Insignia PAINTERS training swa article 3 19 Aug 15-final.doc

5
Mkakati wa Insignia kuinua maisha ya mafundi rangi nchini Kampuni inayoongoza kwa uzalishaji wa rangi Maalum, Insignia Limited imeendelea kuonesha nia yake ya kutoa huduma zinazomjali mteja, ubunifu na pia mapinduzi katika soko la rangi nchini Tanzania kwa ujumla. Hivi karibuni kampuni hii imewapatia mafunzo zaidi ya mafundi rangi 50 mwishoni mwa wiki hii mjin Dar es salaam,yaliyoandaliwa maalumu kwa ajili ya wakazi wa mbagala yakiwa na lengo la kuinua kiwango cha mafundi rangi katika sekta hii na kuboresha maisha yao kwa ujumla hapa Tanzania. Kwa mujibu wa Meneja mauzo na Masoko kutoka kampuni ya Insignia Limited, Bw Sanjay Babuta, lengo kuu la kampuni hiyo kuandaa mafunzo kwa mafundi rangi ni kuelimisha na kujenga uelewa zaidi kuhusu hatua za upakaji rangi zinazotakiwa ili kuiwezesha rangi kudumu zaidi. "Tunatoa mafunzo ya bure ambayo kwa kawaida hufanyika kati ya saa 4:00 asubuhi- 8:00mchana. Mafunzo yetu kwa kawaida yako wazi kwa mafundi rangi wote wa Tanzania pamoja na wauzaji katika maduka mbalimbali ya rangi. Tumeandaa kalenda ya mwaka mzima kwa ajili ya miji katika mikoa mbalimbali (kwa makundi), hivyo ni zoezi endelevu linalofanyika katika vipindi tofautitofauti. Tarehe huamuliwa mapema ili kufanikisha zoezi kwa ubora zaidi na ambapo mialiko hutolewa mapema kwa mafundi rangi”. Anaeleza Bw. Sanjay. Kwa mujibu wa mtoa mafunzo mkuu kutoka kampuni ya insiginia Bw. Mpoki Mwangosi anasema wamelenga kuwapa ujuzi zaid mafundi, kutokana asilimia 99 ya matatizo ya rangi husababishwa na mafundi wenyewe. Mjini Dar es Salaam kampuni hiyo imepanga kuwatoa mafunzo hayo maeneo ya Temeke na Kigamboni hivi karibuni. Lakini pia wanatarajia kufanya mafunzo mikoa mingine, kuanzia tarehe za 20 na kuendelea mkoa wa Mwanza.

Transcript of Insignia PAINTERS training swa article 3 19 Aug 15-final.doc

Page 1: Insignia PAINTERS training  swa article 3 19 Aug 15-final.doc

Mkakati wa Insignia kuinua maisha ya mafundi rangi nchini

Kampuni inayoongoza kwa uzalishaji wa rangi Maalum, Insignia Limited imeendelea kuonesha nia yake ya kutoa huduma zinazomjali mteja, ubunifu na pia mapinduzi katika soko la rangi nchini Tanzania kwa ujumla. Hivi karibuni kampuni hii imewapatia mafunzo zaidi ya mafundi rangi 50 mwishoni mwa wiki hii mjin Dar es salaam,yaliyoandaliwa maalumu kwa ajili ya wakazi wa mbagala yakiwa na lengo la kuinua kiwango cha mafundi rangi katika sekta hii na kuboresha maisha yao kwa ujumla hapa Tanzania.

Kwa mujibu wa Meneja mauzo na Masoko kutoka kampuni ya Insignia Limited, Bw Sanjay Babuta, lengo kuu la kampuni hiyo kuandaa mafunzo kwa mafundi rangi ni kuelimisha na kujenga uelewa zaidi kuhusu hatua za upakaji rangi zinazotakiwa ili kuiwezesha rangi kudumu zaidi.

"Tunatoa mafunzo ya bure ambayo kwa kawaida hufanyika kati ya saa 4:00 asubuhi- 8:00mchana. Mafunzo yetu kwa kawaida yako wazi kwa mafundi rangi wote wa Tanzania pamoja na wauzaji katika maduka mbalimbali ya rangi. Tumeandaa kalenda ya mwaka mzima kwa ajili ya miji katika mikoa mbalimbali (kwa makundi), hivyo ni zoezi endelevu linalofanyika katika vipindi tofautitofauti. Tarehe huamuliwa mapema ili kufanikisha zoezi kwa ubora zaidi na ambapo mialiko hutolewa mapema kwa mafundi rangi”. Anaeleza Bw. Sanjay.

Kwa mujibu wa mtoa mafunzo mkuu kutoka kampuni ya insiginia Bw. Mpoki Mwangosi anasema wamelenga kuwapa ujuzi zaid mafundi, kutokana asilimia 99 ya matatizo ya rangi husababishwa na mafundi wenyewe.

Mjini Dar es Salaam kampuni hiyo imepanga kuwatoa mafunzo hayo maeneo ya Temeke na Kigamboni hivi karibuni. Lakini pia wanatarajia kufanya mafunzo mikoa mingine, kuanzia tarehe za 20 na kuendelea mkoa wa Mwanza.

Mkurugenzi Mtendaji wa Insignia Limited, Bw. Kishan Dhebar, anasema kuwa wamebaini kiwango cha ujuzi unaohitajika katika upakaji rangi na ukosefu wake kwa sasa ndani ya nchi. Kama kampuni inayoongoza waliona inafaa kujenga jukwaa la mafundi rangi kupokea mafunzo ya kutosha ambayo yatawafaidisha sio tu wao bali sekta ya rangi kwa ujumla.

“Wakati sekta ya rangi na inakuwa, vivyo hivyo mahitaji ya wafanyabiashara wenye ujuzi yanaongezeka. Ni muhimu kwamba ubora wa bidhaa zetu

Page 2: Insignia PAINTERS training  swa article 3 19 Aug 15-final.doc

hauathiriki na hili ndilo linalotuhamasisha kutoa mafunzo kwa mafundi rangi. Kwa kufanya kwao kazi kwa ubora tunaipatia sekta hii sifa chanya inazohitaji”. Anasema Bw Kishan

Watanzania wanatarajiwa kufaidika na mafunzo ya mafundi rangi kutoka Insignia Limited kwa kuwa wanatoa elimu sahihi ya namna ya utumiaji rangi na ubora ambao utawawezesha mafundi rangi hao kufanya kazi bora kwa wateja wao. Ukosefu wa ujuzi maarifa muhimu kwa mafundi rangi mara nyingi umekuwa ukisababisha misuguano kati yao na wamiliki wa nyumba, makandarasi na sekta ya rangi kwa ujumla. Mbinu zisizo sahihi, njia ya mkato zisizo muafaka ni miongoni mwa sababu zinazochangia kiwango cha chini cha kazi.

"Tunatarajia mafundi rangi kutumia taratibu sahihi ambazo zitawasaidia kujenga uhusiano mzuri na wateja wao na kupunguza migogoro. Kwa zoezi hili tunajenga mafundi rangi wengi ambao watakuwa kama mabalozi wa bidhaa za Insignia”. Anasema Bw. Sanjay.

Mafunzo ya Insignia Limited kwa mafundi rangi yanalenga masuala ya msingi katika rangi na sekta ya upakaji rangi, kama vile rangi ni nini, manufaa, mchanganyiko, kuoanisha rangi, aina mbalimbali za nyuso sifa zao na namna ya kuzipaka na sifa za makundi mbalimbali na matumizi ya rangi ikiwa ni pamoja na kuongeza thamani inayofaa kwa wateja wao. Mafunzo haya pia yanakuwa kama jukwaa la kupatia maoni ya soko, kutambulishwa kwa bidhaa mpya, mbinu na hatua za usalama.

Kidaba Mzee, fundi rangi ambaye alikuwa na nafasi ya kuhudhuria mafunzo yaliyoandaliwa na kampuni amepongeza hatua hiyo kubwa iliyoletwa na Insignia Limited.

"Nimekuwa nikifanya kazi kama mpaka rangi kwa miaka 8 lakini sikuwa na ujuzi wa kutosha katika fani hii. Sikujua njia sahihi zinaohitajika katika kudumisha kiwango cha juu katika sekta ya upakaji wa rangi. Pamoja na mafunzo yanayotolewa na Insignia Limited sasa naweza kusimama na kujivunia taaluma yangu. Nashukuru Uongozi wa kampuni ya Insignia Limited kwa mawazo yao bunifu ya kutuelimisha". Anasema.

Mpango huu ulianzishwa na kampuni mwaka 2003 na umesaidia kama jukwaa kuu kwa kuongeza maarifa ya namna ya kupiga hatua zaidi. Toka mwaka 2003 hadi 2014 kampuni hiyo ilifanya mafunzo zaidi ya 2,000 na kuwafundisha zaidi ya mafundi rangi 100,000.

Insignia Limited inatoa mafunzo haya si tu ndani ya nchi; pia hufanyika katika nchi nyingine kutokana na kuwepo kwa bidhaa zao ndani ya masoko hayo. Mwaka 2014 pekee jumla ya Mafunzo 175 yalifanywa nchini Tanzania, Malawi na Zambia ambapo mpaka Februari mwaka 2015 jumla ya mafunzo 28 ya tayari yamefanyika katika mikoa na nchi jirani. Katika shughuli zote hizi jumla ya mafundi rangi 3,778 walipewa mafunzo juu ya mbinu

Page 3: Insignia PAINTERS training  swa article 3 19 Aug 15-final.doc

mbalimbali mwaka 2014 ambapo mpaka Februari 2015 kampuni imetoa mafunzo kwa mafundi rangi 992. Mafunzo pia yamekuwa na thamani kifedha kwa mafundi rangi ambapo mbinu walizofundishwa zinawaruhusu kuwa na ufahamu zaidi juu ya kudhibiti gharama ikiwa ni pamoja na kupunguza makosa katika kazi ili kupata matokeo mazuri mwishoni. Utoaji wa vyeti vya ushiriki mwishoni mwa mafunzo kutoka kwa kampuni kumewanufaisha watu wengi zaidi katika kupata ajira.

Insignia Limited inatarajia kuhakikisha kwamba rangi zenye ubora wa juu wanazotengeneza zinatumika kwa ustadi na mtu mwenye ufahamu wa kutosha ili kufanikisha matokeo bora iwezekanavyo kulingana na makusudio wakati wa uzalishaji na kuacha muonekano unaovutia. Kampuni hiyo ina nia ya kuendeleza mafunzo haya kwa kuwa kila siku watu wapya wanaingia katika biashara ya rangi na hivyo kuhitaji ushauri unaofaa wa jinsi ya kufanya vizuri zaidi katika taaluma yao. Hatua kama hii wakati wa mabadiliko chanya lazima ipongezwe na kuigwa ili kuhakikisha sekta inaendelea kupiga hatua katika mwelekeo sahihi.

Kuhusu Insignia

Mwaka 1989, Tanzania ilishuhudia kuzaliwa Coral Paints, kampuni ndogo ambayo ingeweza kubadilisha uso wa sekta ya rangi nchini. Ikiendeshwa na dhamira ya kipekee na ubora, kampuni ambayo kwa sasa inajulikana kama Insignia Limited, ilikua kwa kiwango kikubwa na kuvuka mipaka.

Hivi leo, Insignia imefikia moja ya malengo yake; ni moja ya kampuni kubwa nchini Tanzania inayoongoza katika utengenezaji wa rangi mbalimbali. Uamuzi wake wa kuleta bidhaa zenye viwango vya hali ya juu nchini Tanzania umewezeshwa na ushirikiano na makampuni makubwa ya kimataifa kama Marmoran (Pty) Ltd, iliyopo Africa ya kusini, Ronseal iliyopo nchini Uingereza na Pat’s Deco ya Ufaransa.

Bidhaa mbili za Coral na Galaxy, zinafafanua ubora wa kampuni ya Insignia. Chini ya majina haya, kampuni inatengeneza rangi na bidhaa nyingine nyingi. Teknolojia ya hali ya juu ipatikanayo katika kampuni hiyo inaipatia kampuni hiyo msaada mkubwa sana katika ushindani. Rangi ya Galaxy inatngenezwa kiufundi, inatumia ujuzi, pembejeo na washauri wa kimataifa, inawapatia wateja wake teknolojia ya kisasa kwenye rangi. Rangi ya Coral paint ni bidhaa inayoongoza katika soko nchini Tanzania. Imepata kibali, na kuimarisha sifa yake kama bidhaa yenye ubora inayoedana na thamani- ya -fedha.

Kiufanisi, miundombinu ya Insignia inajulikana kwa ubora wake. Viwanda vyake vina vifaa vyenye ubora na vya kisasa vinavyotengeneza bidhaa zenye viwango vya kimataifa.

Page 4: Insignia PAINTERS training  swa article 3 19 Aug 15-final.doc

Kampuni hii ina viwanda jijini Dar es Salaam, Moshi, Mwanza na Zambia pia ina Vituo vya usambazaji mkoani Moshi, Arusha, Mbeya na Mwanza mikoa mikubwa nchini. Pia kuna uwepo wa mtandao mpana wa wafanyabiashara na malori ya kisasa kuwahakikishia usambazaji wa bidhaa nchini kote. Kampuni hiyo pia ina vituo nchini Rwanda, Burundi na Malawi.