ar-Radd al-Jawaab Ahmad an-Najmiy - Firqatu Nnajia |...
Transcript of ar-Radd al-Jawaab Ahmad an-Najmiy - Firqatu Nnajia |...
ar-Radd al-Jawaab
Ahmad an-Najmiy
1
www.firqatunnajia.com
ar-Radd al-Jawaab
Mwandishi:
´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
Kimefupishwa na kufasiriwa na:
Firqatunnajia.com
ar-Radd al-Jawaab
Ahmad an-Najmiy
2
www.firqatunnajia.com
Barua Ya Ibn Jibriyn Kwa Ahmad an-Najmiy ........................................................................................ 3
Ahmad an-Najmiy anamjibu Ibn Jibriyn 1 ............................................................................................. 5
Ahmad an-Najmiy anamjibu Ibn Jibriyn 2 ............................................................................................. 7
Ahmad an-Najmiy anamjibu Ibn Jibriyn 3 ........................................................................................... 12
Ahmad an-Najmiy anamjibu Ibn Jibriyn 4 ........................................................................................... 14
Ahmad an-Najmiy anamjibu Ibn Jibriyn 5 ........................................................................................... 20
Ahmad an-Najmiy anamjibu Ibn Jibriyn 6 ........................................................................................... 22
Ahmad an-Najmiy anamjibu Ibn Jibriyn 7 ........................................................................................... 25
Ahmad an-Najmiy anamjibu Ibn Jibriyn 8 ........................................................................................... 26
Ahmad an-Najmiy anamjibu Ibn Jibriyn 9 ........................................................................................... 29
Ahmad an-Najmiy anamjibu Ibn Jibriyn 10 ......................................................................................... 31
Ahmad an-Najmiy anamjibu Ibn Jibriyn 11 ......................................................................................... 33
Ahmad an-Najmiy anamjibu Ibn Jibriyn 12 ......................................................................................... 35
´Allaamah al-Fawzaan kuhusu kitabu ambacho Ibn Jibriyn alikuwa hataki kichapishwe ........... 38
ar-Radd al-Jawaab
Ahmad an-Najmiy
3
www.firqatunnajia.com
Barua Ya Ibn Jibriyn Kwa Ahmad an-Najmiy
[Baada ya salaam za kidugu na utangulizi...
Nimepata kitabu chako "al-Mawrid al-´Adhb az-Zulaal intuqida ´alaa ba´dhw-il-
Manaahij ad-Da´wiyyah min al-´Aqaa´id wal-A´maal". Nilifurahishwa na kichwa
cha khabari hichi chenye kuvutia ambacho kilinifanya kutaka kusoma kitabu
chote. Mwanzoni nilifikiri kuwa ni maudhui yenye faida kuhusiana na
kulingania katika Tawhiyd na mifumo ya Da´wah.
Nilipofika kwenye mlango wa tisa, nilikutana na kitu ambacho sikukitarajia
kutoka kwa mtu kama wewe. Inahusiana na kumsema vibaya Hasan al-Bannaa.
Unamshambulia na kufasiri maneno yake kimakosa.
Miaka kumi iliyopita nilipata khabari kuhusu mtu huyu kutoka kwa wanachuoni
waheshimiwa kama Shaykh ´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy, Shaykh ´Abdur-Rahmaan
ad-Dawsaariy, Shaykh ´Abdullaah bin Humayd, Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Baaz
na watu mfano wao. Walichunguza kisa chake na kumpa udhuru kwa makosa
aliyotumbukiaemo. Walikuta maneno yake yanaashiria kuwa alikuwa ni mtu
mwenye Ikhlaasw na mpwekeshaji. Allaah Amenufaisha watu kwa ulinganizi
wake na Amewaongoza watu wengi kupitia kwake. Nyakati zote anasifiwa
katika vikao na vitabu vyake vinasomwa.
Lakini tokea miaka saba ya nyuma ndugu wengi wamemshambulia na
kumpokonya haki yake. Haieleweki kabisa. Kuna vitabu vinavyojulikana
ambavyo ni vibaya zaidi kuliko vitabu vyake. Kuna walinganizi, walio hai maiti,
waliopinda zaidi kuliko yeye.
ar-Radd al-Jawaab
Ahmad an-Najmiy
4
www.firqatunnajia.com
Hivyo basi, mimi ninakunasihi, ee Shaykh, kuchunga ulimi wako na
kumzungumza vibaya mtu huyu ambaye Allaah Amewanufaisha na
Kuwaongoza wengi kupitia yeye. Usichapishe kitabu hiki ambacho kitakuja
kukupa tetesi mbaya na kukufanya kusema vibaya heshima ya ndugu yako
Muislamu.
Nasikitika siwezi kukutumia nuskha [uliyonitumia] kwa sababu nimeiwekea
taaliki ambayo sitaki ije kuonekana. Allaah Akitujaalia kuweza kukutana,
ninatumai majadiliano ya kimdomo.
´Abdulaah bin ´Abdir-Rahmaan al-Jibriyn
Mwanachama wa Daar-ul-Iftaa´ wad-Da´wah wal-Irshaad.
ar-Radd al-Jawaab
Ahmad an-Najmiy
5
www.firqatunnajia.com
Ahmad an-Najmiy anamjibu Ibn Jibriyn 1
[Baada ya salaam za kidugu na utangulizi...
Unasema kwenye barua yako:
"Nimepata kitabu chako "al-Mawrid al-´Adhb az-Zulaal intuqida ´alaa ba´dhw-il-
Manaahij ad-Da´wiyyah min al-´Aqaa´id wal-A´maal". Nilifurahishwa na kichwa
cha khabari hichi chenye kuvutia ambacho kilinifanya kutaka kusoma kitabu
chote. Mwanzoni nilifikiri kuwa ni maudhui yenye faida kuhusiana na
kulingania katika Tawhiyd na mifumo ya Da´wah.
Nilipofika kwenye mlango wa tisa, nilikutana na kitu ambacho sikukitarajia
kutoka kwa mtu kama wewe. Inahusiana na kumsema vibaya Hasan al-Bannaa.
Unamshambulia na kufasiri maneno yake kimakosa."
Nilisikitika pindi niliposoma barua yako na vipi inaweza kutoka kwa mtu kama
wewe ulie na elimu na nafasi kama ulonayo.
Lau ungeliendelea kusoma na kuona kama nimesema haki au batili. Ikiwa ni
haki, basi nitakuwa nimetekeleza kutokana na kauli ya Mtume (Swalla Allaahu
´alayhi wa sallam):
"Mnusuru ndugu yako sawa akiwa ni mwenye kudhulumu au mwenye
kudhulumiwa." Kukasemwa: "Tunajua anavyonusuriwa mwenye kudhulumiwa,
vipi ananusuriwa ikiwa ni mwenye kudhulumu?" Akasema: "Mzuie na
dhulumu yake."
Na ikiwa nimesema batili, basi utanisaidia kwa kunionyesha haki kwa dalili na
hoja. Niko tayari kupokea hilo kutoka kwako. Nitakushukuru kwa hilo na
kukuombea du´aa kwa kuwa utakuwa umeniokoa kutokana na dhambi na
dhuluma ambayo nitakuwa nimetumbukiamo. Hata hivyo nina sharti. Ninataka
ar-Radd al-Jawaab
Ahmad an-Najmiy
6
www.firqatunnajia.com
uje na ukosoaji uliofafanulia ulio na hoja na dalili za wazi kabisa zenye
kubainisha kosa langu.
Ama kufika tu kwenye mlango wa tisa kisha unaacha kusoma na kunishambulia
tu pasina dalili yoyote, hili ni jambo ambalo sikukubalii. Sintoafikiana na wewe
kabisa.
ar-Radd al-Jawaab
Ahmad an-Najmiy
7
www.firqatunnajia.com
Ahmad an-Najmiy anamjibu Ibn Jibriyn 2
Unasema:
"Nilifurahishwa na kichwa cha khabari hichi chenye kuvutia ambacho kilinifanya
kutaka kusoma kitabu chote. Mwanzoni nilifikiri kuwa ni maudhui yenye faida
kuhusiana na kulingania katika Tawhiyd na mifumo ya Da´wah.
Nilipofika kwenye mlango wa tisa, nilikutana na kitu ambacho sikukitarajia
kutoka kwa mtu kama wewe. Inahusiana na kumsema vibaya Hasan al-Bannaa."
1- Allaah Anajua fika ya kwamba sikusudii kuvunja heshima ya yeyote, si Hasan
al-Bannaa wala mtu mwingine. Ninajua kuwa haki zitachukuliwa siku ya
Qiyaamah kwa matendo mema na mabaya.
2- Unajua kuwa kutaja kasoro za mtu inajuzu ikiwa kuna faida ya kufanya hivo.
Ni miongoni mwa usengenyaji unaojuzu. Dalili ya hilo ni maneno ya Mtume
(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumwambia Faatwimah bint Qays wakati
alipokuja na kumuomba ushauri (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wa kuolewa
na nani. Akamwambia (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
"Ama Mu´aawiyah ni mtu taabani hana mali. Ama Abu Jahm ni mtu anawapiga
wanawake. Olewa na Usaamah bin Zayd."
3- Unajua kuwa Muhaddithuun wamezungumzia juu ya wapokezi kwenye
minyororo kwa njia yenye kupelekea mapokezi yao kurudishwa au
kudhoofishwa. Wamesema fulani ni mwongo, mzushi, hifdhi dhaifu, anakosea
sana, mghafilikaji na kadhalika. Wamefanya hivo kwa nasaha kwa ajili ya Allaah,
Mtume Wake, waislamu na kuilinda Sunnah ya Mtume wa Allaah (Swalla
Allaahu ´alayhi wa sallam) ili kusiingizwe ndani yake yasiyokuwemo.
4- Wewe mwenyewe umesema kwenye kitabu chako "Akhbaar-ul-Aahaad" (uk.
30):
ar-Radd al-Jawaab
Ahmad an-Najmiy
8
www.firqatunnajia.com
"Inatakiwa kuchunguza hali za wapokezi na kutafiti nafasi zao katika Hadiyth na
upeo wao. Wanachuoni wamezungumza juu yao kwa ajili ya kutoa nasaha kwa
Ummah kwa vile wamejivisha jukumu la kufikisha sehemu ya dini ilio na
hukumu. Wamekhusisha aina hii [kuwa inajuzu] kwa makatazo ya kijumla ya
kusengenya kutokana na faida inayopatikana kwa Ummah."
Hili ni sahihi kabisa.
5- Jifikirie ni kitu gani kilichonifanya mimi kumraddi mtu huyu ambaye amekufa
pindi nilipokuwa mtoto. Hakumwaga damu yangu. Hakuvunja heshima yangu.
Hakuchukua mali yangu. Ni kitu gani kimechonifanya mimi kutahadharisha juu
yake ilihali hakunifanya lolote? Ikiwa nimemsema vibaya bila ya yeye kunifanya
chochote na bila ya maslahi ya kidini yanayopatikana, basi mimi nimemdhulumu
na Allaah Atachukua haki yangu na kumpa yeye.
6- Leo tumewekwa katika mtihani na mifumo mbali mbali ya ki-Da´wah.
Imetoka nje ya nchi yetu. Inachukulia usahali wa shirki kubwa. Wanachukulia
usahali wa Tawhiyd na Bid´ah. Miongoni mwa mifumo hiyo muhimu na ilioenea
sana kwa kueneza ufisadi na uharibifu mkubwa ni mfumo wa al-Ikhwaan al-
Muslimuun. Wanasafisha akili za vijana wanaolelewa humo. Wanawafanya
kuwa watu wa mapinduzi, Takfiyriyyuun, maigaidi na Khawaarij. Kuna dalili
nyingi juu ya hilo. Katika dalili zilizo muhimu zaidi ni kukubali kwa wahalifu
waliolipua ´Ulayyaa ar-Riyaadh kama ´Abdul-´Aziyz al-Mu´thim na marafiki
zake. Hili ndio limelonifanya kuandika juu yake na chama chake kabla ya
kutokea ulipuaji huu.
7- Umeandika:
"Nilipofika kwenye mlango wa tisa, nilikutana na kitu ambacho sikukitarajia
kutoka kwa mtu kama wewe. Inahusiana na kumsema vibaya Hasan al-Bannaa.
Unamshambulia na kufasiri maneno yake kimakosa."
ar-Radd al-Jawaab
Ahmad an-Najmiy
9
www.firqatunnajia.com
a) Lau ungelisoma kitabu chote kwa inswafu, basi ungelijua kuwa nilichofanya ni
mimi kubainisha tu jinsi mfumo huu na muasisi wake anavotumbukia kwenye
makosa yanayoenda kinyume na Shari´ah ya Kiislamu na ´Aqiydah ya Salaf.
Yeye ndiye ambaye amesema, na kaka yake amekubali na kujifakharisha kwa
hilo na ni jambo limeenea katika vitabu vya mapote:
"Ee Allaah! Sema na uache uwepo na yale yaliyomo. Ikiwa umeelewa, basi
utaona kuwa hakuna aliyepo isipokuwa Allaah, si maalum wala jumla."1
Ikiwa wewe unaonelea kuwa nimeyafasiri maneno yake kimakosa, ninakuomba
unifasirie wewe maneno yake haya kwa njia inayokubalika Kishari´ah na kiakili
pasina kuingia kwenye Wahdat-ul-Wujuud.
b) Vilevile yeye ndiye alikuwa akiimba:
"Ee Allaah, swalia nuru (yaani Mtume) Ulioifanya kuja kwa walimwengu na
inayoangazia kwa jua na mwezi. Mpenzi huyu (yaani Mtume) amehudhuria
pamoja na wapenzi wake na amemsamehe kila mmoja kwa yaliyopitika."
Nifasirie matamshi haya kwa njia ambayo haina shirki kubwa pindi anaposema:
"Mpenzi huyu (yaani Mtume) amehudhuria pamoja na wapenzi wake na
amemsamehe kila mmoja kwa yaliyopitika."?
Unaweza kunifasiria matamshi haya kwa njia isiyokuwa ya kumzulia uongo
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na uongo wa Suufiyyah pindi
wanaposema kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anahudhuria
sherehe zao za uzushi wakati wanaposherehekea kuzaliwa kwa Mtume
[Maulidi]?
1 Hasan al-Bannaa bi Aqlaam Talaamiydhih wa Mu´aaswiriyh,uk 70-71.
ar-Radd al-Jawaab
Ahmad an-Najmiy
10
www.firqatunnajia.com
c) Unaweza kunifasiria kumsifu kwake al-Marghaniy ambaye alikuwa
anajulikana kwa Wahdat-ul-Wujuud kwa tafsiri anayoiridhia Allaah, Mtume
Wake na waumini pasina kuridhia Wahdat-ul-Wujuud na kuwasifu wenye nayo?
d) Unaweza kunifasiria maneno yake "Kati yetu sisi na mayahudi hakuna uadui
wa kidini" kwa tafsiri anayoiridhia Allaah, Mtume Wake na waumini isiyokuwa
ya kupakana mafuta na mayahudi na manaswara na kumsemea uongo Allaah,
Mtume Wake na Uislamu?
e) Unaweza kunifasiria muhadhara wake kwenye kaburi la Zaynab katika
mnasaba wa kusherehekea mwaka mpya wa Kiislamu bila ya kutaja shirki na
kukataza hilo pamoja na kwamba anaona jinsi watu wanavolizunguka kaburi na
kuliomba kitu ambacho hakiombwi isipokuwa kutoka kwa Allaah Pekee?
Nifasirie muhadhara huo kwa tafsiri anayoiridhia Allaah, Mtume Wake na
waumini pasina kuridhia shirki kubwa na kujijuzishia na mfumo wake?
f) Unaweza kunifasiria kwenda kwake kwenye kaburi la ad-Dasuuqiy na Sanjar
kwa umbali wa kilomita 40 kwenda na kurudi kwa tafsiri anayoiridhia Allaah,
Mtume Wake na waumini bila ya matembezi ya kishirki au ya kizushi?
g) Unaweza kunifasiria njama zake za kufanya Ahl-us-Sunnah na Raafidhwah
wakaribiane kwa tafsiri anayoiridhia Allaah, Mtume Wake na waumini pasina
ujinga wa Bid´ah na upotevu wa Raafidhwah, au kuchukulia usahali upotevu
wao, na kwa hivyo kuitoa fidia ´Aqiydah ya Kiislamu kwa ajili ya kuwaridhisha
Raafidhwah?
h) Unaweza kunifasiria kujigonga kwake anaposema kuwa Da´wah yake ni
Salafiyyah, njia yake ni ya ki-Sunnah na uhakika wake ni Suufiyyah? Je, ni jambo
linalowezekana Suufiyyah ikawa pamoja na Salafiyyah na Suufiyyah na Sunnah?
Ni kama mfano wa kukutanisha moto na maji!
ar-Radd al-Jawaab
Ahmad an-Najmiy
11
www.firqatunnajia.com
i) Unaweza kunifasiria nguzo kumi ambazo utiifu wake na usikivu [bay´ah]
umejengwa juu yake kwa tafsiri anayoiridhia Allaah, Mtume Wake na waumini
pasina kuleta Da´wah ilio na Shari´ah mpya?
j) Unaweza kunifasiria maneno yake anaposema kuwa madhehebu ya Salaf wote
katika Sifa ni Tafwiydh kwa tafsiri anayoiridhia Allaah, Mtume Wake na
waumini bila ya ujinga juu ya madhehebu ya Salaf katika Sifa, au kuwasemea
uongo, kwa vile tunajua kuwa Salaf wanaamini maana pasina kujua namna
yake?
Ukinifasiria maneno haya kwa tafsiri isiyopingana na Shari´ah na lugha,
ninastahiki maneno yako pale ulipoandika kuwa nimefasiri maneno yake
kimakosa. Ukishindwa kufanya hivo, itabainika kuwa umenizulia uongo.
Utambue kuwa sintokuomba haki yangu isipokuwa mbele ya Allaah siku ya
Qiyaamah. Hata hivyo nataka tumuweke Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah
bin Baaz, Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aal ash-Shaykh, Shaykh Swaalih
bin Fawzaan al-Fawzaan, Shaykh ´Abdullaah al-Ghudayyaan na Shaykh Swaalih
al-Atram kati yako wewe na mimi ili wasome mlango wa tisa kuanzia mwanzo
wake mpaka mwisho. Wakiona kuwa nimefasiri maneno ya al-Bannaa kimakosa,
basi wanihukumu. Na wakiona kuwa mtu ambaye amesema hivo ndio
amenidhulumu na kunisemea uongo, basi wamhukumu.
ar-Radd al-Jawaab
Ahmad an-Najmiy
12
www.firqatunnajia.com
Ahmad an-Najmiy anamjibu Ibn Jibriyn 3
Umeandika kwenye barua yako:
"Nilipofika kwenye mlango wa tisa, nilikutana na kitu ambacho sikukitarajia
kutoka kwa mtu kama wewe."
Je, waonelea kuwa nimemuasi Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi
wa sallam) na kwenda kinyume na Shari´ah ya Kiislamu pindi nilipobainisha
haki? Si Allaah ndiye alichukua ahadi kutoka kwa watu wa Kitabu ya kubainisha
haki na wasiifiche. Si ahadi hiyo hiyo iliyochukuliwa kwetu? Si Mtume (Swalla
Allaahu ´alayhi wa sallam) ndiye aliomba kutoka kwa Maswahabah zake (Swalla
Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati walipokuwa wanataka kumpa kiapo cha
usikivu na utiifu katika Hadiyth ambayo imepokelewa na ´Ubadah bin as-
Swaamit:
"... na tuzungumze haki popote tulipo pasina kuchelea lawama za mwenye
kulaumu."?
Allaah (´Azza wa Jalla) hakuwalaani wale wanaoficha haki wakati (Jalla wa
´Alaa) Aliposema:
عنون و ي لع ن هم الل ه ي لع ن هم أول ئك الكت اب ف للن اس ب ي ن اه م ا ب عد من و الد ى الب ين ات من أ نز لن ا م ا ي كتمون ال ذين إن الل
"Hakika wale wanaoficha yale Tuliyoyateremsha katika hoja bayana na uongofu baada ya kuwa Tumeyabainisha kwa watu katika Kitabu, hao Anawalaani Allaah na wanalaaniwa na kila mwenye kulaani."2
2 02:159
ar-Radd al-Jawaab
Ahmad an-Najmiy
13
www.firqatunnajia.com
Si jambo la wajibu kwa wanachuoni kuwaraddi wale wenye kwenda kinyume na
Shari´ah na hukumu zake? Wakighafilika nalo, basi wameghafilikia wajibu
uliofaradhishwa. Baadhi wakifanya hivo, haiwawajibikii wengine. Hata hivyo
wanatakiwa kumuombea du´aa kwa kubainisha haki na kumshukuru baada ya
kumshukuru Allaah badala ya kumtuhumu na kumjengea dhana mbaya.
Salaf siwalijisalimisha na jambo hili? Je, hawakutekeleza wajibu huu? Waliandika
vitabu visivyohesabika kuwaraddi Ahl-ul-Bid´ah tokea wakati wa Taabi´uun
mpaka hii leo na bado wanafanya hivo.
Ee Shaykh! Hukuandika vitabu viwili ukiwaraddi Ahl-ul-Bid´ah? Kitabu
"Khabaar-ul-Aahaad" ambapo umewaraddi Mu´tazilah na wale wenye
kuwafuata na kitabu "al-Faaiq fiy ar-Radd ´alaa man baddal al-Haqaaiq".
Ninaapa kwa Allaah ya kwamba ninampenda mtu anayeitetea dini na kumraddi
yule anayeingiza ndani kisichokuwemo.
Pamoja na hivyo sijui ni kwa nini baadhi ya Mashaykh - Allaah Awaongoze -
wanapinda katika haki na kumkemea yule mwenye kutekeleza wajibu huu na
kumzingatia kuwa ni mchokozi na mwenye kudhulumu. Lau mtu angelisema
kitu cha ubinafsi juu yao, basi dunia nzima ingelisimama. Lakini wakati ambapo
dini inatumiwa vibaya, haina neno! Je, namna hii ndivyo tumevoshikamana
kiuadilifu na dini? Namna hii ndivyo tunavotekeleza wajibu wake? Au hii ni njia
ya kuikandamiza dini na kupuuzia haki zake na kuacha mafundisho yake
yakapotea hewani? Hili ni khaswa pale ambapo itakuwa inahusiana na misingi
ya dini, kanuni zake na misingi yake inatumiwa vibaya na besi ya Tawhiyd
inayovunjwa na shirki kubwa na Sunnah inayovunjwa na Bid´ah na haki
inayovunjwa na batili. Unaonelea tunyamazie mambo kama hayo? Ninaapa kwa
Allaah hatuwezi. Mmoja wenu ni lazima afanye faradhi hii. Mwenye kufanya
hilo analipwa ujira na thawabu nyingi na Allaah.
ar-Radd al-Jawaab
Ahmad an-Najmiy
14
www.firqatunnajia.com
Ahmad an-Najmiy anamjibu Ibn Jibriyn 4
Umeandika kwenye barua yako:
"Miaka kumi iliyopita nilipata khabari kuhusu mtu huyu kutoka kwa
wanachuoni waheshimiwa kama Shaykh ´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy, Shaykh
´Abdur-Rahmaan ad-Dawsaariy, Shaykh ´Abdullaah bin Humayd, Shaykh
´Abdul-´Aziyz bin Baaz na watu mfano wao. Walichunguza kisa chake... "
Mosi ni kuwa uliwauliza Mashaykh hawa kabla ya kujua hali yake.
Pili pengine ilikuwa hivo pale ambapo mtu alikuwa tu na uelewa wa kijumla juu
ya ulinganizi wake. Ni kitu ambacho watu wengi wamedanganyika nacho
mpaka hii leo. Hawajui mfumo huu vizuri kwa vile walikuwa hawajausoma.
Tatu walikuwa kimya kwa sababu walikuwa hawajui makosa yake. Katika hali
hii mtu anatakiwa kunyamaza.
Nne makosa mengi ya mfumo wake yamejitokeza na yule aliyehifadhi ni hoja juu
ya yule ambaye hakuhifadhi. Hii ni kanuni inayojulikana kwa Muhaddithuun na
ni wajibu kuitendea kazi katika hali kama hii.
Tano Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz bado yuhai. Ni jambo
lisilokuwa na shaka anajua waliyomo. Aliulizwa swali lifuatalo:
"al-Ikhwaan al-Muslimuun wameingia Saudi Arabia tangu muda kidogo.
Wamekuwa ni wenye bidii kati ya wanafunzi. Unasemaje juu ya harakati hizi na
ni kiasi gani imeafikiana na mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah?"
Akajibu:
"al-Ikhwaan al-Muslimuun wamekosolewa na wanachuoni wakubwa kwa kuwa
hawatilii umuhimu kulingania katika Tawhiyd na kukemea shirki na Bid´ah.
Wana njia maalum ambazo nafasi zake zinafanya kutolingania kwa Allaah na
ar-Radd al-Jawaab
Ahmad an-Najmiy
15
www.firqatunnajia.com
´Aqiydah sahihi walio nayo Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. al-Ikhwaan al-
Muslimuun wanatakiwa kutilia umuhimu wa kulingania kwa mujibu wa
ulinganizi wa Salafiyyah na kulingania kwa Allaah na kukataza kuabudu
makaburi, kuwategemea maiti, kuwataka msaada maiti kama al-Husayan, al-
Badawiy au wengine. Hili ndio linalotakikana kufikisha."3
Mpendwa ndugu Muislamu! Umesikia alivojibu Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Baaz?
Ni kwa nini husemi aliyosema kuhusu ulinganizi wa al-Ikhwaan al-Muslimuun
na yale yanayoenda kinyume na mfumo wa Salaf?
Kuhusiana na Mashaykh wengine uliyowataja mbali na Shaykh ´Abdul-´Aziyz,
basi wamedanganyika kama wewe ikiwa kama ni kweli wametaja athari zake
nzuri. Lakini yanayodhihiri kwenye maneno yako ni kwamba wewe ni mwenye
kukinaika juu ya kwamba alikuwa na athari nzuri. Ndio maana nina maswali
kadhaa ya kukuuliza ambayo nilikuwa nataka unijibu kwa ukweli:
1- Je, ni katika athari zake nzuri kunyamazia kwake shirki ambayo ilikuwa
inafanywa na watu kwenye makaburi Misri pasina kukataza hilo?
2- Je, ni katika athari zake nzuri kuasisi kwake chama ambacho amekiacha baada
yake kikafarikanisha Ummah?
3- Je, ni katika athari zake nzuri kuita katika ukhaliyfah badala ya Tawhiyd
iliyolinganiwa na Mitume?
4- Je, ni katika athari zake nzuri kuwafanya watu wakawachukia watawala na
wanachuoni kuzipindua nchi zilizoko sasa ili, kama wanavodai, waanzishe
khilaafah?
3 al-Majallah/ash-Shaykh Ibn Baaz: Lastu muta´asswiban…
ar-Radd al-Jawaab
Ahmad an-Najmiy
16
www.firqatunnajia.com
5- Je, ni katika athari zake nzuri kupekua kasoro za watawala na wanachuoni,
jambo ambalo linafanywa na wafuasi wake, na kudai ya kwamba hawastahiki
kuwa na uongozi na kwamba wanachuoni ni wenye kuwapaka tu mafuta?
6- Je, ni katika athari zake nzuri kuwadanganya watu na kuwaacha wakalingania
katika Uislamu ilihali ni wajinga?
7- Je, ni katika athari zake nzuri kujiwajibishia yeye mwenyewe kiapo cha utiifu
na usikivu na kuwaacha watawala?
8- Je, ni katika athari zake nzuri kuhamasisha Shiy´ah na Ahl-us-Sunnah kuwa na
ukaribu? Hii ina maana ya kila kundi liache baadhi ya I´tiqaad zake ili kati yao
wawe na ukaribu.
9- Je, ni katika athari zake nzuri kudai kwake ya kwamba Salaf walikuwa
hawajui ni nini maana ya Sifa za Allaah?
10- Je, ni katika athari zake nzuri kusema kuwa hakuna uadui wowote wa kidini
kati yetu sisi na mayahudi? Hii ina maana ya kwamba mayahudi ni ndugu zetu.
11- Je, ni katika athari zake nzuri kusema kwamba twashirikiana kwa yale
tunayoafikiana na kupeana udhuru kati yetu kwa yale tunayotofautiana? Hii ina
maana ya kuacha kuamrisha mema na kukataza maovu ambako Allaah
Amewasifu kwa ajili yake waumini na kuwatapa kwalo:
ي ر كنتم عروف ت مرون للن اس أخرج ت أم ة خ بلل ه و ت ؤمنون المنك ر ع ن و ت ن ه ون بلم
"Mmekuwa Ummah bora kabisa uliotolewa [mfano] kwa watu: mnaamrisha mema na mnakataza maovu na mnamwamini Allaah."4
4 03:110
ar-Radd al-Jawaab
Ahmad an-Najmiy
17
www.firqatunnajia.com
12- Je, ni katika athari zake nzuri kukusanya I´tiqaad zote kama Ahl-us-Sunnah,
Shiy´ah, Suufiyyah, Jahmiyyah, Mu´tazilah na kadhalika na kudai ya kwamba
wote ni ndugu kwa sababu wote wanashuhudia ya kwamba hapana mola
mwenye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni
Mtume wa Allaah hata kama watakuwa wanavunja Shahaadah hii?
13- Je, ni katika athari zake nzuri kuhuisha Bid´ah kama ya Maulidi na mfano
wake?
14- Je, ni katika athari zake nzuri kusema kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi
wa sallam) anahudhuria sherehe zao na kuwabariki na kuwasamehe madhambi
yao?
15- Je, ni katika athari zake nzuri alivokuwa amekolea katika Suufiyyah,
kuipenda na kuwaunga kwake mkono?
16- Je, ni katika athari zake nzuri kuukomeka Uislamu kwenye nukta ishirini na
kufanya hayo ni Shari´ah kwa wafuasi wake?
17- Je, ni katika athari zake nzuri kufanya bay´ah kuwa na masharti kumi
yanayokosa msingi katika Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume Wake (Swalla
Allaahu ´alayhi wa sallam)?
18- Je, ni katika athari zake nzuri pindi alipofanya utiifu kuwa ni moja katika
sharti na kusema:
"Ninachokusudia kwa utiifu ni kujisalimisha na maamrisho na kuyatekeleza
kwa khiyari katika kipindi kizito na chepesi. Hilo ni kwa sababu ngazi za
Da´wah hii ni tatu... Ngazi ya pili ni ya malezi. Hapa ndipo kulipo muundo wa
Da´wah kutokana na Suufiyyah iliosafi inapokuja katika kiroho na kijeshi
inapokuja katika kuitendea kazi."?5 5 Majmuu´-ur-Rasaa-il/at-Ta´aaliym, uk. 268.
ar-Radd al-Jawaab
Ahmad an-Najmiy
18
www.firqatunnajia.com
Pamoja na kwamba ni wajibu kumsikiliza na kumtii mtawala pale
kunapotimizwa masharti mawili:
1. Kitendo kiwe kinajuzu. Hakuna utiifu katika kumuasi Allaah.
2. Mja awe anaweza kitendo hicho.
19- Je, ni katika athari zake nzuri kuhudhuria kaburi la Zaynab katika mnasaba
wa mwaka mpya wa Kiislamu bila ya kutaja shirki hata moja iliyopo hapo? Bali
uhakika wa mambo ni kwamba alikuwa akiwaamrisha wahudhuriaji kujisafisha
wao wenyewe na nafsi zao kutokamana na chuki na nia mbaya.
20- Je, ni katika athari zake nzuri kuwaacha manaswara wa Misri kuingia katika
shirika lake na kuinusuru Da´wah yake? Kuna yeyote katika wanaolingania
katika dini ya Allaah alofanya kitu kama hicho?
21- Je, ni katika athari zake nzuri kufanya sherehe kwa ajili ya Muhammad
´Uthmaan al-Marghaniy ambaye alikuwa anajulikana kuamini Wahdat-ul-
Wujuud? Amemsifu na kusema kwenye sherehe hiyo:
"Sisi, al-Ikhwaan, tuna mapenzi masafi na heshima kubwa kwa kiongozi
Marghaniyyah."
22- Je, ni katika athari zake nzuri kwenda katika sherehe ya usiku tarehe moja
Rabiy´-ul-Awwaal na kubaki huko mpaka tarehe kumi na mbili na kuimba kwa
nyimbo zilizo na shirki kubwa:
"Ee Allaah, swalia nuru (yaani Mtume) Ulioifanya kuja kwa walimwengu na
inayoangazia kwa jua na mwezi. Mpenzi huyu (yaani Mtume) amehudhuria
pamoja na wapenzi wake na amemsamehe kila mmoja kwa yaliyopitika."
23- Je, ni katika athari zake nzuri kutembea kwake masaa matatu kwenda na
kurudi kutembelea makaburi ya waonaji kutoka Hassaafiyyah na Shaadhiliyyah?
ar-Radd al-Jawaab
Ahmad an-Najmiy
19
www.firqatunnajia.com
Endapo kuna ambaye atasema kuwa matembezi yake yalikuwa ya Sunnah, hivyo
nitasema kuwa haijuzu kusafiri kuyaendea makaburi.
24- Je, ni katika athari zake nzuri kuimba nyimbo zilizo na Wahdat-ul-Wujuud
wazi wazi:
"Ee Allaah! Sema na uache uwepo na yale yaliyomo. Ikiwa umeelewa, basi
utaona kuwa hakuna aliyepo isipokuwa Allaah, si maalum wala jumla."?
25- Je, ni katika athari zake nzuri kuonelea kuwa kutawassul kupitia jaha ya watu
wema, ambayo ndio moja ya sababu kubwa ya shirki, ni jambo dogo tu ambalo
halitakiwi kutiliwa umuhimu kiasi hicho?
Ee Shaykh! Ninakuuliza kama mambo haya yanaafikiana na dini au hapana?
Heshima ya Hasan al-Bannaa ina umuhimu mkubwa wa kulindwa kuliko dini?
Mtu mwenye kuwabainishia watu haki na kutetea ´Aqiydah anazingatiwa kuwa
ni mkoseaji na alofanya jarima? Anastahiki kukatazwa na kulaumiwa na
kutoshauriwa kuchapisha kitabu?
ar-Radd al-Jawaab
Ahmad an-Najmiy
20
www.firqatunnajia.com
Ahmad an-Najmiy anamjibu Ibn Jibriyn 5
Umeandika kwenye barua yako:
"Walichunguza kisa chake na kumpa udhuru kwa makosa aliyotumbukiaemo."
1- Ni makosa yepi anayotakiwa kupewa udhuru? Si ni makosa madogo madogo
yanayotokamana na Ijtihaad? Je, makosa ya al-Bannaa ni mdogo ili aweze
kupewa udhuru? Je, al-Bannaa alikuwa ni Mujtahid mwenye haki juu ya hilo? Ni
wanachuoni wepi alisoma elimu ya Kishari´ah kwao?
2- Wanachuoni wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wamekubaliana juu ya kwamba
hakuna kupewa udhuru katika makosa ya ki-´Aqiydah. Vitabu visivyoweza
kuheasabika ambavyo ambavyo vimewaraddi watu wa Bid´ah, kuanzia wakati
wa Taabi´uun mpaka hii leo, vinatolea ushahidi juu ya hilo.
3- Mashaykh uliyowataja ni katika Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Lau wangelijua
kuwa al-Bannaa alikosea katika mambo ya kimsingi na ´Aqiydah, basi
wasingelimpa udhuru.
4- Kusema ya kwamba walimpa udhuru haya ni madai yako tu. Kama una
linalothibitisha hilo, basi onyesha. Hili unaweza kulikwepa kwa [kuleta] wale
ambao wameshafariki. Ama Shaykh ´Abdul-´Aziyz, yupo na unajulikana
msimamo wake juu ya watu hawa. Yeye ndio kiongozi na kiigizo chetu. Tunajua
kuwa anaraddi kila kosa analosikia na kulijua pasina kujali linatoka kwa nani.
Anaraddi hata kwa kosa katika mambo madogo madogo. Ameraddi makosa
yasiyohesabika. Ninaweza kumwandikia na kumuuliza kama ni kweli kwamba
fulani anadai kuwa unampa udhuru Hasan al-Bannaa kwenye makosa ya ki-
´Aqiydah.
5- Lau tutachukulia kuwa ni kweli kuna mwanachuoni anayempa udhuru
kwenye makosa yake ya ki-´Aqiydah, basi udhuru wake unazingatiwa kuwa ni
wenye kwenda kinyume na mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah.
ar-Radd al-Jawaab
Ahmad an-Najmiy
21
www.firqatunnajia.com
6- Anayempa udhuru anasema kuwa mtu asimraddi? Ikiwa anaema hivo, basi
amewasaidia watu wa Bid´ah wenye kueneza ufisadi katika ardhi.
ar-Radd al-Jawaab
Ahmad an-Najmiy
22
www.firqatunnajia.com
Ahmad an-Najmiy anamjibu Ibn Jibriyn 6
Unasema kwenye barua yako:
"Walikuta maneno yake yanaashiria kuwa alikuwa ni mtu mwenye Ikhlaasw na
mpwekeshaji."
Kusema kuwa alikuwa na Ikhlaasw au hapana hili ni jambo analojijua Allaah peke
yake. Ikhlaasw ni kitendo kilichojificha na hakuna akijuae isipokuwa Allaah
Pekee. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema katika Hadiyth
Swahiyh:
"Hakika ya kila kitendo kinategemea na nia na kila mtu atalipwa kwa kile
alichonuia."
Abu Muusaa amepokea ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)
amesema:
"Yule mwenye kupigana ili neno la Allaah liweze kuwa juu, huyo ndiye
anapigana katika njia ya Allaah."
Ahmad amepokea kupitia Ibn Mas´uud ambaye ameeleza kuwa Mtume (Swalla
Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
"Allaah ndiye mwenye kujua zaidi ni nia ipi alokuwa nayo yule mwenye
kuuliwa kati ya safu mbili."
Vilevile umesema:
"... alikuwa mpwekeshaji."
Huu ni ushuhuda na mapendekezo yako ambayo Allaah atakuja kukuuliza juu
yake. Ilikuwa ni wajibu kwako kujifikiria kabla ya kuzungumza namna hiyo.
Hivi kweli umetia mapendekezo haya nafasi inayostahiki? Mimi sielewi kama
wewe hutambui kuwa al-Bannaa alitumbukia kwenye shirki na kwamba alikuwa
ar-Radd al-Jawaab
Ahmad an-Najmiy
23
www.firqatunnajia.com
na anasa na washirikina na shirki zao na kuwachagua kuwa wanachama katika
mfumo wake. Pamoja na yote hayo alikuwa akisema kwenye sherehe ya mazalio
ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
"Mpenzi huyu (yaani Mtume) amedhuhuria pamoja na wapenzi wake na
amemsamehe kila mmoja kwa yaliyopitika."
Bi maana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anahudhuria sherehe zao
na kuwabariki na kuwasamehe madhambi yao. Ee Shaykh! Hii ni shirki au
hapana? Mtu anayezungumza na kuimba hivi ni mpwekeshaji? Mtu mwenye
kuahidi kiapo cha utiifu na usikivu Hassaafiyyah na Shaadhiliyyah anahesabika
kuwa ni mpwekeshaji? Je, unajua kuwa Suufiyyah ni wapwekeshaji na
wanalingania katika Tawhiyd au ni washirikina na wanalingania katika shirki na
Bid´ah? Unajua kuwa Suufiyyah imejengwa juu ya shirki na imechanganyika na
shirki na Bid´ah? Unajua kuwa Hasan al-Bannaa alikuwa akienda kila Ijumaa
kilomita 20 kwenye makaburi ya waonaji wa Suufiyyah, kama ad-Dasuuqiy na
Sanjar, na kilomita 20 kurudi? Mpwekeshaji hufanya hivo?
Ee Shaykh! Mche Allaah na tambua kuwa umeisononesha Tawhiyd yako na
kuitukana Shahaadah yako kwa kusema kuwa washirikina na watu wa Bid´ah ni
wapwekeshaji. Tubu kwa Allaah na urejee Kwake kabla haijachelewa.
Mtu aliyekuwa akilingania katika Uislamu na akimpwekesha Allaah ilikuwa ni
Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) na wale waliopita
katika njia yake miongoni mwa wanachuoni na viongozi katika wakati wake na
wakati wa Muhammad bin Su´uud mpaka hii leo.
Mtu aliyekuwa akilingania katika Uislamu na akimpwekesha Allaah ilikuwa ni
Shaykh ´Abdullaah bin Muhammad al-Qar´aawiy aliyeeneza Tawhiyd kusini
kwa msaada wa mfalme ´Abdul-´Aziyz.
ar-Radd al-Jawaab
Ahmad an-Najmiy
24
www.firqatunnajia.com
Ee Shaykh! Ninakuuliza kwa jina la Allaah; lau muulizaji angelikuuliza juu ya
mtu mwenye kwenda kuanzia tarehe moja Rabiy´-ul-Awwaal mpaka tarehe
kumi na mbili na kuimba kwa nyimbo zilizo na yafuatayo:
"Mpenzi huyu (yaani Mtume) amehudhuria pamoja na wapenzi wake na
amemsamehe kila mmoja kwa yaliyopitika."
Ungelimhukumu kwa shirki au Tawhiyd6? Ungelijibu nini?
Vipi ungelijibu lau ungeliulizwa juu ya mtu mwenye kutembea kilomita 20 kwa
wiki ili kutembelea makaburi ya Suufiyyah na kimomita 20 kurudi? Je,
ungelisema kuwa ni Sunniy au ni mtu wa Bid´ah? Je, ungelisema kuwa ni
mpwekeshaji au ni mshirikina7?
Ee Shaykh! Mche Allaah na rejea katika usawa. Tubu kwa Allaah kwani hakika
anaikubali Tawbah. Usiwapoteze watu, na khaswa wanafunzi, kwa kuwatetea
watu wa Bid´ah.
6 Sisemi kuwa Hasan al-Bannaa alikufa akiwa kafiri kwa vile sijui alivokufa. Hata hivyo ninasema kuwa
haijuzu kumsifu kuwa ni Muwahhid - mtu mwenye kumuabudu Allaah Pekee [mpwekeshahi] - wakati
imepothibiti kuwa alitumbukia kwenye yale yaliyopokelewa kutoka kwa wafuasi na wanusuraji wake.
7 Hapa ninahukumu maneno, au kitendo, yanayotoka kwa mtu huyu na ambayo yamethibitishwa kuwa
ni shirki kubwa. Ama kuhusu mtu huyu kwa dhati yake, sionelei kuwa ni kafiri kutokana na shirki yake
kwa vile sijui alikufa kwa hali gani.
ar-Radd al-Jawaab
Ahmad an-Najmiy
25
www.firqatunnajia.com
Ahmad an-Najmiy anamjibu Ibn Jibriyn 7
Unasema kwenye barua yako:
"Allaah Amewanufaisha na Kuwaongoza wengi kupitia yeye."
Wamenufaishwa kivipi? Je, ni manufaa kuwa na anasa na shirki kubwa na
kuwanyamazia watu wa Bid´ah na makhurafi?
Je, ni manufaa kutokataza maovu na badala yake kutendea kazi kanuni iliyounda
Hasan al-Bannaa:
"Twashirikiana kwa yale tunayoafikiana na kupeana udhuru kati yetu kwa yale
tunayotofautiana."
Je, ni manufaa kuita katika khilaafah na kuacha kulingania katika Tawhiyd
ambayo ndio njia ya Mitume?
Je, ni manufaa kuita katika mapinduzi ya nchi zilizoko sasa hata kama kutakuwa
nchi za Kiislamu zinazohukumu kwa Shari´ah ya Allaah na kusimamisha adhabu
ya Kiislamu?
Da´wah ya al-Ikhwaan al-Muslimuun imewaharibu vijana na haikuwanufaisha
lolote na kuwafisidi pasina kuwaboresha.
ar-Radd al-Jawaab
Ahmad an-Najmiy
26
www.firqatunnajia.com
Ahmad an-Najmiy anamjibu Ibn Jibriyn 8
Unasema kwenye barua yako:
"Nyakati zote anasifiwa katika vikao na vitabu vyake vinasomwa."
Je, hii ni hoja kwa mimi kusifu mfumo wake? Je, hii ni hoja kwa mtu anayemsifu
bila ya kujua makosa makubwa yanayopatikana kwenye mfumo wake? Hii sio
hoja ya kwamba mfumo wake ni sahihi. Wewe mwenyewe unajua ndani ya nafsi
yako kuwa hii sio hoja na kwamba wamemsifu pindi walipokuwa
wamedanganyika na muonekano wa kijumla wa mfumo wake. Wakati walipojua
yalio nayo, wakaukemea kwa haki zote.
Ee Allaah! Hakika wewe unajua kuwa sikusudii kumjeruhi wala kumtukana
yeyote. Ninacholenga tu ni kubainisha haki na kuwatahadharisha vijana juu ya
mifumo ilio na Bid´ah na upotevu. Tunawazindua tu juu ya makosa yaliyo
kwenye mifumo ili wasije kudanganyika nayo na wakajiunga nao na matokeo
yake wakaja kupotea wao na wakawapoteza wengine.
Kuhusiana na kwamba wamempokonya haki yake, sio sahihi kabisa. Wao
wamesema tu yaliyopokelewa kutoka kwake kutoka kwenye vyanzo sahihi,
majina ya vitabu vyake na namba za kurasa. Je, wamempokonya haki yake pindi
waliponukuu maneno hayo ili kuwakinaisha vijana ya kwamba huo ni mfumo
wa kimakosa kwa sababu uko na haki na batili? Wewe mwenyewe utapendelea
kunywa nini lau uko na kinywaji kilichochanganyika na uchafu na kinywaji
kingine ni kisafi na hakina uchafu? Hivyo watakuwa wamempokonya haki yake?
Lengo la kuumbwa mbingu, ardhi na kutumwa Mitume na kuteremshwa vitabu
ni ili kuhakikisha haki na kuivunja batili. Hali kadhalika kuamrisha mema na
kukataza maovu. Ikiwa juu ya ardhi hakuna yeyote mwenye kuamrisha mema na
kukataza maovu, hakika kuna ghadhabu. Kukiwepo ghadhabu, basi adhabu ya
Allaah ndio itashuka. Allaah (Ta´ala) Amesema:
ar-Radd al-Jawaab
Ahmad an-Najmiy
27
www.firqatunnajia.com
م أ خر جن ا ع ل يهم الق ول و ق ع و إذ ا انوا الن اس أ ن تك لمهم ال رض من د اب ة ل تن ا ك يوقنون ل بي
"Na itakapowaangukia kauli [kwa uwazi wake] Tutawatolea mnyama atembeaye katika ardhi atakayewasemezesha [aseme] kwamba watu walikuwa hawana yakini na alama Zetu."8
Qataadah amesema:
"Itapowaangukia kauli maana yake watapofikwa na ghadhabu."
Ibn ´Umar na Abu Sa´iyd al-Khudriy wamesema:
"Pale ambapo hawatoamrishana mema na kukatazana maovu, basi ghadhabu
itawawajibikia."
´Abdullaah bin Mas´uud amesema:
"Wataangukiwa na kauli kwa kufa kwa wanachuoni, elimu kupotea na Qur-aan
kunyanyuliwa."
Hili linapata kubainisha ya kwamba kuamrisha mema na kukataza maovu ni
kinga dhidi ya kuteremka kwa adhabu na ghadhabu za Allaah (´Azza wa Jalla)
juu ya waja Wake.
Miongoni mwa kuamrisha mema na kukataza maovu ni pamoja na kuraddi
makosa ya ki-´Aqiydah pasina kujali ni ya nani. Je, wataka watu wa Haki
wanyamazie hilo pasina kulibainisha na kulichuja na uchafu na yasiyostahiki?
Hili kamwe - Allaah Akitaka - halitopitika maadamu Hadiyth na haki ina
wanaume wake.
8 27:82
ar-Radd al-Jawaab
Ahmad an-Najmiy
28
www.firqatunnajia.com
ar-Radd al-Jawaab
Ahmad an-Najmiy
29
www.firqatunnajia.com
Ahmad an-Najmiy anamjibu Ibn Jibriyn 9
Umeandika kwenye barua yako:
"Kuna vitabu vinavyojulikana ambavyo ni vibaya zaidi kuliko vitabu vyake.
Kuna walinganizi, walio hai maiti, waliopinda zaidi kuliko yeye."
Himdi zote ni za Allaah ambaye amekufanya ukatamka haki pasina wewe
kutambua hilo. Umekubali mwenyewe kuwa kuna shari kwenye vitabu vyake na
upindaji kwenye mfumo wake. Maneno yako yameshabihiana na kujigonga kwa
Ahl-ul-Bid´ah. Hivyo basi, kuwa mwangalifu!
Pili ni wajibu kwa wanachuoni kuwabainishia watu haki kwa kadri na
wawezavyo.
Tatu mfumo huu umetutia kwenye mitihani kwenye majumba yetu. Umeharibu
akili za wana wetu. Wamekuwa tena hawamtambui baba yake, rafiki yake
mwenye kumjali na mwalimu wake mwenye kulea. Hawaamini nasaha za
wanasihiaji wala ukosoaji wa wakosoaji ikiwa mtu si kutoka kwenye kundi lao.
Wanafanana na wale ambao Allaah Amesema juu yao:
دين كم ت بع لم ن إل ت ؤمنوا و ل
“Na wala msimwamini isipokuwa yule anayefuata dini yenu."9
Watu hawa walisema:
"Msimwamini yeyote isipokuwa yule ambaye yuko katika pote lenu."
Hili liliwajibisha matahadharisho juu ya mfumo huu, muasisi wake na matawi
yake kama Suruuriyyah na Qutbiyyah. Hili limewajibisha ukhusishaji huu kwa
9 03:73
ar-Radd al-Jawaab
Ahmad an-Najmiy
30
www.firqatunnajia.com
vile mfumo huu umeenea katika mji wetu wote na kuharibu akili za vijana wetu.
Imewageuza kuwa wapinduaji Takfiyriyyuun na magaidi. Ndio maana sio ajabu
wanafunzi Salafiyyuun kukataza mfumo huu na kuonyesha makosa yake ili
kuhakikisha haki na kuwanasihi viumbe ili kujikurubisha kwa Allaah (Ta´ala) na
kupigana vita katika njia Yake:
ع م ل أ حس ن م ن أ جر نضيع ل إن الص ال ات و ع ملوا آم نوا ال ذين إن
"Hakika wale walioamini na wakatenda mema, hakika Sisi Hatupotezi ujira wa anayetenda ‘amali nzuri."10
10 18:30
ar-Radd al-Jawaab
Ahmad an-Najmiy
31
www.firqatunnajia.com
Ahmad an-Najmiy anamjibu Ibn Jibriyn 10
Unasema kwenye barua yako:
"Kuna vitabu vinavyojulikana ambavyo ni vibaya zaidi kuliko vitabu vyake.
Kuna walinganizi, walio hai maiti, waliopinda zaidi kuliko yeye."
Nimeshakubainishia sababu ya yote hayo na kwamba Salafiyyuun
hawakunyamazia batili na himdi zote ni Zake Allaah. Siku zote wameraddi
makundi ya batili kadri na wanavoweza.
Leo ni khaswa Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz ambaye amefanya
hivo. Baada ya hapo ni baraza na Kibaar-ul-´Ulamaa´. Yule mwenye kupitia
kurasa za Fataawaa za Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Baaz, basi ataona ni Ruduud
ngapi alizowapiga watu wa batili. Hali kadhalika baraza la Kibaar-ul-´Ulamaa´.
Maneno yako "Lakini tokea miaka saba ya nyuma ndugu wengi
wamemshambulia na kumpokonya haki yake. Haieleweki kabisa. Kuna vitabu
vinavyojulikana ambavyo ni vibaya zaidi kuliko vitabu vyake. Kuna walinganizi,
walio hai maiti, waliopinda zaidi kuliko yeye" haina maana hakuwaraddi. Haya
ni maneno yasiyostahiki. Wanachuoni hawahoji namna hii. Hoja zao kwa yale
wanayoyathibitisha na kupinga yale wanayopinga inakuwa kwa Qur-aan na
Sunnah kwa ufahamu wa Salaf.
Ee ndugu mpendwa! Ikiwa unaona kuwa ni mashambulizi kwa Hasan al-Bannaa
na mfumo wake na wafuasi wake mtu akimraddi na wafuasi wake wanaotendea
kazi Suufiyyah na shirki na kuzusha Bid´ah na kuweka katika Shari´ah mambo
ambayo hayakuweka Allaah katika Kitabu Chake wala Mtume Wake (Swalla
Allaahu ´alayhi wa sallam) kwenye Sunnah zake, hatuwezi kukuongoza. Pamoja
na hivyo tunatakiwa kukwombea kwa Allaah (´Azza wa Jalla) akuondoshe
kwenye fikira yako hii ya ajabu na ufahamu wako wenye kubabaisha ambao
umekufanya ukachanganya mambo. Wakati huo huo tunachelea fikira hizi
kukufanya ukaingia ndani ya Aayah:
ar-Radd al-Jawaab
Ahmad an-Najmiy
32
www.firqatunnajia.com
بيل غ ي ر و ي ت بع الد ى ل ه ت ب ي م ا ب عد من الر سول يش اقق و م ن ن م و نصله ت و ل م ا ن و له المؤمني س م صري ا و س اء ت ج ه
"Na atakayempinga Mtume baada ya kuwa umeshambainikia uongofu na akaifuata njia isiyokuwa ya Waumini, Tutamgeuza alikogeukia na [baada ya hapo] Tutamuingiza [Moto wa] Jahannam - Na uovu ulioje marudio ya mwisho!"11
Utambue kwamba kuwa na mapenzi na kuwatetea watu wa batili sio katika njia
ya waumini sawa ikiwa ni washirikina au watu wa Bid´ah waliotoka katika
Uislamu au ambao hawakutoka. Ninakunasihi, ee ndugu yangu, na kumuomba
Allaah Akurejeshe katika haki na kuinusuru. Tunamuomba Allaah Akupe umaizi
na akuondoshee pazia.
Hii ni nasaha yangu kwako. Ni nasaha vilevile kwa kila mtu Salafiy anayekutakia
kheri na kuchelea juu yako fikira zako hizi za ajabu na ufahamu wenye
kubabaisha.
11 04:115
ar-Radd al-Jawaab
Ahmad an-Najmiy
33
www.firqatunnajia.com
Ahmad an-Najmiy anamjibu Ibn Jibriyn 11
Umesema kwenye barua yako:
"Hivyo basi, mimi ninakunasihi, ee Shaykh, kuchunga ulimi wako na
kumzungumza vibaya mtu huyu ambaye Allaah Amenufisha kupitia kwake."
Hii ni nasaha nzuri lau ingeliweka mahala pake stahiki. Ni zawadi yenye
thamani kwa yule anayetaka kuihifadhi dini yake. Lakini unaninasihi nisitoe
nasaha. Je, hii ni nasaha? Hii ni njia ya kurudisha kheri na kukimbiza katika njia
ya Allaah.
Mche Allaah, ee Shaykh ´Abdullaah, na rejea katika haki. Ninaapa kwa Allaah ya
kwamba sina chembe ya shaka kwa niliyofanya. Bali uhakika wa mambo
naonelea kuwa ni wajibu wangu. Ninajua mengi ya kutosha juu ya mtu huyu na
mfumo wake ili inistahikie kuwanasihi wengine na kubainisha ni makosa yepi
yanayopatikana katika mfumo huu. Ninafanya hivo ikiwa ni nasaha kwa
wanafunzi walodanganyika nao na ili kutekeleza haki ya Allaah kutetea Uislamu
na Tawhiyd kama ambavo alivofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
Ni kipi kilicho na haki zaidi kutetewa? Tawhiyd na ´Aqiydah sahihi, ´Aqiydah ya
Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah, au heshima ya Hasan al-Bannaa. Allaah
Hakuamrisha kuwapiga vita washirikina na makafiri kwa ajili ya ´Aqiydah
sahihi? Allaah (Ta´ala) Amesema:
ن ة ت كون ل ح ت و ق اتلوهم ين و ي كون فت لل ه الد
"Na piganeni nao mpaka kusiweko fitina na Dini iwe kwa ajili ya Allaah Pekee."12
12 02:193
ar-Radd al-Jawaab
Ahmad an-Najmiy
34
www.firqatunnajia.com
Fitina imefasiriwa kuwa ni shirki. Allaah hakuhalalisha kuchukua uhai wa
makafiri na wanawake na watoto wao kuwafanya watumwa na mali zao
kuzifanya ni ngawira kwa waislamu kwa ajili ya ´Aqiydah?
Je, haki ya mtu imeharamishwa kuvunjwa akifanya shirki kubwa na kukubaliana
na matendo yao na akazusha katika dini Bid´ah na akaweka Shari´ah mambo
yasokuwepo? Imeharamishwa kuvunjwa ikiwa mtu anataka kuwabainshia watu
waliodanganywa na mtu huyu haki na mfumo wake?
Ninaapa kwa Allaah ya kwamba wajibu nilio nao mimi, wewe na wanafunzi
wengine wote, ni kuinusuru dini kutangulizwe juu ya mambo mengine yote
katika ardhi ili kumtii Allaah, kutimiza haki Yake, kuinusuru dini Yake na
kuihifadhi ´Aqiydah ya waislamu.
ar-Radd al-Jawaab
Ahmad an-Najmiy
35
www.firqatunnajia.com
Ahmad an-Najmiy anamjibu Ibn Jibriyn 12
Unasema kwenye barua yako:
"Usichapishe kitabu hiki ambacho kitakuja kukupa tetesi mbaya na kukufanya
kusema vibaya heshima ya ndugu yako Muislamu."
Mosi ninachukulia kuwa unawazuia watu na njia ya Allaah kwa kufanya hivi.
Ninazingatia kuwa kitabu hiki ni miongoni mwa vitabu vyangu bora kabisa.
Humo nimeinusuru haki na kuitetea Tawhiyd na ´Aqiydah ya Kiislamu. Ninataji
nimefanya hivo hali ya kuwa ni mwenye kumtakasia nia Allaah na nimetekeleza
haki Yake na kuitetea dini Yake. Hata hivyo sisemi kuwa mimi sina mapungufu
na makosa.
Pili ninaonelea kuwa kwa kufanya hivi unaiacha haki na kuwanusuru na
kuwasaidia watu wa batili. Inatosheleza kule tu kutangamana na dini na watu
wake kimakosa. Allaah Amesema juu ya watu hawa:
المسلمي من إن ن و ق ال ص ال ا و ع مل الل ه إل د ع ا م ن ق ول أ حس ن و م ن
"Na nani mwenye kauli nzuri zaidi kuliko yule anayelingania [watu] kwa Allaah na akatenda mema, na akasema: “Hakika mimi ni miongoni mwa Waislamu?"”13
Tatu nimesikia kuwa baadhi ya Hizbiyyuun wananunua vitabu vingi vikubwa
ambavyo vimetahadharisha mfumo wao kisha wanavichoma moto. Kuna tofauti
gani kati ya kuchoma kitabu baada ya kuwa kimeshachapishwa na kunasihi
kisichapishwe?
13 41:33
ar-Radd al-Jawaab
Ahmad an-Najmiy
36
www.firqatunnajia.com
Nne ninaonelea kuwa unajiingiza kwenye jambo lisilokuhusu ili kuzuia kheri.
Hadiyth tukufu inasema:
"Moja ya sifa nzuri za Muislamu ni kuachana na yale yasiyomuhusu.”
Tano kitabu kitachapishwa na kuenezwa ili kuthibitisha Tawhiyd na kukataza
shirki, kuthibitisha Sunnah na kukataza Bid´ah, kuthibitisha haki na kukataza
batili. Lililo la wajibu kwako badala yake unatakiwa kuharakisha kukichapa ili
kuinusuru Tawhiyd, Sunnah na haki. Pamoja na hivyo umefanya kinyume kabisa
na kuomba kisichapishwe. Kwa hivyo umewanusuru kidhuluma Ahl-ul-Bid´ah
na Hizbiyyah dhidi ya Ahl-ut-Tawhiyd was-Sunnah na wale wenye kuwafuata
Salaf. Mtake Allaah msamaha na utubie Kwake kabla haijachelewa. Hatokufaa
fulani wala fulani. Kitachokufaa ni kusimama kwa haki na kuinusuru na watu
wake.
Kuhusiana na kwamba unachelea kikichapishwa kukaeneza tetesi mbaya juu
yangu, basi utambue kuwa tetesi mbaya inakuwa kwa kuinusuru batili,
kuizungumza au kuitendea kazi. Namshukuru Allaah kuona sikufanya makosa
wala sikuwanusuru watu wa batili mpaka tetesi mbaya iweze kuenea kwa
waumini ambao ndio mashahidi wa Allaah juu ya ardhi. Pamoja na hivyo
nimetenda haki na kuinusuru haki na ninataraji thawabu kutoka kwa Allaah kwa
hilo. Ama kuhusu watu wa batili, sijali watavyoonelea.
Ninamuomba Allaah mtukufu, Mola wa ´Arshi kubwa, Anikinge na shari zao na
Alinde na kampeni zao. Nitachapisha kitabu na kukieneza - Allaah Akitaka na
ninamtegemea Allaah ambaye Yeye ndiye aliye na usimamizi kwa walimwengu
wote.
Swalah na salaam zimwendee Mtume wetu Muhammad, ahli zake na
Maswahabah zake
Ahmad bin Yahyaa Muhammad Shubayr an-Najmiy
ar-Radd al-Jawaab
Ahmad an-Najmiy
37
www.firqatunnajia.com
ar-Radd al-Jawaab
Ahmad an-Najmiy
38
www.firqatunnajia.com
´Allaamah al-Fawzaan kuhusu kitabu ambacho Ibn Jibriyn
alikuwa hataki kichapishwe
Kwa muheshimiwa Shaykh na ndugu mtukufu Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy -
Allaah amuhifadhi na ampe mafanikio. Aamiyn.
as-Salaam ´alaykum wa Rahmatullaahi wa Barakaatuh
Ama ba´d:
Nimesoma kitabu chako chenye thamani "al-Mawrid al-´Adhb az-Zulaal" na
kuona kuwa ni chenye thamani na faida. Ni kitabu muhimu sana kwa leo
ambapo kuna makundi na mapote mengi ambayo kwa masikitiko makubwa
yanajinasibisha na Da´wah ya Uislamu. Hata hivyo ni jambo lenye kujulikana ya
kwamba katika Uislamu kuna kundi na mfumo mmoja tu.
Kundi lenyewe ni la Ahl-us-Sunnah na mfumo ni wa Mtume (Swalla Allaahu
´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake. Namna hiyo ndivyo alivowasifu
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pindi alipotaja makundi na mapote
yenye kwenda kinyume:
"Ni wale wenye kufuata yale niliyomo mimi hii leo na Maswahabah zangu."
Sisi hatuna isipokuwa kundi limoja ambalo ni kundi la Ahl-us-Sunnah wal-
Jamaa´ah, mfumo mmoja ambao ni mfumo wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi
wa sallam) na Imaam mmoja ambaye ni Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu
´alayhi wa sallam). Hatuyatambui makundi mengine yote, mifumo na kiongozi.
ar-Radd al-Jawaab
Ahmad an-Najmiy
39
www.firqatunnajia.com
Kitabu chenu - Allaah akuhifadhi - ni chenye kutosheleza kwa kubainisha haki
na kuraddi batili katika maudhui haya14. Allaah akujaze kheri kwa kazi nzuri
ulioifanya ya kuweka haki wazi na kuraddi batili.
Swalah na salaam zimwendee Mtume wetu Muhammad, ahli zake na
Maswahabah zake.
Ndugu yenu katika Uislamu: Swaalih bin Fawzaan bin ´Abdillaah al-Fawzaan
1414/11/2715
14 Miongoni mwa kubanisha haki na kuraddi batili katika kitabu hiki ni pamoja vilevile na Radd ya
´Allaamah an-Najmiy kwa ´Aa´idh al-Qarniy, Hasan al-Bannaa, Qutbiyyah na al-Ikhwaan al-Muslimuun.
15 al-Mawrid al-´Adhb az-Zulaal, uk. 14-15