BULLETIN 93 Print.pdf

7
Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali kwa ajili ya News Bullettin hii ya Wizara ya Nishati na Madini Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected] HABARI ZA NISHATI &MADINI Toleo No. 93 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Novemba 13 - 19, 2015 Bulletin News http://www.mem.go.tz Soma habari Uk. 3 Tuwahudumie watanzania kwa moyo wa dhati Baadhi ya wajumbe kutoka EWURA wakimsikiliza katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo (wa kwanza kulia). Ataka kauli za “njoo kesho” zikome Msicheleweshe wawekezaji- Chambo Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo (kulia) akipokea nyaraka mbalimbali kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi- EWURA, Profesa Jamidu Katima. Anayeshuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Felix Ngalamgosi.

Transcript of BULLETIN 93 Print.pdf

Page 1: BULLETIN 93 Print.pdf

Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali kwa ajili ya News Bullettin hii ya Wizara ya Nishati na Madini

Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]

HABARI ZA NISHATI &MADINI

Toleo No. 93 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Novemba 13 - 19, 2015

BulletinNews

Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizara ya Nishati na Madini

Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]

http://www.mem.go.tz

HABARI ZA NISHATI &MADINI

Toleo No. 51 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Tarehe - 23-29 Januari , 2015

JWTZ wapongezwa kunusuru mtambo wa Msimbati-Uk4

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, anayeshughulikia Madini Stephen Masele

Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Charles Kitwanga

Mkurugenzi Mtend-aji wa TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba

Mkurugenzi Mkuu wa REA, Dk. Lutengano Mwakahesya

Wabunge Soma habari Uk. 2

Waimwagia sifa MEM, TANESCO, REA

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AZINDUA RASMI BODI YA TANESCO -Uk2

Soma habari

Uk. 3Tuwahudumie watanzania kwa moyo wa dhati

Baadhi ya wajumbe kutoka EWURA wakimsikiliza katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo (wa kwanza kulia).

Ataka kauli za “njoo kesho” zikome

Msicheleweshe wawekezaji- Chambo

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo (kulia) akipokea nyaraka mbalimbali kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi- EWURA, Profesa Jamidu Katima. Anayeshuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Felix Ngalamgosi.

Page 2: BULLETIN 93 Print.pdf

2 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHABARI ZA NISHATI/MADINI

Mohamed Saif na Nuru Mwasampeta, Dar es Salaam

Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati na Madini zimeagizwa kutochelewesha kushughulikia maombi ya wawekezaji pale wadau

mbalimbali wa ndani na nje ya nchi wanapoonesha dhamira ya kuwekeza.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo ametoa agizo hilo hivi karibuni wakati wa kikao chake na Watendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi hiyo.

Mhandisi Chambo aliwaagiza watendaji hao kuacha kufanya kazi kwa mazoea, na badala yake wazingatie Sheria na maadili ya kazi zao, kutokana na ukweli kwamba sekta ya Nishati ni sekta nyeti inayohitaji watendaji waadilifu na wabunifu.

“Akitokea mwekezaji ambaye ameonesha nia ni vema ajibiwe haraka bila kuchelewa iwe amekubaliwa au kukataliwa ombi lake; hakuna sababu ya kumzungusha mwekezaji; tuzidishe kasi ya uwajibikaji,” alisema Mhandisi Chambo.

Alisema lengo la Serikali ni kuongeza uwekezaji hususan kwenye sekta za Nishati na Madini na hivyo hakuna sababu ya kuchelewesha uwekezaji kwani fursa za uwekezaji zilizopo nchini ni nyingi.

Aliwaasa EWURA na Taasisi

nyingine kuacha tabia ya woga, na kusema kwamba endapo itatokea mwekezaji akatuma maombi ya kuwekeza nchini, wanapaswa kupitia maombi husika, kujiridhisha na kutoa maamuzi kwa haraka na kwa kujiamini.

“Tufikie mahali tufanye maamuzi. Msiwe na woga kwenye kutekeleza jambo lenye maslahi mapana ya Kitaifa;

majibu ya njoo kesho hatutayavumilia,” alisema.

Vilevile Mhandisi Chambo alisema ni vyema taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati na Madini zikashirikiana na Wizara katika kufanya upembuzi yakinifu wa miradi katika maeneo

ambayo yanahitaji uwekezaji.Aidha, aliwaagiza watendaji kukaa

pamoja kujadili maeneo ya kipaumbele ili upembuzi yakinifu ufanyike kwa lengo la kurahisisha majadiliano na wawekezaji.

Alisema ni vyema ikaundwa timu ya wataalamu kutoka katika Taasisi na Wizara ambao watahusika moja kwa moja na suala la kubaini maeneo pamoja na kufanya upembuzi yakinifu kwa miradi yenye tija na manufaa na hivyo kufikia mwafaka mapema na kuanza utekelezaji wa mradi husika pale mwekezaji anapojitokeza.

“Ikitokea mwekezaji akaonesha dhamira ya kuwekeza kwenye maeneo husika ni vema taarifa za awali zikawepo. Hii itavutia wawekezaji wengi zaidi lakini pia itaharakisha majadiliano,” alisema.

Aidha, Mhandisi Chambo aliwapongeza EWURA kwa kufanya vizuri kwenye masuala ya mafuta na kuwaasa kujitahidi kufanya vizuri katika majukumu mengine yaliyo chini yao.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Felix Ngalamgosi aliahidi kufanya kazi kwa uadilifu na kuzingatia maelekezo yaliyotolewa na Katibu Mkuu pamoja na kumpatia ushirikiano wa kutosha.

Kikao hicho ni mwendelezo wa vikao vya Katibu Mkuu huyo na Menejimenti pamoja na Bodi za Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati na Madini ili kupata ufumbuzi wa changamoto zinazozikabili.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo (kushoto) akijadiliana jambo na Kamishna wa Nishati, Mhandisi Hosea Mbise (katikati). Wa kwanza kulia ni Kamishna Msaidizi anayeshughulikia Maendeleo ya Nishati, James Andilile.

Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Felix Ngalamgosi (kushoto) akizungumza wakati wa kikao na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo (kulia). Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi- EWURA, Profesa Jamidu Katima.

Msicheleweshe wawekezaji- chambo

Page 3: BULLETIN 93 Print.pdf

3BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHABARI ZA NISHATI/MADINI

TahaririMEM

Na Badra Masoud

FIVE PILLARS OF REFORMS

KWA HABARI PIGA SIMU KITENGO CHA MAWASILIANO

BODI YA UHARIRI

MHARIRI MKUU: Badra MasoudMSANIFU: Lucas Gordon

WAANDISHI: Veronica Simba, Asteria Muhozya, Greyson Mwase Teresia Mhagama, Mohamed Saif, Rhoda James ,

Nuru Mwasampeta na Zuena Msuya

INCREASE EFFICIENCYQUALITY DELIVERY

OF GOODS/SERVICE

SATISFACTION OF THE CLIENT

SATISFACTION OF BUSINESS PARTNERS

SATISFACTION OF SHAREHOLDERS

TEL-2110490FAX-2110389

MOB-0732999263

Tuwahudumie Watanzania kwa dhati na moyo thabiti

TEL-2110490FAX-2110389

MOB-0732999263

Zaidi ya leseni 8000 zasajiliwa mfumo mpya wa madini

Mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli kuapishwa, alianza kazi mara moja ya kuwatumikia Watanzania bila kuchoka ili kuhakikisha kwamba Watanzania wanapata huduma bora na ya kuridhisha ndipo alipoamua kufanya ziara za kushtukiza katika baadhi ya taasisi za Serikali ikiwamo hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Wizara ya fedha.

Aidha, Mhe. Rais alikutana na Makatibu Wakuu wa Wizara zote ambao ndiyo watendaji wakuu wa Wizara ambapo pamoja na mambo mengine aliwataka wakawasimamie watumishi wa Wizara zao katika kuwahudumia Watanzania kwa dhati na kuacha uzembe na ubinafsi huku akionya watumishi wazembe kuchukuliwa hatua ikiwamo kuachishwa kazi.

Ili kuongeza ufanisi kazini pamoja na kudhibiti matumizi ya fedha za Serikali Mhe. Rais pia alisitisha safari zote za nje ya nchi ikiwemo Warsha kwa watumishi wote wa Serikali.

Hatua zote hizo alizochukua Mhe. Rais zilipokelewa kwa furaha isiyo na kifani na Watanzania na kusema hayo ndiyo mabadiliko waliyokuwa wakiyataka na wanaamini hatua mbalimbali zaidi zitaendelea kuchukuliwa kwa maslahi ya Watanzania

Katika ziara hizo za Mhe. Rais katika taasisi pia alitoa maelekezo na maamuzi mbalimbali ikiwamo ya kuwataka watumishi wa umma kutambua na kutekeleza wajibu wao ipasavyo wa kuwahudumia Watanzania.

Ziara ya Mhe. Rais kwa taasisi za umma itukumbushe sisi watumishi wa umma kwamba tumepewa dhamana kubwa ya kuwahudumia Watanzania ambao ndiyo waajiri wetu (bosi namba moja) hivyo ni lazima tuheshimu kazi na kuzitekeleza kwa weledi mkubwa bila kuchoka.

Kama hiyo haitoshi ni lazima tufanye kazi kwa kuzingatia miiko na maadili ya utumishi wa umma na kuacha kabisa kufanya kazi kwa mazoea na wakati mwingine kutowajali watanzania kwa kuwapatia huduma duni.

Ni lazima tutambue kwamba sisi watumishi wa umma tuliomba kazi wenyewe ya kuwatumikia Watanzania hivyo tunapaswa kutekeleza majukumu yetu ipasavyo pasipo kungoja kusukumwa na kufuatiliwa na viongozi wetu akiwamo Mhe. Rais, bali kinachotakiwa ni kila mmoja wetu kujitambua yeye binafsi pamoja na kuelewa vema wajibu wake na hatimaye kuutekeleza kwa nafasi yake.

Inasikitisha kuona kwamba kuna baadhi ya watumishi wa Serikali ni wazembe, wabinafsi kwa Watanzania wanaohitaji kupata huduma fulani katika maeneo yao ya kazi.

Nikirejea katika upande wa Wizara yetu ya Nishati na Madini pamoja na taasisi zilizo chini yake, lazima tutambue kuwa sisi pia ni sehemu ya watumishi wa umma au Serikali ambapo huduma tunazozisimamia zinamgusa kila Mtanzania hivyo lazima tuendelee kufanya kazi kwa weledi, maadili, lugha nzuri na kwa kasi kubwa.

Tunaamini Watumishi wa Wizara ya Nishati na Madini pamoja na taasisi zake wataendelea kufanya kazi kwa bidii kubwa na kama wapo baadhi ya wazembe watabadilika haraka kabla hawajawajibishwa.

Katika nchi nyingi zilizoendelea duniani wamefikia maendeleo hayo kutokana na kila Mwananchi kuwajibika kwa nafasi yake na kila mmoja akitanguliza uzalendo, utaifa na ustaarabu mbele huku watoa huduma nao wakiwamo watumishi wa umma wakitoa huduma husika kwa weledi mkubwa na maarifa bila kuchoka kwani nchi hujengwa na wananchi wake na si wananchi wa nchi nyingine.

Tubadilike tufanye kazi kwa weledi na kwa kufuata maadili katika kuwahudumia Watanzania ambao ndiyo walipa kodi ambazo mwisho wa siku tunapata mishahara. Tanzania itajengwa na Watanzania wenyewe na si vinginevyo.

Na Veronica Simba

Imeelezwa kuwa hadi kufikia mwanzoni mwa mwezi Novemba mwaka huu, jumla ya leseni 8205 za madini nchini zimesajiliwa katika mfumo mpya wa utoaji huduma za leseni za madini

kwa njia ya mtandao ujulikanao kama Online Mining Cadastre Transactional Portal (OMCTP). Idadi hiyo inajumuisha leseni za kampuni, vikundi na watu binafsi.

Kamishna Msaidizi wa Madini, Sehemu ya Leseni, Mhandisi John Nayopa aliyasema hayo mapema wiki hii jijini Dar es Salaam alipozungumza na MEM News Bulletin kuhusu tathmini ya mwitikio wa wadau kujisajili katika mfumo huo toka ulipoanza kutumika rasmi mwezi Septemba mwaka huu.

Mhandisi Nayopa aliwataka wachimbaji na wamiliki wa leseni za madini ambao hawajajisajili katika mfumo huo, kuhakikisha wanajisajili kwa wakati ili waweze kuutumia kama Serikali ilivyoelekeza kwa lengo la kuboresha huduma za utoaji na usimamizi wa leseni za madini nchini.

Akifafanua zaidi kuhusu zoezi hilo linaloendelea la usajili wa leseni za madini kwa njia ya mtandao, Mhandisi Nayopa alitaja idadi ya leseni hai zilizosajiliwa kuwa ni 2971 na kwamba hadi kufikia sasa jumla ya maombi ya leseni yaliyosajiliwa ni 621.

Aliendelea kuchanganua kuwa, leseni hai

za uchimbaji madini mdogo zilizosajiliwa kwenye huduma hiyo ni 1206 na kwamba maombi ya leseni za uchimbaji mdogo yaliyosajiliwa kwenye mfumo mpya ni 533.

“Ni jambo jema kwamba wachimbaji wadogo wameitikia vema zoezi hili la kujisajili kwenye mfumo wetu mpya wa utoaji leseni za madini. Nawashauri wale ambao hawajajitokeza kujisajili, wafanye hivyo mapema kwani wasiposajiliwa hawatapata huduma stahiki,” alisisitiza Mhandisi Nayopa.

Akizungumzia kuhusu leseni za utafutaji wa madini zilizosajiliwa hadi kufikia sasa, Nayopa alisema kwa upande wa leseni hai, jumla ya leseni 1618 zimesajiliwa wakati maombi 82 ya leseni za utafutaji yamesajiliwa.

Alitaja makundi mengine ya leseni zilizosajiliwa kuwa ni pamoja na za Milipuko (88) pamoja na Biashara ya Madini ambazo ziko 14.

Alisema, jumla ya Kampuni hai 313 zimekwishasajiliwa katika mfumo huo mpya na kuongeza kwamba katika kipindi cha mwezi Oktoba mwaka huu, jumla ya watumiaji wa mfumo waliosajiliwa ni 244, mwezi Novemba wako 20 wakati idadi ya barua pepe zinazosubiri uhakiki ni 348.

Mfumo wa kutoa huduma za leseni kwa njia ya mtandao ulizinduliwa mapema mwezi Juni mwaka huu mjini Dodoma ili kutoa huduma za haraka, kuongeza uwazi na kumuwezesha mteja kusimamia leseni zake mwenyewe.

Baadhi ya wachimbaji wadogo wa madini wa Mkoani Katavi wakifuatilia mafunzo ya matumizi ya Mfumo wa Huduma ya Leseni kwa njia ya Mtandao yaani Online Mining Cadastre Transactional Portal (OMCTP) yaliyokuwa yakiendeshwa na Wizara ya Nishati na Madini

Page 4: BULLETIN 93 Print.pdf

4 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHABARI ZA NISHATI/MADINI

Na Greyson Mwase, Dar es Salaam

Wataalam kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) wametakiwa kutoa

elimu zaidi kuhusu gesi kwa wadau mbalimbali ili kukidhi matarajio ya wananchi kuhusu manufaa ya sekta hiyo.

Wito huo ulitolewa hivi karibuni jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo alipofanya ziara katika ofisi za TPDC ili kupata taarifa ya maendeleo ya utelekezaji wa majukumu ya shirika hilo.

Mhandisi Chambo alisema kuwa sekta ya gesi ina changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na wananchi kuwa na matarajio makubwa ya matunda ya sekta hiyo tofauti na uhalisia.

“ Wananchi wengi wana matarajio makubwa katika sekta ndogo ya gesi asilia kwa kudhani kuwa inaweza kubadilisha nchi na kuwa tajiri ndani ya muda mfupi mno, hivyo ninawataka kuongeza kasi ya kuelimisha wananchi ili kuepusha migongano inayoweza kujitokeza kutokana na kutokuwa na taarifa sahihi,” alisisitiza Mhandisi Chambo.

Aliongeza kuwa elimu inaweza kutolewa kwa viongozi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mashirika na Taasisi, Wabunge na viongozi wengine wenye ushawishi katika jamii ili waweze kutoa elimu kwa jamii inayowazunguka.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya TPDC Michael Mwanda, alisema kuwa shirika hilo limekuwa likitoa elimu kuhusiana na uwekezaji katika sekta ya gesi kwa makundi mbalimbali ikiwa ni pamoja na viongozi wa dini, wananchi pamoja na kuandaa ziara mbalimbali kwa viongozi mbalimbali katika maeneo kilipo kiwanda cha kuchakata gesi cha Madimba mkoani Mtwara na kwenye miundombinu ya gesi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo (mbele)akiwa kwenye kikao na Menejimenti ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) mara alipofanya ziara katika shirika hilo ili kupata taarifa ya utekelezaji wa majukumu yake.

Chambo aagiza elimu zaidi kuhusu gesi

Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), James Mataragio (kushoto) akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya shirika hilo mbele ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo (hayupo pichani). Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya TPDC, Michael Mwanda.

Sehemu ya wajumbe wa Menejimenti ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) wakifuatilia kwa makini maelekezo yaliyokuwa yakitolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo (hayupo pichani)

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo akizungumza na wajumbe wa menejimenti ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) (Hawapo pichani)

Page 5: BULLETIN 93 Print.pdf

5BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHABARI ZA NISHATI/MADINI

Ufahamu Mradi wa SMMRP

Asteria Muhozya na Teresia Mhagama

Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini, (SMMRP), ulianza kutekelezwa Septemba mwaka

2009, ambapo wazo la kuanzishwa kwake lilichochewa na changamoto mbalimbali zilizokuwepo katika sekta ya madini ikiwemo ongezeko la uhitaji wa taarifa na takwimu za kijiolojia; uendelezaji wachimbaji wadogo na uchangiaji mdogo wa sekta.

Mradi wa SMMRP unatekelezwa chini ya Wizara ya Nishati na Madini, kwa ufadhili wa Benki ya Dunia (WB). Kwa kipindi cha mwaka 2009-2014 na baada ya kuongezewa muda wa utekelezaji wake hadi Juni, 2015, mradi huo ulilenga kuongeza uwezo wa Serikali katika kusimamia sekta ya madini ili kuboresha manufaa ya kijamii yatokanayo na uchimbaji wa madini nchini.

Mbali na hilo, mradi ulilenga kuongeza ustawi wa sekta na kuvutia wawekezaji wa ndani na nje; kukuza uchumi na kugeuza uchimbaji wa madini kuwa kichocheo cha maendeleo na kupunguza migogoro itokanayo na uchimbaji na pia kuboresha usimamizi wa masuala ya mazingira na ya kijamii yanayohusiana na uchimbaji.

Tangu kuanzishwa kwake, mradi wa SMMRP umefanikiwa kutekeleza malengo yaliyokusudiwa kwa kiwango kikubwa, hususani katika utekelezaji wa Awamu ya Kwanza ya mradi huo. Miongoni mwa masuala kadhaa yaliyotekelezwa kwa awamu ya kwanza ni pamoja na kuhamasisha

uongezaji thamani madini, ambapo umefanikiwa kukiimarisha Kituo cha Jimolojia Tanzania, (TGC) kilichopo jijini Arusha na kukifanya kuwa kituo bora cha mafunzo kwa ajili ya ukataji na ung’arishaji wa madini ya vito (lapidary), usonara, utengenezaji wa

bidhaa za mapambo (jewelry design and manufacturing); na uchongaji wa vinyago vya mawe (Stone & Gems Carving).

Akizungumza katika mahojiano maalum na MEM Bulletin, Mratibu wa Kituo cha TGC, Mussa Shanyangi, alieleza kuwa, kituo hicho ni cha pekee na bora kinachotoa mafunzo ya ukataji na ung`arishaji wa madini ya vito (lapidary), usonara, utengenezaji wa bidhaa za mapambo (jewelry design and manufacturing); na uchongaji wa vinyago vya mawe (Stone & Gems Carving), kwa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

“Mafunzo ya ukataji na ung`arishaji wa madini ya vito yalianza mwaka 2014 kukiwa na idadi ya wanafunzi 15. Mwezi Agosti mwaka huu tumepata wanafunzi 18 na watakapohitimu tutachukua wengine. Lakini pia yapo mafanikio ambayo yametokana na kundi la kwanza la wanafunzi wetu kwani baadhi tayari wamepata ajira kwa wafanyabiashara wa madini,” alieleza Shanyangi.

Aidha, mradi wa SMMRP, ulifanya ukarabati mkubwa wa majengo ya TGC ili kuhakikisha kituo kinakuwa na miundombinu bora na ya kisasa. Mbali na hayo mradi umefanikiwa kununua vifaa vya kisasa vitakavyotumika kwa ajili ya utoaji mafunzo ya uongezaji thamani madini.

Akizungumzia kuhusu wakufunzi wa kituo hicho, alisema mbali na

mkufunzi kutoka nchini Sri-Lanka aliyebobea katika masuala hayo, kituo hicho kipo kwenye maandalizi ya kuwawezesha wataalam wakitanzania watatu (3) ili waweze kuwa miongoni mwa wakufunzi wa kutoa mafunzo katika kituo hicho.

Wakati wa kikao cha ufungaji wa Awamu ya Pili ya Mradi (Additional Financing), kilichofanyika tarehe 22 Septemba, 2015, mjini Morogoro, ilielezwa kuwa, mradi wa SMMRP utaendelea kuhamasisha uongezaji thamani madini kwa kuendelea kukiwezesha kituo cha TGC ili kuwa bora zaidi.

Wawezesha uwepo wa kituo bora cha Jimolojia Afrika Mashariki na Kati

Mratibu wa Kituo cha TGC, Mussa Shanyangi (katikati) akionesha moja ya mapambo ya vinyago vilivyochongwa katika kituo hicho kwa kutumia madini ya mawe. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Manunuzi, Amon MachAyo na kulia ni mtendaji kutoka Kampuni iliyofanya ukarabati wa majengo ya Kituo hicho ya Kiure Engineering.

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Paul Masanja (wa nne kutoka kushoto mstari wa pili) akiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi 15, wa awamu ya kwanza, waliopata ufadhili wa masomo ya uongezaji thamani madini yanayoendeshwa katika Kituo cha Jimolojia (TGC) jijini Arusha. Wengine katika picha ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Madini nchini, Richard Kasesera (wa pili kushoto mstari wa pili),Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa Madini nchini (TAMIDA), Sammy Mollel (wa tatu kushoto mstari wa pili),Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Maonesho ya Kimataifa ya Vito Arusha, (AGF), Peter Pereirra(wa tatu kulia mstari wa pili) Mwalimu anayefundisha masomo hayo kutoka nchini Sri Lanka, Pathmasiri Alwis (wa kwanza kushoto mstari wa pili) pamoja na watendaji Kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Kituo cha Jimolojia (TGC) na Wakala wa Ukaguzi wa Madini nchini (TMAA).

Picha Na. 1na 2 ni miongoni mwa wanafunzi 15 waliopata mafunzo ya ukataji na unga’rishaji wa madini ya vito kwa awamu ya kwanza katika kituo cha TGC .

Gari linalotumika kubeba madini ya mawe yanayotumika kwa ajili ya mafunzo ya kuchonga vinyago vya mawe katika kituo cha TGC. Gari hilo lilitolewa kwa kituo hicho kupitia mradi wa SMMRP.

1

2

Page 6: BULLETIN 93 Print.pdf

6 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHABARI ZA NISHATI/MADINI

MATUKIO KATIKA PICHA:

Mkurugenzi wa Idara ya Ufundi kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Bengiel Msofe akieleza jambo wakati wa kikao kati ya Wakala huo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo. REA wamekutana na Katibu Mkuu kueleza majukumu ya Wakala huo ikiwemo taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali inayosimamiwa na Wakala. Wengine katika picha ni baadhi ya watendaji wa REA na Wizara.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo, akiongoza kikao kati wa Watendaji Wakuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na baadhi ya watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini. Kikao hicho kilijadili majukumu ya Wakala huo, utekelezaji wa miradi mbalimbali, changamoto na kujadili namna bora ya kutekeleza miradi inayosimamiwa na Wakala huo.

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Dkt. Lutengano Mwakahesya, akizungumza jambo wakati wa kikao baina ya REA na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo. Kushoto kwa Dkt. Mwakahesya ni Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli, Mhandisi Hosea Mbise.

Watendaji REA

Page 7: BULLETIN 93 Print.pdf

7BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHABARI ZA NISHATI/MADINI

Kwa wadau wa sekta za Nishati na Madini, tembelea kurasa mpya za Wizara kwenye Mitandao ya Kijamii ya Twitter na Facebook kwa anuani ya ‘Nishati na Madini’ Karibu tuhabarishane na

tujadili kuhusu sekta za Nishati na Madini kwa maendeleo ya Watanzania wote.Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

Na Rhoda James

Serikali imeiagiza Kampuni ya kuhifadhi Mafuta Tanzania (TIPER) kuhakikisha inaboresha shughuli zake

kwa kuongeza idadi ya matenki ya kuhifadhia mafuta.

Wito huo umetolewa hivi

karibuni na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo wakati wa kikao chake na uongozi wa kampuni hiyo.

“Tunahitaji tuwe na akiba ya kutosha kwa hivyo mjitahidi kuhakikisha mnajenga matenki mengine ili kuongeza wigo wa uhifadhi wa mafuta ,” alisema

Mhandisi Chambo.Naye Mkurugenzi Mtendaji

wa Kampuni hiyo Stephane Gay, alimuhakikishia Katibu Mkuu kwamba kampuni yake itajenga matenki mengine kwa kuwa dhamira ya kampuni yake hiyo ni kuhakikisha kwamba mafuta yanapatikana kwa wakati.

Gay alisema pia watahakikisha

kuwa ukusanyaji wa mapato na kodi zinakusanywa na Mamlaka ya Mapato (TRA) kwa urahisi ili kuwezesha Wananchi kunufaika na mapato hayo.

Aidha, Mkurugenzi huyo alieleza kusikitishwa kwake na wizi wa mabomba ya mafuta unaofanyika mara kwa mara jambo ambalo anasema linasababisha kupotea kwa mapato ya kampuni hiyo na hivyo kumuomba Katibu Mkuu kuingilia kati suala la ulinzi.

Akizungumzia suala la ulinzi, Mhandisi Chambo alisema suala la ulinzi ni jukumu la Serikali na Watanzania kwa ujumla kwa kuwa Serikali ina ubia wa asilimia 50.

Mkutano huo wa Katibu Mkuu na kampuni hiyo ulihudhuriwa pia na Mkurugenzi Mtendaji Msaidizi wa Kampuni hiyo, Paulo Mnzava na Mwenyekiti wa Bodi ya TIPER, Profesa Abdulkarim Mruma lengo likiwa ni kujadili shughuli zinazofanywa na kampuni hiyo.

Vile vile Chambo alisema kuwa lengo kuu la kikao hicho ni kufahamiana na uongozi wa Kampuni hiyo ya kuhifadhia mafuta ya TIPER na ameahidi ya kufanya nao kazi kwa karibu ili kutatua matatizo yaliyopo likiwemo la ulinzi.

TIPER waagizwa kujenga matenki zaidi ya kuhifadhi mafuta

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo (kulia) akizungumza katika mkutano na viongozi wa TIPER na Viongozi waandamizi kutoka Wizara ya Nishati na Madini. Wa pili kulia kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni hiyo ya TIPER Prof. Abdulkarim Mruma, anayemfuatia ni Mkurugenzi Mtendaji wa TIPER, Stephane Gay akifuatiwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Kampuni hiyo, Paul Mnzava.

Wa kwanza kushoto ni Kamishna wa Nishati, Mhandisi Hosea Mbise, wa pili ni Kamishna Msaidizi anayeshughulikia masuala ya Petroli, Mhandisi Stanley Marisa, wa tatu Afisa kutoka Idara ya Nishati Arthur Lyatuu na wa nne ni Fadhili Kilewo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo katika kikao hicho akisisitiza jambo kwa Uongozi wa Kampuni ya TIPER.