ANNUUR 1183.pdf

20
ISSN 0856 - 3861 Na. 1183 RAMADHAN 1436, IJUMAA , JUNI 126-JULAI 2, 2015 BEI TShs 800/=, Kshs 50/= Sauti ya Waislamu www.annuurpapers.co.tz au facebook:[email protected] AHLU SUNNA WAL JAMAA HAJJ AND UMRA TRUST Kijana Usamah Abdullah Rahim... Amiminiwa risasi na Polisi, afariki Apachikwa ugaidi kwa kukutwa na kisu 'John' auwa watu 9 kwa risasi wakisali Aambiwa labda alikosea tu. Sio gaidi Kamishna Magereza ashikilia uhai wa Sheikh Hajatoa uamuzi ‘Sheikh’ akatibiwe au la Bassaleh, Kilemile wataka haki itendeke Na Bakari Mwakangwale Hali si shwari Zanzibar Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha. Soma Uk. 8. Maalim Seif Sharif Hamad. WAKATI mtuhumiwa wa kesi ya ugaidi Said Amour, akishindwa kufika Mahakamani kutokana na maradhi gerezani, juhudi za kupata kibali kwa ajili ya matibabu yake zimekuwa kitendawili. Imeelezwa kuwa tangu kuwasilishwa kwa ombi la kupatiwa kibali kwa ajili ya mtuhumiwa huyo kutibiwa pia wameshindwa kufika Mahakama ya Kisutu, wiki iliyopita, kutokana na kuwa wagonjwa. “Mshitakiwa namba 12 Said Amour, ni muda sasa hajahudhuria Mahakamani Inaendelea Uk. 2 KAMISHNA Mkuu wa Magereza Jonh Casmir Minja. katika hospitali maalum, ni mwezi sasa kibali hicho hakijatolewa. Mbali na mtuhumiwa huyo, imedaiwa kuwa watuhumiwa wengine wawili ambao ni mshitakiwa namba 16 Alawi Othman Amir na mshitakiwa namba 18 Amiri Hamisi Juma, Usamah Abdullah Rahim Mtume(saw) aliwahimiza Masahaba kuwahijia wenzao wasioweza kwa ugonjwa au uzee na waliokufa katika Uislamu. Waislamu wengi wanakufa bila kuhiji wakati waliwahi kupata uwezo wa kuhiji. Umeshawaokoa wazazi wako na MOTO? Muda unakwisha! Gharama zote kwa Hijja ni Dola 4,500. Umra ya Ramadhani ni Dola 2,300. Karibuni Ahlu Sunna Wal Jamaa kwa huduma nzuri na uongozi bora. Wasiliana nasi: Tanzania Bara: 0765462022;0782804480; 0717224437. Zanzibar:0777468018;0777458075;0777845010. (14) WASITIRI WAZAZI WAKO! Seif akataliwa kuingia Barazani Tuhuma nzito kwa Jecha, ZEC CUF wampa orodha ya ‘maluki’

Transcript of ANNUUR 1183.pdf

  • ISSN 0856 - 3861 Na. 1183 RAMADHAN 1436, IJUMAA , JUNI 126-JULAI 2, 2015 BEI TShs 800/=, Kshs 50/=

    Sauti ya Waislamuwww.annuurpapers.co.tz au facebook:[email protected]

    AHLU SUNNA WAL JAMAA HAJJ AND UMRA TRUST

    Kijana Usamah Abdullah Rahim...

    Amiminiwa risasi na Polisi, afarikiApachikwa ugaidi kwa kukutwa na kisu'John' auwa watu 9 kwa risasi wakisaliAambiwa labda alikosea tu. Sio gaidi

    Kamishna Magereza ashikilia uhai wa SheikhHajatoa uamuzi Sheikh akatibiwe au laBassaleh, Kilemile wataka haki itendeke

    Na Bakari Mwakangwale

    Hali si shwari Zanzibar

    Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha. Soma Uk. 8. Maalim Seif Sharif Hamad.

    WA K AT I m t u h u m i w a wa kesi ya ugaidi Said Amour, akishindwa kufika Mahakamani kutokana na maradhi gerezani, juhudi za kupata kibali kwa ajili ya matibabu yake zimekuwa kitendawili.

    Imeelezwa kuwa tangu kuwasilishwa kwa ombi la kupatiwa kibali kwa ajili ya mtuhumiwa huyo kutibiwa

    pia wameshindwa kufika Mahakama ya Kisutu, wiki iliyopita, kutokana na kuwa wagonjwa.

    Mshitakiwa namba 12 Said Amour, ni muda sasa hajahudhuria Mahakamani

    Inaendelea Uk. 2

    KAMISHNA Mkuu wa Magereza Jonh Casmir Minja.

    katika hospitali maalum, ni mwezi sasa kibali hicho hakijatolewa.

    Mbali na mtuhumiwa huyo, imedaiwa kuwa watuhumiwa wengine wawili ambao ni mshitakiwa namba 16 Alawi Othman Amir na mshitakiwa namba 18 Amiri Hamisi Juma,

    Usamah Abdullah Rahim

    Mtume(saw) aliwahimiza Masahaba kuwahijia wenzao wasioweza kwa ugonjwa au uzee na waliokufa katika Uislamu. Waislamu wengi wanakufa bila kuhiji wakati waliwahi kupata uwezo wa kuhiji. Umeshawaokoa wazazi wako na MOTO? Muda unakwisha! Gharama zote kwa Hijja ni Dola 4,500. Umra ya Ramadhani ni Dola 2,300. Karibuni Ahlu Sunna Wal Jamaa kwa huduma nzuri na uongozi bora. Wasiliana nasi: Tanzania Bara: 0765462022;0782804480; 0717224437.Zanzibar:0777468018;0777458075;0777845010.

    (14) WASITIRI WAZAZI WAKO!

    Seif akataliwa kuingia Barazani Tuhuma nzito kwa Jecha, ZEC CUF wampa orodha ya maluki

  • 2 AN-NUURRAMADHAN 1436, IJUMAA JUNI 26- Julai 2, 2015AN-NUUR

    S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM.

    www.annuurpapers.co.tz E-mail: [email protected] zetu zipo: Manzese Tip Top

    Usangi House, barabara ya Morogoro, D'Salaam

    Tahariri/Habari

    A M E S E M A k w e l i Mtume (s .a .w) : Lai t i watu wangeaminiwa kwa madai yao tu, kuna watu wangedai damu na mali za wengine.

    Basi na iwe juu ya mwenye kudai, kuleta ushahidi wa madai yake.

    Kanuni hii ya Uislamu, ndiyo inayojenga msingi w a m w e n e n d o w a mashitaka na kesi katika mahakama, katika nchi nyingi zinazoongozwa kwa misingi ya Utawala Bora, Haki na Sheria.

    Kuwa mtu atakuwa hana hatia mpaka atakapotiwa hatiani na vyombo vya kisheria vinavyohusika na kutambulika.

    Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, i n a m t u h u m u S h e i k h Msellem Ali na wenzake kadhaa kuwa ni magaidi.

    N i m wa k a wa p i l i sasa, serikali haijafikisha u s h a h i d i w a k e mahakamani kuthibitisha madai yake.

    Hata hivyo, kwa kipindi chote hicho, watuhumiwa wameendelea kuteseka gerezani huku familia zao nazo zikiishi katika tabu kwa kukosa wasimamizi na watafuta Rizki wakuu wa familia.

    Hii ni dhulma ya wazi kwa misingi ya Kiislamu, Utawala Bora, uadilifu na UBINADAMU kwa ujumla.

    Ndio pale mafundisho ya Uislamu yakaagiza kuwa, yeyote mwenye kumtuhumu mtu, basi haraka alete ushahidi kuthibitisha madai yake.

    Na ikatolewa sababu kuwa kwa maumbi le yake mwanadamu, lau ataaminiwa tu kwa kila analosema, basi kuna watu watadai mpaka damu ya watu wengine kuwa ni mali na haki yao.

    Na ili kuepuka adhabu mbele ya Mwenyezi Mungu hiyo siku ya Hukumu, ambayo inaanzia mara tu baada ya kutiwa kaburini, Uislamu ukatoa angalizo

    Vigogo wa Serikali wafutarishe familia za Masheikh wa Uamsho

    na mwongozo muhimu sana:

    Kuwa, ni bora mtu ukosee umwachie huru (usimuadhibu) mtu mkosaji kwa kukosa ushahidi wa madhubuti, kuliko ufanye kosa la kumwadhibu mtu asiye na hatia.

    Na tunaambiwa Dua ya mwenye kudhulumiwa haina pazia baina yake na Mungu wake.

    Hivi wenye mamlaka na hasa walio Waislamu, a m b a o h i v i s a s a watakuwa katika Funga ya Ramadhani, wanajisikiaje wakitia nia ya funga na jioni wakifuturu huku wakijua kuwa kuna Waislamu wenzao wasio na hatia wapo ndani, wanafunga na kuftari kwa chakula cha gerezani wakati sio wafungwa!

    Wanakosa tarawehe na Qiyamul Lail katika misikiti yao. Wanakosa kuendesha darsa za Quran katika kipindi hiki cha Shahru Ramadhaan ladhii unzila fiihi lQuran!

    Ule ukarimu na huruma t u n a y o t a k i w a t u w e nayo wakati wa Funga ya Ramadhani, ipo wapi iwapo tunafutari kwa kila aina ya viliwa, vitafunwa na v inywewa, l ak in i haitupitikii kuwa kuna akina mama na watoto ambao huenda hawakupata cha kuftaria kwa sababu waume zao wapo ndani, sio kama wafungwa, lakini kwa tuhuma tu!

    Maadhali mwenzi wa Ramadhani umeanza, punde tu tutashuhudia wanasiasa wakipigana vikumbo kuandaa futari, kuanzia za Ikulu, Wakuu wa Mikoa, waliotangaza nia za Ubunge na Urais, mpaka za mitaani.

    Ni maoni yetu kuwa labda Masheikh wetu wa n g e wa e l i m i s h a n a kuwashauri viongozi wetu hawa na wale watarajiwa, kuwa badala ya kuandaa futari za kisiasa zisizo na tija mbele ya Mwenyezi

    Mungu (ila kwa tija ya hapa hapa duniani tu), wangepeleka huruma yao kwa akina mama, watoto na watu wazima wanaoteseka kwa vile waume zao na vijana wao wanaowategemea wapo ndani. Wapeleke futari zao za kisasia katika familia hizo.

    Wa l i o m a d a r a k a n i w a k i o n y e s h a m f a n o huo, hapana shaka na waliotangaza nia watafuata nyayo. Na hiyo itakuwa msaada mkubwa kwa familia za watuhumiwa hao, japo haitaondoa dhambi ya kuwafunga watu kwa tuhuma tu.

    K i d u n i a t u n a w e z a kujifariji kuwa tunafuata sheria (ya ugaidi), lakini kwa Mwenyezi Mungu, huo hautakuwa utetezi.

    Mwenyezi Mungu anajua siri zilizomo katika vifua vyetu mpaka sababu yenyewe ya kuwatuhumu huo ugaidi, kama ni tuhuma za kweli au la. Anajua pia nia ya hao wababe waliobuni vita dhidi ya ugaidi , wanavyopiga propaganda na namna sisi tulivyotoswa kuitumikia agenda hiyo (kwa malipo gani?)

    Ni juzi tu tumemzika Mzee wetu, Sheikh Issa Shaaban Simba, ambaye tunaambiwa katika moja ya usia wake aliagiza kuwa akifa azikwe haraka kama Uislamu unavyoagiza.

    Tunajua , kwa watu wema kaburi ni viwanja katika viwanja vya Peponi. Lakini kwa watu waovu, waliodhulumu nafsi zao, kaburi ni shimo katika

    mashimo ya Moto wa Jahannam.

    Wakati tukiwa tumo ndani ya Ibada hii kubwa ya Funga ya Ramadhani, ni vyema kila mmoja wetu akajihesabu ni kwa namna gani anafanya maandalizi, ili kaburi lake lije kuwa Bustani katika Bustani za Peponi.

    Lakin i p ia , n i kwa kiwango agani anajitahidi kuepuka yale ambayo y a t a h e s a b i k a k u w a ni dhulma, iwe ni ya k u wa f a n y i a we n g i n e au kuifanyia nafsi yake mwenyewe. Kwani hayo n d i o y a t a m f u n g u l i a milango ya Jahannam mara tu akiingia kaburini.

    Tu m w o m b e A l l a h atutakabalie Funga zetu na Ibada zetu kwa ujumla. Na atuepushe na kila aina ya dhulma.

    Mkuu Magereza ashikilia uhai wa Sheikh SaidInatoka Uk. 1kutokana na kusumbuliwa na maradhi, ambayo mpaka sasa hayajapatiwa tiba inayostahili akiwa humo gerezani.

    L a k i n i p i a k u n a washitakiwa namba 16 na 18 nao hawakufika Mahakamani kwani pia ni wagonjwa.

    A m e s e m a Wa k i l i wa watuhumiwa hao Abdul-fatah Abdallah.

    Akizungumzia suala la maombi ya kupatiwa kibali kwa ajili ya kupatiwa rufaa mtuhumiwa namba 12 kwa ajili ya matibabu, Katibu wa Kamati ya Maafa ya Shura ya Maimamu, Ustadhi Ally Mbaruku, alisema suala hilo limekwamia kwa Kamishna wa Magereza.

    A l i s e m a , k i l a wanapofuatilia wanapewa matumaini kwamba kibali kinashughulikiwa kulingana na taratibu za Magereza, hata hivyo alistaajibu kuona suala hilo linalohusu uhai wa mtu kupelekwa kwa kasi ndogo.

    Alisema, awali katika Ofisi hiyo ya Kamishna Mkuu wa Magereza, waliwasilisha maombi ya aina mbili, kwa nyakati tofauti likiwemo ombi la kupatiwa kibali cha kupeleka msaada katika gereza hi lo la Segerea, ambapo ombi hilo lishajibiwa na misaada imeshapelekwa.

    Alisema, maombi ya kibali cha matibabu ya Ust. Salumu, ndiyo yalitangulia ambapo yalipelekwa mwanzoni mwa mwezi wa tano, mwaka huu na maombi ya kibali cha kupeleka misaada kilipelekwa mwishoni mwa mwezi huo wa tano.

    Hatuelewi taratibu zao zikoje yaani maombi ya kibali cha matibabu ndio

    kilitangulia lakini mpaka sasa hakijatolewa na mtu anazidi kuathirika kiafya, lakini hiki cha kupeleka msaada kimetoka haraka wakati barua yake ilikwenda mwisho. Alisema mmoja wa wajumbe wa Kamati hiyo.

    Alisema, mara ya mwisho wal ie lezwa na maof i sa wa Ofisi ya Kamishna wa Magereza, kuwa wanasubiri ripoti kutoka kwa daktari wa Magereza ili wafahamishwe kuna wagonjwa wangapi, hata hivyo alisema hadhani kama hiyo ni hoja ya msingi, kwani suala la Ust. Salumu, lipo wazi na tatizo lake ni kubwa hata Mahakama, inalijua.

    Katika barua hiyo kwa Ofisi ya Kamishna Jenerali w a M a g e r e z a , y e n y e Kumbukumbu namba 009/KMS/2015, imeeleza hitajio la Kamati hiyo kupatiwa kibali mtuhumiwa huyo apewe rufaa, ili wampeleke katika hospitali yoyote kubwa.

    Kamati ya Maafa Shura ya Maimamu (T) kwa heshima kubwa kabisa tunaomba k iba l i i l i ndugu Sa id i , apatiwe rufaa katika hospitali yoyote kubwa kwa ajili ya uchunguzi na matibabu na kamati inachukua dhamana ya kul ip ia gharama za matibabu. Imesema sehemu ya barua hiyo.

    Barua hiyo inayoonesha kuwa ilipokelewa Mei 4, 2015, katika Ofisi hiyo ya Kamishna wa Magereza, imeainisha k u w a S a i d A m o u r n i mshitakiwa namba 12 katika kesi namba 29/2014, aliyepo katika gereza la Segerea, ambaye kwa muda mrefu anasumbuliwa na Korodani (Scrotal Swelling).

    Hali ambayo inazidi kuwa tete siku hadi siku, pia wanalalamika ya kuwa hawapatiwi matibabu ya kina.

    Imesema barua hiyo ya Mei 4, 2015, ambayo An nuur, inayo nakala yake iliyosainiwa na Katibu, Ally Mbaruku.

    Kamati ya Maafa, ilifikia hatua ya kuwasilisha ombi hilo kwa Kamishina wa Magereza, kufuatia watuhumiwa hao kulalamika mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Kisutu, Janet Kaluyenda, kuwa hawapati matibabu.

    Watuhumiwa hao mbele ya Mahakama hiyo, walikwenda mbali zaidi wakidai kuwa wananyimwa mat ibabu yanayostahi l i kutokana na Uislamu wao ambapo wa l i wa o m b a Wa i s l a m u kuwachangia i l i wapate matibabu.

    Waislamu wapo tayari kuwasaidia, ndio maana tulipeleka maombi haraka kwa Kamishna wa Magereza ili atoe kibali cha kuruhusu akatibiwe katika hospitali kubwa kwa gharama za Waislamu, lakini bado kuna ugumu ni mwezi sasa toka tupeleke maombi hayo kibali hakijatoka alisema Ust. Mbaruku.

    S a i d A m o u r , n i miongoni mwa Waislamu wanaotuhumiwa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa makosa ya ugaidi, ambao waliilalamikia Mahakama ya Kisutu kuwa walifanyiwa vitendo vya ukatili wakiwa mikoni mwa Jeshi la Polisi, huku yeye (Said Amour ) inadaiwa aliminywa sehemu za siri na kumsababishia uvimbe.

    Inaendelea Uk. 3

  • 3 AN-NUURRAMADHAN 1436, IJUMAA JUNI 26- Julai 2, 2015Habari

    Kumpachika Muislamu ukafiri ni ujingaHakuna dhana ya siasa kali katika UislamuWafafanua Sheikh Kilemile, Doga, BassalehKUMPACHIKA ukafiri Muislamu mwenzako, ni kielelezo cha ujinga na

    jambo lisilokubalika katika Uislamu.

    Aidha, Siasa kali au msimamo mkali, ni dhana ngeni katika Uislamu kwani Dini hii ya haki inasema wazi kuwa ni ya kati na kati, wema, uadilifu na upole.

    Hayo yamebainishwa k a t i k a K o n g a m a n o lililoandaliwa na Umoja wa Wanazuoni wa Tanzania ( H a y - a t - U l a m a a ) k wa kushir ikiana na Umoja wa Wanazuoni wa Afrika, ambalo lilifanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.

    Akizungumza kat ika kongamano hilo, Sheikh Amran Kilemile, alisema katika Uislamu hakuna kitu kinachoitwa Waislamu wenye Msimamo Mkali.

    Alisema, wamelazimika k u f a n y a K o n g a m a n o hilo kwa kuwashirikisha Wanazuoni wa Kiislamu kwa lengo la kutoa elimu kuhusu msamiati Msimamo mkali katika Uislamu na kwamba hakuna kitu kama hicho katika Uislamu, kwani Uislamu una miongozo yake na taratibu zake katika kuyaendea mambo yake.

    Kutokana na baadhi ya Wais lamu kuwa na elimu ndogo, hupelekea kuyachukua mambo ya Kiislamu kwa nguvu bila ya kuzama katika mambo hayo na hii inatokana na ufahamu wao kuwa ni mdogo katika k u ya e n d e a m a m b o ya Kiislamu. Alisema Sheikh Kilemile.

    Alisema, Wanazuoni wa Kiislamu wanawanasihi vijana wa Kiislamu ambao ndio wanao onekana kuingia zaidi katika mkumbo huo kuwa makini na mitandao ya kijamii katika kuuendea Uislamu wao kwani akasema, Uislamu unahitaji ukati na kati na kila jambo lina hatua yake na utaratibu wake.

    Alisema, mitandao ya kijamii ipo na haiepukiki k a t i k a U l i m we n g u wa s a s a , l a k i n i k wa j i n s i hali ilivyo sasa, inaweza ikakuingiza katika shari ya kuuangamiza Uislamu na unaweza ukaitumia vizuri na ikakupeleka katika kheri ya kuuinua Uislamu.

    W e w e k i j a n a w a Kiislamu, huzuiwi kuwa katika mitandao ya kijamii au kuitumia lakini itumie vizuri ili ilete kheri na manufaa ikusaidie wewe na uisaidie jamii kwa ujumla. Alisema Shkh. Kilemile.

    A l i s e m a , m a k u n d i hayo yenye mtazamo na dhana ya msimamo makali,

    Na Bakari Mwakangwale

    wa m e k u wa n a h a r a k a katika kuyaendea masuala ya dini na kufikia mahali kuwakufurisha Waislamu wenzao, pale wanapojaribu kuwakosoa kwa mujibu wa mafundiso ya Qur an.

    B i l a y a m i z a n i unamkufurishaje Muislamu mwenzako, huu ni uchache wa elimu na kuyafahamu mafundisho ya Uislamu, kwa sababu ukiufahamu Uislamu huwezi kuwa na lugha za kukufurishana. Alisema Shkh. Kilemile.

    Sheikh Kilemile, aliwataka wadau na wanazuoni wa Kiislamu nchini kushirikiana kukemea dhana ya Msimamo Mkali katika Uislamu kwani ni jambo ambalo halipo katika Uislamu na katika zama hizi limesambaa kwa kasi miongoni mwa Waislamu na kuleta sintofahamu.

    S h k h K i l e m i l e akisherehesha mada yake akagusia baadhi ya upotofu unaosambazwa akisema kuwa kuna watu wanadai kusoma elimu ya shule ni ukafiri, huku wakiwalaz imisha Waislamu wengine kutosoma na kuachana na elimu hiyo sambamba na kuwakataza Waislamu kushiriki katika siasa kwamba kufanya hivyo ni ukafiri.

    Akasisitiza kuwa huo ni upotofu na ujinga walio nao wanaosambaza mawazo hayo.

    Wakati huo huo, imeelezwa kuwa baadhi ya Waislamu wa m e k u wa wa k i m b i l i a aya zenye Mutashabiha na

    kuacha Muhakama, hivyo kusababisha migongano kwa Waislamu.

    Hayo yamebainishwa na Sheikh Muharami Juma Doga, wakati akiongea na Waislamu katika kongamano hilo ambapo alisema, lau Waislamu wanashikamana na muhkamat, hakuna sababu ya kufarikiana.

    Akasisi t iza kuwa aya mutashabihat, zinahitaji ujuzi, lakini pia ifahamike kuwa uzito upo katika kufuata aya zilizo wazi ambazo ndio zimebeba roho ya Dini.

    Akisherehesha aya za Qur an na Hadithi za Mtume (s a w), Sheikh Doga, alisema Uislamu unafundisha kuwa usijilazimishe kufanya jambo lililo nje ya uwezo wako kwani kufanya hivyo ni hatari kubwa.

    Alisema, makundi hayo yamekuwa yanatafuta njia zao za kuyaendea mambo ya Uislamu katika mazingira ambayo yanahitaji ueledi na ina le ta p icha kuwa h u e n d a wa n a m a l e n g o yao waliyoyakusudia au w a n a t a k a w a o n e k a n e

    wameleta kitu kipya katika jamii ya Waislamu jambo ambalo ni hatari.

    Ukifatilia nyendo zao u t a b a i n i wa n a ya e n d e a masuala ya Kiislamu kwa njia zao, lakini Muhakama (a ina ya aya ndani ya Qur an) hawazitaki, wao wa n a n g a n g a n a k a t i k a Mutashabiha.

    Bila shaka wana malengo yao waliyoyakusudia ima waonekane wameleta kitu kipya katika jamii na hii ni hatari kubwa kabisa. Alisema Shkh. Doga.

    Mwanazuoni huyo katika dini ya Kiislamu, alisema hakuna kitu kipya katika U i s l a m u b a d a l a y a k e wanaibuka watu (Waislamu) wanodhani wataonyesha kitu ambacho wote hawakijui wala hakuna anayekifanya huku wakitaka kuonyesha njia hiyo ndio njia sahihi kumbe ni kupotoka.

    A l i s e m a , k u t o k u j u a (ujinga) kwa Waislamu, ndio chanzo cha upotoshaji unaotokea miongoni mwa Waislamu hivi sasa, kwani yanayofanyika yanaashiria ni

    ukosefu wa elimu na ufahamu wa mafundisho ya Uislamu.

    N a ye D k t . H a m d u n i Suleiman, akichangia katika Kongamano hilo, alisema yapo matatizo ya uelewa katika kuyaendea masuala ya Uislamu na mbaya zaidi ni kule kijidhania kuwa wana elimu ya Uislamu wakati hawana zaidi ya kuleta migongano miongoni mwa Waislamu.

    Ni vyema Waislamu hao kama wanafahamika waitwe katika hadhara kama hizi zinazokutanisha Jopo la Wanazuoni wa Kiislamu ili wapate majibu na ufafanuzi wa hoja na dhana zao hizo. Alisema Dkt. Hamduni.

    Akitoa maoni yake mara baada ya Kongamano hilo, Maalim Ally Bassaleh, alisema mada mbalimbali zi l izo hudhurishwa na wanazuoni kwa Waislamu zina umuhimu mkubwa kwa wakati uliopo ,hususan suala la misimamo mikali katika Dini.

    A l i s e m a , a n a u n g a n a na watoa mada wote na wachangiaji juu ya kupinga vita dhana hiyo inayokuja kwa kasi miongoni mwa Waislamu, sababu kubwa ikiwa ni ujinga (kutokujua) unaotokana na mtu kutokuwa na elimu na jambo analo lifanya.

    Sheikh Amran Kilemile.

    Mkuu Magereza ashikilia uhai wa Sheikh SaidInatoka Uk. 2

    W a k i w a z u n g u m z i a Waislamu hao walio gerezani kiasi cha mwaka mzima sasa, Sheikh Amran Kilemile na Maalim Bassaleh, kwa nyakati tofauti wameleza kuwa mamlaka husika ziwatendee haki kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi.

    Maalim Bassaleh, alisema watuhumiwa hao waliopo magerezani ni Waislamu wenzao ambao wapo huko kwa muda mrefu bila sababu za msingi kiasi kwamba sasa wanaamua kuchukua maamuzi ambayo s i ya kawaida.

    Maamuzi ya kugoma kula, kugoma kuingia Mahakamani na hata kupanda juu ya mti, yote hiyo ni kutaka kuonyesha hisia zao, zaidi ni kuona hawapati haki zao na hata kufikia kuomba waonane na baadhi ya viongozi wa Serikali ili wapate kuwaeleza shida zao, lakini pia inaonekana kama vile wanapuuzwa. Alisema Maalim Bassale.

    A l i s e m a , w a l e n i wanadamu, hata kama wana makosa, bado wanayo haki ya kusikilizwa lakini kwa hali inavyokwenda hata mtu

    wa kawaida mtaani anaona kuwa kinachotendwa dhidi ya watuhumiwa hao ni dhulma.

    A l i s e m a , m t u anapotuhumiwa huwa bado anakuwa hana makosa mpaka pale Mahakama husika itakapo thibitisha, lakini akasema Muislamu akituhumiwa tu ananyimwa dhamana si ajabu mwaka mzima au zaidi kwa tuhuma zinazo stahili dhamana.

    L a k i n i k u n a m t u mwingine mwenye imani ya Kikristo naye ni kiongozi wa dini amekamatwa na silaha ya moto, na ikaelezwa silaha yenyewe ina matatizo kwamba haijulikani kuwa ni ya halali au la.

    Lakini huyu pamoja na kukutwa na silaha yenye utata anapata dhamana tena ya kujidhamini mwenywe lakini huyu Muislamu au Sheikh hana kosa la kukamatwa na chochote, ni tuhuma tu lakini ananyimwa dhamana. Alisema Maalim Bassaleh.

    Akasema, mwenendo huo ni lazima Waislamu waone kuna uonevu kutokana na tuhuma zao kusimamiwa kwa misingi ya dhulma ili hali wengine wanafatiliwa kwa

    misingi ya sheria na katiba ya nchi.

    Kwa upande wake Sheikh Kilemile, alisema Masheikh na Waislamu hao kama kweli wana kesi, basi ni bora izungumzwe na tatizo lionekane, na kwamba kama unamtuhumu mtu, basi tuhuma zake uziweke wazi.

    E l e z a t u h u m a z a k e ziangaliwe kwa misingi ya haki na kama ana makosa yaonekane, Mahakama zipo kwa ajili hiyo, makosa yawe wazi yafahamike, kuliko hii hali ilivyo sasa dhidi ya Waislamu hao. Alisema.

    Sheria ya kesi ni kuwa inafikia mahali kesi yake inatakiwa izungumzwe kisha Mahakama iamue kama anatuhuma au hana, kisha mtuhumiwa apewe haki yake aidha kutumikia adhabu au aachiwe huru. Aliongeza Sheikh Kilemile.

    Akasema, Waislamu hao wanashikiliwa kwa muda mrefu sasa lakini haieleweki sababu za msingi zinazo kwamisha kesi hiyo, huku siku zinazidi kwenda na kupelekea watuhumiwa na umma hawajui hatima ya suala hilo na kwamba hali hiyo haipendezi katika misingi ya utu na haki.

  • 4 AN-NUURRAMADHAN 1436, IJUMAA JUNI 26- Julai 2, 2015Habari

    Amiminiwa risasi na Polisi, afarikiKIJANA Usamah Abdullah Rahim amepigwa risasi na kuuliwa papo hapo na polisi.

    Baada ya kumuuwa kijana huyo, Polisi walitoa taarifa wakidai kuwa waliwahi kumuuwa ki jana huyo wa Kiislamu kwa sababu alikuwa akipanga kuchinja Wakristo na hata Polisi.

    Kama ushahidi, Polisi hao walionyesha kisu ambacho walidai kuwa walimkuta nacho Rahim na kwamba walipotaka kumsimamisha il i wampekue, Usamah Abdullah Rahim, aliwatisha k wa k i s u h i c h o n d i o wakaamua kumpiga risasi.

    Katika madai zaidi ya Pol is i inaelezwa kuwa m i o n g o n i m w a w a t u ambao Usamah Abdullah Rahim, alipanga kuwachinja ni pamoja na Bi Pamela Geller anayesifika kama manaharakati anayeuchukia Uislamu.

    Terror suspect killed by FBI 'planned to behead Pamela Geller'

    Usaama Rahim allegedly planned to kill anti-Islam activist before his death in Boston on Tuesday.

    Ndio baadhi ya vyombo vya habari vilivyoripoti vikijitahidi kuhalalisha m a u w a j i y a R a h i m yaliyotokea Boston mapema mwanzoni mwa mwezi huu wa sita kwamba alikuwa kapanga kumuuwa Pamela.

    Jihadi Shot Dead in Boston was Plotting to Behead Cops, Another Arrest Made.

    Boston Beheading Plot Jihad in America: Enemy in our Midst.

    Ndivyo vi l ivyokuwa v i m e p a m b wa v y o m b o vingine vya habari vya Marekani vikielemea juu ya madai ya kitisho cha kuchinjwa polisi.

    The man shot and killed Tuesday by Boston police was plotting with another suspect to behead a cop, a law enforcement source told Fox News.

    N d i v y o F O X N e w s walivyoripoti wakisherejesha kwa kudai kuwa kijana huyo na watu wengine wal ikuwa wamepanga kuchinja Wakristo na Polisi kwa kutumia mtindo wa magaidi wa ISIS.

    Tunaamini walikuwa na nia ya kuchinja Polisi, alinukuliwa afisa mmoja wa polisi akisema.

    Tul i jua l i l ikuwa ni tishio la kweli na ilikuwa watekeleze mpango huo Jumanne. Aliongeza afisa huyo.

    Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi wa Boston, Kamishna William Evans alisema

    Na Mwandishi Wetu

    kuwa ilikuwa ni mapema kiasi saa moja asubuhi ambapo maofisa wa kikosi maalum cha kupambana na ugaidi (Joint Terrorism Task Force) walimsimisha Rahim wakimhoji mambo kuhusiana na mwenendo wake unaotia shaka juu ya ugaidi.

    Hata hivyo akadai kuwa Rahim alitoa kisu akitaka kumdhuru po l i s i nd io wakamuwahi kumpiga risasi.

    The terrorism plot was "very real" and "very dangerous."

    Alidai Kamanda William Evans akijitahidi kuonyesha kuwa walikuwa hawana n a m n a i l a k u m u u w a Usaamah Abdullah Rahim, kwa madai kuwa ingekuwa hatari kama wasingefanya hivyo!

    Ili kuthibitisha madai yao, polisi walidai kuwa upo mkanda wa video ukionyesha tukio zima.

    Hata hivyo, video iliyokuja kutolewa haithibitishi madai ya polisi.

    Ukiacha kuwa ki jana Rahim anaonekana kwa shida katika picha hiyo ikionyesha kuwa ilipigwa toka mbali, lakini kisu hakionekani kabisa au silaha ya namna yoyote.

    Wa l a h i c h o k i t e n d o kinachodaiwa kuwa Rahim a l i t a k a k u wa s h a b u l i a , hakionekani katika picha hiyo.

    Hata vile vyombo vya habari ambavyo kwa kawaida hushabikia taarifa za polisi juu ya madai ya kukamata au kuuwa magaidi, viliandika vikisema kuwa video ya polisi haijibu maswali juu ya tukio la kuuliwa Rahim na zaidi vikasema haithibitishi kwa namna yoyote madai kuwa Rahim alipambana na polisi.

    Ukiacha mapungufu hayo, ndugu, jamaa na waumini wa Msikiti anaposwali Usamah, wanasema kuwa madai ya polisi na kikosi chao maalum

    cha kupambana na ugaidi ni urongo mtupu.

    Na kwamba hata kama angekamatwa akiwa na kisu, bado hiyo sio sababu ya kumpachika jinai ya ugaidi na kumuuwa papo hapo.

    Wa n a s e m a , k a m a n i kitisho, basi waseme ni Uislamu wa Usamah, lakini s i o k u m s i n g i z i a k u wa anapanga kuchinja Wakristo na Polisi kwani kukutwa na kisu hilo ni jambo la kawaida hasa kwa jamii ya Wamarekani Weusi, na hasa katika kipindi hiki ambapo wanauliwa ovyo na polisi na hata wananchi wa kawaida Wazungu ambao kila uchao wanazidi kuwa na chuki dhidi ya Weusi (racism)

    Alisema Bi Karen, mmoja wa ndugu wa Usamah kwamba ingawa jamii ya Wamarekani Weusi yote ipo katika kitisho, lakini unapokuwa Muis lamu, kitisho kinakuwa kikubwa zaidi.

    Hoja nyingine ya msingi Waislamu na ndugu wa Usamah wanahoji, kama Polisi na hiyo Task Force yao ya kupambana na ugaidi wanadai kuwa kijana huyo alikuwa na mpango wa kuchinja Wakristo, kwa nini wasimkamate na kumfikisha mahakamani watoe ushahidi na pengine kwa kumhoji m t u h u m i w a w a w e z e kuutambua mtandao wake wa kigaidi na kuuvunja.

    Wakati huo huo, Kijana wa Kizungu Dylann Roof aliingia katika kanisa lijulikanalo kwa jina la Emanuel African Methodist Episcopal Church kule Charleston, South Carolina, na kuwafyatulia risasi waumini ambapo aliuwa watu 9 Wamarekani Weusi wakisali.

    Hata hivyo, tukio hilo limechukuliwa kama uhalifu wa kawaida nchini Marekani na hakuna namna kijana huyu anatuhumiwa kwa

    ugaidi. Kinyume chake, baadhi

    ya taarifa zikijitahidi kumtoa Dylann Roof katika jinai hiyo, zimejaribu kuibua wasiwasi kuwa huenda kijana huyo alifanya tukio hilo akiwa hayupo hadhiri. Kwamba labda kuna jambo lilimchanganya akili ndio akaenda kanisani na kuuwa watu hao.

    Shooters of Color Are Called 'Terrorists' and 'Thugs.' Why Are White Shooters Called Mentally Ill'?

    A n a h o j i m w a n d i s h i Anthea Butler akionyesha k u t o k u r i d h i s h w a n a mwenendo wa vyombo vya habari na baadhi ya maofisa wa v y o m b o v ya d o l a . Anasema, wakati kitendo kilichofanyika ni ugaidi wa dhahiri dhidi ya watu Weusi na Makanisa yao na kwamba sio tukio la mwanzo kwa Marekani, vyombo hivyo, vinakuja na kauli ambazo ni kutaka kumfunika Dylann Roof na kudunisha jinai aliyofanya.

    Hili sio tukio la mwanzo katika historia ya Marekani. Makanisa ya watu Weusi yamekuwa yaki lengwa na wabaguzi wa Kizungu (white supremacists) ambao wamekuwa wakiyachoma moto makanisa hayo au kuyalipua kwa mabomu kama namna moja wapo ya kuwat isha jami i ya Weusi (terrorize the black communities).

    Anasema Anthea Butler akitaja moja ya matukio mabaya ya kigaidi dhidi ya Weusi kuwa ni pamoja na lile la kulipuliwa kanisa la Wamarekani Weusi kule Birmingham, Ala., mwaka 1963 ambapo wasichana wanne (4) waliuliwa.

    W a l i o f a n y a j i n a i hiyo walitajwa kuwa ni wanachama wa kundi la Ku Klux Klan (KKK), au kwa kifupi "the Klan".

    Kundi lenye rekodi na historia chafu ya chuki, u b a g u z i u l i o p i n d u k i a n a m a u wa j i d h i d i ya Wamarekani Weusi.

    Anasema Butler kuwa katika kuripoti tukio hilo la kuuliwa watu 9 ambalo kwa dhahiri kabisa ni la kigaidi, hutakuta vyombo vya habari vikitia neno lolote kuwa huo ni ugaidi. Kinyume chake, pamoja na kuwa hakuna taarifa zozote za kitabibu wala jamaa wa Dylann Roof hawajaleta madai/utetezi kuwa kijana wao alikuwa na ugonjwa wa akili, lakini vyombo vya habari mara tu baada ya kufanyika mauwaji hayo v i l i anza ku ja na misamiati na misemo kama:

    A victim of mistreatment or inadequate mental health resourceswe dont know his

    mental condition."Yote hii anasema, ni kutaka

    kujenga hoja kumnasua kijana Dylann Roof katika jinai inayomkabili.

    Kwa upande mwingine kama Meya Joseph Riley wa Charleston alivyosema, tukio hilo linaonekana kama jambo la bahati mbaya tu la mtu binafsi aliye na matatizo fulani na halina uhusiano na kundi lolote unaloweza kusema ni la kigaidi kama ambavyo matukio ya watu wenye majina ya Kiislamu yanavyoburutwa yakatiwa katika kapu la ISIS, Al Shabaab na Al-Qaida. Kwa watu kama Dylann Roof, wao inakuwa ni kazi ya lone wolfs au "one hateful person".

    Ni kutokana na hali kama hizi na ubalakala kama huu, wasomi na wachambuzi wengi wa siasa za Marekani n a n c h i z a M a g h a r i b i kwa ujumla, wanaitizama inayoitwa Vita dhidi ya ugaidi kama tamthilia fulani na mzaha wa karne hii.

    Ni picha na taswira ya kubuni ambayo inakolezwa na kuvurugwa na wanasiasa.

    K a m a a n a v y o s e m a mwandishi mchokozi wa Uingereza na mchambuzi, Adam Curtis, hili "Ni wingu potofu la f ikra ambalo limesambaa bila kuhojiwa miongoni mwa serikal i duniani kote, majeshi ya usalama na vyombo vya habari."

    Wakati nchi za Magharibi zikitumia Vita ya Msalaba dhidi ya magaidi kuhalalisha uvamizi angamizi ili kupata masilahi yao ya kibeberu, nchi kama yetu zinazochagizwa kushiriki katika Crusade hii kama alivyoiita muasisi wake George W Bush, zinajikuta zikijitosa kibubusa matokeo yake yakiwa ni maangamizi kwa watu wake na nchi kwa ujumla.

    Maangamizi kwa watu k w a s a b a b u , k w a n z a watapandikizwa magaidi watakaoleta maafa kama i n a v y o t o k e a N i g e r i a , Somalia, Yemen, Pakistan na Kenya.

    P i l i , n i m a a n g a m i z i kwa nchi kwa sababu kwa kutumia kisingizio cha kupambana na magaidi, mabeberu huingia kikachero na kijeshi wakazidhibiti nchi wazitakazo zisiweze kufurukuta wala kuwa na uhuru juu ya rasilimali zao na siasa za nchi. Kila kitu wanapangiwa na kupewa maelekezo.

    Kwa hiyo, wakati nchi lengwa ikiangamizwa pamoja na watu wake, mabeberu wanavuna faida isiyo ya kawaida kiuchumi na kisiasa kutimia azma yao ya Global hegemony.

    Usamah Abdullah Rahim

  • 5 AN-NUURRAMADHAN 1436, IJUMAA JUNI 26- Julai 2, 2015Habari za Kimataifa

    SERIKALI ya China imepiga marufuku wanafunzi, walimu na watumishi wa umma katika eneo la Xinjiang lenye Waislamu wengi, kutekeleza ibada ya Saumu katika mwezi h u u m t u k u f u w a Ramadhani.

    Serikali pia imezuia watu kuhudhuria shughuli zozote za kidini ikiwa ni pamoja na ibada za usiku.

    Taar i fa ya ser ika l i imetaka biashara kwenye h o t e l i n a m i k a h a wa kufunguliwa nyakati za mchana kama kawaida.

    Wa n a h a r a k a t i w a Kiislamu wamepinga agizo hilo la serikali wakisema linalenga kuhujumu dini tukufu ya Kiislamu.

    Ingawa serikali inasema lengo la kuweka sheria h iyo n i kuhak ik i sha m a s u a l a y a d i n i hayavurugi muundo wa jamii, duru za kuaminika zinasema sheria hiyo ina malengo ya kiuchumi, kwani imewekwa i l i kuhakikisha nguvu kazi ya taifa haipungui katika mwezi wa Ramadhani.

    C h u o K i k u u c h a K i i s l a m u c h a A l -Azhar cha nchini Misri kimepinga na kulaani dhulma na ukandamizaji wa kidini unaolenga haki za msingi za Waislamu nchini China.

    Al Azhar imeitaka jamii ya kimataifa kama vile Umoja wa Mataifa na asasi mbalimbali za haki za binadamu kulaani kitendo hicho.

    Kwa miaka kadhaa sasa, serikali ya China imekuwa ikitekeleza sheria hiyo ya kibaguzi na mwaka uliopita, watu kadhaa walifikishwa m a h a k a m a n i k w a kufunga Ramadhani na kukaidi sheria hiyo. (Irib)

    MUFTI wa Uganda S h e i k h S h a b a n Ramadhan Mubajje, a m e i t a k a s e r i k a l i n a m a s h i r i k a y a usalama ya nchi hiyo y a n a y o c h u n g u z a mauaji ya viongozi wa Kiislamu, kufanya kazi kwa uadilifu na kwa viwango vya juu vya utaalamu.

    V y o m b o v y a habari vya Uganda vimemnukuu Mufti wa nchi hiyo akiitaka serikali, hususan wale wanaohusika na masuala

    Saudi Arabia inaendeleza na mashambulizi yake ya anga katika maeneo mbalimbali ya Yemen, licha ya kutolewa wito m b a l i m b a l i k a t i k a ukanda huo na kimataifa w a k u s i m a m i s h a mashambuliz i hayo yanayouwa wananchi wasio na hatia kwa mamia ya maelfu.

    Mashambulizi ya anga ya muungano wa Saudia katika maeneo mbalimbali ya Yemen yaliendelea wiki hii ; huku idadi kadhaa ya Wayemeni wakiuawa na kujeruhiwa. M a s h a m b u l i z i h a y o y a n a e n d e l e a h u k u makundi husika kwenye mgogoro wa Yemen yakishindwa kufikia muafaka baada ya siku tano za mazungumzo mjini Geneva Uswisi.

    Saudi Arabia imesema k u w a k u o n d o k a wapiganaji wa Mahouthi wa Ansarullah katika maeneo wanayoyadhibiti ni sharti la usimamishwa vita huko Yemen.

    Ismail Ould Sheikh A h m a d , M j u m b e Maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Yemen, awali alijaribu k u f a n ya j i t i h a d a z a kufikiwa makubaliano ya usitishaji vita huko Yemen na baadaye makundi ya nchi hiyo yakaweza kuketi kwenye meza ya mazungumzo huko Geneva.

    Sambamba na juhudi h i z o z a k u u p a t i a ufumbuzi mgogoro wa Yemen, lakini kutokana na mashambulizi ya Saudia ya n a y o e n d e l e a k i l a uchao nchini humo, hali ya wananchi imekuwa mbaya zaidi hivi sasa kwa kuzingatia uhaba wa chakula uliopo na kuendelea kushambuliwa vituo vya afya na tiba nchini humo.

    Wananchi wa Yemen h a w a p a t i h u d u m a

    Licha ya Ramadhani Saudia yaendelea kuihujumu Yemen

    Waharibu hospitali 62 na zahanati 115Wanaopambana wote wapo kwenye swaumu

    muhimu za kiafya na maji safi ya kunywa kutokana na kushtadi mashambulizi ya utawala wa Aal Saud, huku uhaba wa mafuta pia ukiwafanya raia hao wakabiliwe na hali ngumu ya kimaisha.

    Ta m i m a l S h a m i , msemaji wa Wizara ya Afya ya Yemen alisema

    mwishoni mwa wik i kat ika mahoj iano na televisheni ya al Mayadeen y a L e b a n o n k u w a , mashambulizi ya anga ya Saudia huko Yemen hadi sasa yameharibu na kubomoa hospitali 62 na zahanati 115.

    Ta m i m a l S h a m i aliongeza kuwa, hakuna

    shaka kuwa mashambulizi ya anga ya Riyadh ni sababu kuu ya kuibuka matatizo ya kiafya na kitiba huko Yemen.

    Umoja wa Mata i fa nao umedaiwa kuhusika katika kutokea maafa hayo kwa hatua yake ya kile kilichotafsiriwa kuwa ni kuikingia kifua Saudi Arabia.

    Uchunguzi wa mauaji ya Masheikh UgandaMufti aitaka serikali iwafanye uadilifu

    ya usalama kutumia utaalamu wa hali ya juu katika kazi zao kama kweli wanataka kupata ufumbuzi wa kudumu wa mlolongo wa mauaji ya viongozi wa Kiislamu nchini humo.

    Mufti Mubajje alisema hayo wilayani Kamuli mwishoni mwa wiki wakati wa uzinduzi wa eneo la Waislamu lililojengwa na shirika lisilo la kiserikali NGO la Kamuli Good Hope lililogharimu shilingi milioni 75.

    Matamshi hayo ya Mufti Mubajje, yamekuja kufuatia wimbi la mauaji ya Masheikh katika mkoa wa m a s h a r i k i , h u k u mauaji ya karibuni kabisa yakiwa ni yale ya Sheikh Abdul Rashid Wafula huko Mbale.

    M u f t i M u b a j j e p i a amewataka Waislamu wa madhehebu mbalimbali kuungana na kuweka pembeni tofauti zao ndogo ndogo na kuwa mfano bora kwani Uis lamu inafundisha amani na kuishi na watu kwa wema.

    China yawazuia Waislamu Xinjiang kufunga

    RAIA wa Yemen wakiwa wamebeba mtoto aliyejeruhiwa kutokana na mashambulizi ya majeshi ya Saudi Arabia yanayoendelea nchini humo.

  • 6 AN-NUURRAMADHAN 1436, IJUMAA JUNI 26- Julai 2, 2015Makala/Tangazo

    Mafundisho ya Quran

    Fethullah-Gulen

    HIVI mnawaamrisha watu kufanya wema na hali mnaziacha nafsi zenu na hali y a k u w a n y i n y i mnakisoma kitabu, hivi hamuelewi?. [Al-Baqarah 44]

    Pamoja na kwamba aya hii inawasemesha sehemu katika wana wa Israel kwa sura ya moja kwa moja, lakini ni kwamba aya h i i i n a wa s e m e s h a Waislamu vile vile.

    K wa su r a h i i ya I s h a r a n a j a m b o ambalo linakusudiwa hasa, ni kutuzinduwa j u u ya wa j i b u wa kupatikana umoja na kutovunjana kati ya yale yanayosemwa na yale yanayotendwa. Kwa maana ya umoja katika maneno na matendo.

    Kwa sababu hiyo, tunaona kwamba aya nyingine inaelezea maana haya kwa njia nyingine, inasema : Kwa nini mnasema yale ambayo hamyatendi? [Assaf 2]

    Usiwahamashishe w e n z a k o k u f a n y a wema, wakati wewe mwenyewe unafanya kinyume chake.

    N d i y o h a l i n a maneno au kusema na kutenda ni lugha yenye pande mbili , kwa ajili ya kuinusuru haki na kuwakilisha, i t a k a p o z u n g u m z a hii lugha yenye sura mbili na maonekano mawili, kwa jina la haki na ikapiga kelele kwa hiyo haki taathira yake itakuwa kubwa sana. Kwa sababu kunapasa j u u y a b i n a d a m u k u ya t e k e l e z a ya l e

    ambayo anawalingania wa t u we n g i n e . N a kusiwe na kupingana kati ya maneno yake na matendo yake na kati ya hali yake inayoonekana na maelezo yake.

    Imekuja katika athari kwamba Mwenyezi M u n g u m t u k u f u alimwambia Mtume Issa (a.s.):

    Ionye nafsi yako kwanza, iwapo nafsi y a k o i t a y a k u b a l i mawaidha, hapo wape (wengine) mawaidha yako. Na kama nafsi yako haikukubali, basi ona haya kwangu.

    Kwa msingi huo, i n a p a s a k u i s h i binadamu kufuatana na anavyoamini na aakisi vina vya ulimwngu wake wa ndani miongoni mwa fikra na hisia, itakuwa ni kitendo cha kuitakasa nafsi yake. Yule ambaye hasimami usiku ni juu yake kutoizungumzia swala ya Tahajudi na aone haya kufanya hivyo. Na yule ambaye hawezi kuswali kwa unyenyekevu wote na kwa kujinyongesha na wala hatendi kwa adabu mbele za Mwenyezi Mungu mtukufu, wala haimtishi na kuogopa kumuogopa Mwenyezi Mungu, asizungumze kuhusu sifa kamili za swala. Na akitokuwa ni mwenye ku j i toa muhanga, kunapasa kutozungumza tamko moja kuhusu maudhui ya kuishi kwa ajili ya watu wengine.

    Kwa sababu Mwenyezi M u n g u m t u k u f u a m e f u n g a m a n i s h a kwa hekima fulani n g u v u ya k u a t h i r i yale yanayosemwa, na mfumo wa utendaji wa msemaji.

    H a p a k u n a p a s a kukumbusha jambo jingine, nalo ni kuja u w e z e k a n o w a kuifahamu kimakosa aya hii:

    N i k w a n i n i mnasema yale ambayo hamyatendi? [A-ssaf 2].

    A y a h i i haifahamishi maana ya kuwa tahadhari kulikumbusha jambo ambalo huishi nalo

    kwa sababu kuishi ni ibada na kufikisha ni ibada nyingine. Yule ambaye hakuyatekeleza yote mawili, amebeba dhambi mbili na amekaa mbali na nguvu za kuathiri kwa hatua m b i l i , n a a m b a y e hakulitekeleza moja la hayo mambo mawili, atabeba dhambi moja, na amekuwa mbali na kuathiri kwa hatua m o j a . K wa s a b a b u nguvu ya kuathiri kama tulivyosema inategemea juu ya kutekelezwa yale yanayofikishwa.

    Ndiyo, kwa hakika kuwaamrisha watu wengine kwa kufanya mema na kuwakataza na maovu na kuacha

    kuyatekeleza hayo juu ya nafsi huko, ni kuvunjana kuliko wazi. Na mfano wa utendaji huu wenye makosa, unapunguza taathira ya mambo chanya mengi, kama vile nguvu ya balagha na kuweka wazi na elimu. Haya ndiyo ambayo yanatajwa na aya hii. Ila asije akatumbukia mtu yeyote mwenye akili katika mfano wa kupinga huku na unamtaka binadamu umakini na kufikiri katika kuishi, na kufikisha na yasiyo kuwa hayo miongoni mwa upuuzi na maneno mengi yanayoondoa h a i b a y a m w e n y e kuzungumza. Na hili lina maana kwamba

    yeye ameiacha nafsi yake kikamilifu. Kwa sababu hiyo, imekuwa ni juu ya mtoaji wa mawaidha, na juu ya mtoaji wa nasaha na mwenye kuongoza, na mwenye kufikisha na mwenye kuandika, na mwenye kupanga mambo, awe ni mkweli katika matendo ambayo anasimama nayo ili yachukuliwe machukuo ya ukweli na kwa ajili yasipate kivuli chochote cha shaka juu ya zile m a u d h u u a m b a z o anazizungumzia na kuzitoa.

    (Imenukuliwa kutoka Kitabu: Miyangaza y a Q u r a n k a t i k a mbingu ya hisia, cha Muhammad Fethullah Gullen kilichotafsiriwa k wa K i s wa h i l i n a Sheikh Sule iman Amran Kilemile)

  • 7 AN-NUURRAMADHAN 1436, IJUMAA JUNI 26- Julai 2, 2015Habari

    Profesa Ibrahim Noor Shariff

    Propaganda za udini shuleni Tanzania-8

    T U K U M B U K E p i a kuwa katika miaka hii tuliyonayo hapatakuwa n a k u s h e r e h e k e a , kila mwaka, mauwaji y a k i m a a f a k a m a wanavyosherehekea maafa ya Wazanzibari W a i s l a m u w e n g i waliotolewa roho zao bure 1964. Yakitokea, jua kuwa washiriki wengi watasakwa, kukamatwa n a k u p e l e k w a mahakamani -- The Hague.

    Nastaajabu, lakini sistaajabu sana kuona Waomani wamekaa kimya maana kutokana na us taarabu wao , huwaoni kugombana ovyo na mtu yoyote wala huwasikii kutukanana. Ni watu wakar imu sana kwa vitendo na kwa maneno mazuri. Hivyo basi wanayasikia yasiyokuwa ya kweli yanayosemwa dhidi yao na hawasemi kitu. Lakini, kama ulivyoona wale wenye kutapakaza siasa kali za udini huwa kila kukicha wanazidisha m a o n g o p e ya o n a kufikia hadi ya kuonesha picha za utumwa hata West Indies, ambako Waarabu hawakuweko, na kuonesha kuwa ni Waarabu waliokuwa na Watumwa hata huko katika visiwa vilioko Amerika. Kwa ukosefu wa bahati, ukimya wa Waomani unaotokana na ustaarabu wao wa hali ya juu kabisa wa kutokujibu uwongo wa dhahiri unaosemwa dhidi yao na wenye siasa kali za udini , kumewafanya wenye siasa hizo kuzidisha uwongo wao kila leo.

    Propaganda dhidi ya

    Waislamu si jambo geni kwani zilianzia zaidi ya miaka elfu iliyopita. Propaganda dhidi ya Waislamu wa Afrika Mashariki zinazotokana n a w a k o l o n i n a w a m i s h i n a r i w a o p i a s i j a m b o g e n i kwani zilianza tokea yalipowasili majeshi y a K i p o r t u g i z i mwanzoni mwa karne ya 16 . Propaganda hizi zilizidi kutia fora wakat i wa utawala wa Wa i n g e r e z a n a Wajarumani mwishoni mwa karne ya 19. La kusikitisha ni kuona k u wa wa m i s h i n a r i katika kusomesha kwao waliwafunza wanafunzi wao wa Kiafrika ubaya wa Uislamu na wema wa Ukristo na kuwa dini ya Kiislamu ni batili na dini yao ya Kikristo ndiyo ya kweli na ya haki iliyoletwa Afrika Masharika na Kati kumkomboa Mwafrika na ukatili na ubaya wa Uislamu na Waislamu.

    W a k a t i h u o h u o w a l i p o k u w a wakiwasomesha haya watoto wa Kiafrika, wakoloni wa Kizungu na wamishinari wao waliziteka na kuzitia nchi za Afrika katika ukoloni wao ambao mara nyingi ulisababisha v i f o v ya Wa a f r i k a wengi kwa mauwaji ya kinyama kabisa na utiwaji wa Waafrika wengi utumwani katika n c h i z a o we n ye we Waafrika, na mamilioni wengine ya Waafrika waliotiwa utumwani walipelekwa kwenye nchi zilizotawaliwa na Wazungu Wakristo.

    Kama tulivyokwisha kutaja pia, chini ya utawala wa Mfalme Leopord II (1835 1909) wa Ubiligiji aliwatia utumwani mamilioni ya Wakongo katika m a s h a m b a ya m i t i y e n y e u t o m v u wa kutengenezea mipira; na katika juhudi hizo a l iwauwa Waafr ika wasiopungua milioni kumi, wengi walifungwa na kuadhibiwa vikali s a n a , w a l i p i g w a mboko, wengine wengi walikatwa viganja vya mikono yao walipokataa

    kufanya kazi bila ya malipo. Soma vitabuni na fungua mitandao uangalie mwenyewe n i n i w a m e a n d i k a wanahistoria kukhusu u t u m w a h u u n a ukhabithi wake na idadi ya Waafrika waliouliwa.

    Lakini, wamishinari wa Kizungu jana na wamishinari wa Kiafrika leo hawazungumzii utumwa huu na unyama wake, kwani kufanya h ivyo kutawaweka Wakristo na Ukristo pahala pabaya sana. Na hili ndilo jambo wanalolipiga chenga. Wao wamo kila leo k u s h i n d i l i a k a t i k a bongo za wanafunzi wa Tanzania ubaya wa Waislamu tu hata iwapo Uislamu na Waislamu hawakhusiki na ubaya h u o . K u f a n ya h i l i kunayafanya masomo ya shule ya historia kuwa si masomo yenye kuelezea ukweli uliotokea, bali huyafanya masomo hayo kutiwa katika kumbo la propaganda; na la kusikitisha zaidi ni kuiona Serikali ya Ta n z a n i a a m b a y o inajigamba kuwa haina dini na haipendelei wala kuichukia dini yoyote kuwa inashiriki k iukami l i fu ka t ika k u w a p a k a u c h a f u n a k u wa p i g a v i t a Waislamu na dini yao na kuwapendelea Wakristo wenye siasa kali za udini kwa kuachilia p r o p a g a n d a z e n ye ukweli finyu na uwongo mwingi kusomeshwa katika shule za Tanzania mchana kweupe bila ya kificho na bila ya kuona haya wala kuwa na khofu, kunaifanya Serikali ya Tanzania kuwa mshiriki katika k u j e n g a m s t a k b a l i mbaya kwa nchi ya Tanzania ambayo wao wameapa kuilinda na kila ovu.

    Wa n a p r o p a g a n d a waliopewa fursa ya kuandika vitabu vya h i s t o r i a k w a a j i l i y a k u w a s o m e s h e a wanafunzi wa shule za Tanzania wameitumilia fursa hiyo vibaya sana, kwani wameonesha waziwazi mapendeleo yao juu ya Ukristo na Wakristo na chuki

    zao zinazotokana na vita vyao vya msalaba dhidi ya Uislamu na Waislamu.

    Vita hivi katika Afrika M a s h a r i k i k wa n z a v i l i a n z i s h w a k w a maneno na wamishinari wa Kizungu na serikali zao za kikoloni na z imepokelewa kwa utiifu mkubwa sana na wamishinari wa Kiafrika ambao wamejibebesha vita hivyo vya msalaba na kuviendeleza mbele kwa kadiri ambayo hata waalimu wao wa kikoloni wanaonekana leo kama wanafunzi. Ingelikuwa hayo wanayoyaelezea w a n a p r o p a g a n d a ni ya kwel i mtupu t u s i n g e l i g u t u k a , l ak in i mengi za id i w a l i y o y a c h o r a n a k u y a a n d i k a s i matokeo ya kwel i , kama tulivyokwisha kudhihirisha.

    K w a w e n y e macho, na mwenye m a c h o h a a m b i w i tazama, Tanzania imeshatumbukizwa katika vita vya udini na hawa Watanzania wenye siasa kali za udin i . Tanzania n i nchi yenye Waislamu w e n g i n a u b a y a mkubwa wanaoufanya wanapropaganda hawa kwa propaganda zao dhidi ya Wais lamu n i kuwahamakisha Waislamu na kupalilia mfarakano mkubwa wa kipumbavu kabisa baina ya Wakristo na Waislamu wa Watanzania. Na hili ni jambo la khatari kubwa sana kwa nchi nzima ya Tanzania, na Serikali ya Tanzania ndiyo itakayokuja kulaumiwa na dunia kwa kushiriki ka t ika propaganda hiz i kwa kuonesha kama hawayaoni na hayawakhusu hayo y a n a y o s o m e s h w a s h u l e n i . V i t a v y a maneno vimeanzishwa zamani, jee viongozi wenye busara Tanzania watapigania kiungwana na kwa haki kuviondosha au watashika mirengo na kuvipalilia vita hivi na raia wa kila upande k u k u t i s h wa m a a f a kama waliyokutishwa Waruwanda, Wabosnia, W a z a n z i b a r i n a wengineo?

    Jambo moja wanafaa wenye akili zao timamu w a l i f i k i r i e v i z u r i n i kuwa Wais lamu Tanganyika ni wengi na hawatakubali wachinjwe huku wamelala chali. K i l a m we n ye a k i l i zake timamu anaelewa fika kuwa kukianza chinjachinja Tanganyika, basi watachinjwa watu wa dini zote wa pande zote na misiba itakuwa Ta n g a n y i k a k o t e , hakuna atakayesalimika na ukoo wake wote. Usia wangu ni kuwa w a t u w o t e w e m a wanaoipendelea mema Tanzania watafute kila njia za kuungana na kuwapinga vikali sana wenye kutapakaza siasa kali za chuki, za ukabila, udini na za aina yoyote inayokhatarisha nchi.

    K w a a j i l i y a propaganda za udini ziliomo ndani yake, v i t a b u v y o t e v y a historia vinavyotumiwa shuleni Tanzania leo, vinataka vichomwe moto ili kuondosha na kuuzika mmoja katika mizizi mikuu ya fitina inayopaliliwa katika bongo za wanafunzi; mzizi wa fitina ambao u n a e n d e l e a k u i l a Tanzania ndani kwa ndani na siku moja itakuja kuleta khatari pevu. Inahitajia badala yake viandikwe upya vitabu vya historia na mabingwa wanaoijua historia vizuri sana n a w a s i o p e n d e l e a upande wowote wala propaganda yoyote; mabingwa wa historia watakaoelezea matokeo ya historia kwa ukweli k a m a u t a k a v y o -wezekana na wana Adamu. Huu ndio usia wangu wa dhati. Ukiona nina-shambuliwa mimi binafsi na watu fulani kwa ni l iyoyaelezea humu na kwa usia huu nilioutoa, jua kuwa viumbe hao ama ni wale waliokwisha kupikwa na kupikika vibaya sana na propaganda hizo nil izozielezea, a u n i k a t i k a wa l e w a n a o n u f a i k a n a p r o p a g a n d a h i z o ; v i u m b e a m b a o hawaipendelei mema Tanzania na watu wake.

  • 8 AN-NUURRAMADHAN 1436, IJUMAA JUNI 26- Julai 2, 2015Habari/Tangazo

    KAMATI YA MUUNGANO YA MASHINDANO YA SHULE ZA KIISLAMUAssalaam alaykum warahmatullahi wabarakaatuhUmoja wa shule za msingi za Kiislamu Tanzania (TIPSO) pamoja na

    kamati ya pamoja ya kuhifadhi Quran inawatangazia wazazi, walezi, walimu, wanafunzi na Waislamu wote kufanyika mashindano ya tisa ya kuhifadhi Quran kwa shule za misngi za Kiislamu Tanzania kama ifuatavyo:

    Jumamosi 27/06/2015 katika Msikiti wa Kichangani Magomeni-Dar es Salaam

    Jumapili 28/06/2015-Fainali katika ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam.

    Muda ni kwa siku zote mbili kuanzia saa 2:00 Asubuhi 6:30 mchana. Wote mnakaribishwa.

    Holy Quran Recitation Joint CommitteeMb: Mwenyekiti 0713 334 698, Katibu 0784 211673, Mweka hazina

    (Treasurer) 0717 304 353 Email:[email protected]

    MASHINDANO YA TISA YA KUHIFADHI QURAN

    Hali si shwari ZanzibarWAKATI Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Z a n z i b a r ( C C M ) wakimkataa Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad kuingia katika Baraza wakati wa kufungwa kwa Baraza, ZEC imeshushiwa tuhuma nzito.

    Tuhuma hizo ni ukiukwaji wa sheria na taratibu za uandikishaji wapiga kura ambapo CUF wanadai kuwa ZEC inatumiwa na CCM kuandikisha mamluki wa kukipa chama hicho tawala ushindi.

    Katika kikao chake jana, Wawakilishi hao walikataa uwepo wa Maalim Seif wakati Baraza hilo litakapofungwa leo na kuvunjwa rasmi na Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein.

    Kwa mujibu wa sheria, Rais huingia ndani ya ukumbi wa Baraza akiwa na wageni wake ambapo ni Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu na Mshauri wake Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad.

    Kwa mujibu wa kanuni za Baraza hilo, wageni hao wanapoingia ndani ya ukumbi huo, inabidi kutenguliwa kwa baadhi ya kanuni kwa kuwa sio wajumbe wa Baraza.

    Hivyo, Spika wa Baraza hilo Pandu Ameir Kificho alitoa taarifa ya kuwaarifu wajumbe juu ya ujio wa wageni hao na kutaka waridhie.

    Tunamtegemea Rais wa Zanzibar atakuja na ujumbe wake maalumu, kwa hivyo tunamtegemea pia Jaji Mkuu, Jaji Makungu na tunamtegemea Mshauri Mkuu mmoja wapo wa Rais ambaye ni Makamo wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad ambaye naye tunategemea kuingia humu ndani.

    Spika Kificho akaanza kuwahoj i wajumbe wa baraza hilo kwa mtu mmoja mmoja, kati ya hao wageni watatu akianzia kwa Rais wa Zanzibar, Jaji Mkuu na alipofika kumtaja Maalim Seif hali ikabadilika.

    M g e n i m w e n g i n e maalumu huyu ni mshauri wa Rais ambaye ni Makamo wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad.

    A l i p o a n z a k u m t a j a jina, wajumbe wakaanza kuongea chini kwa chini ikaanza minongono ambapo Spika akaul iza mbona anasikia minongono kama hawamtaki.

    M b o n a n a s i k i a m i n o n g o n o k a m a hamumtaki.. nataka nisikie rasmi, aje au asiingie humu? Alihoji Spika Kificho.

    Hapo Wajumbe wakajibu kwa sauti kwamba asije.

    Na Salma Alghaithiyyah, Zanzibar

    Hawamtaki kuingia ndani ya ukumbi huo.

    Spika akauliza tena, Ina maana Baraza halikuridhia Maalim Seif kuingia humu ndani?

    Wakajibu, ndio hatutaki asije humu ndani, hatumtaki.

    Huku akicheka, Spika Kificho akasema kwa kawaida masuala haya huwa hayana mjadala, na akawaambia wajumbe wa Baraza hilo kwamba kwa kuwa yeye n d i ye a l i ye m u a n d i k i a barua Makamo wa Kwanza kumualika katika kikao hicho, atalazimika kumuandikia barua nyengine ya kutengua mualiko huo kutokana na wajumbe kumkataa asiingie ndani ya ukumbi huo.

    Kikawaida mimi ndiye niliyemuandikia barua ya kumualika kuja hapa, kwa hivyo nitaandika nyengine kwa heshima zote kwamba usije.

    Alisema Spika huku wajumbe hao wakipiga makofi na kuongea kwa furaha.

    Inavyoelekea Wawakilishi h a w a k u p i t i a C C M , wamechukua hatua hi i kufuatia kitendo cha wenzao kupitia CUF kususa vikao vya kumalizia Baraza.

    M a p e m a w i k i h i i , W a w a k i l i s h i h a o kupitia CUF wakiwemo mawaziri, walitoka nje ya kikao na kusema kuwa h a w a t a h u d h u r i a h a t a kikao cha kuvunjwa Baraza kitakacho hutubiwa na Mheshimiwa Rais Shein.

    Walisema, wanafanya hivyo kusajili malalamiko yao kuwa upo ukiukwaji mkubwa wa sheria, kanuni na taratibu katika uandikishaji wapiga kura.

    W a k a t i h u o h u o , Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Mheshimiwa, Jecha Salim Jecha, ametupiwa lawama nzito kuwa Tume ya k e i n a f a n ya m a m b o ambayo yanaweza kuvuruga uchaguzi.

    Moja ya tuhuma hizo ni madai kuwa ZEC inawekewa shinikizo iongeze siku za uandikishaji kutoa fursa kwa CCM kukamilisha kazi ya kuandikisha wapiga kura haramu.

    Katika barua yao kwa Mwenyekiti Jecha, CUF wanadai kuwa wana taarifa za kuaminika kwamba CCM kwa kushirikiana na Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya pamoja na Ofisi ya Usajili wa Vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi iliandaa wapiga kura haramu ambao walipatiwa vitambulisho vya ZAN ID ili kuwawezesha kuandikishwa kuwa wapiga kura kwa lengo la kukisaidia CCM.

    Hata hivyo wanadai kuwa, utolewaji na usambazaji wa vitambulisho hivyo ulikwama na kupelekea vitambulisho hivyo kupatikana ikiwa uandikishaji wa wapiga kura katika majimbo ya Wilaya ya Magharibi A umeshamalizika.

    Ni kutokana na hali hiyo, wanadai kuwa baada ya kupatikana ID hizo, ndio zinafanyika njama kuongeza siku kutoa fursa kwa wenye ID hizo kuandikishwa.

    J u m l a y a Z A N I D zilizochapishwa kwa ajili ya uharamia huu kwa Wilaya za Magharibi A na Magharibi B ni 39,500 na mpaka jioni ya tarehe 23 Juni, 2015 walipatiwa ZAN ID 6,525 ambazo walishindwa kuzi tumia kwa kukosa watu. Kati ya hizo, jumla ya ZAN ID 1,200 zilipelekwa zikagawiwe katika jimbo la Bububu ambako muda wa uandikishaji ulikwisha malizika wakati ZAN ID hizo zinawafikia viongozi wa CCM.

    Wanadai CUF katika barua yao kwa Mheshimiwa Jecha na kuongeza kudai kuwa:

    Baada ya kutofanikiwa kikamilifu, viongozi wa CCM jioni ya siku hiyo hiyo ya tarehe 23 Juni, 2015 walikutana katika Ofisi yao ya Mkoa wa Mjini iliyopo Amani na kupitisha maamuzi ya kuitaka Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar iongeze siku ili kuja kupandikiza wapiga kura haramu kwa idadi ya mkakati iliyokuwa imepangwa.

    Na kwamba, iliamuliwa k u w a Z A N I D h i z o zihamishiwe katika majimbo

    ya Wilaya ya Magharibi B katika uandikishaji ulioanza tarehe 24 Juni, 2015.

    Katika barua hiyo ambayo nakala yake imesambazwa kwa Wahariri wa Vyombo vya Habari, CUF kupitia kwa Naibu Katibu Mkuu w a k e N a s s o r A h m e d Mazrui wanadai kuwa, kazi ya kugawa ZAN ID kwa makundi ya watu walioletwa kwa magari nje ya vituo vya uandikishaji imefanyika ambapo waliambatanisha picha inayomuonesha mmoja wa watu wa CCM akigawa ZAN ID hizo katika kituo cha Shakani, jimbo la Dimani.

    Kwa barua hii , CUF tunaitahadharisha Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar kuacha kuendelea kuitumikia CCM kwa kupokea ag izo la kuongeza siku ili kusaidia kufanikisha mikakati ya CCM inayoshindwa. Ilihitimisha barua hiyo ya CUF.

    Katika barua yao nyingine kwa Mwenyekiti wa ZEC, Chama Cha Wananchi, CUF wanadai kuwa wana taarifa kutoka vyanzo vya habari vilivyomo ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwamba kumeandaliwa mpango wa kuvitumia vikosi kusaidia katika kuipa CCM ushindi.

    W a m e d a i k u w a , utumikaji huo ni pamoja na kuandikishwa katika maeneo ambapo sio wakazi pamoja na kutumika kuwadhibiti mawakala wa CUF ambao w a n a h o j i w a n a p o o n a

    w a k i l e t w a m a m l u k i au kuandikishwa watoto wadogo.

    Wanatoa mfano kuwa wapo watu wanaokuja na ID bandia kwa hiyo, mashine zinakataa kuwatambua.

    H a t a h i v y o , p o l i s i waliopo vituoni hutumika kulaz imisha watu hao waandikishwe na Tume haichukui hatua, kuonyesha kuwa wanajua mpango huo.

    K a t i k a k i t u o c h a Chuini, jimbo la Mfenesini vitambulisho 109 vilikataa kutambuliwa na mashine, hata hivyo nguvu kubwa ilitumiwa na kuhakikisha k u w a w a t u h a o wanaandikishwa. Hatua hiyo ilipelekea mzozo baina ya wananchi na vikosi, na hivyo wananchi waliokataa ukiukwaji huo wa taratibu, uliochochewa na Tume yako, walipigwa na kukamatwa kwa kuwekwa katika vituo vya Polisi na kunyimwa dhamana.

    Ilisema sehemu ya barua kwa Mwenyekiti wa ZEC na kuhitimisha kwa kusema kuwa CUF itaendelea kutoa mashirikiano kwa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar kwa mambo yote yanayofuata misingi ya katiba na sheria na misingi ya uchaguzi huru na wa haki inayotambuliwa kimataifa.

    Miezi miwil i i l iopita akizungumza na waandishi wa habari ofisini kawake, Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Salum Kassim Ali alieleza k u wa t u m e h i o h a i n a mafungamano na taasisi yoyote hile katika ufanyaji kazi wake na wamekuwa wakifanya kazi zao kwa ustadi mkubwa.

  • 9 AN-NUURRAMADHAN 1436, IJUMAA JUNI 26- Julai 2, 2015Makala

    WAISLAMU wa Tanzania leo hii wamepata msiba m k u b w a k u t o k a n a n a k i f o c h a k i o n g o z i mkuu Sheikh Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Sheikh Issa Shaaban bin Simba. Ikubalike kwamba Waislamu wa Tanzania wamempoteza kiongozi wao mashuhuri sana, na labda haitakuwa rahisi kuziba pengo aliloliacha. Alikuwa katika uongozi huo kwa muda mrefu hasa akiwa Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga. Bila sababu za msingi na vikiwa vyombo v y e n y e m a d h u m u n i tofauti, lakini Katiba ya BAKWATA inafanana sana na i le ya TANU/CCM. Unapata Sheikh wa wilaya ikiwa Wilaya ya kiserekali hata kama wilaya ile ina Waislamu wachache sana. Katika Uislamu, Wilaya ni sehemu kubwa sana ya nchi. Idadi ya Waislamu katika Mkoa wa Shinyanga haifahamiki vizuri, lakini inasemekana kuwa kwa D a a w a c h i n i y a A l -Marhum Issa Bin Shaaban Simba, idadi hiyo ilikuwa ikiongezeka kidogo kidogo.

    Lakini wakat i fulani h u k o n y u m a , n i l i p a t a w a r a k a k u t o k a k w a mwanaharakat i mmoja Muislamu aliyewahi kuishi Shinyanga kwa muda mrefu tu. Waraka huu ulijaribu k u n i e l i m i s h a k u h u s u mienendo ya Waislamu wa Shinyanga katika jitihada ya kuusimamaisha Uislamu Mkoani humo. Kweli ama si ya kweli , si dhamiri kuyanukuu hayo yaliyomo katika waraka huo. Hayo si mada ya makala haya. Itoshe tu kusema kuwa kwa maoni ya huyu Muislamu aliyeandika waraka ule, yeye aliona kulikuwa na kasoro kubwa katika ule mwenendo w a k u w a h u d u m i a Waislamu wa Shinyanga na wa Tanzania kwa jumla. Ningependa kusisisitiza tu kwamba, kama kuna kasoro alizozitoa, hazikuwahusu viongozi wote wa Shinyanga wa wakati ule.

    Ni bahati mbaya sana kuwa katika uongozi wa Al Marhum Sheikh Issa Bin Shaaban Simba, ni vigumu sana kutaja kwa uhakika ni wapi Waislamu wanaweza kujivuna angalau kidogo hapa Uislamu na Waislamu wamepiga hatua kubwa ya maendeleo. Wao wenyewe katika hali ya kutaabad ama kujivuna kuwa Uislamu umekuwa na unaheshimika zaidi. Yaani iwe katika daawa ama kwa mfano Waislamu sasa wameongeza shule na vyuo kadhaa. Waislamu wa Tanzania wamshukuru kiasi gani

    Bakwata leo na keshoNa Khalid S. Mtwangi

    Rais Mstaafu Muheshimiwa Benjamin William Mkapa ambaye pamoja na Ukatoliki wake, aliwaonea huruma Waislamu wa nchi hii na kuwapa majengo walioweza kusimika Chuo Kikuu hapo Morogoro. Bahati nzuri Chuo hicho hakimo mikononi mwa BAKWATA. Inasemekana kuwa kulikuwa na upinzani mkubwa kutoka kwa baadhi waliomo Serekali , wale wasio Waislamu. Wakati huo huo Kanisa Katoliki, kwa mfano, leo hii wanaweza kujivunia vyuo vikuu zaidi kumi nchi humu. Labda itakuwa si vibaya kusisitiza kuwa BAKWATA hawana hata Chuo Kikuu kimoja na hii maana yake ni kwamba Waislamu nchini kila siku watakuwa nyuma katika elimu.

    Nadhani Waislamu wa Tanzania hata hawajasikia hiyo BAKWATA ina mipango gani kuwaendeleza upande huo. Kweli ni baada ya ule mzozo wa viwanja vya Changombe ndio Waislamu w a l i p o s i k i a k w a m b a kutakuwa kiwanja mbadala cha kujenga chuo. Taarifa ambayo haikuwa na msingi w o w o t e . L a b d a t o s h a tu Ustadh Issa Ponda na wenzake wameteseka kwa kutetea mali ya Waislamu. Hiyo ndiyo BAKWATA jana na leo. Kesho itakuwaje? Waislamu wasubiri uchaguzi.

    Ki fo cha Sheikh Bin Shaaban Simba, Sheikh Mkuu wa BAKWATA kitaleta uongozi mpya pale kileleleni

    ambao, ni mategemeo ya wengi, labda nao utalazimika k u l e t a m a b a d i l i k o ya uongozi wote wa Chama hicho nchi nzima. Ni hapo ndipo Waislamu wa Tanzania watakuwa wanatazamia mabadiliko makubwa katika musakbali wa Uislamu nchini humu. Huko mbele kuna nini? Watajiuliza.

    Ni ukweli ambao ukubalike kuwa imekuwa vigumu sana huko nyuma kuleta mageuzi katika uendeshaji na utawala wa chombo hiki BAKWATA. Wakati akiwa Rais wa nchi hii Muheshimiwa Al Haj Ali Hassan Mwinyi alijaribu kutaka kuleta mabadiliko ya uongozi humo BAKWATA k wa h i y o u j e u t a wa l a mwingine; na mfumo pia ubadilike. Mzee Rukhsa h a p a a l i k u t a k i z i n g i t i ambacho hakikumpa rukhsa apite. Hakika bila shaka kutakuwa na wasomaji watakaokumbuka hotuba ya Sheikh Mkuu wa wakati u le wakat i wa Maul id iliyosomewa Shinyanga. Sheikh Mkuu yule alisikika akidiriki kusema huyu Rais Mwinyi ataiweza wapi, BAKWATA ina wenyewe. Hakusema hapo wenyewe ni kina nani. Kweli baadae Rais Mwinyi hakutaka kabisa kuigusa BAKWATA ambao wao waliendelea kivyao na mambo yao kama kawaida.

    H u k u W a i s l a m u wamebaki nyuma katika maendeleo ya nchi hii, jambo ambalo linajulikana na kila Muislamu na kulalamikiwa mara kwa mara kama sio kila siku. Naye Rais Jakaya

    Kikwete alitoa malalamiko mengi dhidi ya BAKWATA mara baada ya kushika hatamu za kuiendesha nchi hii Tanzania. Bila shaka wako watakaokumbuka hutuba yake kule Arusha. Alisikika akiwashauri kwa nguvu kabisa kuwa viongozi wa B A K WATA l a z i m a wabadilike na mfumo wao pia ubadilike. Takriban miaka kumi baada ya ushauri huo kutoka kwa Rais wa nchi hii, BAKWATA iko pale pale.

    Ni kweli kuna wakati Al Marhum Sheikh Bin Shaaban Simba alijaribu kutikisa kidogo uongozi wa Makao Makuu, kitendo ambacho kwa muda kilileta tumaini la maendeleo . Wakati fulani al is ikika akiwafokea wale waliokuwa wakipita wakisema ati kuwa BAKWATA ni chombo cha CCM na Serekali. Huko nyuma, takriban miaka minne mitano hivi, nilikutana na sheikh mmoja ambaye wakati huo alikuwa na wadhifa hapo makao makuu ya BAKWATA. Kwa mbwebwe za kujiamini kabisa, alinihakikishia kuwa BAKWATA aliyokuwemo yeye sio sawa na BAKWATA ile ya zamani. Sasa inataka kuleta mapinduzi kweli kweli katika harakati za kuwaletea maendeleo Waislamu wa Tanzania. Sheikh huyu anisamehe sana ataposoma makala haya na kukuta nikiwajulisha wasomaji wenzangu kuwa haukupita muda mrefu sheikh huyu alifukuzwa katika uongozi.

    Kuvuliwa kwake madaraka lilikuwa ni jambo baya sana kwa maoni yangu kwa sababu huyu ni mmoja wa wale masheikh wana elimu na sifa stahiki. Alikuwa ana Diploma ya Ualimu na leo ana degree ya fani hiyo aliyoipata kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

    Na Sheikh Mkuu wa wakati ule alipowaambia Waislamu kuwa BAKWATA ina wenyewe, hakuwataja hao ni kina nani. Hakika asingeweza kutaja siri hiyo hadharani, lakini ni muhimu hao wenyewe watambue kuwa leo hi ni mwaka 2015 hali yake katika nyanja nyingi sio sawa na 1968 BAKWATA ilipozaliwa pale Iringa huku Waislamu wakisimamiwa wakipewa ulinzi na askari wenye ala zao kamili. Ukumbi mzima hapo paliposimikwa uongozi mpya wa Waislamu wa BAKWATA, ulizungukwa na hawa watumishi wa w a n a n c h i s i l a h a z a o (bunduki) zao zikionyeshwa wazi wazi.

    Nimewahi kuambiwa na Sheikh Khamis Mataka kwamba katika utamaduni wa K i i s l a m u k i o n g o z i hachaguliwi kwa kupigiwa kura. Panapotokea kiasi k i k u b wa c h a wa u m i n i wakatoa hisia zao kwa sauti kubwa kumtaja wanayemtaka awe kiongozi wao, basi ndiye huyo atakuwa amechaguliwa na waumini awe kiongozi wao. Sio hivyo alivyopatikana Khalifa wa kwanza Sayyidna Abubakar RA? Labda katika hali tuliyonayo, Waislamu nchini humu uteuzi wa aina hiyo usiwezekane hasa kwa vile BAKWATA kwa mfano itatakiwa kuviridhisha vyombo vingi vikiwemo vya Serekali kwamba uchaguzi wa Sheikh Mkuu mpya wa BAKWATA umefuata misingi ya kidemokrasia kama inavyoeleweka na Serekali na umeendeshwa kama katiba ya BAKWATA inavotaka. Lakini muhimu ni kukumbuka kwamba wale Waislamu wanaoongozwa na BAKWATA watambue kwamba wamepata nafasi nzuri adimu sana ya kuweza kubadili mwenendo mzima wa utawala wa chama chao. Mabadiliko ambayo yataweza kuwavutia labda Waislamu wengi, kama sio wote wa Tanzania. Uje utawala ambao hakika utaleta maendeleo muhimu na makubwa kwa Uislamu na Waislamu wa Tanzania.

    Hapo BAKWATA itaweza kupata heshima kubwa sana labda miongoni mwa Waislamu wote wa Tanzania na bila kuwaudhi wale wanaosemekana kuwa ndio wenyewe.

    ALIYEKUWA Sheikh Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Al-Marhuum Sheikh Issa Shaaban bin Simba .

  • 10 AN-NUURRAMADHAN 1436, IJUMAA JUNI 26- Julai 2, 2015Makala

    Inaendelea Uk. 12

    TANGU enzi za kale jeshi lilikuwa na haja ya msaada wa miundombinu ili kuweza kutekeleza aina yoyote ile ya shughuli za kijeshi la uwanda mpana. Katika Roma ya zamani, mtandao mkubwa wa b a r a b a r a u l i j e n g wa kuwezesha siyo biashara peke yake, bali kuruhusu vikosi vya majeshi ya Roma kwenda haraka m a h a l i wa l i p o k u wa w a n a h i t a j i w a . , n a kuwasilisha mahitaji kwa ajili ya shighuli za kijeshi kufuatilia uwasilishaji huo.

    Kuelekea mwisho wa karne ya 18, jemadari wa Ufaransa, bingwa wa mikakati ya kijeshi na kiongozi, Napoleon Bonaparte akaainisha kuwa "jeshi linatembea kwa tumbo lake," akielezea upana wa miundombinu unaohitajiwa kuwezesha jeshi kuwa na chakula cha kutosha, na hivyo kuwa na uwezo wa kudumisha k i wa n g o c h a k e c h a kuendesha mapigano.

    K w a W a f a r a n s a , kushindwa kupeleka vifaa vinavyohitajiwa kwa wakati kwa majeshi yake yaliyokuwa yakipigana nchini Russia, na maamuzi ya Warussia kuchoma ardhi yao na miundombinu ili isitumiwe na majeshi ya wavamizi, mwishowe iliwezesha kushindwa kwa Wafaransa.

    Ujerumani ya ki-Nazi ilifikia hatma hiyo hiyo wakati ilipotanua vile vile kupita kiasi uwezo wake wa miundombinu wa k a t i wa u va m i z i wake wa Russia katika Operation Barbarossa. Kama awali , majeshi ya uvamizi yalikwama yakiwa na uhaba wa vifaa kabla ya kuzingirwa n a k u t e k e t e z w a a u kulazimishwa kurudi nyuma.

    Na katika nyakati za karibuni wakati wa Vita ya Ghuba mapema miaka ya 1990, kuwepo kwa mkanda mrefu wa kuwasilisha vifaa kwa majeshi ya Marekani ikijumlishwa na kutazamia kukutana n a s e h e m u k u b w a

    Darasa la Miundombinu: Ni wapi ISIS inapata bunduki zake?Na Tony Cartalucci

    Juni 10, 2015 - 'Mtandao wa Kupashana Habari'

    'NEO'

    ya majeshi ya Saddam Hussein, ilipunguza kasi ya uvamizi kasi ambayo wengi walidhani ungefika Baghdad kama dhamira ya kisiasa ingekuwepo. Nia ya kumpiga ilikuwepo, miundombinu ya kumpiga ilikuwa hafifu.

    M a f u n z o k u t o k a h i s t o r i a k w a k i a s i a m b a c h o y a n a w e z a kuyakinishwa, yanaelekea kutokuwa na undani, iwe ni kwa mbumbumbu a u u d a n g a n y i f u wa kushangaza wa waweka sera na vyombo vya habari vya nchi za Magharibi.

    Miundombinu ya ISIS

    Mfarakano mkubwa hivi sasa unaoiangamiza Mashariki ya Kati, hasa katika nchi za Irak na Syria ambako kinachodaiwa ni 'Dola ya Kiislamu\' (ISIS) kinajiendesha na papo hapo kupigana na kuyashinda majeshi ya Syria, Lebanon, Irak na Iran, tunaambiwa, imejengwa kwa miundombinu ya ulanguzi na malipo ya utekaji nyara.

    Uwezo wa kupigana wa ISIS ni wa serikali kamili. Inashikilia eneo pana linalosambaa kote Syria

    na Irak na siyo tu inaweza kulinda kijeshi na kupanua eneo h i l i , l ak in i ina raslimali za kulisimamia eneo hilo, na hata raslimali za kutawala makundi ya wakazi wa maeneo hayo i l iyoteka , Kwa wachambuzi wa masuala ya kijeshi, hasa washiriki wa zamani wa majeshi ya nchi za Magharibi, pamoja na washir ik i wa vyombo vya habari vya nchi za Magharibi waliokuwa katika misafara ya malori ya kijeshi ya mizigo iliyohitajika kwa ajili ya uvamizi wa Irak miaka ya 1990 na halafu

    mwaka 2003 , l az ima watashangaa hayo malori ya ISIS yako wapi leo. Kwa hali yoyote, kama raslimali za kuwezesha uwezo wa kuendesha shughuli za kijeshi ulioonyeshwa na ISIS ulikuwa unapatikana katika maeneo ya Syria na Irak pekee, basi kwa hakika majeshi ya Syria na Irak yangekuwa na uwezo wa kupigana kama huo au zaidi lakini kimsingi hawana.

    Na ingekuwa njia za kupeleka vifaa za ISIS zipo ndani ya maeneo hayo ya Syria na Irak, basi kwa hakika majeshi ya Syria na Irak yangeweza kutumia wanachowazidi ISIS, ndege za kivita - kuvuruga uwezo wa ISIS kutumia njia hizo.

    Lakini yote hii haitokei na kuna sababu kwanini.

    M a g a i d i n a s i l a h a z i l i z o a c h w a k a t i k a uvamizi wa Libya mwaka 2011 hima zilihamishiwa Uturuki na halafu Syria - zikisimamiwa na maofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani na mashirika ya kijasusi huko Benghazi - kituo cha ugaidi kwa miongo kadhaa. Njia za kuwasilisha vifaa za ISIS zinatokea pale ambapo Syria na Irak hazina uwezo wa kupeleka vita vya anga. Kuelekea kaskazini kwa mashirika wa NATO, U t u r u k i , n a k u s i n i mashariki kwa washirika wa Marekani wa Jordan na Saudia. Nje ya mipaka hii kuna mtandao wa miundombinu unaoenea ukanda mzima ikiwa ni pamoja na Ulaya Mashariki na Afrika Kaskazini.

    Gazet i la ki la s iku la London Telegraph l i k a t a n g a z a k a t i k a m a k a l a m wa k a 2 0 1 3 kuwa CIA inaendesha kituo cha kupeleka silaha hapo Benghazi wakati ubalozi (wa Marekani) unashambuliwa. Ilinukuu shirika la utangazaji la Marekani, CNN likisema kuwa timu-kazi ya CIA il ikuwa ikifanya kazi zake kando ya ubalozi huo kuandaa mradi wa kupeleka makombora kutoka maghala ya silaha ya Libya kuelekea kwa waasi nchini Syria.

    Silaha pia zimetokea Ulaya Mashariki, kwa

    MAMA Usamah (katikati) na wanawake wenzake wakiswalia jeneza la mwanae.

    MAMA yake Usamah (katikati) baada ya mkutano na waandishi wa habari.

  • 11 AN-NUURRAMADHAN 1436, IJUMAA JUNI 26- Julai 2, 201511 AN-NUURMakala

    Ugaidi kama tamthiliya

    Vi t a d h i d i ya u g a i d i inaendelea kuwa habari yenye mashiko na ufanisi katika kukusanya hisia za watu pande mbili zinazohusika. "Ugaidi wa kimataifa ni taswira ya kubuni ambayo imekolezwa na kuvurugwa na wanasiasa," anaainisha mwandishi mchokozi wa Uingereza na mchambuzi, Adam Curtis.

    "Ni wingu potofu la fikra ambalo limesambaa bila kuhojiwa miongoni mwa serikali duniani kote, majeshi ya usalama na vyombo vya habari."

    Kisiasa, nchi za Magharibi zimetumia vita hii ya msalaba dhidi ya magaidi kuhalalisha uvamizi angamizi mara kadhaa pamoja na ukiukwaji wa haki za binadamu ndani ya nchi na ng'ambo. Pia inavuna

    Tamthiliya pevu ya vita dhidi ya ugaidiNa Peter Bloom

    KIJANA Usamah wakati akiwa shuleni.

    HIVI karibuni katika eneo la Boston, kijana mweusi wa Kiislamu mwenye umri wa miaka 26, alipigwa risasi na kuuawa na maofisa wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI) na Idara ya Polisi ya Boston (BDP). Kama ilivyoonyeshwa siku iliyofuata, vyombo vikubwa vya habari kwa haraka, kwa mhemko na bila kutafakari, vikarudia madai ya utekelezaji wa sheria za nchi (mara nyingine hutumwa bila msemaji kujitaja) kuhusu k i l i c h o t o k e a : k u wa mtu huyo aliyekufa, Usaamah Rahim, alikuwa anakaribia kutekeleza mauaji yanayotokana na ushabiki wake kwa ISIS au kwa kuhusika na kundi hilo la kigaidi, k u w a k a t a v i c h w a maofisa wa polisi bila mpangilio halisi, akiwa anashirikiana na takriban watu wawili wengine. Wakati Rahim anatembea kwenda kazini karibu na duka la dawa la CVS majira ya saa moja asubuhi, maofisa hao wa polisi walimfuata Rahim kumuuliza tu kuhusu

    Maswali tata yatanda kuhusu kuuawa Boston kwa 'mkata kichwa' wa ISISGlenn Greenwalld na Murtaza Hussain

    mpango huo; ghafla, akatoa 'sime' au 'kisu cha kijeshi' ambacho alikataa kukiangusha, na kuwalazimisha maofisa hao kumpiga r i sas i

    kichwani.K u l i k u wa n a k i l a

    a i n a ya m a s wa l i ya wa z i ya s i y o e l e we k a kuhusu madai haya , n a b a d o y a l i a c h w a

    tu na kilichosikika ni k i w e w e k u w a ' I S I S iko Massachusetts!' na m i h a n g a i k o m i n g i kuhusu watu kukatwa vichwa. Hii ni moja ya mambo yanayosumbua sana kuhusu tukio hili: polisi sasa wanaweza k u m s i m a m i s h a m t u b a r a b a r a n i a m b a y e , kwa ushahidi wowote uliopo, hakuwa anafanya lolote baya wakati huo, wamwue, halafu wapaze sauti tu "ISIS' na 'Gaidi' na 'kukatwa kichwa' n a k u r u d i a r u d i a n a hakuna maswali yoyote yatakayoulizwa.

    K u w a s h a w i s h i waandishi wa habari wakubali madai yao, FBI na BDP walisisitiza kuwa kulikuwa na mkanda wa kamera ya ufuatiliaji ambao ungeondoa shaka kuhusu ki l ichotokea, wakidai kuwa "ufuatiliaji kwa kamera ya video u m e d h i h i r i s h a k i l e maofisa walichosema." L a k i n i h a w a k u t o a mkanda huo, na badala yake wakatumia karibu wiki mbili kulainisha na kuvuruga akili za watu kwa kurudia madai kuhusu kile ambacho video hiyo ambayo haijaonekana inachoonyesha.

    Video hiyo mwishowe

    ilitolewa. Kuiita video hiyo kuwa ni kichekesho, ingekuwa upendeleo. Kamera ipo umbali wa mita 50 kutoka tukio l i l ipotokea. Kioo cha kamera kimefichwa na matone ya mvua. Viwiliwili vya watu vinatambulika kwa taabu. Hakuna silaha zinazoonekana, ikiwa ni pamoja na silaha yoyote aliyokuwa nayo Rahim. Wa k a t i i n a o n y e s h a kuwa Rahim hakupigwa risasi kwa nyuma kama kaka yake alivyosema mwanzo (na baadaye akakiri kuwa hakuwa na ufahamu sahih i ) , ha ionyesh i chochote k ingine . Kwa jumla , ha iwezekani kusema nini kilitokea kutokana na video hii iliyopigiwa chapuo sana , n je ya kuwa Rahim anaonekana alikuwa akitembea kwa amani wakati alipofuatwa na watu kadhaa, ambao hawakuwa wamevaa sare za polisi, katika mfumo wa kutishia, kijeshi:

    Vyombo vya habari vilivyokuwa vinaikuza v i d e o h i y o k a m a uthibitisho wa kile polisi wa l i c h o s e m a h a r a k a wakaona kuwa inaonyesha kinyume chake. "Kutoa

    faida isiyo ya kawaida ya fedha ambayo hatua hizo za uvamizi zimewezesha baadhi ya makundi yenye nguvu ya maslahi katika nchi za Magharibi.

    Wakati huo huo, serikali za nchi za Magharibi na makundi ya kiharakat i sawia yameendelea kutumia uzungumzaji huu kuelekea malengo yao ya kisiasa na kiuchumi. Usawiri wa Vita dhidi ya Ugaidi kama mapambano ya kimataifa "imefanya hata mashambulizi ya kigaidi ya ndani ya nchi kuonekana kama sehemu ya mapambano haya mapana." Kinacholeta wasiwasi kwa kiasi kikubwa pia ni kuwa mitandao hii ya kimataifa i n a e n d e l e a k w a k a s i kubadilika kuwa jitihada ya kuunda 'Dola ya Kiislamu (bandia)' ya kudumu katika o m b we l i l i l o a c h wa n a uvamizi wa Marekani nchini Irak.

    Pia, inabidi iainishwe kuwa kuuawa kwa Osama bin Laden na kupunguzwa kwa kiasi kikubwa nguvu za Al Qaeda kama taaisi ya kisiasa na kijeshi, haijaifikisha v i t a h i i k a t i k a t a m a t i yake. Badala ya kufunga mitiririko ya fedha za vita, sasa kuna "maadui" wapya kama ISIS ambao lazima wateketezwe. Vita dhidi ya ugaidi imeondoka katika mfumo wa sinema kubwa ya mamilioni ya dola za Marekani na kuwa mtiriririko wa tenda unaolipiwa kwa damu na dhahabu.

    Mpango halisi ni kuwa hakuna mpango kama huo. Ni ukweli unaoonekana kuwa nchi za Magharibi na makundi ya washirika ni heri waendeleze tamthiliya k u h u s u u g a i d i k u l i k o k u r u h u s u n g u v u z a k e za kiuchumi na kisiasa kuingizwa mashakani kwa kiwango kikubwa. Marekani

    Inaendelea Uk. 17

    na washirika wake wanaamini kuwa wanaweza kutesa, kuvamia, kuua, kukandamiza na kulitumia tatizo hili la ugaidi lisionekane; kuwa kinachohitajika tu ni kuua na kupiga marufuku wanasiasa kali wa kutosha na ustawi wake (bila kuzungumzia kuendelea kui tamalaki dunia) utahakikishwa.

    Kinachotakiwa sasa ni habari mpya ya tumaini na harakati - ambayo haitokani na hadithi tupu zenye vitendo vya kiharamia, ambako taifa lenye nguvu zaidi ndiyo bora zaidi kimaadili, ila ambalo badala yake linaangalia kwa ukweli nini kinachojificha nyuma ya uhar ib i fu huu i l i kutekeleza mabadiliko ya kina kwa ajili ya ustawi wa pamoja na uhuru halisi wa kisiasa.

    T u n a c h o h i t a j i n i m t i r i r i k o w a f i k r a ambacho kinachosukuma

    maendeleo haya siyo taifa la kibeberu linaloendeleza vita ya msalaba lenye dhamira isiyopindika ya kufikia 'haki' yake ya kisasi, lakini makundi ya kidemokrasia na haki za kijamii yakiunganika pamoja kubadili dunia kutoka chini hadi juu.

    Bila kujali Bin Laden alikufa kwa njia gani, Vita dhidi ya Ugaidi ndiyo hasa 'tamthiliya' inayohuzunisha.

    (Hii ni sehemu ya makala Fairy Tale of the War on Terror kama ilivyoandikwa na Peter Bloom. Peter Bloom ni mhadhiri katika Idara ya Watu na Taasisi katika C h u o K i k u u H u r i a . Anaandika katika fani za i t ikadi , mamlaka na siasa za ubepari na hivi sasa anakamilisha tungo kuhusu 'Ubepari wa Ki imla Zama za Utandawazi.')

  • 12 AN-NUURRAMADHAN 1436, IJUMAA JUNI 26- Julai 2, 201512 MAKALA

    SWAUMU NA NDIMI ZETUUlimi tunu adhimu, ya MANANI kwa insani,Ulimi tangu kadimu, kwa uneni namba 'wani',Ulimi MWEMA mwalimu, na MUOVU kwa waneni,NDIMI zetu TUCHUNGENI, WAFUNGAJI Ramadhani.

    Ulimi johari njema, tukufu yenye thamani,Ulimi kwa watu wema, u lulu na marijani,Ulimi kwa taadhima, kwa kweli wakuthamini,NDIMI zetu TUCHUNGENI, WAFUNGAJI Ramadhani.

    Ulimi wainajisi, waovu yako thamani, Ulimi wanakutusi, kwa kukupa sui nduni,Ulimi u IBILISI, eti mkubwa SHETANI,NDIMI zetu TUCHUNGENI, WAFUNGAJI Ramadhani.

    Ulimi u sura mbili, kwa ya INSAFU mizani,Ulimi anokujali, kwa KHERI wamuauni,Ulimi asokujali, kwa SHARI haumukhini,NDIMI zetu TUCHUNGENI, WAFUNGAJI Ramadhani.

    Ulimi sasa kwanini, tuutie lawamani,Ulimi mimi sioni, ulaumiwe kwanini,Ulimi kosale nini, nijuzeni ikhiwani,NDIMI zetu TUCHUNGENI, WAFUNGAJI Ramadhani.

    Ulimi wa RAMADHANI, WAFUNGAJI uchungeni,Ulimi kwa QUR-ANI, KUSOMA utumieni,Ulimi za ADINANI, kwao HADITHI someni,NDIMI zetu TUCHUNGENI, WAFUNGAJI Ramadhani.

    Ulimi utumieni, kumdhukuru MANANI,Ulimi uzuieni, kuwasengenya INSANI,Ulimi ukalifuni, mema unene JAMANI,NDIMI zetu TUCHUNGENI, WAFUNGAJI Ramadhani.

    Ulimi nanezo beti, zimefika ukingoni, Ulimi kwa KHAIRATI, nifanye MWENZO mwandaniUlimi kwa SHURURATI, uwe ADUI mubini,NDIMI zetu TUCHUNGENI, WAFUNGAJI Ramadhani

    ABUU NYAMKOMOGI MWANZA

    1.Leo naja na shauri , tusikilize usiaNi maneno ya Ghafuri, yasiyopatwa na doaTukajitia kiburi, mwisho wetu ni balaaHalali halali yetu, haramu tuikimbie

    2.Mola ametudhukuri, bure hakutuachiaKatufunza ya fakhari, vya halali kutumiaHaramu na vitu shari, laana vimetiliwaHalali halali yetu, haramu tuichukie

    3. Halali kitu kizuri, Allah ametuleteaHalali haina siri, kweupeni hutokeaHalali hua dhahiri, haijifichi na juaHalali halali yetu, haramu ichukieni

    4.Tuitafute halali, popote ilipokaaIkibidi kwenda mbali, pembe zote za duniaGharama tusizijali, muhimu ni manufaaHalali halali yetu, haramu tuichukie

    5. Haramu tusijadili, haifai kutumiaHaramu kwetu dajali, Mola hakuiridhiaHaramu japo ni mali, acha ndugu nakwambiaHalali halai yetu, haramu tuichukie

    6. Halali iwe awali, tunapo pambaukiwaIsijekuwa ya pili, kinyume tukachaguaHayo nayo tuyajali, yafaa kuzingatiwaHalali halali yetu, haramu tuichukie

    7. Machumo tutafakari, kabla ya kuchukuaTunakokwenda shubiri, na muda umewadiaTukijifanya ayari, moto unatungojeaHalali halali yetu, haramu ichukieni

    8. Yatosha nilohubiri, ndugu kuwafikishiaYapo kwenye mstari, na hayaja expireSi ya kale yalojiri, bado yanaendeleaHalali halali yetu, haramu tuichukie

    Mtunzi ni:-Zainab H. Mtima

    Mbweni, Zanzibar0717 165 602

    HALALI NA HARAMU

    Darasa la Miundombinu: Ni wapi ISIS inapata bunduki zake?Inatoka Uk. 10

    mfano gazeti la New York Times likitoa taarifa mwaka 2013 katika makala "Upelekaji wa silaha kwa waasi wa Syria wapanuka, kwa msaada wa CIA," kwamba:

    Kutoka katika ofisi za siri, maofisa wa kijasusi wa Marekani wamesaidia serikali za nchi za Kiarabu kununua silaha, ikiwa ni pamoja na manunuzi makubwa kutoka Croatia, na wamewapa kibal i makamanda na vikundi vya waasi kuamua nani achukue s i laha hizo wakati zikiwasili, kwa mujibu wa maofisa wa Marekani wakizungumza kwa sharti la kutokutajwa.

    Na wakati mashirika ya habari ya nchi za Magharibi wakati wote yanazungumzia ISIS na makundi mengine yanayoendesha shughuli zao chini ya mwavuli wa Al Qaeda kama 'waasi' au 'wenye siasa za wastani,' ni wazi kama silaha zenye thamani ya mabilioni ya dola za Marekani zinaelekezwa kwa 'wenye siasa za wastani,'ni wao, n a s i y o I S I S a m b a o wangetamalaki katika eneo hilo.

    Ta a r i f a z i l i z o v u j a s i k u z a k a r i b u n i zilisema kuwa kuanzia mapema 2012 Wizara ya Ulinzi ya Marekani siyo tu ilianza kuweka mkakati wa kuundwa kwa 'eneo la kisultani la Salafi' linaloenea nchi za 'Syria na Irak, eneo ambalo hasa ndiyo ISIS i l iko, i la i l ikaribisha ISIS kwa mikono miwili na kuchangia kujenga mazingira yaliyoiwezesha kuzuka.

    Njia za uwasilishaji vifaa za ISIS ni pana kiasi gani?

    Wakati wadadisi wengi katika nchi za Magharibi wanapendelea kusema kuwa hawajui ISIS hasa inapata mahitaji yake kutoka wapi ili iweze k u e n d e l e z a u w a z o wake wa kushangaza wa kupigana, baadhi ya waandishi wa habari wametembelea eneo hilo na kuchukua picha na maelezo na kutoa taarifa

    za milolongo ya magari ya vifaa yanayofikishwa kwa majeshi ya kigaidi. Magari hayo yalikuwa yanatokea katika viwanda katika maeneo yanayoshikiliwa na ISIS ndani kabisa ya nchi za Syria na Irak? Katu. Yalikuwa yanatokea ndani kabisa ya Uturuki, kuvuka mpaka wa Syria bila kusumbuliwa na kitu chochote, na kuendelea na njia yake yakiwa na ulinzi usio rasmi wa vikosi vya majeshi ya Uturuki hapo kando.

    Majaribio ya Syria kushambulia misafara h i i n a m a g a i d i wanaomiminika pamoja nayo, yamekabiliwa vikali na ulinzi wa anga wa Uturuki.

    Shirika la Utangazaji la Ujerumani, Deutsche We l l e ( D W ) l i l i t o a mkanda wa sauti wa kwanza kutoka kianzio muhimu cha habari nchi za Magharibi kuonyesha kuwa ISIS inapata vifaa siyo kutoka 'ulanguzi wa mafuta' au 'malipo ya utekaji nyara', ila ni vifaa vyenye thamani ya mabilioni ya dola za Marekani vinavyopelekwa Syria kupitia mipaka ya mwanachama wa NATO, Uturuki, kwa njia ya mamia ya malori kwa siku.

    Ripot i h iyo yenye kichwa cha habari "Njia za kupokea vifaa za ISIS kupitia Uturuki," i n a y a k i n i s h a k i l e ambacho kilishatajwa na wachunguzi wa ramani ya kisiasa kuanzia hata 2001 - kuwa ISIS inaishi kwa ufadhili mkubwa wa nchi kadhaa, ikiwemo bila shaka, Uturuki yenyewe.

    Ukiangalia ramani ya maeneo yaliyoshikwa n a I S I S n a k u s o m a taarifa za mapito yake na mashambulizi kote katika ukanda huo na hata mbali zaidi, mtu a n a w e z a k u d h a n i a kuwa mamia ya malori kwa siku yangehitajika kuwezesha kiwango hiki cha uwezo wa kupigana. Mtu angeweza kufikiria misa fara kama h iyo ikiingia Irak kutoka Jordan na Saudia. Misafara kama hiyo ingeweza kuingia Syria kutoka Jordan.

    Kwa jumla, ukizingatia hali halisi ya miundombinu n a u m u h i m u w a k e usioisha kwa kampeni za kijeshi katika historia y o t e y a b i n a d a m u , hakuna maelezo mengine yanayokidhi kuhusu uwezo wa ISIS kuendesha vita ndani ya Syria na Iraq, nje ya kiwango kikubwa cha raslimali kinachopelekwa kwake kutoka ng'ambo.

    Kama jeshi linatembea kwa tumbo lake , na tumbo la ISIS limejaa vifaa kutoka NATO na nchi za Ghuba, ISIS itaendelea kutembea moto mdundo kwa muda mrefu. Kiini cha kuweza kuvunja nguvu za ISIS ni kuvunja uti wa mgongo wa njia zake za kupokea vifaa. Kufanya hivyo hata hivyo, na ndiyo maana mgogoro huu umeendelea kwa muda mrefu, Syria, Irak, Iran na wengine ingebidi hatimaye wafunge mipaka na kuwalazimisha ISIS kupigana ndani ya mipaka ya Uturuki, Jordan na Saudia, mkakati mgumu kuufikia kwani nchi kama Uturuki zimeunda maeneo ya kujihami ya kudumu ndani ya Syria a m b a y o ya n g e h i t a j i mkabiliano wa ana kwa ana na Uturuki yenyewe ili kuyaondoa.

    Huku Iran ikiingia katika mapambano hayo kwa kuhamisha maelfu ya askari kuinua operesheni za kijeshi za Syria, kanuni muhimu za t ishio la usalama zinaweza kuizuia Uturuki kutumia kwa dhamira halisi maeneo hayo ya kujihami.

    Tul ichobaki nacho wakati huu, ni NATO kimsingi ikiwa imeshikilia eneo hilo nyara kwa u we z e k a n o wa v i t a mbaya sana ya kikanda katika juhudi za kulinda na kuendeleza uharibifu u l i o f a n y wa n a I S I S ndani ya Syria, ikiwa imefadhiliwa kikamilifu kwa mtandao mkubwa wa miundombinu ikitoa katika maeneo ya NATO.

    ( T o n y C a r t a l u c c i , anayeishi Bangkok, Thailand, ni mtafiti wa ramani za kisiasa na mwandishi, hasa kwa jarida la mtandao, "New Eastern Outlook.' Makala hii imetafsiriwa Kiswahili na Anil Kija.)

  • 13 AN-NUURRAMADHAN 1436, IJUMAA JUNI 26- Julai 2, 2015MAKALA/Matangazo

    Hakuna jengo la Msikiti wala Madrasa, kuna kiwanja kilichotolewa (WAQFU) miaka mitatu iliyopita. wanafunzi wanasomea Quran katika majani kama wanavyoonekana katika picha. Pamoja na kuisoma Quran katika mazingira magumu, lakini kwa kuwa huu ni mwezi wa Quran, tumeandaa mashindano ya kuhifadhi Quran kwa vijana wote wa eneo la Hondogo na maeneo ya jirani kuanzia Ramadhan 10-17. Lakini hatuna mdhamini wa kutuwezesha zawadi kwa washindi watakaopatikana katika shindano hilo.Hivyo basi tunaomba mchango wako wa chochote ulicho nacho ili tununue zawadi kwa ajili ya watoto hao na kuzidi kuwatia moyo na kuwa na mapenzi na Quran yao.kwa mawasiliano zaidi tupigie simu No. 0715 259635 au 0757 375993

    CHANGIA MASHINDANO YA QURAN AL MADRASATIL FADHAKIR HONDOGO DAR

    Jumuiya na Taasisi za Kiislamu (T), imeandaa Dua maalumu, itakayowashirikisha Waislamu wote leo siku ya IJUMAA, katika Msikiti wa Mtambani, Kinondoni.Waislamu wametakiwa kushiriki kwa wingi ili kumlilia Allah (s.w) ndani ya Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani kwa kuzingatia uzito na utufukufu wake, hii ni kufuatia kadhia mbalimbali walizokutana nazo kabla ya Mwezi huu.Pia Viongozi wa Jumuiya (Masheikh) watazungumzia: Waislamu na uchaguzi Mkuu wa Urais na Madiwani.Dua itaanza mara baada ya mshuko wa Ibada ya Swala ya Ijumaa, Msikitini hapo.

    Sheikh Rajab Katimba.

    Dua Maalum Masjidi Mtambani (Leo)

    KUTOA ni jambo gumu sana kwa mwanadamu h a s a i w a p o n i k i t u anachokipenda. Na vilevile ni jambo linalopendwa sana na Uislamu. Kwa ajili hii, ndio tunaona kuwa Uislamu umelitilia nguvu sana jambo hili na kuliandalia malipo makubwa.

    Allah SW amelipangia njia tofauti jambo hili kwa kumfanya mtu wepesi wa kumfanya na asiwe bakhili na hili ni kwa kumuekea njia ya wajibu na njia za suna. Hakika kutoa kumeandaliwa malipo makubwa ambayo ni tofauti na ibada nyengine na hili lipowazi.

    Mfano wa wanao tumia mali zao katika Njia ya Mwenyezi Mungu, ni kama mfano wa punje moja iliyo chipuza mashuke saba. Katika kila shuke zimo punje mia. Na Mwenyezi Mungu humzidishia amtakaye, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa na Mwenye kujua. (2:261.

    Hili ni moja miongoni m w a f a i d a n y i n g i zipatikanazo kwa kutoa sadaka. Nyengine miongoni mwa faida hizo, nikujenga mahaba na mapenzi kati ya wanaopeana. Ndio Mtume SAW alivyozijenga imani za Masahaba mpaka zikafikia daraja ya kupendana na kupeana bila kujali, huku wakitarajia malipo makubwa mbele ya Allah SW.

    Jambo hili la kutoa kwa hakika lina faida nyingi kubwa zaidi katika hizo ni kufunikwa na kivuli cha Arshi ya Allah SW siku ambayo hapatakuwa na kivuli ila hicho. Nayo ni s iku ya Kiama ambapo jua litawakaribia viumbe kiasi ya shubiri moja juu ya vichwa vyao. Kwenye hadithi iliopokewa na Imam Bukhari na Muslim wamelezewa watu wa aiana 7 watakao funikwa nna kivuli hicho, mmoja wao ni mtu aliyetoa sadaka akaificha mpaka ikafika kutojua mkono wa kushoto kilichotoa mkono wa kulia.

    Jambo hili tukufu tunapata fursa ya kujifunza katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani na inapomalizika Ramadhani hugeuka hali zetu tukawa wagumu wa kutoa kama kwamba wale waliokuwa wakitoa katika mwezi wa Ramdhani sio sisi bali ni watu wengine. Inatakiwa kwa Muislamu kuwa mwepesi wa kutoa kwani kila unachokitoa kwa a j i l i ya Al lah SW h u wa h u j a p o t e z a b a l i ni akiba kubwa ambayo umejiwekea ya kukusaidia siku ambayo hapana cha kukusaidia isipokuwa kile u l i c h o k i t a n g u l i z a k wa mikono yako.

    Kuwa na subiraMuislamu anatakiwa

    kuwa mwenye kusubiri baala zote zinazomkumba katika maisha yake ya hapa duniani, kwa kiasi kile ambacho Muislamu anachokumbwa na balaa na mitihani na akasubiri, ndio huwa daraja yake inapanda mbele ya Allah SW. Ndio kwa maana hii akasema Mtume SAW:

    Allah anapowapenda waja wake, huwajaribu kwa kuwapatia mitihani ya kila

    Ramadhani ni Darasa -Kutoa sadakaaina.

    Na hili ni moja miongoni mwa faida nyingi zipatikazo katika kusubiri kwa kuwa karibu na Allah SW hii ni faida nyengine inayopatikana kwa kusubiri kwani Muislamu kiasi ambacho atakuwa ni mwenye kumkumbuka Allah SW wakati wa raha hailingani na kiasi atakavyo mja kumkumbuka Allah SW wakati atakapo kuwa na matatizo kisha akawa ni mwenye kusubiri huku akifahanu wazi kuwa yote ni yake yeye Allah SW, Hakika Allah y