Darasa la 1 Kiswahili - Teachersupdates.co.ke...Darasa la 1 Kiswahili Darasa la 1 Kitabu hiki...
Transcript of Darasa la 1 Kiswahili - Teachersupdates.co.ke...Darasa la 1 Kiswahili Darasa la 1 Kitabu hiki...
![Page 1: Darasa la 1 Kiswahili - Teachersupdates.co.ke...Darasa la 1 Kiswahili Darasa la 1 Kitabu hiki kimechapishwa kwa ufadhili kutoka kwa Shirika la maendeleo ya kimataifa la Marekani (USAID/Kenya)](https://reader033.fdocument.pub/reader033/viewer/2022061611/6129c8ba60b3c5209737872a/html5/thumbnails/1.jpg)
Vitabu vya hadithi vya Tusome vimeandikwa kwa ustadi wa hali ya juu ili kusaidia kuinua kiwango cha kusoma kwa wanafunzi wa darasa la 1 na la 2. Hadithi hizi zinawapa wanafunzi nafasi ya kufurahia hadithi na kuinua uelewa wa hadithi nje ya masomo ya kawaida darasani. Vitabu hivi vinaweza kutumiwa na yeyote anayejifunza Kiswahili. Tunashukuru kwa usaidizi wa SIL LEAD kwa mchango wao katika kuandika hadithi hizi. Ili kusaidia katika juhudi hii, hadithi hizi zimeandikwa kwa kuzingatia yafuatayo:-• Lugha rahisi kwa wanafunzi na sentensi zenye urefu unaofaa,• Picha za kuvutia ambazo hazielezi hadithi kikamilifu lakini zinamwezesha
msomaji kusoma zaidi ili aelewe hadithi,• Hadithi za kufurahisha zenye maudhui na dhamira ambazo msomaji
anayeanza kusoma ataweza kulinganisha na maisha yake ya kila siku,• Vichwa vya hadithi ambavyo vinamwezesha msomaji kutabiri.
Hadithi katika msururu huu ni:Darasa la 1: ‣ Fisi Mjinga na Chura na Kiboko ‣ Mchezaji Banda na Kisa cha Simba na Mbuni ‣ Faida za Ng’ombe na Siku za Wiki ‣ Kwa nini Mzee Kobe ana magamba na Jitu la MtoniDarasa la 2: ‣ Shujaa Musa na Mnyama Nimpendaye ‣ Mama Mzee na Nguruwe na Juma na Sungura ‣ Fisi na Mbuzi na Kuku na Mwewe Wakosana ‣ Sababu ya Paka Kupenda Kukaa Jikoni na Kwa nini Twiga
ana Shingo Ndefu ‣ Safari ya Mombasa na Masaibu ya Musa
Tusome Early Literacy Programme
Darasa la 1
KiswahiliDarasa la 1
Kitabu hiki kimechapishwa kwa ufadhili kutoka
kwa Shirika la maendeleo ya kimataifa la
Marekani (USAID/Kenya) na Idara ya maendeleo
ya kimataifa ya Uingereza (DFID/Kenya) kupitia
mradi wa Tusome Early Grade Reading Activity.
Kitabu cha hadithi 1
Kitabu cha hadithi 1
![Page 2: Darasa la 1 Kiswahili - Teachersupdates.co.ke...Darasa la 1 Kiswahili Darasa la 1 Kitabu hiki kimechapishwa kwa ufadhili kutoka kwa Shirika la maendeleo ya kimataifa la Marekani (USAID/Kenya)](https://reader033.fdocument.pub/reader033/viewer/2022061611/6129c8ba60b3c5209737872a/html5/thumbnails/2.jpg)
1
Fisi MjingaMwandishi: Stephen Kwoma
Mchoraji: Simon Ndonye
Hapo kale Fisi na Sungura
walikuwa marafiki.
Marafiki hao waliishi pamoja.
![Page 3: Darasa la 1 Kiswahili - Teachersupdates.co.ke...Darasa la 1 Kiswahili Darasa la 1 Kitabu hiki kimechapishwa kwa ufadhili kutoka kwa Shirika la maendeleo ya kimataifa la Marekani (USAID/Kenya)](https://reader033.fdocument.pub/reader033/viewer/2022061611/6129c8ba60b3c5209737872a/html5/thumbnails/3.jpg)
2
Siku moja Sungura alienda kutafuta
chakula.
Fisi naye alibaki akifagia nyumba.
![Page 4: Darasa la 1 Kiswahili - Teachersupdates.co.ke...Darasa la 1 Kiswahili Darasa la 1 Kitabu hiki kimechapishwa kwa ufadhili kutoka kwa Shirika la maendeleo ya kimataifa la Marekani (USAID/Kenya)](https://reader033.fdocument.pub/reader033/viewer/2022061611/6129c8ba60b3c5209737872a/html5/thumbnails/4.jpg)
3
Jioni Sungura alirudi nyumbani.
Sungura alileta asali nyingi.
![Page 5: Darasa la 1 Kiswahili - Teachersupdates.co.ke...Darasa la 1 Kiswahili Darasa la 1 Kitabu hiki kimechapishwa kwa ufadhili kutoka kwa Shirika la maendeleo ya kimataifa la Marekani (USAID/Kenya)](https://reader033.fdocument.pub/reader033/viewer/2022061611/6129c8ba60b3c5209737872a/html5/thumbnails/5.jpg)
4
Fisi alifurahia sana. Alitaka kujua
Sungura alitoa wapi ile asali.
Sungura akamwambia kuwa
alitingisha mzinga wa nyuki.
![Page 6: Darasa la 1 Kiswahili - Teachersupdates.co.ke...Darasa la 1 Kiswahili Darasa la 1 Kitabu hiki kimechapishwa kwa ufadhili kutoka kwa Shirika la maendeleo ya kimataifa la Marekani (USAID/Kenya)](https://reader033.fdocument.pub/reader033/viewer/2022061611/6129c8ba60b3c5209737872a/html5/thumbnails/6.jpg)
5
Siku iliyofuata Fisi alienda kutafuta
chakula.
Aliona mzinga na akaanza
kuutingisha.
![Page 7: Darasa la 1 Kiswahili - Teachersupdates.co.ke...Darasa la 1 Kiswahili Darasa la 1 Kitabu hiki kimechapishwa kwa ufadhili kutoka kwa Shirika la maendeleo ya kimataifa la Marekani (USAID/Kenya)](https://reader033.fdocument.pub/reader033/viewer/2022061611/6129c8ba60b3c5209737872a/html5/thumbnails/7.jpg)
6
Nyuki walitoka ndani ya mzinga
na kumuuma Fisi.
Fisi alikimbia hadi nyumbani huku
akilia.
![Page 8: Darasa la 1 Kiswahili - Teachersupdates.co.ke...Darasa la 1 Kiswahili Darasa la 1 Kitabu hiki kimechapishwa kwa ufadhili kutoka kwa Shirika la maendeleo ya kimataifa la Marekani (USAID/Kenya)](https://reader033.fdocument.pub/reader033/viewer/2022061611/6129c8ba60b3c5209737872a/html5/thumbnails/8.jpg)
7
Sungura alimwona Fisi akija mbio
huku Nyuki wakimfukuza.
Sungura alimcheka Fisi.
![Page 9: Darasa la 1 Kiswahili - Teachersupdates.co.ke...Darasa la 1 Kiswahili Darasa la 1 Kitabu hiki kimechapishwa kwa ufadhili kutoka kwa Shirika la maendeleo ya kimataifa la Marekani (USAID/Kenya)](https://reader033.fdocument.pub/reader033/viewer/2022061611/6129c8ba60b3c5209737872a/html5/thumbnails/9.jpg)
8
Fisi alikasirika na kumfukuza
Sungura kutoka nyumbani mwao.
Wanyama hawa hawakuishi
pamoja tena.
Maswali1. Sungura alileta nini?
2. Kwa nini Nyuki walimfukuza Fisi?
3. Kwa nini Sungura alimcheka Fisi?
![Page 10: Darasa la 1 Kiswahili - Teachersupdates.co.ke...Darasa la 1 Kiswahili Darasa la 1 Kitabu hiki kimechapishwa kwa ufadhili kutoka kwa Shirika la maendeleo ya kimataifa la Marekani (USAID/Kenya)](https://reader033.fdocument.pub/reader033/viewer/2022061611/6129c8ba60b3c5209737872a/html5/thumbnails/10.jpg)
9
Chura na KibokoMwandishi: Flavia Nanzala
Mchoraji: Simon Ndonye
Hapo zamani, Chura na Kiboko
walikuwa marafiki.
Wanyama hao walikuwa majirani.
Chura alikuwa na sauti nyororo.
Kiboko naye alikuwa na sauti nzito.
![Page 11: Darasa la 1 Kiswahili - Teachersupdates.co.ke...Darasa la 1 Kiswahili Darasa la 1 Kitabu hiki kimechapishwa kwa ufadhili kutoka kwa Shirika la maendeleo ya kimataifa la Marekani (USAID/Kenya)](https://reader033.fdocument.pub/reader033/viewer/2022061611/6129c8ba60b3c5209737872a/html5/thumbnails/11.jpg)
10
Siku moja, Kiboko alialikwa katika
mashindano ya kuimba.
Aliogopa kushindwa kwa sababu
ya sauti yake nzito.
Kiboko alimuomba Chura sauti
yake nyororo.
Chura alimpa Kiboko sauti yake
nyororo.
Kiboko alienda kwa mashindano
akiwa na furaha.
![Page 12: Darasa la 1 Kiswahili - Teachersupdates.co.ke...Darasa la 1 Kiswahili Darasa la 1 Kitabu hiki kimechapishwa kwa ufadhili kutoka kwa Shirika la maendeleo ya kimataifa la Marekani (USAID/Kenya)](https://reader033.fdocument.pub/reader033/viewer/2022061611/6129c8ba60b3c5209737872a/html5/thumbnails/12.jpg)
11
Kiboko aliimba vizuri sana akawa
mshindi.
Baada ya mashindano, Kiboko
hakurudisha sauti ya Chura.
Kiboko alitoroka na kwenda kuishi
majini.
![Page 13: Darasa la 1 Kiswahili - Teachersupdates.co.ke...Darasa la 1 Kiswahili Darasa la 1 Kitabu hiki kimechapishwa kwa ufadhili kutoka kwa Shirika la maendeleo ya kimataifa la Marekani (USAID/Kenya)](https://reader033.fdocument.pub/reader033/viewer/2022061611/6129c8ba60b3c5209737872a/html5/thumbnails/13.jpg)
12
Chura alimngoja Kiboko lakini
Kiboko hakurudi.
Siku iliyofuata, Chura alienda
mtoni kuchota maji.
Chura alimwona Kiboko mtoni.
Chura alimwambia Kiboko
amrudishie sauti yake.
Kiboko akajificha ndani ya maji.
Tangu siku hiyo, Chura hulia majini
akidai sauti yake.
Maswali1. Kiboko alimuomba Chura nini?
2. Kiboko alikuwa anaenda mashindano
ya nini?
3. Kwa nini Chura hulia majini?
![Page 14: Darasa la 1 Kiswahili - Teachersupdates.co.ke...Darasa la 1 Kiswahili Darasa la 1 Kitabu hiki kimechapishwa kwa ufadhili kutoka kwa Shirika la maendeleo ya kimataifa la Marekani (USAID/Kenya)](https://reader033.fdocument.pub/reader033/viewer/2022061611/6129c8ba60b3c5209737872a/html5/thumbnails/14.jpg)