilisha kijinsia mwanafunzi, mtumishi au mteja kwa kuomba kufanya naye
ngono, na matendo mengine yote yanayoashiria uhitaji wa kufanya ngono.10
Kwa mujibu wa Mkakati wa Kitaifa wa Kupambana na Rushwa na Mpango wa Utekelezaji:
Awamu ya tatu 2017-2022, taasisi zote za umma vikiwemo vyuo vikuu vyote nchini vinatakiwa
10 Rule 3.10 of The University of Dodoma, 2012
9
kuwa na kamati za kudhibiti uadilifu. Kamati hizi ni muhimu katika kuandaa, kutekeleza na
kutathmini mkakati wa mapambano dhidi ya rushwa.
2.3 Ukubwa wa tatizo
Mara nyingi rushwa ya ngono ni eneo tete ambalo taarifa zake haziwafikii watendaji kwa sababu
ya ukimya wa wahanga. Kwa mfano, kuanzia mwaka 2013 hadi Machi 2020, Taasisi ya Kuzuia
na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imeshughulikia taarifa za malalamiko ya rushwa ya
ngono ambapo majalada 23 yalifunguliwa katika mikoa ifuatayo: Mwanza (4), Kagera (3),
Mtwara (3), Mara (3), Mara (3), Arusha (1), Dodoma (1), Geita (1), Iringa (1), Katavi (1),
Kinondoni (1), Manyara (1), Rukwa (1), Singida (1) na Temeke (1). Jumla ya Kesi 10
zilifunguliwa mahakamani, ambapo Kesi 5 zilishinda (Conviction), na kati ya hizo, nne zilihusu
Taasisi za Elimu. Utafiti uliofanywa na Chama cha Wanahabari Wanawake (TAMWA) nchini
ulieleza kuwa wanawake asilimia 89 walioajiriwa katika sekta ya umma nchini wamewahi
kuombwa rushwa ya ngono wakati wa kuajiriwa, kupandishwa vyeo au wakati wakihitaji
huduma fulani (TAMWA, 2012). Utafiti mwingine uliofanywa nchini Rwanda na shirika
linalojihusisha na tafiti za masuala ya rushwa duniani la Transparent International (TI)
unaonesha kuwa jinsi ya kike ni waathirika wakubwa wa vitendo vya rushwa ya ngono nchini
humo. Utafiti huo unaonesha kuwa asilimia 84.5 ya vitendo vya rushwa ya ngono hufanyika
kwa wanawake ambapo asilimia 15.4 hufanywa kwa wanaume11
. Tafiti hizo zote zinaonesha
kuwa jinsi ya kike imekuwa ikiathiriwa zaidi na vitendo vya rushwa ya ngono kuliko jinsi ya
kiume katika maeneo mbalimbali. Hali kadhalika, katika Taasisi za elimu za juu, wanafunzi wa
jinsi ya kike wamekuwa wakilalamika zaidi kuwa wanatakwa rushwa ya ngono na wahadhiri au
watumishi wengine wa Taasisi hizo.
Aidha, Hoyce Temu (2007), mmoja wa waandishi maarufu wa habari za kijamii katika kitabu
chake kiitwacho “Nayakumbuka yote” ameeleza kuwa, aliwahi kusitisha masomo katika moja ya
Taasisi ya elimu ya juu nchini kutokana na kubughudhiwa na wahadhiri kwa lengo la kutoa
rushwa ya ngono.
11
Transparency International (7 march, 2016) Sextortion: Undermining Gender Equality
https://www.transparency.org/news/feature/sextortion_undermining_gender_equality
10
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan wakati akifungua Mkutano wa Nane wa Chama cha
Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA), alikiri kwamba suala la rushwa ya ngono limeendelea
kuwa tishio nchini hadi kusababisha wanawake wengi kujiengua katika nafasi zao. Mheshimiwa
Samia alisema “Ni jambo la kuvunja moyo, kuona kwamba katika Karne ya 21 suala la rushwa
ya ngono, linaendelea na kusababisha wanawake wengi kujiengua katika nafasi zao. Matumaini,
matarajio na ndoto za wanawake, zimekuwa zikikatishwa na watu wachache ambao ni hatarishi,
hivyo tunahitaji kufanya kazi kuhakikisha kwamba tunawasaidia kwa hali na mali kwa sababu
wahanga hao wanaweza kuwa mama yako, dada, mke na binti yako,‟‟12
Utafiti huu ulilenga kutoa taarifa zaidi kuhusu kuwepo kwa tatizo lenye madhara makubwa kwa
taifa letu ili kuendelea kuchukua hatua stahiki za kupambana nalo. Rushwa ya Ngono ina
madhara kwa jamii kiuchumi, kisiasa, kiustawi wa jamii, kidemokrasia na kiutekelezwaji wa
haki za binadamu. Licha ya athari kwa wahanga wa rushwa ya ngono, rushwa hii huathiri taifa
katika ngazi mbalimbali ikiwa ni pamoja na ngazi ya taifa, mhanga na jamii.
Katika ngazi ya Taifa, rushwa ya ngono inadhalilisha taifa zima kiujumla: pale ambapo taifa na
vyombo vya dola vinapopuuza hali hii inakinzana na matamko mbalimbali ambayo nchi
imeridhia kimataifa, kikanda na kwa kupita Katiba ya nchi. Kwa hivyo basi, rushwa ya ngono ni
ukiukwaji wa haki za binadamu.
Kiuchumi nchi inashindwa kutumia vipaji vyake kiufanisi pale ambapo wasio na sifa wanapewa
nafasi na kuwanyima wenye sifa. Au pale ambapo nguvu kazi kubwa inatumika kushughulikia
rushwa ya ngono. Vilevile, inadumaza jitihada za kupambana na umaskini, kujenga na
kuimarisha demokrasia shirikishi na utawala bora.
Katika ngazi ya Mhanga, rushwa ya ngono hugeuza haki za wahanga kuwa ni upendeleo na siyo
stahiki yake. Inapohusu kumpokonya mtu haki yake husababisha madhara kwenye nyanja
mbalimbali: inamnyima huyu mhanga stahiki yake hivyo inagusa maisha ya mhusika kwani
anapolazimika kushiriki kwenye rushwa ya ngono, anaweza kupata jeraha lisilotibika kwenye
12
Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu Hassan aliyasema hayo wakati akifungua Mkutano wa Nane wa chama cha
Majaji Wanawake Tanzania 2017. http://mwaseba5.blogspot.com/2017/01/rushwa-ya-ngono-bado-ni-tishio-
nchini.html
11
maisha yake, mahala pengine anaweza kugeuzwa mtumwa wa ngono, na hivyo kushindwa
kukuza vipaji vyake vya uhalisia.
Katika ngazi ya Jamii, rushwa ya ngono husababisha jamii kukosa huduma bora kutokana na
watoa huduma waliopatikana kutokana na rushwa ya ngono kutokuwa na weledi na maadili ya
kutosha. Aidha, baadhi ya waathirika waliolazimishwa rushwa ya ngono wanakuwa na msongo
wa mawazo kitu kinachosababisha magonjwa ya afya ya akili.
Kwa muhtasari rushwa ya ngono ina madhara mengi yakiwemo ya kunyima haki za kikatiba
kama kugeuza stahiki kuwa upendeleo, kudhalilisha utu wa waathirika, kusabisha matumizi
mabaya ya rasilimali watu pamoja na kudumaza uchumi na maendeleo ya nchi kwa ujumla.
2.4 Kiunzi cha dhana
Rushwa ya ngono ni matokeo ya mambo makuu matatu: Kwanza, mtu mwenye mamlaka
ambapo kwa mazingira ya Taasisi za Elimu ya juu ni Wahadhiri na Watawala. Pili, katika
utekelezaji wa majukumu yake kama vile kutoa alama kwenye mitihani, kupandisha vyeo,
uhamisho na malazi. Tatu, kumwekea sharti la ngono mtaka huduma kama mwanafunzi au
mtumishi wa chuo ili kupata huduma au upendeleo wowote.
2.5 Maana tumizi
2.5.1 Rushwa ya ngono
Katika utafiti huu, rushwa ya ngono inamaanisha matumizi mabaya ya madaraka ili kujinufaisha
kingono isivyo halali. Aidha rushwa ya ngono hugeuza haki na stahiki kuwa ni upendeleo. Aina
hii ya rushwa haitumii fedha au vitu kushawishi ila hutumia nguvu ya kisaikolojia kumshawishi
mhanga kutoa mwili wake kingono ili kupata huduma au haki. Aidha, mhusika anayedai aina hii
ya rushwa ni lazima awe na madaraka au mamlaka ambayo anaamua kuyatumia vibaya kwa
kudai ngono ili atoe upendeleo kwa asiyestahili, au kumnyima haki anayestahili kwa kitendo cha
kukataa rushwa ya ngono.
12
2.5.2 Huduma
Huduma katika utafiti huu ni mahitaji ambayo anayahitaji mtumishi wa chuo au mwanafunzi
anapokuwa katika mazingira ya chuo kama vile kudahili, malazi, mikopo, kufundisha, kutunga
mitihani, kusahihisha, kutoa alama, ufadhili wa masomo, kupandisha vyeo, kuhamisha na kuajiri.
2.5.3 Mamlaka
Katika utafiti huu, Mamlaka ni dhamana ya kufanya au kutoa maamuzi kuhusu huduma
zinazotolewa na chuo.
13
SURA YA TATU
3.0 MBINU ZA UTAFITI
Sura hii inaainisha eneo la utafiti, mbinu za kukusanya taarifa, vyanzo vya taarifa, sampuli na
mbinu za uchambuzi wa matokeo ya utafiti.
3.1 Usanifu wa utafiti
Utafiti huu ulitumia mbinu ya uchunguzi kifani (case study) kukusanya taarifa za utafiti. Kupitia
mbinu hii data za kitaamuli (qualitative data) na data za kitakwimu (quantitative data)
zilikusanywa ili kujibu maswali ya utafiti. Njia hii ilitumika kuchunguza kwa kina vyuo vikuu
viwili vya umma nchini, kulinganisha na kutofautisha namna, aina, na sababu za vitendo vya
rushwa ya ngono katika vyuo hivyo. Matumizi ya mbinu hii yalizingatia manufaa ya kupata
taarifa za kina kuhusu rushwa ya ngono na namna inavyotendeka katika vyuo vikuu na matumizi
ya njia zaidi ya moja ya ukusanyaji wa taarifa – mfano; mahojiano, uchambuzi wa nyaraka,
mijadala ya vikundi ya wazi na ushuhudiaji ili kufikia malengo ya utafiti.
3.2 Eneo na muda wa utafiti
Utafiti huu ulifanyika katika vyuo vikuu vya Dar es Salaam na Dodoma kwa kipindi cha Januari
na Februari 2020. Chuo kikuu cha Dar Es Salaam ndiyo chuo kikuu cha kwanza cha umma hapa
nchini kilichozalisha viongozi wengi kuliko vyuo vyote. Vilevile, ni chuo kikubwa nchini na
kinachodahili wanafunzi wengi zaidi. Kwa mwaka 2017/2018 pekee, chuo hiki kilifanya udahili
wa wanafunzi 13,626 ambao ni sawa na 21% ya wanafunzi wote waliodahiliwa kwenye taasisi
za elimu ya juu nchini kwa mwaka.
Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ni chuo cha pili cha umma kilichopo makao makuu ya nchi.
Chuo hiki kina ndaki saba ambazo zinapokea wanafunzi kila mwaka wa masomo. Kwa mwaka
wa masomo 2017/2018, chuo hiki kilidahili wanafunzi 9,151 (Tanzania Commission for
Universities – TCU, 2018).
Hivyo, vyuo hivi viwili vilihusishwa katika utafiti huu kutokana na historia ya vyuo hivi,
umiliki wake (vyuo vya umma) na wingi wa udahili wa wanafunzi. Hivi ndivyo vyuo vikuu
vikubwa viwili vinavyomilikiwa na Serikali na vinavyoongoza kwa kudahili wanafunzi wengi
zaidi nchini. Aidha, kutokana na ukubwa wake na idadi kubwa ya wanafunzi nchini, utafiti
14
uliona kuwa ni sehemu sahihi ya kuweza kuchunguza na kujenga msingi wa kisayansi kuhusu
rushwa ya ngono nchini.
3.3 Sampuli
Sampuli iliyohusika katika utafiti huu ilipatikana kwa utaratibu wa mpangilio maalum
(Purposive sampling), usampulishaji tajwa (snowball sampling) na usampulishaji nasibu tabaki
(Stratified random sampling). Utaratibu wa mpangilio maalum ulitumika kuwapata wasailiwa
waliopatikana kutokana na vyeo vyao au nafasi zao na uzoefu wao katika Taasisi za elimu ya
juu. Usampulishaji tajwa ulitumika kupata waathiriwa wa vitendo vya rushwa ya ngono. Aidha,
usampulishaji nasibu tabaki ulitumika kupata wanafunzi na watumishi katika maeneo ya utafiti
waliofikiwa na utafiti huu ambapo waligawanywa kwenye tabaki kwa kuzingatia ndaki, vitivo,
shule na idara zao.
3.4 Ukubwa wa sampuli
Utafiti huu uliwahusisha wahojiwa 589: kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam (352) na chuo
kikuu cha Dodoma (237). Utafiti huu umetumia mbinu ya uchunguzi kifani (case study) kwa
lengo la kupata taarifa za kina juu ya namna rushwa ya ngono inavyotendeka katika taasisi za
elimu ya juu zilizofikiwa na utafiti. Waandishi Yin (2012); Crouch and Mckenzie (2006) na
Guest et al., (2006) wanasisitiza kuwa, mbinu hii inataka watafiti kutumia njia mbalimbali
kukusanya data za kina kujibu malengo ya utafiti kuliko kuangalia idadi ya sampuli. Utafiti huu
ulikusanya taarifa za kina na za kutosha kutoka kwa wanafunzi na watumishi 589 wa Vyuo
Vikuu vya Dar es Salaam na Dodoma.
3.5 Mbinu za ukusanyaji wa taarifa
Utafiti huu ulikusanya taarifa za msingi kwa namna tatu: kwanza, kwa kutumia hojaji kwa
watumishi na wanafunzi 589 kama Jedwali 1 linavyoainisha.
15
Jedwali 1: Mgawanyo wa hojaji
Na Mhusika UDOM UDSM Jumla Jumla
kuu Me Ke Me Ke Me Ke
1 Wahadhiri/watumishi 40 34 40 46 80 80 160
2 Wanafunzi 70 93 132 134 202 227 429
Jumla 110 127 172 180 282 307 589
Me = Wanaume Ke = Wanawake
Pili, kupitia mijadala ya wazi ya vikundi (Focus Group Discussion) tisa (9) ikiwahusisha
watumishi, wahadhiri na wanafunzi (Jedwali 2).
Jedwali 2: Idadi ya makundi kwenye majadiliano ya vikundi
Na. Chuo Idadi ya makundi ya
majadiliano
Idadi ya washiriki
1 UDSM 6 47
2 Dodoma 3 36
Jumla 9 83
Mijadala ya wazi ilifanyika kwa wahadhiri, wanafunzi na watumishi wengine wa vyuo vikuu.
Mijadala hii ilifanyika katika mgawanyo wa kundi la watu kuanzia sita (6) hadi kumi na mbili
(12) kwa kila kundi. Kila kundi la watu lilipatikana kwa kutumia usampulishaji nasibu sahihi
(Simple random sampling) ambapo wanafunzi, wahadhiri na watumishi walichaguliwa kwa
kuzingatia ndaki, vitengo, na idara zao. Mijadala ilifanyika kwa kila kundi kwa kuzingatia jinsi
za washiriki ambapo wahadhiri wa kiume walipatikana kuanzia sita (6), wahadhiri wa kike
kuanzia sita (6), wanafunzi wa kike kuanzia sita (6), wanafunzi wa kiume kuanzia sita (6),
watumishi wasio wahadhiri kuanzia sita (6) wa kiume na wa kike halikadhalika.
Tatu, mahojiano na Wahojiwa Lengwa (key informants) 55 ambao walipatikana kwa njia mbili
za usampulishaji tajwa (snow balling) na kwa utaratibu wa mpangilio maalumu (Purposive
sampling) kama jedwali 3 linavyoonesha.
16
Jedwali 3: Idadi ya wahojiwa lengwa
Na. Mhusika UDSM UDOM
Idadi Idadi
1 Viongozi wa ngazi ya juu Chuoni
(Makamu Mkuu wa Chuo na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo)
3 3
2 Rasi/Amidi 8 6
3 Kamati ya Maadili, Wakurugenzi wa vitengo mbalimbali na
Mshauri wa Wanafunzi
3 5
4 Viongozi wa Serikali ya Wanafunzi na Klabu ya wapinga
rushwa chuoni
3 8
5 Watalaam wengine wenye uelewa wa kina kuhusu vitendo vya
rushwa ngono Chuoni
9 7
Jumla Kuu 26 29
Taarifa za upili zilikusanywa kwa kupitia nyaraka zinazohusu sheria, kanuni na kumbukumbu
mbalimbali za malalamiko ya vitendo vya rushwa ya ngono. Aidha, takwimu hizo
zilichambuliwa na kutafsiriwa kwa ajili ya kuandaa taarifa ya utafiti.
3.6 Uchambuzi wa taarifa
Utafiti ulitumia programu tumizi ya kuchambua takwimu za kisayansi jamii (SPSS) kuchambua
taarifa zilizokusanywa kwa njia ya madodoso. Aidha, taarifa zilizopatikana kwa njia ya
mahojiano, usaili, na mijadala ya wazi zilichambuliwa kwa kutumia uchanganuzi maudhui
(content analysis).
17
SURA YA NNE
4.0 MATOKEO YA UTAFITI
4.1 Wasifu wa wahojiwa
Jedwali 4 linaonesha wasifu wa wahojiwa kwa njia ya hojaji kutoka katika vyuo vikuu viwili vya
Umma ambavyo ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Chuo Kikuu cha Dodoma. Kwa kuzingatia
vigezo vya jinsi, umri, mwaka wa masomo na muda kazini wa wahojiwa hakuna shaka taarifa
zilizopatikana zinajibu malengo ya utafiti huu.
Jedwali 4: Wasifu wahojiwa kwa njia ya hojaji
Kundi Kigeu (variable) Mwitiko
Mdafao
(Frequency)
Chuo
Kikuu
cha Dar
es
Salaam
Mdafao
(Frequency)
Chuo
Kikuu
cha
Dodoma
Wastani
(%)
Wanafunzi Jinsi Wanaume 132 49 70 46 47.5
Wanawake 134 51 93 54 52.5
Umri 18 – 25 237 89 149 91 90.0
26 – 30 22 8 11 7 7.5
31 – 35 7 3 3 2 2.5
Mwaka
wa
masomo
Mwaka wa
kwanza
37 14 50 31 22.5
Mwaka wa
pili
81 31 43 26 28.5
Mwaka wa
tatu
110 41 60 36 38.5
Mwaka wa
nne
38 14 10 7 10.5
Watumishi Jinsi Wanaume 40 46.5 40 53.9 50.2
Wanawake 46 53.5 34 46.1 49.8
Umri 18 – 30 21 24 13 17.5 20.8
31 – 40 31 36 39 52.5 44.3
41 – 50 27 34 16 21.8 27.9
51– 60 5 6 6 8.2 7.1
Muda wa
utumishi
< Mwaka 1 9 11 0 0.0 5.5
Mwaka 1 – 5 21 24 23 25.0 24.5
> Miaka 5 56 65 51 75.0 70.0
Kwa upande wa jinsi, kuna uwiano kati ya wanawake na wanaume kunakosaidia kuaminika kwa
matokeo. Kuhusu umri, wahojiwa wote wapo kwenye rika la watu wazima (majority age) hivyo
taarifa zao ni za kuaminika (Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - JMT, 1977). Aidha, kwa
18
kuzingatia kigezo cha mwaka wa masomo na muda wa watumishi kazini, wahojiwa wana uzoefu
wa kutosha kuweza kutoa taarifa za kuaminika.
4.2 Uwepo wa rushwa ya ngono
Kifungu cha 25 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11/2007 kinatamka
“Any person being in a position of power or authority, who in the exercise of his authority,
demands or imposes sexual favours or any other favour on any person as a condition for giving
employment, a promotion, a right, a privilege or any preferential treatment, commits an offence”.
Kimsingi kifungu hiki kinaharamisha kitendo chochote cha mtu mwenye mamlaka kumuwekea
kigezo cha ngono mtu yeyote anayetaka huduma yake. Kwa mujibu wa kifungu hiki, rushwa ya
ngono hutokea pale mtu yeyote aliye na mamlaka au madaraka akiyatumia mamlaka hayo kwa
kumlazimisha au kumshawishi mtu mwingine kufanya naye tendo la ngono kwa ahadi ya
kumpatia ajira, promosheni, au upendeleo fulani. Hivyo, mtumishi yeyote wa chuo kikuu
mwenye mamlaka/madaraka anayetumia nafasi yake kumuwekea kigezo cha kupewa ngono
mwanafunzi au mtumishi mwenzake anayetaka huduma anakuwa ametenda kosa kwa mujibu wa
sheria hii. Kwa mantiki hii utafiti ulilenga kujua uwepo wa rushwa ya ngono katika vyuo vikuu
kwa kuangalia iwapo wadau wana uelewa wa dhana hii ya rushwa ya ngono na hali ya tatizo la
rushwa ya ngono.
Matokeo ya utafiti yanaonesha wahojiwa wengi (wanafunzi 81.6% na watumishi 91.4%)
walikuwa na uelewa wa dhana ya rushwa ya ngono (Jedwali 5). Aidha, matokeo yanashabihiana
kwa vyuo vyote viwili vilivyotafitiwa, na yanabainisha kuwa wahojiwa wanaifahamu rushwa ya
ngono kwa mujibu wa kifungu cha 25 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na.
11/2007.
19
Jedwali 5: Mwitiko wa uelewa wa dhana ya na uwepo wa rushwa ya ngono
Kigeu (variable) Kundi Mwitiko
Mdafao
(Frequency)
*Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam
(%)
Mdafao
(Frequency)
*Chuo
Kikuu
cha
Dodoma
(%)
Wastani
Uelewa wa dhana ya rushwa ya
ngono
Wanafunzi 230 86.4 125 76.7 81.6
Watumishi 82 95.3 65 87.6 91.4
Uwepo wa matukio ya rushwa ya
ngono
Wanafunzi 153 57.5 89 54.6 56.1
Watumishi 59 68.6 52 63.1 65.9
Aidha, matokeo yanaonesha zaidi ya 50% ya wahojiwa (wenye uelewa) walieleza uwepo wa
rushwa ya ngono katika vyuo vikuu vilivyofanyiwa utafiti. Matokeo haya yanamaanisha kwamba
rushwa ya ngono ni tatizo katika vyuo vikuu hivi.
Matokeo haya yanathibitishwa na taarifa za kitaamuli (Qualitative data) ambapo wahojiwa
walionesha uelewa na uwepo wa rushwa ya ngono katika vyuo vikuu vilivyofikiwa katika utafiti
huu. Baadhi ya wahojiwa walieleza yafuatayo:
“……rushwa ya ngono ni pale ambapo mtu anahitaji huduma fulani lakini
hapewi na aliye na nafasi ya kumpa huduma hiyo kwa kumtaka kutoa ngono
ndipo apate huduma husika….”
“……rushwa ya ngono kuwa ni kitendo cha mwenye mamlaka kulazimisha
ngono ndipo atoe haki……”
“…rushwa ya ngono ni mtu kutumia nafasi yake ya kimadaraka ili
kujinufaisha kingono….”
“………. rushwa ya ngono ipo na kwa sasa hali ni tete …mtu akijitokeza
kufuatilia rushwa ya ngono anakuwa amejiingiza katika hatari kubwa hata
kutishiwa maisha ……ni sawasawa na kupambana na madawa ya kulevya….”
“……. Mwalimu alimtongoza mwanafunzi wa kigeni katika programu ya
postgraduate, wakati wanafanya majadiliano ya Tasnifu (dessertation) yake,
mwalimu alianza kumshikashika, mwanafunzi alipiga kelele baada ya taarifa
kuenea mwalimu huyo alipelekwa mafichoni kwa muda wa miaka mitatu na
baadaye kurudishwa chuoni hapo.”
20
Kutokana na taarifa za kitakwimu na kitaamuli, dhana ya rushwa ya ngono katika vyuo vikuu
inaeleweka na kwamba tatizo la rushwa ya ngono lipo katika vyuo vikuu na linatakiwa
kuwekewa mkakati wa kulidhibiti. Matokeo ya utafiti huu yanashabihiana na utafiti uliowahi
kufanywa na Mukama (2017) kuhusu mapambano dhidi ya rushwa ya ngono kwa wanafunzi wa
Taasisi za elimu ya juu nchini Tanzania. Katika utafiti wake alibaini kuwa kuna rushwa ya ngono
katika Taasisi za elimu ya juu na kwamba waathirika wakuu ni wanafunzi wa kike. Aidha,
watafiti walitajiwa majina ya watu wanaotuhumiwa kujihusisha na vitendo vya rushwa ya ngono,
hata hivyo kutokana na maadili ya utafiti majina hayo yamehifadhiwa. Matokeo haya
yanadhihirisha kukiukwa kwa kifungu cha 25 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
Namba 11/2007 kulikofanywa na baadhi ya watu wenye mamlaka katika vyuo hivi.
Hivyo, ni muhimu kutafuta vyanzo/sababu za kuwepo kwa vitendo vya rushwa ya ngono,
kuchunguza mifumo iliyopo ya udhibiti ili kupima ufanisi wake na kubaini mbinu zinazotumika
kuendeleza vitendo vya rushwa ya ngono katika vyuo hivi. Kwa kufanya hivyo kutasaidia
kuweka mikakati ya kudhibiti na kuondoa athari zitokanazo na rushwa ya ngono. Kuna athari
nyingi zinazotokana na rushwa ya ngono katika taasisi za elimu ya juu zikiwemo: vyuo kuzalisha
watendaji wenye uwezo mdogo kifikra; kuathiri utendaji wa taasisi; kudhalilisha utu wa mtu na
kusababisha mtu kushindwa kujiamini; kuathiri saikolojia ya waathiriwa wa vitendo vya rushwa
ya ngono; magonjwa ya kuambukiza kama UKIMWI; mimba zisizotarajiwa; kushusha morali ya
utendaji kazi kwa watumishi; upendeleo kwa baadhi ya wanafunzi wanaotoa rushwa ya ngono;
kuporomoka kwa maadili ya wanafunzi, wahadhiri na watumishi wasio wahadhiri na kuharibu
taswira ya vyuo ndani na nje ya nchi. Kwa upande mwingine, Mukama (2017) katika utafiti
wake ameeleza kuwa rushwa ya ngono huvunja heshima ya mtu binafsi na Taasisi.
4.3 Sababu za kuwepo vitendo vya rushwa ya ngono
Kwa mujibu wa modeli ya Klitgaard (1998), rushwa hushamiri katika mazingira ya ukiritimba,
uhuru wa kufanya maamuzi usiodhibitiwa na mahali ambapo hakuna uwazi na uwajibikaji. Kwa
kuzingatia modeli hii, utafiti ulitaka kujua sababu zinazochochea rushwa ya ngono katika vyuo
vikuu kwa kuwataka wahojiwa kueleza chanzo cha kuwepo vitendo vya rushwa ya ngono.
Matokeo yanashabihiana kwa vyuo vyote viwili vilivyotafitiwa. Aidha, kwa mujibu wa matokeo
ya kitakwimu matokeo yanaonesha kuwepo kwa sababu tano ambazo ni ukosefu wa maadili,
ushawishi wa mtu mwenye mamlaka, mfumo wa utoaji taarifa kutokuwa rafiki, mifumo dhaifu
21
ya kushughulikia rushwa ya ngono na mamlaka ya kutoa alama za mitihani kuachwa chini ya
walimu pekee (Jedwali 6).
Jedwali 6: Mwitiko wa wahojiwa kuhusu sababu za rushwa ya ngono
Kundi Sababu Mwitiko
Mdafao
(Frequency)
*Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam
(%)
Mdafao
(Frequency)
*Chuo
Kikuu cha
Dodoma
(%)
Wastani
Wanafunzi Ukosefu wa maadili 118 56.7 43 26.4 63.0
Ushawishi wa mtu
mwenye mamlaka
75 36.1 30 19.3 27.7
Mfumo wa utoaji
taarifa kutokuwa rafiki
15 7.2 18 11.3 9.3
Watumishi Ukosefu wa Maadili 44 74.6 25 66.1 76.5
Mifumo dhaifu ya
kushughulikia rushwa
ya ngono
8 13.5 2 6.2 9.8
Mamlaka ya kutoa
alama za mitihani
kuachwa chini ya
walimu pekee
7 11.9 4 15.5 13.7
*Multiple Responses
Matokeo yanaonesha kuwa hududi (range) ya mwitiko ni 9.3% hadi 76.5% kwa maana ya
mfumo wa utoaji taarifa kutokuwa rafiki na ukosefu wa maadili mtawalia. Ukosefu wa maadili
umejitokeza zaidi kwenye utafiti huu kuwa miongoni mwa sababu zinazochochea rushwa ya
ngono kwenye vyuo vikuu, ukifuatiwa na matumizi mabaya ya madaraka/mamlaka na udhaifu
wa mifumo. Sababu hizi zinaweza kudhoofisha misingi ya uwajibikaji na uwazi katika vyuo hivi.
Kwa upande kwa taarifa za kitaamuli (Qualitative data) utafiti ulibaini sababu za kuendelea
kuwepo kwa vitendo vya rushwa ya ngono licha ya kuwepo kwa sera, miongozo, na hata sheria
ndogondogo zenye kuharamisha rushwa ya ngono. Sababu hizo ni: mapungufu kwenye mifumo
ya kuthibiti matumizi mabaya ya mamlaka, kwenye eneo la kutahini, hususani madaraka
makubwa wanayopewa wahadhiri kwenye eneo la kutahini, mapungufu yatokanayo na mifumo
ya kusimamia uwajibikaji katika utoaji wa huduma, ufinyu wa huduma kama vile nyumba za
bweni kwa wanafunzi wa kike, udhaifu wa mifumo ya ajira hasa wakufunzi inayojali zaidi
ufaulu wa darasani bila kujali weledi, uwezo wa kufundisha na maadili ya wanaoajiriwa.
22
Vilevile, ongezeko la wanafunzi ambalo halikuenda sambamba na ongezeko la waalimu wenye
uwezo wa kumudu mzigo wa kazi kwa ueledi na nidhamu pamoja na mmomonyoko wa maadili
kwa jumla.
Matokeo haya yanashadidishwa na baadhi ya shuhuda ambazo wahojiwa walieleza kuwa ni
visababishi vya rushwa ya ngono katika vyuo vikuu vilivyofikiwa katika utafiti huu. Baadhi ya
wahojiwa walieleza yafuatayo:
“………...kuna vinara wa rushwa ya ngono ambao tunapishana nao kwenye korido
lakini hawastahili kuwepo chuoni maana wanatajwa sana kwenye mitandao na kwenye
taarifa mbalimbali za uchunguzi…….na hakuna pa kukimbilia kwani hata baba
anafanya kwahiyo hakuna wa kulikemea……hii ni sawa na maneno kwenye Biblia
yanayosema kuwa na asiye na dhambi na awe wa kwanza kumrushia mawe mwenye
dhambi…. ninajisikia vibaya kuwa sehemu ya chuo kikuu au kujitambulisha kuwa ni
mhadhiri wa chuo kikuu…...”
“……wahadhiri hawana mafunzo ya maadili ya ufundishaji (teaching ethics) ……. ile
dhana ya mwalimu kuwa mzazi, mlezi na mwenye uadilifu kwa wahadhiri hawa vijana
haipo kwani wamekuwa na tamaa za kingono kwa wanafunzi wao, wanapenda
kubadilisha wanafunzi wa kike kingono kila mwaka wa masomo unapoanza kwa
msemo wa FUSO limetema……”
“……Wahadhiri kuwapata wanafunzi kingono hawatumii fedha au kutongoza bali
wanatumia nafasi zao za uhadhiri…….”
“……….baadhi ya wahadhiri wamekuwa na tabia ya kuwataka kingono watumishi
wanaofanya usafi katika ofisi zao na wanapokataliwa kupewa rushwa ya ngono hutoa
mapendekezo ya kuwatoa katika ofisi walizopangiwa kufanya usafi……wahadhiri
waliokubaliwa ngono walikuwa wakifika ofisini majira ya saa kumi na moja alfajiri
kwa lengo la kupokea rushwa ya ngono…….”
23
Hata hivyo, wakati wa ufuatiliaji ilibainika kuwepo baadhi ya wahadhiri wanaozingatia maadili
ya kazi zao. Baadhi ya wahojiwa walieleza yafuatayo:
“……..kuna mwanafunzi alimuandikia mhadhiri wa somo barua pepe na kumuomba
amsaidie katika somo lake atamlipa chochote lakini sio pesa…….mhadhiri aliamua
kuwashirikisha wanafunzi wengine na baadhi ya wahadhiri idarani…….aliwaasa
wanafunzi wasome kwa bidii na kuzingatia maadili……”
“…….kuna mwanafunzi mmoja alikiri kosa la kumfanyia „Quiz‟ rafiki
yake……mwanafunzi aliyefanyiwa „Quiz‟ alimshawishi mhadhiri kingono baada ya
kubaini kuwa kosa walilofanya ni la kufukuzwa chuo…….mhadhiri huyo
hakushawishika na kuchukua hatua ya kumkabidhi mwanafunzi kwa mkuu wa
idara…….”
Kwa upande wa mifumo wahojiwa walieleza yafuatayo:
“……mfumo bado siyo mzuri maana wanafunzi wengi walioripoti wamekuwa
wakifukuzwa chuoni……na wanaotolewa taarifa wamekuwa wakikingiwa kifua
na uongozi……lazima uwepo mfumo wa kumlinda mtoa taarifa na mtuhumiwa
asijue mtoa taarifa ni yupi…...”
“……kumekuwa na uingiliaji wa mifumo ya matokeo (Academic Registration
Information System, ARIS) na kubadilisha matokeo pasipo kufuata utaratibu…...”
“……...Kuna mwanafunzi ambaye aliombwa ngono na mhadhiri, lakini alikataa
na kusababisha yule mhadhiri kumfelisha (kumkamata) yeye pamoja na
mwanafunzi mwingine wa kiume aliyekuwa mpenzi wake na hata walipofanya
mtihani wa marudio (supplementary) bado hawakufaulu na hivyo kushindwa
kuendelea na somo hilo mpaka mwaka uliofuata……...”
24
Kwa ujumla matokeo haya yanabainisha kuwa rushwa ya ngono katika vyuo vikuu vya Dodoma
na Dar es Salaam inasababishwa na matumizi mabaya ya mamlaka yanayotokana na ukosefu wa
maadili kwa wenye mamlaka na udhaifu wa mifumo ya utoaji taarifa za rushwa ya ngono,
ushughulikiaji wa matukio ya rushwa ya ngono na utungaji na usahihishaji wa mitihani. Hali hii
inaashiria kuwepo kwa uwajibikaji mdogo katika vyuo hivi. Kwa mantiki hii, kuna haja ya
kutazama mifumo ya udhibiti wa rushwa ya ngono kwenye vyuo vikuu vya Dodoma na Dar es
Salaam na hasa kwa kuangalia uwezekano wa kuweka udhibiti katika mchakato wa kutoa
maendeleo ya kitaaluma (course work) ambapo kwa sasa yapo mikononi mwa wahadhiri.
4.4 Mifumo ya udhibiti ya ndani dhidi ya rushwa ya ngono
Kupitia mapitio ya nyaraka, utafiti ulibaini kuwepo kwa kanuni, miongozo, sheria na taratibu
mbalimbali zilizowekwa na nchi pamoja na vyuo ili kuharamisha vitendo vya rushwa ya ngono.
Utafiti ulichambua na kupitia: Kanuni za mienendo na maadili ya utumishi wa umma za mwaka
2014; Sheria ndogo ndogo za vyuo kama sheria za chuo kikuu cha Dar es salaam, 2011 na sheria
za chuo kikuu cha Dodoma, 2012; sera ya kusimamia ubora wa Elimu, 2007 (Chuo kikuu cha
Dar es salaam); Kanuni za maadili kwa watumishi wa Chuo kikuu cha Dar es salaam, 2018; na
Kanuni za maadili za chuo kikuu cha Dodoma, 2012. Nyaraka hizi zote zinaharamisha
mahusiano ya kingono kati ya wanafunzi na watumishi wa chuo, zinapinga unyanyasaji wa
kijinsia, zinakata kutumia rushwa ya ngono kutoa ufaulu, kufanya mawasiliano yoyote
yanayoashiria ngono na kufanya vitendo vyovyote vinavyoashiria ngono. Nyaraka hizi zinalenga
kuweka mazingira salama na rafiki ya kutolea taaluma, kufanya utafiti na kutoa huduma kwa
umma wote wa watanzania na wasio watanzania. Lakini kuwepo kwa vitendo vya rushwa ya
ngono kunafifisha juhudi hizi.
Kutokana na kuwepo kwa nyaraka hizi zinazotoa mwelekeo wa namna vyuo hivi
vinavyowajibika kudhibiti rushwa ya ngono; utafiti ulilenga kupima ufanisi wa mifumo hii
katika kuidhibiti rushwa ya ngono katika maeneo yake. Hivyo, utafiti ulipima ufanisi wa mifumo
hii katika kutoa ulinzi kwa mtoa taarifa juu ya rushwa ya ngono; kutoa ulinzi wa mhanga wa
rushwa ya ngono; kupima uelewa wa wadau (wanafunzi na watumishi) kuhusu uwepo wa
mifumo hii; uzingatiaji wa mifumo hii; uwazi na uwajibikaji katika kutekeleza matakwa ya
mifumo hii.
25
Utafiti ulibaini udhaifu kwenye mifumo ya ndani ya udhibiti wa rushwa ya ngono. Jedwali 7
linaonesha hududi (range) ya 10.7% - 38.2% ya wahojiwa walikubali kuwepo kwa sera,
miongozo na taratibu za udhibiti wa rushwa ya ngono. Hata hivyo, zaidi ya 60% ya wahojiwa
hawakufahamu uwepo wa sera, kanuni, sheria na miongozo ya kudhibiti rushwa ya ngono.
Aidha, matokeo yanashabihiana kwa vyuo vyote viwili vilivyotafitiwa. Hali hii inaweza
kudunisha mifumo ya udhibiti wa rushwa ya ngono katika vyuo hivi. Hii inamaanisha kwamba,
wanajumuiya wa vyuo husika hawawezi kuwawajibisha viongozi wao kwa kutokuchukua hatua
stahiki za kuzuia na kupambana na rushwa ya ngono.
Jedwali 7: Mwitiko wa wahojiwa kuhusu uwepo wa sera, miongozo na taratibu za udhibiti
rushwa ya ngono
Kundi Mfumo Mwitiko
Mdafao
(Frequency)
*Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam
(%)
Mdafao
(Frequency)
*Chuo
Kikuu cha
Dodoma
(%)
Wastani
Wanafunzi Sera inayotoa miongozo ya kukataza
udhalilishaji kijinsia
189 32.9 77 31.3 32.1
Uwepo wa elimu kwa wanafunzi wapya
kuhusu sheria, miongozo inayowalinda
wanafunzi wapya dhidi ya vitendo vya
rushwa ya ngono
203 35.3 101 41.1 38.2
Kuwepo kwa huduma za ushauri nasaha
kwa waathirika wa vitendo vya rushwa
ya ngono
120 20.9 42 17.1 19.0
Kuwepo kwa ulinzi kwa watoa
taarifa/wahanga wa rushwa ya ngono
63 10.9 26 10.5 10.7
Watumishi Sera inayotoa miongozo ya kukataza
udhalilishaji wa jinsia
50 24.4 44 23.0 23.6
Maadili ya kazi yanayobainisha vitendo
vya rushwa ya ngono
51 24.9 48 24.9 24.9
Taratibu na miongozo ya utahini
inayoziba mianya ya kutoa rushwa ya
ngono
37 18.0 32 16.6 17.5
Kuwepo kwa kamati za maadili ya
wahadhiri
41 20.0 47 24.3 22.1
Taratibu zilizo wazi za utoaji wa
rasilimali fedha za kufanya utafiti
26 12.7 22 11.2 11.9
*Multiple Response
26
Taarifa za kitaamuli zinaonesha kuwepo kwa: uadilifu mdogo; ushirika katika kutenda kosa kati
ya watuhumiwa na wenye maamuzi; uvujaji wa taarifa na vitisho kwa watoa taarifa; urasimu wa
mfumo mzima wa utoaji na ushughulikiaji wa malalamiko; ukosefu wa elimu kuhusu sera,
kanuni na taratibu za kudhibiti maadili vyuoni; kutokuwa na takwimu za malalamiko wala hatua
zilizochukuliwa katika madawati ya jinsia/ofisi ya mshauri wa wanafunzi/kamati za maadili;
ukosefu wa mrejesho kuhusu hatua zilizochukuliwa na wenye mamlaka kutokana na
mapendekezo ya kamati za maadili; na imani ndogo kuhusu mfumo wa kushughulikia
malalamiko.
Kwa upande wa uadilifu mdogo, uongozi na kamati za maadili zinatajwa kutokuwa na maadili.
Baadhi ya wahojiwa walieleza:
“……watu wa kamati ya maadili wao wenyewe wanafanya vitu ambavyo
vinawafanya watu wasiwaamini na kuna mhadhiri ana ushawishi mkubwa katika
kutenda vitendo vya rushwa ya ngono……mara nyingi malalamiko yanayopelekwa
hayashughulikiwi…...”
“…...mfumo mzima umeoza…...hakuna pa kukimbilia…...hata wanaopaswa
kushughulikia tatizo hilo nao ni sehemu ya tatizo…...”
“……ebu fikiria mwanafunzi anaenda kwa mshauri wa masomo kuomba ushauri wa
hatua za kuchukua baada ya kutakwa kingono na mhadhiri……lakini „academic
advisor‟ tena mwenye jinsi ya kike anamwambia akubali kwakuwa ni kitendo cha
dakika tano tu kamaliza na anapata „degree‟ yake……ampe tu….”
Mmoja wa wahojiwa alieleza:
“……mfumo hauko wazi……kuna changamoto kubwa ya kumlinda mtoa
taarifa…….muundo wa uongozi unafifisha utoaji wa taarifa…….sanduku la maoni
lipo na husimamiwa na kamati ya maadili...….wanafunzi hawataki kuandika ili tatizo
27
lake lishughulikiwe ila tunashugulikia kwa mjadala kwa kumfuata mlengwa na
kumuonya……”
Ukosefu wa maadili kwa baadhi ya viongozi na wajumbe wa kamati za maadili kunatajwa
kusababisha kukosekana kwa uwajibikaji, jambo linalosababisha watumishi na wanafunzi
kupoteza imani kwa uongozi na kamati hizo. Pamoja na uwepo wa mifumo ya ndani katika
kusimamia maadili ya kiutumishi na kiuwanafunzi katika vyuo vyote viwili, sera bado zina
mianya inayosababisha vitendo hivi kuendelea kutendeka. Baadhi ya wahojiwa walisema
yafuatayo:
“…...tabia ya kulindana miongoni mwa wahadhiri inatokana na hofu ya kufukuzwa
kazi……kulindana kunasababisha wanafunzi na watumishi kupoteza
imani……kuwepo kwa kamati huru na kuwahamisha vituo vya kazi wahadhiri
wanaotuhumiwa kungesaidia kudhibiti vitendo vya rushwa ya ngono…...tusikae na
watu wasio na maadili vyuoni……”
Kulindana na ukosefu wa uwazi katika mifumo kunaelezwa kuwa chanzo cha uvujaji na vitisho
kwa watoa taarifa dhidi ya wahadhiri au watumishi wenye mamlaka. Kwa baadhi ya waliojitolea
kutoa taarifa hizo walipata vitisho vya kuhatarisha kazi, taaluma na maisha yao. Hii inaonesha
kukosekana kwa utaratibu au mfumo wa kulinda watoa taarifa (whistleblower protection) au
wahanga wa vitendo vya rushwa ya ngono. Haya yanadhihirishwa na maelezo ya baadhi ya
wahojiwa:
“…….kuna mwanafunzi alitoa taarifa kwa Rasi wa Ndaki dhidi ya mhadhiri
aliyemnyanyasa mwanafunzi wa kike kijinsia…….lakini Rasi alimjulisha mhadhiri
husika……mhadhiri huyo alianza kutoa vitisho kwa mwanafunzi aliyetoa tuhuma
hizo……”
“…...hata baadhi ya viongozi hapa chuoni wanaogopa kupeleka matukio kwenye
vikao kwa kuhofia kuundiwa zengwe na hatimaye kufukuzwa au kuondolewa
kwenye nafasi walizonazo……”
28
Vyuo kama Taasisi ya Elimu ya juu vina sera na miongozo ila bado upatikanaji wake ni
changamoto, na pale zinapopatikana hazipo kwenye lugha nyepesi. Mmoja wa wahojiwa
alieleza:
“…...sera, kanuni, sheria na miongozo ipo lakini haijulikani kwa wanafunzi na
watumishi, lakini inapotokea umefanya kosa ndipo zinaanza kutumika……”
Kwa mfano, ukipitia sheria ndogo ndogo za wanafunzi za mwaka 2011 za Chuo Kikuu cha Dar
es salaam na sheria ndogo ndogo za wanafunzi za Chuo Kikuu cha Dodoma za mwaka 2012,
lugha iliyopo imekaa kisheria na hivyo kuwa ngumu kueleweka kwa urahisi. Imebainika
kwamba taasisi ya jinsia kwa upande wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam inajitahidi kutoa elimu
ingawa kuna changamoto ya uwezeshaji kifedha na ofisi kwa waratibu wa madawati katika
Ndaki na Shule. Kazi hii inaonekana kama ni kazi ya ziada tu kwa waratibu.
Wahadhiri wapya wanatambua kuwepo kwa miongozo na kanuni za maadili, lakini wanadai
kutoziona kutokana na upatikanaji wake kutokuwa rahisi. Aidha, hali hii ilidhihirika wakati wa
utafiti ambapo ilikuwa vigumu kupata nyaraka hizi zinazosimamia sera, mifumo na miongozo.
Wakati wa utafiti ilibainika kwamba nyaraka hizo hupatikana wakati mtumishi/mhadhiri
anapopata matatizo ya kimaadili.
Vile vile, imebainika kwamba Taasisi ya Jinsia ndio yenye jukumu la kuelimisha wanajumuiya
ya chuo juu ya masuala ya jinsia ikiwepo na rushwa ya ngono. Hata hivyo, hakuna kitengo
maalumu chenye jukumu la kuhakikisha kinatoa elimu kuhusu nyaraka (sera, kanuni na
miongozo mbalimbali).
Kutokana na kuvuja kwa taarifa wahanga wengi wamekuwa waoga kutoa taarifa pale
wanapobaini au wanapoombwa rushwa ya ngono. Aidha, uoga unatajwa kusababishwa na
urasimu wa mfumo wa uwasilishaji na ushughulikiaji wa malalamiko, uelewa mdogo wa watoa
taarifa na mrejesho hafifu wa hatua zilizochukuliwa dhidi ya walalamikiwa. Wahojiwa walikuwa
na haya ya kueleza:
29
“…….mlolongo wa kuwasilisha taarifa ni mrefu ambapo kwa namna moja au
nyingine unasababisha kuvujisha taarifa……mfumo wa utoaji taarifa kwa
“anonymous submission” unaweza kusaidia kukabiliana na uvujaji wa siri……”
“……kuna changamoto kuu mbili katika utendaji kazi wa kamati za maadili ambazo
ni watu kutojitokeza kutoa ushahidi na kutopata mrejesho wa mapendekezo ya
kamati kutoka menejimenti ya chuo…….”
Hata hivyo, wananchi na wanafunzi kwa ujumla bado wana nafasi kisheria kutoa taarifa nje ya
taasisi husika pale wanapoombwa rushwa ya ngono. Kwa mujibu wa kifungu cha 7 cha sheria ya
Mwenendo wa Makosa ya Jinai, sura ya 20 mtu yeyote anayejua au atakayejua kutendeka au
kusudio la mtu yeyote kutenda kosa linaloadhibiwa chini ya Sheria anatakiwa wakati huohuo
kutoa taarifa kwa Afisa wa Polisi au kwa mtu mwenye madaraka katika sehemu hiyo ambaye
atawasilisha taarifa hiyo kwa Afisa wa Polisi msimamizi Msimamizi wa Kituo cha Polisi kilicho
karibu. Hivyo hivyo, chini ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na rushwa Na. 7/2011 kila
mwananchi katika kuzuia na kupambana na rushwa nchini anao wajibu wa kutoa taarifa pale
anapoona rushwa imetendeka, inatendeka au inakaribia kutendeka. Kifungu cha 39 cha sheria hii
kinatamka bayana kwamba kila mtu mwenye taarifa kuhusu kufanyika kwa vitendo vya rushwa
au kuhusiana na mpango wa kufanyika kwa vitendo vya rushwa unaopangwa na mtu au kundi la
watu anawajibika kutoa taarifa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).
Vifungu hivyo vyote vinalenga kwenye kushirikisha jamii katika kupambana na jinai ikiwemo
rushwa ya ngono. Hii inatokana na ukweli kwamba mapambano dhidi ya rushwa nchini
yanaweza yasifanikiwe kama umma wa Watanzania hautoshirikishwa kikamilifu.
Aidha, Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11/2007, inatoa ulinzi kwa watu
wanaotoa taarifa kuhusu rushwa au mashahidi ili kuhakikisha kwamba wananchi wanashiriki
kikamilifu na bila hofu katika vita dhidi ya rushwa. Kifungu cha 51(1)(a) cha sheria hii kinazuia
kutajwa kwa jina, makazi au anwani ya mtu aliyetoa taarifa kuhusu vitendo vya rushwa kwa
shahidi anayetoa ushahidi mahakamani. Hali kadhalika, kifungu cha 51(1)(b) kinazuia shahidi
kujibu swali ambalo jibu lake laweza kusababisha kujulikana kwa mtu aliyetoa taarifa juu ya
vitendo vya rushwa ambavyo vimesababisha kuwepo kwa mashitaka mahakamani. Kifungu cha
30
51(3) cha sheria hii kinafafanua kwamba kama mtoa taarifa atatishiwa kuumizwa au kulipiziwa
kisasi na watu aliowataja au maswahiba wao, basi Serikali itafanya mambo au jambo moja kati
ya haya: itampa mtu huyo ulinzi wa kutosha kulingana na vitisho anavyopata; itamlipa fidia
inayolingana na madhara aliyoyapata; itampatia msaada wa aina nyingine unaolingana na
mahitaji halisi. Kifungu cha 52 cha sheria hii kinatoa ulinzi kwa mtu yeyote anayetoa taarifa au
ushahidi kuhusiana na kufanyika kwa vitendo vya rushwa. Ulinzi huo ni kwamba mtoa taarifa
hatawajibika kwa kosa la jinai au madai kama wakati alipotoa taarifa alikuwa na sababu za
msingi za kuamini kuwa taarifa anazotoa ni za kweli.
Kwa ujumla, vitendo vilivyobainishwa na utafiti vinadhihirisha udhaifu wa mifumo ya ndani ya
udhibiti wa mianya ya rushwa ya ngono. Vitendo hivyo vinachavushwa na kuwepo kwa:-
mmomonyoko wa maadili, mamlaka makubwa ya mhadhiri kuhusu ufaulu wa mwanafunzi,
uvujaji wa taarifa, ufahamu hafifu wa haki za msingi na upendeleo katika utoaji huduma. Mambo
haya yanachangia kupunguza uwajibikaji na hatimae kuongezeka vitendo vya rushwa ya ngono
katika vyuo vilivyotafitiwa. Kwa mujibu wa modeli ya Klitgaard (1998), rushwa hushamiri
katika mazingira ya ukiritimba, uhuru wa kufanya maamuzi usiodhibitiwa na mahali ambapo
hakuna uwazi na uwajibikaji.
Aidha, vitendo vya rushwa ya ngono vinakiuka kifungu cha 25 cha Sheria ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa Namba 11/2007 kinachokataza rushwa ya ngono. Sheria hii
inaharamisha kitendo chochote cha mtu mwenye mamlaka kumuwekea kigezo cha ngono mtu
yeyote anayetaka huduma yake. Hivyo, mtumishi yeyote wa chuo kikuu mwenye
mamlaka/madaraka anayetumia nafasi yake kumuwekea kigezo cha kupewa ngono mwanafunzi
au mtumishi mwenzake anayetaka huduma anakuwa ametenda kosa kwa mujibu wa sheria hii.
Kwa mantiki hiyo, kuna umuhimu wa kuimarisha mifumo ya udhibiti katika vyuo hivi ili
kuimarisha maadili na kuongeza uwajibikaji.
4.5 Mbinu zinazotumika kushawishi rushwa ya ngono
Utafiti ulilenga kubaini njia na mbinu zinazotumiwa kufanya ushawishi wa rushwa ya ngono
katika Taasisi za elimu ya juu. Matokeo yanaonesha kuwa mbinu ya utoaji wa alama za chini
kwenye mitihani iliongoza kwa kutajwa na wahojiwa ikifuatiwa na vitisho vya kutofaulu kwa
wanafunzi kama inavyooneshwa kwenye Jedwali 8.
31
Jedwali 8: Mwitiko wa wahojiwa kuhusu mbinu zinazotumika kushawishi rushwa ya
ngono
Kundi Mbinu Mwitiko
Mdafao
(Frequency)
*Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam
(%)
Mdafao
(Frequency)
*Chuo
Kikuu cha
Dodoma
(%)
Wastani
Wanafunzi Kutoa alama za chini kwenye
mitihani.
240 40.5 61 36.6 38.6
Vitisho vya kutofaulu kwa
wanafunzi.
166 28.0 28 34.1 31.1
Ahadi kama kuolewa, cheo,
chumba chuoni, nafasi ya
uongozi, kuongezewa alama
za ufaulu.
157 26.5 16 18.3 22.4
Ushawishi wa makusudi 130 15.7 44 21.7 18.7
Wahadhiri kuwaita wanafunzi
kwenye mazingira yasiyo
rasmi kwa ajili ya kukagua
Utafiti
(Research/Proposal/Assignme
nt).
23 3.9 44 11.0 7.5
Wahadhiri kujiunga whatsapp
group moja na wanafunzi.
7 1.1 0 0.0 0.6
Watumishi Utoaji wa alama za chini
kwenye mitihani.
56 50.5 29 44.4 47.5
Ushawishi wa makusudi 26 16.1 39 43.8 29.9
Kutoa ahadi kama kumpatia
ajira, cheo, ufadhili wa
masomo n.k.
29 26.1 5 18.5 22.3
Vitisho vya mwalimu dhidi ya
mwanafunzi.
18 16.2 10 26.0 21.1
Ushawishi wa makundi rika 24 14.9 2 6.6 10.8
Kuchelewesha huduma. 8 7.2 3 11.1 9.6
*Multiple Response
Kutokana na kumbukumbu za malazi ya wanafunzi zilizopatikana katika Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam, inaonekana kuwa mwaka 2018/19 kulikuwa na maombi ya malazi ya wanafunzi 16,206
(kiambatisho I). Hata hivyo, wanafunzi 10,384 tu ndio waliopata malazi ya chuo. Matokeo haya
yanabainisha kuwepo kwa idadi kubwa ya wanafunzi waliokosa vyumba ingawa waliomba.
Katika mwaka huo chuo kilikuwa na uwezo wa kulaza wanafunzi 11,277 (kiambatisho II)
tofauti na idadi ya wanafunzi 33,658 waliodahiliwa. Aidha, nafasi za malazi kwa wanafunzi wa
kike zilikuwa 5,547 kati ya 13,497 waliodahiliwa katika mwaka huo. Uhaba huu unaweza
kutumika kama mwanya wa rushwa ya ngono.
32
Taarifa za kitaamuli zinaonesha kuwepo kwa vitisho vya baadhi ya wahadhiri vya kutoa alama
za chini kwa wanafunzi kama mbinu ya kuomba rushwa ya ngono. Wahadhiri wanajua kwamba
mwanafunzi anakuja chuoni na lengo kuu la kupata tuzo za kitaaluma. Wahadhiri hutumia
mwanya huo kwa kuwapa alama ndogo za masomo, kubadilisha alama za ufaulu, kuwafelisha au
kuzuia matokeo yao ili kuandaa mazingira ya kuwashawishi kingono. Baadhi ya wahojiwa
walieleza:
“……kuwepo kwa ucheleweshwaji wa fomu za mikopo kwa makusudi au jina la
mwanafunzi kurukwa ili malipo yake yasikamilike kwa wakati. Hii imekuwa moja
ya njia wanayoitumia kushawishi rushwa ya ngono…….”
“……mwanafunzi alitakwa kingono na mhadhiri akamkatalia, baada ya kumkatalia
mwanafunzi alianza kuona madhara yake kwa kuwekewa alama za chini……”
“…....mhadhiri aliomba rushwa ya ngono kwa mwanafunzi aliyekuwa amefaulu
mtihani wa majaribio (test) alikuwa amepata alama 84……lakini mhadhiri
hakumrudishia karatasi yake ya mtihani wa majaribio (test) na kumweleza kuwa
amefeli mtihani na hivyo yuko tayari kumwongezea alama hadi zifike 84 iwapo
atampa rushwa ya ngono……mwanafunzi alipoenda ofisini kwa mhadhiri alimkuta
na mhadhiri mwingine na alipoomba karatasi yake alikataliwa kwa madai kwamba
ana maongezi na mhadhiri mwenzake……..kwa bahati mhadhiri mwenzake bila
kujua kinachoendelea alimshauri mwahadhiri huyo amsikilize mwanafunzi…….
mwanafunzi alipatiwa karatasi yake na kubaini kuwa alikuwa amefaulu kwa kupata
alama 84……...”
“……kumekuwa na tabia kwa baadhi ya wahadhiri kuwatongoza wanafunzi
mapema kabisa wanapofika kuanza masomo chuoni kwa njia mbalimbali zikiwemo
kuwapigia simu na kuwatumia ujumbe mfupi wa maneno kupitia simu za
kiganjani……wanafunzi wanapokataa wahadhiri hao huwatishia wanafunzi hao
kuwa watahakikisha hawafaulu katika masomo wanayofundisha……...”
“............kuna wanafunzi walilalamika kwa uongozi wa chuo kutokana na kukataa
kutoa rushwa ya ngono kwa mtuhumiwa……uongozi wa chuo ulielekeza
33
usahihishaji wa somo hilo ufanyike upya na matokeo yalionesha kuwa wanafunzi
hao walikuwa wamefaulu…….uongozi ulichukua hatua za kiutawala dhidi ya
mtuhumiwa…...”
Matokeo haya yanaonesha kuwepo kwa vitendo vya makusudi vya baadhi ya wahadhiri
kulazimisha ngono kwa wanafunzi. Vitendo hivi vinakiuka kifungu cha 25 cha sheria ya Kuzuia
na Kupambana na Rushwa namba 11/2007. Sheria hii inaharamisha kitendo chochote cha mtu
mwenye mamlaka kumuwekea kigezo cha ngono mtu yeyote anayetaka huduma yake. Hivyo,
mtumishi yeyote wa Chuo Kikuu mwenye mamlaka/madaraka anayetumia nafasi yake
kumuwekea kigezo cha kupewa ngono mwanafunzi au mtumishi mwenzake anayetaka huduma
anakuwa ametenda kosa kwa mujibu wa sheria hii.
Matarajio ya mwanafunzi anapofika chuoni ni kukutana na wahadhiri na watumishi wenye
maadili. Matokeo ya utafiti yanabainisha kuwepo kwa mmomonyoko wa maadili unaofanywa na
baadhi ya wahadhiri pamoja na watumishi wengine kwa kukiuka misingi ya sera, kanuni na
miongozo inayoongoza vyuo hivyo.
Hata hivyo, Jedwali 8 linaonesha kuwa watumishi 65 (29.9%) na wanafunzi 174 (18.7%)
walieleza kuwepo kwa ushawishi wa makusudi ili kujipatia huduma kutoka kwa wenye
mamlaka. Aidha, watumishi 26 (10.8%) waliyataja makundi rika kuwa nayo yalishiriki
kuwashawishi kingono wenye mamlaka ili kupata huduma. Taarifa za kitaamuli zinaonesha
kuwepo kwa vitendo mbalimbali vya kushawishi ngono ambavyo wapewa huduma wamekuwa
wakivifanya kwa wenye mamlaka ili kujipatia huduma.
Wanafunzi walikuwa na haya ya kusema:
“…….kuna baadhi ya walimu masomo yao ni magumu hivyo tunaamua kumtuma
mwanafunzi ambaye ni mzuri na ambaye anaonekana kumvutia mwalimu
………..mwalimu akinasa tu, ajue somo lake tunabutua maana huyo mwanafunzi
anakuwa na maelekezo maalumu kuhakikisha anatupatia maswali ……si unajua
hakuna mkate mgumu kwenye chai…………tunachagua pini ya ukweli ambayo
mwalimu hawezi kuchomoka…….”
34
“…….kuna mwanafunzi mmoja alikiri kosa la kumfanyia „Quiz‟ rafiki
yake……mwanafunzi aliyefanyiwa „Quiz‟ alimshawishi mhadhiri kingono baada
ya kubaini kuwa kosa walilofanya ni la kufukuzwa chuo…..”
Baadhi ya watumishi walitoa shuhuda zifuatazo:
“……..kuna mwanafunzi alimwandikia mwalimu wa somo Email na kumuomba
mhadhiri amsaidie katika somo lake, atamlipa chochote lakini siyo pesa.
Mwalimu aliamua kuwashirikisha wanafunzi wengine na baadhi ya wahadhiri
katika idara husika. Pia aliwaasa wanafunzi wasome kwa bidii na kuzingatia
maadili……..”
“....... kuna mwanafunzi wa kike aliwahi kumtembelea mhadhiri ofisini kwake
akiwa amevaa kanga mbili, alipoingia ofisini kwake alijifunua kanga hizo
kujaribu kumshawishi mhadhiri kutaka ngono alipoona mhadhiri huyo hashtuki
hata baada ya kuona kajionesha mwili wake kwa mtu asiyetaka na hana haraka ya
kumtaka kingono, mwanafunzi husika aliamua kupiga kelele akidai mhadhiri
alitaka kumbaka. Hata hivyo baada ya waliokuwa jirani na ofisi ya mhadhiri huyo
kufika pale walishangazwa na maneno hayo ilihali binti mwenyewe hakuwa hata
na chupi ya kujisitiri…….”
Pamoja na matokeo haya, mbinu hizi za upande wa wasiokuwa na mamlaka
hazijaharamishwa na kifungu cha 25 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na rushwa
Na. 11/2007 kwani kifungu hicho kinamtaja mtu mwenye mamlaka kuwa ndiye
anaweza kutenda kosa hilo pale anapoweka sharti la ngono wakati wa kutoa huduma.
Matendo ya kushawishi ngono kutoka kwa watu wasio na mamlaka kwenye taasisi za
elimu ya juu, hata kama sio rushwa ya ngono kwa sasa, yakiachwa yaendelee yanaweza
kuchangia kushusha kiwango cha elimu na huduma nchini.
35
SURA YA TANO
5.0 HITIMISHO NA MAPENDEKEZO
5.1 Hitimisho
Kwa ujumla, utafiti umebaini kwamba tatizo la rushwa ya ngono kwenye vyuo vilivyoshiriki lipo
na kwamba tatizo hili ni kubwa na si la kupuuzwa. Shuhuda za waathiriwa wa rushwa ya ngono
pamoja na shuhuda za uwepo wa watuhumiwa ambao hawajachukuliwa hatua zilitolewa.
Vilevile, utafiti ulibaini kuwepo kwa sera, miongozo na sheria ndogondogo zinazoharamisha
rushwa ya ngono kwenye taasisi zote za umma ikiwa ni pamoja na vyuo vikuu. Kwa mfano,
Kanuni za Utumishi wa umma (2014, kanuni ya 36) zimepiga marufuku kwa mwajiri au
mtumishi wa umma kufanya aina yoyote ya udhalilishaji wa kijinsia kwa kumtaka mwajiriwa
kufanya ngono au kufanya aina yoyote itakayopelekea kufanyika ngono kama kigezo cha ahadi
ya kupendelewa kazini, au kulazimisha ngono ili mwajiriwa kuepuka vitisho ambavyo vitaathiri
ajira yake au kutumia kigezo cha ngono ili mwajiriwa aepuke vitisho dhidi ya maslahi ya sasa au
ya baadae katika ajira yake.
Vyuo vyote viwili vina kanuni za maadili za watumishi; Kanuni za Maadili kwa Watumishi wa
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (2018) na kanuni za maadili Chuo Kikuu Dodoma (2012).
Kanuni hizi zinabatilisha na kutoa katazo la kutumia rushwa ya ngono kutoa ufaulu, kufanya
vitendo vinavyoashiria ngono, au kufanya mawasiliano yanayoashiria uhitaji wa rushwa ya
ngono. Aidha, zinakataza kumsumbua au kumnyanyasa mtu yeyote yule anayetoa taarifa juu ya
unyanyasaji wa kingono (UDSM, 2018).
Pamoja na kuwepo kwa miongozo na kanuni zinazokataza rushwa ya ngono, utafiti ulibaini
mapungufu kwenye uwajibikaji wa udhibiti wa matumizi mabaya ya mamlaka hivyo kutoa
mianya inayosababisha kuwepo kwa vitendo vya rushwa ya ngono. Jambo hili linasababishwa na
kutokuwepo utashi wa dhati kwa wale waliopewa dhamana ya uongozi na watoa huduma
kwenye kushughulikia tatizo la rushwa ya ngono kikamilifu. Tabia za kuwalinda wakosaji,
zimesababisha kutokuimarisha ufuatiliaji wa sera na miongozo, kutokusimamia maadili ya
watendaji kwenye suala hili na kushindwa kuchukua hatua stahiki za kinidhamu kwa wale
36
wanaoendeleza vitendo vya rushwa ya ngono kwenye taasisi husika. Mifano ilitolewa ya
wahadhiri wanaodaiwa kujihusisha na rushwa ya ngono wanavyoendelea kupewa nyadhifa
mbambalimbali za uongozi na vyeo vya kitaaluma. Shuhuda zilitolewa kuhusu vitisho kwa
watoa taarifa wakiwa waathiriwa au wahadhiri. Shuhuda zilitolewa kuhusu wanafunzi
waliopendelewa na kupewa aidha ajira au kupewa udhamini wa masomo (scholarship) bila
kustahili pale ambapo wamekubali kutoa rushwa ya ngono. Shuhuda nyingine zilitolewa kwa
kuwepo watuhumiwa waliopewa adhabu kidogo sana kulingana na kosa, kwa mfano mhadhiri
kupewa likizo ya mwaka iliyomwezesha kuendelea na shughuli zake za ushauri na hatimaye
kurudi chuoni kuendelea na shughuli kama kawaida. Ukosefu wa utashi na uwajibikaji
unakatisha tamaa waathiriwa wa rushwa ya ngono au watendaji wenye maadili kutoa taarifa
kuhusu vitendo vya rushwa ya ngono.
Utafiti ulibaini mapungufu kwenye mifumo ya utahini inayotoa mwanya kwa wahadhri kutumia
vibaya mamlaka yao. Shuhuda zilitolewa kuhusu wanafunzi waliofelishwa kutokana na kukataa
rushwa ya ngono au wanafunzi wa kiume kufelishwa kwa vile marafiki wao wa kike wamekataa
kutoa rushwa ya ngono. Shuhuda zilitolewa kuhusu kubadilishwa kwa alama za mitihani hata
baada ya matokeo kutoka rasmi. Shuhuda zilitolewa kuhusu wanafunzi waliopendelewa kwenye
kupewa alama za juu na hatimaye kuajiriwa chuoni bila kustahili.
Mapungufu yamejitokeza kwenye mifumo ya vyombo vya kusimamia utekelezwaji wa sera na
miongozo hususan kwenye suala la rushwa ya ngono. Kamati za maadili kushindwa kudhibiti
rushwa ya ngono, vitengo vya jinsia kukosa nyezo na uwezo wa kuelimisha jamii kuhusu rushwa
ya ngono, ofisi za mshauri wa wanafunzi kukosa kitengo cha kuwasaidia waathiriwa wa rushwa
ya ngono.
Utafiti ulibaini mianya mingine inayosababisha kuendelezwa kwa rushwa ya ngono ikiwa ni
pamoja na ukosefu wa huduma za msingi kwa wanafunzi kama vile nyumba za kulala, mikopo,
pamoja na mifumo ya ajira za wakufunzi isiyozingatia weledi na maadili ya kazi kwenye taasisi
za elimu (teaching ethics).
37
Aidha, utafiti umebaini kuwa Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11/2007 inatoa
mwanya kwa wasio na mamlaka kuwashawishi wenye mamlaka kuwapa ngono na hivyo
kukwamisha juhudi za Serikali za kupandisha ubora wa elimu na huduma pamoja na kudhibiti
vitendo vya rushwa ya ngono.
5.2 Mapendekezo
Kutokana na matokeo tajwa, utafiti umebainisha mapendekezo machache yaliyotokana na
mijadala ya washiriki wa utafiti huu. Aidha, umuhimu wa kuboresha na kuimarisha mifumo ya
uwajibikaji kwenye kupambana na rushwa ya ngono ulijitokeza kama eneo la kipaumbele
kwenye kupambana na tatizo la rushwa ya ngono ndani ya vyuo vya elimu ya juu na taasisi
nyingine za umma na za sekta binafsi. Mapendekezo yamebainishwa kwa kila mdau:
Serikali
Iuwajibishe uongozi wa vyuo vikuu kwenye kujenga mazingira wezeshi na salama kwa
wanafunzi na wafanyakazi katika ngazi zote ili kuwezesha wanafunzi wa kike na kiume
kupata na kufaidi haki ya elimu katika ngazi hii pamoja na kuwezesha upatikanaji wa
elimu bora;
Iimarishe mifumo ya ajira ya wafanyakazi wote, hususan wakufunzi na viongozi kwa
kuwapa mafunzo ya ualimu na uongozi wale wote wenye kuajiriwa chuoni ili kuwapa
nyenzo za uwajibikaji wa kuzingatia maadili ya kufundisha na kuongoza katika taasisi za
elimu;
Iongeze fedha za uendeshaji vyuoni na hususan zinazohitajika kwenye kuimarisha
huduma za kuwezesha kuboresha utoaji wa elimu ikiwa ni pamoja na huduma za malazi
kwa wanafunzi ili kupunguza mianya inayotumiwa na wasimamizi na watoa huduma hizi
kwa kuweka sharti la ngono kwa wanafunzi;
Isimamie uwajibikaji wa uongozi wa chuo kuhusu masuala ya jinsia na hususan rushwa
ya ngono kwa kuwawajibisha viongozi waimarishe Kamati za Maadili ndani ya vyuo;
Kuendelea kuijengea uwezo TAKUKURU wa kuweza kuchunguza na kumfikisha
mtuhumiwa mahakamani bila kuhitaji kibali cha Mkurugenzi wa Mashtaka; na
38
Ifanye mapitio ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11/2007 ili
kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa ya ngono.
Uongozi wa Vyuo
Uboreshe mifumo ya udhibiti na uwajibikaji kwenye kuimarisha mifumo ya kusimamia
maadili, mifumo ya utahini, mifumo ya kutoa taarifa na kulinda watoa taarifa pamoja na
kuwajibisha watuhumiwa wa vitendo hivyo;
Uimarishe taasisi na kamati zinazoshughulikia masuala ya maadili ya watumishi wake
ikiwa ni pamoja na kamati za maadili, vitengo vya jinsia, ofisi ya mshauri wa wanafunzi
kwa kuwapatia nyenzo, vitendea kazi na mafunzo ya kuwawezesha kushughulikia
masuala ya rushwa ya ngono pamoja na unyanyasaji wa kijinsia kwenye vyuo; na
Uimarishe mahusiano na TAKUKURU kwenye kutoa elimu, kupeleleza na kuchukua
hatua stahiki kwa wale wote wenye kutuhumiwa kujihusuisha na vitendo vya rushwa ya
ngono.
Vitengo/Taasisi za Jinsia
Kujijengea uwezo wa uelewa wa Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na.
11/2007 kuhusu rushwa ya ngono ili waweze kusimamia utekelezaji wake vyuoni; na
Kuwajengea wanafunzi na jamii yote ya chuo uelewa wa suala la rushwa ya ngono ili
waweze kujitetea na kupambana nalo.
Asasi za kiraia
Kutumia taarifa hii kuimarisha vita dhidi ya rushwa ya ngono;
Kuendeleza na kuimarisha ubia kati yake na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa (TAKUKURU) kwenye vita dhidi ya rushwa ya ngono, hasa kwenye utafiti na
elimu ya umma; na
39
Kujijengea uelewa wa pamoja wa sheria ya Kuzuia na Kupambana na rushwa hususani
vipengele vinavyoelezea rushwa ya ngono ili kuweza kuendeleza mapambano dhidi ya
rushwa ya ngono.
Wanafunzi wa Vyuo
Waongeze jitihada katika masomo, wazingatie maadili, wasikubali kurubuniwa, wavunje
ukimya na kupaza sauti kunapotokea viashiria vya kuwanyima haki zao, na wachukue
hatua stahiki pale wanapopokonywa hizo haki;
Wadai kuimarishwa kwa mikakati iliyobainishwa katika miongozo na sheria ndogondogo
za kuzuia na kudhibiti rushwa ya ngono;
Wafikishe malalamiko yao TAKUKURU kwa kupitia kamati zao, taasisi za kiraia na hata
wao wenyewe; na
Waungane na kushiriki zaidi kwenye kampeni za kupambana na rushwa ya ngono.
40
MAREJEO
Briggs, S. (2009). Criminology for Dummies; Wiley Publishing Inc.
Crouch, M. and McKenzie, H. (2006). The logic of small samples in interview-based qualitative
research. Social Science Information, 45(4), 18. doi: 10.1177/0539018406069584.
Guest, G., Bunce, A. and Johnson, L. (2006). How many interviews are enough? An experiment
with data saturation and variability. Field Methods, 18(1), 24. doi:
10.1177/1525822X05279903.
http://mwaseba5.blogspot.com/2017/01/rushwa-ya-ngono-bado-ni-tishio-nchini.html
http://mwaseba5.blogspot.com/2017/01/rushwa-ya-ngono-bado-ni-tishio-nchini.html
IPP Media (2011). School pregnancies: A call for reflection on teachers morality. Retrieved from
http://www.ippmedia.com/fronted/index.php on 05 November 2019.
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (2017). Mkakati wa Taifa Dhidi ya Rushwa Na Mpango wa
Utekelezaji: Awamu ya tatu 2017-2022
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania (1977). Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.
Mchapaji Mkuu wa Serikali, Dar es Salaam.
Klitgaard, R. (1988). Controlling Corruption. Berkeley, CA. University of California Press
Levin, J. and Milgion, P. (2004), Introduction to choice theory. Stanford University.
Mandago, B. (2018). Tanzania: Say No to Sextortion https://genderlinks.org.za/news/tanzania-
say-no-to-sextortion/; ilisomwa tarehe 05 Novemba 2019.
Mwai, P. (2018). Vicensia Shule: mhadhiri aliyezua mjadala wa rushwa ya ngono chuoni UDSM
Tanzania ni nani? Imesomwa kutoka http://www.bbc.com/swahili/habari-46368623
ilisomwa tarehe 05 Novemba 2019.
Sabinus, J. (2019). Rushwa ya ngono vyuoni inaangamiza wengi; imesomwa kutoka
http://www.habarileo.co.tz/2019-09-055d70f90061c4f.aspx ilisomwa tarehe 05
Novemba 2019.
Sheikh, L. (2007). Sexual harassment: The salient crime. Dar es Salaam.
TAMWA (2012). Ripoti ya Utafiti wa Tamwa Kuhusu Unyanyasaji wa kijinsia
http://ateen101.blogspot.com/2012/10/ripoti-ya-utafiti-wa-tamwa-kuhusu.html
TAMWA (2014). The campaign against sextortion 3rd
November. Dar es Salaam.
41
Tanzania Women Judge Association (TWJA) (2011). Stopping the abuse of power for purposes
of sexual exploitation; a toolkit available at http://iawj/Tanzania_toolkit_final_pdf
ilisomwa tarehe 05 Novemba 2019.
TCU (2018). Higher Education Students admission, enrollment and education statistics
iliyopatikana kutoka http://www.tcu.go.tz/sites/default/files/admission
%20and%20Graduation%statistics.pdf iliyosomwa tarehe 20 Disemba 2019.
Tem, H. (2007). Nayakumbuka yote. Mkuki na Nyota Publishers.
Yin, R. K. (2014). Case Study Research Design and Methods (5th ed.) .Thousand Oaks, CA:
Sage. 282 pages. (ISBN 978-1-4522-4256-9).
Yusuph, K (2016). Sextortion in education sector and response to criminal legal system in
Tanzania-A Review. Asia Pacific Journal of Education, Arts and Sciences, 3(1):56 - 63
42
VIAMBATISHO
Kiambatisho I: Maombi ya vyumba vya malazi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
2016/17 – 2019/20
Malazi 2016/2017 2017/2018 2018/2019 2019/2020
Idadi ya maombi 10,488 19,050 16,206 27,086
Idadi ya waliopata 7,293 10,245 10,259 10,526
Idadi ya waliokosa 3195 8805 5947 16560
Idadi ya maombi
(mahitaji maalum)
94
198 125 138
Idadi ya walioapata
(mahitaji maalum)
94
198 125 138
Kiambatisho II: Idadi ya mabweni na mgawanyo wa wanafunzi katika Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam 2018/19
Jina la Bweni Uwezo Nafasi za Wanaume Nafasi za Wanawake
Hall one 512 190 322
Hall two 400 400 0
Judge Julie Manning 494 0 494
Hall four 251 73 178
Hall five 400 400 0
Hall six 310 317 7
Hall seven 304 30 274
Mabibo Hostel 4,298 2,580 1,718
Kunduchi Hostel 50 25 25
Water Resources Houses 16 8 8
CoICT Hostel 240 76 160
Magufuli Hostel 3,840 1,536 2,280
Ubungo Hostel 108 54 54
Mikocheni Hostel 54 27 27
JUMLA 11,277 5716 5547